Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

    Report Post
    Page 5 of 9 FirstFirst ... 34567 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 167
    1. #1
      mcfm40's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Posts : 127
      Rep Power : 459
      Likes Received
      59
      Likes Given
      1

      Default Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

      Jamani mimi ni mwalimu nafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama Assistant Lecturer.

      Kusema kweli hii nchi haijui thamani ya madaktari na professionals wengine kwa ujumla.

      Hivi kweli unaweza kulinganisha miaka mitano ya kusomea udaktari na miaka mitatu ya digrii nyingine hizi!?

      Nimeshangaa eti daktari anayeanza kazi analipwa laki 9. Huu ni mshahara mdogo kuliko wa Tutorial Assistant aliyesomea digrii yake kwa miaka mitatu tu tena digirii laini (nimesoma mimi Arts) usinitolee mimacho! Ni laini tu huwezi kulinganisha na nondo za udaktari!

      Kusema ukweli interns wanapaswa kulipwa minimum 2mil. Yaani daktari alipwe sawa na kada nyingine? You are kidding!

      Kazi ya udaktari ni habari nyingine jamani tusidanganyane. Kikwete anachofanya ni kujaribu kugombanisha madaktari na wananchi! Unajua watu wa kawaida hawajui nondo za udaktari zilivyo ngumu na ilivyo ngumu kufaulu! Watu mliokimbia chemistry, physics, biology mnajua habari yake, sio mchezo!

      Hivi inakuwaje serikali imeanza tabia ya kupuuzia kada nyeti kama udaktari? Kiwete anazungumza kwa kubeza tu, anafikiri ni rahisi kama alivyodesa na uchumi wake pale ya Mlimani!? Madaktari pambaneni mtambulikane kama kada maalumu na muwe na commission yenu maalumu ya mishahara.

      Ni kichekesho kwamba mganga wa kienyeji na wenzake wa darasa la saba pale bungeni anakula milioni 7, professionals wanadhihakiwa. What are our priorities?

      Kwa mtindo huu tutaweza kuzuia madaktari wetu kutimkia nje kwenye greener pastures? Na nin nani atapenda hiyo kazi ya udaktari ya kuteseka kusoma mavitu magumu halafu hata hudhaminiwi kwa nini nisichukue kozi laini laini si mshahara ni huo huo?

      Serikali inapaswa kujitathmini upya na kujua vipaumbele vyake. Kazi ya Udakatari haithaminiwi Tanzania! Hatutafika namana hii! Hii ni kazi inayohusisha uhai wa watu lazima tuinvest vya kutosha hapa bial visingizio vyovyote. Kwa hiyo mkishawalazimisha kurudi kazini kwa manunguniko ndiyo watatibia watu kwa juhudi?

      Serikali mnaweka maisha ya wananchi hatarini! Let us be serious. Sidhani kama kuna dakatri analazimisha milioni 3.5; lengo ni kiwango kifikie walau mahali reasonable! Hii inawezekana kabisa, na si kweli kwamba lazima mshahara wa madaktari ukibadilika na kada nyingine zote ubadilike!

      Kama nilivyosema kazi ya udaktari habari nyingine kabisaa! Kuanzia kusomea hadi kazi yenyewe yataka moyo sio sawa na kufundisha darasani!
      Kichuguu, Hofstede, Riwa and 12 others like this.

    2. Miaka 50

    3. Obe
      #81
      Obe's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 31st December 2007
      Posts : 1,421
      Rep Power : 916
      Likes Received
      328
      Likes Given
      185

      Default Re: JK Akana serikali kutaka kumuua Dr. Ulimboka

      Quote By Edson
      labda kama hujaisoma kwa makini.....ipitie tena utakutana na aya hii

      ''Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha mgomo. Anayekaidi amri ya Mahakama ananunua lugomvi na mhimili huo wa dola ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo. ''
      Hapo palipokolezwa, panajieleza vizuri zaidi, na kumfanya kuwa mtu anayefahamu yote kuhusu Dr Uli.

    4. #82
      mcfm40's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Posts : 127
      Rep Power : 459
      Likes Received
      59
      Likes Given
      1

      Default Re: Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

      Quote By webondo
      Ovyo kabisa wewe, labda kama ni mwalimu wa kufundisha mbumbumbu wenzio, kama ungekuwa professional hakika usingeandika huo upumbavu wa ku-criticize taaluma zingine. Umenitia kichefuchefu sana. Huu mgomo unahusika vipi na taaluma zingine, unaona wengine wote waliosoma taaluma zingine ni mavi siyo!
      Tapika kabisa! Sas nikuoneshe umbumbumbu wako na wewe! Naam mtu alipwe kuendana na taaluma na ugumu na umuhimu wa taaluma yake kwa taifa. Kikwete mwenyewe kalisema hili. hata mimi ni mwalimu lakini ualimu na udaktari wala havikaribiani. Penda usipende. Sas nadhani umeshatapika kabisa! Mwite mama watoto afute matapishi!

    5. #83
      Mbalamwezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th September 2007
      Posts : 701
      Rep Power : 739
      Likes Received
      71
      Likes Given
      134

      Default Re: Mgomo wa Madaktari: Kikwete Una Maono Mafupi

      Ozzie, simple, kuna ripoti ya hivi karibuni inaonyesha kiwango kikubwa cha brain drain...we spend a lot training docs yet we fail to retain them...only to be employed by foreign countries. Yaani tunasikitisha sana majibu yaliyotolewa kuhusu trend hiyo.

      Nakubaliana na wewe, na hata CAG ameona kuwa masomo ya sayansi hayapendwi, hivi yanahitaji wasomi wenye kupewa motisha, sasa mkuu wa nchi haoni kama ni muhimu...

    6. #84
      deusgogomoka's Avatar
      Member Array
      Join Date : 31st May 2012
      Posts : 13
      Rep Power : 354
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default

      Kwa nini watu wengine wanachangia bila kufikiria, hata kama mtu amekosea kuelezea mada lakini kila kitu kuhusu madokta kinaeleweka.

      Nyie mnaochangia na kukejeli madaktari mna akili finyu na uwezo mdogo sana wa kufikiria. Sina mengi ya kuwaambia ila inawezekana ni sababu ya malezi kitu ambacho sio makosa yenu, ni wazazi. Kazi wanazofanya madaktari na manesi sio za kubeza, kuna mliochangia vibaya hamuwezi hata kuingia kwenye wodi za wogonjwa achilia mbali kushindwa kufaulu masomo ya sayansi.

      Daktari kama daktari, nesi kama nesi na muuguzi mwingine yoyote wa hospitali anatakiwa apewe maisha mazuri. Kitu kikubwa ni ile kitu tunaita saikolojiko tocha wanayopata madaktari hospitalini.

      Mimi siungi mkono hao wanaoponda na ni vyema wangekaa kimya wangeonekana na busara.

    7. #85
      MkamaP's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2007
      Posts : 4,675
      Rep Power : 1569
      Likes Received
      310
      Likes Given
      93

      Default Re: Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

      Kama ni madaktari wadai tu hayo malipo, nafikiri wasihusishe fani zingine eti rahisi ama miaka mingi ama kazi ngumu, hapana nafikiri waangalie madai yao.

      Sifikiri kama structural engineer amepeta kirahisi, na anafanya kazi ktk mazingira rahisi.

    8. RukaaJuu Final

    9. #86
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,299
      Rep Power : 12584
      Likes Received
      5843
      Likes Given
      771

      Default

      mcfm40

      Mkuu kama dharua huo mshahara ni mdogo nenda kapige kazi Marekani au Ulaya.

    10. #87
      Ozzie's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 9th October 2007
      Location : Jo'burg
      Posts : 1,009
      Rep Power : 795
      Likes Received
      271
      Likes Given
      74

      Default Re: Kikwete: Madokta wanapendelewa sana

      Quote By webondo
      Acha upotoshaji wa kihuni, una hakika kuwa hao wote uliowataja hapo juu wanalipwa laki 9 kwa mtu anayeanza kazi leo.?? Hapo kuna ambao wanaanzia na laki 4.5 anapoanza kazi.
      webondo awatoe Mahakama nadhani.
      "It's not the votes that count. It's who counts the votes" - Josef Stalin

    11. #88
      ITEGAMATWI's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 26th January 2012
      Posts : 1,672
      Rep Power : 0
      Likes Received
      424
      Likes Given
      828

      Default Re: Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

      Quote By Red Giant
      kikwete mwenyewe alisema unapoangalia kiwango cha mshahara unaconsider muda wa mtu kusomea fani hiyo na umuhimu wake kwa jamii sasa umbumbumbu unautoa wapi? hata libya ya ghadafi unakuta dokta alimzidi mshahara waziri!! professa sawa kasoma muda mrefu kuliko daktari na majimarefu nae kasoma muda mrefu kuliko daktari? halafu inategemea professa wa nini huwezi kufananisha prof wa kiswahili na prof wa cardiology,
      Sawa kama unaona Libya ndiyo wanatoa mshahara mnaoutaka, Rais Kikwete anawatakia kila la kheri muende huko.

    12. #89
      Ibrah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd March 2007
      Location : TZ
      Posts : 2,883
      Rep Power : 1199
      Likes Received
      402
      Likes Given
      46

      Default Re: Kikwete: Madokta wanapendelewa sana

      Tujiulize, kama wanapendelewa sana inakuwaje Dk Mwinyi (Mb), Dk Prof Sarungi, Dk Kigwangala nk walikimbilia kwenye siasa?

    13. #90
      robert josephat's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th May 2012
      Posts : 604
      Rep Power : 472
      Likes Received
      74
      Likes Given
      278

      Default Re: Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

      Si dharau ni changamoto mojawapo ya kuwapata madaktari wazalendo na si vinginevyo,uzalendo kwa kada hii ni muhimu sana kuliko kitu chochote (bora utu kuliko kitu) hayo mengineyo ni majaaliwa ya mwenyezi mungu.

    14. #91
      IPECACUANHA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th February 2011
      Posts : 1,098
      Rep Power : 637
      Likes Received
      224
      Likes Given
      50

      Default Re: Madai ya ma daktari --- usanii wa serikali ya jk na ccm yake

      Nimemsikiliza Mheshimiwa Raisi nimegundua mambo yafuatayo
      1. Anaongea kwa namna ya kuonyesha madaktari ndio chanzo cha matatizo na sio serikali. Nasikitika sana hotuba ya Raisi wangu ni uchonganishi na usanii wa hatari sana. Hana nia ya kweli ya kujadili na watu wenye akili. Anafanya usanii aliouzoea
      2. Anatumia majina ya watu kama alivyomtaja Mgaya wakati ule kwa nia ya kuonyesha tatizo ni viongozi
      3. Anatumia vitisho kuiita mgomo ni haramu
      4. Siasa kwetu watanzania in sumu kali na ya kutisha naogopa

    15. #92
      webondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Location : Chini ya mwembe
      Posts : 1,167
      Rep Power : 589
      Likes Received
      178
      Likes Given
      381

      Default Re: Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

      Quote By mcfm40
      Tapika kabisa! Sas nikuoneshe umbumbumbu wako na wewe! Naam mtu alipwe kuendana na taaluma na ugumu na umuhimu wa taaluma yake kwa taifa. Kikwete mwenyewe kalisema hili. hata mimi ni mwalimu lakini ualimu na udaktari wala havikaribiani. Penda usipende. Sas nadhani umeshatapika kabisa! Mwite mama watoto afute matapishi!
      Kilaza mwingine wewe!

    16. #93
      Nzowa Godat's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2011
      Posts : 1,383
      Rep Power : 678
      Likes Received
      229
      Likes Given
      12

      Default

      Quote By Ibrah
      Tujiulize, kama wanapendelewa sana inakuwaje Dk Mwinyi (Mb), Dk Prof Sarungi, Dk Kigwangala nk walikimbilia kwenye siasa?
      Kumbe the solution is so easy! ni kuingia tu kwenye ubunge!

    17. #94
      ITEGAMATWI's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 26th January 2012
      Posts : 1,672
      Rep Power : 0
      Likes Received
      424
      Likes Given
      828

      Default Re: Madai ya ma daktari --- usanii wa serikali ya jk na ccm yake

      Quote By gongolamboto
      Ulitegemea nini kutoka kwa mtu aliyepata GPA ya 2.6
      Balali na Chenge unajua G.P.A zao?

    18. #95
      Lukolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2009
      Location : Iringa
      Posts : 3,871
      Rep Power : 7036
      Likes Received
      2038
      Likes Given
      1570

      Default Re: Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

      Quote By Ng`wanakidiku
      TELO

      Mimi ni mkufunzi (TA) wa Chuo kikuu kimoja hapa bongo.

      Mshahara wangu wa Tutorial assistant nilianza na zaidi ya 1m, kumzidi hata Dr, na course ya undergraduate ilikuwa miaka 3. Na kazini nina nyumba, usafiri, maji, umeme. Na bado nina muda mwingi tu wa kuwa idle (si kama Dr akianza kazi hatoki mpaka usiku). Wakati mwingine Dr anafanya kazi hata weekend, mimi sifanyi.
      Ni chuo gani hicho kinachomlipa tutorial assistant mshahara wa milioni moja halafu kinampa nyumba, usafiri, maji na umeme? Nitajie jina tafadhari ili na mimi niombe kazi huko. Bila shaka si chuo cha serikali. Maana vyuo vya serikali mshahara wa kuanzia wa tutorial assistant haujafika milioni moja. Acheni kupotosha.
      Mtaji mkubwa kabisa wa CCM katika chaguzi zake ni umaskini na ujinga wa watanzania. CCM haitafanya kosa la kuyamaliza matatizo hayo kwa kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wamehatarisha nafasi yao ya kuendelea kutawala

    19. #96
      Ng'wanambula's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd October 2011
      Posts : 85
      Rep Power : 403
      Likes Received
      22
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Muarubaini
      Mimi sio muamini wa serikali hii kutokana na baadhi yamambo mengi ambayo hayako sawa, ila kwa hili la madakitari kutaka kulipwa mara nane ya watumishi wengine wa umma wenye elimu sawa nalikataa. Natambua umuhimu na ugumu wa kada ya udakitari, lakin haiwezi kupelekea kujenga tofauti kubwa kiasi hicho kimasilahi na kada zingine. Kupigania hali bora mazingira ya afya nchini ni muhimu, lakin hayaweza kuboreshwa kwa muda mfupi hivyo, lakini pia haiwezi kuwa sababu ya kuacha watu waendelee kufa kwa kukosa matibabu
      Muarubaini nakuunga mkono,mimi pia niko idara hii ta afya lkn siungi mkono mgomo huu.Inaonekana kuwa madaktari wanataka kujenga matabaka kwa watumishi wa umma ili ionekane kuna walio muhimu na special kuliko wengine.Hili si jambo jema na haliwezi kukubaluka

    20. #97
      johnrobbie's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 31st January 2012
      Posts : 8
      Rep Power : 370
      Likes Received
      2
      Likes Given
      1

      Default Re: Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

      SOMA HII KAMA UNA IQ SCORE ZAIDI YA 190
      Baada ya miaka kumi tu ijayo kuanzia leo wananchi watakuwa wanaandamana kuishinikiza serikali kusolve tatizo la hospitali kutokuwa na madaktari wa kutosha kwani hamna mwanafunzi aliehitimu PCB advanced level atakae taka kusoma fani ambayo ni ngumu, miaka mingi na kipato kidogo...na afterall intellectuals ndo wanachaguliwa kusoma fani hii.. kwa kawaida mtu anasoma kwa bidii akiamini ndo anajitengenezea maisha sasa na digrii yako unapata 900,000Tshs per month nonsense hamna atakae taka fani hii... si busara na hatari zaidi kutokuwa na madaktari kuliko kuwa na madaktari wanaogoma kutaka kuongezewa mshahara na mazingira mazuri ya kazi...kama swala hili halitashughulikiwa ipasavyo unabii huu utatimia soon (2020)

    21. #98
      mwaJ's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th September 2007
      Location : Nowhere
      Posts : 3,450
      Rep Power : 14609
      Likes Received
      2289
      Likes Given
      1501

      Default Re: Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

      Quote By Angel Msoffe
      ndivo alivyokwambia?
      Labda kama hujamsikiliza. Ni kweli amesema kama kuna mtu wa serikali amemfanyia hivyo Dr. Ulimboka yeye hakumtuma, atakuwa amefanya kwa maslahi yake binafsi.
      “Anyone who has never made a mistake has never tried anything new” -
      Albert Einstein

    22. #99
      Ibrah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd March 2007
      Location : TZ
      Posts : 2,883
      Rep Power : 1199
      Likes Received
      402
      Likes Given
      46

      Default Re: Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

      Sijasikiliza hotuba ya Jk lkn inaonekana amezengumzia mishahara ya madk, vipi kuhusu mazingira na vifaa vya kazi? Hajasema kitu?

    23. #100
      Red Giant's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2012
      Posts : 730
      Rep Power : 3610
      Likes Received
      233
      Likes Given
      282

      Default Re: Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

      Quote By ITEGAMATWI
      Sawa kama unaona Libya ndiyo wanatoa mshahara mnaoutaka, Rais Kikwete anawatakia kila la kheri muende huko.
      libya ya ghadafi ulikuwa ni mfano wa nchi zilizokuwa zinatoa mshahara kwa kuangalia elimu ulikuwa ni mfano, sawa?hivi kwanini daktari wa NIMR apewe hela nyingi kuliko wa muhimbili? au muhasibu wa TANAPA hela nyingi kuliko wa hazina. kingine kinachowachochea madaktari ni kuona wengine wakipeta wao wakidai wanaambiwa nchi haina hela!! hili swala linaudhi sana.
      COAL UNDER PRESSURE BECOMES DIAMOND

    Page 5 of 9 FirstFirst ... 34567 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...