Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

    Report Post
    Page 8 of 12 FirstFirst ... 678910 ... LastLast
    Results 141 to 160 of 236
    1. #1
      Return Of Undertaker's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 697
      Rep Power : 553
      Likes Received
      483
      Likes Given
      0

      Default BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Source BBC na Omary Mutasa kutoka Afrika Kusini

      Ni wazi kuwa hali ya Dr. Steven Olimboka ni mbaya na kalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na anapumulia mashine, hajitambui wala haongei.

      Na kulingana na bbc kulingana na hali yake ilivyo hakuruhusiwa na familia yake kumwona na hawakutaka kuongelea swala la kutekwa na kauli ya JK kukana kuhusika.

      Wakati huo huo jeshi la polisi limetoa kauli hii

      ""Upelelezi wa Polisi Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jopo la upelelezi aliloteua hivi karibuni kushughulikia tukio zima la kutekwa kwa Dk Ulimboka litaendelea na kazi yake hadi mwisho na hatasikiliza kelele za wanaodai kutokuwa na imani nalo. Alisema madai yanayotolewa na watu mbalimbali akiwemo Dk Ulimboka mwenyewe kuwa hana imani na jopo hilo hazitabadili chochote kwani kinachofanyika hivi sasa ni kazi ya kawaida ya upelelezi ya jeshi hilo... “Hao wanaosema hawana imani na jopo hilo hawana hoja isipokuwa waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake."""

      Concern
      Ninashaka hapa hivi uchunguzi wa jeahi la polisi kama mimi mtendwa sitaki kwanini unalazimisha wakati sina imani na ulichokiunda na cha ajabu nawe unanambia hata kama hutaki sie tunaendelea.

      Nini kipo nyuma ya pazia la polisiiiiiii???
      Quote By TONGINDI View Post
      Hali ya afya ya Dk. Steven Ulimboka ambaye anatibiwa Afrika Kusini, imebadilika ghafla na kuna habari kuwa yuko mahututi.

      Habari zilizoifikia Tanzania Daima kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi, zimesema kuwa Dk. Ulimboka alikuwa amepoteza fahamu, na juhudi za kuokoa maisha yake zilikuwa zikiendelea chini ya jopo la madaktari bingwa wa nchi hiyo na wale wa Tanzania.

      Inadaiwa kwamba hali ya kiongozi huyo wa jumuiya ya madaktari nchini ambaye alikimbizwa nchini humo wiki iliyopita, awali ilielezwa kuwa inaendelea vema, lakini ghafla ikabadilika na kufikia kiwango cha kupoteza fahamu.

      Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC) alikaririwa akisema kuwa hali ya Ulimboka ilikuwa mbaya, na kwamba kulikuwa na ulinzi na usiri mkubwa kuhusiana na hali hiyo.

      Jijini Dar es Salaam, mmoja wa madaktari aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina, alisema kuwa walipata taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kutoka kwa ndugu yake aliyeko Afrika Kusini kwamba alikuwa yuko kwenye hali mbaya, hali iliyowachanganya mno.

      Mmoja wa madaktari alikiri kupokea taarifa za kuzidiwa kwa mwenyekiti wao kutoka kwa kaka wa Dk. Ulimboka.

      “Leo asubuhi baada ya kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kikaitishwa kikao cha dharura cha madaktari wote tunaelekea huko,” alisema.

      Hata hivyo, majira ya mchana habari zilivuma kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, hali iliyozidi kuzusha wasiwasi mwingi miongoni mwa madaktari, viongozi wa vyama vya kijamii na wananchi wa kawaida waliokuwa wakihaha kupata ukweli wake.

      Uvumi huo hata hivyo, ulikanushwa baadaye na msemaji wa Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa MOI Almasi Jumaa lakini akakiri kupata taarifa za kubadilika kwa hali ya mgonjwa huyo.

      Huduma za matibabu MOI zasimama tena
      Taarifa za kutatanisha kuhusiana na hali ya Dk. Ulimboka, zilisababisha kusitishwa kwa huduma za matibabu katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) baada ya madaktari karibuni wote kwenda katika mkutano wa dharura kujadili tukio hilo.

      Habari za kuaminika kutoka MOI, zimethibisha kuwa taarifa za kuzidiwa na hata kuzuka kwa habari nyingine kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, ziliwachanganya kwa kiasi kikubwa madaktari hao, ambao walilazimika kusitisha huduma na kuwapangia wagonjwa tarehe nyingine za kurudi.

      Kutokana na hatua hiyo ya madaktari, wagonjwa waliofika MOI baada ya kusikia kwamba huduma zimerejea, walishindwa kupata tiba badala yake waliandikishwa majina, wakalipia na kupewa tarehe ya kurudi kwa madai kwamba hakuna madaktari wa kuwahudumia.
      Taarifa ya kurejea kwa madaktari hao ilitolewa juzi hospitalini hapo jana na Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Balozi Charles Mtalemwa na kusisitiza kwamba hospitali hiyo haiko katika mgomo kwa sasa.

      Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa waliokosa tiba, walidai kuchoshwa na usumbufu huo huku wakiwaomba madaktari hao kurejea kazini.

      “Nimekuja hapa tangu saa moja kulikua na foleni; wenzetu waliowahi walionana na madaktari lakini ilipofika saa nne tukaambiwa wote tuliojiandikisha turudi Alhamisi ijayo kwa sababu madaktari wanaenda kwenye kikao,” alisema Abdallah Haji mkazi wa Kimara.

      Kwa upande wake Jenipher Suka alisema inasikitisha kuona hivyo kwa sababu mama yake ambaye ni mgonjwa mkazi wa Dodoma amekuja akitegemea kupata tiba matokeo yake ameambiwa arudi tarehe 10 mwezi huu kwa kuwa hakuna madaktari kwa sasa.

      “Kwa nini serikali isiseme ukweli maana tunahangaika kuja mpaka huku halafu hakuna huduma? Vyombo vya habari vimetangaza kwamba mgomo umesitishwa lakini bado wanatudanganya wananchi kwa faida ya nani?” alilalamika Jenipher.

      Akizungumza kwa sharti la kutochapisha jina lake gazetini mmoja wa maofisa waandamizi wa hospitali hiyo alikiri kutokuwepo kwa huduma baada ya madaktari kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Unajua huduma zinazoendelea kwa sasa ni kliniki na upasuaji kwa waliowahi lakini hawa madaktari wamechanganyikiwa baada ya daktari mwenzao aliyeongozana na Dk. Ulimboka kuwaeleza kwamba hali ya mgonjwa ni mbaya mno.

      Kukosekana kwa huduma kulichangiwa na madaktari wanafunzi ambao hupokea na kuwahudumia wagonjwa kuwa katika maandalizi ya mitihani ya mwisho wa mwaka itakayoanza Jumatatu ya Julai 9, 2012 hivyo kusababisha huduma utoaji wa huduma kutokuwepo kabisa.

      Pinda abanwa
      MJINI Dodoma, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameshindwa kuliambia Bunge endapo serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dk. Ulimboka.

      Waziri Mkuu Pinda, alishindwa kutoa kauli wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (CHADEMA).
      Katika swali lake la nyongeza, Mbowe alisema kumekuwa na ongezeko la vitendo vya mauaji yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi.
      Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alitolea mfano wa tukio la kupigwa kwa wabunge wawili wa CHADEMA mkoani Mwanza na tukio la hivi karibuni la kutekwa na kupingwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Kwa kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio ya mauaji kwa raia wasio na hatia na kumekuwa na hisia kwamba matendo hayo yanafanywa na Jeshi la Polisi. Mfano wa matukio hayo ni pamoja na lile la kupigwa kwa wabunge wawili na hili la hivi karibuni la kutekwa kwa Dk. Ulimboka, tukio ambalo limelichafua taifa; je, serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza matukio hayo?” alihoji Mbowe.

      Akijibu swali hilo, Pinda kwanza alisema sio kweli kwamba tukio la kupigwa kwa Dk. Ulimboka limechafua sifa nzuri ya taifa.
      “Mh. Mbowe, kwanza tukio la Ulimboka sio mfano mzuri sana kwa sababu hakuna mwenye ushahidi wa serikali kuhusika kumteka na kumpiga Dk. Ulimboka.

      “Kama nilivyosema awali, sioni sababu ya serikali kuhusika na kipigo cha Ulimboka ambaye tulikuwa tukishirikiana naye vizuri kwenye vikao vya majadiliano,” alisema Pinda.

      Hata hivyo katika kujibu swali hilo, Pinda hakusema chochote kuhusu swali la Mbowe aliloitaka serikali kuunda tume huru kuchunguzwa tukio la Dk. Ulimboka.

      Badala yake alisisitiza kuwa serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika kumipiga Dk. Ulimboka.

      Akijibu swali la msingi la Mbowe aliyehoji utekelezaji wa sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata, Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwa mwaka jana aliahidi Bungeni kwamba serikali ingelikuja na sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata ili kuharakisha matokeo ya uchunguzi huo.

      Alisema serikali bado inaendelea na mchakato wa kuandaa sheria hiyo ili ianze kutumika.

      Mbowe alisema kumekuwa na kasi ya ongezeko la vifo vyenye utata vya raia wasio na hatia na vyombo vya dola, hasa polisi wamekuwa wakihusishwa na vifo hivyo.

      Alisema kuwa Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwapo na hali hiyo na kuahidi kuwa serikali ingekuja na sheria ya kuchunguza vifo vya aina hiyo.

      Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, kisha kutupwa katika msitu wa Pande, nje kidogo ya jiji Dar es Salaam.

      Jeshi la Polisi limeunda jopo kuchunguza tukio la utekaji nyara na shambulio la kudhuru mwili wa Dk. Ulimboka.

      Tangu kuibuka kwa tukio hilo, wabunge mbalimbali kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiibua hoja ya mgomo wa madaktari na kipigo cha Ulimboka, lakini kiti cha Spika kimekuwa kikizima kwa hoja kuwa jambo hilo liko mahakamani.


      CHANZO: Mwananchi
      Last edited by Return Of Undertaker; 5th July 2012 at 06:43.


    2. #141
      valour's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd August 2010
      Posts : 142
      Rep Power : 479
      Likes Received
      48
      Likes Given
      10

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Quote By kimweri Jr View Post
      Mungu ni muweza wa yote, amini usiamini ulimboka atapona.
      Naamini hivyo pia.

    3. #142
      Zanta's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th April 2011
      Posts : 1,329
      Rep Power : 757
      Likes Received
      434
      Likes Given
      369

      Default Re: BBC Hawana nia njema na Watanzania

      Quote By Lastname View Post
      BBC leo mtangazaji anasema alienda kumuona Ulimboka akiwa ICU na hali yake si nzuri, mbona taarifa zingine hawafuatilii??? Kuhusu yanayosemwa na watu kuhusu kutekwa kwake??

      Na huyu Mtangazaji wa BBC kwa nini anasema madaktari wamegoma kudai mishahara? Ni uvivu wa kutafuta habari au kuhingwa au kutishiwa?

      Kwa sababu nilitegemea chombo kama kile kisema "madaktari wanadai mazingira mazuri ya kazi including vitendea kazi lakini kataja lile ambalo madaktari wakianza kusema wanalisema la nne na si la kwanza.

      BBC sasa hivi nawachukia.
      Acha unafiki wewe Madai ya ma docta umeyaona? kati yake 11 ni kwa ajili ya maslai yao na moja la kumi na mbili ndio mazingira bora ya kazi, sasa kosa la BBC nini hapo?
      Better to have a Good Dictatorship than Bad Democracy !!!!

    4. #143
      valour's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd August 2010
      Posts : 142
      Rep Power : 479
      Likes Received
      48
      Likes Given
      10

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Edson View Post
      mkuu saa tisa nilikuwa niko macho nimeshaoga ..nimekuwekea clipi hapo juu isikilize tena ...hakuna ndugu aliyempa taarifa ya maendeleo ya mgonjwa .alitolewa mkuku
      Inaonyesha ni sehemu inayoweza kujulikana kwa urahisi. Mtangazaji wa BBC aliijuaje hii hospitali wakati inapasawa iwe siri kwa usalama wa Dr. South Africa ni kubwa na ina hospitali nyingi, isiwe kuna mtu wanamwamini ndiye anayetoa siri. Kuvuka hapa ni maombi tu, mkono wa Mungu wenye rehema ndio umlinde na kumponya. Ninaamini kabisa atarudi salama.

    5. #144
      Asa'rile's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 29th June 2012
      Posts : 141
      Rep Power : 379
      Likes Received
      21
      Likes Given
      2

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Jeshi la polisi linafanya kazi zake kwa mjibu wa sheria. Sheria iliyoanzisha jeshi hili, ililipa majukum yafuatayo:-
      1. kulinda maisha ya watu na mali( kudumisha amani)
      2. kukamata/kuwaweka chini ya ulinzi wa polisi watuhumiwa wa makosa ya jinai
      3. kupeleleza au kukusanya ushahidi wa makosa ya jinai
      4. kusimamia utii wa sheria (ikibidi ushurutishaji wa utii wa sheria za nchi)
      5. kudhibiti matukio ya uhalifu.
      ...Yaani Misitari hii..inanikumbusha Mhe. Zombe!! ...Aliipenda!

    6. #145
      Sn2139's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th April 2010
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 805
      Rep Power : 2871
      Likes Received
      237
      Likes Given
      1400

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Quote By Bajabiri View Post
      Jamani kuna taarifa zimeanza kuzagaa na mimi kuna mtu ameni text amenambia dr Amefariki,nikamwambia subiri nijiridhishe,what i know jf ndo huwa ya kwanza kupata news,najiridhisha kwa comment za hapa kuwa he's alive
      jamaniiiiiiiiiiiiii
      Bajabiri, kifo kwa bin-Adam kinawezekana. Kila mtu atakufa. Lakini, Mungu anaweza kuhuisha na kuponya pia. Hivyo turuhusu mapenzi ya Mungu na makusudi yake yatimizwe.

      Lakini jambo moja la hakika, Mungu amefanya muujiza kwa Dr Ulimboka. Dr Uli, hakupaswa kuwa anaishi hadi sasa, akiongea na kueleza yote aliyoeleza. Huu ni muujiza wa wazi. Mungu atukuzwe sana. Watu waliomteka walitumwa kumwua. Waling'oa meno, na kucha ! Walivunja mbavu na kumnywesha sumu (iliyoonekana kwenye damu yake). Mateso yote hayo yalifanywa na watu wenye miraba minne, lakini bado Dr Uli aliweza saa ya asubuhi kufufuka na kuzungumza! Huu ndio muujiza uliotendeka..

      Hadi sasa Dr Ulimboka amefanya kazi kubwa ya kuiumbuwa serikali kwa mambo yafuatayo.. (1) Viongozi wa serikali ya TZ ni waongo (2) Serikali haina nia njema na watu wake (3) Serikali inatesa na kuua watu wake (4) Serikali haina malengo ya maisha bora kwa kila mtu bali kwa baadhi ya wateule na watu wa karibu na mfalme.

      Sasa watu hawataweza kuiamini tena serikali yetu. Jambo hili ni kama vita ... ni mfarakano kati ya watawala na watawaliwa. Hii inaweza kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe...

      Sasa hivi nchi imegawanyika makundi mbalimbali. Wanaounga mkono serikali na wanaoilaani na kuipinga. UWT umegawanyika, JWTZ limegawanyika, POLICE wamegawanyika, CCM wamegawanyika na huwezi kuamini kuwa hata baraza la mawaziri limegawanyika... Huu ni MGAWANYIKO ulio kinyume na UMOJA na MSHIKAMANO tuliokuwa tumezowea miaka mingi. Sasa hatupo wamoja teana, na huko tuendako ni KIZA

      Tuzidi kuomba na kumwombea Dr Ulimboka. Kama akifa, ni mapenzi ya Mungu. Lakini muujiza umefanyika. Na serikali imeumbuliwa na kuwekwa wazi. Kama akipona serikali itabaki imeumbuka vilevile. Na ni afadhali akipona serikali inaweza kupumua ...
      Last edited by Sn2139; 5th July 2012 at 11:43.
      Dingswayo and valour like this.
      the fool collects facts, the wise selects them


    7. #146
      reformer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd July 2011
      Posts : 296
      Rep Power : 459
      Likes Received
      79
      Likes Given
      6

      Default Re: CURRENT NEWS : BBC wagundua alipo Dr. Ulimboka na hali yake si mahamumu

      Quote By Tume ya Katiba View Post
      RIP Hitler wa tanzania.

      Mgomo umeisha, LUGALO imekuwa ya rufaa now.
      A referral hospital is a major hospital that usually has a full complement of services including pediatrics, obstetrics, general medicine, gynecology, various branches of surgery and psychiatry or a specialty hospital dedicated to specific sub-specialty care (pediatric centers, Oncology centers, psychiatric hospitals).

      Patients will often be referred from smaller hospitals to a tertiary hospital for major operations, consultations with sub-specialists and when sophisticated intensive care facilities are required.

      Haya yote yanafanyika lugalo sasa hivi..au kuongea tu inatosha kuifanya hospitali iwe ya rufaa?
      Naona mnaijenga TZ kama Mungu alivoumba dunia..Mungu alisema na iwe usiku ikawa usiku.
      valour likes this.

    8. #147
      Kasimba G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 19th January 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 918
      Rep Power : 610
      Likes Received
      277
      Likes Given
      265

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Nasikia dr kishafariki! Itakuwa mshikemshike!

    9. #148
      zumbemkuu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 11th September 2010
      Location : street dweller
      Posts : 5,425
      Rep Power : 2024
      Likes Received
      2168
      Likes Given
      7955

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Quote By Sn2139 View Post
      Bajabiri, kifo kwa bin-Adam kinawezekana. Kila mtu atakufa. Lakini, Mungu anaweza kuhuisha na kuponya pia. Hivyo turuhusu mapenzi ya Mungu na makusudi yake yatimizwe.

      Lakini jambo moja la hakika, Mungu amefanya muujiza kwa Dr Ulimboka. Dr Uli, hakupaswa kuwa anaishi hadi sasa, akiongea na kueleza yote aliyoeleza. Huu ni muujiza wa wazi. Mungu atukuzwe sana. Watu waliomteka walitumwa kumwua. Waling'oa meno, na kucha ! Walivunja mbavu na kumnywesha sumu (iliyoonekana kwenye damu yake). Mateso yote hayo yakifanywa na watu wenye miraba minne, bado alifufuka asubuhi na kuzungumza! Huu ndio muujiza uliotendeka..

      Hadi sasa Dr Ulimboka amefanya kazi kubwa sana. (1) Ameiumbua serikali kuwa ni serikali ya waongo (2) Serikali haina nia njema na watu wake (3) Serikali inatesa na kuua watu wake (4) Serikali haina malengo ya maisha bora kwa kila mtu bali kwa baadhi ya wateule na watu wa karibu na mfalme.

      Sasa watu hawataweza kuiamini tena serikali yetu. Jambo hili ni kama vita ... ni mfarakano kati ya watawala na watawaliwa. Hii inaweza kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe...

      Sasa hivi nchi imegawanyika makundi mbalimbali. Wanaounga mkono serikali na wanaoilaani na kuipinga. UWT umegawanyika, JWTZ limegawanyika, POLICE wamegawanyika, CCM wamegawanyika na huwezi kuamini kuwa hata baraza la mawaziri limegawanyika...

      Tuzidi kuomba na kumwombea Dr Ulimboka. Kama akifa, ni mapenzi ya Mungu. Lakini muujiza umefanyika. Na serikali imeumbuliwa na kuwekwa wazi. Kama akipona serikali itabaki imeumbuka vilevile. Na ni afadhali akipona serikali inaweza kupumua ...
      nakubaliana na wewe, watu waliotumwa kumuua walimuua na walihakikisha amekufa, ila kwa mapenzi ya Mungu akafufuka asubuhi na mapema na kuiumbua serikali, vinginevyo tungekuwa tumeshamzika na hadi sasa watu wangeamini kuwa ameuawa na majambazi, kwa ufupi kifo chake kingekuwa na utata coz ahkungekuwa na ushahidi wa moja kwa moja kuwa serikali imehusika. kwa ufupi hakuna mlalahoi mwenye uwezo wa kukodi wauaji eti kisa kafiwa na nduguye kwa kukosa tiba, kama ana uwezo huo basi hata nduguye asingekufa coz hizo hela za kukodi wauaji angempelekea nduguye hospital za kulipia.
      "watakaotubeza na kututukana wasameheni wanahitaji ukombozi wa fikra" Mh.G.Lema

    10. #149
      Kasimba G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 19th January 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 918
      Rep Power : 610
      Likes Received
      277
      Likes Given
      265

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Mazishi yake kama ni mbeya naomba serikali nao wapeleke wawakirishi, ili tujue hawakushiriki kwenye uuaji huo walio ufa

    11. #150
      KAFWIMBI's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 57
      Rep Power : 375
      Likes Received
      10
      Likes Given
      4

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Watanzania amkeni hii Sirikali yetu ni janja sana kwa kuwatoa watu wake nje ya reli kila linapotokea jambo kubwa. Sasa hivi kuna suala la wanachi kutoa maoni yao kuhusu maoni ya kuandikwa kwa katiba mpya. Sasa wanatumia suala la Uli kupotosha umma ili uache kujadili mambo muhimu kwa mustakabali wa ustawi wa Taifa letu

    12. #151
      Kidogo chetu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2009
      Location : DAR ES SALAAM
      Posts : 478
      Rep Power : 581
      Likes Received
      53
      Likes Given
      130

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Bwana tia mkono wa uponyaji kwa ULIMBOKA

    13. #152
      Froida's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Posts : 3,854
      Rep Power : 1343
      Likes Received
      758
      Likes Given
      153

      Default Re: CURRENT NEWS : BBC wagundua alipo Dr. Ulimboka na hali yake si mahamumu

      Quote By Tume ya Katiba View Post
      We hujui, wajibu wa wanajeshi sio kupigana vita tu, kuokoa maisha ya wananchi kwa aina yoyote ni wajibu wa jeshi.
      Haya nendeni na bendera zenu za Chadema Lugalo mkawashawishi Majemedali wagome.

      SHAME.
      jeshi wamejichokea hawana hata nia na serikali hii ndio maana walimkatalia kuruhusu wanajeshi kwenda kutibu Muhimbili the only National hospital totally is closed na msanii wetu IkuLU anazungusha viti pale IKULU akipanga Kum limboka daktari mwingine what a shame Kwa merit zozote Lugalo haiwezi kuwa referal hospital tunaifahamu vizuri in and out

    14. #153
      MNYISANZU's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 6,311
      Rep Power : 0
      Likes Received
      593
      Likes Given
      76

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Tumwombee uzima "the hero" Dr Ulimboka apone haraka. Mungu yupo.

    15. #154
      El Toro's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2009
      Location : Here in Bongoland
      Posts : 5,060
      Rep Power : 1864
      Likes Received
      476
      Likes Given
      370

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Habari za kuaminika toka kwa dr. Muhimbili ni kuwa dr uli is no more ( r.i.p)
      Don't be a WOMAN that needs a man but the WOMAN a man needs



    16. #155
      Bujibuji's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 4th February 2009
      Location : NYUMBANI PANONO
      Posts : 14,415
      Rep Power : 0
      Likes Received
      7414
      Likes Given
      5746

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Jah Kayaman a.k.a Born Town utamaliza wa Tanzania wa ngapi kwa kuwaua??
      Kwa hili la Ulimboka huna mlango wa kutokea.
      Ukitaka utoke salama, tujulishe.
      Ulimboka alimwibia nani??
      Ulimboka kafumaniwa na mke wa nani??
      Je kwanini haya yamkute yeye tu na yawaruke waTanzania wote wanaokaribia milioni hamsini?
      Nivea likes this.

    17. #156
      mwana wa mtu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th March 2008
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 219
      Rep Power : 620
      Likes Received
      51
      Likes Given
      97

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By El Toro View Post
      Habari za kuaminika toka kwa dr. Muhimbili ni kuwa dr uli is no more ( r.i.p)
      Ahh, No!, kweli?

    18. #157
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,310
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1806
      Likes Given
      433

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By mwana wa mtu View Post
      Ahh, No!, kweli?

      si kweli
      I'm Naturaly Evasive..

    19. #158
      Joyum's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th October 2007
      Posts : 152
      Rep Power : 625
      Likes Received
      11
      Likes Given
      6

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By El Toro View Post
      Habari za kuaminika toka kwa dr. Muhimbili ni kuwa dr uli is no more ( r.i.p)
      ndiko alikolazwa, so it's true.....hongera kwa taarifa murua

    20. #159
      sulphadoxine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 2,191
      Rep Power : 942
      Likes Received
      565
      Likes Given
      2058

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Dr.Riwa njoo thibitisha hizi habari kama ni kweli.
      CHUKI NA UADUI NI MATOKEO YA UPUMBAVU:

    21. #160
      nkyalomkonza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2012
      Posts : 762
      Rep Power : 604
      Likes Received
      274
      Likes Given
      89

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By El Toro View Post
      Habari za kuaminika toka kwa dr. Muhimbili ni kuwa dr uli is no more ( r.i.p)
      Wewe sio Reliable Source. Huwezi aminika hata siku moja.

    Page 8 of 12 FirstFirst ... 678910 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...