Mnyika Kwishney, awasilisha ushahidi mwepesi na kwa sasa asubiri huruma ya spika tu
Jana trh 10.07. 2012 kwenye mida ya saa 11.10 jioni, Mh. Mnyika aliwasilisha ushahidi wa utetezi wake wa kuthibitisha uhusikaji wa Mh. Mwigulu Mchemba na kashfa ya EPA. Kwenye dodosa zangu na wahusika wa ofisi ya katibu wa Bunge, walinihabarisha kuwa mambo yaliyoandikwa na Mnyika ni too general, ambayo ni yale yale yanayosemwa magazetini, mitandaoni, na ushahidi wake mkubwa ni ripoti ya BOT kuhusiana na sakata la EPA.
Kwa minajili hiyo basi, ushahidi wa Mnyika wa kumuhusisha Mh. Mwigulu moja kwa moja na ushiriki wake kwenye EPA waonyesha haupo, na hili ndilo lilikuwa agizo la Mh. Mhagama ambalo alilo toa kuwa Mnyika aonyeshe ushiriki wa Mwigulu Mchemba personally na kashfa ya EPA na sio ushahidi wa BOT kwa ujumla wake.
My take: Kwa hali hii ni wazi kabisa Mh. Mnyika amejiabisha yeye mwenyewe, amewaibisha wananchi wa ubungo, amewaibisha vijana, amewaibisha CDM, amewaibisha wabunge vijana nk kwa kutokuwa na hoja zenye mashiko na zisizo kweli na uhakika. Kwa sasa anategemea huruma ya spika tu kwenye jambo hili.
Re: Mnyika Kwishney, awasilisha ushahidi mwepesi na kwa sasa asubiri huruma ya spika tu
By Ritz
Mnyika toka alipojitukana mwenyewe nimemweweka kwenye kundi la waropokaji...Badala angejikita kutatua kero za wana Ubungo hawana maji ya uhakika, barabara nyingi za barabara kuu ni mbovu zinapitika kwa taabu isiyoelezeka, mabomba ya umma karibu yote hayatoi maji ndoo moja ya maji 2,000 wasaidie wana ubungo sio kila kukicha muongozo spika.
Well said, ndio nasema ni aibu kwake, wana ubungo, wabunge vijana, cdm nk
Re: Mnyika Kwishney, awasilisha ushahidi mwepesi na kwa sasa asubiri huruma ya spika tu
Hata Mnyika hasingesema dili nzima ya EPA hiko wazi sana na Nchemba alikuwa anapewa hints tuuu kwamba ishu zako zinajulikana so husijifanye bingwa wa matusi............mfuatilie kuanzia that day hadi leo kama utamsikia Nchemba na vijembe vyake.....governor noma mdau.
Re: Mnyika Kwishney, awasilisha ushahidi mwepesi na kwa sasa asubiri huruma ya spika tu
Nchi hii weacha tu. Richmond ilimhusisha dhahir JK kwa mikataba ya mchomekeo ya IPTL yeye akiwa waziri mwenye dhamana. Kwa kujua hivyo ikabidi kupindapinda ukweli na mambo yakapoa. ALipokuja Kiwira akahusishwa BWM kwa nguvu nyingi sana, kutambua wakazugazuga na hatimaye "Mambo? POAAAAA!" Airport scandle nayo Lyatonga akaihusisha na Mzee Ruksa, walipogundua Augustine king'ang'anizi wakajaribu kumpooza asipozeke akachomoa ccm na uwaziri aliopewa kama demotion kutoka Naibu waziri mkuu wa heshima, nayo serikali ikaangalia kushoto na kulia na kumtwanga Mrema upofu, ikawa "Kula vyuraRUKSA, Nguruwe au konokono RUKSAAAA" Watu wakasahau na siku zikasonga mbele. Sitaki kumsema marehemu hayati ng'walimuunaweza kujazia. Lakini JK hata formula ya mambo yake ni very copmplex kiasi kwamba wazungu tu ndo wanaweza kuelezea (umeshawasikia wamanavyomuelezea) ama sivyo kwa visasi vyake ukieleza hapa jioni tu utakuwa mabwepande au sitakishari. Nani anataka kung'olewa meno na makucha na kuminywa ndendeko kavukavu? Haya sasa nako JF ukieleza sana sio ajabu ukajikuta wanakuban. Nani kakuambia unao uhuru kamili?
"Uwe na Bidii kama vile utaishi milele, uwe mwaminifu kama vile utakufa kesho" (Indira Gandhi)
Re: Mnyika Kwishney, awasilisha ushahidi mwepesi na kwa sasa asubiri huruma ya spika tu
By dumela mbegu
jana trh 10.07. 2012 kwenye mida ya saa 11.10 jioni, mh. Mnyika aliwasilisha ushahidi wa utetezi wake wa kuthibitisha uhusikaji wa mh. Mwigulu mchemba na kashfa ya epa. Kwenye dodosa zangu na wahusika wa ofisi ya katibu wa bunge, walinihabarisha kuwa mambo yaliyoandikwa na mnyika ni too general, ambayo ni yale yale yanayosemwa magazetini, mitandaoni, na ushahidi wake mkubwa ni ripoti ya bot kuhusiana na sakata la epa. Kwa minajili hiyo basi, ushahidi wa mnyika wa kumuhusisha mh. Mwigulu moja kwa moja na ushiriki wake kwenye epa waonyesha haupo, na hili ndilo lilikuwa agizo la mh. Mhagama ambalo alilo toa kuwa mnyika aonyeshe ushiriki wa mwigulu mchemba personally na kashfa ya epa na sio ushahidi wa bot kwa ujumla wake.my take: Kwa hali hii ni wazi kabisa mh. Mnyika amejiabisha yeye mwenyewe, amewaibisha wananchi wa ubungo, amewaibisha vijana, amewaibisha cdm, amewaibisha wabunge vijana nk kwa kutokuwa na hoja zenye mashiko na zisizo kweli na uhakika. Kwa sasa anategemea huruma ya spika tu kwenye jambo hili.
kete muhimu kwetu cdm,sasa wananchi na wananhrakati tutadai ushahidi wa lema juu ya uongo wa mzee wa liwalo naliwe!
NADHANI ULE USEMI WA KALE UNASEMA HIVI "TOA KWANZA BORITI KWENYE JICHO LAKO, NDIPO UTAONA KIBANZI KWENYE JICHO LA MWENZAKO" Ukiwa kama mwana harakati kijana na unayetafuta njia YOU CANT AFFORD TO DO MISTAKES, YO DO NOT HAVE THE LUXURY OF PETTY MISTAKES!! Gud Day
Re: Mnyika Kwishney, awasilisha ushahidi mwepesi na kwa sasa asubiri huruma ya spika tu
Huyu Mkulima Dumela Mbegu anakimbilia kuanzisha thread ili ionekane imechangiwa sana na hawana uwezo wa kuanzisha thread zaidi ya cdm ipate wa kuichangia Lakini pro-CDM wanauwezo ya kuanzisha thread inayohusu CDM na ikawa na comment Nyingi lakini CCM hawana ubavu huo
Re: Mnyika Kwishney, awasilisha ushahidi mwepesi na kwa sasa asubiri huruma ya spika tu
Huyu Mabwepande kajibiwa vizuri na weye, ahsante kwa kuyaona haya. Sijuhi kilaza huyu amwelewi Bi-kiroboto na liwalo na liwe
By Bobuk
CCM ilishajitia KITANZI siku nyingi. Wether ushahidi wa Mnyika ni mwepesi hautakaa usomwe bungeni, because kabla ya ushahidi wa Mnyika kusomwa lazima shahidi nyingine zilizotangulia zisomwe kwanza. Vinginevyo wananachi tutaamini kwamba ushahidi ule ambayo hauthibitishi ndiyo husomwa. Hivyo shahidi zilizotangulia zilithibitisha ndiyo maana hadi leo hazijasomwa. Hivyo Bunge kabla ya kusoma ushahidi wa Mnyika inabidi kwanza isome zifuatazo ;-)
1. Ushahidi wa Lema dhidi ya Pinda Kusema uongo
2. Ushahidi wa Magdallena Sakaya dhidi ma-DC kuhongwa
3. Ushahidi wa Zitto Kabwe dhidi ya Baraza la waziri kurubuniwa(?)
Baada ya hapo ndiyo uje Ushahidi wa Mnyika dhidi ya Nchemba. Ni Spika gani mwenye GUTS ya kusoma hizo shahidi? Labda kama ile SERA ya nambari ONE KULINDANA iwe imekufa.
"Mtoto wa Maskini Hachagui Malezi, Tanganyika siyo Masikini Masikini ni wewe Unayehonga Haki yako Kwa Mafisadi" Bamugileki
Re: Mnyika Kwishney, awasilisha ushahidi mwepesi na kwa sasa asubiri huruma ya spika tu
By Ritz
Mnyika toka alipojitukana mwenyewe nimemweweka kwenye kundi la waropokaji...Badala angejikita kutatua kero za wana Ubungo hawana maji ya uhakika, barabara nyingi za barabara kuu ni mbovu zinapitika kwa taabu isiyoelezeka, mabomba ya umma karibu yote hayatoi maji ndoo moja ya maji 2,000 wasaidie wana ubungo sio kila kukicha muongozo spika.
Vipi yule aliyekuta Nchi ina deni zero 2005 akakopa mpaka 2012 nchi inadaiwa trilioni 23 umemuweka kwenye kundi gani
Re: Mnyika Kwishney, awasilisha ushahidi mwepesi na kwa sasa asubiri huruma ya spika tu
By Ndukidi
Kwa taarifa yako, Mnyika hata kama asingepeleka huo ushahidi. Hajajiaibisha yeye wala hakuna mwana Ubungo hata mmoja atakayeona aibu eti kwa kuwa Mnyika kamshutumu huyo Mchemba. Nina uhakika kabisa kwa chama chake CDM wala hakuna tone la aibu kwa Mnyika kwa ajili ya issue hiyo. Aliyofanya na anayoendelea kufanya bungeni pamoja na kuwa anakwazwa na wabunge mbumbu wengi wa Chama Cha Mbwepande, lakini bado amefanya makubwa zaidi ya wabunge wengine 200 wa Mabwepande.
Mwanasiasa mahiri hufanya vitu kwa uangalifu na si kukurupuka, maoni yako ni kutokana na mapenzi, kipofu huita chongo. Kama thread hii ni kweli Mnyika ajipange asijepotelea chaka la wanasiasa wepesiwepesi, ajifunze kwa Zito na Halima
Re: Mnyika Kwishney, awasilisha ushahidi mwepesi na kwa sasa asubiri huruma ya spika tu
By dumela mbegu
jana trh 10.07. 2012 kwenye mida ya saa 11.10 jioni, mh. Mnyika aliwasilisha ushahidi wa utetezi wake wa kuthibitisha uhusikaji wa mh. Mwigulu mchemba na kashfa ya epa. Kwenye dodosa zangu na wahusika wa ofisi ya katibu wa bunge, walinihabarisha kuwa mambo yaliyoandikwa na mnyika ni too general, ambayo ni yale yale yanayosemwa magazetini, mitandaoni, na ushahidi wake mkubwa ni ripoti ya bot kuhusiana na sakata la epa.
Kwa minajili hiyo basi, ushahidi wa mnyika wa kumuhusisha mh. Mwigulu moja kwa moja na ushiriki wake kwenye epa waonyesha haupo, na hili ndilo lilikuwa agizo la mh. Mhagama ambalo alilo toa kuwa mnyika aonyeshe ushiriki wa mwigulu mchemba personally na kashfa ya epa na sio ushahidi wa bot kwa ujumla wake.
my take: Kwa hali hii ni wazi kabisa mh. Mnyika amejiabisha yeye mwenyewe, amewaibisha wananchi wa ubungo, amewaibisha vijana, amewaibisha cdm, amewaibisha wabunge vijana nk kwa kutokuwa na hoja zenye mashiko na zisizo kweli na uhakika. Kwa sasa anategemea huruma ya spika tu kwenye jambo hili.
funguka mama nchemba funguka tukusikie. Funguka mama. Tuambie na adhabu aliyopangiwa.
Follow Us Here