Kiongozi wa upinzani nchini na Katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbrod Slaa amelaani vikali kushambuliwa na kuteswa kiongozi wa madaktari nchini Dr Ulimboka Stephen.
Kiongozi huyo amesema hakuna njia zaidi ya kuunda tume huru kuchunguza tukio zima la utekaji kwani Mtuhumiwa namba moja ni serikali na kamwe haiwezi kujichunguza yenyewe. Dr. Slaa amesema vinginevyo matokeo ya tume hiyo ya serikali ambayo si huru hayatatambuliwa wala kukubaliwa na wananchi.
Dr Slaa amesema anashangaa kusikia serikali haina fedha za kuwaongezea madaktari huku katika bajeti ya mwaka huu ikitenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya chai tu.
Source: Mwanahalisi

Reply With Quote





Follow Us Here