Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka; Yadaiwa yupo Ujerumani na si Afrika Kusini

    Report Post
    Page 4 of 6 FirstFirst ... 23456 LastLast
    Results 61 to 80 of 106
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,707
      Rep Power : 3660
      Likes Received
      3225
      Likes Given
      473

      Default Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka; Yadaiwa yupo Ujerumani na si Afrika Kusini

      • TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI,
      • RAFIKI YAKE ATOA USHUHUDA MPYA WA JINSI ALIVYOTEKWA


      Waandishi wetu | Mwananchi | 04 July 2012

      WAKATI ikielezwa kwamba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka anatibiwa Afrika Kusini, kuna taarifa kwamba amelazwa katika hospitali moja ya huko Ujerumani.

      Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa Dk Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini lakini alikaa kwa muda mfupi tu kabla ya kupelekwa Ujerumani anakoendelea na matibabu yake sasa.

      Awali, jopo la madaktari waliokuwa wanamtibu Dk Ulimboka hapa nchini lilieleza kuwa baada ya hali yake kuendelea kuwa mbaya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, waliamua kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

      “Ni kweli alikwenda kwanza Afrika Kusini, lakini hapo alipita tu. Ndege ilitua na akaunganisha ndege nyingine kwenda Ujerumani,” kilisema chanzo kimoja cha habari.

      Hata hivyo wakati chanzo hicho kikieleza hivyo, mmoja wa wanafamilia yake, alisema: “Sisi katika level (ngazi) ya familia tunajua yuko Afrika Kusini lakini hii haiwazuii madaktari kumhamishia kwenye hospitali nyingine wanayoona inafaa.”

      Mwanafamilia huyo ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alisema suala la Dk Ulimboka kuhamishiwa Ujerumani si la ajabu kwani anachotafuta ni matibabu ya uhakika.

      Alipoulizwa kuhusu habari hizo, Kiongozi wa Jopo la Madaktari waliokuwa wakimtibu, Profesa Joseph Kahamba alisema: Mimi ndiyo kwanza nasikia, lakini kwa nature (aina) ya tukio lake, si vyema ikaanikwa amepelekwa wapi. Pia si vizuri ikaelezwa yuko wapi ingawa tayari watu wanajua yuko Afrika Kusini.”

      “Kama kiongozi wa jopo la madaktari wanaomtibu Dk Ulimboka ninajua kwamba yuko Afrika Kusini ingawa hata hiyo taarifa tusingependa watu waijue kwa jinsi tukio lilivyokuwa.”

      Mmoja wa madaktari ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alipoulizwa juu ya suala hilo alipinga na kusema; “Habari za aina hiyo mtakuwa mnazipata nyingi, najua mtaandika, ndiyo maana mnaandika madaktari Muhimbili wanafanya kazi wakati si kweli”.

      Alisisitiza kuwa Dk Ulimboka yupo Afrika Kusini anakopatiwa matibabu na kusisitiza kuwa habari alizokuwa nazo tangu juzi jioni ni kwamba anaendelea vizuri.

      Katibu wa Chama cha Taifa cha Madaktari (MAT), Dk Rodrick Kabangila alipoulizwa juu ya hali ya Dk Ulimboka alisema kwa mujibu wa taarifa za juzi jioni alikuwa anaendelea vizuri.

      Alipoulizwa juu ya taarifa za kupelekwa Ujerumani aliguna kisha akasema: “Naomba ieleweke kuwa yupo Afrika ya Kusini kwa matibabu.

      Rafiki asimulia mkasa

      Rafiki wa karibu wa Dk Ulimboka aliyekuwa naye wakati mkasa wa kutekwa ukitokea, Dk. Deogratius Michael ameelezea tukio zima lilivyotokea na kusema ulikuwa wa kitaalamu na ulifanywa na watu wenye ujuzi na mambo hayo.

      Dk Deogratius alisema jana kwamba siku ya tukio walikuwa wametokea kwenye msiba wa ndugu wa mwalimu wao Profesa Yongolo na baada ya msiba walikwenda Viwanja vya Leaders saa moja usiku kuangalia taarifa ya habari na mambo mengine.

      Huko walikutana na madaktari wengine na ilipofika saa 4:00 usiku, Dk Ulimboka aliwaambia kwamba kuna jamaa alikuwa akimtafuta hivyo angependa kwenda kukutana naye.

      “Tukamwuliza anamtafutia nini? Akatueleza kuwa kwa siku tatu huyo jamaa anamtafuta. Wenzangu wakasema asiende mwenyewe na mimi ndiyo nikamsindikiza. Mara ya kwanza huyo jamaa alisema anaitwa Abeid na alisema yuko Sterio, tukaenda huko hatukumkuta tukaenda Hugo hatukumkuta lakini baadaye tukakutana naye maeneo ya Barabara ya Tunis karibu na Ofisi za Ultimate Security.”

      Dk Deogratius alisema wakati wakiendelea na mazungumzo, Abeid alikuwa akitaka kujua nini kinachotakiwa ili kutatua mgogoro uliopo wa madaktari.

      “Wakati tunamalizia mazungumzo nilikwenda msalani, niliporudi Abeid alikuwa akizungumza na simu kila wakati, tuliendelea na mazungumzo hadi tukamaliza na kuanza kuagana,” alisema.

      Alisema wakati wakiagana bado walikuwa wamekaa katika viti pamoja na Abeid... “Ghafla kuna watu walifika na kusema kuwa wanamtaka Dk Ulimboka. Walimchukua na kwenda naye katika gari. Walikuwa watano, walikuwa ‘giant’ (miili mikubwa) na ‘very skilled’ ( wenye uzoefu) wakamchukua Dk Ulimboka wakaenda naye kwenye gari,” alisema Dk Deogratius.

      Alisema wakati huo Abeid alikuwa anakimbia hivyo akamkimbilia ili ampe namba yake ya simu ambayo ingemsaidia kwa mawasiliano.

      “Alinipa namba yake nikampigia muda huohuo lakini nilipokuja kumpigia tena sikumpata na mpaka leo hapatikani,” alisema.

      Alisema baada ya tukio hilo alimpigia mke wa Dk Ulimboka na kumweleza na pia alipiga simu polisi kuwaeleza.

      “Nilikwenda polisi kutoa maelezo na nikawapa namba zangu za simu zote ili wanipigie kama watapata chochote, lakini mtu wa kwanza kunipigia asubuhi (kesho yake) alikuwa Juma Mgaza (aliyemwokota Dk Ulimboka) ambaye alinieleza kuwa kuna rafiki yangu amempa hiyo namba na kwamba yuko hoi amepigwa.”

      Alisema baada ya kupata simu hiyo aliwasiliana na watetezi wa haki za binadamu ambao walimtaka waende pamoja na kwamba walipokuwa njiani kuelekea Kituo cha Polisi Bunju alipigiwa simu na polisi wa kituo hicho.

      Kutokana na hali hiyo aliomba iundwe tume huru ikijumuisha wanasheria, madaktari na watu wengine ili ukweli ujulikane.

      Upelelezi wa Polisi
      Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jopo la upelelezi aliloteua hivi karibuni kushughulikia tukio zima la kutekwa kwa Dk Ulimboka litaendelea na kazi yake hadi mwisho na hatasikiliza kelele za wanaodai kutokuwa na imani nalo.

      Alisema madai yanayotolewa na watu mbalimbali akiwemo Dk Ulimboka mwenyewe kuwa hana imani na jopo hilo hazitabadili chochote kwani kinachofanyika hivi sasa ni kazi ya kawaida ya upelelezi ya jeshi hilo... “Hao wanaosema hawana imani na jopo hilo hawana hoja isipokuwa waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake.

      Kiongozi huyo wa mgomo wa madaktari alitekwa na kisha kujeruhiwa vibaya na baadaye kutelekezwa katika Msitu wa Pande.

      Habari hii imeandikwa na Geofrey Nyang’oro, Boniface Meena na Joseph Zablon


    2. #61
      abdulahsaf's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st August 2010
      Posts : 860
      Rep Power : 723
      Likes Received
      123
      Likes Given
      1

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka

      Munapoambiwa Watanzania kuwa ccm ni kundi la MAFIA huleta zarau na kusema ccm ndio mama na ndio Baba, Vitendo hivi vya kuwahujumu wapigania haki Freedom fighter akina Dk Steven Ulimboka na wengine huko Nyuma Mh Mwakiembe ni vitendo vya kijasusi na vyakikatili.

      Tukiruhusu hali hii Tanzania iendelee basi genge la unyama huu zidi ya viongozi wazalendo itakuwa nchi hii haikaliki na tutatoka katika bad na kuingia katika warst , hujuma zote hizi zinaongozwa na usalama wa taifa na kupata baraka zote kwa vigogo wa Serekali.

      Muarubaini pekeyake na dawa mujarabu wa matatizo yaloikumba Tanzania kwa miaka mingi nikuiondowa ccm chama cha majasusi 2015 na Chama cha democrasia na maendeleo Chadema kuchukuwa nchi.

    3. #62
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,798
      Rep Power : 19852
      Likes Received
      4414
      Likes Given
      1744

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka

      Heeee mungu mnusuru kijana wako!

    4. #63
      Ndekirhepva's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th May 2012
      Location : Lubumbash
      Posts : 329
      Rep Power : 422
      Likes Received
      28
      Likes Given
      92

      Default Re: Dr. Ulimboka ahamishiwa Ujerumani.

      kwani BBC walimtembelea leo??
      au lini????/

    5. #64
      Kirode's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th March 2011
      Posts : 1,117
      Rep Power : 640
      Likes Received
      65
      Likes Given
      38

      Default

      Bbc wamekuhakkikishia vipi wao ni mdr. Mbona unashilia sana afya yake ni mbaya we ni mungu. Mwachie mungu uhai wa dr. Uli
      Quote By PJ View Post
      Habari za uhakika yuko Africa kusini Kwenye coma, according to BBC this morning.

      His condition is critical

    6. #65
      Elli's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 17th March 2008
      Location : Kijito-Upele
      Posts : 9,028
      Rep Power : 2646
      Likes Received
      2321
      Likes Given
      2103

      Default Re: Dr. Ulimboka ahamishiwa Ujerumani.

      Msimamo wangu ni ule ule, hata kama yeye atakufa leo (MUNGU epusha) au kesho au ataishi daima, bado chachu ya ukombozi na uonevu uliofanywa na serikali dhidi yake akiwakilisha mateso ya wengi tuliyowahi kuyapata, tunayoyapata na tutakayoyapata hayataishia kwake.

      Ni mbegu bora na ya ukombozi, at least tutakua na mtu wa ku-refer kwa kizazi hiki na kizazi kijacho, kwamba serikali ya CCM iliyatenda haya, tumeutangazia ulimwengu na hatutaacha kuusema ukweli.

      MUNGU wangu naomba amrehemu Ulimboka, wewe ndio mwenye uhai wetu na sio mwanadamau awaye yote na kama nikifa leo kwa kuuliwa basi pia wewe MUNGU ni Mapenzi yako na kwamba waweza ruhusu jambo hilo ili jambo kubwa zaidi liweze kutokea kwa faida ya wengi zaidi.
      franksarry likes this.
      ...but what MAN is entirely without Evil intent in the Silence of his Soul???


    7. #66
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,053
      Rep Power : 14671
      Likes Received
      2955
      Likes Given
      2099

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka; Yadaiwa yupo Ujerumani na si Afrika Kusini

      Quote By ruttashobolwa View Post
      what does that assasination attempt help us?

      We know u don care but soon he will be back, i know you will get angry to see him walking and talking.
      Ask those who are meeting with doctors in Dodoma guest houses.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    8. #67
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,053
      Rep Power : 14671
      Likes Received
      2955
      Likes Given
      2099

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By Ronal Reagan View Post
      Zomba, si serikali yako sikivu imesema hakuna mgomo na madaktari wote wako kazini? sasa hao unaosema wameumizwa (kufa?) ni nini kimesababisha maumivu/vifo vyao? Maana kwa mujibu wa taarifa zote za serikali hakuna mgomo wa madaktari.
      Sasa hivi ukiwa haupo kazini hauna kazi, sasa ambae hana kazi anagoma? Fikiri!
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    9. #68
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,053
      Rep Power : 14671
      Likes Received
      2955
      Likes Given
      2099

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By reformer View Post
      Mtafute Lusinde, Maji marefu na Komba wakufindishe kiingereza
      Ungejuwa maana ya ku "fill" pity na si ku "feel" pity usingesema unayoyasema, naona wewe huelewi nilichokiandika. Kajifunze.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    10. #69
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,053
      Rep Power : 14671
      Likes Received
      2955
      Likes Given
      2099

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By reformer View Post
      Kwani mwanaume anayeweza kukuna vizuri ni Uli peke yake..si utafute mwingine?
      Mwanamme anakwenda "kuyamaliza" klabu? kwi kwi kwi teh teh teh!
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    11. #70
      Precise pangolin's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 4th January 2012
      Posts : 5,761
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1609
      Likes Given
      684

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba View Post
      Mwanamme anakwenda "kuyamaliza" klabu? kwi kwi kwi teh teh teh!
      Mkuu zomba jaribu kubadilika wewe hapa jamvini ni mgovi na huwa unafurahi ukiona watu wakipata ban zinazo sababishwa na wewe

    12. #71
      theROOM's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 100
      Rep Power : 458
      Likes Received
      35
      Likes Given
      54

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba View Post
      So what?
      The Government seems to be the Prime suspect..
      If you can't explain it simply, you don't understand it well enough. Albert Einstein

    13. #72
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,053
      Rep Power : 14671
      Likes Received
      2955
      Likes Given
      2099

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By theROOM View Post
      The Government seems to be the Prime suspect..
      So what?
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    14. #73
      Wile GAMBA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th September 2011
      Posts : 734
      Rep Power : 539
      Likes Received
      213
      Likes Given
      760

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka; Yadaiwa yupo Ujerumani na si Afrika Kusini

      Zomba sukutaka kabisa kuingilia mabishano yenu, lakji katiak kufuatilia, tukiacha mambo ya kishabiki lazima unatatizo fulani katika ubongo wako siyo kawaida au unayafanya haya kwa maslai binafsi, lakini unatusaidia sana kuonesha selikali imehusimka moja kwa moja na swala hili lakishetani, Mungu lazima atajibu, pamoja na kova kung'ang'ania kuchunguza watu wasio na imani nae, kwa mtu mwenye akili timamu iliswala lina sikitihsa sana na ni aubu kubwa sana kwa serikali

    15. #74
      SUWI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th September 2010
      Posts : 491
      Rep Power : 541
      Likes Received
      21
      Likes Given
      65

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba View Post
      So what?
      Anayeua kwa upanga atauliwa kwa upanga....kazi ya kutoa roho ya mtu ni ya Muumba.. Watch out!
      Refer kwa Saddam Hussein na wengine wanaofanana na wewe..

      Mnataka kutoa roho ya Mtu anayedai haki yake tena ndani ya nchi yake!!... shame on you.. kama alikuwa anafanya kinyume na sheria kwa nini asipelekwe mahakamani badala ya kutaka kumuua.

      Siku moja mtatoa hesabu za matendo ya kazi za mikono yenu mbele ya muumba. Kila mtu ataonja mauti kumbuka,,, tena hujui saa wala wakati...

      Koma kabisa kushabikia mauaji.

    16. #75
      reformer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd July 2011
      Posts : 296
      Rep Power : 459
      Likes Received
      79
      Likes Given
      6

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba View Post
      Ungejuwa maana ya ku "fill" pity na si ku "feel" pity usingesema unayoyasema, naona wewe huelewi nilichokiandika. Kajifunze.
      Naona unazidi kuanika ukilaza wako na kupigilia mstari kuwa akili zako ni sawa na akina Lusinde na maji marefu..that could only be correct if used it as "filled with pity, anger, fear etc.

    17. #76
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,053
      Rep Power : 14671
      Likes Received
      2955
      Likes Given
      2099

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By SUWI View Post
      anayeua kwa upanga atauliwa kwa upanga....
      kazi ya kutoa roho ya mtu ni ya Muumba.. Watch out!
      Refer kwa Saddam Hussein na wengine wanaofanana na wewe..
      Mnataka kutoa roho ya Mtu anayedai haki yake tena ndani ya nchi yake!!... shame on you.. kama alikuwa anafanya kinyume na sheria kwa nini asipelekwe mahakamani badala ya kutaka kumuua.. Siku moja mtatoa hesabu za matendo ya kazi za mikono yenu mbele ya muumba. Kila mtu ataonja mauti kumbuka,,, tena hujui saa wala wakati...

      Koma kabisa kushabikia mauaji............
      Kumbuka, hayo yanaanzia kwa wanaouwa wagonjwa kwa migomo yao isiyo na maana.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    18. #77
      Tume ya Katiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Location : Chumbuni-Zanzibar
      Posts : 2,840
      Rep Power : 0
      Likes Received
      565
      Likes Given
      295

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka; Yadaiwa yupo Ujerumani na si Afrika Kusini

      Kuendelea Kuzungumza kuhusu ULIMBOKA ni kupoteza muda.

      Ninawashauri, tujielekeze zaidi katika masuala ya maendeleo na yenye manufaa kwa taifa.

      Mgomo umeisha jamani.
      zomba likes this.

    19. #78
      Miya's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 29th March 2011
      Posts : 194
      Rep Power : 455
      Likes Received
      28
      Likes Given
      11

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Nani kawauwa wagonjwa?wagonjwa wamekufa kwa kukosa huduma bora za matibabu ila serikali ya kikwete imemchezea rafu Dr.Ulimboka.

    20. #79
      daby mouser's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 9th February 2012
      Posts : 129
      Rep Power : 396
      Likes Received
      20
      Likes Given
      15

      Default

      Quote By zomba View Post
      Aliyepotea ni huyo asiyejijuwa saa hizi yuko hali gani wala wapi. Na mliyepotea zaidi ni nyinyi mnaoshadidia wagonjwa wazidi kukosa matibabu na mnaodhani kuwa alikuwa akifanya jambo la maana.

      Mnashindwa kufikiri kitu kidogo tu, ni nini kilimpeleka usiku klabu ya ulevi kwa kuitwa "tuyamalize"? Fikiri na uwe mkweli wa nafsi yako.
      haahahah zomba ungekuwa karib ningekupa glas ya chipumu..unanipa raha sana...big salutation!
      zomba likes this.

    21. #80
      Kazakuku's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th June 2011
      Posts : 255
      Rep Power : 458
      Likes Received
      10
      Likes Given
      1

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka; Yadaiwa yupo Ujerumani na si Afrika Kusini

      acheni migomo jaman madaktal wenzenu walimu mbona wametulia..

    Page 4 of 6 FirstFirst ... 23456 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...