Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mahakama ni kichaka cha serikali cha kujificha

    Report Post
    Results 1 to 3 of 3
    1. #1
      mangifera's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th October 2011
      Posts : 47
      Rep Power : 394
      Likes Received
      34
      Likes Given
      1

      Default Mahakama ni kichaka cha serikali cha kujificha

      Mahakama ni kichaka cha serikali cha kujifichia

      Kuna imani kuwa taifa limeundwa na mihimili mitatu mikuu yaani BUNGE, MAHAKAMA na EXECUTIVE(BARAZA LA MAWAZIRI) ambalo rais ndo mwenyekiti. Tunadanganywa kuwa mihimili hii ni huru, yaani haiingiliani katika maamuzi na kazi zake. Lakini tunachoshuhudia si kweli. Ni vigumu mtanzania kutofautisha kati ya katibu mkuu wa CCM, jaji wa mahakama, waziri au spika wa bunge. Wote wanafanana kiitikadi kisera na kimtizamo. Na huenda wanakula meza moja.
      Ukiangalia upande wa mahakama ndiyo mbaya kabisa, viongozi wote wa juu kuanzia jaji mkuu huteuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala. Rais huingilia kwa urahisi sana maamuzi ya mahakama kama tulivyoona alivyoingilia mgomo wa madaktari kwa kutoa maamuzi huku akitudanganya kuwa kesi iko mahakamani. Mahakama haijakemea wala kusema lolote. Pia muhimili mwingine wa serikali ambao ni bunge kwa kupitia spika umekuwa ukiilinda sana serikali(executive) pale ambapo amekuwa akiitetea serikali au kuzuia majadiliano yoyote katika hoja ambayo serikali inaelekea kushindwa.
      Hata pale ambapo waziri mkuu aliulizwa swali la msingi la kutakiwa ajiuzulu kwa kushindwa kutatua matatizo ya wananchi (mgomo) spika alimlinda kwa kumwambia "hilo usijibu mh. W/K"

      Sasa tunashuhudia serikali kuitumia mahakama kama kichaka chake cha kujificha baada ya kushindwa kutatua matatizo ya afya za wananchi na madaktari kwa kufungua kesi za uongo zisizokuwa na kichwa wala miguu, yaani kosa kafanya kenge, anashtakiwa mjusi eti kwa sababu wote ni damu baridi na wana magamba. Kila ikiambiwa jibuni hoja wanasema kesi ipo mahakamani. Lakini wakitaka kujinufaisha huvunja mwiko wa mahakama bila kuulizwa!!

      Kwa sababu hii mahakama inatumika kama kichaka cha serikali kujifichia na imeshafanya hivyo mara nyingi hata wakati ule wa mgomo ulioitishwa na TUCTA.
      KOMBESANA likes this.

    2. Miaka 50

    3. #2
      Kiti's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Posts : 216
      Rep Power : 477
      Likes Received
      31
      Likes Given
      0

      Default Re: Mahakama ni kichaka cha serikali cha kujificha

      Rais dhaifu, serikali legelege

    4. #3
      Communist's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st June 2012
      Location : Ubungo
      Posts : 2,729
      Rep Power : 2267
      Likes Received
      601
      Likes Given
      783

      Default Re: Mahakama ni kichaka cha serikali cha kujificha

      Simple life is healthier than egoism.

    5. RukaaJuu Final

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...