MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania Dk. Steven Ulimboka ameombewa ulinzi kwenye Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International.Vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka ndani ya jopo la wataalam na jumuia hiyo kwa nyakati tofauti vimeliambia Tanzania Daima Jumatano kwamba wamelazimika kuomba ulinzi wa kimataifa ili kukabiliana na watu wabaya wanaotaka kumdhuru.Vyanzo hivyo vilisema watu waliomdhuru wanataka kummaliza kabisa ili kuficha ukweli kwani kabla ya kuondoka Dk. Ulimboka alieleza ukweli wa tukio hilo hivyo wabaya wake hao wanatumia baadhi ya watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kuhakikisha wanampata.
“Hii ya kuomba ulinzi ni ‘latest’; Amnesty International ni wabishi lakini katika hili wameombwa naamini watakubali kumlinda… maombi yamepelekwa jana.“Kabla ya kupelekwa Afrika Kusini Dk. Ulimboka alieleza ukweli wa tukio zima kuanzia walivyomkamata na mateso waliyompa hadi walipotaka kumzika akiwa hai.“Wameshajulikana sasa wanatumia ubalozi wetu kutaka kupenya kwenda kumwona hospitalini ndiyo maana haisemwi yuko hospitali gani… ukweli ni kwamba usalama wa Dk. Ulimboka uko hatarini,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.Bila kujua kwamba hizo ni habari chanzo hicho kiliendelea kueleza kwamba akiwa njiani kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dk. Ulimboka aliwataka viongozi na madaktari wengine ndani ya jumuia kupigania haki zao.Kwa mujibu wa chanzo hicho mwenyekiti huyo wa jumuia aliwasihi waliobaki wasikubali damu yake imwagike bure, wahakikishe maslahi ya madaktari yanaboreshwa.
“Msikubali damu yangu imwagike bure; endeleeni kupigania haki zenu…,” chanzo hicho kilimnukuu Dk. Ulimboka.Hata hivyo ilielezwa kwamba jumuia hiyo ilishirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binaadam (LHRC) kuomba ulinzi huo kutoka Amnesty International.
Chanzo: Tanzania Daima
WAKATI HUO HUO
“Taarifa tulizozipata kutoka Afrika Kusini zinasema kwamba, hali ya Dk Ulimboka imezidi kuimarika tofauti na alivyokwenda, figo zimeanza kufanya kazi ingawa kwa polepole na amefanyiwa vipimo vingine,” alisema Dk Kabangila na kuongeza:
“Pia ameanza kuzungumza, anawatambua watu vizuri na zaidi amewaomba Watanzania wamuombee apone haraka.”
Awali, chanzo kimoja cha habari kilidokeza kwamba hali ya Dk Ulimboka imeimarika kutokana na kupatiwa huduma za matibabu kwa haraka kwa kufanyiwa pamoja na vipimo vingine, kile cha usafishaji damu na figo (Dalysis), mara kwa mara. Kabla ya kuondoka nchini, Dk Ulimboka alifanyiwa usafishaji huo mara mbili.
Madaktari walisema kuwa, kipimo hicho kililenga kupunguza kiwango cha sumu iliyoonekana kwenye damu, ambayo haikutambulika mara moja kama ilitengenezwa ndani ya mwili au vinginevyo kwa kuwa hakuna kipimo cha kubaini tatizo hilo nchini.
Chanzo: Mwananchi

Reply With Quote



Follow Us Here