Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchunguzi

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 33 of 33
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,209
      Rep Power : 3556
      Likes Received
      3058
      Likes Given
      462

      Default Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchunguzi

      NA THOBIAS MWANAKATWE

      6th July 2012

      Sakata la meli za mafuta zinazodaiwa kuwa ni za Iran kupeperusha bendera ya Tanzania kwa lengo la kufanikisha biashara ya nishati hiyo limezidi kuikoroga serikali ambayo sasa imezipigia ‘magoti’ nchi wanachama wa Baraza la Umoja wa Mataifa kusaidia kufanya uchunguzi ili kuthibitisha iwapo kuna ukweli kuwa meli hizo ni za Iran.

      Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimelazimika kuomba msaada huo kwa sababu Tanzania ina uwezo mdogo wa kufanya uchunguzi na kuthibitisha suala hilo.

      Membe alisema iwapo uchunguzi huo utabaini kuwa kweli meli hizo ni za Iran, Serikali ya Mapinduzi ya Zanziar (SMZ) pamoja na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitachukua hatua ya kuzifutilia mbali meli hizo.

      “Hivyo tunahitaji ushirikiano kati ya serikali zetu mbili, serikali ya Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) kusaidia katika kuthibitisha taarifa hizi kwa sababu wao wana uzoefu mkubwa wa ‘verification’ wa kukanusha ama kuthibitisha ya kuwa meli zinazopeperusha bendera ya Tanzania ni meli za Iran au la”, alisema Membe.

      Alisema Serikali ya Tanzania itahakikisha inafanya utafiti wa kina na wa kuaminika kwa kushirikiana na nchi za Marekani na za Umoja wa Ulaya ili kupata ukweli wa meli hizo.

      Membe alisema zipo sababu tatu zinazosababisha kufanyika kwa utafiti huo ambapo moja ni kwamba wakala wa kampuni ya Philtex ya Dubai ambaye ameingia mkataba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amekataa kwamba meli hizo ni za Iran.

      Alisema sababu ya pili ni kwamba Julai 2 mwaka huu Wizara yake ilipomwita Balozi wa Iran kujadili utata wa meli hizo ili athibitishe au akanushe taarifa hizo alikataa.

      Membe alitaja sababu ya tatu ya kufanya uchunguzi huo kuwa ni kutokana na kwamba sheria ya kimataifa hasa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inayozikataza nchi wanachama kuruhusu Iran au meli zake kutumia jina la nchi kwenda katika maji ya kina kirefu kupakuwa na kupakia bidhaa zake ili kukwepa vikwazo walivyowekewa.

      “Vipo vikwazo vilivyowekwa na jumuiya ya kimataifa hasa Umoja wa Mataifa kulingana na azimio namba 1929 la mwana 2010 inayozikataza nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuruhusu Iran au meli zake kutumia jina la nchi kwenda katika maji ya kina kirefu kupakuwa na kupakia bidhaa zake ili kukwepa vikwazo alivyowekewa,” alisema Membe.

      Membe aliwaomba Watanzania jambo hili lisizushe mtafaruku ndani ya nchi na kutetemesha Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar na kuwahakikishia kuwa litamalizwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

      Aliongeza kuwa lazima ifahamike Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hazitaki kupuuza taarifa ya kuwepo kwa meli hizo zinazopeperusha bendera ya Tanzania kwenye maji marefu na ndiyo maana zimeamua kufanya utafiti wa suala hilo.

      Mgogoro huu umezidi kupamba moto hapa nchini hasa baada ya Mbunge Marekani ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Howard Berman, kuweleza wazi kuwa kitendo cha kusajiliwa kwa meli za Iran na kupeperusha bendera ya Tanzania ni kuvunja vikwazo vya kiuchumi vya Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) dhidi ya Iran.

      Berman katika barua yake ya Juni 29, mwaka huu aliyomwandikia Rais Jakaya Kikwete alieleza masikitiko yake kwamba Tanzania imeruhusu Kampuni ya Taifa ya Meli za Iran (NITC) kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye walau meli sita na zinatarajiwa kufikia 10 na zimesajiliwa nchini.

      “Kwa kuruhusu meli hizo kuwa chini ya miliki ya NITC na kuendelea kusafirisha mafuta ghafi ya Iran, kitendo hiki kwa serikali yako kina madhara ya kuisaidia Serikali ya Iran kukwepa vikwazo vya Marekani na EU ili ipate mapato zaidi ya kugharimia mpango wake wa kutengeneza silaha za nyukilia na pia kusaidia ugaidi wa kimataifa,” imesema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Rais Kikwete.

      Kadhalika, alisema inasikitisha kuona kwamba serikali ya Tanzania imekiuka makubaliano ya pamoja ya jamii ya kimataifa ambayo inafanya kazi kwa pamoja kutumia njia za amani zikihusisha vikwazo vya kiuchumi ili kubadili tabia ya Iran ya kuhatarisha amani duniani.

      “Kitendo cha kuruhusu meli za NITC kupeperusha bendera ya Tanzania inatia shaka hadhi ya Tanzania katika jamii ya kimataifa,” inasema barua hiyo.

      Kwa maana hiyo, Berman alimuomba Rais Kikwete kufuta usajili wa meli hizo zinazopeperusha bendera ya Tanzania, kwani kwa mujibu wa uamuzi wa Rais wa Marekani, Barack Obama, wa 13608 ambao aliusani Mei mosi mwaka huu unajumuisha nchi zote na mashirika yote katika ukiukaji wa vikwazo dhidi ya Iran kama watakuwa wanaisaidia nchi hiyo kukwepa vikwazo hivyo.”

      Kadhalika, mbunge huyo ameonya kwamba endapo Tanzania itaamua kuziacha meli hizo kuwa na usajili nchini na kuendelea kupeperusha bendera yake, basi wao katika Bunge la Marekani hawatakuwa na njia nyingine isipokuwa ni kutafakari kama bado mipango ya maendeleo baina ya Marekani na Tanzania kama bado inahitajika.

      Hata hivyo baada ya suala hili kuibuliwa na vyombo vya habari, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iliibuka na kutoa taarifa kuwa kwa kuzingatia sheria ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (Maritime Authority – ZMA) iliyoundwa kwa sheria No. 3 ya mwaka 2009 ambayo pamoja na kazi nyingine inasimamia utekelezaji wa Sheria ya usafiri wa Bahari Zanzibar ya mwaka 2006 (Zanzibar Maritime Transport Act 2006).

      Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa SMZ, Hamad Masoud Hamad, aliwasilisha taarifa yake kwa Baraza la Wawakilishi Julai 2, mwaka huu akithibitisha kusajiliwa kwa meli 10 za Zanzibar ambazo zinapeperusha bendera ya Tanzania, lakini siyo za Iran ila zimetokea Malta na Syprus.

      Alisema SMZ imetiliana mkataba na kampuni ya PHILTEX ya Dubai kufanya usajili wa meli za kimataifa (Open Registry). Usajili huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2009 na mpaka sasa kupitia Wakala wake imesajili meli 399 ikiwa ni pamoja na meli za mafuta, makontena, za mizigo ya jumla na meli za abiria.

      Alitaja meli hizo kuwa ni Daisy 81479 Daisy Shipping Co. Ltd Malta; Justice 164241 Justice Shipping Co. Ltd Cyprus; Magnolia 81479 Magnolia Shipping Co. Ltd Malta; Lantana 81479 Lantana Shipping Co. Ltd Malta; Leadership 164241 Leadership Shipping Co. Ltd Cyprus; Companion 164241 Companion Shipping Co. Ltd Malta; Camellia 81479 Camellia Shipping Co. Ltd Malta; Clove 81479 Clove shipping Co. Ltd Malta; Courage 163660 Courage Shipping Co. Ltd Cyprus; Freedom 163660 Freedom shipping Co. Ltd Cyprus na Valor 160930 valor Shipping Co. Ltd. Cyprus.

      Waziri huyo alisema walimtaka wakala wao Philtex Corporation kuwaita wenye meli hizo na kuwataka kujieleza kuhusu uhusuiano wao na Serikali ya au makampuni ya mafuta ya Iran na walisema kuwa hawana uhusiano na Serikali au mamlaka yoyote nchini Iran na wameamua kuja kusajili meli Zanzibar kwa ridhaa yao.

      Jana katika sehemu ya habari kuhusu meli hizi tulisema kuwa Waziri Hamad alisema Barazani kuwa meli hizo ni za Iran. Tunasikitika kwa upungufu wa aya hiyo katika habari yetu ya jana. Mhariri.

      CHANZO: NIPASHE

      Sn2139 likes this.

    2. Miaka 50

    3. #21
      mwana wa africa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th April 2011
      Posts : 429
      Rep Power : 495
      Likes Received
      56
      Likes Given
      4

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      hapa sijui kutakuwa na tume huru? au ndo kina kova wataingia studio.

    4. #22
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,209
      Rep Power : 3556
      Likes Received
      3058
      Likes Given
      462

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      Quote By mob
      sisi tuna madini ya uraniam ni vyema tukawaomba wenzetu watu wa jumuia ya iran kuja kutusaidia kuchimba ili tuweze kupata umeme wa uhakika kila wakati.si vizuri kuona watu wanasema hawa watu ni wabaya nasisi tukaingia mkumbo huo huo kusema ivyo ivyo. kuiona unasapoti kila kitu wewe una tabia ya uoga.

      IRAN haina Technolojia ya kuweza kutengeneza Umeme wa Nucklea; wao wenyewe wanawatumia wataalamu toka

      URUSI, Iran wanahitaji raw materials kuendesha mitambo yao hawana utaalamu wowote; wana Engineers wa kuendesha

      Hiyo Mitambo lakini sio Wajenzi wa Hiyo Mitambo; Sasa sijui ni Nani alikuambia hayo?

      Na IRAN wamewekewa SANCTIONS kwanini uende kwa watu wenye SANCTIONS?

    5. #23
      masopakyindi's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 5th July 2011
      Posts : 3,725
      Rep Power : 4193
      Likes Received
      1000
      Likes Given
      415

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      Quote By Mtumbatu
      kwani UAMSHO ina tatizo gani na nyinyi kama mkweli mnataka Tanganyika yenu muazishe somesing like, bila hivyo mpaka kiyama mtakuwa chini ya himaya ya Tanzania na vizazi vyenu havitajua asili yenu kama sisi tunajisifia uzanzibari wetu, aidha katika hili la meli mnapoteza muda tu na kama ilivyo sifa za watanganyika ni kuongea, basi mtaongea na mtaongea.

      Zanzibar imeshatoa tamko na lipo mpaka kwenye hansard za Baraza la Wawakilishi, mnataka kusema waziri kutoka Zanzibar kasema uwongo, hatuzifuti hizo meli, mkitaka itabidi mtulipe fidia kwa kukosa mapato, vikwanzo si vya UN ni vya USA na EU ndio maana China bado inanunua mafuta kutoka Iran, nyie watanganyika kazi yenu ngonjera basi sisi hazituyumbishi hizo, mara hii ngangari hatutokli kama tulivyotoka OIC, anayetujua sisi Nyerere na keshakufa nyie hamtujui sisi.
      Si muda mrefu jeuri hii ya Zanzibar itapata jibu.
      Masuala ya uamsho, meli na choko choko za kuchoma makanisa karibu itajibiwa , tena kwa kichapo cha kidplomasia.
      "If you don't know where you are going, any road will get you there-nowhere”

    6. #24
      Electron's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd July 2012
      Posts : 91
      Rep Power : 365
      Likes Received
      48
      Likes Given
      59

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      Amekiri udhaifu..... ndiyo hatuwezi kufanya uchunguzi, lakini walikuwa wapi miaka yote 50 kutokuandaa watu mpaka nchi kama hii yenye ukanda mrefu wa bahari na bandari kadhaa kutokuwa na wataalam wa mambo kama haya.... Hicho ni kitu ambacho kiko obvious kabisa vipi kwa utaalamu sekta zingine (elimu, afya, madini, utalii, misitu, uvuvi, ICT etc0 si ndio kabisa... . DDuh tunapelekwa wapi sisi na hili kundi la watu dhaifu wa fikra....

    7. #25
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,209
      Rep Power : 3556
      Likes Received
      3058
      Likes Given
      462

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      Quote By Mkandara
      Nampongeza Membe kwa maelezo yake maana anajua kinachofanyika. Swala hapa ni kwamba Marekani hawataki kabisa nchi yoyote ishirikiane na Iran ktk kuhakikisha hawauzi Mafuta nje. Inajulikana wazi kwamba mashirika ya Meli ni ya watu binafsi wafanya biashara ambao hutafuta kazi ya usafirishaji ndani na nje ya nchi zao. Kwa hiyo swla hapa ni mbinu za kujaribu kuikomoa Iran na sii Tanzania wala shirika la meli kwa sababu Marekani inaweza kabisa kuelekeza malalamiko yake kwa shirika hilo. Tukikataa sisi wataenda kusajili nchi nyingine..

      Hapa Canada kuna mashrika mengi sana ya Marekani, China, Japan Uingereza na kadhalika, tena naweza kusema robo tatu ya mashirika makubwa Canada ni ya Kimarekani ikiwepo Barricks. Hivyo, kuilaumu Canada kwa sababu ya vitendo ama maamuzi ya Barricks wakati sisi wenyewe ndio tumeingia mkataba na Barricks sio Canada wala Marekani ni kukosa kuelewa usajili unafanyika vipi. Maadam Barricks wanafuata sheria zote za usajili Canada na wanalipa kodi, serikali ya Canada haitajali ni kiasi gani tunapewa iwe ruzuku au hatupewi kitu kabisa.. Ila watajali tu kama kuna ukiukaji wa sheria na haki za binadamu..

      Mbona Wayahudi (Jews) kote duniani hulipa kodi nchini kwao japokuwa ni raia wa nje na wanaishi na kufanya biashara nchi za nje?.. Sijasikia mtu hata mmoja akipinga Myahudi anayewekeza Tanzania, Canada au Marekani kujihusisha na ulipaji kodi kwa Israel wakati sisi tukifanya hivyo tu tunaambiwa Alqaeda na itachunguzwa hizo fedha zinakwenda Tz kufanya nini pengine hata kufungiwa accounts. Ifike mahala tuuthamini Uhuru wetu sisi wa tu huru na raia wa Tanzania, nchi huru yenye sovereign yake na tunafanya maamuzi kwa maslahi ya nchi yetu sio kuwaridhisha Marekani au EU. Kuna madai ya ukweli yapelekwe UN na maamuzi yafanyike kwa wanachama wote wa jumuiya hiyo.. Hivi kweli mkichukua nchi mtaweza kuongoza kwa maslahi ya Watanzania au tutakuwa vibaraka?
      IRAN ni tofauti IRAN ni JUMUIA haina Individual Investor ni Kama Ilivyokuwa Libya ni Taifa ndilo linalo Invest; Ukienda

      Mto Rufiji hayo Mashamba ya Umwagiliaji yote ni ya Nchi ya IRAN sio ya Mfanyabiashara wa IRAN wao ni kama vile

      Wasocialist in Islamic nature; Hata Machimbo yao yote ya Mafuta Waliyataifisha lakini Wameacha kama 4% kwa

      Makampuni ya nje ili kuyatengeneza, kununua vipuri n.k; Hakuna Major Private Business Man kama alivyokuwa

      Adnan Kashoggi tajiri wa kiiran aliyekimbia baada ya Islamic Revolution.

      Tatizo IRAN ndio inauzia Silaha SYRIA;

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      Quote By nngu007

      Mkuuu wangu hizi habari umezipata wapi?.. Iran ni capitalist kaa capitalist nyingine sema wao mashirika mengi wamewauzia wananchi wao kwanza shares. Hakuna Ujamaa unaofikiria wewe isipokuwa wao kama mataifa mengine wanauza shares ktk soko lao. Mashirika yote haya ya mafuta yako Iran na yana operate iwe Shell au jinginelo. Sema wao kama Barricks ingekuwa Kwao wangelazimika kuingia ktk soko lao. Kama Tanesco ingekuwa private public company ikauza shares zake DSE wananchi wakapewa kipaumbele kununua kwanza kuna tatizo?. Hii haiwafanyi wao Wajamaa hata kidogo..

      Tukirudi ktk swala la Islamic revolution.. Ni kitu gani wewe unaona hawana haki ya mageuzi yale. Wakati British walipomwondoa Mossadeq ili wao wa control mafuta ya Iran wakiwapa only pound 4 kwa kila tani ya crude oil ilikuwa halali?.. Je sii kama sisi leo tunalia na Barricks kutupa ruzuku ya asilimia 3 na bado Sinclair anachukua asilimia 1.9. wameahidi kulipa corporate taxes hadi leo hawajalipa kitu for the last 10 yrs, sorry 20 years?. Je tukifanya mapinduzi kwa sababu hiyo ni kosa? Wala sintoshangaa kama Nyerere aliondolewa kama Mossadeq wa Iranb ili wao wpate ku control rasilimali zetu..

      Haya unazungumzia Adnan Kashogi, Je, unajua kwamba yeye ni major shareholder wa Barricks na tukiichukua Barricks tutaaandikwa kwa mabaya yetu na unyama wake kwetu hautahesabika. Wameua watu wangapi Bulyanhulu na Mara mabli kabisa na kuiba dhahabu yetu...Iran waliamua kweli wakawafukuza na wakaweza kuifanya kazi wao wenyewe...Haya ndio mageuzi ya kweli sio porojo..

      Jamani jamani hii chuki kwa Wairan sisi imetoka wapi? Wairan wametufanyia nini sisi baya kiasi kwamba nasi tuwe vibaraka wa Marekani na EU wakati wametusaidia wakati wote wa shida iwe wakati wa great depression (!982) wakati nchi za magharibi ndio kwanza walituwekea vikwazo kwa kuwa tu sisi ni Wajamaa..Hayo mashirika ya nje kupewa asilimia 4 washukuru ingekuwa mimi ningewanyima hata hiyo - wezi tu hawa mafuta yangu halafu watake niwape wao umiliki kwa kisa gani?..Swala la Syria kwani lilianzishwa na Iran au Marekani?.. wao hawauzi silaha Syria mbona hawaandiki wanavyouza hizo silaha zao hadi Libya na Congo?

      Inachukiza na kuudhi sana ku judge nchi kwa sababu ni nchi ya kiislaam wakati tuna ushirikiano kama huo na Vaticanmsiseme ni nchi ya Kikristu halafu kwa kutumia Ukristu tunataka kujipendekeza kwa Marekani who careless of us being Christians. Sii mnasema nchi yetu haina dini sasa chuki ya dini moja inatoka wapi?..Kama kweli hawa wanakujali wewe ama wanajali uongozi wa Kikristu basi Haiti ingekuwa tajiri maana Marekani wana ushirikiano na Haiti kwa zaidi ya miaka 100. Leo nchi hiyo bado ni maskini kuliko zote duniani..

      Majority ya Wamarekani weusi ni Wakristu tena wa Ibada sio kwa jina, mbona ndio maskini kuliko wote na wanatukanwa kila siku.. Msitake sana kudanganywa na hawa Jews ambao wanaumwa sana kuona Utajiri mkubwa wa Iran unawapita machoni mwao. Kama kweli wanachukia Uislaam basi wangeichukia Saudia kuliko nchi zote maana huko ndiko Ulikoanzia.. lakini mbona ndio wanaipenda sana na wako tayari kuingia vita na yeyote kuitetea Saudia na utawala wa Sultan ambao wanamiliki utajiri wote za nchi hiyo.. Acheni kuwa watumwa wa kifira, Mungu kawapoeni akili mfiirie na mfanye maamuzi ya maana kwa maisha yenu wenyewe..Nigger please!
      Last edited by Mkandara; 7th July 2012 at 19:53.
      Bantugbro likes this.
      Exploration of reality

    10. #27
      OPTIMUS TZ's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th January 2012
      Posts : 390
      Rep Power : 447
      Likes Received
      60
      Likes Given
      1

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      Quote By Mkandara
      Nampongeza Membe kwa maelezo yake maana anajua kinachofanyika. Swala hapa ni kwamba Marekani hawataki kabisa nchi yoyote ishirikiane na Iran ktk kuhakikisha hawauzi Mafuta nje. Inajulikana wazi kwamba mashirika ya Meli ni ya watu binafsi wafanya biashara ambao hutafuta kazi ya usafirishaji ndani na nje ya nchi zao. Kwa hiyo swla hapa ni mbinu za kujaribu kuikomoa Iran na sii Tanzania wala shirika la meli kwa sababu Marekani inaweza kabisa kuelekeza malalamiko yake kwa shirika hilo. Tukikataa sisi wataenda kusajili nchi nyingine..

      Hapa Canada kuna mashrika mengi sana ya Marekani, China, Japan Uingereza na kadhalika, tena naweza kusema robo tatu ya mashirika makubwa Canada ni ya Kimarekani ikiwepo Barricks. Hivyo, kuilaumu Canada kwa sababu ya vitendo ama maamuzi ya Barricks wakati sisi wenyewe ndio tumeingia mkataba na Barricks sio Canada wala Marekani ni kukosa kuelewa usajili unafanyika vipi. Maadam Barricks wanafuata sheria zote za usajili Canada na wanalipa kodi, serikali ya Canada haitajali ni kiasi gani tunapewa iwe ruzuku au hatupewi kitu kabisa.. Ila watajali tu kama kuna ukiukaji wa sheria na haki za binadamu..

      Mbona Wayahudi (Jews) kote duniani hulipa kodi nchini kwao japokuwa ni raia wa nje na wanaishi na kufanya biashara nchi za nje?.. Sijasikia mtu hata mmoja akipinga Myahudi anayewekeza Tanzania, Canada au Marekani kujihusisha na ulipaji kodi kwa Israel wakati sisi tukifanya hivyo tu tunaambiwa Alqaeda na itachunguzwa hizo fedha zinakwenda Tz kufanya nini pengine hata kufungiwa accounts. Ifike mahala tuuthamini Uhuru wetu sisi wa tu huru na raia wa Tanzania, nchi huru yenye sovereign yake na tunafanya maamuzi kwa maslahi ya nchi yetu sio kuwaridhisha Marekani au EU. Kuna madai ya ukweli yapelekwe UN na maamuzi yafanyike kwa wanachama wote wa jumuiya hiyo.. Hivi kweli mkichukua nchi mtaweza kuongoza kwa maslahi ya Watanzania au tutakuwa vibaraka?

      Mzazi kila mtu anapenda kuwa huru lakini sisi ombaomba hatuko huru ilo dili la irani serikali inalijua na ni njaa ndo zimetuponza mtu wangu USA ikisema Tz ni kuitikia ndio mzee issue ya wayahudi haiingii hapa kama wanalipa kodi kwao ni safi sana wanauzalenda kaka;hapa ni meli irani,zenji na bongo.............membe kama anajitaka na Mr mdhaifu dawa ni kufuta huo usajili wa meli na kuomba msamaha haraka sana kwa Obama la sivyo tutakula mchanga.

    11. #28
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      Quote By OPTIMUS TZ

      Huelewi nimetokea wapi. Wayahudi ndio wenye kulianzisha hili kwa sababu ya maslahi yao. Wanachotaka ni ku control dunia, ku control mafuta na utajiri wote wa rasilimali duniani. Ndio maana walifukuzwa Ulaya kwa hofu hiyo hiyo wakapewa Uganda kwanza kisha wakatafutiwa Israel (Palestine)lakini hawa sii watu hata kidogo inapofikia swlaa la fedha na utajiri. Kama ulaya ingekuwa na mapenzi nao sana kwa nini wasiwape Uraia huko badala yake wakatafutiwa nchi nyingine ilihali hawakufika hata millioni, yaani nchi zote za Ulaya walikosa mahala pa kuwapa hifadhi?..Historia ya Ulaya inajulikana sana kwa kila mtu anayewapa taabu humfukuza na kumtafutia makazi mapya toka wauaji na majambazi (criminals) wa Kiholanzi na kiingereza kupelekwa na kutupwa South Afrika, New Zealand na Australia halafu wanalindwa.

      Kama Iran inafanya kosa lolote Umoja wa Mataifa upo, sisi ni wanachama na sio wanachama wa EU wala Nato. Wameshindwa kuwakilisha kesi huko sasa wanatafuta kulazimisha kama walivyoingia Iraq na Afghanstan - Hatudanganyiki. Na kama Chadema wanaunga mkono swala hili bila kupima basi inanipa mashaka makubwa ktk maamuzi ya viongozi wangu itakapo fika kuongoza nchi - Kuna harufu ya kina Morgan Tsvangirai ktk maswala ya foreign policies..
      Bantugbro likes this.
      Exploration of reality

    12. #29
      measkron's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 1,558
      Rep Power : 11271
      Likes Received
      676
      Likes Given
      1255

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      Quote By Recover
      Hawana uwezo aw kuficha..hawana hiyo akili..labda kwa msaada aw Irani
      mkuu kama ilivyoahidi kuwaletea madaktari 1000 huo pia ni msaada, ha ha ha

    13. #30
      Interested Observer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th March 2006
      Posts : 975
      Rep Power : 873
      Likes Received
      91
      Likes Given
      99

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      Quote By Mkandara
      Nampongeza Membe kwa maelezo yake maana anajua kinachofanyika. Swala hapa ni kwamba Marekani hawataki kabisa nchi yoyote ishirikiane na Iran ktk kuhakikisha hawauzi Mafuta nje. Inajulikana wazi kwamba mashirika ya Meli ni ya watu binafsi wafanya biashara ambao hutafuta kazi ya usafirishaji ndani na nje ya nchi zao. Kwa hiyo swla hapa ni mbinu za kujaribu kuikomoa Iran na sii Tanzania wala shirika la meli kwa sababu Marekani inaweza kabisa kuelekeza malalamiko yake kwa shirika hilo. Tukikataa sisi wataenda kusajili nchi nyingine..

      Hapa Canada kuna mashrika mengi sana ya Marekani, China, Japan Uingereza na kadhalika, tena naweza kusema robo tatu ya mashirika makubwa Canada ni ya Kimarekani ikiwepo Barricks. Hivyo, kuilaumu Canada kwa sababu ya vitendo ama maamuzi ya Barricks wakati sisi wenyewe ndio tumeingia mkataba na Barricks sio Canada wala Marekani ni kukosa kuelewa usajili unafanyika vipi. Maadam Barricks wanafuata sheria zote za usajili Canada na wanalipa kodi, serikali ya Canada haitajali ni kiasi gani tunapewa iwe ruzuku au hatupewi kitu kabisa.. Ila watajali tu kama kuna ukiukaji wa sheria na haki za binadamu..

      Mbona Wayahudi (Jews) kote duniani hulipa kodi nchini kwao japokuwa ni raia wa nje na wanaishi na kufanya biashara nchi za nje?.. Sijasikia mtu hata mmoja akipinga Myahudi anayewekeza Tanzania, Canada au Marekani kujihusisha na ulipaji kodi kwa Israel wakati sisi tukifanya hivyo tu tunaambiwa Alqaeda na itachunguzwa hizo fedha zinakwenda Tz kufanya nini pengine hata kufungiwa accounts. Ifike mahala tuuthamini Uhuru wetu sisi wa tu huru na raia wa Tanzania, nchi huru yenye sovereign yake na tunafanya maamuzi kwa maslahi ya nchi yetu sio kuwaridhisha Marekani au EU. Kuna madai ya ukweli yapelekwe UN na maamuzi yafanyike kwa wanachama wote wa jumuiya hiyo.. Hivi kweli mkichukua nchi mtaweza kuongoza kwa maslahi ya Watanzania au tutakuwa vibaraka?
      Kama umesoma kwa makini Marekani halalamiki wewe kuvunja sheria. Anacholalamika wewe kunywa pombe za bure na kula kwake halafu ukamtumikie mume mwingine. You have to draw a line, who you deal with and who feeds you. Si unaona wachina wamekaa kimya wakati Marekani analalamika kuhusu Iran. Wewe utaweza?
      Mkandara likes this.

    14. #31
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      Quote By Interested Observer
      Kama umesoma kwa makini Marekani halalamiki wewe kuvunja sheria. Anacholalamika wewe kunywa pombe za bure na kula kwake halafu ukamtumikie mume mwingine. You have to draw a line, who you deal with and who feeds you. Si unaona wachina wamekaa kimya wakati Marekani analalamika kuhusu Iran. Wewe utaweza?
      Hapa kwa maswali na majibu ktk mifano kama hii ndio umefika mwanangu,
      Kwanza kabisa hii akili ya kutufanya sisi wanawake tunaofanya umalaya wa kunywesha pombe ili kutoa au kugawa mchezo ndizo nisizokubaliana nazo. Ndio maana nasema kwa nini sisi tusiwe wanaume japo maskini, na kama wanatununulia Pombe ni ktk mapenzi na urafiki wa kiume. Tunakunywa pamoja halafu kila mtu natazama ustaarabu wake sio kunatoa offer ya pombe ukitegemea nitakukidhi haja zako..Bora hata ingekuwa ukuhadi lakini mchezo tuutoe sisi kwa sababu wao wanapenda Ushoga! aaah kaka hatudanganyiki.

      Hakuna misaada ya bure hilo tunalijua sana na ndio maana tunataka kuikata isipokuwa ile yenye manufaa kwetu - Mtaji, sasa kama nitautumia mtaji huo vibaya au nje ya makusudio niloombea hapo una haki ya kukata urafikina misaada sio kunilazimisha mimi maadui zako wawe maadui zangu, hizo siasa za maji baridi zimekwisha longtime. Hata mwanamke sii binadamu wa kutumiwa kwa Pombe, ana haki ya kumpenda mtu tena basi yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuchagua ampendaye.. Hivyo kama sisi Tanzania ni wanawake tutamchagua mume tumpendaye iwe kwa mapenzi ya pesa au ya dhati na sii kuwa raped na mtu ati katununulia pombe..

      Huyo Mchina mbona ndiye contractor na ndiye mnunuzi mkubwa wa mafuta yao sasa hivi, kama Marekani mwanaume kweli sii awaambie Wachina wasinunue hizo meli zitakosa kazi!
      Exploration of reality

    15. #32
      asigwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Location : TANDHANIYA
      Posts : 4,389
      Rep Power : 1265
      Likes Received
      1208
      Likes Given
      1253

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      mkubwa ni mkubwa tu akikohoa lazima weye ushituke...naona MK'WERE alikuwa yuko hatiani kubaniwa visit za ulaya kama mugabe...hongera sana kwa kujikomba kwa wakubwa ili muonewe huruma...............

    16. #33
      sheky's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 175
      Rep Power : 395
      Likes Received
      38
      Likes Given
      10

      Default Re: Sakata meli za Iran ngoma nzito; Serikali imezipigia 'magoti' nchi wanachama UN kusaidia Uchungu

      mmmmmhhhhhhhhhhhhhhhhhh, kazi kweli kweli

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...