Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka; Yadaiwa yupo Ujerumani na si Afrika Kusini

    Report Post
    Page 3 of 6 FirstFirst 12345 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 106
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,258
      Rep Power : 3566
      Likes Received
      3073
      Likes Given
      463

      Default Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka; Yadaiwa yupo Ujerumani na si Afrika Kusini

      • TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI,
      • RAFIKI YAKE ATOA USHUHUDA MPYA WA JINSI ALIVYOTEKWA


      Waandishi wetu | Mwananchi | 04 July 2012

      WAKATI ikielezwa kwamba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka anatibiwa Afrika Kusini, kuna taarifa kwamba amelazwa katika hospitali moja ya huko Ujerumani.

      Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa Dk Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini lakini alikaa kwa muda mfupi tu kabla ya kupelekwa Ujerumani anakoendelea na matibabu yake sasa.

      Awali, jopo la madaktari waliokuwa wanamtibu Dk Ulimboka hapa nchini lilieleza kuwa baada ya hali yake kuendelea kuwa mbaya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, waliamua kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

      “Ni kweli alikwenda kwanza Afrika Kusini, lakini hapo alipita tu. Ndege ilitua na akaunganisha ndege nyingine kwenda Ujerumani,” kilisema chanzo kimoja cha habari.

      Hata hivyo wakati chanzo hicho kikieleza hivyo, mmoja wa wanafamilia yake, alisema: “Sisi katika level (ngazi) ya familia tunajua yuko Afrika Kusini lakini hii haiwazuii madaktari kumhamishia kwenye hospitali nyingine wanayoona inafaa.”

      Mwanafamilia huyo ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alisema suala la Dk Ulimboka kuhamishiwa Ujerumani si la ajabu kwani anachotafuta ni matibabu ya uhakika.

      Alipoulizwa kuhusu habari hizo, Kiongozi wa Jopo la Madaktari waliokuwa wakimtibu, Profesa Joseph Kahamba alisema: Mimi ndiyo kwanza nasikia, lakini kwa nature (aina) ya tukio lake, si vyema ikaanikwa amepelekwa wapi. Pia si vizuri ikaelezwa yuko wapi ingawa tayari watu wanajua yuko Afrika Kusini.”

      “Kama kiongozi wa jopo la madaktari wanaomtibu Dk Ulimboka ninajua kwamba yuko Afrika Kusini ingawa hata hiyo taarifa tusingependa watu waijue kwa jinsi tukio lilivyokuwa.”

      Mmoja wa madaktari ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alipoulizwa juu ya suala hilo alipinga na kusema; “Habari za aina hiyo mtakuwa mnazipata nyingi, najua mtaandika, ndiyo maana mnaandika madaktari Muhimbili wanafanya kazi wakati si kweli”.

      Alisisitiza kuwa Dk Ulimboka yupo Afrika Kusini anakopatiwa matibabu na kusisitiza kuwa habari alizokuwa nazo tangu juzi jioni ni kwamba anaendelea vizuri.

      Katibu wa Chama cha Taifa cha Madaktari (MAT), Dk Rodrick Kabangila alipoulizwa juu ya hali ya Dk Ulimboka alisema kwa mujibu wa taarifa za juzi jioni alikuwa anaendelea vizuri.

      Alipoulizwa juu ya taarifa za kupelekwa Ujerumani aliguna kisha akasema: “Naomba ieleweke kuwa yupo Afrika ya Kusini kwa matibabu.

      Rafiki asimulia mkasa

      Rafiki wa karibu wa Dk Ulimboka aliyekuwa naye wakati mkasa wa kutekwa ukitokea, Dk. Deogratius Michael ameelezea tukio zima lilivyotokea na kusema ulikuwa wa kitaalamu na ulifanywa na watu wenye ujuzi na mambo hayo.

      Dk Deogratius alisema jana kwamba siku ya tukio walikuwa wametokea kwenye msiba wa ndugu wa mwalimu wao Profesa Yongolo na baada ya msiba walikwenda Viwanja vya Leaders saa moja usiku kuangalia taarifa ya habari na mambo mengine.

      Huko walikutana na madaktari wengine na ilipofika saa 4:00 usiku, Dk Ulimboka aliwaambia kwamba kuna jamaa alikuwa akimtafuta hivyo angependa kwenda kukutana naye.

      “Tukamwuliza anamtafutia nini? Akatueleza kuwa kwa siku tatu huyo jamaa anamtafuta. Wenzangu wakasema asiende mwenyewe na mimi ndiyo nikamsindikiza. Mara ya kwanza huyo jamaa alisema anaitwa Abeid na alisema yuko Sterio, tukaenda huko hatukumkuta tukaenda Hugo hatukumkuta lakini baadaye tukakutana naye maeneo ya Barabara ya Tunis karibu na Ofisi za Ultimate Security.”

      Dk Deogratius alisema wakati wakiendelea na mazungumzo, Abeid alikuwa akitaka kujua nini kinachotakiwa ili kutatua mgogoro uliopo wa madaktari.

      “Wakati tunamalizia mazungumzo nilikwenda msalani, niliporudi Abeid alikuwa akizungumza na simu kila wakati, tuliendelea na mazungumzo hadi tukamaliza na kuanza kuagana,” alisema.

      Alisema wakati wakiagana bado walikuwa wamekaa katika viti pamoja na Abeid... “Ghafla kuna watu walifika na kusema kuwa wanamtaka Dk Ulimboka. Walimchukua na kwenda naye katika gari. Walikuwa watano, walikuwa ‘giant’ (miili mikubwa) na ‘very skilled’ ( wenye uzoefu) wakamchukua Dk Ulimboka wakaenda naye kwenye gari,” alisema Dk Deogratius.

      Alisema wakati huo Abeid alikuwa anakimbia hivyo akamkimbilia ili ampe namba yake ya simu ambayo ingemsaidia kwa mawasiliano.

      “Alinipa namba yake nikampigia muda huohuo lakini nilipokuja kumpigia tena sikumpata na mpaka leo hapatikani,” alisema.

      Alisema baada ya tukio hilo alimpigia mke wa Dk Ulimboka na kumweleza na pia alipiga simu polisi kuwaeleza.

      “Nilikwenda polisi kutoa maelezo na nikawapa namba zangu za simu zote ili wanipigie kama watapata chochote, lakini mtu wa kwanza kunipigia asubuhi (kesho yake) alikuwa Juma Mgaza (aliyemwokota Dk Ulimboka) ambaye alinieleza kuwa kuna rafiki yangu amempa hiyo namba na kwamba yuko hoi amepigwa.”

      Alisema baada ya kupata simu hiyo aliwasiliana na watetezi wa haki za binadamu ambao walimtaka waende pamoja na kwamba walipokuwa njiani kuelekea Kituo cha Polisi Bunju alipigiwa simu na polisi wa kituo hicho.

      Kutokana na hali hiyo aliomba iundwe tume huru ikijumuisha wanasheria, madaktari na watu wengine ili ukweli ujulikane.

      Upelelezi wa Polisi
      Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jopo la upelelezi aliloteua hivi karibuni kushughulikia tukio zima la kutekwa kwa Dk Ulimboka litaendelea na kazi yake hadi mwisho na hatasikiliza kelele za wanaodai kutokuwa na imani nalo.

      Alisema madai yanayotolewa na watu mbalimbali akiwemo Dk Ulimboka mwenyewe kuwa hana imani na jopo hilo hazitabadili chochote kwani kinachofanyika hivi sasa ni kazi ya kawaida ya upelelezi ya jeshi hilo... “Hao wanaosema hawana imani na jopo hilo hawana hoja isipokuwa waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake.

      Kiongozi huyo wa mgomo wa madaktari alitekwa na kisha kujeruhiwa vibaya na baadaye kutelekezwa katika Msitu wa Pande.

      Habari hii imeandikwa na Geofrey Nyang’oro, Boniface Meena na Joseph Zablon

    2. RukaaJuu Final

    3. #41
      reformer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd July 2011
      Posts : 296
      Rep Power : 456
      Likes Received
      79
      Likes Given
      6

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba
      So what?
      Mabumba vp..mbona unawashwa? Tafuta mwanaume akukune.

    4. #42
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1844
      Likes Received
      593
      Likes Given
      413

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Jambo la msingi ni matibabu utata uko wapi wa kuikumba nchi !!!!!!! Udaku newspapers ....

    5. #43
      reformer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd July 2011
      Posts : 296
      Rep Power : 456
      Likes Received
      79
      Likes Given
      6

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By Imany John
      Unadhihirisha usiku waleo ulinyimwa unyumba,kwanini usipeleke hasira kwa mkeo? Au Dr Uli alikuumizia na mkeo?
      Jamaa si rizki..anamuonea wivu mke wa uli

    6. #44
      miss strong's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2012
      Posts : 667
      Rep Power : 480
      Likes Received
      136
      Likes Given
      62

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Mungu amewaumbua,Mliua haohao wauza madin ktk ule msitu lkn hili mmechemsha na ushahid upo!Damu ya mtu haimwagik bure na ukumbuke DKT ULI sio israili mpk mseme wagonjwa wamekufa kwa ajil yke!

    7. #45
      reformer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd July 2011
      Posts : 296
      Rep Power : 456
      Likes Received
      79
      Likes Given
      6

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba
      Silali "mpaka kieleweke". Jee, wewe unalala?
      Kwani mwanaume anayeweza kukuna vizuri ni Uli peke yake..si utafute mwingine?
      zomba likes this.

    8. Miaka 50

    9. #46
      Bishop Hiluka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 1,497
      Rep Power : 5985
      Likes Received
      492
      Likes Given
      154

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba
      Silali "mpaka kieleweke". Jee, wewe unalala?
      Mkuu, mtatoana roho bure kwa mambo yasiyowahusu,
      usilale kwa sababu ya Ulimboka? Pigania kwanza maisha
      yako mengine yatakuja yenyewe...
      It's better to be hated for who you are,
      than to be loved for someone you are not...

    10. #47
      Imany John's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th July 2011
      Posts : 1,971
      Rep Power : 2977
      Likes Received
      471
      Likes Given
      4

      Default

      Quote By HOPECOMFORT
      Then matusi yako yasaida nn sasa!!!Halafu mkiambiwa nyie na chama chenu dhaifu mnausika mnakuja juu??? Duh
      Kama huwezi kumpinga ZOBA,Ungana nae.

    11. #48
      WISDOM SEEDS's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st June 2011
      Location : Sweden
      Posts : 609
      Rep Power : 525
      Likes Received
      113
      Likes Given
      66

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba
      Germany or South Africa, what does that help us? he was sent out of the country by his beloved to try and rescue him from death? or is it his health?
      Does he realize now that many were in his position and could not afford to be even transferred to other hospitals?
      I don't give a damn wherever he is. What does that help us?
      Hizi zote ni frustration za kupanda kwa gharama za maisha zinazosababishwa na serikali
      ya CCM. Soma signature yangu hapo chini utapata jibu!
      "Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, kwa uzembe wa Bunge, na kwa sababu ya upuuzi wa CCM" John Mnyika

    12. #49
      reformer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd July 2011
      Posts : 296
      Rep Power : 456
      Likes Received
      79
      Likes Given
      6

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba
      Humanity? do you call it humanitarian when doctors refuse to treat the sick and ill just because they demand extravagant and luxurious demands? And you want me to fill pity for the evil who leads them?

      Wouldn't they be in a better position to negotiate while treating?
      Mtafute Lusinde, Maji marefu na Komba wakufindishe kiingereza

    13. #50
      Laurence's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th June 2011
      Location : ULIMWENGUNI
      Posts : 2,043
      Rep Power : 1394
      Likes Received
      175
      Likes Given
      41

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Mnapoteza kubishana na huyu KIZIWI Zomba? mpuuzeni huyu kilaza!

    14. #51
      LiverpoolFC's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2011
      Posts : 6,705
      Rep Power : 11284
      Likes Received
      1483
      Likes Given
      574

      Default

      Quote By zomba
      Wewe unajibu kikubwa inatosha. Si mimi, si wewe, si Mtanzania mwingine yeyote, awepo Afrika Kusini, Ujerumani au Uchina inatusaidia nini?

      Mimi nasema sasa ataelewa kuwa uchochezi wake umemfanya ahisi (kama anazo hizo hisia) ni vipi mtu akikosa afya kwa kuumwa anavyokuwa.

      Katika madai 12 aliyoyabuni, 11 ni ya kipato kwa madaktari, sasa hicho kipato kimpe uzima.


      Unatoa mapofu utafikiri unapekechwa!
      Tumia akili ktk kufikiri kubwa jinga wewe!
      Ama unatumika nini?

    15. #52
      Lion's Claws's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 30
      Rep Power : 366
      Likes Received
      14
      Likes Given
      0

      Default Dr. Ulimboka ahamishiwa Ujerumani.

      Kutokana na sababu za kiusalama na watekaji kuzidi kufuatilia hospitali alipo huko South. Source Gazeti la Mwananchi. Naomba wanajamvi mtupashe mkipata ukweli. Mungu ni Mwema na atawaumbua Wahusika mchana kweupe.

    16. #53
      Ndoa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2011
      Posts : 630
      Rep Power : 504
      Likes Received
      120
      Likes Given
      46

      Default Re: Dr. Ulimboka ahamishiwa Ujerumani.

      Leo asubuhi bbc swahili inasema walimtembelea ulimboka south jana. Au kahamaishwa leo?

    17. #54
      Ronal Reagan's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 2,636
      Rep Power : 961
      Likes Received
      615
      Likes Given
      256

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba
      Amewaumiza si wake za watu tu, watoto, wazee, vijana. Kwa ufupi wote waliokosa matibabu kwa uchochezi wake wa kujitafutia umaarufu na tamaa zake binafsi. Sasa hivi anajuwa kuumwa ni nini.

      Matusi hayasaidii, mnajulikana mnapokuwa hamna hoja mnaanza kutukana.
      Zomba, si serikali yako sikivu imesema hakuna mgomo na madaktari wote wako kazini? sasa hao unaosema wameumizwa (kufa?) ni nini kimesababisha maumivu/vifo vyao? Maana kwa mujibu wa taarifa zote za serikali hakuna mgomo wa madaktari.
      Last edited by Ronal Reagan; 5th July 2012 at 09:07.

    18. PJ
      #55
      PJ's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th October 2007
      Location : EVERY WHERE
      Posts : 274
      Rep Power : 648
      Likes Received
      19
      Likes Given
      9

      Default Re: Dr. Ulimboka ahamishiwa Ujerumani.

      Habari za uhakika yuko Africa kusini Kwenye coma, according to BBC this morning.

      His condition is critical
      Victory has a hundred fathers, but defeat is an orphan. Win a hundred and they shower praise on, but lose one and they will forget they ever know you.

    19. #56
      Mbutunanga's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 15th February 2011
      Posts : 182
      Rep Power : 524
      Likes Received
      45
      Likes Given
      65

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba
      Germany or South Africa, what does that help us? he was sent out of the country by his beloved to try and rescue him from death? or is it his health?

      Does he realize now that many were in his position and could not afford to be even transferred to other hospitals?

      I don't give a damn wherever he is. What does that help us?


      Mkuu leo upo bungeni au kwa kikao cha usalama na mikakati ya propaganda?

    20. #57
      Mbutunanga's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 15th February 2011
      Posts : 182
      Rep Power : 524
      Likes Received
      45
      Likes Given
      65

      Default Re: Utata watanda nchi anakotibiwa Ulimboka;TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI

      Quote By zomba
      Wewe unajibu kikubwa inatosha. Si mimi, si wewe, si Mtanzania mwingine yeyote, awepo Afrika Kusini, Ujerumani au Uchina inatusaidia nini?

      Mimi nasema sasa ataelewa kuwa uchochezi wake umemfanya ahisi (kama anazo hizo hisia) ni vipi mtu akikosa afya kwa kuumwa anavyokuwa.

      Katika madai 12 aliyoyabuni, 11 ni ya kipato kwa madaktari, sasa hicho kipato kimpe uzima.
      Du! nyie viongozi sijui ni lini mtajifunza kuchuja mnachokiongea. hebu ona tamko la RAIS wetu kwetu sisi watanzania

      "Kutokana na ukweli huo basi kama mgonjwa anayeona kuwa hawezi kutibiwa katika hospitali ya Serikali bila kulala kwenye kitanda chake, bila kupata vipimo kupitia vifaa bora, bila kupata dawa na hayupo tayari kuona daktari hana vitendea kazi, awe huru kuachana na hospitali za serikali na kwenda kwenye hospitali zinazoweza kumuhudumia hivyo. Hana sababu ya kulalamika ili ashinikize kuboresha kwa miundombinu na vitendea kazi. Asisumbuke, hatapewa huduma hizo"

    21. #58
      promiseme's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th March 2010
      Posts : 1,083
      Rep Power : 683
      Likes Received
      306
      Likes Given
      12

      Default Re: Dr. Ulimboka ahamishiwa Ujerumani.

      Mwenyezi mungu inshallah atampa nafuu..
      "It is better to be hated for what you are then to be loved for what you are not."

    22. #59
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,497
      Rep Power : 19788
      Likes Received
      4313
      Likes Given
      1263

      Default

      Quote By zomba
      Tena sana tu, ametuumizia na kutuulia wagonjwa wetu wengi kwa maslahi yake binafsi, halafu eti alikuwa anakwenda kilabu cha pombe kutatua matatizo ya wagonjwa? Huyo alikuwa anakwenda kupokea rushwa. Halafu bado nimhurumie?
      pole sana kumbe ulikuwa na wagonjwa wengi siku hiyo! Kwani walikufa?

      Ila usijali atapona ili arudi kuendelea kuwatibu wagonjwa wako!

    23. #60
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,497
      Rep Power : 19788
      Likes Received
      4313
      Likes Given
      1263

      Default

      Quote By zomba
      Germany or South Africa, what does that help us? he was sent out of the country by his beloved to try and rescue him from death? or is it his health?

      Does he realize now that many were in his position and could not afford to be even transferred to other hospitals?

      I don't give a damn wherever he is. What does that help us?
      what does that assasination attempt help us?

      We know u don care but soon he will be back, i know you will get angry to see him walking and talking.

    Page 3 of 6 FirstFirst 12345 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...