Re: Lisu amwaga tindikali bungeni

By
OSOKONI
Tukiweka ushambenga na ushabiki kando Lissu ana hoja nzito sana kuhusu mustakabali wa taifa na muungano wetu! hizo ndio hoja ambazo mwanasheria mkuu AG Alitakiwa kuzi adress na ku clarify wakati anachangia sio kumrukia prof. Shivji na kuanza kumkashifu lissu! Kuna mgongano mkubwa sana wa kisheria kati ya katiba ya zanzibar ya sasa na katiba ya JMT! Haya mambo yakiendelea kufumbiwa macho yafumuka yenyewe na madhara yake ni makubwa sana kuliko ambavo yangejadiliwa sasa!!
Ujasiri wa Lissu ni kuwa yupo katika kufuata katiba yenu ya Muungano na siku zote anasimamia hapa
sharia hiyo ya Muungano inayobainisha Mamlaka ya JMTz No 15 Ibara ya 9 ya mwaka 1984. Kifungu cha 34. inayonena hivi
34.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano
katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yote
yahusuyo Tanzania Bara.
(2) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu
utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengineyo yote
ambayo Bunge lina mamlaka ya kuyatungia sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya
mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia
juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara,
yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii,
madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa
ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu
madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika
utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.
Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul
Follow Us Here