Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: CCM Mwanza haijatulia

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 23 of 23
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,706
      Rep Power : 3660
      Likes Received
      3225
      Likes Given
      473

      Default CCM Mwanza haijatulia







      JUMATANO, JULAI 11, 2012 06:24 NA JOHN MADUHU, MWANZA

      WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, wamemtuhumu mwenyekiti wa chama hicho mkoa, Clement Mabina kuwa ni mmoja wa viongozi wanaokiangusha chama chao.

      Mabina, alishushiwa tuhuma hizo nzito katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho, kilichofanyika Chuo cha Veta Nyakato, kilitawaliwa na maneno ya kejeli,vurugu na ubabe, huku baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakitishiana kutaka kupigana ngumi kavu kavu kutokana na kutofautiana kauli.


      Wajumbe wa kikao hicho, inaelezwa walikuwa wakitofautiana na wakati mwingine kuzomeana au kupigiana makofi kutokana na tofauti zilizopo.

      Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zinasema tuhuma za Mwenyekiti kujihusisha na rushwa na kushindwa kukiongoza chama hicho na kukisababishia kupoteza baadhi ya majimbo zilirushwa kwake na wajumbe wa Halmashauri ya Mkoa, Richard Rukambura pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athuman.

      Taarifa za uhakika, zinasema aliyeanza kumshambulia Mabina ni Rukambura ambaye alikieleza kikao hicho kuwa suala la kupinga rushwa katika chaguzi limekuwa zito kutokana na viongozi waliopewa dhamana ya kupiga vita rushwa wamekuwa wakijihusisha na rushwa.

      “Tuanze nawe Mabina,wewe ni mpokeaji wa kitu kidogo namba moja,umekuwa ukipokea rushwa katika chaguzi mbalimbali kwa ajili ya kuwapendelea baadhi ya wagombea,hivyo hufai kuendelea kuwa Mwenyekiti",alisema Rukabura.

      Kutokana na madai hayo, alikuja juu na kumtaka mjumbe huyo aketi chini ambapo hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu, Kache aliingilia kati na kumtaka Mabina kumuacha mjumbe huyo azungumze suala hilo hadi mwisho.

      Kiongozi mwingine, aliyemtuhumu Mabina ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Zebedayo Athuman alidai mwenyekiti huyo ameshindwa kuunganisha chama.

      Akijibu tuhuma hizo, Mabina aliiambia MTANZANIA kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake hazina msingi wowote, zaidi ya wajumbe hao kuwa na chuki zao.

      “Haya ni mambo ya kupangwa ili kuvuruga kikao,mimi sio mla rushwa, nafuata taratibu katika kusimamia haki na sio vinginevyo",alisema Mabina




    2. #21
      kijereshi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Location : bubinza
      Posts : 206
      Rep Power : 405
      Likes Received
      54
      Likes Given
      5

      Default

      Quote By mzungukichaa View Post
      kweli ccm imejaa rejects,hadi huyu ? Mwizi maarufu toka niko darasa la kwanza pale nyamagana miaka hiyo ? Lol. Ccm is like music, no matter what the music changes,it keep on dancing !
      umenifurahisha mkuu kumbe nyamagana product kwa mwl.paschal hehehe nakupa tano huko ulipo

    3. #22
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,712
      Rep Power : 15286
      Likes Received
      3768
      Likes Given
      2906

      Default Re: CCM Mwanza haijatulia



      Wakitaka kutulia vizuri inabidi waombe ushauri kwa Dr. Slaa atawasaidia sana vinginevyo wataendelea kujichanganya tu.

    4. #23
      IWILL's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd June 2011
      Posts : 181
      Rep Power : 444
      Likes Received
      34
      Likes Given
      51

      Default Re: CCM Mwanza haijatulia

      Quote By Nyangomboli View Post
      Jamaa wa Magnum alikuwa anaitwa Mamata na walikuwa kundi moja na wahaya fulani jina sina na Polly mwenyekiti wa Misungwi akiwemo.
      Huyo polly sina shaka ni benard poli kam ni yeye. alikuwa ni kibaka aliyejipendekeza vibaya sana kwa magnum(matata) mpaka akafanikiwa kuingia kwenye genge hilo. sasa huu mtandao unaongoza ccm mwanza ni last chapter kwa chama hicho...let us see this drama.

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...