Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

    Report Post
    Page 18 of 26 FirstFirst ... 81617181920 ... LastLast
    Results 341 to 360 of 509
    1. #1
      Dingswayo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th May 2009
      Location : Tanzania/Europe
      Posts : 2,630
      Rep Power : 5719
      Likes Received
      1060
      Likes Given
      2495

      Default Hotuba ya Rais, 30 June 2012

      Ndugu Wananchi,

      Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza nusu ya kwanza ya mwaka 2012 salama. Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza nanyi kila mwisho wa mwezi, leo napenda kuzungumzia mambo mawili. Jambo la kwanza ni suala la usafirishaji haramu wa binadamu nchini na la pili ni la mgomo wa madaktari.

      Usafirishaji Haramu wa Binadamu Nchini

      Ndugu Wananchi;
      Bila ya shaka mtakuwa mmezisikia taarifa za tukio la kushtusha na kuhuzunisha la kukutwa maiti 43 za watu wasiojulikana, zilizotupwa katika kichaka kilichopo kijiji cha Chitego, Wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma tarehe 26 Juni, 2012. Pamoja na maiti hao, walipatikana watu 84 wakiwa hai lakini wote wakiwa wamedhoofu na baadhi yao wakiwa mahututi. Hatua za haraka zilichukuliwa kuwasafirisha watu hao hadi Dodoma ambapo wale waliokuwa mahututi walifikishwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu na wengine walihifadhiwa katika Kituo cha Kati cha Polisi, Dodoma. Maiti 22 zilipelekwa Dodoma na 21 zilipelekwa Morogoro kuhifadhiwa.

      Taarifa zilizopatikana kutoka kwa wale walionusurika zimebainisha kuwa watu hao ni raia wa Ethiopia ambao walikuwa safarini kwenda Malawi na baadaye Afrika ya Kusini ambako wangetengenezewa utaratibu wa kwenda kuishi Marekani na Ulaya. Kwa mujibu wa maelezo yao, safari yao ilianza miezi mitano iliyopita. Mwezi mmoja waliutumia Ethiopia na miezi minne waliitumia Kenya kabla ya kuletwa Arusha ambako walipakiwa kwenye lori na kuanza safari ya kuelekea Malawi lakini ikaishia Chitego. Lori walilopanda lilikuwa limezibwa kabisa na hivyo kusababisha vifo kwa kukosa hewa.


      Tukio la Chitego, Dodoma la wahamiaji haramu kukamatwa na wengine kukutwa wamekufa si la kwanza kutokea hapa nchini. Kwa jumla, katika kipindi cha takriban miaka 10 sasa kumekuwepo na tatizo kubwa la wahamiaji haramu kuingia nchini. Kwa mfano, kati ya mwaka 2005 na hivi sasa jumla ya wahamiaji haramu 19,683 wamekamatwa. Karibu wote wameshaondoshwa nchini na hivi sasa wapo karibu watu 1,500 tu magerezani wanaotumikia adhabu na kusubiri kurejeshwa makwao. Wengi wa watu hao wanatoka Ethiopia na Somalia na baadhi kutoka Pakistan na Bangladesh.

      Wahamiaji haramu wamekuwa wanaingia nchini kwa kupitia njia zisizo rasmi. Wapo wanaotumia nchi kavu hasa kupitia mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga. Na, wapo wanaopitia baharini kwa kutumia fukwe za Pemba, Unguja na za mikoa ya ukanda wa Pwani ya Tanzania Bara yaani Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.

      Ndugu Wananchi;

      Kwa mujibu wa kauli zao, watu hao wamekuwa wanaeleza kuwa hawaji nchini kuhamia bali wao ni wapita njia tu. Wanaelekea Afrika ya Kusini ambako wameahidiwa kuwa watatengenezewa mipango ya kuhamia Marekani na Ulaya. Watu hao pia wamethibitisha kuwepo kwa watu maalum wanaojihusisha na usafiri wao tangu nchi watokako na zote wanazopitia mpaka kule waendako. Aidha, wamesema kuwa wao wanawalipa watu hao ili wawasafirishe na hakika si kiwango kidogo. Kwa jumla ni kwamba hili si suala la uhamiaji haramu bali ni la biashara haramu ya kusafirisha binadamu.

      Ndugu Wananchi;

      Kufuatia vyombo vyetu vya usalama kuwa makini na watu wengi kukamatwa ndipo wasafirishaji walipobuni njia za kuwasafirisha kama mizigo. Makontena, malori yaliyofunikwa nyuma na matenki ya mafuta na ya maji yamekuwa yanatumika kwa ajili hiyo. Usafiri wa aina hiyo ndiyo uliosababisha vifo vilivyotokea Dodoma tarehe 26 Juni, 2012 na vya watu 21 vilivyotokea mwezi Desemba, 2011 Mkoani Morogoro, na vile vya watu 12 vilivyotokea katika matukio mawili ya Mkoa wa Mbeya, mwezi Mei, 2012.

      Ndugu Wananchi;

      Tarehe 27 Juni, 2012 nilikutana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuzungumzia tukio la Chitego na suala zima la biashara hii haramu na hasa mbinu mpya inayotumiwa na wasafarishaji. Nilitoa pongezi kwa vyombo vya dola kwa kazi nzuri waifanyayo kudhibiti shughuli za biashara hii haramu hapa nchini. Tulielewana kuwa waendelee kuimarisha udhibiti huo kwa lengo la kukomesha kabisa biashara hii.

      Niliagiza pia kwamba kikundi kazi nilichokiunda mwaka 2006 kushughulikia ujambazi sasa kielekeze sehemu ya nguvu zake kukabili tatizo hili. Aidha, kwa pamoja tulikubaliana kuwa nchi yetu ishirikiane na wenzetu wa Ethiopia, Kenya, Malawi, Msumbiji na Afrika ya Kusini kutambua mawakala na kuwabana kwa mujibu wa sheria. Tayari nimeshaanza kufanya mawasiliano na baadhi ya Wakuu wa Nchi hizo kuhusu ushirikiano huo. Nashukuru wote wameafiki nchi zetu zishirikiane kwa pamoja kuvunja mtandao huu mchafu na kutokomeza biashara hii haramu na inayodhalilisha utu wa mwanadamu.

      Ndugu Wananchi;

      Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wenzetu, wakazi wa vijiji vya Chitego na Mkoka kwa kazi nzuri walioifanya. Kwa kweli, wenzetu wameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kutoa taarifa mapema juu ya jambo lenyewe, lakini pia wameonesha utu kwa kuwajali wageni waliokumbwa na janga hili. Naushukuru pia uongozi wa Mkoa wa Dodoma na Morogoro ikiwa ni pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kulishughulikia tatizo hilo kwa umakini mkubwa. Nimefurahishwa sana na ushirikiano ulioonyeshwa na vyombo na taasisi mbalimbali za Serikali katika kushughulikia suala hili.


      Mgomo wa Madaktari

      Ndugu Wananchi;
      Jambo la pili ni kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini hivi sasa. Nilipozungumza na Wazee wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 12 Machi, 2012, kuhusu mgomo wa Madaktari uliokuwa unaendelea wakati ule pamoja na kuelezea chimbuko la mgomo na hatua iliyokuwa imefikiwa, nilielezea mazungumzo yangu na viongozi wa Chama cha Madakari wakiwemo pia viongozi wa Jumuiya ya Madaktari. Nilitoa taarifa kuwa tumeelewana kuwa watasitisha mgomo na watarudi kwenye meza ya majadiliano na Serikali. Siku ile pia nilielezea matumaini yangu kuwa mgomo ule utakuwa wa mwisho katika nchi yetu. Bahati mbaya matumaini yangu hayo hayakuwa na hivi sasa tunashuhudia tena wagonjwa wakiteseka, kuhangaika na wengine kufa kwa sababu ya kukosa huduma wanazostahili kwa vile madaktari wao wamegoma tena.

      Ndugu Wananchi;

      Kama walivyoniahidi, madaktari waliacha kugoma na viongozi wao walirudi kwenye mazungumzo na Serikali. Kama ilivyoagizwa na Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi tarehe 8 Machi, 2012, kwa mujibu wa Sheria ya Mahusiano Kazini, Namba 6 ya mwaka 2004. Chama cha Madaktari na Serikali walifika katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Commission for Mediation and Arbitration) kwa ajili ya majadiliano. Kwa pamoja na kwa ridhaa yao wote, pande hizo mbili ziliiomba Tume hiyo iwape fursa ya kuzungumza wao wenyewe na wakimaliza mazungumzo wataenda kusajili makubaliano yao. Tume ikawakubalia. Ni vizuri ikakumbukwa kuwa siku ile ya tarehe 8 Machi, 2012 Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, ilitoa zuio la mgomo pamoja na kuagiza kuwepo mazungumzo baina ya pande mbili.

      Ndugu Wananchi;

      Kati ya tarehe 10 Aprili, 2012 na tarehe 30 Mei, 2012, vilifanyika vikao sita vya majadiliano kati ya Serikali na Chama cha Madaktari. Katika mazungumzo hayo hoja au madai 12 ya madaktari yalizungumzwa. Mambo hayo ni haya yafuatayo:

      1.
      Posho ya kuitwa kazini (on call allowance) iwe asilimia 10 ya mshahara.
      2.Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (Risk allowance) iwe asilimia 30 ya mshahara.
      3.Madaktari wapatiwe nyumba grade A au posho ya makazi ambayo iwe asilimia 30 ya mshahara.
      4.Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu iwe asilimia 40 ya mshahara.
      5.Madaktari walipwe posho ya usafiri ya asilimia 10 ya mshahara au wakopeshwe magari.
      6.Madaktari wanaoanza kazi walipwe mshahara wa shilingi 3,500,00/= kwa mwezi.
      7.Madaktari wapatiwe Green Card za Bima ya afya.
      8.Hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
      9.Viongozi wa Kisiasa kulazimisha kupewa rufaa nje.
      10.Madaktari waliofukuzwa warudishwe kazini.
      11.Huduma za afya ziboreshwe nchini.
      12.Posho ya uchunguzi wa maiti iongezwe.

      Ndugu Wananchi;
      Katika mambo hayo 12 pande zote mbili zilifikia muafaka na kukubaliana wa pamoja kwa mambo saba. La kwanza, ni kuhusu usafiri wa kwenda na kurudi kazini. Serikali ilieleza kuwa upo utaratibu kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi wa Serikali Na. 3 wa mwaka 2011 wa kuwakopesha wafanyakazi wa Serikali fedha za kununulia magari au pikipiki, samani na matengenezo ya magari. Ilikubaliwa kuwa madaktari waitumie fursa hiyo.

      Jambo la pili
      , ni kuhusu madaktari kupatiwa Green Card za Bima ya Afya. Jambo hili lilikubaliwa na Serikali na Wizara ya Afya imekwishachukua hatua za utekelezaji wake.


      Jambo la tatu
      , ni kuhusu hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya. Kwa pamoja walikubaliana kuwa suala hilo liko nje ya mamlaka ya Kamati yao ya pamoja, waziachie mamlaka husika za uteuzi. Uongozi wa juu wa Wizara umebadilishwa na sasa kuna uongozi mpya. Lakini, jambo la kustaajanisha hata Waziri mpya wa Afya alipowataka waonane kuzungumzia hoja walikataa kumuona. Kwanza walisema hawaoni sababu kwa vile wameyazungumza na Kamati yake kwa miezi mitatu bila ya mafanikio


      Jambo la nne
      walilokubaliana ni kuhusu viongozi kulazimisha kupewa rufaa ya kutibiwa nje. Walikubaliana mambo mawili. Kwanza, kwamba maelekezo ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kuwa madaktari wazingatie maadili ya kazi zao na kukataa kutoa rufaa kwa mtu asiyestahili awe kiongozi au asiwe kiongozi. Pili, walikubaliana kuwa hospitali zilizopo ziboreshwe ili viongozi watibiwe hapa nchini. Ukweli ni kwamba kufanya hivyo ndiyo sera ya Serikali. Nililieleza hili mwezi Desemba 30, 2005 katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza nchi yetu.


      Tumeiongeza sana bajeti ya sekta ya afya kutoka shilingi bilioni 300 2005/2006 hadi shilingi trilioni 1.2 mwaka 2011/12 na imekuwa ya tatu baada ya miundombinu na elimu. Tumeziimarisha hospitali za Mikoa kwa vifaa tiba na wataalamu wa afya. Kazi inaendelea katika hospitali za Wilaya. Tumewekeza katika Hospitali ya Muhimbili. Hospitali hiyo ilivyo leo sivyo ilivyokuwa miaka sita nyuma. Na kazi inaendelea hasa katika maeneo ambayo tunapeleka wagonjwa nje. Matunda yake yanaanza kuonekana kwa upande wa figo, moyo, kinywa na mipango inaendelea kwa upande wa ubongo na mishipa ya fahamu. Tunaendelea kuimarisha mafunzo ya madaktari na madaktari bingwa, yote kwa nia hiyo hiyo. Hivi sasa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba,Muhimbili kinachukua wanafunzi wengi zaidi ya ilivyokuwa siku za nyuma na makazi mapya ya chuo yanaendelea kuandaliwa ili kuchukua wanafunzi wengi zaid. Mwaka 2005 tulikuwa na madaktari bingwa 46 mwaka huu tunao 520.


      Ndugu Wananchi;

      Jambo la tano ambalo pande zote mbili zilikubaliana ni kuhusu madaktari waliofukuzwa. Hawa ni wale Interns waliokuwa wamerudishwa Wizarani kutoka Muhimbili na kupangiwa hospitali za Temeke, Ilala, Mwananyamala na Lugalo. Hili ni jambo ambalo lilikuwa limemalizika kitambo na wote walikuwa wamerudi Muhimbili.

      Jambo la sita
      ni kuhusu mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na madaktari kuhusu kuboresha huduma ya afya. Mapendekezo hayo yalihusu kutathmini sera na mpango wa afya ya msingi, bajeti ya afya kuwa asilimia 15 ya bajeti ya Serikali, kuwepo na utaratibu mzuri wa kuajiri madaktari na kuboresha viwango vya ubora wa madaktari na kadhalika. Serikali imeyaafiki mapendekezo hayo na yatafanyiwa kazi.


      Jambo la saba,
      ambalo pande zote walilokubaliana ni kuhusu kuongeza posho ya uchunguzi wa maiti. Hili ni jambo jipya halikuwepo mwazoni. Hata hivyo, Serikali imelikubali na posho hiyo imeongezwa kutoka shilingi 10,000/= hadi kufikia shilingi 100,000/= kwa daktari na shilingi 50,000/= kwa wasaidizi wake.


      Ndugu Wananchi;

      Kuna masuala matatu ambayo yamekuwa na muafaka kwa kiasi fulani na kutoafikiana kwa baadhi ya mambo. La kwanza ni suala la kufanya kazi katika mazingira hatarishi. Serikali imekubali hoja ya kuchukua hatua ya kuwalinda madaktari wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi. Serikali iliwaeleza kuwa watumishi wa kada zote za afya watapatiwa chanjo dhidi ya maambukizi ya Hepatitis B na fedha zimetengwa katika bajeti ya 2012/13.

      Aidha, Serikali imeeleza dhamira ya kurudisha posho ya mazingira hatarishi kwa watumishi wa umma wanaostahili. Utekelezaji wake utafanyika baada ya uchambuzi wa kina wa kubainisha mazingira hatarishi ni yepi, viwango stahiki viwe vipi na nani hasa wahusike. Madaktari wamekataa hili la kufanya uchambuzi, wanataka kiwango kiwe kama wanavyotaka wao, yaani asilimia 30 ya mshahara na kianze mara moja.

      Jambo la pili ambalo wamekubaliana nusu nusu ni kuhusu nyumba za kuishi. Serikali imekiri wajibu wake wa kuwapatia madakari nyumba za kuishi. Aidha, imeeleza mpango ulioanza wa kujenga nyumba 700 za madaktari kote nchini na kwamba hivi sasa ujenzi wa nyumba 90 unaendelea, 50 katika mkoa wa Mtwara na 40 katika mkoa wa Rukwa.

      Kwa maeneo ambayo madaktari wanalipwa posho ya pango Serikali imesema waajiri wataendelea kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu zilizopo kwa watumishi wa umma wenye stahili ya kupewa nyumba. Jambo hilo limekataliwa na Madakari na kutaka lazima walipwe asilimia 30 ya mshahara kama posho ya nyumba. Serikali kwa upande wake imeona vigumu kufanya hivyo na kuwasihi wakubali wanayotendewa wafanyakazi wengine wote wa umma.


      Jambo lingine
      ambalo lilikuwa na makubaliano ya nusu nusu ni kuhusu posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu. Pande zote mbili ziliafikiana kuwa yapo baadhi ya maeneo nchini yanayo mazingira magumu kwa watumishi wa umma hivyo hatua zichukuliwe kuwasaidia watumishi hao. Serikali imekubali wajibu wa kuweka utaratibu wa kuboresha maisha ya watumishi katika maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, Serikali itatoa mwongozo kwa mamlaka za ajira kuhusu namna ya kuwasaidia watumishi hao kupunguza makali ya maisha katika kila eneo badala ya kutegemea posho peke yake.


      Kuhusu posho, Serikali imeeleza kuafiki kuwepo posho ya aina hiyo ila itatekelezwa baada ya kufanya uchambuzi wa kuainisha mazingira husika, kutambua watumishi waliopo na gharama zake.

      Madaktari hawajakubali kusubiri zoezi la uchambuzi lifanyike, wanataka Serikali ilipe posho hiyo sasa. Tofauti hapa si posho hiyo kuwepo, bali ni rai ya Serikali ya kubaini maeneo yenyewe na kupanga aina ya hatua na viwango vya posho kulingana na mazingira halisi ya maeneo. Madaktari hawaoni haja ya kufanya hayo.

      Ndugu Wananchi;

      Mambo mawili hayakuwa na muafaka kabisa kati ya pande zetu mbili. Jambo la kwanza ni posho ya kuitwa kazini (on call allowance). Kwanza sina budi kueleza kuwa Serikali imekubali kuongeza posho hiyo. Tangu Februari, 2012 posho iliongezwa kutoka shilingi 10,000/= hadi shilingi 25,000/= kwa daktari bingwa (Specialist), shilingi 20,000/= kwa dakari mwenye usajili wa kudumu (Registrars) na shilingi 15,000/= kwa madaktari waliohitimu ambao wapo katika kipindi cha mafunzo kazini (Interns). Viwango hivyo vya posho vinatumika hivi sasa.

      Madaktari kwa upande wao hawakukubali uamuzi huo wa Serikali na kusisitiza walipwe asilimia 10 ya mshahara. Ugumu wa kukubali pendekezo la madakari ni kuwa sharti la malipo haya ni mtu kuitwa kazini. Ukitaka ilipwe kiwango cha mshahara ina maana kuwa hata kama daktari hakupangwa kuitwa au alipangwa na hakutokea aendelee kulipwa. Hili haliwezi kuwa sahihi kufanya. Linaweza kuwafanya baadhi ya madaktari kutokutimiza wajibu wao kwa vile wana hakika mwisho wa mwezi malipo yako pale pale.


      Ndugu Wananchi;

      Jambo la pili ambalo muafaka haukufikiwa baina ya Serikali na madaktari ni kuhusu mshahara wa kuanzia kazi wa daktari. Madaktari wanataka uwe shilingi 3,500,000/= wakati Serikali inasema kiasi hicho hatukiwezi. Serikali imeeleza utayari wake wa kuongeza mshahara kwa kati ya asilimia 15 mpaka 20 kama ambavyo itafanya kwa watumishi wote wa umma katika mwaka huu wa fedha. Kwa kiwango cha sasa cha mshahara wao, daktari ataanzia kati ya shilingi 1,100,000/= na 1,200,000/= kutegemea kiwango kipi hatimaye kitaamuliwa. Madaktari wamekataa katakata na wameng’ang’ania shilingi 3,500,000/=.

      Ndugu Wananchi;

      Huo ndiyo mlolongo wa mambo yaliyozungumzwa na pande zote mbili na matokeo ya mazungumzo yenyewe. Katika kikao cha sita kilichofanyika tarehe 30 Mei, 2012, upande wa Chama cha Madaktari ulisema kuwa kwa vile hoja ya nyongeza ya mshahara haina mabadiliko hawakuona haja ya kuendelea na majadiliano mpaka watakapowasiliana na wenzao. Waliahidi kutoa taarifa ndani ya wiki mbili. Tarehe 12 Juni, 2012, Rais wa MAT aliandika barua kwa Katibu Mkuu Utumishi ambaye ndiye kiongozi wa majadiliano kwa upande wa Serikali, kuwa Madaktari wameikataa taarifa na ufafanuzi waliopewa kutoka Serikalini kwa ujumla wake.

      Ndugu Wananchi;

      Baada ya majibu yale ya madaktari, tarehe 19 Juni, 2012, Serikali na Madaktari walikwenda kwa Msuluhishi (CMA) kutoa taarifa kuwa mgogoro umekosa usuluhishi kama sheria inavyotaka. Kwa pamoja pande zote mbili zilikubaliana suala hilo lifikishwe Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi. Wakati pande zote zinasuburi mgogoro huu kufikishwa ngazi hiyo ya juu, upande wa Madaktari ukatangaza kuwepo kwa mgomo kuanzia saa sita ya usiku tarehe 23 Juni, 2012. Hatua hiyo haikustahili kwani suala lenyewe halijafika mwisho wa kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria za Mahusiano ya Kazi nchini.

      Ndugu Wananchi;

      Tarehe 22 Juni, 2012, Mwanasheria Mkuu wa Serikali akaenda Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kulifikisha suala la tishio la mgomo na kuomba zuio la muda kufanywa. Mahakama Kuu ilikubali ombi hilo na kuagiza kuwa mgomo usitishwe. Juhudi za kumtafuta Rais wa MAT, Dkt. Namala Mkopi na viongozi wengine wa MAT hazikufanikiwa, Ofisi ya MAT ilikuwa imefungwa na simu zote za viongozi wa MAT zilikuwa zimezimwa. Hatimaye tarehe 25 Juni, 2012, alipatikana na kupewa amri hiyo ya Mahakama. Tarehe 26 Juni, 2012, Dkt. Mkopi alifika Mahakamani ambapo alikana kuwa yeye hahusiki na kuitisha huo mgomo lakini hakumtaja aliyehusika. Pamoja na rai hiyo, Jaji alimuamuru Rais wa MAT akawatangazie wanachama wake kusitisha mgomo. Dkt. Namala Mkopi hajafanya hivyo hadi leo na mgomo umekuwa unaendelea kinyume cha Sheria.

      Ndugu Wananchi;

      Wagonjwa wanateseka na wengine kupoteza maisha kwa mgomo huu usiokuwa halali kisheria ambao pia haustahili kuwepo hata kwa mujibu wa maadili ya udaktari. Viongozi wa MAT na wenzao wanawaingiza Madaktari katika mgogoro na Mahakama na waajiri wao isivyostahili. Ni vyema viongozi wa Madaktari na madaktari wakatambua kuwa wanashiriki katika mgomo usiokuwa halali ambao pia kiongozi wao mkuu amekana Mahakamani kuwa hahusiki nao. Madaktari lazima watambue pia kwamba ajira zao wanaziweka hatarini. Mfanyakazi ana kinga ya kutofukuzwa kazi na mwajiri kwa kushiriki mgomo unaokubalika kisheria. Huu siyo. Watapoteza ajira, hawana pa kukimbilia, hawana cha kiwalinda. Kwa madaktari interns, wanahatarisha maisha yao kwani hawatapata cheti cha kudumu wakishiriki mgomo usiokuwa halali. Lazima watafakari sana kwa hayo wafanyayo.

      Ndugu Wananchi;

      Napenda kurudia maneno niliyoyasema tarehe 12 Machi, 2012, kuwa kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi ni Sera ya Serikali yetu kwa maelekezo ya Ilani ya Chama Tawala (CCM). Tumeitekeleza kwa vitendo sera hiyo, hata hivyo ni ukweli ulio wazi kuwa nia yangu njema tu pekee haitoshi, lazima uwezo wa kufanya hivyo uwepo. Kwa kulingana na uwezo uliopo, tumeendelea kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi hatua kwa hatua tangu tuingie madarakani. Tumefanya hivyo kwa jumla kwa wafanyakazi wote na kwa kada mbalimbali za watumishi wa umma.

      Miongoni mwa wafanyakazi wa umma walionufaika na hatua hizo za Serikali ni madaktari na watumishi wa kada nyingine za huduma ya afya. Tena nadiriki kusema madaktari tumewapa upendeleo mkubwa kuliko watumishi wengine wa umma. Upendeleo upo kwenye mafunzo ambapo wanafunzi wa udaktari wanagharimiwa na Serikali kwa asilimia mia moja wakati wanafunzi wenzao wa taaluma nyingine hawako hivyo.


      Ndugu Wananchi;

      Mwaka 2004/2005, mshahara wa kuanzia wa daktari ulikuwa shilingi 178,700/=, mwaka 2005/ 2006 tuliupandisha na kuwa shilingi 403,120/=. Tuliendelea kuupandisha mwaka hadi mwaka mpaka kufikia shilingi 957,700/= wanazolipwa sasa. Kiasi hicho ni mara mbili ya mishahara ya watumishi wa taaluma nyingine wenye shahada ya kwanza wanaoanza kazi ambao kwa wastani hupata shilingi 446,100/=.

      Tunafanya hivyo kwa kutambua na kuthamini nafasi maalum ya madaktari katika jamii na ukweli kwamba bado tunayo safari ndefu ya kuziba pengo la madaktari nchini. Lakini inaonekana juhudi zetu zote hizo hazithaminiwi.

      Ndugu Wananchi;

      Sina budi kusisitiza kwamba tunapofanya hivyo tunaongozwa na uwezo tulio nao wa kulipa. Kwa sasa hatuwezi kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi 3,500,000/= na posho zote zile. Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa shilingi 7,700,000/=. Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari.

      Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo. Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka. Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24. Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na sheria za kazi na maadili ya kazi ya udaktari.


      Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma. Najua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi. Vinginevyo atakuwa anajidanganya kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.


      Ndugu Wananchi;

      Napenda kuwathibitishia kwamba dhamira ya Serikali ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wakiwemo madaktari iko wazi. Tumekuwa tunafanya hivyo, na tutaendelea kufanya hivyo kulingana na uwezo wa kibajeti. Ni vyema watumishi wa umma wakatambua kuwa hatuwezi kutumia fedha zote au kiasi kikubwa mno cha pesa za umma kulipana mishahara. Tukifanya hivyo, Serikali itashindwa kutoa huduma muhimu kwa wananchi ambao ndiyo wengi na wanastahili kuhudumiwa. Hata hizo huduma za afya tunazosema ni duni tuziboreshe, hatutaweza kuziboresha kama tutatumia sehemu kubwa ya pesa za Serikali kuwalipa mishahara wafanyakazi.

      Hivi sasa matumizi ya mishahara ni asilimia 48 ya bajeti ya Serikali. Kiwango hicho ni kikubwa mno. Uwiano mzuri ni kuwa na matumizi ya mishahara yasiyozidi asilimia 35 ya bajeti na asilimia 65 zitumike kugharimia huduma na shughuli nyingine za maendeleo ya wananchi na taifa. Sisi tumezidi kwa asilimia 13. Hivyo, hatuna budi tukubali kujinyima kwa manufaa ya walio wengi.



      Suala la Dkt. Steven Ulimboka

      Ndugu Wananchi;
      Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Steven Ulimboka usiku wa tarehe 26 Juni, 2012. Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.

      Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa kiungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na Madkatari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.


      Ndugu Wananchi;

      Kama nilivyoeleza, mazungumzo yalienda vizuri na mafanikio makubwa yamepatikana. Yapo maeneo machache na hasa eneo la mshahara ambalo hatukuweza kukubaliana. Hapo tulipofikia si pabaya na tulikubaliana sote kurudi kwenye mkondo wa Sheria kusaidiwa. Kwa nini Serikali imdhuru Dkt. Ulimboka?

      Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha mgomo. Anayekaidi amri ya Mahakama ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo. Hivi baada ya kufika hapo Serikali iwe na ugomvi na Dkt. Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo lipi hata iamue kumdhuru? Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali.


      Ndugu Wananchi;

      Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali natoa mkono wa pole kwa Dkt. Steven Ulimboka na kumuombea apone haraka ili aungane na familia yake na Watanzania wenzake katika ujenzi wa taifa. Kwa namna ya pekee namshukuru na kumpongeza Bwana Juma Mgaza, kwa moyo wake wa huruma na upendo na kwa hatua alizochukua za kumsaidia Dkt. Ulimboka.

      Naomba kumaliza kwa kuwasihi madaktari kuacha mgomo na kurejea kazini. Watanzania wenzenu wanateseka na kupoteza maisha. Muwe na moyo wa huruma na upendo na msaada kwa wagonjwa kama kiapo chenu kinavyowataka.



      Mungu Ibariki Afrika!
      Mungu Ibariki Tanzania!
      Asanteni kwa Kunisikiliza.
      Ogah, zomba, Balantanda and 8 others like this.
      Semper fi!

    2. Miaka 50

    3. #341
      Eng. Y. Bihagaze's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 8th September 2011
      Location : Czech(but now in DAR)
      Posts : 766
      Rep Power : 5116
      Likes Received
      583
      Likes Given
      111

      Default Re: Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

      Nchi ya Maneno.Watu Wa maneno. Maneno maneno kila raia maneno.. Mafundi kweli Wa maneno..

      Kwani Maneno yanasaidia kuponya wagonjwa?. Watu wanakata roho huku ati, watu wanaotakiwa kufanyiwa operations hawajui hatma zao Na Hali zao zinazidi kudorora.. Hapa watu walioshiba ugali Na Kauzu wanapiga domo tu..

      Sikilizeni enyi mbweha.. Hatutaki maneno tena, Kama mnaona madai ya madaktari ni chachu tupilieni mbali wao Na madai Yao kwenye dustbins.. Na muajiri madaktari wengine Na raia tuendelee kupata matibabu ..

      Mambo ya maneno ni upuuzi .. Upuuzi mtupu, huyu namlipa sana, sijui yule kidogo, ah ni majungu tu yote hayo.. ilihali wananchi maskini ya mungu tusio Na hatia tunakwisha Kwa kukosa stahiki ya tiba..

      Sina Shaka kesho wahandisi nao watalianzisha.. Mhandisi kuanza Na 420,000 Na baada ya makato anakwenda hom Na 320,000 aiseee.. Hata house-girl Wa hapa masaki wanamzidi kipato mhandisi.. Erb mpo au mnachangisha michango ya stickers tu..

    4. #342
      kindafu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th November 2010
      Posts : 256
      Rep Power : 488
      Likes Received
      83
      Likes Given
      62

      Default Re: Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

      Quote By Osaka
      Tatizo ni kupata habari au tatizo ni Michuzi's Blog?
      Tatizo ni kwamba tuliambiwa atahutubia live kama kawaida, watu wamekesha wakikodelea macho Runinga zao na haikuwa hivyo! Asubuhi ndo tunaisoma Hotuba hiyo kwenye Michuzi's Blog!

    5. #343
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,024
      Rep Power : 0
      Likes Received
      227
      Likes Given
      1

      Default Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      "Daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara wa LAKI TISA U NUSU awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri" - Jakaya Mrisho Kikwete.


    6. #344
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,024
      Rep Power : 0
      Likes Received
      227
      Likes Given
      1

      Default Re: Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      Huna sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo. Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka. Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24. Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini

      Maundumula likes this.

    7. #345
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,024
      Rep Power : 0
      Likes Received
      227
      Likes Given
      1

      Default Re: Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua za kuwafukuza na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma. Najua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi. Vinginevyo atakuwa anajidanganya kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.

      Maundumula likes this.

    8. FemaTV & Radio

    9. #346
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,024
      Rep Power : 0
      Likes Received
      227
      Likes Given
      1

      Default Re: Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua za kuwafukuza na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma. Najua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi. Vinginevyo atakuwa anajidanganya kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.

    10. #347
      Escherichia Coli's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 67
      Rep Power : 383
      Likes Received
      26
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By ELIESKIA
      ninavyofahamu Dr ni mkit wa umoja wa madaktar ila nimeshangazwa na kauli ya Jk kuwa dr ulimboka hauhusiki na si mwajiriwa wa serikal . kutokuwa mwajiriwa kuna thibitisha kuwa wanachokitaka madaktar si mshahara tu maana wengne haitawahusu kwa vile wao serikal si mwajir wao bali wanagombania kuboreshwa kwa sekta ya afya . naomba kusadiwa na tuwekane sawa hasa wahusika wenyew
      Umenena vema rafiki!Dr Ulimboka ni mwajiriwa wa NGO,siyo mwajiriwa wa serikali(JK hajakosea kwa hili).Kinachomsukuma Dr Ulimboka kusimamia madai ya madaktari ni kiu yake ya kuona huduma bora za afya ktk hospitali za umma na maisha bora kwa watumishi wa afya TZ.Hana maslahi yoyote ya moja kwa moja ktk harakati hizi,isipokuwa yale ambayo watanzania wote watayapata iwapo serikali itatekeleza wajibu wake(kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wake).

    11. #348
      BONGOLALA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th September 2009
      Posts : 4,851
      Rep Power : 1467
      Likes Received
      1004
      Likes Given
      128

      Default Re: Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      mbona jk hajasema wagonjwa watatibiwa na nani iwapo madaktari wataacha kazi?
      MziziMkavu likes this.

    12. #349
      Judgement's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th November 2011
      Location : Town
      Posts : 7,019
      Rep Power : 7211
      Likes Received
      2774
      Likes Given
      12

      Default Re: Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      Option makini, imetulia.
      Haina makidai, makeke wala vitisho!
      Doctor aamue mwenyewe cha kufanya.
      Hawabebeki hawa watu.
      Maundumula likes this.

    13. #350
      Njangula's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 20th October 2011
      Posts : 179
      Rep Power : 418
      Likes Received
      16
      Likes Given
      1

      Default Re: Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      Tuendelee kuangalia senema ya huzuni.

    14. #351
      Mafuluto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th August 2009
      Posts : 797
      Rep Power : 2973
      Likes Received
      165
      Likes Given
      306

      Default Re: Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      Join June 2012, ndo umetumwa kuja kuelezea sera za Dhaifu ? Haya sasa subiri muumbuliwe na kontena la madawa sijui ile list aliyonayo miaka nenda rudi ataifanyia kazi lini, maana imejaa ndg, jamaa na marafiki !!

    15. #352
      LiverpoolFC's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2011
      Posts : 6,690
      Rep Power : 11281
      Likes Received
      1474
      Likes Given
      570

      Default Re: Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      Kichwa cha hbr haijaenda sawa na post!

      Nilitegemea kuona majina ya Madaktari ambao wangeacha kazi.

    16. #353
      Makala Jr's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th August 2011
      Posts : 1,616
      Rep Power : 714
      Likes Received
      334
      Likes Given
      0

      Default Re: Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      Kukimbia tatizo siyo njia ya kutatua tatizo.Serikali gani inakimbia kufanya negotiation na raia wake? Tunakubali kwamba nchi yetu ni masikini ni vigumu kuwalipa watumishi kama nchi zilizoendelea.

      Tatizo la serikali ni UPUUZI, kama tetesi kwamba mtawaleta madokta 1000 toka Iran,kifupi ni kwamba mtakuwa mmeanzisha kabila jipya la wairan nchini kwetu unless ibakie kuwa tetesi. Tatizo lingine ni UONGO,serikali inawezaje kuwa na fedha za kukimbizia mwenge,ikakosa fedha za kuboresha mazingira ya kazi ya waalimu na madaktari? Mnapataje fedha kumsafirisha Lowassa na Kamati yake kwenda kwenye balozi za Tanzania nje na mkakosa fedha za kuongeza mishahara?

      Mbona mawaziri hatuwasikii wakilia maisha magumu kutokana na kuwa na mshahara mnono,posho,madurufu,n.k Washauri wa Rais madudu matupu.Huwezi kufananisha mazingira ya kazi ya udaktari na watumishi wengine hivyo hata nyongeza ya mshahara ilitakiwa iwe zaidi ya watumishi wengine.

    17. #354
      MDAU JR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2011
      Posts : 323
      Rep Power : 480
      Likes Received
      40
      Likes Given
      25

      Default Re: Rais Kikwete ni sahihi tamko kuhusu Madaktari

      Quote By mamayeyo
      MDAU JR, Kwa hiyo ni sahihi kuwatoa kafara wagonjwa eti kwa sababu wabunge wanapewa mil10? Hakuna njia nyingine za kufanya hadi wagonjwa wafe? Kwani hizo pesa wanazofaidi wabunge ni za madaktari tu? Ni za wananchi wote. Itafutwe njia sahihi ya kukomesha mpango wa wachache kufaidi keki ya taifa wakati wengine wanaumia na si njia hii ya kuchezea roho za watu wasio na hatia. AMKA MDAU JR.
      Nimeamka ck nyingi ndo maana nina ufahamu juu ya jambo hili, Mkuu njia ndo hiyo, hizo zingine unazosema zimeshindikana. Mgomo wa kada yoyote una athari, walimu wakigoma kunakuwa hakuna elimu, madereva wa mabasi nao kunakuwa hakuna safari, Daktari naye wagonjwa wanakufa hiyo ndo kada yake, we unataka agome kula? nani atamsikiliza.

      Na hayo ndo malengo ya mgomo wowote ili haki husika inayodaiwa ipatikane. Huwezi kuwazuia kudai haki zao kwa kisingizio cha watu kufa halafu madai yao yanashughulikiwa kisiasa, eti tunaendelea na mazungumzo,mpaka lini? hadi kufikia watu wakaamua kugoma ni kwamba haya madai ni ya muda mrefu. Mliolala amkeni sasa msikubali kuwa foolled kila siku kuwa serk haina uwezo ili hali fedha zinalundikwa kwe akaunt za viongozi huko uswisi na kujinunulia makasri hapa nchini na nje ya nchi, vijana wetu wanasoma kwa shida vyuoni ili hali tuna rasilimali nyingi ambazo iwapo mikataba isingalifungwa ktk misingi ya rushwa na ubadhirifu yasingalitokea hayo.

      Wakati umefika sasa Kila mmoja asimame pale alipo adai stahili yake(wakulima, wanafunzi,wafanyakazi) M/mungu atalipa juhudi InshaAllah. mamayeyo usiogope kufa, wacha siye tufie wodini, lakini watoto na wajukuu zetu wanufaike hapo baadae na mgao sawa wa raslimali za Taifa letu.Hakuna anaye sapoti mauaji lakini fahamu kwamba hakuna kudai haki kwa lelemama, ikifikia hatua hii ni lazima watu wafe ili kupata mapinduzi ya kweli na ufumbuzi wa kudumu wa suala husika(watu wangapi walikufa South Afrika wakati wa kupinga ubaguzi wa rangi? lakini leo ni historia na kamwe ubaguzi ule haurudi tena mpaka kiama I swear, lakini kwa kuwa watu waliamua kukataa bila kujali watu wangapi watakufa) .

      Kwa kuwa watawala tulionao wamekwisha fahamu watu wlionao ni wa aina ya mamayeyo ndo maana wanatuburuza. Tubadilike sasa tuache uoga usio na msingi ambao ndo umetufikisha hapa tulipo, Wanasiasa wanatuona waTZ kuwa ni watu mabongolala tusiojuwa haki zetu, tuziondoe hizi mindset kwenye vichwa vyao.
      LAA ILAHA ILLALLAH MUHAMMADUR RASULULLAH

    18. #355
      ELIESKIA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 21st July 2011
      Posts : 107
      Rep Power : 417
      Likes Received
      14
      Likes Given
      0

      Default

      huu upotoshaji wa mishahara kama kigezo cha kuficha ukwel. ndo maana watekaji wanadhan anatumika?

    19. #356
      nndondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st February 2010
      Posts : 613
      Rep Power : 687
      Likes Received
      145
      Likes Given
      1

      Default Re: Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      hivi nashindwa kabisa kuwashangaa wadanganyika wanaochangia mada hii na kujiumbua, hivi ni kweli kuna wengine zaidi ya JK wasiojua mpaka leo ni nani muajiri na muajiriwa kati ya yeye na wakina ulimboka na sisi? Jamani how can you be so empty? mnaomdanganya chukueni hayo malip haraka maana soon ukweli utakuja kuonekana na sio kujulikana tena.

      Huyu bwana ni kibarua wetu, kama hajawahi kuambiwa na wakina omba omba na atambue sasa, hili swala la madaktari ndio Tahriri yake, jamani hapa nimekuja kutamka sio kutabiri, huyu jamaa ni bai bai yake hopeless kabisa eti waondoke kama hawataki, yeye nani atake? he lives enzi za madictator wasiokua na akili madikteta wa leo wanatutawala kwa technolojis, look at him sasa, he is an embarrassment look at him, yaani hajui kwamba anakula na kusaza na kusomesha watoto wake wasiokua na akili kwa hela za baba yake Ulimboka na baba za madaktari wengine wote anaowatukana na kuwadharau wakati yeye hakuwa na akili za kusomea udaktari wala sayansi tunaambiwa ni mchumi, my foot, wachumi wakina Lipumba wameonyesha uwezo wao

    20. #357
      MDAU JR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2011
      Posts : 323
      Rep Power : 480
      Likes Received
      40
      Likes Given
      25

      Default Re: Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

      Quote By Eng. Y. Bihagaze
      Nchi ya Maneno.Watu Wa maneno. Maneno maneno kila raia maneno.. Mafundi kweli Wa maneno..

      Kwani Maneno yanasaidia kuponya wagonjwa?. Watu wanakata roho huku ati, watu wanaotakiwa kufanyiwa operations hawajui hatma zao Na Hali zao zinazidi kudorora.. Hapa watu walioshiba ugali Na Kauzu wanapiga domo tu..

      Sikilizeni enyi mbweha.. Hatutaki maneno tena, Kama mnaona madai ya madaktari ni chachu tupilieni mbali wao Na madai Yao kwenye dustbins.. Na muajiri madaktari wengine Na raia tuendelee kupata matibabu ..

      Mambo ya maneno ni upuuzi .. Upuuzi mtupu, huyu namlipa sana, sijui yule kidogo, ah ni majungu tu yote hayo.. ilihali wananchi maskini ya mungu tusio Na hatia tunakwisha Kwa kukosa stahiki ya tiba..

      Sina Shaka kesho wahandisi nao watalianzisha.. Mhandisi kuanza Na 420,000 Na baada ya makato anakwenda hom Na 320,000 aiseee.. Hata house-girl Wa hapa masaki wanamzidi kipato mhandisi.. Erb mpo au mnachangisha michango ya stickers tu..
      Wahandisi mnakula 10% kutoka kwa makandarasi sorry ni 20% siku hizi, hamna shida ya mishahara hata kama msipolipwa kabisa, kwa hiyo usitegemee mgomo kutokea kwa wahandisi.
      LAA ILAHA ILLALLAH MUHAMMADUR RASULULLAH

    21. #358
      Topical's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd December 2010
      Posts : 5,050
      Rep Power : 1231
      Likes Received
      853
      Likes Given
      707

      Default Re: Madaktari wafuatao kuacha kazi rasmi kesho

      Quote By nndondo
      hivi nashindwa kabisa kuwashangaa wadanganyika wanaochangia mada hii na kujiumbua, hivi ni kweli kuna wengine zaidi ya JK wasiojua mpaka leo ni nani muajiri na muajiriwa kati ya yeye na wakina ulimboka na sisi? Jamani how can you be so empty? mnaomdanganya chukueni hayo malip haraka maana soon ukweli utakuja kuonekana na sio kujulikana tena. Huyu bwana ni kibarua wetu, kama hajawahi kuambiwa na wakina omba omba na atambue sasa, hili swala la madaktari ndio Tahriri yake,jamani hapa nimekuja kutamka sio kutabiri, huyu jamaa ni bai bai yake hopeless kabisa eti waondoke kama hawataki, yeye nani atake? he lives enzi za madictator wasiokua na akili madikteta wa leo wanatutawala kwa technolojis, look at him sasa, he is an embarrassment look at him, yaani hajui kwamba anakula na kusaza na kusomesha watoto wake wasiokua na akili kwa hela za baba yake Ulimboka na baba za madaktari wengine wote anaowatukana na kuwadharau wakati yeye hakuwa na akili za kusomea udaktari wala sayansi tunaambiwa ni mchumi, my foot, wachumi wakina Lipumba wameonyesha uwezo wao
      Tahrir utaenda na nani wewe?

      Tumeanza kufuatilia deal zote za madaktari Tanzania kwa ufupi

      a. Hawafanyi kazi masaa yanayotakiwa katika hospitali ya taifa muda mwingi wako katika hospitali binafsi wanavuta kati ya tsh 300,000-1,000,000/- kwa siku huku wananchi maskini wakiwapa foleni na kuwapangaia tarehe bila sababu afadhali tuajiri wageni ambaye atafanya kazi full time na wagonjwa wetu watatibiwa

      b. Wanatumia vifaa vya serikali (hospitali ya serikali) kufanya diagnosis ya wagonjwa kutoka kwenye hospitali na dispensary zao bila kuilipa Muhumbili chochte, hivyo kufichakaza vifaa vya hospitali, kuongeza foleni kwa wagonjwa muhimbili kupata majibu yao vipimo vyao..tabia chafu na morally inaapropriate..

      c. Viongozi wa vitengo (wakuu wa idara) ambao ni madrs kuuza vifaa na spea za goverment hospital facilities kwa private hospital hivyo serikali kuishia kuwa na hasara ya kununua kila mwaka, ...

      Bado mengi yataibuka..bado saana..issue yao
      norbit likes this.
      "Mbowe for Presidency 2015""

    22. #359
      Mbogela's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th January 2008
      Location : Tanzania
      Posts : 1,151
      Rep Power : 808
      Likes Received
      70
      Likes Given
      37

      Default JK amezuia uchunguzi huru wa Kesi ya Dr. Ulimboka!

      Katika Hotuba yake JK amekiri kuwa Serikali ni mmoja wa watuhumiwa wa watekaji nyara na watesaji wa Dr. Ulimboka. Nadhani kwa hilo yupo sahihi kabisa. Pia amesema akiwa kama Rais wa Nchi ameagiza vyombo vya usalama kufanya uchunguzi na kutoka na majibu haraka iwezekanavyo ili kuweza kuwapa wananchi ukweli wa nini kilitokea. Hilo nalo nakubaliana naye kuwa ni jambo sahihi.

      Baada ya hapo akatumia muda mwingi kujitetea yeye mwenyewe, serikali yake na vyombo vya dola.

      Sasa ninapata wasi wasi kama uchunguzi wa vyombo vya dola utakuwa huru na wa haki. Maana tayari katika hotuba ya Rais ya leo, Rais ameshavikataza vyombo vya dola visiichunguze serikali, pia ameshavikataza vyombo hivyo kumchunguza yeye kama anahusika kwa namna moja am nyingine kupitia utetezi alioutoa katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi.

      Nadhani kama Rais angekuwa na nia ya dhati na kama angetaka kuwa mkweli asingesema lolote kuhusu kuhusika au kutohusika kwa serikali na vyombo vyake na hata yeye mwenyewe ili vyombo vinavyohusika na uchunguzi vifanye kazi yake vikiwa huru na bila influence ya maneno yake ya ukali kuwa hajahusika na wala serikali yake na vyombo vyake haijahusika.

      Mpaka hapo sina imani na vyombo vya uchunguzi vya ndani ya nchi, kwani usalama wa Taifa wanawajibika kwake, polisi wanawajibika kwa Raisi. Na kwa Hotuba ya Leo naona kabisa karibpio, Katazo la Rais kwa vyombo vya uchunguzi na upelelezi kuichunguza serikali na watumishi wake akiwem Rais.
      4 UR Business Solution

    23. #360
      Papizo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th February 2008
      Location : What for??
      Posts : 3,309
      Rep Power : 1235
      Likes Received
      406
      Likes Given
      2254

      Default re: JK amezuia uchunguzi huru wa Kesi ya Dr. Ulimboka!

      Anajuwa kinachoendelea huyu DHAIFU ndio maana amepiga mkwara wasiichunguze serikali wala yeye mwenyewe..Siku zinahesabika kaka yeye ni zaidi ya Ghadafi then tutaona ukweli

    Page 18 of 26 FirstFirst ... 81617181920 ... LastLast

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...