Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

    Report Post
    Page 2 of 4 FirstFirst 1234 LastLast
    Results 21 to 40 of 71
    1. #1
      VUTA-NKUVUTE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2011
      Posts : 1,703
      Rep Power : 723
      Likes Received
      892
      Likes Given
      125

      Default Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Ingawa ni maelezo marefu,si vibaya tukajikumbusha mambo haya kutoka kwenye Hansard za MKUTANO WA NANE

      Kikao cha Tano – Tarehe 19 Juni, 2012

      VIDEO:




      MHE. MCH. PETER S. MSIGWA:

      Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi.Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuanza kwa nukuuambayo naipenda sana inayosema:-


      “Insanity is keeping doing the same thing in the same way and expecting different result”

      ambazo zinalikabili taifa lakini kwa bahati mbaya nimeona yaani uwendawazimu nikufanya jambo lilelile kwa njia ileile huku ukitegemea matokeo tofauti.

      Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanafalsafa Albert Einstein anasema:-“Problems can not be solved by the same level of thinking that creates them”. Ndugu zangu, kabla sijawa Mbunge kama alivyosema kaka yangu Mheshimiwa Akunaay, nilikuwa nawa-admire sana Wabunge wanavyokuwa Bungeni, wakivaa suti, nilikuwa naona hapa ni mahali ambapo tuna reason, mahali ambapo tuna question na mahali ambapo tunatoka na solutions


      is the opposite, binafsi najisikia vibaya sana. Kama taifa tupohapa, we are dealing na future ya taifa hili, tunashughulika namamia ya maskini wa Tanzania, tunashughulika na barabarambovu za Watanzania, tunashughulika na hospitali mbovu zaWatanzania, halafu tunakuja hapa tunaongea mambo yakhanga!

      Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma historia, nchi za Ulayakarne ya 14, Marekani na Ulaya na nchi zilizoendelea, zilikuwana fikra na mawazo kama tunavyofanya sasa hivi lakini ilipofikakarne ya 18, inaitwa age of enlightenment, reasoning age, walianza kufikiri, kuhoji na kudadisi. Tunapofika katika karne hiikatika Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania,tunapojadili bajeti maana yake tunazo changamotozinazotukabili kama taifa.

      Badala ya kukaa na kujiuliza kwa ninitupo hapa, tunatokaje hapa tulipo, tunaanza kuongeangonjera na maneno ya uswahiliuswahili yaani unafiki, woga,kujipendekeza na kutokujadili mambo ya msingi.


      (Makofi)


      Mheshimiwa Mwenyekiti, najisikia uchungu sana mamiaya wananchi wametuamini tuje tujadili vitu vya maana hapalakini tunakubaliana akili ndogo itawale akili kubwa. JamesMadison mwaka 1822 alisema, “
      knowledge forever will governignorance”.

      Tumekubali Bunge hili knowledge ndogo i-governknowledge kubwa, tumekubali ignorance i-govern knowledge,tunalipeleka wapi taifa? Akichangia professor hapa hanatofauti na mtu wa darasa la pili. Huwezi kutofautisha mtumwenye masters na mtu wa darasa la pili, where are we takingthis nation? Watu wametupa kura, tunapoteza fedha zaWatanzania, tumekaa hapa tunaacha kujadili mambo yamsingi kwamba tunawezaje kutoka kwenye matope haya? Karne hiyo ya 18 ninayoisema walipoanza kuhoji, walipoanzakudadisi ndipo mapinduzi ya viwanda yalivyojitokeza, no wonder watu wanaosema ni wataalamu wa uchumi wametufikisha hapa tulipo, if that is the case, haya ndiyo masuala ambayo tunapaswa tuyajadili kama taifa.

      Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti inaonyesha hapa, kitabu cha uchumi cha Mheshimiwa Wassira kwamba deni limekuwa shilingi trilioni 20. Ukigawanya ni kama karibu kila Mtanzania anadaiwa shilingi laki nne na themanini na zaidi, hata mimba inadaiwa, ndiyo taifa tulipofika hapa sasa hivi.

      Pianinashangaa katika mpango wake wa bajeti taifa hili kamatunafuatilia na tunakwenda na takwimu, mdogo wangu amezungumza hapa kwamba tunatumia takwimu za nyuma, unawezaje kupanga mambo na takwimu za nyuma?

      Leo hii katika taifa hili 44.2% ni watoto walio chini ya miaka 15 maanayake hawa ni consumers, wanakula zaidi hawa-produce, wakoshuleni na wanao-produce katika nchi hii ni wachache sanakuliko wanaokula ukijumlisha na wazee tuna mzigo mkubwasana. (Makofi)



      Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa utaratibu wabajeti tulio nao hapa,
      there is no way kama tunaweza tukafanya maendeleo, it will take ages kubadilisha taifa hili kama tunaendelea na ngonjera za namna hii na kuruhusu akili ndogo itawale akili kubwa.

      Watu wenye akili kubwawanaweka akili zao mfukoni kwa sababu ya ushabiki wakivyama badala ya kukaa tuka-discuss namna ya kutatuamatatizo yetu.Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama wanao-consume niwengi na wanao-produce ni wachache maana yake nini?

      Tutaendelea kuomba fedha nje na kukopa fedha nje ilituwalishe kwa sababu ni wajibu wa Serikali kusomesha watoto,ni wajibu wa Taifa kuhakikisha watoto wanavaa na kusomashule nzuri lakini mpango mzima wa uchumi uko kimya,hauzungumzi.

      Hapa watu wasomi ambao tupo 350 taifalimetuamini tukae hapa tunatakiwa tujihoji, ndiyo maananimesema problems can not be solved by the same level ofthinking that created them, you guys you are tired!

      Kwasababu hamuwezi kutetea matatizo haya, mmetuwekakwenye mess ninyi wenyewe, ni lazima akili ya juu zaidi iwezekutatua, ni principle hii yaani huwezi kubadilisha that is theprinciple, iwe ni mwanamahesabu na nikiunganisha na insanityis keeping doing the same thing in the same way andexpecting different results and this is what we are doing.



      Tunafanya hayohayo kila mwaka bajeti ya namna hiyohiyo.Ukienda kwenye elimu ni matatizo, ukienda kwenye kilimo nimatatizo, ukienda kwenye afya ni matatizo mwaka baada yamwaka ni matatizo yaleyale,
      why can’t we think a little bitmore?

      We can’t stretch our brain a little bit more kama taifa?(Makofi)



      Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeongea na watu wengineambao ni ma-professor wanasema mara nyingi wakitoaushauri wa kitaalamu, Serikali hamsikilizi na inawezekanawanakaa watu wachache, wanajifungia halafu wanatoamaamuzi kwa sababu wanajua mambo ni yaleyale, business asusual. Ndugu zangu, where are we going? Where are weheading?

      165

      Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu zinaonyesha tenakaribu 42% ya watoto wanaozaliwa wanadumaa,


      they can notthink properly, they can not question, they can not ask.

      Ubongo aliotupa Mungu ni lazima uwestretched ili uwezekuchambua kwani tumeumbwa ili tutatue matatizo hapaduniani na siyo tu-create matatizo. Tulipokuja hapa Bungenitunatakiwa tu-solve problems, Bunge hili naliomba liwe Bungela kimapinduzi, tu-change namna ya kufikiri na tu-change


      namna ya kufanya vitu na wengine wanapata taabu hapakwa sababu tumezoea Bunge la chama kimoja.

      Tuna mfumona traditional ya chama kimoja cha zamani, ulimwengu umechange
      halafu tumesimama mahali pamoja hatuendi naulimwengu unavyokwenda. Maendeleo duniani yamekuja kwakuwa na mawazo tofauti yanayopingana, badala yakutuzomea mtusikilize, huu ndiyo wajibu wetu. Mimi kama opposition

      siwezi kusifia bali nakukosoa ili ufanye kazi yako vizuriili na wewe utimize wajibu wako. (Makofi)



      Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa deni kama hili kila mwakalinaongezeka halafu tunakaa hapa tunasema Serikali ya CCMitaendelea kutawala, so what? Ili iweje? Kwa sababu lengo laSerikali kuwepo ni kutatua matatizo ili tuhakikishe tuna-improve maisha ya watu lakini watu kwa sababu wanalinda vyeo, kunammoja amesema Mchungaji, lakini nitasema tu hata kamamtasema au kunitoa nje ya Bunge lakini kama ukweli unakosewa


      I will speak out kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya Wachungaji vilevile. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mbunge mmoja alishaurihapa tuombewe lakini sioni hata theory ya uchumi inayosemakama unataka kutatua matatizo ya uchumi eti ufanyemaombi, ninashangaa huyu amepata wapi hilo?

      As aTheologians hata Paul anasema asiyefanya kazi na asile siyo aombewe, unamnyima chakula lakini yeye anasema watu waombewe. Mimi kama Mchungaji naombea wazinzi, wanaofumaniwa na wake za watu, ndiyo tunawaombea, mimi kama Mchungaji tunawaombea wenye mapepo na hii ni
      principle tuna apply, una-consumers wengi lakini producers wachache maana yake you have to produce more tafuta njiaza ku-produce zaidi, we don’t pray for this, we don’t have topray for this. (Makofi)


      Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu tumekaa hapatumezalisha taifa la watu waoga, wanafiki nawanajipendekezapendekeza, mimi sijaja hapa kwa kupewafedha bali wananchi wa Iringawamenichangua, wananiaminina ninajua wananiunga mkono, wananisikiliza. Sasa sihitajikujipendekeza nitaeleza ukweli as a nation tupo kwenyematatizo. Wehave to address this problems lakini siyo tunakujahapa tunaweka ngonjera maneno ya khanga halafu watumnawapigia makofi, tunalipeleka wapi taifa hili? (Makofi)


      Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajisikia uchungu, naomba

      niachie hapo. Ahsante sana. (Makofi)
      Uongo huonekana na kuaminiwa haraka.Ukweli ndio mwisho wa yote!

    2. Miaka 50

    3. #21
      Mandingo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd September 2011
      Posts : 927
      Rep Power : 572
      Likes Received
      186
      Likes Given
      52

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Kuna tofauti kubwa sana kati ya wabunge wachungaji wa cdm na ccm mfano Msigwa Vs Mama Rwakatale.
      Big up Msigwa!

    4. #22
      Jile79's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2009
      Posts : 3,758
      Rep Power : 1263
      Likes Received
      210
      Likes Given
      9

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Ndiyo raha ya kuwa na watu km hawa....wachungaji wana reasoning saana....msigwa big up sana

    5. #23
      Fekifeki's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 18th November 2011
      Posts : 547
      Rep Power : 488
      Likes Received
      81
      Likes Given
      366

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      namwomba Mungu ampe mh. Mch. Msigwa maisha marefu mpaka ukombozi wa nchi upatikane, daima na milele, Amina.

    6. #24
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,466
      Rep Power : 19781
      Likes Received
      4294
      Likes Given
      1229

      Default

      Quote By Starn
      Kazi aliyotumwa kuifanya hapa duniani imemshinda sasa kajikuta yupo sehemu ambayo hakutakiwa kuwepo. Anaanza kuongea utumbo. ni rahisi binadamu kumsikiliza kiongozi wa dini kuliko viongozi wa nchi, na yeye ameacha kuchunga kondoo kwa kutafuta uongozi wa nchi. Rudi kafanye kazi ya Mungu kaombee wazinzi ili wapate kumrudia Mungu.
      akili ndogo kuongoza kubwa we can expect this

    7. #25
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,466
      Rep Power : 19781
      Likes Received
      4294
      Likes Given
      1229

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Cdm nooooooooooooooooooooooooooooo oooooooomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa aaaaa

      kila mbunge anatema nondo mbayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa aaaaaaaaaaaa

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      Njowepo's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 26th February 2008
      Location : Santiago
      Posts : 7,601
      Rep Power : 22056
      Likes Received
      995
      Likes Given
      777

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Starn kumbuka ata Melkizedek alikuwa kuhani na mfalme wa Salem!
      Na pia kumbuka wabunge ni sehemu ya Kondoo ambao wanatakiwa kuchungwa!

      "Problems can not be solved by the same level of thinking that creates them” this was my favourite part on a seroius note problems currently Tz is invlved in most of them can not be solved by CCM as the rulling part!
      WB Tanzania lead economist Jacques Morisset said the GDP doubled in 10 years, but it has failed to produce any significant decline in poverty levels.

    10. #27
      wade kibadu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 102
      Rep Power : 379
      Likes Received
      5
      Likes Given
      11

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Msigwa ni mbunge makini siku zote nikiandika post kuhusu msigwa huwa nasisitiza
      :MSIGWA NI MBUNGE MAKINI:
      hotuba nzima ipo makini kama alivyo yeye na umakini wake BUT kwa UNTHINKABLE PEOPLE THEY WILL SAY THAT THERE IS NOTHING IN THE SPEECH OF MSIGWA,IF THAT YOU WILL BE DEADLY WRONG FOR THAT MENTALITY. Kupiti speech ya msigwa kama wewe ni mbunge jipime na msigwa hasa wabunge wa sisisisisisisisisisisisisis emuemuemuemuemuemuemuemu.
      Last edited by wade kibadu; 5th July 2012 at 14:30.

    11. #28
      Hebron Caleb's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th June 2012
      Posts : 171
      Rep Power : 384
      Likes Received
      43
      Likes Given
      3

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Dear All,
      Can i get the cv of this man of God. He can take us very far, we are tired of doing the same thing in the same way expecting different results.

    12. #29
      Hebron Caleb's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th June 2012
      Posts : 171
      Rep Power : 384
      Likes Received
      43
      Likes Given
      3

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Nimeisoma najisikia kulia watanzania tunatumbukizwa shimoni kwani tunaongozwa na vipofu na kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenziwe. Ni mpaka ccm waamke wamtoe mtu kama Mwigulu aache upuuzi wake mbele ya kadamnasi.

    13. #30
      tabu kuishi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st June 2012
      Posts : 211
      Rep Power : 393
      Likes Received
      12
      Likes Given
      10

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Quote By starn
      kazi aliyotumwa kuifanya hapa duniani imemshinda sasa kajikuta yupo sehemu ambayo hakutakiwa kuwepo. Anaanza kuongea utumbo. Ni rahisi binadamu kumsikiliza kiongozi wa dini kuliko viongozi wa nchi, na yeye ameacha kuchunga kondoo kwa kutafuta uongozi wa nchi. Rudi kafanye kazi ya mungu kaombee wazinzi ili wapate kumrudia mungu.
      hivi wewe timamu kweli wewe ulivyozaliwa ulikuwa umeshapangiwa kazi toka tumboni mwa mama yako?tena ingewezekana viongozi wetu wengi wangekuwa ni viongozi wa dini yawezekana nchi ingekuwa mbali,maana hofu ya mungu ingewatafuna siyo hiyo mijizi yenu inayony'ata bila kupuliza

    14. #31
      Starn's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th October 2011
      Posts : 376
      Rep Power : 524
      Likes Received
      51
      Likes Given
      42

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Quote By tabu kuishi
      hivi wewe timamu kweli wewe ulivyozaliwa ulikuwa umeshapangiwa kazi toka tumboni mwa mama yako?tena ingewezekana viongozi wetu wengi wangekuwa ni viongozi wa dini yawezekana nchi ingekuwa mbali,maana hofu ya mungu ingewatafuna siyo hiyo mijizi yenu inayony'ata bila kupuliza
      Ungekuwa unahudhuria makanisani na kichwa chako kingekuwa sawa ungesikia wachungaji wakisema wametumwa na Mungu kufanya kazi hiyo.

    15. #32
      KALYOVATIPI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th August 2011
      Posts : 1,184
      Rep Power : 590
      Likes Received
      136
      Likes Given
      0

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Bado watajambamaputo sana magamba

    16. #33
      kitero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st February 2012
      Location : Kaskazini
      Posts : 516
      Rep Power : 469
      Likes Received
      97
      Likes Given
      48

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      yani mashine za CDM na mashine nyingine zilizopo nje zikiingia bungeni zote then wakapata spika fear na dani kunawabunge watakaotoka nje wenyewe maana hakuna wakuweza kupangua hoja zao

    17. #34
      blue arrow's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 236
      Rep Power : 407
      Likes Received
      10
      Likes Given
      3

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      huyu jamaaa anazidi kukomaa kisiasa hasa kadri anavyoendelea kukaa bungeni.
      Namkubali sana huyu kamanda

    18. #35
      ndenga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th December 2010
      Location : Kigamboni New City
      Posts : 1,049
      Rep Power : 636
      Likes Received
      269
      Likes Given
      84

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Quote By Starn
      Kazi aliyotumwa kuifanya hapa duniani imemshinda sasa kajikuta yupo sehemu ambayo hakutakiwa kuwepo. Anaanza kuongea utumbo. ni rahisi binadamu kumsikiliza kiongozi wa dini kuliko viongozi wa nchi, na yeye ameacha kuchunga kondoo kwa kutafuta uongozi wa nchi. Rudi kafanye kazi ya Mungu kaombee wazinzi ili wapate kumrudia Mungu.
      Mbona hata hii anayofanya ni kazi ya mungu pia mkuu. Hapa amabalisha approach tu lakini zote ni kazi za Mungu wala sioni kama ameacha, tena hii approach ndio inawafikia wengi zaidi na ina impact kubwa kwa nchi na jamii yake.

    19. #36
      Fidel80's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2008
      Location : UVUNGUNI
      Posts : 19,024
      Rep Power : 9492
      Likes Received
      3149
      Likes Given
      1224

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Nondo kama hizi magamba wao wanaona kama ni mashudu kwao zinaingia sikio la kulia na kutokea sikio la kushoto
      **^^+..Ukiuza Utumbo usiogope nzi..+^^**
      Chuda Raha
      Email: [email protected]

    20. #37
      Ramso5's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th December 2011
      Posts : 39
      Rep Power : 383
      Likes Received
      5
      Likes Given
      0

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      Kwa kweli inasisimua.sikubahatika kuisikiliza.inasikitisha ujumbe kama huu unapuuzwa na matokeo yake utumbo wa kina mwigulu unajadiliwa zaidi na kuacha mambo ya muhimu kama haya.Nchi hii tunaipeleka wapi?

    21. #38
      SoNotorious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th September 2011
      Posts : 750
      Rep Power : 507
      Likes Received
      184
      Likes Given
      241

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      msigwa is next level of thinking, ulikuwa wapi mchungaji? una akili za ki einstain.

    22. #39
      kilawe's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 6
      Rep Power : 361
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default re: Mch. Msigwa 'afyatuka' Bungeni...

      This is wonderful speech which I never heard it before, big up Msigwa! Know I agree that Msigwa, Lisu, Mnyika and Mdee = 250 CCM MP's..

    23. #40
      DCONSCIOUS's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th October 2010
      Posts : 297
      Rep Power : 497
      Likes Received
      85
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By Starn
      Kazi aliyotumwa kuifanya hapa duniani imemshinda sasa kajikuta yupo sehemu ambayo hakutakiwa kuwepo. Anaanza kuongea utumbo. ni rahisi binadamu kumsikiliza kiongozi wa dini kuliko viongozi wa nchi, na yeye ameacha kuchunga kondoo kwa kutafuta uongozi wa nchi. Rudi kafanye kazi ya Mungu kaombee wazinzi ili wapate kumrudia Mungu.
      Kwan mfalme daudi alikuaje?

    Page 2 of 4 FirstFirst 1234 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...