Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

    Report Post
    Page 3 of 10 FirstFirst 12345 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 189
    1. #1
      Kadu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th January 2011
      Location : Kibaha
      Posts : 20
      Rep Power : 428
      Likes Received
      15
      Likes Given
      14

      Default MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      MGOMO:Madaktari 319 wafutiwa leseni
      Waandishi Wetu
      BARAZA la Madaktari Tanganyika limewafutia usajili madaktari wote waliokuwa katika mafunzo ya vitendo (Internship), baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mgomo wakiwa kazini.Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa Dar es Salaam jana imeeleza kuwa madaktari 319 wamepoteza sifa ya kuendelea na taaluma hiyo hivyo usajili wao umesitishwa rasmi kuanzia jana.Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk Donan Mmbando amewataka madaktari hao kurudisha hati zao za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari.

      “Kwa kuzingatia masharti ya sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhia kwamba madaktari wote ambao walijihusisha na mgomo, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo usajili wao umesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012.”

      “Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya terehe 17 Julai, 2012.”

      Dk Mmbando alisema, awali Baraza hilo lilipokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba baadhi ya madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship), waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kati ya Juni 23 na Juni 29 mwaka huu.

      Alisema madaktari hao walipangiwa kutoa huduma katika Hospitali za Muhimbili, KCMC, Rufaa Mbeya, Sekou Toure na Bugando za Mwanza, Amana, Temeke na Mwananyamala za Dar es Salaam, Haydom - Arusha, St Francis-Ifakara na Dodoma.

      Alisema kutokana na mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo huo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Dk Mmbando alisema kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa kwenye Baraza hilo, Msajili wa Baraza, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la kufanya Uchunguzi dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

      Alisema baada ya kuyafanyia kazi malalamiko hayo, Baraza limebaini kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda.

      Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania (MAT), Dk Edwin Chitage alisema alikuwa hajapata rasmi taarifa hizo licha ya kusikia fununu... “Sijapata taarifa rasmi lakini ni jambo tulilolitarajia na hatutashangaa tukisikia hilo kwa sasa subiri nithibitishe halafu nitatoa msimamo wetu.”
      Kiongozi wa madaktari kortini

      Katika hatua nyingine, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kudharau amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi ya kuwataka kusitisha mgomo kupitia vyombo vya habari.

      Amri hiyo ilitolewa Juni 22, mwaka huu na Jaji Sekela Moshi na kuwataka madaktari kurejea kazini mara moja, lakini amri hiyo haikutekelezwa.

      Jana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka alimsomea Dk Mkopi hati ya mashtaka na kumweleza Hakimu Faisal Kahamba kuwa kati ya Juni 26 na 28, mwaka huu, Dk Mkopi akiwa Rais wa MAT, alidharau amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi Juni 26, mwaka huu ikimtaka kutoa tangazo kwa wanachama wa chama hicho kupitia vyombo vya habari kwamba wasishiriki katika mgomo.

      Kweka alidai kuwa Juni 27, mwaka huu Dk Mkopi aliwashawishi wanachama kushiriki kufanya mgomo kitu ambacho ni kinyume na amri iliyotolewa Juni 26, mwaka huu.

      Hata hivyo, Dk Mkopi alikana mashtaka hayo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kiongozi huyo wa madaktari yupo nje kwa dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 8, mwaka huu itakapotajwa na kuangaliwa kama upelelezi utakuwa umekamilika au la.

      Afya ya Dk Ulimboka
      Wakati huo huo, afya ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka imezidi kuimarika.
      Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitage alisema jana kwamba: “Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, kwa sasa afya yake imezidi kuimarika, anakula mwenyewe lakini pia anazungumza mwenyewe na rafiki zake wa hapa nchini kwa njia ya simu.”

      Katika siku za karibuni, hali ya Dk Ulimboka ilielezwa kubadilika ghafla na kulazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kutokana matatizo mbalimbali, yaliyotokana na kupigwa ikiwamo figo kushindwa kufanya kazi.

      Alisafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi Juni 28, mwaka huu kwa ushauri uliotolewa na jopo la madaktari lililokuwa likimhudumia.

      UN yanena
      Katika hatua nyingine, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Dk Alberic Kacou amepokea barua ya MAT kuomba ulinzi kwa Dk Ulimboka anayeendelea na matibabu Afrika Kusini kwa madai kuna kikosi kilichotumwa kuhakikisha harudi nchini akiwa hai.

      Akizungumza jana Dar es Salaam jana, Dk Kacou alisema suala hilo la kutoa ulinzi watalitoa baada ya kuwasiliana na wote waliohusishwa kwenye waraka wa ombi hilo.

      Mgomo wamalizika
      Mgomo uliokuwa ukiendelea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Mifupa (Moi), Dar es Salaam umemalizika na huduma katika hospitali hizo zimerejea kama kawaida jana.

      Waandishi wa habari waliotembelea hospitali hizo waliona wagonjwa wakiwa wanaendelea kupokewa na kupatiwa huduma kama ilivyokuwa awali, kabla ya mgomo uliodumu kwa takriban majuma mawili yaliyopita
      Habari hii imeandikwa na Tausi Mbowe, Tausi Ally, Leon Bahati na Issa Lazaro, Geofrey Nyang’oro
      Source: gazeti la mwananchi

    2. Miaka 50

    3. #41
      hippocratessocrates's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2012
      Posts : 1,489
      Rep Power : 2121
      Likes Received
      572
      Likes Given
      163

      Default

      Quote By Ritz
      Kuna Interns 700 mwezi ujao wanaanza kazi.
      mkuu intern 700 uwatolee wapi?!
      waliomaliza;
      muh2 ni 170
      bugando 50
      KCMC 80
      HKMU 59
      IMTU 65
      UDOM HAKUNA
      jumla ni wangapi hao?? ---kuna foreigners wanarudi makwao,!!
      -kuna watu wenye supplementary so hawawezi kumaliza!!
      -kuna wengine wanaanza research ktk NGO( kumbuka internship unafanya muda wowote)
      -kuna ambao watafanya internship katika private hospitals!!
      ngoja serikali iendelee kuwadanganya..

    4. #42
      mangikule's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th June 2012
      Posts : 917
      Rep Power : 533
      Likes Received
      175
      Likes Given
      236

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Ritz
      Haki yao milioni 7,700,000 kwa mwezi mmeishaambiwa muajiri wako hana uwezo wa kutoa mshahara huo kama mnataka masalahi zaidi ruksa kwenda sehemu ingine wanapolipa vizuri.
      Akili nzuri sana!! walikuwa wakidai jumla ya 70bn! suluhisho tutaajiri wageni na tumetenga 700bn!! hata kuku angefikiri tofauti na kufanya busara!!

    5. #43
      Kakulwa P's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th February 2012
      Posts : 201
      Rep Power : 407
      Likes Received
      69
      Likes Given
      10

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Hapo hakuna Baraza la Madaktari, labda kama walioandika ni watu wa Serikalini, maana kama baraza linaongozwa na madaktari ambao wanaona shida kwenye tasnia ya utabibu hawawezi kuandika hiyo barua. Kama aliyeandika ni KONDAKTA wa daladala sawa maana hajui kinachowasibu.

    6. #44
      hippocratessocrates's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2012
      Posts : 1,489
      Rep Power : 2121
      Likes Received
      572
      Likes Given
      163

      Default

      hahaha
      .uajiri kutoka wapi?! nchi gani haina upungufu wa madaktari?
      angalia current statistics za WHO za doctor to patient ratio!!
      - afu hata kama wakija, unadhani utawalipa sawa na mshahara wa kwao(kumbuka TZ ndio inamalipo madogo ktk nchi za sekta ya Afya ktk East and central Africa)? makazi na usafiri wao je? wakalimani? malipo ya wakalimani? afu unadhani watakaa TZ milele?

    7. #45
      Safari_ni_Safari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2007
      Location : Kibaruani
      Posts : 11,931
      Rep Power : 24141
      Likes Received
      4652
      Likes Given
      2637

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Hii ni sawa na mtu anayeamua KUJICHINJA......yaani anakata kichwa chake mwenyewe......just because of a SIMPLE HEADACHE...that an ASPRIN can cure

      Soki Ozali Mwasi Yaka, Soki Ozali Mobali Koya Te


    8. FemaTV & Radio

    9. #46
      ikingura's Avatar
      Member Array
      Join Date : 10th July 2012
      Posts : 13
      Rep Power : 348
      Likes Received
      3
      Likes Given
      1

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Janjaweed
      interns huwa hawana liseni... serikali sasa iache ujinga wa kuhadaa kwani wananchi watajua inawahadaa na chuki itaongezekaleseni yua practice hutolewa baada ya dr kumaliza intern na kufanya kazi miaka miwili na kuendelea na kupata approval THIS IS ANOTHER CHEAP LIE TO PEOPLE
      Ni kweli interns huwa hawana leseni bali wana vyeti vya usajili wa muda tu (Provision reg certificate) hata mi niliemaliza intern mwaka jana cijapata leseni mpaka after one year. Serikali inadanganya

    10. #47
      jogi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2010
      Posts : 3,987
      Rep Power : 1213
      Likes Received
      973
      Likes Given
      247

      Default

      Bob marley aliimba na leo wimbo wake naona unareflect reality
      "running away" album = kaya
      mgomo wa madaktari ni sahihi, do not be mixed up by the consequence of the strike, nikikosa ama kuyapata hayo matibabu duni ninayoyagrade group moja na polonium.

    11. #48
      iseesa's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 940
      Rep Power : 0
      Likes Received
      204
      Likes Given
      53

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Mzee wa Rula
      Sijui akili za mbayuwayu alizosema akichanganya na zake ndiyo mwisho wa panel ya urais ilipofikia katika kusuluhisha hili!!!!!
      Dhaifu yuko kwenye mkutano wa WAZAZI Uingereza!

    12. #49
      lunyamu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 7th July 2012
      Posts : 17
      Rep Power : 349
      Likes Received
      3
      Likes Given
      1

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      It is a government body, working under the ministry of health.. the chairperson of the council is the chief medical officer who is the presidential appointee. Na miongoni ya maorodhesho yaliyotolewa na madaktari na kuchukuliwa na kamati ya bunge ni kuhusu ku'review structure na function ya baraza lenyewe.... Sishangai uamuzi huu, nashauri madaktari wasife moyo wajipange upya kuna uozo mwingi sana unaoendelea

      Quote By simplemind
      Medical council has acted unfairly. Mimi nilidhani hili baraza ni similar to institituion of Engineers ambayo inasajili wahandisi and as such should not be playing politics(revoking en mass usajili wa interns wote is suspect). Which begs the question is medical council a goverment body or a proffesional body?

    13. #50
      masabo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 8th July 2012
      Posts : 59
      Rep Power : 357
      Likes Received
      11
      Likes Given
      5

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      kwa sisi madaktari inabidi tufanye kitu kunusuru hawa wenzetu wliofutiwa leseni za muda.Ni lazima mgomo huanze upya wakitaka watufute wote ili wanajeshi na polisi ndo watibu wagonjwa.Hii inamaanisha kilio chetu hawakioni.Liwalo na liwe

    14. #51
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,252
      Rep Power : 12575
      Likes Received
      5796
      Likes Given
      758

      Default

      Quote By Ndambonyiliva
      So what?
      Voluntary is better than force!

    15. #52
      Careboy wamuntere's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 9th July 2012
      Posts : 160
      Rep Power : 378
      Likes Received
      30
      Likes Given
      95

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Mzee wa Rula
      Sijui akili za mbayuwayu alizosema akichanganya na zake ndiyo mwisho wa panel ya urais ilipofikia katika kusuluhisha hili!!!!!
      Sidhani kama unafuatilia mambo, kumbuka mara ya kwanza waligoma kuongea hadi na waziri mkuu, rais akakutana nao, wakatulia, awamu hii waliambiwa waendelee na mazungumzo huku huduma zikiendelea kutolewa, wakasema wanaendelea na mgomo ambao hauna kikomo,

      Mahakama imechukua nafasi yake ili sheria ichukue mkondo wake kusitisha mgomo na kuamuru maongezi yaendelee, bado madaktari wamekaidi, sasa ndg zangu tuwe wakweli na tusiwe biased, hivi katika hali ambayo sheria na chombo cha kusimamia haki vinakiukwa ni hatua gani zichukuliwe ili watu washerekee ama wafurahi, tukumbuke hii migomo tuliyokuwa yunaishabikia, sasa hivi tena imekuwa lawama, nchi hii tumezidi kelele hata pale ambapo hapastahili hadi tunasahau hata mambo ya msingi na yasiyo ya msingi. Tafakari.

    16. #53
      Safari_ni_Safari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2007
      Location : Kibaruani
      Posts : 11,931
      Rep Power : 24141
      Likes Received
      4652
      Likes Given
      2637

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Ritz
      Voluntary is better than force!
      Kujitolea ni bora kuliko kutumia nguvu! (ungesema hivi kuliko kuharibu lugha ya watu)

      Soki Ozali Mwasi Yaka, Soki Ozali Mobali Koya Te


    17. #54
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,252
      Rep Power : 12575
      Likes Received
      5796
      Likes Given
      758

      Default

      Quote By jogi
      Bob marley aliimba na leo wimbo wake naona unareflect reality
      "running away" album = kaya
      mgomo wa madaktari ni sahihi, do not be mixed up by the consequence of the strike, nikikosa ama kuyapata hayo matibabu duni ninayoyagrade group moja na polonium.
      Kaya man.

    18. #55
      Mkirua's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2010
      Posts : 3,421
      Rep Power : 1035
      Likes Received
      1173
      Likes Given
      599

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By ZeMarcopolo
      Ritz, kuna makosa yamefanyika, lakini kuhusu interns nakuomba tujaribu kuangalia swala tofauti kidogo. Lets do a little bit more kuhusu hawa interns. Tukumbuke kuwa interns wako katika kujifunza, kujifunza sio kutibu tu bali hata jinsi ya kuishi kazini. Sasa hawa wanaowafundisha kazi wamewaambia kuwa hapa mambo ni kugoma, interns hawezi kumbishia senior wake anayemfundisha. Kumbuka wamekabishidwa kwa registrars na specialists ili wawafundishe na wao wamewafundisha kugoma.
      Ndiposa Mbayuwayu akatufundisha kuwa ...changanya na za kwako....LOL!
      The world suffers a lot. Not because of the violence of bad people, but because of the silence of good people!

    19. #56
      Mkirua's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2010
      Posts : 3,421
      Rep Power : 1035
      Likes Received
      1173
      Likes Given
      599

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By jogi
      Bob marley aliimba na leo wimbo wake naona unareflect reality
      "running away" album = kaya
      mgomo wa madaktari ni sahihi, do not be mixed up by the consequence of the strike, nikikosa ama kuyapata hayo matibabu duni ninayoyagrade group moja na polonium.
      Kwahiyo wanafanya kazi kwa kufuata ushauri uliopo kwenye ujumbe wa bob?? I wish kama wewe ni lawyer then ukawadefend mahakamani kwa hoja hiyo unayoitumia kuhalalisha mgomo.....
      The world suffers a lot. Not because of the violence of bad people, but because of the silence of good people!

    20. #57
      Mkirua's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2010
      Posts : 3,421
      Rep Power : 1035
      Likes Received
      1173
      Likes Given
      599

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By masabo
      kwa sisi madaktari inabidi tufanye kitu kunusuru hawa wenzetu wliofutiwa leseni za muda.Ni lazima mgomo huanze upya wakitaka watufute wote ili wanajeshi na polisi ndo watibu wagonjwa.Hii inamaanisha kilio chetu hawakioni.Liwalo na liwe
      Tatizo daktari (if at all u are....) mnacheza na dubwana linaloitwa State tena kwenye nchi isiyo na utamaduni wa viongozi kuwajibika..... You will be on the losing side angalia wasiwape kichwa humu jukwaaani at the end it will remain to be your own issue (personal) though kwa sasa unatumia wingi...kilio chetu.... yakishatimia inakuwa kilio changu...Ivi hata kama Labour law huijui hata mkataba wako hukuuusoma vizuri?? na kiapo uliapa tu bila kujua maana yake?? Maana hivyo mwisho wa siku ndivyo vinavyotumika kukuhukumu...
      The world suffers a lot. Not because of the violence of bad people, but because of the silence of good people!

    21. #58
      chama's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 6th August 2010
      Posts : 4,908
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1165
      Likes Given
      912

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Bodi imefanya maamuzi kwa mujibu wa sheria; ila katika mazingira ya kibinadamu wawasemehe vijana; kwani walishatii amri ya kurudi kazini; wapewe karipio kali na wawe chini ya ungalizi wa serikali kwa kipindi cha miaka 5 ili liwe fundisho kwa wengine; hasa ukizingatia chanzo cha mgomo ulishinikizwa na wanasiasa wenye agenda zao; vijana walipotoshwa wasamehewe warudi kazini kuwatumikia watanzania.

      Chama
      Gongo la mboto DSM

    22. #59
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      590
      Likes Given
      413

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Waende hospitali binafsi wana mishahara mizuri kuliko serikali

    23. #60
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,252
      Rep Power : 12575
      Likes Received
      5796
      Likes Given
      758

      Default

      Quote By Safari_ni_Safari
      Kujitolea ni bora kuliko kutumia nguvu! (ungesema hivi kuliko kuharibu lugha ya watu)
      Hiari ya shinda utumwa..

    Page 3 of 10 FirstFirst 12345 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...