Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

    Report Post
    Page 4 of 10 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 189
    1. #1
      Kadu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th January 2011
      Location : Kibaha
      Posts : 20
      Rep Power : 428
      Likes Received
      15
      Likes Given
      14

      Default MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      MGOMO:Madaktari 319 wafutiwa leseni
      Waandishi Wetu
      BARAZA la Madaktari Tanganyika limewafutia usajili madaktari wote waliokuwa katika mafunzo ya vitendo (Internship), baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mgomo wakiwa kazini.Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa Dar es Salaam jana imeeleza kuwa madaktari 319 wamepoteza sifa ya kuendelea na taaluma hiyo hivyo usajili wao umesitishwa rasmi kuanzia jana.Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk Donan Mmbando amewataka madaktari hao kurudisha hati zao za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari.

      “Kwa kuzingatia masharti ya sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhia kwamba madaktari wote ambao walijihusisha na mgomo, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo usajili wao umesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012.”

      “Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya terehe 17 Julai, 2012.”

      Dk Mmbando alisema, awali Baraza hilo lilipokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba baadhi ya madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship), waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kati ya Juni 23 na Juni 29 mwaka huu.

      Alisema madaktari hao walipangiwa kutoa huduma katika Hospitali za Muhimbili, KCMC, Rufaa Mbeya, Sekou Toure na Bugando za Mwanza, Amana, Temeke na Mwananyamala za Dar es Salaam, Haydom - Arusha, St Francis-Ifakara na Dodoma.

      Alisema kutokana na mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo huo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Dk Mmbando alisema kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa kwenye Baraza hilo, Msajili wa Baraza, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la kufanya Uchunguzi dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

      Alisema baada ya kuyafanyia kazi malalamiko hayo, Baraza limebaini kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda.

      Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania (MAT), Dk Edwin Chitage alisema alikuwa hajapata rasmi taarifa hizo licha ya kusikia fununu... “Sijapata taarifa rasmi lakini ni jambo tulilolitarajia na hatutashangaa tukisikia hilo kwa sasa subiri nithibitishe halafu nitatoa msimamo wetu.”
      Kiongozi wa madaktari kortini

      Katika hatua nyingine, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kudharau amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi ya kuwataka kusitisha mgomo kupitia vyombo vya habari.

      Amri hiyo ilitolewa Juni 22, mwaka huu na Jaji Sekela Moshi na kuwataka madaktari kurejea kazini mara moja, lakini amri hiyo haikutekelezwa.

      Jana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka alimsomea Dk Mkopi hati ya mashtaka na kumweleza Hakimu Faisal Kahamba kuwa kati ya Juni 26 na 28, mwaka huu, Dk Mkopi akiwa Rais wa MAT, alidharau amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi Juni 26, mwaka huu ikimtaka kutoa tangazo kwa wanachama wa chama hicho kupitia vyombo vya habari kwamba wasishiriki katika mgomo.

      Kweka alidai kuwa Juni 27, mwaka huu Dk Mkopi aliwashawishi wanachama kushiriki kufanya mgomo kitu ambacho ni kinyume na amri iliyotolewa Juni 26, mwaka huu.

      Hata hivyo, Dk Mkopi alikana mashtaka hayo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kiongozi huyo wa madaktari yupo nje kwa dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 8, mwaka huu itakapotajwa na kuangaliwa kama upelelezi utakuwa umekamilika au la.

      Afya ya Dk Ulimboka
      Wakati huo huo, afya ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka imezidi kuimarika.
      Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitage alisema jana kwamba: “Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, kwa sasa afya yake imezidi kuimarika, anakula mwenyewe lakini pia anazungumza mwenyewe na rafiki zake wa hapa nchini kwa njia ya simu.”

      Katika siku za karibuni, hali ya Dk Ulimboka ilielezwa kubadilika ghafla na kulazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kutokana matatizo mbalimbali, yaliyotokana na kupigwa ikiwamo figo kushindwa kufanya kazi.

      Alisafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi Juni 28, mwaka huu kwa ushauri uliotolewa na jopo la madaktari lililokuwa likimhudumia.

      UN yanena
      Katika hatua nyingine, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Dk Alberic Kacou amepokea barua ya MAT kuomba ulinzi kwa Dk Ulimboka anayeendelea na matibabu Afrika Kusini kwa madai kuna kikosi kilichotumwa kuhakikisha harudi nchini akiwa hai.

      Akizungumza jana Dar es Salaam jana, Dk Kacou alisema suala hilo la kutoa ulinzi watalitoa baada ya kuwasiliana na wote waliohusishwa kwenye waraka wa ombi hilo.

      Mgomo wamalizika
      Mgomo uliokuwa ukiendelea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Mifupa (Moi), Dar es Salaam umemalizika na huduma katika hospitali hizo zimerejea kama kawaida jana.

      Waandishi wa habari waliotembelea hospitali hizo waliona wagonjwa wakiwa wanaendelea kupokewa na kupatiwa huduma kama ilivyokuwa awali, kabla ya mgomo uliodumu kwa takriban majuma mawili yaliyopita
      Habari hii imeandikwa na Tausi Mbowe, Tausi Ally, Leon Bahati na Issa Lazaro, Geofrey Nyang’oro
      Source: gazeti la mwananchi

    2. Miaka 50

    3. #61
      chama's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 6th August 2010
      Posts : 4,974
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1180
      Likes Given
      917

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By iseesa
      Dhaifu yuko kwenye mkutano wa WAZAZI Uingereza!
      Kuna haja ya mh. Raisi kuhudhuria mkutano wa uzazi wa mpango hii itasaidia sana kuepuka kuzaa watu wenye akili chafu kama yako. Tunahitaji vizazi makini kwa maendeleo ya taifa hili.

      Chama
      Gongo la mboto DSM

    4. #62
      MTAZAMO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th February 2011
      Posts : 4,251
      Rep Power : 2207
      Likes Received
      1828
      Likes Given
      2540

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Hiki ndio kipindi madaktari wanapaswa kuwa pamoja kuliko wakati wowote ule!

    5. #63
      MVUMBUZI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th January 2011
      Posts : 2,586
      Rep Power : 1090
      Likes Received
      685
      Likes Given
      374

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Waombe Mungu 2015 ifike watarudi wote na wale waliokimbilia nje miaka ya nyuma kuja kutumikia nchi yao. Hii inaweza kuwa temporary casuality ila yenye manufaa ya muda mrefu kwa hiyo vijana wasife moyo wajue tuko nyuma yao na Mungu ataendelea kuwapigania

    6. #64
      only83's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Dodoma-Mjengoni
      Posts : 4,157
      Rep Power : 1847
      Likes Received
      1431
      Likes Given
      1539

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Si muda wa kuchekea hii serikali ya CCM iliyochoka. Nasubiri tamko la MAT.
      "Problems can not be solved by the same level of thinking that created them"
      "Matatizo hayawezi kutatuliwa na uwezo ule ule mdogo wa watawala wa CCM walioyasababisha"




    7. #65
      Tume ya Katiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Location : Chumbuni-Zanzibar
      Posts : 2,690
      Rep Power : 0
      Likes Received
      542
      Likes Given
      273

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Greats,

      Hongera sana Baraza la madaktari Tanganyika, Huu ni uamuzi mzuri ila umechelewa sana.

      Pongezi zenu madaktari kitengo cha MOI kwa kusitisha mgomo.

      Uamuzi mzuri na wa kungwa mkono sana.


    8. #66
      Meking's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th May 2011
      Posts : 166
      Rep Power : 438
      Likes Received
      13
      Likes Given
      1

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Excellent
      hawawezi wakafanya suluhu kwa mtindo huu
      Mtindo gani unaofaa ambao serikali haijautumia?
      "LIFE ISN'T GOOD BY DEFAULT, MAKE IT!!" The King...

    9. #67
      jogi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2010
      Posts : 4,032
      Rep Power : 1223
      Likes Received
      982
      Likes Given
      247

      Default

      Quote By chama
      Kuna haja ya mh. Raisi kuhudhuria mkutano wa uzazi wa mpango hii itasaidia sana kuepuka kuzaa watu wenye akili chafu kama yako. Tunahitaji vizazi makini kwa maendeleo ya taifa hili.

      Chama
      Gongo la mboto DSM
      jk, naamini hana tunachoweza kumuheshimia, kwani heshima yetu ni kwa gharama ya dharau yake, halafuuu, kwani salima a.k.a mama mwanaasha si ana ana ana ana anaaa ujaumimba kwa hisani ya watu wa marekani! Atakuwa anahudhuria na kuonyesha kwa mfano bandugu. Heshima ya taifa ilijengwa kwa miaka mingi, sasa nashuhudia ikiporomoshwa kama senema!!!!!!!!!!!!

      Kweli sikitiko oh sikitiiko ooh, na machozii yanatutoka mama!
      mbona wale wenzetu wanatesekaa mama!
      Wako katika makucha ya watu weupe wachacheee mamah!

      Witoooooooo, witoooo mama mama, wito,
      tanganyika lazima tuikomboe mama! Lazima tuikomboe.
      Kwa mitutu na mikuki na mapanga mama! Lazima tuikomboe! -Dar Internatinal-

    10. #68
      asungwilemwaifunga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th February 2012
      Posts : 347
      Rep Power : 502
      Likes Received
      119
      Likes Given
      35

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Baraza la Madaktari Tanganyika haliko huru kutoa maamuzi huru. Mwenyekiti wake ni Dr. Donan Mbando Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, alikuwemo kwenye timu ya majadiliano kati ya madaktari na serikali yeye akiwa upande wa serikali. Serikali inapeleka mashitaka ya madaktari kwa mtu ambaye ana interest katika shauri hilo. Nobody can be a judge on his own case.

      Ikiwa serikali haiwezi kuliona hata hili dogo sijui umakini wake. Katika macho ya kisheria hukumu hiyo ni batili

    11. #69
      Maundumula's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 5,050
      Rep Power : 3122
      Likes Received
      1377
      Likes Given
      5834

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Mimi nataka hizo leseni wasipewe tena ili iwe fundisho kusiwe na migomo huko mbele.

      Kama wanaona hawajatendewa haki waende mahakamani ooops waende UN si ndio wanapokimbilia siku hizi.

    12. #70
      Meking's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th May 2011
      Posts : 166
      Rep Power : 438
      Likes Received
      13
      Likes Given
      1

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Kama makaratasi yangekuwa siyo dili basi hata babu wa Loliondo angekuwa daktari bingwa pale Muhimbili.
      Halafu hii ni fursa kwa vijana wetu kwenda Trinidad, kiroho safi...
      "LIFE ISN'T GOOD BY DEFAULT, MAKE IT!!" The King...

    13. #71
      Maundumula's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 5,050
      Rep Power : 3122
      Likes Received
      1377
      Likes Given
      5834

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Kuna vijana walifanya wabishi hapo UDSM enzi za Nyerere. Wakaanzisha mgomo wa kijinga kama huu wa madaktari. Alichofanya Nyerere ni kuwafungulia mlango wa Ikulu wakaingia pale na akahakikisha wanazomewa njia nzima hadi wanarudi Mlimani na walipofika makazini wakawa wanatengwa hawapandishwi vyeo. Nendeni mkawaulize wajomba zenu na baba zenu waliofikwa na hii zahma watawahadithia ilivyowagharimu.

    14. #72
      Maundumula's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 5,050
      Rep Power : 3122
      Likes Received
      1377
      Likes Given
      5834

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Meking
      Kama makaratasi yangekuwa siyo dili basi hata babu wa Loliondo angekuwa daktari bingwa pale Muhimbili.
      Halafu hii ni fursa kwa vijana wetu kwenda Trinidad, kiroho safi...
      Hawawezi kupokelewa huko kirahisi rahisi hadi wawe cleared huku kwetu.

    15. #73
      Meking's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th May 2011
      Posts : 166
      Rep Power : 438
      Likes Received
      13
      Likes Given
      1

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By BAK
      Ndio matatizo ya kuwa na Kiongozi DHAIFU na Serikali DHAIFU siku zote haina utaratibu wa kukaa meza moja na wadau mbali mbali ili kutafuta suluhisho la matatizo husika kwa amani wao wanaona ubabe tu wa kutishana na kukomoana ndiyo njia muafaka. Wangekuwa wanatibiwa nchini sidhani kama wangefikia uamuzi wa hovyo kama huu.
      Saa hizi serikali ndo imekuwa "haina utaratibu wa kukaa meza moja na wadau mbalimbali?!!
      Nyie watu kwa kugeuza maneno, hivi ni serikali ndiyo ilikataa kuongea na madaktari pale Karimjee siyo?
      "LIFE ISN'T GOOD BY DEFAULT, MAKE IT!!" The King...

    16. #74
      Elungata's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th January 2011
      Posts : 3,736
      Rep Power : 0
      Likes Received
      418
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Ralphryder
      Ilichofanya serikali ni sawasawa,hawa watoto hawajui kama serikali ipo! wanafanya watakacho kiholela tu, wacha sasa wasage rumba mtaani mpaka visigino viende upande! wanafata mkumbo tu kazi yenyewe hawajapata, haya sasa! hawajui mgoma u,meathiri watu kiasi gani! watalijua jiji.
      si waende kwa Dr slaa akawape hata udiwani wa kuteuliwa jamani.

    17. #75
      Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2006
      Posts : 1,725
      Rep Power : 1022
      Likes Received
      54
      Likes Given
      6

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Kichuguu
      Ubabe wa serikali utawaumiza zaidi wananchi wanaotegemea hospitali za serikali, siyo hawa madaktari waliofutiwa leseni kwani bado wana ubongo wao. Leseni ni karatasi tu, kulifuta hakuondoi knowledge ambayo madaktari hawa wameshajisheenza vichwani mwao. Time will tell!! Miaka kadhaa iliyopita, Mwinyi mdogo aliwafukuza madakatri Tanzania kutokana na mgomo kama huu; baada ya muda kidogo nikakutana na dakatri mmoja aliyefukuzwa Tanzania akiwa anaendelea na taaluma yake huko Trinidadi tena kwa heshima kubwa sana....
      Mwalimu,
      Kila Fani au tasnia ina sheria na muongozo,msilaumu tu serikali kwa hatua waliyoichukua ktk kufuata sheria iliyopo kupitia vyombo husika na sheria kufuata mkondo wake.

      Kwanza naweza kusema wamekuwa wavumilivu sana na wengine mkauita UDHAIFU,ni uamuzi mgumu kwa serikali kuuchukuwa DHIDI ya watu wake ,Lakini was the right thing to do........................,sas a wafuate sheria kuomba tena hizo leseni nafikiri milango haijafungwa kabisa.

      Na hata wakiamua kwenda kufanya kazi nchi nyingine bado wataomba leseni kwa kufuata sheria za nchi husika na hawa itabidi waombe kufanya Intern ,kwani hawakumaliza intern sasa sijui wapi watakuajiri hata hujamaliza Intern!
      UKIJUA UNAPOKWENDA NI RAHISI KUFIKA!

    18. #76
      simplemind's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2009
      Posts : 2,854
      Rep Power : 1157
      Likes Received
      509
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By lunyamu
      It is a government body, working under the ministry of health.. the chairperson of the council is the chief medical officer who is the presidential appointee. Na miongoni ya maorodhesho yaliyotolewa na madaktari na kuchukuliwa na kamati ya bunge ni kuhusu ku'review structure na function ya baraza lenyewe.... Sishangai uamuzi huu, nashauri madaktari wasife moyo wajipange upya kuna uozo mwingi sana unaoendelea
      Poleni madaktari. University grants you the power to read and write and all that apertains my degree then out of blue comes damn political appointee and says thou shall not practice. Where is the justice?
      Last edited by simplemind; 11th July 2012 at 10:05.

    19. #77
      Meking's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th May 2011
      Posts : 166
      Rep Power : 438
      Likes Received
      13
      Likes Given
      1

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Njoka Ereguu
      Mimi nadhani uamuzi wa kuwafutia lesseni ni hasara kwa serikali yenyewe, imetumia muda na gharama kuwasomesha,bado tunaupungufu mkubwa wa madaktari na hilo pengo la madaktari 319 pengo lao ki-uhalisia haliwezi kuzibika kwa muda mfupi. Ndiyo tunasema wapo 700 wanaomaliza mwezi ujao lakini bado uwepo wao ulikuwa hauwaondowi hao 319 kazini bali ilikuwa inapunguza uhaba mkubwa wa madaktari Tanzania.

      Ni vyema uamuzi huu ukaangaliwa kwa njia pana zaidi ili kuepuka maamuzi ya kukomoana, mgomo umeisha wapewe onyo la waruhusiwe kuendelea na kazi. Katika hali ya kawaida ni kwa vile tu hana tabia ya kufanya tathmini ya maamuzi yetu, kufukuza madk 319 kunaathiri pia uchumi wa nchi kwa namna moja au nyingine.
      Tuseme walipokuwa wanaajiriwa hawakujua kama watalipwa "kiduchu". Kwa sababu sasa wanajua, na mwajiri anasisitiza kutoweza kuwalipa kwa matakwa yao, zaidi anawashauri watafute mwajiri mwenye uwezo. Hapo tena mgogoro wa nini. Mbona wanakuwa kama wanataka na hawataki? Tuumize vichwa kupunguza tofauti ya vipato na mfumuko wa bei. Kuzidi kuwaongezea pesa madaktari kutaongeza matatizo yote mawili...
      "LIFE ISN'T GOOD BY DEFAULT, MAKE IT!!" The King...

    20. #78
      Manyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th December 2011
      Posts : 1,747
      Rep Power : 726
      Likes Received
      292
      Likes Given
      267

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Hili suala ni kwa muda tu! Watapewa tu reguistration! Ingawaje sometimes inabidi ufanye maamuzi magumu

    21. #79
      Mr.Mak's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd February 2011
      Posts : 1,150
      Rep Power : 652
      Likes Received
      157
      Likes Given
      84

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Kichuguu
      Ubabe wa serikali utawaumiza zaidi wananchi wanaotegemea hospitali za serikali, siyo hawa madaktari waliofutiwa leseni kwani bado wana ubongo wao. Leseni ni karatasi tu, kulifuta hakuondoi knowledge ambayo madaktari hawa wameshajisheenza vichwani mwao. .
      Kaka umekosea kuelewa kuwa bila wao kupata hiyo leseni watakuwa hawaruhusiwi kuajirika katika hospital yoyote. akifanya kazi atafanya kama kishoka kiasi kwamba serikali ikigundua hata huyo mwajiri wake atakuwa hatarini. sasa kwanini ajihatarishie kazi kwa kumchukua mtu ambaye sifa zake hazijakamilika? Hili kaka ni tatizo labda sisi kama taifa tutumie wazee wenye busara wamfate rais kumueleza kuwa kwa hili, hilo baraza limetumia hasira kubwa zaidi. Tukirudi nyuma ivi hawa madaktari hawakuzijua hizi sheria za chama chao?

    22. #80
      utantambua's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st August 2011
      Posts : 1,272
      Rep Power : 649
      Likes Received
      272
      Likes Given
      752

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      halafu bado tunaongelea utawala bora tanzania wakati hata utatuzi wa migogoro ya kiwango hiki tu ubabe unatumika....kwanini sasa kupoteza pesa na muda kujiunga na vyombo kama african peer review mechanism ilhali tunafahamu kabisa kuwa tunasoma sifuri katika governancemeter?

    Page 4 of 10 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...