Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

    Report Post
    Page 10 of 10 FirstFirst ... 8910
    Results 181 to 191 of 191
    1. #1
      hippocratessocrates's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2012
      Posts : 1,508
      Rep Power : 2129
      Likes Received
      582
      Likes Given
      166

      Default Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

      Ningependa kutoa pole kwa yale yaliyotokea na yanayoendeleakutokea katika nchini na nje ya nchi kuhusu sisi(madaktari).Pole kwa kumuuguzamwenzetu Ulimboka Steven(Dkt), Kushtakiwa kwa MAT, Kuhojiwa kwa Rais wetu NamalaMkopi(Dkt), Kufukuzwa kwa madaktari walio mafunzoni (Intern doctors), vitisho kwa wakuu wa idara n.k.

      Mwaka huu Vyuo vikuu na shirikishi vya afya na tibavinategemea kutoa wahitimu kama ifuatavyo:

      -MUHAS (150), KCMC(80), WBUCHS(50), HKMU(55), IMTU(45) naUDOM(0).
      Kati ya hawa wapo wageni(foreigners) watakaorudi ktk nchizao, wapo ambao watakwenda kufanya internship katika hospitali za binafsi, nawapo wataenda kufanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali(NGO)-kwaniinternship si lazima kufanya, ila hadi pale utakapoamua kufanya kazi katikahospitali. Kinachonishangaza serikali inasema inategemea madaktari 700 kutokavyuoni, inawatoa wapi?

      MAONI:
      Inawezekana katika kila jambo la nchi hii siasa(propaganda)imeingizwa, lakini si katika fani ya udaktari, hii ni fani(Profession) nainapaswa kuheshimiwa kama ilivyo. Si ajabu kiongozi kufika pale Hospitali yaTaifa na kukosa kipimo na kuambiwa kwenda Aga Khan au Regency, utamsikiaakisema “kwani havipo hapa” ukimweleza kuwa ni vibovu utasikia “wanapaswakuwakumbuka”..h ii ni moja ya kauli ya kiongozi mmoja mkubwa serikalini!

      -Si ajabu kumkutaSpecialist akifatilia damu kule Bloodbank,
      -Si ajabu kumkuta Specialist analalamika hawezikuendelea na upasuaji kwani gloves zimembana sana(Sio saizi yake) nakushindwa kutumia vifaa vizuri,

      Si ajabu kumkuta Specialist akisubiri hadi nguo za upasuajieti nguo hakuna!
      Si ajabu kumkuta Specialist amejifunga shirt kichwani kamakofia, Si ajabu kumkuta specialist amevaa gauze kama mask!!
      Si ajabu kumkuta Daktari amejihatarisha(being exposed) na damulakini hakuna Post Exposure Prophylaxis(PEP)

      Hii ni katika hopitali ya Taifa, sasa jiulize kama hospitaliya Taifa hali ni hii, katika hospitali nyingine hali ikoje??

      Kwa specialist, resident, registrar, interns wenye tabia ya kulalamika na kudaimabadiliko, ni mabadiliko yapi mnayoyadai ili hali muda wa mabadiliko hamsimamiimara katika kudai haki yenu??

      Sitegemei madaktari wote kudai haki yao (kwani najua wasalitiwapo tu) lakini zaidi ya yote ni hawa wanaokuwa vuguvugu na wanafiki!!


      KAMA WAZAZI/WALEZI
      :

      Mnawafundisha nini hawa wadogo wenu na watoto wenu, kuhusu kudai haki yako ya kikazI, “I know it is wisdom that takes courage to sit down and listen but it is the same wisdom which takes courage to stand for your right”.

      KAMA VIONGOZI/WALIMU:
      Unapokuwa ukipita round na wanafunzi wako(medical students,interns, registrar, residents), unajisikia nini pale wagonjwa wanapokufiakatika round, kwa sababu tu ya kukosa huduma ambayo ungeweza kutoa kwa mgonjwana kuwa chahu kwa wanafunzi wako? Wanafunzi wanakuonaje wakati ukisema, “in other countries they could have done soand so” wakati muda wa kudai hivyo vifaa na dawa hizo ndio huu? Wanafunziwako wankuonaje wewe kama specialistwakati wenzako wako katika mgomo wewe unapita round, tena wanafunzi wako wakiwana vitambulisho tu bila makoti, wewe ukiwa na koti?

      KAMA WASTAAFU NAMADAKTARI BINGWA WATARAJIWA:
      Wakati wadogo/watoto wetu(intern doctors) waakiwa wameachiwamzigo huu, najiuliza kwa mfano tunapokuwa katika MWR, Discussion Panel huwatunapima uwiano wa wagonjwa na treatment options:
      Leo hii tukipima Option ya MASS RESIGNATION inashindikana?

      -Neurosurgeons(4),
      -Orthopeadicsurgeons(15),
      -Pediatricians(30),
      -ObGynaecologists(45),
      -Physicians(60)regardless of subspeciality ie Neurolgist, Gastroenterologist,etc.
      -Psychiatrist(30)-notpsychologist,
      -Surgeons (40)-regardlessof subspecialty like Cardiothoracic, Plastic surgeons etc,
      -Otorhinolaryngologist(20),
      - Anaesthiologist 25(notanaeshetist),
      -Opthamologist 30(notoptician,optometrist)…HII NI IDADI KWATANZANIA NZIMA.

      Hofu kwetu kama specialists na hawa residents ni kwamba mafao, lakini tujiulize leo kama Profesa anapewa mafao ya 50,000/=Tshs kwamwezi hii ndiyo inayokufanya usigome au kuamua kuresign? Kweli?

      -Cha kushangaza kuna megabrains nyingi sana za kutegemewa lakini wanaact kama hawajui hili, naamini specialists, Residents, registrar nainterns pamoja na medical students tulikuwa na APGAR SCORE ya 10 – 10!! Sasa inakuwaje microbrains ifanye hivi kwa megabrains.

      If I weigh the option of mass resignation I believe it fits the puzzle, because I believe it won't take even a month for the government to call us back to the discussion table (UNDER OUR TERMS THIS TIME) , and in the mean time(I dare to believe that none of us can perish because of financial crisis).

      On the other side the Government cant import other doctors,look at WHO doctor-patient ratio, every country needs one, and for those whothink they will import, ask yourself these questions from which country? Will theybe able to pay them(THIS should be above their home salary), accommodation,transport?

      This is a profession(medical terminologies) and not just mere English, I bet they might needtranslators, how many? Will they pay them? Will those doctors work in thisenvironment or they have to come with medical equipments, medicine? For howlong will they have to stay here? Will they gain trust to people(rapport etc)?

      Hebu tusimame pamoja katika hili, mengi yanafanyika bila mpango hukumu kusomwa mahakamani wakati huo huo, interns kufukuzwa ..sasa unajiuliza kesi ya nini kama tayari wameshafukuzwa, na Rais kuingilia madaraka ya mahakama (kutoa hukumu wakati jambo hilo hilo kukataliwa bungeni), lakini kuumizwa sana kwa Dkt,UlimbokaSteven.

      PLEAD/CALL: LET US STAND TOGETHER NOW MORE THAN EVER, THIS TIME NOT IN TOTAL TOOLS DOWN BUT IN MASSRESIGNATION.
      Last edited by hippocratessocrates; 11th July 2012 at 11:44.


    2. #181
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default Re: Lawama ya madaktari kwa wananchi

      Quote By BULOLE BUKOMBE View Post
      Mkuu mawazo ni mazuri sana lakini hilo haliwezekanio tz hakuna ushirikiano wa wafanyakazi na ndani ya wafanyakazi hao kuna system at work kwa hiyo mobilization ni ngumu sana bora hivyo walivyofanya ujumbe umefika japo kwa ghrama ya watz wenzao ilikuwa hakuna namna nyingine ya kufikisha ujumbe ispokuwa mgomo
      Sio kweli kabisa kwa sababu nakumbuka vizuri Jumuiya ya Wafanyakazi nchini TUCTA waliomba kuhusishwa, Chadema waliomba kuhusishswa wakiwakilishwa na mjumbe wetu Mnyika wote wakapigwa chini tena wakisisitiza kwamba hili sio swala la kisiasa wala hawataki kusaidiwa. Ni lao wao na watakwenda nalo sambamba.

      Kama unakumbuka toka siku ile mimi sikukubaliana na PR yao, na baadaye taasisi ya haki za Binadamu ambao walikuwa wakijihusisha kulingana na kazi zao wakaandaa maandamano lakini hakuna jumuiya yoyote iliungana nao isipokuwa baadhi watu wachache sana.. Ni muhimu sana ukumbuke tu ya kwamba UNION zinaundwa kutambua na kulinda haki za wafanyakazi hasa ktk mfumo huu wa Kibepari na kama jumuiya hizi hazipati nguvu ya wananchi wenyewe kwa kupitia jumuiya hizi hakuna litakalo fanyika...

      Kifupi tazama matatizo tulokuwa nayo tumeshindwa tu ku coordinate maanake Madaktari hawaridhiki na mishahara, walimu, Polisi, watumishi wote wa serikali ngazi za chini wote hawa wanalia na joto la jiwe kwa maisha magumu. Na wote hawa ni waajiriwa wa serikali iweje useme haiwezekani wakati wote wanapanga kufanya migomo wakisikilizia mgomo wa kwanza utatoa matunda gani?

      Serikali hii sii wajinga, wanajua fika wakiwakubalia Tucta, wengine watafuata ndio maana JK akaweka ngumu lakini akipanga kuongeza mishahara chini chini, halafu Madaktari nao waliposikia posho za Wabunge wakaja juu..maana haingii akilini mbunge kuvuta karibu mil 7 kwa mwenzi wakati Daktari hafiki mil1.5 kwa mwaka. The only way out ni wananchi wenyewe kuwa kitu kimoja na muhimu zaidi ni kuonyesha kwamba mnathamini UTU (Humanity) hapo lazima mtazoa walalahoi.

      Jambo moja baya sana lililotokea nchini ni kuzaliwa kwa Taifa jipya lililotengana - A Devided society - Mfumol uliopo tunatengeneza kundi la MATAJIRI na jingine la MASKINI kwa kugawana umaskini ambao mwenye nguvu ndiye anayekula nyama ktk sinia hili la biriani..

      Madaktari wameshindwa kuelewa hivyo kwamba tupo kt process, transition of making millionaires in a poor country tofauti kabisa na nchi tajiri ambazo kuna utajiri na The rich getting richer through their investment and the poor getting poorer for not having Capital.
      Sasa in the making ya Matajiri ndani ya umaskini hapa ni uwanja wa fisi..hakuna mtu anayejali profession ya mtu wala elimu bali nguvu ya kunyakua na obvious Politician are winners maan wako jikoni wao! Huwezi kushindana nao kwa madai kama ilivyo nchi za magharibi ambao wanajali profession ili kuboresha na kuimarisha investment zao ktk dunia hii ya ushindani.

      Sisi bado tupo ktk Ujamaa wa kisiasa wakati wananchi wanaibiwa na hivyo Madaktari walitakiwa kutumia elimu zao kutambua kwamba njia pekee wanayoweza kushinda mgogoro huu ni kutumia vigezo vya HUDUMA..Kuonyesha hali za Wagonjwa na Mazingira mabaya ktk kutoa huduma za Afya na hapo kupata support kubwa ya wananchi walalahoi wakati mawaziri, makatibu wakuu na Wabunge wanatumia mabillioni ya fedha kwa posho na mafuta ya magari.

      Na hakuna madai yoyote yanayoweza kuwekwa dhidi ya serikali yasiwe Political.. Hakuna. Unapoilaumu serikali ktk uongozi wake hata iwe mishahara ni lazima iwe political maana serikali ndio siasa yenyewe haiendeshwi bila sera. Let them say Chadema na CUF wamehusika kuweka madai ya huduma bora lakini mnapiga pale panapoumiza zaidi. Kam serikali itashindwa kukata matumizi yake yasiyokuwa ya lazima, kujipangia mishahara mikubwa na anasa za posho za vikao visivyokuwa lazima, safari zisizokuwa lazima, chai na kadhalika tunaweza kabisa kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi..

      Bila shaka wananchi watajiunga nanyi, walimu, Polisi na watumishi wote nchini watagundua kumbe tunaliwa kiasi hiki! Hapo ndipo mwanzo wa mabadiliko ya jumla na sii mabadiliko ya kundi moja moja la watu kwa sababu uwanja wa fisi hauchaguwi profession ya mtu.

      Na ndio maana kuna walalahoi ambao wanaona mshahara wa daktari wa Laki 9 na posho juu za Ths 20,000 kwa kikao ni mkubwa sana maana wao wanakula wali mkavu. Na mkisema Viongozi mbona hivi maa vile wanashindwa kuwaelewa kwa sababu wao wanajua viongozi ndio wako jikoni.. utauliza kweli shibe ya mpishi? au ugonvi wetu ni sisi tulokuwa janvini tukigombania nyama walizotuletea. Waheshimiwa ni wa kuheshimiwa na jukumu lao kubwa kuliko daktari kwa sababu ndio wanaogawa chakula, kwani hujasikia CCM wakitangaza kwamba wao ndio wanapeleka maendeleo kwa wananchi sio Chadema wala CUF?.

      Narudia kusisitiza siku zote tazama WATU na MAZINGIRA kisha jenga PR yenye kulingana na sura kamili inayojitokeza mbele yako..Na kikubwa zaidi never underestimate power of the people!
      Exploration of reality

    3. #182
      BULOLE BUKOMBE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th April 2011
      Posts : 365
      Rep Power : 488
      Likes Received
      63
      Likes Given
      293

      Default Re: Lawama ya madaktari kwa wananchi

      Quote By Mkandara View Post
      Sio kweli kabisa kwa sababu nakumbuka vizuri Jumuiya ya Wafanyakazi nchini TUCTA waliomba kuhusishwa, Chadema waliomba kuhusishswa wakiwakilishwa na mjumbe wetu Mnyika wote wakapigwa chini tena wakisisitiza kwamba hili sio swala la kisiasa wala hawataki kusaidiwa. Ni lao wao na watakwenda nalo sambamba......
      Kaka umeniandikia ukurasa mzima nashukuru kwa kutumia muda wako juu ya jambo hili lakini swali langu ni moja tu kwamba kama utafahamu nini kinafanya ushirikiano usiwepo katika makundi haya yanayo lalamikia mishahara midogo lakini hayaungani kudai wanachotaka, ndiyo utajua system ni nini!!

      Tofauti ya hapo sina lugha ya kukuelewesha kwa njia hii tunayotumia mfano mzuri Walimu walisema July wanagoma kimetokea nini? Kama hujui siri ya urembo sitaki niwe mwalimu wako.

      Mgomo uliofanikiwa katika historia ya nchi hii ni wa madaktari na wafanyakazi wa benki NMB basi hakuna cha tucta wa cwt wote wako undercontrol by system. Chukua muda mwingi kufanya utafiti utapata jb.

    4. #183
      hippocratessocrates's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2012
      Posts : 1,508
      Rep Power : 2129
      Likes Received
      582
      Likes Given
      166

      Default Re: Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

      mkuu Bulole Bukombe..it seems kugoma kwa pamoja kama agency(TUCTA) ni ngumu kwani viongozi wakirubuniwa au kutishwa hupoteza mwelekeo na hivyo bora kugoma selfwise kama vile waalimu, polisi, madaktari nk lakini kwa pamoja baada ya kuanza hawa wafuate hawa, simaanishi nchi isikalike na kutawalika bali viongozi watatambua kilio cha wananchi!

    5. #184
      Mwananchi Mtanzania's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd July 2012
      Location : Tanzania
      Posts : 92
      Rep Power : 369
      Likes Received
      13
      Likes Given
      2

      Default Re: Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

      Wazo zuri, anza ntakuunga mkono!
      "If real development is to take place, the people have to be involved."
      (J.K. Nyerere)

    6. #185
      Mwananchi Mtanzania's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd July 2012
      Location : Tanzania
      Posts : 92
      Rep Power : 369
      Likes Received
      13
      Likes Given
      2

      Default Re: Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

      Quote By hippocratessocrates View Post
      Ningependa kutoa pole kwa yale yaliyotokea na yanayoendeleakutokea katika nchini na nje ya nchi kuhusu sisi(madaktari).Pole kwa kumuuguzamwenzetu Ulimboka Steven(Dkt), Kushtakiwa kwa MAT, Kuhojiwa kwa Rais wetu NamalaMkopi(Dkt), Kufukuzwa kwa madaktari walio mafunzoni (Intern doctors), vitisho kwa wakuu wa idara n.k.

      Mwaka huu Vyuo vikuu na shirikishi vya afya na tibavinategemea kutoa wahitimu kama ifuatavyo:

      -MUHAS (150), KCMC(80), WBUCHS(50), HKMU(55), IMTU(45) naUDOM(0).
      Kati ya hawa wapo wageni(foreigners) watakaorudi ktk nchizao, wapo ambao watakwenda kufanya internship katika hospitali za binafsi, nawapo wataenda kufanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali(NGO)-kwaniinternship si lazima kufanya, ila hadi pale utakapoamua kufanya kazi katikahospitali. Kinachonishangaza serikali inasema inategemea madaktari 700 kutokavyuoni, inawatoa wapi?......
      Wazo zuri, tafadhali anza na tukuunge mkono!
      "If real development is to take place, the people have to be involved."
      (J.K. Nyerere)


    7. #186
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default Re: Lawama ya madaktari kwa wananchi

      Quote By BULOLE BUKOMBE View Post
      Kaka umeniandikia ukurasa mzima nashukuru kwa kutumia muda wako juu ya jambo hili lakini swali langu ni moja tu kwamba kama utafahamu nini kinafanya ushirikiano usiwepo katika makundi haya yanayo lalamikia mishahara midogo lakini hayaungani kudai wanachotaka, ndiyo utajua system ni nini!! Tofauti ya hapo sina lugha ya kukuelewesha kwa njia hii tunayotumia mfano mzuri Walimu walisema July wanagoma kimetokea nini? Kama hujui siri ya urembo sitaki niwe mwalimu wako. Mgomo uliofanikiwa katika historia ya nchi hii ni wa madaktari na wafanyakazi wa benki NMB basi hakuna cha tucta wa cwt wote wako undercontrol by system. Chukua muda mwingi kufanya utafiti utapata jb.
      Tatizo wewe una underestamate nguvu ya Umma. Na pengine unashindwa kuelewa kwamba palipo na nia siku zote ipo njia...Nitakueleza tena napokataa mimi..

      Wakati Tucta wanajiandaa na malalamiko ya Wafanyakazi wa serikali, MAT, sijui chama cha walimu na wengine wote walisikilizia Upepo wakati hawa wote ni watumishi wa serikali. Kama kweli kuna sababu ya watu kufikia kugoma kufanya kazi kwa sababu sawa nini wanafanya kwa ubinafsi!...

      Tatizo lipo kwa waajiriwa wote wa serikali ngazi zote sasa kama system ndio una control vyombo hivi mnavitumia vya nini? Jiungeni wenyewe mfanya maandamano na poengine mgomo kwa pamoja ndivyo wenzenu hufanya..Na huu mgomo wa Madaktari huwezi kusema umeleta mafanikio yoyote kwa sababu hakuna kilichoongezeka kwa wananchi pengine wao wameongezewa mishahara japokuwa sii kwa kiwango walichotaka.

      Kifupi maandalizi ya migomo yote hii ni mibovu na kama unasema System ina control vyombo hivi then kuna haja gani ya kufanya migomo wakati wawakilishi ndio hawa wanaokwenda kuongea na viongozi?. Sisi Ubinafsi wetu ndio sababu hakuna jingine kila mmoja amebeba msalaba wake. Na hili ndio CCM imefanikiwa sana kutika kuwategeni. Mkianza tu maandamano mnadaiwa kushirikiana na chama cha Upinzani, kwa hofu mnajitoa haraka kwamba hatushirikiani na mtu wala chama chochote.. Hivyo mnajiengua wenyewe na kubakia wepesi...Ndio hayo tu..
      Last edited by Mkandara; 18th July 2012 at 01:12.
      Exploration of reality

    8. #187
      hippocratessocrates's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2012
      Posts : 1,508
      Rep Power : 2129
      Likes Received
      582
      Likes Given
      166

      Default Re: Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

      haya sasa, kule Geita ..mama kujinyonga kutokana na kukosekana na huduma kwa mtoto!

    9. #188
      mswald's Avatar
      Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Location : Kilwa
      Posts : 42
      Rep Power : 449
      Likes Received
      6
      Likes Given
      29

      Default Re: Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

      You dont have to mobilise peopple to table 'Mass resignation'. The message is crystal clear, 'If you feel & think that this little you get as salary isnt enough just table your letter and move foward' We all know that our claims are far beyond gvt budget, a wise thing would be 'HOW TO IMPROVE OUR ECONOMY SO THAT OUR SPENDING POWER IMPROVE'

      Gvt is me, you and others, Let us work hard and put reality on table rather than looking selfish.
      Teachers are now on strike demanding 150-155% increment.Arent they special tooo????????would you be there????????

      TULICHAGUA CHANNEL MBAYA, we should have known this.

    10. #189
      KAFWIMBI's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 57
      Rep Power : 375
      Likes Received
      10
      Likes Given
      4

      Default Re: Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      Hii imewekwa vizuri, kiakili na ukiisoma inasikitisha. Inatoa wito kwa madaktari kuangalia wanachogombania ni nini hasa na kwa manufaa ya nani. Kama madaktari hawawezi kulazimisha serikali kukaa nao chini hakuna mfanyakazi wa kada nyingine yoyote atakayeweza kufanya hivyo.

      I support the doctors!
      Nawaunga mkono madr wa bongo katika madai yenu yote dhidi ya serikali,ni dhahiri serikali yetu sasa inaendeshwa kibabe. Drs jiulizeni baada ya Dr. Uli kuteswa na kuumizwa kiasi kile na Dr. Mkopi kupelekwa mahakamani kwa ajili yenu na kufutwa kwa leseni za madr walioko mafunzoni ndiko kumewafanya kunyamaza kimya?

      Nadhani hii si sahihi kwenu wala kwa mstakabali wa kile mlichokuwa mnakipigania. Nadhani mpango mbadala umekwisha ainishawa hapo juu, wenzenu wa Kenya walithubutu na serikali yao ikashika adabu.

      Jipangeni na kuwa na dhamira moja ya kuwasilisha barua za kuacha kazi kwa notice ya 24 hrs kwa pamoja then kitaeleweka na hapo ndipo tutajua unafiki wa viongozi wa serikali yetu.

    11. #190
      hippocratessocrates's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2012
      Posts : 1,508
      Rep Power : 2129
      Likes Received
      582
      Likes Given
      166

      Default Re: Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

      well, said

    12. #191
      hippocratessocrates's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2012
      Posts : 1,508
      Rep Power : 2129
      Likes Received
      582
      Likes Given
      166

      Default Re: Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

      Tanzania bila migomo ya wafanyakazi haiwezekani!!Wafanya kazi kutumikishwa kama punda bila kujali ugumu wakazi zao, muda wa kazi n.k..viongozi walioko madarakani wanasahau nani aliyewaweka, na wanadhani watakaa madarakani milele na kwamba hawatarudi huku mitaani!!
      kamili likes this.

    Page 10 of 10 FirstFirst ... 8910

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...