Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

    Report Post
    Page 5 of 8 FirstFirst ... 34567 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 151
    1. #1
      Sigma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2011
      Location : The 2nd House on the Left
      Posts : 4,470
      Rep Power : 1379
      Likes Received
      994
      Likes Given
      664

      Default MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Ni baada ya mabadiliko ya hali ya Ulimboka.

      Wagonjwa waliokwishalipia tu ndo wanaonwa leo.

      Emergence yasimama.

      Source: Mimi niko ground zero

      UPDATE:
      Kutoka gazeti la Mwananchi
      Huduma za matibabu MOI zasimama tena
      Taarifa za kutatanisha kuhusiana na hali ya Dk. Ulimboka, zilisababisha kusitishwa kwa huduma za matibabu katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) baada ya madaktari karibuni wote kwenda katika mkutano wa dharura kujadili tukio hilo.

      Habari za kuaminika kutoka MOI, zimethibisha kuwa taarifa za kuzidiwa na hata kuzuka kwa habari nyingine kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, ziliwachanganya kwa kiasi kikubwa madaktari hao, ambao walilazimika kusitisha huduma na kuwapangia wagonjwa tarehe nyingine za kurudi.

      Kutokana na hatua hiyo ya madaktari, wagonjwa waliofika MOI baada ya kusikia kwamba huduma zimerejea, walishindwa kupata tiba badala yake waliandikishwa majina, wakalipia na kupewa tarehe ya kurudi kwa madai kwamba hakuna madaktari wa kuwahudumia.

      Taarifa ya kurejea kwa madaktari hao ilitolewa juzi hospitalini hapo jana na Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Balozi Charles Mtalemwa na kusisitiza kwamba hospitali hiyo haiko katika mgomo kwa sasa.

      Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa waliokosa tiba, walidai kuchoshwa na usumbufu huo huku wakiwaomba madaktari hao kurejea kazini.

      “Nimekuja hapa tangu saa moja kulikua na foleni; wenzetu waliowahi walionana na madaktari lakini ilipofika saa nne tukaambiwa wote tuliojiandikisha turudi Alhamisi ijayo kwa sababu madaktari wanaenda kwenye kikao,” alisema Abdallah Haji mkazi wa Kimara.

      Kwa upande wake Jenipher Suka alisema inasikitisha kuona hivyo kwa sababu mama yake ambaye ni mgonjwa mkazi wa Dodoma amekuja akitegemea kupata tiba matokeo yake ameambiwa arudi tarehe 10 mwezi huu kwa kuwa hakuna madaktari kwa sasa.

      “Kwa nini serikali isiseme ukweli maana tunahangaika kuja mpaka huku halafu hakuna huduma? Vyombo vya habari vimetangaza kwamba mgomo umesitishwa lakini bado wanatudanganya wananchi kwa faida ya nani?” alilalamika Jenipher.

      Akizungumza kwa sharti la kutochapisha jina lake gazetini mmoja wa maofisa waandamizi wa hospitali hiyo alikiri kutokuwepo kwa huduma baada ya madaktari kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Unajua huduma zinazoendelea kwa sasa ni kliniki na upasuaji kwa waliowahi lakini hawa madaktari wamechanganyikiwa baada ya daktari mwenzao aliyeongozana na Dk. Ulimboka kuwaeleza kwamba hali ya mgonjwa ni mbaya mno.

      Kukosekana kwa huduma kulichangiwa na madaktari wanafunzi ambao hupokea na kuwahudumia wagonjwa kuwa katika maandalizi ya mitihani ya mwisho wa mwaka itakayoanza Jumatatu ya Julai 9, 2012 hivyo kusababisha huduma utoaji wa huduma kutokuwepo kabisa.
      Daudi Mchambuzi likes this.


    2. #81
      GeniusBrain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Location : CHADEMA Makao Makuu
      Posts : 3,842
      Rep Power : 1155
      Likes Received
      194
      Likes Given
      0

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By Froida View Post
      Si ndio maana wamemuachia Muhimbili yake hawana shida na mshahara wake akawaleta hao wa Iran waliomhonga suti watibu wananchi
      Well done , ndivyo wanavyotakiwa kufanya na mie nawapongeza kwa hatua yao hiyo, ila mpaka sasa hakuna aliyeandika barua yakuacha kazi , na naomba uwashauri sasa waandike barua ili km kuna mafao yao yaweze kuwa processed , wapewe na waondoke wakatafute maslahi wayatakayo.
      Manyi likes this.

    3. #82
      SHEMGUNGA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th January 2012
      Posts : 334
      Rep Power : 441
      Likes Received
      21
      Likes Given
      0

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Oyoo! walimu lin jama tunasubiri? je wafanyakaz? vp kuhusu wanafunz? duu mkulima mbona kimya? na bado bas ziendao mkoan

    4. MTK is online now
      MTK
      #83
      MTK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th April 2012
      Posts : 1,002
      Rep Power : 4513
      Likes Received
      317
      Likes Given
      365

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By Kengemumaji View Post
      Kwani afya ya Ulimboka ni muhimu sana kuliko afya za wagonjwa walioko hapo muhimbili?
      Tafakari!! utapata jibu.

    5. #84
      Nyakageni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st February 2011
      Posts : 5,581
      Rep Power : 1612
      Likes Received
      817
      Likes Given
      52

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      piganieni haki yenu!

    6. #85
      wakuziba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th June 2012
      Posts : 123
      Rep Power : 585
      Likes Received
      42
      Likes Given
      43

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      mi nilikua muhimbili mida ya asubuhi kujionea mwenyewe kinacho endelea. nimefanya ukaguzi wangu kama raia mwenye haki hiyo. mbona kazi inaendelea kama kawaida. madaktari waliovaa makoti meue nimewaona wengi. nimehoja baadhi ya wagonjwa wanahudumiwa. labda kama mgomo umeanza mida hii!

      jambo lingine ni kwamba wale madaktari ni wasomi. sidhani kama wanaweza kukubali kisha baada ya muda wakagoma tena. tuache kupotosha umma wa watanzania
      Manyi likes this.


    7. #86
      Mtumpole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2010
      Location : Dreamland
      Posts : 547
      Rep Power : 556
      Likes Received
      102
      Likes Given
      333

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By Dumela Mbegu View Post
      Msimamo mbona JK aliisha utoa kwenye hotuba yake ? alisema hawana haja yakugoma na kumsumbua mwajiri kuwaandikia barua nk, wao waache kazi waende kwenye maslahi bora wayatakayo,.....
      Yaani awa madaktari kama wangeitisha mgomo wa kutaka bei za bidhaa na kodi zipunguzwe tungewaelewa ila wamekuwa wabinafsi sana, nadhani sio kosa lao ila kumbukeni hii awamu ya JK imezalisha vichaa wengi nadhani kutokana na ugumu wa maisha.
      Mwenye dhambi hana raha

    8. #87
      mopaozi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2010
      Posts : 2,564
      Rep Power : 785
      Likes Received
      274
      Likes Given
      51

      Default

      Quote By pgasper View Post
      Homa inapanda na kushuka,
      Wananchi sasa ndo watagoma barabarani kwa niaba ya madokta
      Peleka mawazo ya ndumu na viroba huko.WAGOME wananchi ili iweje na wagome nini usitufanye na sisi mapoyoyo kama nyie CDM

    9. #88
      aduwilly's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th March 2009
      Posts : 718
      Rep Power : 667
      Likes Received
      111
      Likes Given
      39

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      7.7 m kwa alietoka direct from school, je mwenye miaka 30 ya uzoefu analipwa shilingi ngapi?

      Tafakari chukua hatua

      say no to boycott, say no to mob psychology

      say yes to humanity, say yes to logical thinking

    10. #89
      yutong's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th April 2011
      Posts : 1,364
      Rep Power : 690
      Likes Received
      244
      Likes Given
      99

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By Dumela Mbegu View Post
      Hayo maslahi wanayoyataka Rais JK aliisha waambia hayawezekani, na akawapa na suluhisho kuwa kama hayawezekani na wao waache kazi, mbona kitu ni rahisi tu na ww kwa nn usitumie muda wako kuwashauri waache kazi tu?
      Mbona yeye na mawaziri wake wamekuwa wakitakiwa kujiuzuru hawajiuzuru/hawataki unadhani kwa nini? hebu tafakari hapo?
      Sign of Victory - R. Kelly

    11. #90
      Froida's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Posts : 3,854
      Rep Power : 1343
      Likes Received
      758
      Likes Given
      153

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By Dumela Mbegu View Post
      Well done , ndivyo wanavyotakiwa kufanya na mie nawapongeza kwa hatua yao hiyo, ila mpaka sasa hakuna aliyeandika barua yakuacha kazi , na naomba uwashauri sasa waandike barua ili km kuna mafao yao yaweze kuwa processed , wapewe na waondoke wakatafute maslahi wayatakayo.
      Waandike barua kwa nani wao siwameondoka Huyo Mbuzi wako Kikwete si awafukuze hana jpya amebaki kutumbua mimacho he has failed the nation poor leader

    12. #91
      Lubaluka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th May 2009
      Posts : 474
      Rep Power : 608
      Likes Received
      22
      Likes Given
      19

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Nadhani sio kujiunga tena na mgomo, la hasha mgomo bado unaendele na hukuwai kwisha toka umeanza!!!! na kwa sasa Lugalo imepewa hadhi ya hospitali ya rufaa....haaaa!!! kuokoa jahazi....!!!!
      Always The Silence of Our Friends Hurts more than the Noise of Our Enemy.

    13. #92
      yutong's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th April 2011
      Posts : 1,364
      Rep Power : 690
      Likes Received
      244
      Likes Given
      99

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By Dumela Mbegu View Post
      Hayo maslahi wanayoyataka Rais JK aliisha waambia hayawezekani, na akawapa na suluhisho kuwa kama hayawezekani na wao waache kazi, mbona kitu ni rahisi tu na ww kwa nn usitumie muda wako kuwashauri waache kazi tu?
      msiongee kwa ushabiki angalieni hali halisi hata hao anajeshi wenyewe wanahali mbaya usifikiri kuwa wanaraha sana. Taaluma za watu ziheshimike sasa wanateua hospitali ya Lugalo kuwa ya Rufaa je inawataalamu wenye sifa za Rufaa? wanavifaa? Kama walishindwa kununua vyombo kuweka muhimbili je wataweza kuweka Lugalo? Ama nini maana ya Hospitali kuitwa ya Rufaa?
      Sign of Victory - R. Kelly

    14. #93
      Froida's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Posts : 3,854
      Rep Power : 1343
      Likes Received
      758
      Likes Given
      153

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By yutong View Post
      msiongee kwa ushabiki angalieni hali halisi hata hao anajeshi wenyewe wanahali mbaya usifikiri kuwa wanaraha sana. Taaluma za watu ziheshimike sasa wanateua hospitali ya Lugalo kuwa ya Rufaa je inawataalamu wenye sifa za Rufaa? wanavifaa? Kama walishindwa kununua vyombo kuweka muhimbili je wataweza kuweka Lugalo? Ama nini maana ya Hospitali kuitwa ya Rufaa?
      Juzijuzi hapa wajerumani ndio waliiboresha Lugalo hata grade one haizidi vyumba 20

    15. #94
      Ndakilawe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2011
      Location : Kumasi
      Posts : 481
      Rep Power : 499
      Likes Received
      53
      Likes Given
      64

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      hatari hatari, maisha ya ndugu zetu hatarini....

    16. #95
      BornTown's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th May 2008
      Location : ???
      Posts : 1,484
      Rep Power : 868
      Likes Received
      283
      Likes Given
      104

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By afwe View Post
      MOI hawakujua kuwa kurudi jana kazini ilikuwa ni mbinu ya kukatisha mwendelezo wa kutokuwepo kazini kwa zaidi ya siku tatu kinyume cha sheria mwajiriwa anahesabika kuwa amejifukuza kazi. Wanaanza tena leo na wataaendelea na mgomo mpaka wiki ijayo ambapo watarudi tena siku moja au mbili wanagoma tena
      Sheria ni siku 5 hujaonekana kazini unajifukuzisha kazi walishaifanyia marekebisho na imeshaanza kutumika muda mrefu, kuwa usipoonekana kazini siku 5 mfululuzo umejifukuzisha kazi. So walichofanya MOI n kuonekana kazini then wanarudi tena kwenye A kama wameanza mgomo leo unaesabu siku 5 za kazi wanarudi tena mchezo huo wataucheza weee hadi watakapo pata majibu ya matakwa yao

      Crashwise likes this.
      "DONT BE A WOMAN THAT NEEDS A MAN BE A WOMAN A MAN NEEDS!!!!"

    17. #96
      Precise pangolin's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 4th January 2012
      Posts : 5,761
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1609
      Likes Given
      684

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By Dumela Mbegu View Post
      Msimamo mbona JK aliisha utoa kwenye hotuba yake ? alisema hawana haja yakugoma na kumsumbua mwajiri kuwaandikia barua nk, wao waache kazi waende kwenye maslahi bora wayatakayo, shida iko wapi ? na kwa nn usiwashauri wafuate ushauri wa Rais wakuacha kazi?
      Waache kazi kwasababu ya udhaifu wa mtu ambaye ameshindwa kutawala?

    18. #97
      yutong's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th April 2011
      Posts : 1,364
      Rep Power : 690
      Likes Received
      244
      Likes Given
      99

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By Lubaluka View Post
      Nadhani sio kujiunga tena na mgomo, la hasha mgomo bado unaendele na hukuwai kwisha toka umeanza!!!! na kwa sasa Lugalo imepewa hadhi ya hospitali ya rufaa....haaaa!!! kuokoa jahazi....!!!!
      Ni rahisi tu mbona; sekondari nyingi sasa hivi zinaitwa vyuo, shule za msingi nyingi sasa zinaitwa sekondari, vyuo vingi sasa hivi vinaitwa vyuo vikuu ila hawana majengo na hata vifaa vya maabara hii ndo tanzania bhana. Miji mingi sasa hivi inaitwa majiji. Pale Lugalo wameongeza wodi? maaabara ama wameiita tu ya Rufaa? Tatizo letu la kutibu dalili badala ya chanjo
      MANI likes this.
      Sign of Victory - R. Kelly

    19. #98
      jogi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2010
      Posts : 4,085
      Rep Power : 1237
      Likes Received
      988
      Likes Given
      247

      Default

      Quote By aduwilly View Post
      7.7 m kwa alietoka direct from school, je mwenye miaka 30 ya uzoefu analipwa shilingi ngapi?

      Tafakari chukua hatua

      say no to boycott, say no to mob psychology

      say yes to humanity, say yes to logical thinking
      wewe umesoma na Mwigulu nchemba, nimeambiwa alikuwa anadesa kwako, naamini kwa jinsi mnavyofanana iq.

    20. #99
      Precise pangolin's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 4th January 2012
      Posts : 5,761
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1609
      Likes Given
      684

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By Tume ya Katiba View Post

      Nasisitiza


      Hakuna mgomo muhimbili, after all wagonjwa wa rufaa wanapelekwa LUGALO.
      Vip ule Mgomo wenu wa Sensa bado mmeshikilia ule msimamo wenu? Naona lile zoezi lenu la kujihesabu limekuwa gumu mlikuwa mnafikiri zoezi la sensa ni sawa na kuhesabu vikombe vya kahawa na kashata?

    21. #100
      Crashwise's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2007
      Location : Safarini
      Posts : 13,486
      Rep Power : 19247
      Likes Received
      4202
      Likes Given
      3379

      Default Re: MOI Wajiunga Tena na MGOMO

      Quote By GateCrasher View Post
      Ni baada ya mabadiliko ya hali ya Ulimboka.
      Wagonjwa waliokwishalipia tu ndo wanaonwa leo.
      Emergence yasimama.
      Source: Mimi niko ground zero
      Mimi na familia yangu tunawaunga mkono, komaeni.....................
      Nobody can give you freedom. Nobody can give you equality or justice or anything. If you're a man, you take it.... Malcolm X





    Page 5 of 8 FirstFirst ... 34567 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...