Sipati picha iwapo Waalimu nao watagoma; hivi Serikali itaagiza Waalimu toka nchi gani?
Serikali ina mpango wa kuagiza Madaktari kutoka nje ya nchi kuziba pengo lililoachwa na Madaktari waliogoma. Tumesikia pia Waalimu nao iwapo hawatatimiziwa madai yao watagoma ktk wiki mbili zijazo,jambo ambalo linawezekana kutokana na ukweli kuwa madai yao hayapishani sana na yale ya Madaktari. Pamoja na raslimali tulizo nazo Tz tunaambiwa nchi hii haina pesa na ni maskini!
Nina maswali yananitatiza katika njia bora za kutatua matatizo yetu, naomba Wanajamvi mnisaidie maswali yafuatayo:
Kuna mikakati gani ya kuhakiki ili kujua Madaktari wanaokuja toka nje ni qualified? Nachojua mimi ukiombwa upunguze manpower yako utatoa wale usiowataka,hutatoa jembe unalolitegemea na badala yake utatoa jembe dhaifu, legelege,lisilo na tija;
Ni gharama kiasi gani itatumika kuwaagiza, kuwalipa Madaktari hao wa kigeni? Je, watalipwa mishahara kama waliyokuwa wakilipwa Madaktari waliogoma au watalipwa kama Experts (TX?
Madaktari hao wageni wakija watakuja na dawa? watakuja na vifaa? Wataondoa kero ya wagonjwa kulala chini au watatu watatu vitandani? Watapunguzaje vifo vingi vya akina mama na watoto walio chini ya miaka 5? Wataboresha miundombinu ya hospitali zetu?
Ikitokea Waalimu nao wakagoma, Serikali itaagiza Waalimu wangaoi na kutoka nchi gani? je, watatosheleza mahitaji hasa ya shule za watoto wetu akina Kayumba?
Iwapo Waalimu watatoa nje Serikali ina mikakati gani ktk somo la Kiswahili na lile la Civic Education? Au masomo hayo yatafutwa kwenye mitaala ya Elimu?
Kwa Maswali yote hapo juu Serikali imetenga kiasi gani kutumia manpower ya kutoka nje kwenye sekta hizo hadi hapo itakaposomesha waaalimu na madaktari wa kutosha sijuwi miaka mingapi ijayo? Je, ikitokea Watumishi wa Serikali ktk sekta nyingine nao wakagoma (hatuombi hayo)serikali imejizatiti vipi?
Kwakweli sipati picha! Naogopa!
Laughing Faces Do Not Mean That There Is Absence of Sorrow! But it Means That They have The Ability to Deal With It!
Re: Sipati picha iwapo Waalimu nao watagoma; hivi Serikali itaagiza Waalimu toka nchi gani?
By Return Of Undertaker
Watafanya voda faster
Kwa mtindo huo ndio maana tupo hapa tulipo! Vodafaster itafyatua madaktari vodafaster, Waalimu vodafaster, mainjinia vodafaster....ndio maana sipati picha!
Laughing Faces Do Not Mean That There Is Absence of Sorrow! But it Means That They have The Ability to Deal With It!
Re: Sipati picha iwapo Waalimu nao watagoma; hivi Serikali itaagiza Waalimu toka nchi gani?
walimu walishagoma siku nyingi; kinachotokea sasa hivi ni usanii tu. Ebu angalia idadi ya wanaoingia kidato cha kwanza bila kujua kusoma na kuandika. Walimu mgomo wao ni silent na madhara yake yataonekana taratibu kadri muda unavyosonga mbele.

U r right! Pata picha wakiuhalalisha mgomo huo, amini nakuambia hakuna Mwl wa kutoka nje ya nchi atastahimili mazingira wanayofundishia waalimu Wa Tz. Hapo ndipo panaponitisha zaidi. Naona anguko kuu!
Re: Sipati picha iwapo Waalimu nao watagoma; hivi Serikali itaagiza Waalimu toka nchi gani?
wanaogoma wanfuataga huu usemi there is nothing to loose .Jiulize ni kwa nini kwenye vyuo si rahis walimu kugoma ila ni rahisi kwa college nyingine kugoma.au angalia watu walio na familia wengi si rahisi kugoma ila wengine ni rahis sana kugoma
Re: Sipati picha iwapo Waalimu nao watagoma; hivi Serikali itaagiza Waalimu toka nchi gani?
By +255
Watu wa kufundisha wapo wengi sana mitaani...Kuna graduates kibao hawana kazi..
Hata hao graduates wakiingia bila kuboresha mfumo mzima wa elimu na maslahiya waalimu nao wataingia mitini tu. Fikiria mwl. anayepelekwa Tandahimba, Nkasi na kwingineko, ambako hakuna nyumba za waalimu, hakuna huduma thabiti za kijamii nani atakaa? Shule hazina maabara, maktaba na nyingine watoto wanasomea kwenye vibanda kama si chini ya miti. Mwl anaweza kukata miezo 3-6 bila mshahara, hao graduates wataweza?
Laughing Faces Do Not Mean That There Is Absence of Sorrow! But it Means That They have The Ability to Deal With It!
Watu wa kufundisha wapo wengi sana mitaani...Kuna graduates kibao hawana kazi..
Ndivyo tunavyoamini kuwa ualimu anafanya yeyote. Graduates tuko wengi na tuna knowledge tatizo ni skills za ku impart hiyo knowledge kwa mtoto ndio shida. Tuwaheshimu tu.
Re: Sipati picha iwapo Waalimu nao watagoma; hivi Serikali itaagiza Waalimu toka nchi gani?
You can count on my word wakuu, "walimu wetu wa hapa bongo hawawezi kugoma hata siku moja" sijawahi ona tasnia ambayo watu wake ni waoga na wasio na umoja kama waalimu. Siwapondi ila ndo ukweli, wakitishwa au kupewa chai kidogo tu wanafyata. Na hakuna wafanyakazi wa serikali yetu hapa wenye matatizo katika kazi zao kama waalimu!!!!
The future of this country is being jeopardized by the intellectual slavery of our top leaders
Follow Us Here