SIKIKA ni shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza shughuli mbali mbali zenye lengo la kuchochea upatikanaji wa huduma za afya zenye uwiano, viwango na ubora unaokubalika, gharama nafuu na zilizo endelevu. SIKIKA imekuwa mstari wa mbele kufanya tafiti katika sekta ya afya na kuhimiza utekelezaji wa sera, uwajibikaji na upatikanaji wa huduma bora nchini Tanzania.
Kama neno ‘afya’ lilivyo tafsiriwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Mwaka 1948, sera ya afya ya Taifa (Tanzania Health Policy) ya mwaka 2007, nayo pia inatambua ‘afya’ kama hali ya ukamilifu wa binadamu kiakili, kimwili, kijamii na siyo tu kutokuwepo kwa maradhi.
Afya bora ni mhimili wa maendeleo ya mtu binafsi, familia na taifa zima kwa ujumla hasa katika harakati za kuondoa umasikini uliokithiri katika taifa letu.
Katika nchi yetu, mfumo wa utoaji huduma katika sekta ya afya umegawanyika katika ngazi tatu yaani ngazi ya afya ya msingi kama vile zahanati na vituo vya afya, ngazi ya pili kama vile hospitali za wilaya au mikoa na ngazi ya hospitali za rufaa kama vile hospitali ya Muhimbili, Mbeya, Bugando, KCMC na hospitali maalumu kama taasisi ya magonjwa ya kansa ya Ocean Road au hospitali ya magonjwa ya akili ya Milembe.
Hospitali hizi za rufaa hushughulika na magonjwa ambayo ama yameshindikana katika hospitali za ngazi za chini au wataalamu waliopo katika ngazi hizo na vifaa vilivyopo haviwezi kutoa huduma stahili kwa magonjwa hayo.
Hivyo basi, iwapo kutakuwa na matatizo yanayoathiri utendaji wao wa kazi wa kila siku na kwa kuwa wagonjwa walioletwa katika hospitali hizi za rufaa hawawezi kurudishwa kule walikotoka (ngazi za chini), wagonjwa hawa wasio na hatia ndiyo waumiao kutokana na matatizo hayo.
Bofya Link hii kwa taarifa kamili: http://www.sikika.or.tz/sw/publicati...ad.php?uid=235
Huu ni Mfululizo wa Wanaharakati kutoa matamko yao ya kuibana Serikali itatue Mgogoro na Madaktari kwa amani. Tamko hili la 10 pages, limetoa takwimu za kuridhisha na kuonyesha udhaifu mkubwa wa Serikali.

Reply With Quote
Follow Us Here