Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

    Report Post
    Page 5 of 12 FirstFirst ... 34567 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 236
    1. #1
      Return Of Undertaker's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 659
      Rep Power : 541
      Likes Received
      462
      Likes Given
      0

      Default BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Source BBC na Omary Mutasa kutoka Afrika Kusini

      Ni wazi kuwa hali ya Dr. Steven Olimboka ni mbaya na kalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na anapumulia mashine, hajitambui wala haongei.

      Na kulingana na bbc kulingana na hali yake ilivyo hakuruhusiwa na familia yake kumwona na hawakutaka kuongelea swala la kutekwa na kauli ya JK kukana kuhusika.

      Wakati huo huo jeshi la polisi limetoa kauli hii

      ""Upelelezi wa Polisi Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jopo la upelelezi aliloteua hivi karibuni kushughulikia tukio zima la kutekwa kwa Dk Ulimboka litaendelea na kazi yake hadi mwisho na hatasikiliza kelele za wanaodai kutokuwa na imani nalo. Alisema madai yanayotolewa na watu mbalimbali akiwemo Dk Ulimboka mwenyewe kuwa hana imani na jopo hilo hazitabadili chochote kwani kinachofanyika hivi sasa ni kazi ya kawaida ya upelelezi ya jeshi hilo... “Hao wanaosema hawana imani na jopo hilo hawana hoja isipokuwa waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake."""

      Concern
      Ninashaka hapa hivi uchunguzi wa jeahi la polisi kama mimi mtendwa sitaki kwanini unalazimisha wakati sina imani na ulichokiunda na cha ajabu nawe unanambia hata kama hutaki sie tunaendelea.

      Nini kipo nyuma ya pazia la polisiiiiiii???
      Quote By TONGINDI
      Hali ya afya ya Dk. Steven Ulimboka ambaye anatibiwa Afrika Kusini, imebadilika ghafla na kuna habari kuwa yuko mahututi.

      Habari zilizoifikia Tanzania Daima kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi, zimesema kuwa Dk. Ulimboka alikuwa amepoteza fahamu, na juhudi za kuokoa maisha yake zilikuwa zikiendelea chini ya jopo la madaktari bingwa wa nchi hiyo na wale wa Tanzania.

      Inadaiwa kwamba hali ya kiongozi huyo wa jumuiya ya madaktari nchini ambaye alikimbizwa nchini humo wiki iliyopita, awali ilielezwa kuwa inaendelea vema, lakini ghafla ikabadilika na kufikia kiwango cha kupoteza fahamu.

      Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC) alikaririwa akisema kuwa hali ya Ulimboka ilikuwa mbaya, na kwamba kulikuwa na ulinzi na usiri mkubwa kuhusiana na hali hiyo.

      Jijini Dar es Salaam, mmoja wa madaktari aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina, alisema kuwa walipata taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kutoka kwa ndugu yake aliyeko Afrika Kusini kwamba alikuwa yuko kwenye hali mbaya, hali iliyowachanganya mno.

      Mmoja wa madaktari alikiri kupokea taarifa za kuzidiwa kwa mwenyekiti wao kutoka kwa kaka wa Dk. Ulimboka.

      “Leo asubuhi baada ya kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kikaitishwa kikao cha dharura cha madaktari wote tunaelekea huko,” alisema.

      Hata hivyo, majira ya mchana habari zilivuma kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, hali iliyozidi kuzusha wasiwasi mwingi miongoni mwa madaktari, viongozi wa vyama vya kijamii na wananchi wa kawaida waliokuwa wakihaha kupata ukweli wake.

      Uvumi huo hata hivyo, ulikanushwa baadaye na msemaji wa Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa MOI Almasi Jumaa lakini akakiri kupata taarifa za kubadilika kwa hali ya mgonjwa huyo.

      Huduma za matibabu MOI zasimama tena
      Taarifa za kutatanisha kuhusiana na hali ya Dk. Ulimboka, zilisababisha kusitishwa kwa huduma za matibabu katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) baada ya madaktari karibuni wote kwenda katika mkutano wa dharura kujadili tukio hilo.

      Habari za kuaminika kutoka MOI, zimethibisha kuwa taarifa za kuzidiwa na hata kuzuka kwa habari nyingine kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, ziliwachanganya kwa kiasi kikubwa madaktari hao, ambao walilazimika kusitisha huduma na kuwapangia wagonjwa tarehe nyingine za kurudi.

      Kutokana na hatua hiyo ya madaktari, wagonjwa waliofika MOI baada ya kusikia kwamba huduma zimerejea, walishindwa kupata tiba badala yake waliandikishwa majina, wakalipia na kupewa tarehe ya kurudi kwa madai kwamba hakuna madaktari wa kuwahudumia.
      Taarifa ya kurejea kwa madaktari hao ilitolewa juzi hospitalini hapo jana na Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Balozi Charles Mtalemwa na kusisitiza kwamba hospitali hiyo haiko katika mgomo kwa sasa.

      Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa waliokosa tiba, walidai kuchoshwa na usumbufu huo huku wakiwaomba madaktari hao kurejea kazini.

      “Nimekuja hapa tangu saa moja kulikua na foleni; wenzetu waliowahi walionana na madaktari lakini ilipofika saa nne tukaambiwa wote tuliojiandikisha turudi Alhamisi ijayo kwa sababu madaktari wanaenda kwenye kikao,” alisema Abdallah Haji mkazi wa Kimara.

      Kwa upande wake Jenipher Suka alisema inasikitisha kuona hivyo kwa sababu mama yake ambaye ni mgonjwa mkazi wa Dodoma amekuja akitegemea kupata tiba matokeo yake ameambiwa arudi tarehe 10 mwezi huu kwa kuwa hakuna madaktari kwa sasa.

      “Kwa nini serikali isiseme ukweli maana tunahangaika kuja mpaka huku halafu hakuna huduma? Vyombo vya habari vimetangaza kwamba mgomo umesitishwa lakini bado wanatudanganya wananchi kwa faida ya nani?” alilalamika Jenipher.

      Akizungumza kwa sharti la kutochapisha jina lake gazetini mmoja wa maofisa waandamizi wa hospitali hiyo alikiri kutokuwepo kwa huduma baada ya madaktari kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Unajua huduma zinazoendelea kwa sasa ni kliniki na upasuaji kwa waliowahi lakini hawa madaktari wamechanganyikiwa baada ya daktari mwenzao aliyeongozana na Dk. Ulimboka kuwaeleza kwamba hali ya mgonjwa ni mbaya mno.

      Kukosekana kwa huduma kulichangiwa na madaktari wanafunzi ambao hupokea na kuwahudumia wagonjwa kuwa katika maandalizi ya mitihani ya mwisho wa mwaka itakayoanza Jumatatu ya Julai 9, 2012 hivyo kusababisha huduma utoaji wa huduma kutokuwepo kabisa.

      Pinda abanwa
      MJINI Dodoma, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameshindwa kuliambia Bunge endapo serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dk. Ulimboka.

      Waziri Mkuu Pinda, alishindwa kutoa kauli wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (CHADEMA).
      Katika swali lake la nyongeza, Mbowe alisema kumekuwa na ongezeko la vitendo vya mauaji yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi.
      Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alitolea mfano wa tukio la kupigwa kwa wabunge wawili wa CHADEMA mkoani Mwanza na tukio la hivi karibuni la kutekwa na kupingwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Kwa kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio ya mauaji kwa raia wasio na hatia na kumekuwa na hisia kwamba matendo hayo yanafanywa na Jeshi la Polisi. Mfano wa matukio hayo ni pamoja na lile la kupigwa kwa wabunge wawili na hili la hivi karibuni la kutekwa kwa Dk. Ulimboka, tukio ambalo limelichafua taifa; je, serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza matukio hayo?” alihoji Mbowe.

      Akijibu swali hilo, Pinda kwanza alisema sio kweli kwamba tukio la kupigwa kwa Dk. Ulimboka limechafua sifa nzuri ya taifa.
      “Mh. Mbowe, kwanza tukio la Ulimboka sio mfano mzuri sana kwa sababu hakuna mwenye ushahidi wa serikali kuhusika kumteka na kumpiga Dk. Ulimboka.

      “Kama nilivyosema awali, sioni sababu ya serikali kuhusika na kipigo cha Ulimboka ambaye tulikuwa tukishirikiana naye vizuri kwenye vikao vya majadiliano,” alisema Pinda.

      Hata hivyo katika kujibu swali hilo, Pinda hakusema chochote kuhusu swali la Mbowe aliloitaka serikali kuunda tume huru kuchunguzwa tukio la Dk. Ulimboka.

      Badala yake alisisitiza kuwa serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika kumipiga Dk. Ulimboka.

      Akijibu swali la msingi la Mbowe aliyehoji utekelezaji wa sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata, Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwa mwaka jana aliahidi Bungeni kwamba serikali ingelikuja na sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata ili kuharakisha matokeo ya uchunguzi huo.

      Alisema serikali bado inaendelea na mchakato wa kuandaa sheria hiyo ili ianze kutumika.

      Mbowe alisema kumekuwa na kasi ya ongezeko la vifo vyenye utata vya raia wasio na hatia na vyombo vya dola, hasa polisi wamekuwa wakihusishwa na vifo hivyo.

      Alisema kuwa Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwapo na hali hiyo na kuahidi kuwa serikali ingekuja na sheria ya kuchunguza vifo vya aina hiyo.

      Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, kisha kutupwa katika msitu wa Pande, nje kidogo ya jiji Dar es Salaam.

      Jeshi la Polisi limeunda jopo kuchunguza tukio la utekaji nyara na shambulio la kudhuru mwili wa Dk. Ulimboka.

      Tangu kuibuka kwa tukio hilo, wabunge mbalimbali kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiibua hoja ya mgomo wa madaktari na kipigo cha Ulimboka, lakini kiti cha Spika kimekuwa kikizima kwa hoja kuwa jambo hilo liko mahakamani.


      CHANZO: Mwananchi
      Last edited by Return Of Undertaker; 5th July 2012 at 06:43.

    2. FemaTV & Radio

    3. #81
      sir.JAPHET's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th May 2012
      Posts : 608
      Rep Power : 474
      Likes Received
      90
      Likes Given
      43

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      eeh mwenyezi mungu uumbae mbingu na nchi mponye na umuokoe mtanzania mwenzetu dk,ulimboka.. ...! Na wagonjwa wote wape na wajalie afya njema wapate kuishi tena.. Mungu tunaamini upo na utatusaidia katka kipindi hiki kigum na siku za uson

    4. #82
      hans79's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2011
      Posts : 1,495
      Rep Power : 767
      Likes Received
      143
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By zomba
      Hizo nilizokuwekea rangi nyekundu ndio nini? fafanua.
      Huna hoja kaa kimya.

    5. #83
      miss strong's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2012
      Posts : 648
      Rep Power : 476
      Likes Received
      131
      Likes Given
      62

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Tunamwombea sana tu dkt Uli na atapona tuu!Familia kuwen makini sana kumwangalia mgonjwa maana bado wanatutafuta ubaya....!

    6. #84
      reformer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd July 2011
      Posts : 296
      Rep Power : 455
      Likes Received
      79
      Likes Given
      6

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By zomba
      Hizo nilizokuwekea rangi nyekundu ndio nini? fafanua.
      Na ww kamuombe Maji marefu akusaidie kufafanua maana ya 'fill pity'.

    7. #85
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      592
      Likes Given
      413

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Maundumula
      Huko South Africa analipiwa na nani gharama za matibabu?
      Analipiwa na serikali

    8. Miaka 50

    9. #86
      GeniusBrain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Location : CHADEMA Makao Makuu
      Posts : 3,820
      Rep Power : 1147
      Likes Received
      188
      Likes Given
      0

      Default CURRENT NEWS : BBC wagundua alipo Dr. Ulimboka na hali yake si mahamumu

      Leo (05.07.2012) nilipokuwa nasikiliza kipindi cha BBC Swahili , Mwandishi wa habari wake Ally Mukhtasa aliweza kugundua hospitali (hakuitaja) ambapo Dr Ulimboka amelazwa. Kwa habari aliyoitoa ni kuwa amelazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini, na aliweza mpaka kufanikiwa kwenda kuonana na Ndugu zake wanao muuguza huko, ambapo aliongea nao , lakini hawakufurahishwa na yeye kwenda kuwaona na kugundua chumba cha ICU alicholazwa na kuchungulia ndani na kumkuta Dr. Ulimboka akiwa amezungukwa na mashine zinazo msaidia kupumua. Kwa hali aliyosema Ally Mukhtasa ni kuwa hali yake si nzuri, na watanzania tuendelee kumuombea, kwani hali yake si mahamumu (i.e. hali tete).

    10. #87
      reformer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd July 2011
      Posts : 296
      Rep Power : 455
      Likes Received
      79
      Likes Given
      6

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Maundumula
      Huko South Africa analipiwa na nani gharama za matibabu?
      Analipiwa na mmeo

    11. #88
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2884
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By Mtambuzi
      Bajabiri awali aliweka maneno matatu tu kama inavyosomeka hapo chini......

      Je hapo ungeelewa kitu gani?
      kweli kaka ila jf inapaswa kutupa nyenzo za kutumia habari

    12. #89
      Yummy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2011
      Posts : 1,751
      Rep Power : 1895
      Likes Received
      1274
      Likes Given
      983

      Default Re: CURRENT NEWS : BBC wagundua alipo Dr. Ulimboka na hali yake si mahamumu

      Is this true???!!! Ee Mungu mpelekee msaada wako Dr Ulimboka
      God can heal a broken heart but you have to give him all the pieces.

    13. #90
      Hute's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Posts : 1,409
      Rep Power : 711
      Likes Received
      354
      Likes Given
      23

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Mungu amsaidie apone, asijekwenda kuungana na mamia ya wale waliokufa pale muhimbili kwasababu ya mgomo wa madaktari, manake kama akienda kukutana nao huko ahera watamwuliza kwanini ameendesha mgomo ukawaharakisha wao kwenda ahera.
      Kama huna meno,usile bisi, kula Bwimbwi yaani kimbugi. Uongozi ukikushinda waachie wanaoweza!

    14. #91
      Mzalendo JR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th June 2012
      Posts : 906
      Rep Power : 532
      Likes Received
      277
      Likes Given
      213

      Default Re: CURRENT NEWS : BBC wagundua alipo Dr. Ulimboka na hali yake si mahamumu

      The truth will never be ruined, Son u need to fight back coz we all know how strong u are. May God lead u and come back home with that smiling face again.....

      We pray 4 you Dr Ulimboka!

    15. #92
      miss strong's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2012
      Posts : 648
      Rep Power : 476
      Likes Received
      131
      Likes Given
      62

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Madaktari msiyumbishwe kumbukeni kauli ya mwisho aliyoitoa dkt ULIMBOKA wkt akisafirishwa kwenda kwenye matibabu!

    16. #93
      john tongo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th April 2012
      Location : I.T room
      Posts : 334
      Rep Power : 426
      Likes Received
      46
      Likes Given
      16

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Wasitudanganye kama daud balali

    17. #94
      Godlisten Masawe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th July 2011
      Location : Hapa Hapa
      Posts : 607
      Rep Power : 518
      Likes Received
      220
      Likes Given
      2877

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Edson
      bahari nzuri nimerekodi hiyo taarifa ya bbc na ninayo hapa...

      Ali mtasa mtangazaji wa bbc alikwenda hosp.moja huko africa ya kusini alokolazwa dr ulimboka.alipofika alienda maulizo na kuonyeshwa chumba alicholazwa. wakati akielekea huko alikutana n ndugu wa ulimbo walioko hapo hosp na yeye alimuona ulimboka kupitia kwenye vioo na wala hakuingia chumbani kabisa.

      alipojitmbulisha kwa ndugu wa ulimboka, mara moja walimuambia aondoke hosp hapo maana hawahitaji mtu na wala asifatilie lolote kuhusu maendeleo ya ulimboka.alipoulizia hali yake inakwendaje hakujibiwa kitu isipokuwa aliambiwa aondoke mara moja. na akaondoka....

      hiyo ya kusema kuwa dr uli yuko kwenye koma ameipika mwenyewe maana dr uli alikuwa amepumzika na wala hakunandugu hata mmoja aliyemwambia kuwa yuko kwenye koma..
      Asante sana kamanda Edson, kuna watu walishaanza kupotosha kuhusu hali ya Dr. Pumbavu kabisa.
      [[MUFC]]

    18. #95
      Nkoma's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 35
      Rep Power : 367
      Likes Received
      9
      Likes Given
      123

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Ni Kweli BBC Idhaa ya Kiswahili ktk taarifa zake za saa 12 leo asubuhi wamesema kuwa Dr. Ulimboka yuko Afrika ya Kusini, na hali yake iko ktk (KOMA) na Mwandishi/Mtangazaji hakuweza kuongea naye. Aliongea na Ndg tu, Japo hawakufurahishwa kwa Mwandishi huyo kufika hapo.

      Tuombe Mungu amjaliye KUPONA ili kuleta ukurasa mpya wa utatuzi wa matatizo ya waliowengi wasionacho, wagandamizwaji.

    19. #96
      GeniusBrain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Location : CHADEMA Makao Makuu
      Posts : 3,820
      Rep Power : 1147
      Likes Received
      188
      Likes Given
      0

      Default Re: CURRENT NEWS : BBC wagundua alipo Dr. Ulimboka na hali yake si mahamumu

      Quote By Yummy
      Is this true???!!! Ee Mungu mpelekee msaada wako Dr Ulimboka
      Mkuu ambacho huamini ni kipi ? source nimeiweka ni bbc swahili leo asubuhi, au na waandishi wa bbc huwaamini? hali ndivyo ilivyo

    20. #97
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,170
      Rep Power : 24271
      Likes Received
      4677
      Likes Given
      2296

      Default Re: CURRENT NEWS : BBC wagundua alipo Dr. Ulimboka na hali yake si mahamumu

      Mwenyenzi Mungu amponye kwa mapenzi yake!
      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    21. #98
      fikirikwanza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th January 2012
      Posts : 642
      Rep Power : 498
      Likes Received
      149
      Likes Given
      17

      Default Re: CURRENT NEWS : BBC wagundua alipo Dr. Ulimboka na hali yake si mahamumu

      Ina maana hadi sasa hakuna suspect yeyote aliyekamatwa

    22. #99
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Godlisten Masawe
      Asante sana kamanda Edson, kuna watu walishaanza kupotosha kuhusu hali ya Dr. Pumbavu kabisa.

      kuna watu raha yao ni kusikia na kukutakia matatizo...yaani akikusalimia ukijibu hujambo na familia haijambo huwa wanajisikia vibaya...huyu bwana alitaka kupotosha wakat mtangazi alichoripot juu ya hali ya mgonjwa ni mawazo yake ..ndugu wa dr uli walmtoa nduki...nimemuwekea clip hapo juu asikilize hiy taarifa kwa uzuri.
      I'm Naturaly Evasive..

    23. #100
      Maundumula's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 4,920
      Rep Power : 3095
      Likes Received
      1340
      Likes Given
      5654

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By reformer
      Analipiwa na mmeo
      Jazba imeshika kasi

    Page 5 of 12 FirstFirst ... 34567 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...