Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

    Report Post
    Page 2 of 12 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 236
    1. #1
      Return Of Undertaker's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 695
      Rep Power : 553
      Likes Received
      483
      Likes Given
      0

      Default BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Source BBC na Omary Mutasa kutoka Afrika Kusini

      Ni wazi kuwa hali ya Dr. Steven Olimboka ni mbaya na kalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na anapumulia mashine, hajitambui wala haongei.

      Na kulingana na bbc kulingana na hali yake ilivyo hakuruhusiwa na familia yake kumwona na hawakutaka kuongelea swala la kutekwa na kauli ya JK kukana kuhusika.

      Wakati huo huo jeshi la polisi limetoa kauli hii

      ""Upelelezi wa Polisi Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jopo la upelelezi aliloteua hivi karibuni kushughulikia tukio zima la kutekwa kwa Dk Ulimboka litaendelea na kazi yake hadi mwisho na hatasikiliza kelele za wanaodai kutokuwa na imani nalo. Alisema madai yanayotolewa na watu mbalimbali akiwemo Dk Ulimboka mwenyewe kuwa hana imani na jopo hilo hazitabadili chochote kwani kinachofanyika hivi sasa ni kazi ya kawaida ya upelelezi ya jeshi hilo... “Hao wanaosema hawana imani na jopo hilo hawana hoja isipokuwa waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake."""

      Concern
      Ninashaka hapa hivi uchunguzi wa jeahi la polisi kama mimi mtendwa sitaki kwanini unalazimisha wakati sina imani na ulichokiunda na cha ajabu nawe unanambia hata kama hutaki sie tunaendelea.

      Nini kipo nyuma ya pazia la polisiiiiiii???
      Quote By TONGINDI View Post
      Hali ya afya ya Dk. Steven Ulimboka ambaye anatibiwa Afrika Kusini, imebadilika ghafla na kuna habari kuwa yuko mahututi.

      Habari zilizoifikia Tanzania Daima kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi, zimesema kuwa Dk. Ulimboka alikuwa amepoteza fahamu, na juhudi za kuokoa maisha yake zilikuwa zikiendelea chini ya jopo la madaktari bingwa wa nchi hiyo na wale wa Tanzania.

      Inadaiwa kwamba hali ya kiongozi huyo wa jumuiya ya madaktari nchini ambaye alikimbizwa nchini humo wiki iliyopita, awali ilielezwa kuwa inaendelea vema, lakini ghafla ikabadilika na kufikia kiwango cha kupoteza fahamu.

      Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC) alikaririwa akisema kuwa hali ya Ulimboka ilikuwa mbaya, na kwamba kulikuwa na ulinzi na usiri mkubwa kuhusiana na hali hiyo.

      Jijini Dar es Salaam, mmoja wa madaktari aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina, alisema kuwa walipata taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kutoka kwa ndugu yake aliyeko Afrika Kusini kwamba alikuwa yuko kwenye hali mbaya, hali iliyowachanganya mno.

      Mmoja wa madaktari alikiri kupokea taarifa za kuzidiwa kwa mwenyekiti wao kutoka kwa kaka wa Dk. Ulimboka.

      “Leo asubuhi baada ya kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka kikaitishwa kikao cha dharura cha madaktari wote tunaelekea huko,” alisema.

      Hata hivyo, majira ya mchana habari zilivuma kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, hali iliyozidi kuzusha wasiwasi mwingi miongoni mwa madaktari, viongozi wa vyama vya kijamii na wananchi wa kawaida waliokuwa wakihaha kupata ukweli wake.

      Uvumi huo hata hivyo, ulikanushwa baadaye na msemaji wa Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa MOI Almasi Jumaa lakini akakiri kupata taarifa za kubadilika kwa hali ya mgonjwa huyo.

      Huduma za matibabu MOI zasimama tena
      Taarifa za kutatanisha kuhusiana na hali ya Dk. Ulimboka, zilisababisha kusitishwa kwa huduma za matibabu katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) baada ya madaktari karibuni wote kwenda katika mkutano wa dharura kujadili tukio hilo.

      Habari za kuaminika kutoka MOI, zimethibisha kuwa taarifa za kuzidiwa na hata kuzuka kwa habari nyingine kwamba Dk. Ulimboka alikuwa amefariki, ziliwachanganya kwa kiasi kikubwa madaktari hao, ambao walilazimika kusitisha huduma na kuwapangia wagonjwa tarehe nyingine za kurudi.

      Kutokana na hatua hiyo ya madaktari, wagonjwa waliofika MOI baada ya kusikia kwamba huduma zimerejea, walishindwa kupata tiba badala yake waliandikishwa majina, wakalipia na kupewa tarehe ya kurudi kwa madai kwamba hakuna madaktari wa kuwahudumia.
      Taarifa ya kurejea kwa madaktari hao ilitolewa juzi hospitalini hapo jana na Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Balozi Charles Mtalemwa na kusisitiza kwamba hospitali hiyo haiko katika mgomo kwa sasa.

      Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa waliokosa tiba, walidai kuchoshwa na usumbufu huo huku wakiwaomba madaktari hao kurejea kazini.

      “Nimekuja hapa tangu saa moja kulikua na foleni; wenzetu waliowahi walionana na madaktari lakini ilipofika saa nne tukaambiwa wote tuliojiandikisha turudi Alhamisi ijayo kwa sababu madaktari wanaenda kwenye kikao,” alisema Abdallah Haji mkazi wa Kimara.

      Kwa upande wake Jenipher Suka alisema inasikitisha kuona hivyo kwa sababu mama yake ambaye ni mgonjwa mkazi wa Dodoma amekuja akitegemea kupata tiba matokeo yake ameambiwa arudi tarehe 10 mwezi huu kwa kuwa hakuna madaktari kwa sasa.

      “Kwa nini serikali isiseme ukweli maana tunahangaika kuja mpaka huku halafu hakuna huduma? Vyombo vya habari vimetangaza kwamba mgomo umesitishwa lakini bado wanatudanganya wananchi kwa faida ya nani?” alilalamika Jenipher.

      Akizungumza kwa sharti la kutochapisha jina lake gazetini mmoja wa maofisa waandamizi wa hospitali hiyo alikiri kutokuwepo kwa huduma baada ya madaktari kupokea taarifa za kuzidiwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Unajua huduma zinazoendelea kwa sasa ni kliniki na upasuaji kwa waliowahi lakini hawa madaktari wamechanganyikiwa baada ya daktari mwenzao aliyeongozana na Dk. Ulimboka kuwaeleza kwamba hali ya mgonjwa ni mbaya mno.

      Kukosekana kwa huduma kulichangiwa na madaktari wanafunzi ambao hupokea na kuwahudumia wagonjwa kuwa katika maandalizi ya mitihani ya mwisho wa mwaka itakayoanza Jumatatu ya Julai 9, 2012 hivyo kusababisha huduma utoaji wa huduma kutokuwepo kabisa.

      Pinda abanwa
      MJINI Dodoma, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameshindwa kuliambia Bunge endapo serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dk. Ulimboka.

      Waziri Mkuu Pinda, alishindwa kutoa kauli wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (CHADEMA).
      Katika swali lake la nyongeza, Mbowe alisema kumekuwa na ongezeko la vitendo vya mauaji yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi.
      Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alitolea mfano wa tukio la kupigwa kwa wabunge wawili wa CHADEMA mkoani Mwanza na tukio la hivi karibuni la kutekwa na kupingwa kwa Dk. Ulimboka.

      “Kwa kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio ya mauaji kwa raia wasio na hatia na kumekuwa na hisia kwamba matendo hayo yanafanywa na Jeshi la Polisi. Mfano wa matukio hayo ni pamoja na lile la kupigwa kwa wabunge wawili na hili la hivi karibuni la kutekwa kwa Dk. Ulimboka, tukio ambalo limelichafua taifa; je, serikali iko tayari kuunda tume huru kuchunguza matukio hayo?” alihoji Mbowe.

      Akijibu swali hilo, Pinda kwanza alisema sio kweli kwamba tukio la kupigwa kwa Dk. Ulimboka limechafua sifa nzuri ya taifa.
      “Mh. Mbowe, kwanza tukio la Ulimboka sio mfano mzuri sana kwa sababu hakuna mwenye ushahidi wa serikali kuhusika kumteka na kumpiga Dk. Ulimboka.

      “Kama nilivyosema awali, sioni sababu ya serikali kuhusika na kipigo cha Ulimboka ambaye tulikuwa tukishirikiana naye vizuri kwenye vikao vya majadiliano,” alisema Pinda.

      Hata hivyo katika kujibu swali hilo, Pinda hakusema chochote kuhusu swali la Mbowe aliloitaka serikali kuunda tume huru kuchunguzwa tukio la Dk. Ulimboka.

      Badala yake alisisitiza kuwa serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika kumipiga Dk. Ulimboka.

      Akijibu swali la msingi la Mbowe aliyehoji utekelezaji wa sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata, Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwa mwaka jana aliahidi Bungeni kwamba serikali ingelikuja na sheria ya uchunguzi wa vifo vyenye utata ili kuharakisha matokeo ya uchunguzi huo.

      Alisema serikali bado inaendelea na mchakato wa kuandaa sheria hiyo ili ianze kutumika.

      Mbowe alisema kumekuwa na kasi ya ongezeko la vifo vyenye utata vya raia wasio na hatia na vyombo vya dola, hasa polisi wamekuwa wakihusishwa na vifo hivyo.

      Alisema kuwa Waziri Mkuu Pinda alikiri kuwapo na hali hiyo na kuahidi kuwa serikali ingekuja na sheria ya kuchunguza vifo vya aina hiyo.

      Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, kisha kutupwa katika msitu wa Pande, nje kidogo ya jiji Dar es Salaam.

      Jeshi la Polisi limeunda jopo kuchunguza tukio la utekaji nyara na shambulio la kudhuru mwili wa Dk. Ulimboka.

      Tangu kuibuka kwa tukio hilo, wabunge mbalimbali kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiibua hoja ya mgomo wa madaktari na kipigo cha Ulimboka, lakini kiti cha Spika kimekuwa kikizima kwa hoja kuwa jambo hilo liko mahakamani.


      CHANZO: Mwananchi
      Last edited by Return Of Undertaker; 5th July 2012 at 06:43.


    2. #21
      genekai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th February 2010
      Location : Loitering!
      Posts : 7,690
      Rep Power : 2122
      Likes Received
      1158
      Likes Given
      1601

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Pole Dr Uli, huyo Kova akae kimya tu!!!!
      The future of this country is being jeopardized by the intellectual slavery of our top leaders

    3. #22
      wakuziba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th June 2012
      Posts : 123
      Rep Power : 585
      Likes Received
      42
      Likes Given
      43

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      hata mimi nimesikia kwenye taarifa ya habari ya bbc leo saa 12 asubuhi. mwandishi wa bbc afrika ya kusini Omar Mutaasa alizuru jana jioni hospitali aliko lazwa ulimboka. alimkuta icu akipumulia mashine na hajitambui

    4. #23
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2888
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By WA-UKENYENGE View Post
      Duh, Mungu atusaidie na kumponya ndugu yetu!! I don't trust these guys from SA.
      tell us whom u trust mdau....apelejwe wapi sasa????ambako kuna usalama wake

    5. #24
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2888
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By WA-UKENYENGE View Post
      Duh, Mungu atusaidie na kumponya ndugu yetu!! I don't trust these guys from SA.
      tell us whom u trust mdau....apelejwe wapi sasa????ambako kuna usalama wake....
      gazeti la nipashe lasema AFYA YA DR ULIMBOKA YAZIDI KUIMARIKA

    6. #25
      Mnyamahodzo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd May 2008
      Posts : 1,458
      Rep Power : 978
      Likes Received
      356
      Likes Given
      217

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Mkuu RoU, kupumulia mashine, kutokujitambua na kushindwa kuongea kwa mgonjwa aliye ICU siyo KOMA (coma as described in medicine)


    7. #26
      WA-UKENYENGE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2011
      Location : Inside a Smart Grid
      Posts : 2,486
      Rep Power : 5056
      Likes Received
      804
      Likes Given
      1889

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Bajabiri View Post
      tell us whom u trust mdau
      Quote By Bajabiri View Post
      tell us whom u trust mdau....apelejwe wapi sasa????ambako kuna usalama wake
      Hawa hawa waSA wanaotuibia mali ghafi zetu kupitia wakala wao wa serikali yetu watafurahia kuona wakala wao wakipata misukosuko kweli!! swali lako gumu!! However, our prayer for Dr. Ulli! Get well soon Dr.
      "The usual conclusion is that you can't put a price on a human life. But you can if you must".

    8. #27
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2888
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By wakuziba View Post
      hata mimi nimesikia kwenye taarifa ya habari ya bbc leo saa 12 asubuhi. mwandishi wa bbc afrika ya kusini Omar Mutaasa alizuru jana jioni hospitali aliko lazwa ulimboka. alimkuta icu akipumulia mashine na hajitambui
      gazeti la mwananch nalo linasema utata watanda nchi anayotibiwa ULIMBOKA,wasema yupo UJERUMAN,ILA S.A alikaa kwa muda mfupi

    9. #28
      Precise pangolin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 4th January 2012
      Posts : 5,758
      Rep Power : 1931
      Likes Received
      1609
      Likes Given
      684

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By zomba View Post
      Hizo nilizokuwekea rangi nyekundu ndio nini? fafanua.
      Hapa ndio huwa unatafutia watu ban

    10. #29
      WA-UKENYENGE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2011
      Location : Inside a Smart Grid
      Posts : 2,486
      Rep Power : 5056
      Likes Received
      804
      Likes Given
      1889

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Bajabiri View Post
      tell us whom u trust mdau....apelejwe wapi sasa????ambako kuna usalama wake....
      gazeti la nipashe lasema AFYA YA DR ULIMBOKA YAZIDI KUIMARIKA
      That's good news, unajua hizi habari zinachanganya, sijui ndo kuna mamluki yanasambaza hizi propaganda mbaya!! Hii serikali yetu imeishiwa mbinu za kutuongoza!!
      "The usual conclusion is that you can't put a price on a human life. But you can if you must".

    11. #30
      Return Of Undertaker's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 695
      Rep Power : 553
      Likes Received
      483
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Precise pangolin View Post
      Hapa ndio huwa unatafutia watu ban
      Kukaa kimya ni jibu la mjinga

    12. #31
      WA-UKENYENGE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2011
      Location : Inside a Smart Grid
      Posts : 2,486
      Rep Power : 5056
      Likes Received
      804
      Likes Given
      1889

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Bajabiri View Post
      gazeti la mwananch nalo linasema utata watanda nchi anayotibiwa ULIMBOKA,wasema yupo UJERUMAN,ILA S.A alikaa kwa muda mfupi
      Naweza kuamini hilo la Ujeruman!!
      "The usual conclusion is that you can't put a price on a human life. But you can if you must".

    13. #32
      Ubungo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 1,151
      Rep Power : 593
      Likes Received
      204
      Likes Given
      185

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Mwenyezi Mungu amjalie apone na arudi salama

    14. #33
      Determine's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th April 2012
      Posts : 238
      Rep Power : 407
      Likes Received
      76
      Likes Given
      96

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Doctor anaendelea vzr,sema hatuwataki hawa BBC waende kumuona@ km kuna mtu hataki Dr ulimboka kupona bora ajinyonge make Doctor kashaanza kuimarika
      Manyi likes this.
      Kikwete ni Jasiri Sana

    15. #34
      Kigogo's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 14th December 2007
      Location : Calabash
      Posts : 8,484
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1302
      Likes Given
      318

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Ritz View Post
      Wewe mbona ueleweki kila muda unakuja na habari za kushtua auminiki jinsi unavyoleta habari inawezekana unaongeza na yako, jana tumeambiwa anaendelea vizuri na figo zake zimeanza kufanya kazi.

      Wengine wanasema Dr Ulimboka yupo Ujerumani.
      teeh si umuulize baba au naye hajui..hahaaaaa

    16. #35
      Asprin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 8th March 2008
      Location : Psychiatric Ward
      Posts : 25,635
      Rep Power : 32119
      Likes Received
      14716
      Likes Given
      22280

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Mijamaa itakuwa imemuwekea dawa ya kumuua taratibu au???
      ....Shimo La Panya Halizibwi Kwa Mkate.....

    17. #36
      Ciril's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2011
      Posts : 2,013
      Rep Power : 892
      Likes Received
      252
      Likes Given
      19

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Get well soon Dkt Ulimboka

    18. #37
      OSOKONI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2011
      Posts : 3,911
      Rep Power : 1169
      Likes Received
      1056
      Likes Given
      804

      Default Re: Ulimboka mahututi

      Mbona hali ya huyu bwana haistabilize?? huenda watesaji wake walimuumiza sana! watu wote wapenda haki na wenye mapenzi mema tumuombee apone haraka! mungu amuwekee mkono wake wa uponyaji aweze kupona na kuungana na familia na watanzania kwa jumla!!
      Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

    19. #38
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,182
      Rep Power : 27035
      Likes Received
      8457
      Likes Given
      17777

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Bajabiri View Post
      habari imeeleweka,habar ziko 2,ya kwanza inahusu hali ya ulimboka south afrika na ya 2 inahusu kauli ya jeshi la polisi
      Bajabiri awali aliweka maneno matatu tu kama inavyosomeka hapo chini......
      Ni wazi kuwa
      Je hapo ungeelewa kitu gani?

    20. #39
      Mnyamahodzo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd May 2008
      Posts : 1,458
      Rep Power : 978
      Likes Received
      356
      Likes Given
      217

      Default

      Quote By Return Of Undertaker View Post
      Source BBC na Omary Mutasa kutoka Afrika Kusini

      Ni wazi kuwa hali ya Dr. Steven Olimboka ni mbaya na kalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na anapumulia mashine, hajitambui wala haongei.

      Na kulingana na bbc kulingana na hali yake ilivyo hakuluhusiwa na familia yake kumwona na hawakutaka kuongelea swala la kutekwa na kauli ya JK kukana kuhusika.
      Msimamo wa Three Doctors waliompeleka Dr Stephen, nimeupenda. Keep it up!!

      Mutasa unajiaibishakuripoti kitu asichokijua au kuwa mzushi.
      Last edited by Mnyamahodzo; 5th July 2012 at 07:59.

    21. #40
      ntamaholo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2011
      Location : Mwilavya
      Posts : 4,119
      Rep Power : 1391
      Likes Received
      919
      Likes Given
      412

      Default re: BBC: Dr. Ulimboka yuko ICU (yuko kwenye koma) anasaidiwa na mashine

      Quote By Return Of Undertaker View Post
      Source BBC na Omary Mutasa kutoka Afrika Kusini

      Ni wazi kuwa hali ya Dr. Steven Olimboka ni mbaya na kalazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na anapumulia mashine, hajitambui wala haongei.

      Na kulingana na bbc kulingana na hali yake ilivyo hakuluhusiwa na familia yake kumwona na hawakutaka kuongelea swala la kutekwa na kauli ya JK kukana kuhusika.

      Wakati huo huo jeshi la polisi limetoa kauli hii

      ""Upelelezi wa Polisi Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema jopo la upelelezi aliloteua hivi karibuni kushughulikia tukio zima la kutekwa kwa Dk Ulimboka litaendelea na kazi yake hadi mwisho na hatasikiliza kelele za wanaodai kutokuwa na imani nalo. Alisema madai yanayotolewa na watu mbalimbali akiwemo Dk Ulimboka mwenyewe kuwa hana imani na jopo hilo hazitabadili chochote kwani kinachofanyika hivi sasa ni kazi ya kawaida ya upelelezi ya jeshi hilo... “Hao wanaosema hawana imani na jopo hilo hawana hoja isipokuwa waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake."""

      Concern
      Ninashaka hapa hivi uchunguzi wa jeahi la polisi kama mimi mtendwa sitaki kwanini unalaImisha wakati sina imani na ulichokiunda na cha ajabu nawe unanambia hata kama hutaki sie tunaendelea. Nini kipo nyuma ya pazia la polisiiiiiii???
      Jeshi la polisi linafanya kazi zake kwa mjibu wa sheria. Sheria iliyoanzisha jeshi hili, ililipa majukum yafuatayo:-
      1. kulinda maisha ya watu na mali( kudumisha amani)
      2. kukamata/kuwaweka chini ya ulinzi wa polisi watuhumiwa wa makosa ya jinai
      3. kupeleleza au kukusanya ushahidi wa makosa ya jinai
      4. kusimamia utii wa sheria (ikibidi ushurutishaji wa utii wa sheria za nchi)
      5. kudhibiti matukio ya uhalifu.

      sasa kova anaposema hata kama wakilalamika hatobadilisha YUKO SAHIHI, kwani hayupo kisiasa, bali yupo kiutendaji kukidhi matakwa ya sheria inayomfanya aitwe kamanda, anatekeleza wajibu wake.

      Cha kushauri, ni kuunda tume huru ya uchunguzi ambayo haitakuwa inafanya kazi za KIPOLISI, bali itafanya kazi zilizoainishwa na aliyewatuma. Kama ni bunge au rais. Lakini sioni aliyetayari kulifanyia kazi suala hili.
      UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

    Page 2 of 12 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...