Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

    Report Post
    Page 3 of 12 FirstFirst 12345 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 236
    1. #1
      Return Of Undertaker's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 654
      Rep Power : 539
      Likes Received
      448
      Likes Given
      0

      Default BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Source BBC na Omary Mutasa kutoka Afrika Kusini

      Ni wazi kuwa hali ya Dr. Steven Olimboka ni mbaya na kalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na anapumulia mashine, hajitambui wala haongei.

      Na kulingana na bbc kulingana na hali yake ilivyo hakuruhusiwa na familia yake kumwona na hawakutaka kuongelea swala la kutekwa na kauli ya JK kukana kuhusika.

      Wakati huo huo jeshi la polisi limetoa kauli hii

      ""Upelelezi wa Polisi Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jopo la upelelezi aliloteua hivi karibuni kushughulikia tukio zima la kutekwa kwa Dk Ulimboka litaendelea na kazi yake hadi mwisho na hatasikiliza kelele za wanaodai kutokuwa na imani nalo. Alisema madai yanayotolewa na watu mbalimbali akiwemo Dk Ulimboka mwenyewe kuwa hana imani na jopo hilo hazitabadili chochote kwani kinachofanyika hivi sasa ni kazi ya kawaida ya upelelezi ya jeshi hilo... “Hao wanaosema hawana imani na jopo hilo hawana hoja isipokuwa waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake."""

      Concern
      Ninashaka hapa hivi uchunguzi wa jeahi la polisi kama mimi mtendwa sitaki kwanini unalazimisha wakati sina imani na ulichokiunda na cha ajabu nawe unanambia hata kama hutaki sie tunaendelea.

      Nini kipo nyuma ya pazia la polisiiiiiii???
      Quote By TONGINDI
      Hali ya afya ya Dk. Steven Ulimboka ambaye anatibiwa Afrika Kusini, imebadilika ghafla na kuna habari kuwa yuko mahututi.

      Habari zilizoifikia Tanzania Daima kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi, zimesema kuwa Dk. Ulimboka alikuwa amepoteza fahamu, na juhudi za kuokoa maisha yake zilikuwa zikiendelea chini ya jopo la madaktari bingwa wa nchi hiyo na wale wa Tanzania.

      Inadaiwa kwamba hali ya kiongozi huyo wa jumuiya ya madaktari nchini ambaye alikimbizwa nchini humo wiki iliyopita, awali ilielezwa kuwa inaendelea vema, lakini ghafla ikabadilika na kufikia kiwango cha kupoteza fahamu.

      Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC) alikaririwa akisema kuwa hali ya Ulimboka ilikuwa mbaya, na kwamba kulikuwa na ulinzi na usiri mkubwa kuhusiana na hali hiyo.

      Jijini Dar es Salaam, mmoja wa madaktari aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina, alisema kuwa walipata taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kutoka kwa ndugu yake aliyeko Afrika Kusini kwamba alikuwa yuko kwenye hali mbaya, hali iliyowachanganya mno.

      Mmoja wa madaktari alikiri kupokea taarifa za kuzidiwa kwa mwenyekiti wao kutoka kwa kaka wa Dk. Ulimboka.

      “Leo asubuhi baada ya kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kikaitishwa kikao cha dharura cha madaktari wote tunaelekea huko,” alisema.

      Hata hivyo, majira ya mchana habari zilivuma kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, hali iliyozidi kuzusha wasiwasi mwingi miongoni mwa madaktari, viongozi wa vyama vya kijamii na wananchi wa kawaida waliokuwa wakihaha kupata ukweli wake.

      Uvumi huo hata hivyo, ulikanushwa baadaye na msemaji wa Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa MOI Almasi Jumaa lakini akakiri kupata taarifa za kubadilika kwa hali ya mgonjwa huyo.

      Huduma za matibabu MOI zasimama tena
      Taarifa za kutatanisha kuhusiana na hali ya Dk. Ulimboka, zilisababisha kusitishwa kwa huduma za matibabu katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) baada ya madaktari karibuni wote kwenda katika mkutano wa dharura kujadili tukio hilo.

      Habari za kuaminika kutoka MOI, zimethibisha kuwa taarifa za kuzidiwa na hata kuzuka kwa habari nyingine kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, ziliwachanganya kwa kiasi kikubwa madaktari hao, ambao walilazimika kusitisha huduma na kuwapangia wagonjwa tarehe nyingine za kurudi.

      Kutokana na hatua hiyo ya madaktari, wagonjwa waliofika MOI baada ya kusikia kwamba huduma zimerejea, walishindwa kupata tiba badala yake waliandikishwa majina, wakalipia na kupewa tarehe ya kurudi kwa madai kwamba hakuna madaktari wa kuwahudumia.
      Taarifa ya kurejea kwa madaktari hao ilitolewa juzi hospitalini hapo jana na Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Balozi Charles Mtalemwa na kusisitiza kwamba hospitali hiyo haiko katika mgomo kwa sasa.

      Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa waliokosa tiba, walidai kuchoshwa na usumbufu huo huku wakiwaomba madaktari hao kurejea kazini.

      “Nimekuja hapa tangu saa moja kulikua na foleni; wenzetu waliowahi walionana na madaktari lakini ilipofika saa nne tukaambiwa wote tuliojiandikisha turudi Alhamisi ijayo kwa sababu madaktari wanaenda kwenye kikao,” alisema Abdallah Haji mkazi wa Kimara.

      Kwa upande wake Jenipher Suka alisema inasikitisha kuona hivyo kwa sababu mama yake ambaye ni mgonjwa mkazi wa Dodoma amekuja akitegemea kupata tiba matokeo yake ameambiwa arudi tarehe 10 mwezi huu kwa kuwa hakuna madaktari kwa sasa.

      “Kwa nini serikali isiseme ukweli maana tunahangaika kuja mpaka huku halafu hakuna huduma? Vyombo vya habari vimetangaza kwamba mgomo umesitishwa lakini bado wanatudanganya wananchi kwa faida ya nani?” alilalamika Jenipher.

      Akizungumza kwa sharti la kutochapisha jina lake gazetini mmoja wa maofisa waandamizi wa hospitali hiyo alikiri kutokuwepo kwa huduma baada ya madaktari kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Unajua huduma zinazoendelea kwa sasa ni kliniki na upasuaji kwa waliowahi lakini hawa madaktari wamechanganyikiwa baada ya daktari mwenzao aliyeongozana na Dk. Ulimboka kuwaeleza kwamba hali ya mgonjwa ni mbaya mno.

      Kukosekana kwa huduma kulichangiwa na madaktari wanafunzi ambao hupokea na kuwahudumia wagonjwa kuwa katika maandalizi ya mitihani ya mwisho wa mwaka itakayoanza Jumatatu ya Julai 9, 2012 hivyo kusababisha huduma utoaji wa huduma kutokuwepo kabisa.

      Pinda abanwa
      MJINI Dodoma, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameshindwa kuliambia Bunge endapo serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dk. Ulimboka.

      Waziri Mkuu Pinda, alishindwa kutoa kauli wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (CHADEMA).
      Katika swali lake la nyongeza, Mbowe alisema kumekuwa na ongezeko la vitendo vya mauaji yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi.
      Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alitolea mfano wa tukio la kupigwa kwa wabunge wawili wa CHADEMA mkoani Mwanza na tukio la hivi karibuni la kutekwa na kupingwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Kwa kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio ya mauaji kwa raia wasio na hatia na kumekuwa na hisia kwamba matendo hayo yanafanywa na Jeshi la Polisi. Mfano wa matukio hayo ni pamoja na lile la kupigwa kwa wabunge wawili na hili la hivi karibuni la kutekwa kwa Dk. Ulimboka, tukio ambalo limelichafua taifa; je, serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza matukio hayo?” alihoji Mbowe.

      Akijibu swali hilo, Pinda kwanza alisema sio kweli kwamba tukio la kupigwa kwa Dk. Ulimboka limechafua sifa nzuri ya taifa.
      “Mh. Mbowe, kwanza tukio la Ulimboka sio mfano mzuri sana kwa sababu hakuna mwenye ushahidi wa serikali kuhusika kumteka na kumpiga Dk. Ulimboka.

      “Kama nilivyosema awali, sioni sababu ya serikali kuhusika na kipigo cha Ulimboka ambaye tulikuwa tukishirikiana naye vizuri kwenye vikao vya majadiliano,” alisema Pinda.

      Hata hivyo katika kujibu swali hilo, Pinda hakusema chochote kuhusu swali la Mbowe aliloitaka serikali kuunda tume huru kuchunguzwa tukio la Dk. Ulimboka.

      Badala yake alisisitiza kuwa serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika kumipiga Dk. Ulimboka.

      Akijibu swali la msingi la Mbowe aliyehoji utekelezaji wa sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata, Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwa mwaka jana aliahidi Bungeni kwamba serikali ingelikuja na sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata ili kuharakisha matokeo ya uchunguzi huo.

      Alisema serikali bado inaendelea na mchakato wa kuandaa sheria hiyo ili ianze kutumika.

      Mbowe alisema kumekuwa na kasi ya ongezeko la vifo vyenye utata vya raia wasio na hatia na vyombo vya dola, hasa polisi wamekuwa wakihusishwa na vifo hivyo.

      Alisema kuwa Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwapo na hali hiyo na kuahidi kuwa serikali ingekuja na sheria ya kuchunguza vifo vya aina hiyo.

      Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, kisha kutupwa katika msitu wa Pande, nje kidogo ya jiji Dar es Salaam.

      Jeshi la Polisi limeunda jopo kuchunguza tukio la utekaji nyara na shambulio la kudhuru mwili wa Dk. Ulimboka.

      Tangu kuibuka kwa tukio hilo, wabunge mbalimbali kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiibua hoja ya mgomo wa madaktari na kipigo cha Ulimboka, lakini kiti cha Spika kimekuwa kikizima kwa hoja kuwa jambo hilo liko mahakamani.


      CHANZO: Mwananchi
      Last edited by Return Of Undertaker; 5th July 2012 at 06:43.

    2. Study Abroad

    3. #41
      Ubungo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 1,151
      Rep Power : 589
      Likes Received
      204
      Likes Given
      185

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Mwenyezi Mungu amjalie afya njemaDr Steven.

    4. #42
      Duduwasha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Posts : 2,620
      Rep Power : 6248
      Likes Received
      523
      Likes Given
      418

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Nilisikiliza BBC Pia

    5. #43
      OLUKUNDO's Avatar
      Member Array
      Join Date : 25th January 2012
      Posts : 53
      Rep Power : 379
      Likes Received
      6
      Likes Given
      10

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Tunamwombea kwa mungu apone haraka.
      Waliofanya kitendo hiki watambue kwamba nao siku zao zinahesabika.

    6. #44
      Mzalendo Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Posts : 547
      Rep Power : 547
      Likes Received
      91
      Likes Given
      285

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Concern
      Ninashaka hapa hivi uchunguzi wa jeahi la polisi kama mimi mtendwa sitaki kwanini unalaImisha wakati sina imani na ulichokiunda na cha ajabu nawe unanambia hata kama hutaki sie tunaendelea. Nini kipo nyuma ya pazia la polisiiiiiii???[/QUOTE]

      Bro sisi sote tunatakiwa kuonyesha uelewa wetu. Unachosema ni kuwa mtu UNAWEZA KUMUUA MWANAO NA KUSEMA KUWA NI MWANANGU. Au unaweza kunywa sumu na ukasema NIMEJIDHURU MWENYEWE! Mambo hayaendi hivyo. Polisi kazi yake ni kufanya uchunguzi hata kama wasingetangaza. Hiyo ni kazi yao ya msingi. Jambo la muhimu ni kuwa mazingira ya jambo lenyewe ni vigumu sana kupata ukweli wa mambo. Nionavyo mimi hata kama uchunguzi ufanywe na madaktari wenye bado ni VIGUMU KUPATA MAJIBU. Waacheni polisi wafanye na majibu yao KWA VYOVYOTE VILE HAYATAMSAIDIA ULIMBOKA. Ni fomalities tu.
      Straight corner likes this.

    7. #45
      Kiumbo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2012
      Posts : 478
      Rep Power : 463
      Likes Received
      71
      Likes Given
      0

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Determine amesema hali ya uli inaimarika na kwa bbc hali yake ni tete na huku hawakuruhusiwa kumwona. Je bbc walijuaje km ni mahututi icu. Tumwamini nani jamani. Tunataka mpiganaji wetu apone.Mungu amsaidie uli.
      MAMA POROJO likes this.

    8. Miaka 50

    9. #46
      Mamndenyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 11,898
      Rep Power : 31776
      Likes Received
      5876
      Likes Given
      19165

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      wana maombi fanyeni kazi yenu.
      "Mpingeni shetani naye atakimbia"
      SIYO WOTE WANAOTANGATANGA WAMEPOTEA

    10. #47
      kapotolo's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 19th September 2010
      Location : Tanzania
      Posts : 2,405
      Rep Power : 1195
      Likes Received
      1281
      Likes Given
      390

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Bajabiri
      tell us whom u trust mdau....apelejwe wapi sasa????ambako kuna usalama wake....
      gazeti la nipashe lasema AFYA YA DR ULIMBOKA YAZIDI KUIMARIKA
      vyombo vya habari vyote vya Tanzania havina maana, njaa inavimaliza, vimekuwa vinaendesha tu propaganda kuhusu huu mgomo. Hii serikali naishangaa sana, pesa za kuhonga vyombo vyote vya habari wanazo lakini kutengeneza mazingira bora ya kufanyia kazi hawana. Huu ni ujuha wa dhaifu na serikali yake.

      Mimi binafsi nimemsikia mtangazaji wa BBC aliyemtembelea Uli hospitali akisema ulimboka yuko kwenye 'coma, na anapumua kwa kusaidiwa na mashine, wao wanasema hali yake inaimarika. Kweli Propaganda mpaka kwenye uhai wa mtu?.

      Angalia Jambo leo linavyoripoti kwe kejeli hali ya Afya ya ulimboka. Angalia jinsi Umma unavyopotoshwa kuhusu mgomo. Mgomo unaendelea ingawa kuna baadhi ya madaktari wa MOI walisaini mahudhurio na kuondoka, hakuna daktari anaefanya kazi, msiwadanganye watu wakatoka mikoani kwenda Muhi2.

      La kushangaza hata wanataaluma kama Prof Museru na Mwafongo nao wameingia kwenye usaliti wa taaluma na kuendelea propaganda za serikali. Hivi kufikia kumnyima hata ambulance colleague kwa sababu ya cheo au pesa ni ujuha au ni nini. Mwafongo, Museru na wengine Muhimbili, kumbukeni serikali hii ya kifisadi na kigaidi haina rafiki wa kudumu, itakapowageuka mtakumbuka ubaya mnaowafanyia wanataaluma wenzenu.
      Kiongozi shupavu hawezi kutumia mabavu kuongoza, ni kiongozi dhaifu tu ndio atatumia mabavu kuficha udhaifu wake - Jenerali Ulimwengu

    11. #48
      Gwallo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Posts : 661
      Rep Power : 568
      Likes Received
      79
      Likes Given
      86

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Mungu uliyemwokoa Ulimboka na kifo pale msituni tunakuomba umponye sasa..Amina!!!!!!!

    12. #49
      Ryaro wa Ryaro's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th October 2010
      Location : Musoma Majita
      Posts : 184
      Rep Power : 473
      Likes Received
      52
      Likes Given
      31

      Default Re: Ulimboka mahututi

      SASA HUO UCHUNGUZI AU TUME ILIYOUNDWA NA POLISI UHALALI WAKE HUKO WAPI MAANA WAO NI WATUHUMIWA. KATIKA NCHI YETU HAPAJAWAHI TOKEA POLISI WAKACHUNGUZI SWALA LOLOTE LINALOWAGUSA NA MATOKEO YAKAWA FAIR. BASI TUMWOMBE MUNGU NDG YETU APATE KUPONA MAANAKE IKITOKEA IKAWA VINGINEVYO KUNASITOFAHAMU KWA WAPENZI, NDUGU , MARAFIKI NA WAPENA HAKI. MATAMUSHI YA WATAWALA YANAONYESHA ''Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyohakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo,lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemeavizuri zaidi kuliko wao wenyewewalioajiriwa na Serikali.'

    13. #50
      Mwikimbi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2008
      Posts : 1,543
      Rep Power : 948
      Likes Received
      346
      Likes Given
      128

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Natamani kumowna akishuka kwenye ndege alitembea mwenyewe na kuzungumza na waandishi wa habari pale jk nyerere airport, ee mungu tunkuomba utimize ndoto yetu waja wako iwe kweli!
      HOPECOMFORT likes this.

    14. #51
      miss strong's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2012
      Posts : 637
      Rep Power : 473
      Likes Received
      127
      Likes Given
      62

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Yan watu wengne wanaleta siasa ht kwenye uhai wa mtu.Tunawawahis kuwa nao ni wahusika lakin bdo wanajichunguza....Naomba Mungu dkt MBOKA apone la sivyo tutaandamana mpk ikulu watu wa Mbeya mnatunyanyasa kwa kutuulia rasilimal zetu!

    15. #52
      iseesa's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 940
      Rep Power : 0
      Likes Received
      204
      Likes Given
      53

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Quote By Ryaro wa Ryaro
      SASA HUO UCHUNGUZI AU TUME ILIYOUNDWA NA POLISI UHALALI WAKE HUKO WAPI MAANA WAO NI WATUHUMIWA. KATIKA NCHI YETU HAPAJAWAHI TOKEA POLISI WAKACHUNGUZI SWALA LOLOTE LINALOWAGUSA NA MATOKEO YAKAWA FAIR. BASI TUMWOMBE MUNGU NDG YETU APATE KUPONA MAANAKE IKITOKEA IKAWA VINGINEVYO KUNASITOFAHAMU KWA WAPENZI, NDUGU , MARAFIKI NA WAPENA HAKI. MATAMUSHI YA WATAWALA YANAONYESHA ''Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyohakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo,lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemeavizuri zaidi kuliko wao wenyewewalioajiriwa na Serikali.'
      Kutokuwa mtumishi wa serikali hakumuondolei U-Tanzania wake na ubinadamu wake

    16. #53
      andrewk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th April 2010
      Posts : 2,220
      Rep Power : 906
      Likes Received
      283
      Likes Given
      59

      Default Re: Ulimboka mahututi

      sasa huyo wa BBC karuhusiwaje kumuona huko? na si wanasema yuko Ujerumani? ina maana kuna mtu anatuchakachua hapa na habari sio! ngoja tuone

    17. #54
      cacico's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th March 2012
      Location : DSM
      Posts : 7,044
      Rep Power : 14517
      Likes Received
      6408
      Likes Given
      4998

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Determine
      Doctor anaendelea vzr,sema hatuwataki hawa BBC waende kumuona@ km kuna mtu hataki Dr ulimboka kupona bora ajinyonge make Doctor kashaanza kuimarika
      at least utanifanya ninywe chai! natamani kusikia jk ndiyo anapumulia mashine, nitashinda nikinywa calabash!
      Tuko and Determine like this.
      "the problem is not me! the problem is you understading me!"

    18. #55
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,154
      Rep Power : 24267
      Likes Received
      4668
      Likes Given
      2294

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Mungu mtakatifu aliyemwepusha na kifo katika msitu wa mabwepande awe pamoja naye hata SA.
      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    19. #56
      Join Date : 25th February 2012
      Posts : 279
      Rep Power : 420
      Likes Received
      49
      Likes Given
      11

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Eee Mwenyenzi Mungu msaisaidie.

    20. #57
      King2's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2011
      Posts : 1,280
      Rep Power : 635
      Likes Received
      159
      Likes Given
      0

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Kikwete, Pinda, mtoto wa Mwinyi, kova. Kweli wanajisikiaje kumuona mwenzao anateseka.

    21. #58
      HOPECOMFORT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2012
      Posts : 279
      Rep Power : 420
      Likes Received
      49
      Likes Given
      11

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Quote By Mwikimbi
      Natamani kumowna akishuka kwenye ndege alitembea mwenyewe na kuzungumza na waandishi wa habari pale jk nyerere airport, ee mungu tunkuomba utimize ndoto yetu waja wako iwe kweli!
      Aaamen

    22. #59
      PakaJimmy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2009
      Posts : 14,681
      Rep Power : 22519
      Likes Received
      6338
      Likes Given
      2831

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Mungu mponye kijana huyu. Imani yetu ni kwamba atapona na kurudi nyumbani salama.

    23. #60
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      bahari nzuri nimerekodi hiyo taarifa ya bbc na ninayo hapa...

      Ali mtasa mtangazaji wa bbc alikwenda hosp.moja huko africa ya kusini alokolazwa dr ulimboka.alipofika alienda maulizo na kuonyeshwa chumba alicholazwa. wakati akielekea huko alikutana n ndugu wa ulimbo walioko hapo hosp na yeye alimuona ulimboka kupitia kwenye vioo na wala hakuingia chumbani kabisa.

      alipojitmbulisha kwa ndugu wa ulimboka, mara moja walimuambia aondoke hosp hapo maana hawahitaji mtu na wala asifatilie lolote kuhusu maendeleo ya ulimboka.alipoulizia hali yake inakwendaje hakujibiwa kitu isipokuwa aliambiwa aondoke mara moja. na akaondoka....

      hiyo ya kusema kuwa dr uli yuko kwenye koma ameipika mwenyewe maana dr uli alikuwa amepumzika na wala hakunandugu hata mmoja aliyemwambia kuwa yuko kwenye koma..
      I'm Naturaly Evasive..

    24. FemaTV & Radio
    Page 3 of 12 FirstFirst 12345 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...