Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

    Report Post
    Page 1 of 12 12311 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 236
    1. #1
      Return Of Undertaker's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 659
      Rep Power : 541
      Likes Received
      462
      Likes Given
      0

      Default BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Source BBC na Omary Mutasa kutoka Afrika Kusini

      Ni wazi kuwa hali ya Dr. Steven Olimboka ni mbaya na kalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na anapumulia mashine, hajitambui wala haongei.

      Na kulingana na bbc kulingana na hali yake ilivyo hakuruhusiwa na familia yake kumwona na hawakutaka kuongelea swala la kutekwa na kauli ya JK kukana kuhusika.

      Wakati huo huo jeshi la polisi limetoa kauli hii

      ""Upelelezi wa Polisi Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jopo la upelelezi aliloteua hivi karibuni kushughulikia tukio zima la kutekwa kwa Dk Ulimboka litaendelea na kazi yake hadi mwisho na hatasikiliza kelele za wanaodai kutokuwa na imani nalo. Alisema madai yanayotolewa na watu mbalimbali akiwemo Dk Ulimboka mwenyewe kuwa hana imani na jopo hilo hazitabadili chochote kwani kinachofanyika hivi sasa ni kazi ya kawaida ya upelelezi ya jeshi hilo... “Hao wanaosema hawana imani na jopo hilo hawana hoja isipokuwa waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake."""

      Concern
      Ninashaka hapa hivi uchunguzi wa jeahi la polisi kama mimi mtendwa sitaki kwanini unalazimisha wakati sina imani na ulichokiunda na cha ajabu nawe unanambia hata kama hutaki sie tunaendelea.

      Nini kipo nyuma ya pazia la polisiiiiiii???
      Quote By TONGINDI
      Hali ya afya ya Dk. Steven Ulimboka ambaye anatibiwa Afrika Kusini, imebadilika ghafla na kuna habari kuwa yuko mahututi.

      Habari zilizoifikia Tanzania Daima kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi, zimesema kuwa Dk. Ulimboka alikuwa amepoteza fahamu, na juhudi za kuokoa maisha yake zilikuwa zikiendelea chini ya jopo la madaktari bingwa wa nchi hiyo na wale wa Tanzania.

      Inadaiwa kwamba hali ya kiongozi huyo wa jumuiya ya madaktari nchini ambaye alikimbizwa nchini humo wiki iliyopita, awali ilielezwa kuwa inaendelea vema, lakini ghafla ikabadilika na kufikia kiwango cha kupoteza fahamu.

      Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC) alikaririwa akisema kuwa hali ya Ulimboka ilikuwa mbaya, na kwamba kulikuwa na ulinzi na usiri mkubwa kuhusiana na hali hiyo.

      Jijini Dar es Salaam, mmoja wa madaktari aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina, alisema kuwa walipata taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kutoka kwa ndugu yake aliyeko Afrika Kusini kwamba alikuwa yuko kwenye hali mbaya, hali iliyowachanganya mno.

      Mmoja wa madaktari alikiri kupokea taarifa za kuzidiwa kwa mwenyekiti wao kutoka kwa kaka wa Dk. Ulimboka.

      “Leo asubuhi baada ya kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kikaitishwa kikao cha dharura cha madaktari wote tunaelekea huko,” alisema.

      Hata hivyo, majira ya mchana habari zilivuma kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, hali iliyozidi kuzusha wasiwasi mwingi miongoni mwa madaktari, viongozi wa vyama vya kijamii na wananchi wa kawaida waliokuwa wakihaha kupata ukweli wake.

      Uvumi huo hata hivyo, ulikanushwa baadaye na msemaji wa Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa MOI Almasi Jumaa lakini akakiri kupata taarifa za kubadilika kwa hali ya mgonjwa huyo.

      Huduma za matibabu MOI zasimama tena
      Taarifa za kutatanisha kuhusiana na hali ya Dk. Ulimboka, zilisababisha kusitishwa kwa huduma za matibabu katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) baada ya madaktari karibuni wote kwenda katika mkutano wa dharura kujadili tukio hilo.

      Habari za kuaminika kutoka MOI, zimethibisha kuwa taarifa za kuzidiwa na hata kuzuka kwa habari nyingine kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, ziliwachanganya kwa kiasi kikubwa madaktari hao, ambao walilazimika kusitisha huduma na kuwapangia wagonjwa tarehe nyingine za kurudi.

      Kutokana na hatua hiyo ya madaktari, wagonjwa waliofika MOI baada ya kusikia kwamba huduma zimerejea, walishindwa kupata tiba badala yake waliandikishwa majina, wakalipia na kupewa tarehe ya kurudi kwa madai kwamba hakuna madaktari wa kuwahudumia.
      Taarifa ya kurejea kwa madaktari hao ilitolewa juzi hospitalini hapo jana na Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Balozi Charles Mtalemwa na kusisitiza kwamba hospitali hiyo haiko katika mgomo kwa sasa.

      Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa waliokosa tiba, walidai kuchoshwa na usumbufu huo huku wakiwaomba madaktari hao kurejea kazini.

      “Nimekuja hapa tangu saa moja kulikua na foleni; wenzetu waliowahi walionana na madaktari lakini ilipofika saa nne tukaambiwa wote tuliojiandikisha turudi Alhamisi ijayo kwa sababu madaktari wanaenda kwenye kikao,” alisema Abdallah Haji mkazi wa Kimara.

      Kwa upande wake Jenipher Suka alisema inasikitisha kuona hivyo kwa sababu mama yake ambaye ni mgonjwa mkazi wa Dodoma amekuja akitegemea kupata tiba matokeo yake ameambiwa arudi tarehe 10 mwezi huu kwa kuwa hakuna madaktari kwa sasa.

      “Kwa nini serikali isiseme ukweli maana tunahangaika kuja mpaka huku halafu hakuna huduma? Vyombo vya habari vimetangaza kwamba mgomo umesitishwa lakini bado wanatudanganya wananchi kwa faida ya nani?” alilalamika Jenipher.

      Akizungumza kwa sharti la kutochapisha jina lake gazetini mmoja wa maofisa waandamizi wa hospitali hiyo alikiri kutokuwepo kwa huduma baada ya madaktari kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Unajua huduma zinazoendelea kwa sasa ni kliniki na upasuaji kwa waliowahi lakini hawa madaktari wamechanganyikiwa baada ya daktari mwenzao aliyeongozana na Dk. Ulimboka kuwaeleza kwamba hali ya mgonjwa ni mbaya mno.

      Kukosekana kwa huduma kulichangiwa na madaktari wanafunzi ambao hupokea na kuwahudumia wagonjwa kuwa katika maandalizi ya mitihani ya mwisho wa mwaka itakayoanza Jumatatu ya Julai 9, 2012 hivyo kusababisha huduma utoaji wa huduma kutokuwepo kabisa.

      Pinda abanwa
      MJINI Dodoma, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameshindwa kuliambia Bunge endapo serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dk. Ulimboka.

      Waziri Mkuu Pinda, alishindwa kutoa kauli wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (CHADEMA).
      Katika swali lake la nyongeza, Mbowe alisema kumekuwa na ongezeko la vitendo vya mauaji yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi.
      Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alitolea mfano wa tukio la kupigwa kwa wabunge wawili wa CHADEMA mkoani Mwanza na tukio la hivi karibuni la kutekwa na kupingwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Kwa kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio ya mauaji kwa raia wasio na hatia na kumekuwa na hisia kwamba matendo hayo yanafanywa na Jeshi la Polisi. Mfano wa matukio hayo ni pamoja na lile la kupigwa kwa wabunge wawili na hili la hivi karibuni la kutekwa kwa Dk. Ulimboka, tukio ambalo limelichafua taifa; je, serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza matukio hayo?” alihoji Mbowe.

      Akijibu swali hilo, Pinda kwanza alisema sio kweli kwamba tukio la kupigwa kwa Dk. Ulimboka limechafua sifa nzuri ya taifa.
      “Mh. Mbowe, kwanza tukio la Ulimboka sio mfano mzuri sana kwa sababu hakuna mwenye ushahidi wa serikali kuhusika kumteka na kumpiga Dk. Ulimboka.

      “Kama nilivyosema awali, sioni sababu ya serikali kuhusika na kipigo cha Ulimboka ambaye tulikuwa tukishirikiana naye vizuri kwenye vikao vya majadiliano,” alisema Pinda.

      Hata hivyo katika kujibu swali hilo, Pinda hakusema chochote kuhusu swali la Mbowe aliloitaka serikali kuunda tume huru kuchunguzwa tukio la Dk. Ulimboka.

      Badala yake alisisitiza kuwa serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika kumipiga Dk. Ulimboka.

      Akijibu swali la msingi la Mbowe aliyehoji utekelezaji wa sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata, Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwa mwaka jana aliahidi Bungeni kwamba serikali ingelikuja na sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata ili kuharakisha matokeo ya uchunguzi huo.

      Alisema serikali bado inaendelea na mchakato wa kuandaa sheria hiyo ili ianze kutumika.

      Mbowe alisema kumekuwa na kasi ya ongezeko la vifo vyenye utata vya raia wasio na hatia na vyombo vya dola, hasa polisi wamekuwa wakihusishwa na vifo hivyo.

      Alisema kuwa Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwapo na hali hiyo na kuahidi kuwa serikali ingekuja na sheria ya kuchunguza vifo vya aina hiyo.

      Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, kisha kutupwa katika msitu wa Pande, nje kidogo ya jiji Dar es Salaam.

      Jeshi la Polisi limeunda jopo kuchunguza tukio la utekaji nyara na shambulio la kudhuru mwili wa Dk. Ulimboka.

      Tangu kuibuka kwa tukio hilo, wabunge mbalimbali kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiibua hoja ya mgomo wa madaktari na kipigo cha Ulimboka, lakini kiti cha Spika kimekuwa kikizima kwa hoja kuwa jambo hilo liko mahakamani.


      CHANZO: Mwananchi
      Last edited by Return Of Undertaker; 5th July 2012 at 06:43.

    2. FemaTV & Radio

    3. #2
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,094
      Rep Power : 27014
      Likes Received
      8230
      Likes Given
      17325

      Default Re: BBC; Dr. Olimboka yuko ICU (yuko kwenye koma)

      Unatuchanganya na taarifa zako nusu nusu...........

    4. #3
      Nyakageni's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 1st February 2011
      Posts : 5,248
      Rep Power : 0
      Likes Received
      769
      Likes Given
      52

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      eeh Mola mbariki mja wako!

    5. #4
      WA-UKENYENGE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2011
      Location : Inside a Smart Grid
      Posts : 2,417
      Rep Power : 5038
      Likes Received
      782
      Likes Given
      1788

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Duh, Mungu atusaidie na kumponya ndugu yetu!! I don't trust these guys from SA.
      "The usual conclusion is that you can't put a price on a human life. But you can if you must".

    6. #5
      Imany John's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th July 2011
      Posts : 1,971
      Rep Power : 2977
      Likes Received
      471
      Likes Given
      4

      Default

      Quote By Return Of Undertaker
      Source BBC na Omary Mutasa kutoka Afrika Kusini

      Ni wazi kuwa hari ya Dr. Steven Olimboka ni mbaya na kalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na anapumulia mashine, hajitambui wala haongei
      "BBC Swahili~ Mwenyekiti wa chama cha
      madaktari nchini Tanzania
      Steve Ulimboka anaendelea
      kupokea matibabu katika
      hospitali moja mjini
      Johanesburg Afrika Kusini alikolazwa katika chumba cha
      wagonjwa mahututi.
      1 hour ago"

      Mwisho wa kunukuu

      Source:BBC PAGE FB.

    7. Miaka 50

    8. #6
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,269
      Rep Power : 12578
      Likes Received
      5812
      Likes Given
      768

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Wewe mbona ueleweki kila muda unakuja na habari za kushtua auminiki jinsi unavyoleta habari inawezekana unaongeza na yako, jana tumeambiwa anaendelea vizuri na figo zake zimeanza kufanya kazi.

      Wengine wanasema Dr Ulimboka yupo Ujerumani.
      Last edited by Ritz; 5th July 2012 at 06:34.
      mizambwa and MAMA POROJO like this.

    9. #7
      CHABURUMA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 26th June 2012
      Posts : 128
      Rep Power : 373
      Likes Received
      13
      Likes Given
      8

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Mwenyezi mungu msaidie dr Ulimboka.
      Mponella likes this.

    10. #8
      BHULULU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th June 2012
      Posts : 3,014
      Rep Power : 8379
      Likes Received
      833
      Likes Given
      696

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Tuzidi kumuombea

    11. #9
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Return Of Undertaker
      Source BBC na Omary Mutasa kutoka Afrika Kusini

      Ni wazi kuwa hari ya Dr. Steven Olimboka ni mbaya na kalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na anapumulia mashine, hajitambui wala haongei.

      Na kulingana na bbc kulingana na hari yake ilivyo hakuluhusiwa na familia yake kumwona na hawakutaka kuongelea swala la kutekwa na kauli ya JK kukana kuhusika.
      Hizo nilizokuwekea rangi nyekundu ndio nini? fafanua.
      Boflo, Wakuti and Mawaiba like this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    12. #10
      Imany John's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th July 2011
      Posts : 1,971
      Rep Power : 2977
      Likes Received
      471
      Likes Given
      4

      Default

      Quote By zomba
      Hizo nilizokuwekea rangi nyekundu ndio nini? fafanua.
      Haitakusaidia,jadili mada we mang'aa.

    13. #11
      Return Of Undertaker's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 659
      Rep Power : 541
      Likes Received
      462
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Imany John
      Haitakusaidia,jadili mada wa mang'aa.
      Aksante mkuu kwa kuliona

    14. #12
      MNYISANZU's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 6,311
      Rep Power : 0
      Likes Received
      592
      Likes Given
      76

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Ritz, fahamu kwamba ya jana si ya leo. Now yuko ICU, tumwombee.

    15. #13
      Amiliki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2011
      Posts : 1,470
      Rep Power : 764
      Likes Received
      717
      Likes Given
      33

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Inatisha na kusikitisha! Doa la wazi kwa serikali ya dhaifu hilo. Kwa mbaaali naiona The Hague ndani ya TZ.

    16. #14
      MSOROPOGAS's Avatar
      Member Array
      Join Date : 7th March 2012
      Posts : 41
      Rep Power : 372
      Likes Received
      8
      Likes Given
      17

      Default Ulimboka mahututi

      Dr ulimboka amewekewa mashine ya kupumulia na yuko mahututi (koma), mwandishi alimtembelea SA.
      Source: BBC idhaa ya kiswahili

    17. #15
      Amiliki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2011
      Posts : 1,470
      Rep Power : 764
      Likes Received
      717
      Likes Given
      33

      Default Re: Ulimboka mahututi

      JK na Pinda wajiandae kupokea samansi toka The Hague.
      Stiphan likes this.

    18. #16
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2884
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By Mtambuzi
      Unatuchanganya na taarifa zako nusu nusu...........
      habari imeeleweka,habar ziko 2,ya kwanza inahusu hali ya ulimboka south afrika na ya 2 inahusu kauli ya jeshi la polisi
      Mtambuzi likes this.

    19. BAK
      #17
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,603
      Rep Power : 44965
      Likes Received
      8346
      Likes Given
      8336

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Hii (kama ni kweli) inakatisha tamaa kusema kweli...Namuombea Mungu amponye.
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    20. #18
      Angel Msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Posts : 6,266
      Rep Power : 1826
      Likes Received
      1397
      Likes Given
      0

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Habari hii inaumiza sana moyo wangu lkn serikali inafurahi sana

    21. #19
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2884
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By WA-UKENYENGE
      Duh, Mungu atusaidie na kumponya ndugu yetu!! I don't trust these guys from SA.
      tell us whom u trust mdau

    22. #20
      genekai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th February 2010
      Location : Loitering!
      Posts : 7,521
      Rep Power : 2084
      Likes Received
      1070
      Likes Given
      1571

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Inaumiza na kusikitisha sana!!!!
      zimwimtu likes this.
      The future of this country is being jeopardized by the intellectual slavery of our top leaders

    Page 1 of 12 12311 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...