Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

    Report Post
    Page 8 of 17 FirstFirst ... 678910 ... LastLast
    Results 141 to 160 of 332
    1. #1
      Gambas's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2011
      Location : Malimbe, Nyegezi Mwanza
      Posts : 955
      Rep Power : 2449
      Likes Received
      191
      Likes Given
      17

      Default UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      "NI saa 12:45 asubuhi, bado kiza kimetanda katika eneo hili la Msitu wa Mabwepande. Mbele yangu namwona mtu akiwa amekaa chini, pembeni ya barabara akiwa amelowa damu mwili mzima.

      "Ninapomkaribia nasikia sauti ya mtu huyo ikisema kwa taabu; naomba msaada jamani… naomba msaada jamani", hivi ndivyo anavyoanza kusimulia Juma Mgaza Abdallah, mtu wa kwanza kumwona Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka baada ya kutekwa, kupigwa na kutupwa katika Msitu wa Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

      Abdallah, anasema mara baada kumwona daktari huyo akiwa katika hali hiyo, alijaribu kumkokota kumtoa eneo hilo, lakini alishindwa kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo.

      Baada ya hapo, aliamua kusubiri mtu mwingine apite eneo hilo ili amwombe wasaidiane kumpeleka Kituo cha Polisi Bunju.

      Anasema muda mfupi baadaye aliona gari likija mbele yao, akalinyooshea mkono kulisimamisha. Liliposimama, akamweleza dereva hali aliyokuwa nayo Dk Ulimboka na kwamba anahitaji msaada wa haraka.

      Abdallah ambaye hadi wakati huo alikuwa hamfahamu mtu ambaye alikuwa akimsadia kuwa ni kiongozi wa madaktari kutokana na sura yake kuvimba, anasema walimwingiza katika gari hilo na kumpeleka Kituo Kidogo cha Polisi Bunju.

      Anasema, Dk Ulimboka wakati huo alikuwa akiendelea kuvuja damu katika baadhi ya majeraha yake huku akiwa hana suruali na kubaki na bukta tu, huku akizungumza kwa taabu.

      Kituo cha Polisi Bunju

      Baada ya kumfikisha kituoni hapo, walitoa maelezo namna walivyomwokota na kumsaidia kumfikisha hapo.

      Polisi baada kumhoji Dk Ulimboka, aliwatajia namba ya simu ya rafiki yake aitwaye Dk Deo. Walipompigia na kumweleza tatizo hilo, aliamua moja kwa moja kwenda Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kutoa taarifa hizo na hatimaye kuandamana na watu kadhaa kutoka hapo akiwamo Mkurugenzi wake, Hellen-Kijo Bisimba.

      Wawasili kituoni
      Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania wa kituo hicho, Onesmo Olengurumwa, anasema waliwafika Polisi Bunju saa 3:36 asubuhi na kumkuta Dk Ulimboka akiwa amekalishwa kwenye benchi huku damu ikiwa imeganda kwenye majeraha mwilini.

      Olengurumwa anasema waliwahoji polisi waliokuwa kituoni hapo kwa nini wakae na mtu aliyeumia kiasi hicho muda mrefu bila ya kuita gari la wagonjwa kumchukua ili kuwahi kupatiwa matibabu.

      Olengurumwa anasema polisi walisema kwamba, walikuwa wanawasubiri ndugu zake wafike.

      Baada ya muda mfupi, akiwa ameingizwa kwenye gari kupelekwa hospitali, Dk Ulimboka aliomba maji ya kunywa akisema ana kiu sana, lakini alipopewa, alikunywa kidogo akashindwa.

      Anasema wakiwa njiani, alikuwa akilalamika kuwa anasikika maumivu makali huku akisisitiza kuwa tukio la kutekwa na kupigwa lilikuwa la kumuua.

      "Jamani hawa watu walitaka kuniua walikuwa wamepanga kuniua," alisikika mara kwa mara akisema Dk Ulimboka wakati anapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu.

      Maelezo ya Dk Ulimboka
      Baada ya Dk Ulimboka kuokotwa aliweza kuzungumza na kurekodiwa muda mfupi baada ya kutolewa msituni na mazungumzo yake yalikuwa hivi;

      “Nilikamatwa na watu hao usiku wa Jumanne nikiwa maeneo ya Leaders Club, Kinondoni na daktari mwenzangu baada ya kupigiwa simu na mtu mmoja ambaye alidai kuwa anafanya kazi Ikulu.

      “Kuna jamaa mmoja anafanya kazi Ikulu, kama siku tatu mfululizo alikuwa akitaka kukutana na mimi ila nilishindwa kukutana naye kwa kuwa nilikuwa na kazi nyingi na wakati mwingine mpaka usiku,” alisema Dk Ulimboka.

      Huku akizungumza kwa taabu kutokana na mdomo wake kuvimba, alisema siku hiyo mtu huyo alimpigia tena simu na kumtaka wakutane.

      “Jana (Jumanne) alinipigia simu na nikamwambia daktari mwenzangu twende tukaonane naye, wakati huo alitueleza kuwa alikuwa maeneo ya Kinondoni Stereo,” alisema Ulimboka na kuongeza:

      “Tulipofika maeneo hayo tukampigia simu na akatueleza kuwa alikwisha ondoka, baadaye tukamweleza sehemu tulipo mimi pamoja na mwenzangu.”

      Alisema kuwa, wakati anakutana na mtu yule maeneo ya Leaders Club, hakuwa na amani.

      “Kwa kweli siku ile nilivyoonana na mtu yule sikuwa na amani kabisa ya kukaa eneo lile,” alisema Dk Ulimboka.

      Alisema kuwa wakati wakiendelea na maongezi ya kawaida, bado aliendelea kuwa na mashaka na mtu yule.

      “Katikati ya maongezi nikaona ameanza kuzungumza na simu, kila tukitaka kuagana alikuwa akizungumza na simu, sijui nini kilikuwa kinachelewesha sisi kuagana,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza:

      “Ghafla walitokea watu kama watano na kusema kuwa hawana tatizo na mtu yeyote katika eneo hilo isipokuwa mimi.

      Wakati sijakaa sawa, waliniburuza hadi barabara ya lami kwa kuwa eneo hilo lilikuwa karibu na barabara.”

      Aliongeza, “Nilipowauliza wananipeleka wapi, wakaniambia kuwa mimi nasumbua sana na nitajua hukohuko, waliniingiza katika gari jeusi, lakini halikuwa na namba. Niliwauliza kosa gani nimefanya? Hawakunijibu kitu na kusema, we twende utajua hukohuko.’’

      Alisema alipokuwa ndani ya gari hilo watu hao walimpiga na kwamba walipofika maeneo ya Victoria, walichukua sweta nyeusi na kumfunga usoni, jambo lililomfanya ashindwe kuona kinachoendelea ikiwa ni pamoja na alikokuwa akipelekwa.

      “Walinipiga mateke ya mbavuni, wakati mwingine walitumia vitako vya bunduki, kila nilipokuwa najaribu kuangalia ninapokwenda nilishindwa,” alisimulia Dk Ulimboka.

      Alisema kuwa watu hao walimpeleka katika nyumba moja ambayo hakujua iko sehemu gani ambapo walimshusha na kuanza kumshambulia kwa mateke mfululizo kila sehemu ya mwili. Wakati huo, wote walimshinikiza awaambie nani yupo nyuma ya mgomo wa
      madaktari.

      “Tangu saa sita usiku mpaka saa 9:00 alfajiri walikuwa wananipiga tu, kuna wakati nilijaribu kukimbia wakapiga risasi juu nikasimama na sikuweza kukimbia tena,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza:

      “Nilisimama, wakaendelea kunipiga, niliwasikia wakisema ama wanichome sindano ya sumu nife au kunikanyaga na gari. Baadaye wakaanza kuning’oa meno na kucha kwa kolea huku wakinilazimisha kusema nani yupo nyuma ya mgomo wa madaktari."

      Alisema kuwa, watu hao walikuwa na bunduki kubwa ambayo hakuweza kuitambua ni aina gani.

      “Waliniambia kuwa ninajua ninachokifanya hivyo wanaweza kunichoma sindano ya sumu nife au wanikanyage na gari nife,” alisimulia.

      Dk Ulimboka alisema kuwa awali hakuwa na shaka na watu hao kwa kuwa alidhani ni polisi, lakini baadaye alishindwa kuwaelewa kwani watu hao walimchanganya.

      “Sikuweza kuwatambua ila naweza kusema ni askari, walipokuwa wananipeleka niliwauliza mnanipeleka wapi na wakati huo nilikuwa sioni mbele ila ilikuwa kama maeneo ya Mwenge hivi,” alisema Dk Ulimboka.

      Alisema kuwa baadaye alipoteza fahamu na hakuweza kuona chochote zaidi ya kusikia sauti za watu hao kwa mbali.

      “Nilikuwa sioni na nilipoteza fahamu nikawa nasikia tu wakinibeba, gari lilitembea muda mrefu, sikujua ni wapi tunakwenda, kumbe ndio huko Mabwepande,” alisema.

      Alisema kuwa walifika maeneo ya barabara ya vumbi na baadaye wakamshusha na kumbeba hadi msituni.

      “Waliniburuza na kuniacha huko na muda wa saa kumi alfajiri ndipo nikazinduka na kuanza kujiburuza kuelekea barabarani ambako nilisaidiwa na mtu mmoja ambaye simtambui,” alisema Dk Ulimboka.

    2. Study Abroad

    3. #141
      PakaJimmy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2009
      Posts : 14,680
      Rep Power : 22519
      Likes Received
      6336
      Likes Given
      2831

      Default Re: mwenye uhakika na waliomtesa dr. ulimboka atujuze

      Mkuu
      Suala hili linafanyiwa uchunguzi na Tume ya mapolisi, akiwemo ndani Kamanda Msangi. Tuwe na subira, majina yatajulikana soon.

    4. #142
      Elungata's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th January 2011
      Posts : 3,659
      Rep Power : 1238
      Likes Received
      411
      Likes Given
      0

      Default Re: Siku ya kuketekwa dk.ulimboka alikuwa na wenzake wawili

      Inaonekana walikua tungi sana.
      Hivi kwani walimkeketa?

    5. #143
      Pinokyo Jujuman's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2012
      Posts : 511
      Rep Power : 470
      Likes Received
      64
      Likes Given
      5

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Hii taarifa ya Dr.Uli kuna kitu hapa kati yake kimejificha; Muda wa saa sita usiku walikutana maeneo ya Leaders kwa mazungumzo ya namna gani, na kwa nini iwe wao watatu tu, na huyu Dr.Deo ni nani katika uongozi wa Madaktari, huko Leaders ni baa au nyumba ya nani walipoenda kukutania, Je walikua wao watatu tu hakukuwa na watu wengine?
      Kama walikuwepo mbona hawakutoa msaada hata wa kupga kelele au wa kutoa taarifa police usiku ule?
      Je tukisema Dr's hawa wawili walikua na mpango binafsi tunakosea?

    6. #144
      MTU WA VITA's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 8
      Rep Power : 353
      Likes Received
      1
      Likes Given
      1

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      nafikili kwa uchungu sana lakini damu itwalipwa si mda mrefu kwani hata MUNGU wa haki sio mdhalimu kiasi hicho kuacha jambo baya kama hilo naam hakika yake p na k wapaswa kujibu kama si kwa wannchi basi wakiwa pekeyao MUNGU ata wadhibu vikali
      Last edited by MTU WA VITA; 2nd July 2012 at 10:27. Reason: un finished

    7. #145
      OPORO's Avatar
      Member Array
      Join Date : 22nd April 2012
      Posts : 59
      Rep Power : 367
      Likes Received
      14
      Likes Given
      5

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Serikali ya Kikwete imehusika na unyama huu wala hakuna namna ya kukwepa

    8. FemaTV & Radio

    9. #146
      Mwanahisa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th June 2012
      Posts : 1,149
      Rep Power : 576
      Likes Received
      314
      Likes Given
      129

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By Chipukizi
      Somebody did it to please his boss He ordered ****ing POP OO to do It. But Mungu ni Mkubwa,Magamba 2015 is so near,Tunisia and Iraq or Lybia not too far from Tanzania,chezeni na wadanganyika ila yupo Mungu anae wajari watu wake.Farao was so powerfull,Sadam was so powerfull, Gadafi was so powerfull,Samweli do was so power full alitembezwa na toroli nchi nzima,Gadafi ....... Hawa wote wamekufa vifo vya ajabu na familia zao kupotea mbele ya uso wa dunia,Leo hii MToto wa Nyerere au Mandela anaweza kujitambulisha ata manzese au soweto akapewa geto akalala na msosi akapewa! Je mtoto wa abacha,samweli Dore,sadam,gadafi au Mubarak atatjitaja wapi wampokee? Mungu awape ufaamu wanasiasa wajue kuwa vijisent wanavyojikusanyia ni umauti wao na damu ya watoto wao CCM hoyeeee
      Chipukizi Unaufahamu wakuona mbali sio kama hiyo Avatar yako haipumziki?

    10. #147
      Sashimi's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 2nd July 2012
      Posts : 1
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      huu ni unyama wa kutisha..

    11. #148
      Njoka Ereguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 503
      Rep Power : 459
      Likes Received
      167
      Likes Given
      30

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By Azimio Jipya
      Kukeketwa ndio nini kwenye taarifa yako? NONSENSE!
      Mkuu soma vizuri taarifa yangu nionyeshe hilo neno kukeketwa katika taarifa uliyo-quote.

    12. #149
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By NasDaz
      Jambo moja ama mawili bado hayajaniingia akilini kuhusu sakata hili:
      1. Dr. Ulimboka alikwenda Leaders na rafiki daktari mwenzake. Baada ya kuongea na mtu anayedaiwa kuwa ni wa Ikulu, baadae wakatokea watu wengine watano wenye silaha na kusema hawana s hida na hao wengine isipokuwa Ulimhoka. Wakamkokota hadi barabarani.
      Shari tayari ilishaonekana. Sasa ni kwanini huyo daktari mwenzake aliyekuwa nae Leaders aliamua kukaa kimya licha ya kwamba mazingira aliyochukuliwa Ulimboka yalikuwa ya shari?! Ilikuwaje Dk Deo apate taarifa asubuhi wakati Ulimboka alikuwa na mwenzake pale Leaders na yeye alikuwa huru?! Kwanini mwenzake huyu hakwenda kutoa taarifa kituo cha polisi au sehemu yoyote ambayo kwao inaaminika na badala yake akaamua kupotezea.

      2. Baada ya Dokta Deo kupigiwa simu na kuambiwa kuhusu hali ya Ulimboka, yeye aliamua kukimbilia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu badala ya kuchukua hatua ya kwenda kumwona Ulimboka na ikiwezekana kunusuru maisha yake kwanza. Nini maana yake hii?!

      nafikiri unafanya makusudi kutokuelewa...imeshasema sana kuwa baada ya kutekwa dr deo alienda polisi usiku ule ule na akawasilina na wanaharakati....
      I'm Naturaly Evasive..

    13. #150
      chuwaalbert's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th September 2010
      Posts : 295
      Rep Power : 499
      Likes Received
      52
      Likes Given
      129

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By Mwea
      "NI saa 12:45 asubuhi, bado kiza kimetanda katika eneo hili la Msitu wa Mabwepande. Mbele yangu namwona mtu akiwa amekaa chini, pembeni ya barabara akiwa amelowa damu mwili mzima.


      Abdallah, anasema mara baada kumwona daktari huyo akiwa katika hali hiyo, alijaribu kumkokota kumtoa eneo hilo, lakini alishindwa kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo. Baada ya hapo, aliamua kusubiri mtu mwingine apite eneo hilo ili amwombe wasaidiane kumpeleka Kituo cha
      Polisi Bunju.


      Anasema, Dk Ulimboka wakati huo alikuwa akiendelea kuvuja damu katika baadhi ya majeraha yake huku akiwa hana suruali na kubaki na bukta tu, huku akizungumza kwa taabu.

      Baada ya kumfikisha kituoni hapo, walitoa maelezo namna walivyomwokota na kumsaidia kumfikisha hapo. Polisi baada kumhoji Dk Ulimboka, aliwatajia namba ya simu ya rafiki yake aitwaye
      Dk Deo. Walipompigia na kumweleza tatizo hilo, aliamua moja kwa moja kwenda Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kutoa taarifa hizo na hatimaye kuandamana na watu kadhaa kutoka hapo akiwamo Mkurugenzi wake, Hellen-Kijo Bisimba.


      Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania wa kituo hicho,
      Onesmo Olengurumwa, anasema waliwafika Polisi Bunju saa 3:36 asubuhi na kumkuta Dk Ulimboka akiwa amekalishwa kwenye benchi huku damu ikiwa imeganda kwenye majeraha mwilini.

      Olengurumwa anasema waliwahoji polisi waliokuwa kituoni hapo kwa nini wakae na mtu aliyeumia kiasi hicho muda mrefu bila ya kuita gari la wagonjwa kumchukua ili kuwahi kupatiwa matibabu.

      "Jamani hawa watu walitaka kuniua walikuwa wamepanga kuniua," alisikika mara kwa mara akisema Dk Ulimboka wakati anapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu.



      “Nilikamatwa na watu hao usiku wa Jumanne nikiwa maeneo ya Leaders Club, Kinondoni na
      daktari mwenzangu baada ya kupigiwa simu na mtu mmoja ambaye alidai kuwa anafanya kazi Ikulu.

      “Kuna jamaa mmoja anafanya kazi Ikulu, kama siku tatu mfululizo alikuwa akitaka kukutana na mimi ila nilishindwa kukutana naye kwa kuwa nilikuwa na kazi nyingi na wakati mwingine mpaka usiku,” alisema Dk Ulimboka.

      Dk Ulimboka alisema kuwa awali hakuwa na shaka na watu hao kwa kuwa alidhani ni polisi, lakini baadaye alishindwa kuwaelewa kwani watu hao walimchanganya.

      Kwa kuwa Mwenyekiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu alikwenda Bunju Polisi stesheni kumpokea Dr. Ulimboka na kumpeleka MOI, na kwa kuwa Daktari huyo alipotekwa alikuwa na rafiki yake (Huyu ni shahidi aliyeshuhudia tukio la utekaji ambaye bila shaka aliliripoti), BASI, ingefaa shauri hili lipelekwe Mahakamani ili sheria ichukue Mkondo wake! Mashahidi wengine wawe Juma Abdallah, Onesmo Olengurumwa na Dk Deo.

    14. #151
      yatima's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2011
      Location : small room
      Posts : 352
      Rep Power : 486
      Likes Received
      106
      Likes Given
      121

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      POLE sana Dr. Ulimboka; Pole sana Mama yake Dr. Ulimboka; Pole sana Baba yake - pole kwa mashangazi zake, wajomba zake, dada zake na kaka zake. Pole kwa watanzania wote walioguswa na jambo hili na hasa wale wanaochukia mambo ya kijambazi katika maisha.

      Kama vile Mungu alivyoingilia kati - na kuwazuia wale MAKATILI wasimuue Dr. Ulimboka - ili ukweli ujulikane kuhusu Serikali ya CCM na Rais wake ........ NDIVYO ATAKAVYOWEKA MAMBO YOTE PEUPE.............waswahili wanasema "HAKUNA SIRI DUNIANI" - hata kama wangemuua - wangeweweseka na kujitaja tu wenyewe .... DAMU YA MTU INA NGUVU SANA .....

      Tuzidishe maombi - Mungu anajibu maombi!!!

      DONT BE A WEAPON TO INFLICT PAIN IN OTHER PEOPLE HEARTS

    15. #152
      JOSEYS's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 2nd July 2012
      Posts : 1
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Hali kama hii inayoendelea Nvhini mwetu Tz,inaondoa kabisa uzalendo na kujituma kulitumikia taifa hili, haina maana kwa mtu kujisomesha kwa dhiki na taabu nyingi, huku watoto wa rais wanasomeshwa na bodi ya mikopo, halafu wewe kajamba nani uliyejisomesha mwenyewe inakuja tokea unafanyiwa unyama kama huu.
      But God is watching over us, yeye ni hakimu wetu -atawasukumia nguvu za kuchanganyana mpaka wapotee kabisa-ibaki historia tz.

    16. #153
      Mkomamanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th December 2011
      Posts : 361
      Rep Power : 448
      Likes Received
      58
      Likes Given
      0

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By georgeallen
      Hata tukijua (100%) ni serikali imefanya hivyo kuna lolote la kuifanya? nauliza tu.
      Kujua ukweli si kwa sababu ya kutaka kufanya kitu fulani, lakini kujua ni kukidhi hitaji la akili na utashi wa binadamu. Ukisha ujua ukweli utakusaidia kufanya maamzi katika matukio yanayohusu maisha yako na si lazima kufanya kitu kwa aliyesababisha matukio. Ukweli utawaweka huru! Yoh. 8:32

    17. #154
      piper's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th January 2012
      Posts : 1,587
      Rep Power : 763
      Likes Received
      241
      Likes Given
      39

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Ama kweli mahakama ya chui mbuzi hana sheria

    18. #155
      PMNBuko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th December 2010
      Posts : 907
      Rep Power : 606
      Likes Received
      120
      Likes Given
      28

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Mimi bado sakata la Dr. Ulimboka linaniacha na maswali mengi sana. Labda tumsubiri yeye atatueleza, la msingi tumwombee apone haraka arejee nchini akiwa mzima wa afya.
      ".....development is the growth of thoughts....." Yes. We can!!

    19. #156
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4015
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By NasDaz
      Jambo moja ama mawili bado hayajaniingia akilini kuhusu sakata hili:
      1. Dr. Ulimboka alikwenda Leaders na rafiki daktari mwenzake. Baada ya kuongea na mtu anayedaiwa kuwa ni wa Ikulu, baadae wakatokea watu wengine watano wenye silaha na kusema hawana s hida na hao wengine isipokuwa Ulimhoka. Wakamkokota hadi barabarani.
      Shari tayari ilishaonekana. Sasa ni kwanini huyo daktari mwenzake aliyekuwa nae Leaders aliamua kukaa kimya licha ya kwamba mazingira aliyochukuliwa Ulimboka yalikuwa ya shari?! Ilikuwaje Dk Deo apate taarifa asubuhi wakati Ulimboka alikuwa na mwenzake pale Leaders na yeye alikuwa huru?! Kwanini mwenzake huyu hakwenda kutoa taarifa kituo cha polisi au sehemu yoyote ambayo kwao inaaminika na badala yake akaamua kupotezea.

      2. Baada ya Dokta Deo kupigiwa simu na kuambiwa kuhusu hali ya Ulimboka, yeye aliamua kukimbilia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu badala ya kuchukua hatua ya kwenda kumwona Ulimboka na ikiwezekana kunusuru maisha yake kwanza. Nini maana yake hii?!
      Ngumu sana kuielewa picha hii kwa haraka haraka...ila as time goes on taratibu kuna picha inayoanza kujionyesha.Kukamilika kwake sijui itakuwa lini tena
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    20. #157
      tripojo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 4th January 2008
      Posts : 61
      Rep Power : 593
      Likes Received
      5
      Likes Given
      95

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By Kiby
      .
      Hivi gazeti la Kubenea litatoka lini? Nalisubiri kwa hamu kwani ndilo lenye uthubutu thabiti!!
      .
      Ngoja tuone Jumatano hii Mwana Halisi itasema nini kuhusu tukio hili la kinyama. Kumbuka Saed Kubenea naye aliponea chupu chupu kunyofolewa uhai wake kwa tindikali!

    21. #158
      Chesty's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2009
      Posts : 1,037
      Rep Power : 701
      Likes Received
      155
      Likes Given
      18

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By Nambombe
      Usalama wa Taifa ilikuwa zamani enzi ya vita baridi,siku hizi wanapeana tu maadamu ni mtoto wa mjomba.usalama wa Taifa unatakiwa utumie akili ili uunganishe vipande upate kitu kizima,lakini kwa vile wanapeana hata kwenye sekta nyeti kama hii...madhala yake ndio hayo,yaani,nguvu nyingi na akili kidogo na matokeo yake wanashindwa kumshauri rais mambo ya manufaa.Mimi ningekuwa boss wa usalama wa taifa ningewafukuza kazi hao wote waliomteka Dr ulimboka sababu hawakutumia akili katika kupata taarifa za msingi na matokeo yake wameharibu kazi.Hata kama angepewa mwendawazimu kumfuatilia Dr ulimboka asinge tumia mbinu za kitahaira kama hizo kupata habari.Hayo ndio madhara ya kupeana kwenye taasisi nyeti kama hiyo na munamuangusha Rais ambae mimi ninadhani ana nia ya dhati ya kumaliza mgomo huu.Rais JK anaangushwa na watendaji wajinga na wasiojua kazi zao kama hao waliompiga Dr ulimboka.Hakukuwa na haja ya kutumia nguvu kubwa kiasi hicho,walitakiwa watumie akili nyingi na wangejua kila kitu.Dr ulimboka inawezekana anatumiwa yeye mwenyewe bila kujua na hapo inaitajika akili kuunganisha vipande upate kitu kamili na sio mabavu,jamani hii dunia ya sasa ni dunia ya kutumia akili na sio mabavu.Vyombo vya usalama mmetuangusha utazani humo ndani hakuna wasomi...au ndio wale wale wa kununua mitihani na kutoka na first class lakini practical zero.
      Hapo kwenye red naona umelikoroga kabisa, sorry though. Yaani kwa akili yako hao TISS wanaweza tu kuamka asubuhi na kuamua kwenda kumchukua mtu na kumtesa bila the higher authorities kutoa maelekezo. Kweli ndio unavyoamini hivyo?

    22. #159
      Rohombaya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2011
      Posts : 346
      Rep Power : 467
      Likes Received
      52
      Likes Given
      40

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By Tuandamane
      jamani kwann mmemtaja huyu Abdallah, tena majina yake yote.. consider him dead mpaka saivi, nadhani mwawajua hawa watu, imagine mwankyembe ametaka kuuawa ingawa report keshaisoma bungeni..

      muwe unakumbuka hivi vitu jama
      Hii ndio tabu ya waandishi wengi wa bongo. hawajali usalama wa wahusika katika habari zao wao wanachojali ni kuuza tu

    23. #160
      Tangawizi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th June 2009
      Posts : 943
      Rep Power : 692
      Likes Received
      188
      Likes Given
      184

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Jinsi operation nzima ilivyoendeshwa inaonyesha wazi uwezo mdogo wa kimkakati wa vyombo vilivyohusika. Haina shaka nia ilikuwa ni kuua. Lakini Mungu mkubwa jamaa hajafanya. aibu yao aibu yetu,lol! Ushaona wapi mtu anaporwa vile bila kuhusika kwa vyombo vya dola?
      "Carpe Diem...Seize the Day"

    24. Miaka 50
    Page 8 of 17 FirstFirst ... 678910 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...