Naibu Spika Job Ndugai amtoa nje Mbunge wa CCM kwa siku tatu
Ni Faustine Ndugulie mbunge wa Kigamboni. Tulizoea kuona wa CHADEMA tu lakini leo tunamuona na wa CCM.
Nimewahi kuwalletea thread maana nimekikuta hicho kitendo ignawa mwanzo wake sikuwepo kwenye TV.
Ndugai katumia kanuni 73{3}:{ Endapo Mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha ukweli wa maneno aliyoyasema na hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo, Spika anaweza kumsimamisha Mbunge huyo asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano}
Ndugulile out.afukuzwa na naibu spika kwa maelekezo ya ccm
mbunge wa kigamboni ametolewa nje na naibu spika Ndugai baada ya kukataa kufuta kauli yake aliyoambiwa aifute kauli yake kwamba waziri amewahonga madiwani.
Baada ya asubuhi kushindwa kutumia kanuni za Bunge dhidi ya Mnyika na ushahidi wake , jioni hii amethibitisha kuwa amejifunza baada ya kusoma kanuni na kazisoma tena kinyume kwani amemtoa nje Ndungulile kwa siku tatu wakati akijua wazi kuwa kanuni zinaelekeza kitu gani.
Nanukuu kanuni za Bunge 1. Kanuniya Adhabu : hii ni kanuni ya 73 (3) “Endapo mbunge yeyote atatakiwakuthibitisha ukweli wa jambo au suala alilolisema Bungeni na hadi kufikiamwisho wa muda aliopewa amekataa au ameshindwa kutoa uthibitisho huo,Spikaanaweza kumsimamisha Mbunge huyo kuhudhuria vikao vya Bunge visivyozidi vitano”
Ndungulile hakuambiwa athibitishe , ila aliambiwa awaombe radhi sasa kitendo cha kumtoa nje ni kutaka kuaminisha umma kuwa hata wabunge wa CCM wanaweza kutolewa nje na hivyo yuko fair.
kanuni ya 71 (1) "bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 100 na 101 ya KATIBA ,mtu yeyote asiye Mbunge ambaye atajisikia kuwa amepata athari hasi kutokana na kauli au maneno au shutuma zilizotolewa Bungeni kumhusu yeye binafsi ,anaweza kupeleka malalamiko pamoja na maelezo yake ya kujitetea kwa Spika:"
kanuni 71 (2)" mara baada ya kupokea malalamiko yaliyowasilishwa kwake kwa mujibu wa fasili ya (1) ya kanuni hii na kujiridhisha kuwa malalamiko hayo yameandikwa katika lugha ya heshima na ya kistaarabu na yanatoa hoja mahususi na ambayo si ya uzushi ,uongo,uchochezi au chuki binafsi;na kwamba yanastahili kufikiriwa au kufanyiwa kazi na kamati ya haki,maadili na madaraka ya Bunge ,Spika atayapeleka malalamiko hayo kwenye Kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge ili kuyatafakari na kulishauri Bunge"
Hakika Bunge hili kwa ukada huu, kwani Ndungulile alisema kuwa madiwani wa Kigamboni waliletwa bungeni na waziri na hiyo ni rushwa ili waweze kukubaliana naye kuhusu mradi wa mji mpya Kigamboni ambao umewafanya wananchi washindwe kujenga kutokana na kukosekana kwa fidia na kuzuiowa kuendelea na ujenzi.
Badala ya Ndugai kumpeleka Ndungulile kwenye kamati ya maadili anampa adhabu bila kumpa nafasi ya kujitetea , mbona hakupewa siku saba kuonyesha jinsi ambavyo waziri alikuwa amewahonga madiwani hao wa Kigamboni?
Tatizo hiyo jamii ya akina ndugai wabishi sana. wabishi hata wasichokijua
"Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."
dr. Ndugulile wa Kigamboni atolewa nje ya bunge. Mdee aitwa kituko
Baada ya kushindwa kutoa uthibitisho kuhusu serikali kuhonga madiwani wa Kigamboni! Wakati naibu spika akitoa hukumu ndipo Halima Mdee (waziri kivuli wa ardhi) akataka kutoa taarifa, Job Ndugai akamzuia kisheria! Ndipo akawaambia wana Kawe kuwa wamechagua kituko! Eti anataka amtoe nje apate umaarufu na aandikwe kwenye magazeti!
My take: Job Ndugai hongera kwa kuua CCM! Janga la taifa
Kama madiwani waliletwa bungeni kwa gharama za waziri/serikali ili kuwa sehemu ya mjadala ambao ki-msingi unaegemea upande wa serikali basi hiyo ni rushwa. Kama mtakumbuka ile CCCC iliyoleta kasheshe uchukuzi hadi Omar Nundu akaondolewa ofisini imekuwa black-listed kwenye miradi inayofadhiliwa na World Bank kwa sababu ya rushwa. Na aina ya rushwa ya hawa CCCC ni kama hii ya madiwani kwamba walikuwa wanawasafiirisha officials ambao ndio wanatakiwa kufnaya maamuzi.
Nadhani matokeo ya hii adhabu ya huyu mbunge yanaweza kusaidia kumulika wageni wanaoletwa bungeni wakati wa vikao. Kuna rushwa kubwa sana.
Follow Us Here