Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

    Report Post
    Page 4 of 12 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 236
    1. #1
      Return Of Undertaker's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 665
      Rep Power : 543
      Likes Received
      465
      Likes Given
      0

      Default BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Source BBC na Omary Mutasa kutoka Afrika Kusini

      Ni wazi kuwa hali ya Dr. Steven Olimboka ni mbaya na kalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na anapumulia mashine, hajitambui wala haongei.

      Na kulingana na bbc kulingana na hali yake ilivyo hakuruhusiwa na familia yake kumwona na hawakutaka kuongelea swala la kutekwa na kauli ya JK kukana kuhusika.

      Wakati huo huo jeshi la polisi limetoa kauli hii

      ""Upelelezi wa Polisi Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jopo la upelelezi aliloteua hivi karibuni kushughulikia tukio zima la kutekwa kwa Dk Ulimboka litaendelea na kazi yake hadi mwisho na hatasikiliza kelele za wanaodai kutokuwa na imani nalo. Alisema madai yanayotolewa na watu mbalimbali akiwemo Dk Ulimboka mwenyewe kuwa hana imani na jopo hilo hazitabadili chochote kwani kinachofanyika hivi sasa ni kazi ya kawaida ya upelelezi ya jeshi hilo... “Hao wanaosema hawana imani na jopo hilo hawana hoja isipokuwa waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake."""

      Concern
      Ninashaka hapa hivi uchunguzi wa jeahi la polisi kama mimi mtendwa sitaki kwanini unalazimisha wakati sina imani na ulichokiunda na cha ajabu nawe unanambia hata kama hutaki sie tunaendelea.

      Nini kipo nyuma ya pazia la polisiiiiiii???
      Quote By TONGINDI
      Hali ya afya ya Dk. Steven Ulimboka ambaye anatibiwa Afrika Kusini, imebadilika ghafla na kuna habari kuwa yuko mahututi.

      Habari zilizoifikia Tanzania Daima kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi, zimesema kuwa Dk. Ulimboka alikuwa amepoteza fahamu, na juhudi za kuokoa maisha yake zilikuwa zikiendelea chini ya jopo la madaktari bingwa wa nchi hiyo na wale wa Tanzania.

      Inadaiwa kwamba hali ya kiongozi huyo wa jumuiya ya madaktari nchini ambaye alikimbizwa nchini humo wiki iliyopita, awali ilielezwa kuwa inaendelea vema, lakini ghafla ikabadilika na kufikia kiwango cha kupoteza fahamu.

      Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC) alikaririwa akisema kuwa hali ya Ulimboka ilikuwa mbaya, na kwamba kulikuwa na ulinzi na usiri mkubwa kuhusiana na hali hiyo.

      Jijini Dar es Salaam, mmoja wa madaktari aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina, alisema kuwa walipata taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kutoka kwa ndugu yake aliyeko Afrika Kusini kwamba alikuwa yuko kwenye hali mbaya, hali iliyowachanganya mno.

      Mmoja wa madaktari alikiri kupokea taarifa za kuzidiwa kwa mwenyekiti wao kutoka kwa kaka wa Dk. Ulimboka.

      “Leo asubuhi baada ya kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kikaitishwa kikao cha dharura cha madaktari wote tunaelekea huko,” alisema.

      Hata hivyo, majira ya mchana habari zilivuma kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, hali iliyozidi kuzusha wasiwasi mwingi miongoni mwa madaktari, viongozi wa vyama vya kijamii na wananchi wa kawaida waliokuwa wakihaha kupata ukweli wake.

      Uvumi huo hata hivyo, ulikanushwa baadaye na msemaji wa Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa MOI Almasi Jumaa lakini akakiri kupata taarifa za kubadilika kwa hali ya mgonjwa huyo.

      Huduma za matibabu MOI zasimama tena
      Taarifa za kutatanisha kuhusiana na hali ya Dk. Ulimboka, zilisababisha kusitishwa kwa huduma za matibabu katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) baada ya madaktari karibuni wote kwenda katika mkutano wa dharura kujadili tukio hilo.

      Habari za kuaminika kutoka MOI, zimethibisha kuwa taarifa za kuzidiwa na hata kuzuka kwa habari nyingine kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, ziliwachanganya kwa kiasi kikubwa madaktari hao, ambao walilazimika kusitisha huduma na kuwapangia wagonjwa tarehe nyingine za kurudi.

      Kutokana na hatua hiyo ya madaktari, wagonjwa waliofika MOI baada ya kusikia kwamba huduma zimerejea, walishindwa kupata tiba badala yake waliandikishwa majina, wakalipia na kupewa tarehe ya kurudi kwa madai kwamba hakuna madaktari wa kuwahudumia.
      Taarifa ya kurejea kwa madaktari hao ilitolewa juzi hospitalini hapo jana na Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Balozi Charles Mtalemwa na kusisitiza kwamba hospitali hiyo haiko katika mgomo kwa sasa.

      Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa waliokosa tiba, walidai kuchoshwa na usumbufu huo huku wakiwaomba madaktari hao kurejea kazini.

      “Nimekuja hapa tangu saa moja kulikua na foleni; wenzetu waliowahi walionana na madaktari lakini ilipofika saa nne tukaambiwa wote tuliojiandikisha turudi Alhamisi ijayo kwa sababu madaktari wanaenda kwenye kikao,” alisema Abdallah Haji mkazi wa Kimara.

      Kwa upande wake Jenipher Suka alisema inasikitisha kuona hivyo kwa sababu mama yake ambaye ni mgonjwa mkazi wa Dodoma amekuja akitegemea kupata tiba matokeo yake ameambiwa arudi tarehe 10 mwezi huu kwa kuwa hakuna madaktari kwa sasa.

      “Kwa nini serikali isiseme ukweli maana tunahangaika kuja mpaka huku halafu hakuna huduma? Vyombo vya habari vimetangaza kwamba mgomo umesitishwa lakini bado wanatudanganya wananchi kwa faida ya nani?” alilalamika Jenipher.

      Akizungumza kwa sharti la kutochapisha jina lake gazetini mmoja wa maofisa waandamizi wa hospitali hiyo alikiri kutokuwepo kwa huduma baada ya madaktari kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Unajua huduma zinazoendelea kwa sasa ni kliniki na upasuaji kwa waliowahi lakini hawa madaktari wamechanganyikiwa baada ya daktari mwenzao aliyeongozana na Dk. Ulimboka kuwaeleza kwamba hali ya mgonjwa ni mbaya mno.

      Kukosekana kwa huduma kulichangiwa na madaktari wanafunzi ambao hupokea na kuwahudumia wagonjwa kuwa katika maandalizi ya mitihani ya mwisho wa mwaka itakayoanza Jumatatu ya Julai 9, 2012 hivyo kusababisha huduma utoaji wa huduma kutokuwepo kabisa.

      Pinda abanwa
      MJINI Dodoma, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameshindwa kuliambia Bunge endapo serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dk. Ulimboka.

      Waziri Mkuu Pinda, alishindwa kutoa kauli wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (CHADEMA).
      Katika swali lake la nyongeza, Mbowe alisema kumekuwa na ongezeko la vitendo vya mauaji yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi.
      Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alitolea mfano wa tukio la kupigwa kwa wabunge wawili wa CHADEMA mkoani Mwanza na tukio la hivi karibuni la kutekwa na kupingwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Kwa kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio ya mauaji kwa raia wasio na hatia na kumekuwa na hisia kwamba matendo hayo yanafanywa na Jeshi la Polisi. Mfano wa matukio hayo ni pamoja na lile la kupigwa kwa wabunge wawili na hili la hivi karibuni la kutekwa kwa Dk. Ulimboka, tukio ambalo limelichafua taifa; je, serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza matukio hayo?” alihoji Mbowe.

      Akijibu swali hilo, Pinda kwanza alisema sio kweli kwamba tukio la kupigwa kwa Dk. Ulimboka limechafua sifa nzuri ya taifa.
      “Mh. Mbowe, kwanza tukio la Ulimboka sio mfano mzuri sana kwa sababu hakuna mwenye ushahidi wa serikali kuhusika kumteka na kumpiga Dk. Ulimboka.

      “Kama nilivyosema awali, sioni sababu ya serikali kuhusika na kipigo cha Ulimboka ambaye tulikuwa tukishirikiana naye vizuri kwenye vikao vya majadiliano,” alisema Pinda.

      Hata hivyo katika kujibu swali hilo, Pinda hakusema chochote kuhusu swali la Mbowe aliloitaka serikali kuunda tume huru kuchunguzwa tukio la Dk. Ulimboka.

      Badala yake alisisitiza kuwa serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika kumipiga Dk. Ulimboka.

      Akijibu swali la msingi la Mbowe aliyehoji utekelezaji wa sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata, Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwa mwaka jana aliahidi Bungeni kwamba serikali ingelikuja na sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata ili kuharakisha matokeo ya uchunguzi huo.

      Alisema serikali bado inaendelea na mchakato wa kuandaa sheria hiyo ili ianze kutumika.

      Mbowe alisema kumekuwa na kasi ya ongezeko la vifo vyenye utata vya raia wasio na hatia na vyombo vya dola, hasa polisi wamekuwa wakihusishwa na vifo hivyo.

      Alisema kuwa Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwapo na hali hiyo na kuahidi kuwa serikali ingekuja na sheria ya kuchunguza vifo vya aina hiyo.

      Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, kisha kutupwa katika msitu wa Pande, nje kidogo ya jiji Dar es Salaam.

      Jeshi la Polisi limeunda jopo kuchunguza tukio la utekaji nyara na shambulio la kudhuru mwili wa Dk. Ulimboka.

      Tangu kuibuka kwa tukio hilo, wabunge mbalimbali kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiibua hoja ya mgomo wa madaktari na kipigo cha Ulimboka, lakini kiti cha Spika kimekuwa kikizima kwa hoja kuwa jambo hilo liko mahakamani.


      CHANZO: Mwananchi
      Last edited by Return Of Undertaker; 5th July 2012 at 06:43.

    2. Miaka 50

    3. #61
      Mchaka Mchaka's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 20th July 2010
      Location : Ashmore and Cartier Islands
      Posts : 3,660
      Rep Power : 1206
      Likes Received
      918
      Likes Given
      459

      Default Re: Ulimboka mahututi

      kwa uweza wa jina kuu lipitalo majina yote nakemea roho ya mauti, ishindwe kwa jina la yesu! tuna imani yesu u mkuu bwana, nakuomba sasa tenda muujiza wako kwa ndugu yetu huyu, anakwenda kuamka sasa, mapafu na figo zinawekwa mpya! oooh jesus, your doing it! isee, jesus! jesus! jesus! yes yes! dot it for us our lord! nguvu za giza za watawala wa dunia zinakwenda kushindwa sasa, ooh! karaboooo sarabaine &*(&(((*&&*( jesus! asante yesu kwa kunisikia!!!!!!
      Miili ya waliokufa katika ajali ya Meli ya Spice Islander ipimwe DNA ili kutambua Ndugu zao - Dk. Jakaya .M. Kikwete,, September 2011.

    4. #62
      King2's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2011
      Posts : 1,280
      Rep Power : 636
      Likes Received
      159
      Likes Given
      0

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Kova Acha Unafiki. Kila mtu anajua serikali ya Ccm kupitia polisi ndio mmemfanyia huo unyama.

    5. #63
      Maundumula's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 5,050
      Rep Power : 3122
      Likes Received
      1376
      Likes Given
      5834

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Huko South Africa analipiwa na nani gharama za matibabu?

    6. #64
      Return Of Undertaker's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 665
      Rep Power : 543
      Likes Received
      465
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Edson
      bahari nzuri nimerekodi hiyo taarifa ya bbc na ninayo hapa...

      Ali mtasa mtangazaji wa bbc alikwenda hosp.moja huko africa ya kusini alokolazwa dr ulimboka.alipofika alienda maulizo na kuonyeshwa chumba alicholazwa. wakati akielekea huko alikutana n ndugu wa ulimbo walioko hapo hosp na yeye alimuona ulimboka kupitia kwenye vioo na wala hakuingia chumbani kabisa.

      alipojitmbulisha kwa ndugu wa ulimboka, mara moja walimuambia aondoke hosp hapo maana hawahitaji mtu na wala asifatilie lolote kuhusu maendeleo ya ulimboka.alipoulizia hali yake inakwendaje hakujibiwa kitu isipokuwa aliambiwa aondoke mara moja. na akaondoka....

      hiyo ya kusema kuwa dr uli yuko kwenye koma ameipika mwenyewe maana dr uli alikuwa amepumzika na wala hakunandugu hata mmoja aliyemwambia kuwa yuko kwenye koma..
      Bila shaka unasumulia na yawezekana ulikuwa usingizini kama umerekodi anza mwanzo mwisho then urudi ufute usemi wako

    7. #65
      Msafiri Kasian's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2011
      Posts : 1,119
      Rep Power : 613
      Likes Received
      113
      Likes Given
      72

      Default

      Quote By Ryaro wa Ryaro
      SASA HUO UCHUNGUZI AU TUME ILIYOUNDWA NA POLISI UHALALI WAKE HUKO WAPI MAANA WAO NI WATUHUMIWA. KATIKA NCHI YETU HAPAJAWAHI TOKEA POLISI WAKACHUNGUZI SWALA LOLOTE LINALOWAGUSA NA MATOKEO YAKAWA FAIR. BASI TUMWOMBE MUNGU NDG YETU APATE KUPONA MAANAKE IKITOKEA IKAWA VINGINEVYO KUNASITOFAHAMU KWA WAPENZI, NDUGU , MARAFIKI NA WAPENA HAKI. MATAMUSHI YA WATAWALA YANAONYESHA ''Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyohakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo,lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemeavizuri zaidi kuliko wao wenyewewalioajiriwa na Serikali.'
      Polisi/tume iliyoundwa unataka ichunguze nini wakati Rais ameshatoa tamko la serikali eti kutohusika?

    8. RukaaJuu Final

    9. #66
      HOPECOMFORT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2012
      Posts : 279
      Rep Power : 421
      Likes Received
      49
      Likes Given
      11

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Quote By OSOKONI
      Mbona hali ya huyu bwana haistabilize?? huenda watesaji wake walimuumiza sana! watu wote wapenda haki na wenye mapenzi mema tumuombee apone haraka! mungu amuwekee mkono wake wa uponyaji aweze kupona na kuungana na familia na watanzania kwa jumla!!
      kama ulisha wahi ngoa jino kwa ganzi still utakua na maumivu utakayo yapata, Sembuse mwenzetu alie umizwa kikatili kwa kungolewa kucha na jino!!! Hapa ni Mwenyenzi Mungu tu asimame.

      Tunazidi kukuombea ndugu yetu mpendwa Dr Ulimboka.

    10. #67
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1844
      Likes Received
      593
      Likes Given
      413

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      BBC.... Tuwe makini nao sio wasemaje wa familia ya Dr Ulimboka, jeshi la polisi wala serikali...

      Taarifa ambazo hazijachujwa kutoka chanzo kimoja zinaweza kutugombanisha ndani na nje ya JF...

      Tutafute ukweli zaidi kutoka vyanzo vingine ili kujiridhisha.

    11. #68
      English Learner's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st January 2012
      Location : Inside the Laptop
      Posts : 254
      Rep Power : 804
      Likes Received
      269
      Likes Given
      198

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Quote By MSOROPOGAS
      Dr ulimboka amewekewa mashine ya kupumulia na yuko mahututi (koma), mwandishi alimtembelea SA.
      Source: BBC idhaa ya kiswahili
      Luckily, the Ulimboka we LOVE is NOT in South Africa. However, I feel sorry for your Ulimboka!

      Quote By nngu007


      Wednesday, 04 July 2012 21:54



      TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI, RAFIKI YAKE ATOA USHUHUDA MPYA WA JINSI ALIVYOTEKWA

      Waandishi wetu

      WAKATI ikielezwa kwamba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka anatibiwa Afrika Kusini, kuna taarifa kwamba amelazwa katika hospitali moja ya huko Ujerumani.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa Dk Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini lakini alikaa kwa muda mfupi tu kabla ya kupelekwa Ujerumani anakoendelea na matibabu yake sasa.

      Awali, jopo la madaktari waliokuwa wanamtibu Dk Ulimboka hapa nchini lilieleza kuwa baada ya hali yake kuendelea kuwa mbaya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, waliamua kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

      “Ni kweli alikwenda kwanza Afrika Kusini, lakini hapo alipita tu. Ndege ilitua na akaunganisha ndege nyingine kwenda Ujerumani,” kilisema chanzo kimoja cha habari.
      Hata hivyo wakati chanzo hicho kikieleza hivyo, mmoja wa wanafamilia yake, alisema: “Sisi katika level (ngazi) ya familia tunajua yuko Afrika Kusini lakini hii haiwazuii madaktari kumhamishia kwenye hospitali nyingine wanayoona inafaa.”

      Mwanafamilia huyo ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alisema suala la Dk Ulimboka kuhamishiwa Ujerumani si la ajabu kwani anachotafuta ni matibabu ya uhakika.

      Alipoulizwa kuhusu habari hizo, Kiongozi wa Jopo la Madaktari waliokuwa wakimtibu, Profesa Joseph Kahamba alisema: Mimi ndiyo kwanza nasikia, lakini kwa nature (aina) ya tukio lake, si vyema ikaanikwa amepelekwa wapi. Pia si vizuri ikaelezwa yuko wapi ingawa tayari watu wanajua yuko Afrika Kusini.”

      “Kama kiongozi wa jopo la madaktari wanaomtibu Dk Ulimboka ninajua kwamba yuko Afrika Kusini ingawa hata hiyo taarifa tusingependa watu waijue kwa jinsi tukio lilivyokuwa.”

      Mmoja wa madaktari ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alipoulizwa juu ya suala hilo alipinga na kusema; “Habari za aina hiyo mtakuwa mnazipata nyingi, najua mtaandika, ndiyo maana mnaandika madaktari Muhimbili wanafanya kazi wakati si kweli”.

      Alisisitiza kuwa Dk Ulimboka yupo Afrika Kusini anakopatiwa matibabu na kusisitiza kuwa habari alizokuwa nazo tangu juzi jioni ni kwamba anaendelea vizuri.

      Katibu wa Chama cha Taifa cha Madaktari (MAT), Dk Rodrick Kabangila alipoulizwa juu ya hali ya Dk Ulimboka alisema kwa mujibu wa taarifa za juzi jioni alikuwa anaendelea vizuri.

      Alipoulizwa juu ya taarifa za kupelekwa Ujerumani aliguna kisha akasema: “Naomba ieleweke kuwa yupo Afrika ya Kusini kwa matibabu.

      Rafiki asimulia mkasa

      Rafiki wa karibu wa Dk Ulimboka aliyekuwa naye wakati mkasa wa kutekwa ukitokea, Dk. Deogratius Michael ameelezea tukio zima lilivyotokea na kusema ulikuwa wa kitaalamu na ulifanywa na watu wenye ujuzi na mambo hayo.

      Dk Deogratius alisema jana kwamba siku ya tukio walikuwa wametokea kwenye msiba wa ndugu wa mwalimu wao Profesa Yongolo na baada ya msiba walikwenda Viwanja vya Leaders saa moja usiku kuangalia taarifa ya habari na mambo mengine.

      Huko walikutana na madaktari wengine na ilipofika saa 4:00 usiku, Dk Ulimboka aliwaambia kwamba kuna jamaa alikuwa akimtafuta hivyo angependa kwenda kukutana naye.
      “Tukamwuliza anamtafutia nini? Akatueleza kuwa kwa siku tatu huyo jamaa anamtafuta. Wenzangu wakasema asiende mwenyewe na mimi ndiyo nikamsindikiza. Mara ya kwanza huyo jamaa alisema anaitwa Abeid na alisema yuko Sterio, tukaenda huko hatukumkuta tukaenda Hugo hatukumkuta lakini baadaye tukakutana naye maeneo ya Barabara ya Tunis karibu na Ofisi za Ultimate Security.”

      Dk Deogratius alisema wakati wakiendelea na mazungumzo, Abeid alikuwa akitaka kujua nini kinachotakiwa ili kutatua mgogoro uliopo wa madaktari.

      “Wakati tunamalizia mazungumzo nilikwenda msalani, niliporudi Abeid alikuwa akizungumza na simu kila wakati, tuliendelea na mazungumzo hadi tukamaliza na kuanza kuagana,” alisema.

      Alisema wakati wakiagana bado walikuwa wamekaa katika viti pamoja na Abeid... “Ghafla kuna watu walifika na kusema kuwa wanamtaka Dk Ulimboka. Walimchukua na kwenda naye katika gari. Walikuwa watano, walikuwa ‘giant’ (miili mikubwa) na ‘very skilled’ ( wenye uzoefu) wakamchukua Dk Ulimboka wakaenda naye kwenye gari,” alisema Dk Deogratius.

      Alisema wakati huo Abeid alikuwa anakimbia hivyo akamkimbilia ili ampe namba yake ya simu ambayo ingemsaidia kwa mawasiliano.

      “Alinipa namba yake nikampigia muda huohuo lakini nilipokuja kumpigia tena sikumpata na mpaka leo hapatikani,” alisema.

      Alisema baada ya tukio hilo alimpigia mke wa Dk Ulimboka na kumweleza na pia alipiga simu polisi kuwaeleza.

      “Nilikwenda polisi kutoa maelezo na nikawapa namba zangu za simu zote ili wanipigie kama watapata chochote, lakini mtu wa kwanza kunipigia asubuhi (kesho yake) alikuwa Juma Mgaza (aliyemwokota Dk Ulimboka) ambaye alinieleza kuwa kuna rafiki yangu amempa hiyo namba na kwamba yuko hoi amepigwa.”

      Alisema baada ya kupata simu hiyo aliwasiliana na watetezi wa haki za binadamu ambao walimtaka waende pamoja na kwamba walipokuwa njiani kuelekea Kituo cha Polisi Bunju alipigiwa simu na polisi wa kituo hicho.

      Kutokana na hali hiyo aliomba iundwe tume huru ikijumuisha wanasheria, madaktari na watu wengine ili ukweli ujulikane.

      Upelelezi wa Polisi
      Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jopo la upelelezi aliloteua hivi karibuni kushughulikia tukio zima la kutekwa kwa Dk Ulimboka litaendelea na kazi yake hadi mwisho na hatasikiliza kelele za wanaodai kutokuwa na imani nalo.

      Alisema madai yanayotolewa na watu mbalimbali akiwemo Dk Ulimboka mwenyewe kuwa hana imani na jopo hilo hazitabadili chochote kwani kinachofanyika hivi sasa ni kazi ya kawaida ya upelelezi ya jeshi hilo... “Hao wanaosema hawana imani na jopo hilo hawana hoja isipokuwa waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake.

      Kiongozi huyo wa mgomo wa madaktari alitekwa na kisha kujeruhiwa vibaya na baadaye kutelekezwa katika Msitu wa Pande.

      Habari hii imeandikwa na Geofrey Nyang’oro, Boniface Meena na Joseph Zablon
      Last edited by English Learner; 5th July 2012 at 08:41.

    12. #69
      kimweri Jr's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th June 2012
      Location : DODOMA TANZANIA
      Posts : 31
      Rep Power : 357
      Likes Received
      10
      Likes Given
      5

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Mungu ni muweza wa yote, amini usiamini ulimboka atapona.

    13. #70
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,658
      Rep Power : 16780
      Likes Received
      2521
      Likes Given
      1941

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Kumbe hali imekuwa mbaya namna hiyo. jamaa inawezekana bado wanamfuatilia hadi huko ili wammalize.

    14. #71
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1844
      Likes Received
      593
      Likes Given
      413

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Thread hii imeletwa hapa kupima joto la mgomo wa madaktari.

      kuna taarifa kwamba taasisi za nje zina mkono wao katika mgomo huo....BBC....BBC....BBC

    15. #72
      rosemarie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 4,732
      Rep Power : 1367
      Likes Received
      280
      Likes Given
      142

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Imany John
      "BBC Swahili~ Mwenyekiti wa chama cha
      madaktari nchini Tanzania
      Steve Ulimboka anaendelea
      kupokea matibabu katika
      hospitali moja mjini
      Johanesburg Afrika Kusini alikolazwa katika chumba cha
      wagonjwa mahututi.
      1 hour ago"

      Mwisho wa kunukuu

      Source:BBC PAGE FB.
      mbona tumeambiwa yukop ujerumani???
      ccm inakufa,asante mungu umesikia kilio chetu!!!!!!!

    16. #73
      LiverpoolFC's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2011
      Posts : 6,707
      Rep Power : 11284
      Likes Received
      1483
      Likes Given
      574

      Default Re: Ulimboka mahututi

      MUNGU MFARIJI WA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI, TUNA IMANI YA KWAMBA MAUTI HAINA MAMLAKA JUU YAKO MUNGU WETU,TUREHEMU NA HUYU MWENZETU APONE NA KURUDI NYUMBANI SALAMA SALIMINI MUNGU WETU!
      Roho mauti tunaitupilia mbali ktk jina lake YESU KIRSTO BWANA aliyehai sasa na hata milele!
      Tunaenda kinyume kbs na roho ya mauti kwani tuna Imani yupo MUNGU aliyewaepusha wale mafisadi kutomtoa roho huyu ndg yetu ktk ule msitu na leo hata huko alipo ataturudishia salama salimini.

      Kwa kuwa MUNGU upo tuna Imani ya kwmb Dr Ulimboka utaturudishia salama kabisa.

      Amen!
      Yummy likes this.

    17. #74
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1844
      Likes Received
      593
      Likes Given
      413

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By MNYISANZU
      Ritz, fahamu kwamba ya jana si ya leo. Now yuko ICU, tumwombee.
      Mungu atashindwa kujua tunachoomba kati ya maombi ya kuponya au maombi ya kutekwa


      suala la kumuombea ni letu wote lakini tusiongeze chumvi kama njia ya kuchonganisha sio wakati wake huu.

    18. #75
      kiraia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2007
      Location : Kowamrasa
      Posts : 647
      Rep Power : 717
      Likes Received
      83
      Likes Given
      476

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Hii habari imenisikitisha sana asubuhi na jinsi alivyoripoti Mutasa kwa sababu kashuhudia kwa macho, Waandishi wa udaku Bongo wameeandika hali ya ulimboka imezidi kuimarika sijui source ya information zao wanapata wapi.
      The most dangareous position in which to sleep is with your feet on your office desk.

    19. #76
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2885
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By kapotolo
      vyombo vya habari vyote vya Tanzania havina maana, njaa inavimaliza, vimekuwa vinaendesha tu propaganda kuhusu huu mgomo. Hii serikali naishangaa sana, pesa za kuhonga vyombo vyote vya habari wanazo lakini kutengeneza mazingira bora ya kufanyia kazi hawana. Huu ni ujuha wa dhaifu na serikali yake.

      Mimi binafsi nimemsikia mtangazaji wa BBC aliyemtembelea Uli hospitali akisema ulimboka yuko kwenye 'coma, na anapumua kwa kusaidiwa na mashine, wao wanasema hali yake inaimarika. Kweli Propaganda mpaka kwenye uhai wa mtu?.

      Angalia Jambo leo linavyoripoti kwe kejeli hali ya Afya ya ulimboka. Angalia jinsi Umma unavyopotoshwa kuhusu mgomo. Mgomo unaendelea ingawa kuna baadhi ya madaktari wa MOI walisaini mahudhurio na kuondoka, hakuna daktari anaefanya kazi, msiwadanganye watu wakatoka mikoani kwenda Muhi2.

      La kushangaza hata wanataaluma kama Prof Museru na Mwafongo nao wameingia kwenye usaliti wa taaluma na kuendelea propaganda za serikali. Hivi kufikia kumnyima hata ambulance colleague kwa sababu ya cheo au pesa ni ujuha au ni nini. Mwafongo, Museru na wengine Muhimbili, kumbukeni serikali hii ya kifisadi na kigaidi haina rafiki wa kudumu, itakapowageuka mtakumbuka ubaya mnaowafanyia wanataaluma wenzenu.
      pesa mdau,,,,,,pesaa acha tu

    20. #77
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1844
      Likes Received
      593
      Likes Given
      413

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By episodes
      mbona tumeambiwa yukop ujerumani???
      pia tuliambiwa alitekwa Leaders Club kumbe ni Club iliyo mkabara na ofisi za Ultermate security zilizopo mtaa wa Tunisia Kinondoni hatua takribani mia 200 kutoka Leaders club.


      chanzo ni Dr Deo alipokuwa anahojiwa na Radio clouds jana. Dr Deo alikuwa na Dr Ulimboka siku ya tukio....

    21. #78
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      clip ya omari mtasa hiyo hapo..wewe mleta mada sikiliza halafu uniambie ni wapi (kama utasikia) ndugu wa dr ulimboka wakimwambia kuwa ulimboko yuko kweye koma....yale yalikuwa mawazo yake hakuna aliyemwambia
      Attached Files
      I'm Naturaly Evasive..

    22. #79
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2885
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By MAMA POROJO
      Thread hii imeletwa hapa kupima joto la mgomo wa madaktari.

      kuna taarifa kwamba taasisi za nje zina mkono wao katika mgomo huo....BBC....BBC....BBC
      duh,,,,,,intelijensia hiyo.....

    23. #80
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default Re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Return Of Undertaker
      Bila shaka unasumulia na yawezekana ulikuwa usingizini kama umerekodi anza mwanzo mwisho then urudi ufute usemi wako
      mkuu saa tisa nilikuwa niko macho nimeshaoga ..nimekuwekea clipi hapo juu isikilize tena ...hakuna ndugu aliyempa taarifa ya maendeleo ya mgonjwa .alitolewa mkuku
      I'm Naturaly Evasive..

    Page 4 of 12 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...