Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

    Report Post
    Page 10 of 10 FirstFirst ... 8910
    Results 181 to 189 of 189
    1. #1
      Kadu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th January 2011
      Location : Kibaha
      Posts : 20
      Rep Power : 427
      Likes Received
      15
      Likes Given
      14

      Default MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      MGOMO:Madaktari 319 wafutiwa leseni
      Waandishi Wetu
      BARAZA la Madaktari Tanganyika limewafutia usajili madaktari wote waliokuwa katika mafunzo ya vitendo (Internship), baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mgomo wakiwa kazini.Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa Dar es Salaam jana imeeleza kuwa madaktari 319 wamepoteza sifa ya kuendelea na taaluma hiyo hivyo usajili wao umesitishwa rasmi kuanzia jana.Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk Donan Mmbando amewataka madaktari hao kurudisha hati zao za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari.

      “Kwa kuzingatia masharti ya sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhia kwamba madaktari wote ambao walijihusisha na mgomo, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo usajili wao umesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012.”

      “Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya terehe 17 Julai, 2012.”

      Dk Mmbando alisema, awali Baraza hilo lilipokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba baadhi ya madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship), waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kati ya Juni 23 na Juni 29 mwaka huu.

      Alisema madaktari hao walipangiwa kutoa huduma katika Hospitali za Muhimbili, KCMC, Rufaa Mbeya, Sekou Toure na Bugando za Mwanza, Amana, Temeke na Mwananyamala za Dar es Salaam, Haydom - Arusha, St Francis-Ifakara na Dodoma.

      Alisema kutokana na mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo huo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Dk Mmbando alisema kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa kwenye Baraza hilo, Msajili wa Baraza, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la kufanya Uchunguzi dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

      Alisema baada ya kuyafanyia kazi malalamiko hayo, Baraza limebaini kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda.

      Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania (MAT), Dk Edwin Chitage alisema alikuwa hajapata rasmi taarifa hizo licha ya kusikia fununu... “Sijapata taarifa rasmi lakini ni jambo tulilolitarajia na hatutashangaa tukisikia hilo kwa sasa subiri nithibitishe halafu nitatoa msimamo wetu.”
      Kiongozi wa madaktari kortini

      Katika hatua nyingine, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kudharau amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi ya kuwataka kusitisha mgomo kupitia vyombo vya habari.

      Amri hiyo ilitolewa Juni 22, mwaka huu na Jaji Sekela Moshi na kuwataka madaktari kurejea kazini mara moja, lakini amri hiyo haikutekelezwa.

      Jana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka alimsomea Dk Mkopi hati ya mashtaka na kumweleza Hakimu Faisal Kahamba kuwa kati ya Juni 26 na 28, mwaka huu, Dk Mkopi akiwa Rais wa MAT, alidharau amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi Juni 26, mwaka huu ikimtaka kutoa tangazo kwa wanachama wa chama hicho kupitia vyombo vya habari kwamba wasishiriki katika mgomo.

      Kweka alidai kuwa Juni 27, mwaka huu Dk Mkopi aliwashawishi wanachama kushiriki kufanya mgomo kitu ambacho ni kinyume na amri iliyotolewa Juni 26, mwaka huu.

      Hata hivyo, Dk Mkopi alikana mashtaka hayo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kiongozi huyo wa madaktari yupo nje kwa dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 8, mwaka huu itakapotajwa na kuangaliwa kama upelelezi utakuwa umekamilika au la.

      Afya ya Dk Ulimboka
      Wakati huo huo, afya ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka imezidi kuimarika.
      Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitage alisema jana kwamba: “Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, kwa sasa afya yake imezidi kuimarika, anakula mwenyewe lakini pia anazungumza mwenyewe na rafiki zake wa hapa nchini kwa njia ya simu.”

      Katika siku za karibuni, hali ya Dk Ulimboka ilielezwa kubadilika ghafla na kulazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kutokana matatizo mbalimbali, yaliyotokana na kupigwa ikiwamo figo kushindwa kufanya kazi.

      Alisafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi Juni 28, mwaka huu kwa ushauri uliotolewa na jopo la madaktari lililokuwa likimhudumia.

      UN yanena
      Katika hatua nyingine, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Dk Alberic Kacou amepokea barua ya MAT kuomba ulinzi kwa Dk Ulimboka anayeendelea na matibabu Afrika Kusini kwa madai kuna kikosi kilichotumwa kuhakikisha harudi nchini akiwa hai.

      Akizungumza jana Dar es Salaam jana, Dk Kacou alisema suala hilo la kutoa ulinzi watalitoa baada ya kuwasiliana na wote waliohusishwa kwenye waraka wa ombi hilo.

      Mgomo wamalizika
      Mgomo uliokuwa ukiendelea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Mifupa (Moi), Dar es Salaam umemalizika na huduma katika hospitali hizo zimerejea kama kawaida jana.

      Waandishi wa habari waliotembelea hospitali hizo waliona wagonjwa wakiwa wanaendelea kupokewa na kupatiwa huduma kama ilivyokuwa awali, kabla ya mgomo uliodumu kwa takriban majuma mawili yaliyopita
      Habari hii imeandikwa na Tausi Mbowe, Tausi Ally, Leon Bahati na Issa Lazaro, Geofrey Nyang’oro
      Source: gazeti la mwananchi

    2. Miaka 50

    3. #181
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,668
      Rep Power : 975
      Likes Received
      580
      Likes Given
      10

      Default

      Quote By MWANAHARAKATI MKWELI
      msiba wa mwenzio sio wa kuufurahia ninasikitika coz ni vijana wenzangu hawa ambao wamepatwa na huu mkasa wa kupokonywa leseni lakini naomba tupate fundisho moja kuwa muda ambao watu wengu wanakushauri kuacha jambo fulani ni vyema ukaacha then ukajiepusha na matatizo kwani hata sasa tunapozungumza hivi sio wote watakaoweza kwenda kutafuta ajila nje wengine watakuwa wameshaharibu ndoto za maisha yao hatakama najua kuna wengine watasema maisha sio udaktari pekeyake.
      but msikate tamaa mungu yupo tuendelee kumuomba may be mtarudishiwa hizo leseni zenu
      POLENI SANA KWA YALIYOWAKUTA
      Fisimaji wewe! Hii ndiyo shida ya vijana hamkupita JKT enzi ile. Serikali ya Tanzania haina jeuri ya kuwafuta leseni hata madaktari 10! Na naamini vijana madaktari hawana uwoga wa kijinga kupigania haki zao!

    4. #182
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,668
      Rep Power : 975
      Likes Received
      580
      Likes Given
      10

      Default

      Quote By ITEGAMATWI
      Unataka kupelekwa mabwepande eenh?Haya kawakusanye wakina Mama Bisimba ulianzishe na wewe!!
      masikini wa akili wewe!

    5. #183
      Micro E coli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2011
      Posts : 552
      Rep Power : 492
      Likes Received
      103
      Likes Given
      88

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Ritz
      Unataka suluhu gani tena wakati Madaktari ndio wameanzisha mgomo wakitaka mshahara mkubwa wewe ulikuwa unataka wanachotaka madaktari wanachotaka wapewe tu sababu ni madaktari serikali hawezi kutoa milioni 7.700.000 subirini Chadema wakichukuwa nchi watawalipa milioni 10.
      Bosi wako legelege,dhaifu milion 7 kwa Doctors haiwezekani Tanapa,TRA,BANDARINI,MAWAZIRI/WABUNGE NA SAFARI ZAKE kwenda kuonana na 50cent kwa millioni 700 inawezekana kweli ni 3Drs JK anamadegree ya ukweli.

    6. #184
      chubulunge's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th December 2011
      Location : mwabepande
      Posts : 132
      Rep Power : 399
      Likes Received
      9
      Likes Given
      23

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Dhaifu ni janga la kitaifa.

    7. #185
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,018
      Rep Power : 0
      Likes Received
      227
      Likes Given
      1

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      ufisadi wa ajira wilaya ya ilala.

      SALUMU KAZUKAMWE ni afisa manunuzi wa wilaya ya ilala,huyu jamaa aliajiriwa kupitia mlango wa nyuma ie kwa rushwa na alibebwa na katanga ambaye sasa ni katibu mkuu wa TAMISEMI, ajira haikutangazwa popote kinyume na taratibu za ajira serikalini.jamaa ali push kwa kumhonga mkurugenzi wa wilaya ya ilala tsh laki sita.

      salum maarufu kwa jina la KAZU aliiba pesa za misaada ya waathirika wa mafuriko ya jangwani akanunulia gari aina ya suzuki vitara nyekundu.

      wanatanuru,tuimulike kwa macho mawili halmashauri ya manispaa ya ilala kuhusu ajira za mlango wa nyuma.



    8. FemaTV & Radio

    9. #186
      Papizo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th February 2008
      Location : What for??
      Posts : 3,298
      Rep Power : 1233
      Likes Received
      401
      Likes Given
      2248

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By Ritz
      Haki yao milioni 7,700,000 kwa mwezi mmeishaambiwa muajiri wako hana uwezo wa kutoa mshahara huo kama mnataka masalahi zaidi ruksa kwenda sehemu ingine wanapolipa vizuri.
      Mkuu wangu hii nchi yetu na sio yako au ya nani, so ukisema kwenda sehemu nyingine nadhani una mean tofauti, zaidi Wabunge hizo hela wanazolipwa kwa mwezi zinatoka wapi??Hapa sasa tuweke ushabiki pembeni, sema ukweli unaona wabunge hela wanazolipwa ni sawa kabisa kutokana na kazi wanazofanya??Mbunge na daktari nani anapaswa kulipwa hela nyingi kutokana na kazi?Wabunge wengine toka bunge lianze hawajawahi kuchangia kitu chochote zaidi ya kupiga makofi nakugonga meza je unaona ni sawa??

    10. #187
      Papizo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th February 2008
      Location : What for??
      Posts : 3,298
      Rep Power : 1233
      Likes Received
      401
      Likes Given
      2248

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By SALOK
      hayo maneno hapo kwenye wino mweusi uliokolea si ya kweli! Mbona hao hao waliojaa maji vichwani wanapochukua kadi za cdm mnawaita majembe/jembe?? haya ndio mambo yanayochelewesha ukombozi wa kweli! Unafiki mwingiiiiiii..!!
      Mkuu wangu jaribu kufikiria saa zingine mtu akiandika kitu, niliavyoandika kumejaa vichwa maji sija mean kila mtu, wengine wapo wengi tu wanapiga kazi na zinaonekana CCM sio wote ni vichwa maji na ndio maana siku sema wote ni vichwa maji.Elewa hapo

    11. #188
      Papizo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th February 2008
      Location : What for??
      Posts : 3,298
      Rep Power : 1233
      Likes Received
      401
      Likes Given
      2248

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By lukindo
      be sincere mkuu, 2015 ni mbali ukilinganisha na matatizo tunayopitia. Chukulia mfano kama mtu anateswa kwa staili ya Dr. Ulimboka Stephen kwa interval ya miezi mitatu mitatu itakuwaje!?

      Lakini pia maswali ya msingi ya kujiuliza hapa:
      1. Inachukua muda gani kumfunza daktari mpaka kufuzu?
      2. Ni wanafunzi wangapi (vijana) wako tayari na wana uwezo wa kusomea hii fani?
      3. Watatumia muda gani na gharama kufidia hilo pengo la madaktari 319?

      Lakini swali zaidi tunaloweza kulitumia kujifunza ni kama serikali ingelitumia strategy hii hii kuwasimamisha/kuwafukuza kazi wabadhirifu serikalini si tungelikuwa tunaizidi China kwa maendeleo!????

      Mkuu wangu nimependa sana comment yako, si umeona mweyewe??Wezi wa EPA sijui Richmond wote hamna aliyeguswa wal kuulizwa, ila madaktari wanadai chao wanakuzwa kazi ni sawa kweli??Inauma sana kwa kweli sio siri, nchi ina kila kitu lakini mambo yanayofanyika ni hatari tu.

    12. #189
      ITEGAMATWI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th January 2012
      Posts : 1,666
      Rep Power : 776
      Likes Received
      421
      Likes Given
      826

      Default Re: MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

      Quote By timbilimu
      masikini wa akili wewe!
      Wewe pompompo sana,kwani hujui anayei-challenge serikali lazima ashughulikiwe?Mbona unacomment as if huijui serikali ya Tanzania.Kwajinsi mlivyo wanafiki mnawajaza wenzenu ujinga halafu mambo yakiharibika mnawakimbia.Oneni sasa wadogo zetu wa Intern wanahangaika peke yao wapuuzi kama wewe mliokuwa mnawadanganya mmekaa kimya kama hamuoni,Wewe wa hovyo sana!!

    Page 10 of 10 FirstFirst ... 8910

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...