Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Waandishi wa Habari Tanzania wamekosa Uzalendo

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 27 of 27
    1. #1
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,826
      Rep Power : 1940
      Likes Received
      1231
      Likes Given
      1193

      Default Waandishi wa Habari Tanzania wamekosa Uzalendo

      Kwa takriban siku mbili nipo Tanzania na napata fursa kubwa kusoma magazeti ya nchi hii na pia kusikiliza radio na kuona TV mbalimbali za Tanzania hususan Bara naona kweli Maadili ya Uandishi wa Habari sio tu wa magazeti lakin pia hata Radio na TV umekosa uzalendo.

      Waandishi wengi sana wamejikita katika USHABIKI na kupenda kufanya BIASHARA ya habari zao na kusahau kabisa miiko na Sharia na kaanun za Uandishi wa habari. Tukumbuke mwiko mkubwa kwa mwandishi yoyote wa habari ni USHABIKI. Mwandishi anatakiwa kutoa ripoti ya kile anachokiona bila kuongeza jambo lake lolote na kama anataka kuripoti tukio ni lazima ahakikishe anatenda haki kwa kila upande kwa kupata maoni na rai zao. Kwani siku zote habari inakuwa na sehemu mbili (mlalamika na mlalamikiwa).

      Inatakiwa ifahamike kuwa kazi ya Mwandishi wa habari ni KUELIMISHA JAMII, KUBURUDISHA JAMII na Kuijuza au KUIPASHA HABARI JAMII. Kwa mantiki hii utaona Kalamu ya mwandishi ni sumu au bomu baya sana kuliko lile la nyuklia. Mwandishi siku zote anatakiwa kutumia busara sana katika kazi zake ikiwemo na kuweka uzalendo wa nchi yake mbele kwa kutoa habari zilizo sahihi zisizo na hata chembe ya ushabiki kwa jamii kwani jamii inataraji kupata habari zilizo sahihi na zisizo na upendeleo wa upande wowote.

      Ukipitia Sharia za Tanzania inaozungumzia Uhuru wa maoni sharia namba 15 ibara ya 6 ya mwaka 1984, kifungu cha 18

      .-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
      kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
      chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wamawasiliano yake kutoingiliwa kati.(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusumatukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimukwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
      muhimu kwa jamii.
      Kwa hicho nilichobainisha Juu utaona karibu kila chombo cha habari tanzania kimekosa uzalendo. Chukulia habari ndogo tu jinsi wanavyoripoti mambo kutoka Bungeni. Waandishi hawa hawana umakini na hawajui kuwa kuna sharia maalum za uandishi wa habari za Bunge na Mahakama. Wao wanajaza ushabiki miongoni mwa jamii za Kitanzania na kuigombanisha Serikali na raia wake kwa manufaa yao ya kibiashara na kisiasa na kusahau Amani ya nchi hiyo.

      Jana nilikuwa napitia habari za Kiongozi wa madaktari Dr Mkopi kufikishwa mahakama ya kisutu. Utaona kila gazeti limeripoti linavyofahamu na kwa mtu makini kama atasoma unaona kabisa waandishi hawa wana nia kubwa ya kuigombanisha Serikali na Madaktari bila kufahamu kuwa watakao umia ni wananchi. Wameshindwa kabisa kujua kuwa Dr Mkopi ameshitakiwa na mahakama kwa kudharau amri halali ya mahakama na sio Serikali.

      Ukisoma kwa kina wanashindwa kabisa kuofautisha Mahakama, Serikali na Bunge. Kwao wao kila kitu ni sawa. Nasikitika sana kuona Baraza la Habari Tz limekaa kimya na hata wizara ya habari Tz zimekaa kimya bila kukemea haya. Kwa tunaamini kuwa msipoziba Ufa basi kifo kitawaumbua.

      nawasihi muwe wazalendo kwa nchi yenu na ondoeni kabisa ushabiki wa Siasa au kidini kwani mnaiangamiza nchi yenu.


      Haya ni maoni yangu kwenu
      Dr Hamza Yousuf Al naamaniy (Barubaru)

      Mwanza Tarabu (Muta) na Nkurukumbi

      Omwana nikalikwela,ina shani ommano,
      Lutiluti nanda maiza, omoyo tigindi munda.
      Owenfundo nyamilinga, lugayo olwo nakubone,
      ijamawe kinyalyana, lugayo ongalule moyo

      Nkurukumbi 2

      hay
      Last edited by Barubaru; 11th July 2012 at 12:08.
      Pascal Mayalla likes this.
      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul


    2. #21
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,826
      Rep Power : 1940
      Likes Received
      1231
      Likes Given
      1193

      Default Re: Waandishi wa Habari Tanzania wamekosa Uzalendo

      Ernesto Che

      Mimi natamka sharia na naita hivyo kama wewe unavvyoitwa Sheria. Hizo hazina tatizo kama vile mimi ninavyoita Skuli na wewe unaita shule au Wewe unaita SOKONI na mimi naitwa marikiti.

      Zote ni lahaja msingi mkuu na kuelewa nimekusudia nini.

      lakin la mwisho mimi nazungumzia MAADILI YA UANDISHI WA HABARI kama taaluma. na nakemea ushabiki kama sumu kuu inayopandwa na waandishi kwa jamii zenu za waTanganyika. Znz hakuna haya.
      Last edited by Barubaru; 14th July 2012 at 16:31.
      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    3. #22
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,826
      Rep Power : 1940
      Likes Received
      1231
      Likes Given
      1193

      Default Re: Waandishi wa Habari Tanzania wamekosa Uzalendo

      Quote By Kaa la Moto View Post
      Umemuuliza swali gumu sana.
      Inabidi arudi chuo kusoma ndipo aweze kulijibu.
      I give u a like!
      S
      uala gani hilo la kunitaka mimi tena kurudi skuli?mbona sijaliona.

      Naomba ujipambanue kwani hapa nimejikita zaidi katika maadili ya UANDISHI na sio vinginevyo.
      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    4. #23
      Ibambasi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th July 2007
      Location : Iponyamakalai - Isungang'holo
      Posts : 752
      Rep Power : 764
      Likes Received
      128
      Likes Given
      823

      Default Re: Waandishi wa Habari Tanzania wamekosa Uzalendo

      Quote By Barubaru View Post
      Ibambasi,

      Inakubidi upitie sharia zenu katika katiba yenu imeweka mambo wazi kabisa kuwa mwenye haki ya Kushitaki ni JMTz kupitia vyombo vyake DPP. Hivyo hata ukikataa kutii amri ya mahakama basi chombo cha Serikali chenye mamlaka hayo.

      Kumbuka hata Mbowe alipokiuka amri za mahakama kule Arusha alikamatwa na Serikali kupitia vyombo vyake na kupelekwa mahakamani.

      Kumbukeni kazi ya Serikali iliyobainisha ni Kulinda na kutetea sharia zilizotungwa na Bunge. Na unatakiwa ukumbuke kuwa Mahakama na Bunge wana kaanun zao zinavyoviongoza na ukienda kinyume navyo basi lazima utaingia matatani.

      nafikiri nimekujibu suala lako.

      Bado hujajibu swali langu. kwanza kabisa kushtaki inategemea na aina ya kosa ambalo mtu ametenda, kama ni madai (civil) au jinai (criminal) >hivyo basi si kweli kwamba "..mwenye haki ya kushtaki ni JMTZ kupita vyombo vyake..."kama unavotaka kudanganya zaidi. Itategemea aina ya kosa na isitoshe katiba hiyo inaruhusu watu binafsi kushtaki pale waonapo hakia zao za kimsingi na kikatiba zinavunjwa...Barubaru usiwe na jazba unapotaka kuandika kitu chochote, inakupofua na unashindwa kuona vitu vilivyo wazi kabisa.

      Just out of curiosity kwa nini unapenda sana kutumia neno "sharia" pale unapomaanisha "sheria"? Pia mbona unasema sheria "zenu" badala ya "zetu"?

    5. #24
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,826
      Rep Power : 1940
      Likes Received
      1231
      Likes Given
      1193

      Default Re: Waandishi wa Habari Tanzania wamekosa Uzalendo

      Quote By Ibambasi View Post
      Bado hujajibu swali langu. kwanza kabisa kushtaki inategemea na aina ya kosa ambalo mtu ametenda, kama ni madai (civil) au jinai (criminal) >hivyo basi si kweli kwamba "..mwenye haki ya kushtaki ni JMTZ kupita vyombo vyake..."kama unavotaka kudanganya zaidi. Itategemea aina ya kosa na isitoshe katiba hiyo inaruhusu watu binafsi kushtaki pale waonapo hakia zao za kimsingi na kikatiba zinavunjwa...Barubaru usiwe na jazba unapotaka kuandika kitu chochote, inakupofua na unashindwa kuona vitu vilivyo wazi kabisa.

      Just out of curiosity kwa nini unapenda sana kutumia neno "sharia" pale unapomaanisha "sheria"? Pia mbona unasema sheria "zenu" badala ya "zetu"?
      Ahali yangu kumbe ujanielewa nimekusudia nini ninapotamya Serikali ya JMTz. sasa hebu pitia katiba yenu Sharia namba 15 Ibara 6 ya mwaka 1984. Kifungu chote cha 8. utaelewa nini Serikali na watu.

      Lakin pia nilishabainisha toka awali Mimi kuita Sharia ni sawa kabisa na wewe kuita Sheria. Kuna mengi tunatofautiana katika kuita kama mimi naita Skuli na wewe unaita Shule. au markiti wewe unaita soko. N.k hizo ni lahja tu zisikutishe kwani msingi mkuu ni kuelewana.

      Vile vile siwezi sema Sharia zetu kwa sababu mimi SIO kabisa Raia wa Tz zaidi ya kuwa na nasaba na Tanzania.

      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    6. #25
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,451
      Rep Power : 717
      Likes Received
      681
      Likes Given
      410

      Default waandishi wa habari wa Tanzania ni sehemu ya matatizo ya nchii hii

      Waandishi wa habari wa Tanzania kwa kiasi kikubwa wanachangia na wanalea uozo wa mambo mbalimbali hasa kauli za wanasiasa.

      Hivi waandishi wa habari huwa wanapata muda wa kutosha kuwahoji viongozi?Huwa wanakuwa na ujasiri wa kuhoji mambo mazito ambayo wao wanakuwa na taarifa nayo?Kwanini wanapopewa majibu ya kisiasa au ya kiubabaishaji huwa hawasemi kilicho moyoni mwao?Ni busara kusubiri mkutano uishe alafu waje na maswali wakati muhusika walishindwa kumhoji kwenye press conference?

      Leo hii katibu wa itikadi na uenezi wa ccm Nape Nauye amekuja na tuhuma nzito dhidi ya chadema.Hii si mara ya kwanza kwa ccm kutoa shutuma kama hizi.Sasa nilitarajia waandishi wa habari wamuulize kwanza athibitishe tuhuma za mwanzo za chadema.Mfano wa tuhuma hizi ni zile za kudai chadema imeleta magaida wakati wa uchaguzi wa Igunga na madai ya sophia simba kuwa chadema wanapewa fedha na mataifa ya ulaya ili waendeshe maandamano mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2010.Hawa waandishi wetu kwanini wasiohoji tuhuma hizi kabla ya kulishwa tuhuma mpya na wao kuziripoti tuu.?Wanasaidia vipi umma kujua nani mkweli na nani mzushi?

      Kuna tuhuma za mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu mpaka leo umma haujui nani mkweli na nani mzushi.Si waandishi wa habari wenye jukumu la kuwahoji wahusika ili ukweli ujulikane?kwanini waandishi wa habari wa Tanzania huwa hawazingatii matukio ya nyuma kabla ya kuyapa nafasi matukio mapya yanayofanana na yale ya awali ambayo wahusika hawajayatolea majibu?

      Waandishi mnapaswa kubadilika na sio kuwa watu wa matukio ya leo na kuacha kufuatili matukio ya jana.


    7. #26
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,826
      Rep Power : 1940
      Likes Received
      1231
      Likes Given
      1193

      Default Re: Waandishi wa Habari Tanzania wamekosa Uzalendo

      Mimi ushauri wangu kwa hili ni kutumia mfumo wenu wa Sharia yaani kufikisha suala hili mahakamani na muhusika kuitwa na kuthibitisha tuhuma hizo. Kwani kwa kulalama hamta fika popote.

      Tumieni fursa hii kwa kuitumia Katiba yenu vizuri.
      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    8. #27
      bagamoyo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2010
      Posts : 1,342
      Rep Power : 1108
      Likes Received
      310
      Likes Given
      374

      Default Re: Waandishi wa Habari Tanzania wamekosa Uzalendo

      Mwanahabari wa siku nyingi Dr. Mwamoyo Hamza anazungumzia wajibu wa waandishi wa habari Tanzania (ikiwemo pia sisi freelance reporters wa JamiiForums) kutokuripoti tu tukio bali pia kwenda mbele zaidi kwa kuripoti maana ya tukio lenye:




      video kwa hisani ya Luke Joe wa Vimeo.com

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...