Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

    Report Post
    Page 14 of 17 FirstFirst ... 41213141516 ... LastLast
    Results 261 to 280 of 332
    1. #1
      Gambas's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2011
      Location : Malimbe, Nyegezi Mwanza
      Posts : 955
      Rep Power : 2449
      Likes Received
      191
      Likes Given
      17

      Default UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      "NI saa 12:45 asubuhi, bado kiza kimetanda katika eneo hili la Msitu wa Mabwepande. Mbele yangu namwona mtu akiwa amekaa chini, pembeni ya barabara akiwa amelowa damu mwili mzima.

      "Ninapomkaribia nasikia sauti ya mtu huyo ikisema kwa taabu; naomba msaada jamani… naomba msaada jamani", hivi ndivyo anavyoanza kusimulia Juma Mgaza Abdallah, mtu wa kwanza kumwona Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka baada ya kutekwa, kupigwa na kutupwa katika Msitu wa Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

      Abdallah, anasema mara baada kumwona daktari huyo akiwa katika hali hiyo, alijaribu kumkokota kumtoa eneo hilo, lakini alishindwa kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo.

      Baada ya hapo, aliamua kusubiri mtu mwingine apite eneo hilo ili amwombe wasaidiane kumpeleka Kituo cha Polisi Bunju.

      Anasema muda mfupi baadaye aliona gari likija mbele yao, akalinyooshea mkono kulisimamisha. Liliposimama, akamweleza dereva hali aliyokuwa nayo Dk Ulimboka na kwamba anahitaji msaada wa haraka.

      Abdallah ambaye hadi wakati huo alikuwa hamfahamu mtu ambaye alikuwa akimsadia kuwa ni kiongozi wa madaktari kutokana na sura yake kuvimba, anasema walimwingiza katika gari hilo na kumpeleka Kituo Kidogo cha Polisi Bunju.

      Anasema, Dk Ulimboka wakati huo alikuwa akiendelea kuvuja damu katika baadhi ya majeraha yake huku akiwa hana suruali na kubaki na bukta tu, huku akizungumza kwa taabu.

      Kituo cha Polisi Bunju

      Baada ya kumfikisha kituoni hapo, walitoa maelezo namna walivyomwokota na kumsaidia kumfikisha hapo.

      Polisi baada kumhoji Dk Ulimboka, aliwatajia namba ya simu ya rafiki yake aitwaye Dk Deo. Walipompigia na kumweleza tatizo hilo, aliamua moja kwa moja kwenda Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kutoa taarifa hizo na hatimaye kuandamana na watu kadhaa kutoka hapo akiwamo Mkurugenzi wake, Hellen-Kijo Bisimba.

      Wawasili kituoni
      Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania wa kituo hicho, Onesmo Olengurumwa, anasema waliwafika Polisi Bunju saa 3:36 asubuhi na kumkuta Dk Ulimboka akiwa amekalishwa kwenye benchi huku damu ikiwa imeganda kwenye majeraha mwilini.

      Olengurumwa anasema waliwahoji polisi waliokuwa kituoni hapo kwa nini wakae na mtu aliyeumia kiasi hicho muda mrefu bila ya kuita gari la wagonjwa kumchukua ili kuwahi kupatiwa matibabu.

      Olengurumwa anasema polisi walisema kwamba, walikuwa wanawasubiri ndugu zake wafike.

      Baada ya muda mfupi, akiwa ameingizwa kwenye gari kupelekwa hospitali, Dk Ulimboka aliomba maji ya kunywa akisema ana kiu sana, lakini alipopewa, alikunywa kidogo akashindwa.

      Anasema wakiwa njiani, alikuwa akilalamika kuwa anasikika maumivu makali huku akisisitiza kuwa tukio la kutekwa na kupigwa lilikuwa la kumuua.

      "Jamani hawa watu walitaka kuniua walikuwa wamepanga kuniua," alisikika mara kwa mara akisema Dk Ulimboka wakati anapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu.

      Maelezo ya Dk Ulimboka
      Baada ya Dk Ulimboka kuokotwa aliweza kuzungumza na kurekodiwa muda mfupi baada ya kutolewa msituni na mazungumzo yake yalikuwa hivi;

      “Nilikamatwa na watu hao usiku wa Jumanne nikiwa maeneo ya Leaders Club, Kinondoni na daktari mwenzangu baada ya kupigiwa simu na mtu mmoja ambaye alidai kuwa anafanya kazi Ikulu.

      “Kuna jamaa mmoja anafanya kazi Ikulu, kama siku tatu mfululizo alikuwa akitaka kukutana na mimi ila nilishindwa kukutana naye kwa kuwa nilikuwa na kazi nyingi na wakati mwingine mpaka usiku,” alisema Dk Ulimboka.

      Huku akizungumza kwa taabu kutokana na mdomo wake kuvimba, alisema siku hiyo mtu huyo alimpigia tena simu na kumtaka wakutane.

      “Jana (Jumanne) alinipigia simu na nikamwambia daktari mwenzangu twende tukaonane naye, wakati huo alitueleza kuwa alikuwa maeneo ya Kinondoni Stereo,” alisema Ulimboka na kuongeza:

      “Tulipofika maeneo hayo tukampigia simu na akatueleza kuwa alikwisha ondoka, baadaye tukamweleza sehemu tulipo mimi pamoja na mwenzangu.”

      Alisema kuwa, wakati anakutana na mtu yule maeneo ya Leaders Club, hakuwa na amani.

      “Kwa kweli siku ile nilivyoonana na mtu yule sikuwa na amani kabisa ya kukaa eneo lile,” alisema Dk Ulimboka.

      Alisema kuwa wakati wakiendelea na maongezi ya kawaida, bado aliendelea kuwa na mashaka na mtu yule.

      “Katikati ya maongezi nikaona ameanza kuzungumza na simu, kila tukitaka kuagana alikuwa akizungumza na simu, sijui nini kilikuwa kinachelewesha sisi kuagana,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza:

      “Ghafla walitokea watu kama watano na kusema kuwa hawana tatizo na mtu yeyote katika eneo hilo isipokuwa mimi.

      Wakati sijakaa sawa, waliniburuza hadi barabara ya lami kwa kuwa eneo hilo lilikuwa karibu na barabara.”

      Aliongeza, “Nilipowauliza wananipeleka wapi, wakaniambia kuwa mimi nasumbua sana na nitajua hukohuko, waliniingiza katika gari jeusi, lakini halikuwa na namba. Niliwauliza kosa gani nimefanya? Hawakunijibu kitu na kusema, we twende utajua hukohuko.’’

      Alisema alipokuwa ndani ya gari hilo watu hao walimpiga na kwamba walipofika maeneo ya Victoria, walichukua sweta nyeusi na kumfunga usoni, jambo lililomfanya ashindwe kuona kinachoendelea ikiwa ni pamoja na alikokuwa akipelekwa.

      “Walinipiga mateke ya mbavuni, wakati mwingine walitumia vitako vya bunduki, kila nilipokuwa najaribu kuangalia ninapokwenda nilishindwa,” alisimulia Dk Ulimboka.

      Alisema kuwa watu hao walimpeleka katika nyumba moja ambayo hakujua iko sehemu gani ambapo walimshusha na kuanza kumshambulia kwa mateke mfululizo kila sehemu ya mwili. Wakati huo, wote walimshinikiza awaambie nani yupo nyuma ya mgomo wa
      madaktari.

      “Tangu saa sita usiku mpaka saa 9:00 alfajiri walikuwa wananipiga tu, kuna wakati nilijaribu kukimbia wakapiga risasi juu nikasimama na sikuweza kukimbia tena,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza:

      “Nilisimama, wakaendelea kunipiga, niliwasikia wakisema ama wanichome sindano ya sumu nife au kunikanyaga na gari. Baadaye wakaanza kuning’oa meno na kucha kwa kolea huku wakinilazimisha kusema nani yupo nyuma ya mgomo wa madaktari."

      Alisema kuwa, watu hao walikuwa na bunduki kubwa ambayo hakuweza kuitambua ni aina gani.

      “Waliniambia kuwa ninajua ninachokifanya hivyo wanaweza kunichoma sindano ya sumu nife au wanikanyage na gari nife,” alisimulia.

      Dk Ulimboka alisema kuwa awali hakuwa na shaka na watu hao kwa kuwa alidhani ni polisi, lakini baadaye alishindwa kuwaelewa kwani watu hao walimchanganya.

      “Sikuweza kuwatambua ila naweza kusema ni askari, walipokuwa wananipeleka niliwauliza mnanipeleka wapi na wakati huo nilikuwa sioni mbele ila ilikuwa kama maeneo ya Mwenge hivi,” alisema Dk Ulimboka.

      Alisema kuwa baadaye alipoteza fahamu na hakuweza kuona chochote zaidi ya kusikia sauti za watu hao kwa mbali.

      “Nilikuwa sioni na nilipoteza fahamu nikawa nasikia tu wakinibeba, gari lilitembea muda mrefu, sikujua ni wapi tunakwenda, kumbe ndio huko Mabwepande,” alisema.

      Alisema kuwa walifika maeneo ya barabara ya vumbi na baadaye wakamshusha na kumbeba hadi msituni.

      “Waliniburuza na kuniacha huko na muda wa saa kumi alfajiri ndipo nikazinduka na kuanza kujiburuza kuelekea barabarani ambako nilisaidiwa na mtu mmoja ambaye simtambui,” alisema Dk Ulimboka.

    2. Miaka 50

    3. #261
      Malaria Sugu's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 2nd August 2009
      Posts : 1,783
      Rep Power : 0
      Likes Received
      246
      Likes Given
      18

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Kaka Masoud Kipanya ametuchorea katuni juzi kutuambia "Filamu ya Mv Skagit imesitishwa tunarejea kwenye filamu ya Ulimboka". Leo Mwanahalisi limeibuka tena na filamu hiyo, Tanzania Daima nalo linadai SIRI IMETOBOLEWA nimelinunua kutaka kujua ukweli hiyo siri nimeitafuta hadi kwa tochi sijaiona zaidi ya kuambulia maelezo ya OC CID wa Kawe kuwa amekiambia chanzo cha gazeti "yeye hahusiki kabisa na hakuwepo ofisini siku ya tukio" nimejiuliza sasa hiyo ndio siri iliyotobolewa? Media zetu bana zina weledi dhaifu mno katika tasnia ya habari na uandishi huu wa kizushi ndio umemfikisha Joshua Arap Sang wa Kenya THE HAGUE akitakiwa kujibu shtaka la uchochezi na mauaji. Mwanahalisi na wengine mjifunze katika hilo. Ukasuku wenu utawatokea puani siku moja

    4. #262
      Malaria Sugu's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 2nd August 2009
      Posts : 1,783
      Rep Power : 0
      Likes Received
      246
      Likes Given
      18

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Kubenea anatuchukulia sisi kama wajinga tusiyejua jana kaandika nini na leo nini mbaya zaidi haeleweki...

    5. #263
      Mwanajamii's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th March 2008
      Posts : 7,085
      Rep Power : 1809
      Likes Received
      24
      Likes Given
      13

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Tukiendelea kumsemea ulimboka huku kila mmoja anasema anawasiliana naye tutataja hata watu ambao hawahusiki

    6. #264
      SJUMAA26's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th January 2012
      Posts : 327
      Rep Power : 622
      Likes Received
      69
      Likes Given
      2

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By tamuchungu
      Kaka Masoud Kipanya ametuchorea katuni juzi kutuambia "Filamu ya Mv Skagit imesitishwa tunarejea kwenye filamu ya Ulimboka". Leo Mwanahalisi limeibuka tena na filamu hiyo, Tanzania Daima nalo linadai SIRI IMETOBOLEWA nimelinunua kutaka kujua ukweli hiyo siri nimeitafuta hadi kwa tochi sijaiona zaidi ya kuambulia maelezo ya OC CID wa Kawe kuwa amekiambia chanzo cha gazeti "yeye hahusiki kabisa na hakuwepo ofisini siku ya tukio" nimejiuliza sasa hiyo ndio siri iliyotobolewa? Media zetu bana zina weledi dhaifu mno katika tasnia ya habari na uandishi huu wa kizushi ndio umemfikisha Joshua Arap Sang wa Kenya THE HAGUE akitakiwa kujibu shtaka la uchochezi na mauaji. Mwanahalisi na wengine mjifunze katika hilo. Ukasuku wenu utawatokea puani siku moja
      Ume-post sana leo hasa baada ya aibu hii kufichuliwa na Mwanahalisi. Hivi unadhani kwa maneno yako hapa utaweza kuuficha huo ukweli? Kama hao waliotajwa wameonewa kwanini wasiende kushitaki mahakamani? Nadhani na wewe ni mmoja wao, sasa nenda kashitaki usitujazie threads kwa upuuzi wako hata kama Nepi imekulipa posho sisi hatutaki kusikia ujinga wako! Ni aibu ya mwaka, serikali ya m.k.w.e.r.e ni kama chizi aliyepotea njia! Mngekuwa Kenya ninyi sasa hivi mngekuwa mifupa tu ikiozea makaburini! Shwaini!
      bob giza likes this.

    7. #265
      kiraia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2007
      Location : Kowamrasa
      Posts : 647
      Rep Power : 717
      Likes Received
      83
      Likes Given
      476

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Hivi Mkampuni ya simu huwa hawaweki record ya sauti kama wanavyofanya kwenye msg?
      The most dangareous position in which to sleep is with your feet on your office desk.

    8. FemaTV & Radio

    9. #266
      tabu kuishi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st June 2012
      Posts : 211
      Rep Power : 393
      Likes Received
      12
      Likes Given
      10

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Nasikia mmoja amevunjika kiuno kwa ajali yupo muhimbili madr wamemsusa anatibiwa na madr kutoka usalama wa taifa,jamani hii ni aibu kwa serikali kufanya tukio kama hili,halafu mbaya zaidi usalama wa siku hizi hakuna siri imeshavuja hiyo kuwa serikali imehusika isipokuwa Mungu ametaka awaumbue tu,siyo kila mtu ni rahisi kuuwawa kama wanavyofikiria, kila mtu anaMungu wake anayemuabudu,wasifikiri kuwa Mungu wao tu ndo anaweza kila jambo,aibu kwa jk,watamkumbuka sana shehe yahya.

      OLE WAKE AMTEGEMEAYE MWANADAMU KUWA KINGA YAKE

    10. #267
      Mimibaba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2009
      Posts : 3,166
      Rep Power : 1531
      Likes Received
      758
      Likes Given
      591

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By tamuchungu
      GAZETI MWANAHALISI NA FILAMU YA ULIMBOKA:

      Mwanzo gazeti hilo lilidai aliyemteka Ulimboka ni Ayubu wa Ikulu lina uhakika.
      Kisha likasema ni ACP Ahmed Msangi lina uhakika ndie alichukua wallet ya Dr.
      Baadae likasema Dr amesisitiza ni Ikulu ndio ilimteka lina uhakika
      Leo linatuambia ni Ramadhani Ighondu wa TISS lina uhakika

      Wakuburuzwa tunangoja kesho liibuke na jipya si filamu inaendelea..........

      1. Ni kweli lakini hizo lead za hizo story mnawapa nyinyi yeye afanyeje?

      2. Yote kwa yote haindoi kuhusika kwa serikali kwenye sakata hili

      3. Zamu yako sasa kanusha kwa taarifa sahihi
      Ukweli utakuweka huru daima

    11. #268
      Chona's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th March 2010
      Posts : 247
      Rep Power : 517
      Likes Received
      79
      Likes Given
      42

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By tamuchungu
      naamini ilo gazeti limenunuliwa na maadui wa serikali ya awamu ya nne. Ili kuichafu kisha wakidhani uyo alie wanunua atashinda ccm awe rais wa nchi limepoteza dira gazeti hili
      Quote By tamuchungu
      Gazeti la Mwanahalisi toleo la leo limeniacha hoi linadai anayehusika kumteka Dr Ulimboka ni Ramadhani Ighulo afisa usalama wa taifa likatoa na ushahidi wakati KAMANDA SULEMANI KOVA alishatuletea mtuhumiwa ambaye ni raia wa kenya JOSHUA tumwamini nani katika sakata hili?
      ...................akili za mbayuwayu changanya na za kwako......................... ................

      Quote By tamuchungu
      GAZETI MWANAHALISI NA FILAMU YA ULIMBOKA:

      Mwanzo gazeti hilo lilidai aliyemteka Ulimboka ni Ayubu wa Ikulu lina uhakika.
      Kisha likasema ni ACP Ahmed Msangi lina uhakika ndie alichukua wallet ya Dr.
      Baadae likasema Dr amesisitiza ni Ikulu ndio ilimteka lina uhakika
      Leo linatuambia ni Ramadhani Ighondu wa TISS lina uhakika

      Wakuburuzwa tunangoja kesho liibuke na jipya si filamu inaendelea..........

      Quote By tamuchungu
      Mwanahalisi hawamjui yeyote aliyehusika wamekazana kupotosha umma na kutaja taja majina ya watu hovyo wakijifanya wanauhakika na habari zao kumbe kanya boya tu
      Quote By tamuchungu
      Kaka Masoud Kipanya ametuchorea katuni juzi kutuambia "Filamu ya Mv Skagit imesitishwa tunarejea kwenye filamu ya Ulimboka". Leo Mwanahalisi limeibuka tena na filamu hiyo, Tanzania Daima nalo linadai SIRI IMETOBOLEWA nimelinunua kutaka kujua ukweli hiyo siri nimeitafuta hadi kwa tochi sijaiona zaidi ya kuambulia maelezo ya OC CID wa Kawe kuwa amekiambia chanzo cha gazeti "yeye hahusiki kabisa na hakuwepo ofisini siku ya tukio" nimejiuliza sasa hiyo ndio siri iliyotobolewa? Media zetu bana zina weledi dhaifu mno katika tasnia ya habari na uandishi huu wa kizushi ndio umemfikisha Joshua Arap Sang wa Kenya THE HAGUE akitakiwa kujibu shtaka la uchochezi na mauaji. Mwanahalisi na wengine mjifunze katika hilo. Ukasuku wenu utawatokea puani siku moja
      Quote By tamuchungu
      Kubenea anatuchukulia sisi kama wajinga tusiyejua jana kaandika nini na leo nini mbaya zaidi haeleweki...
      Ndugu mbona unaonesha kustushwa sana na habari hii? Kiasi kwamba umelazimika kupost tread nyingi bila sababu. Tulia, fanya uchambuzi na wewe umpinge kwa hoja. Jipange na ukosoe pale unapodhani kapotosha. Kwa porojo hizi huwezi kueleweka!! Au nawe unahusika?

    12. #269
      tabu kuishi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st June 2012
      Posts : 211
      Rep Power : 393
      Likes Received
      12
      Likes Given
      10

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By tamuchungu
      Kubenea anatuchukulia sisi kama wajinga tusiyejua jana kaandika nini na leo nini mbaya zaidi haeleweki...
      Kwani kakulazimisha kusoma gazeti lake acha soma ya siiiiiiiisiiiiiiiiieeeeeeeeeem uuuuuuuuuuu yenye habari nzuri za kikubwa

    13. #270
      Bams's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th October 2010
      Posts : 829
      Rep Power : 601
      Likes Received
      333
      Likes Given
      9

      Default

      Quote By tamuchungu
      Kaka Masoud Kipanya ametuchorea katuni juzi kutuambia "Filamu ya Mv Skagit imesitishwa tunarejea kwenye filamu ya Ulimboka". Leo Mwanahalisi limeibuka tena na filamu hiyo, Tanzania Daima nalo linadai SIRI IMETOBOLEWA nimelinunua kutaka kujua ukweli hiyo siri nimeitafuta hadi kwa tochi sijaiona zaidi ya kuambulia maelezo ya OC CID wa Kawe kuwa amekiambia chanzo cha gazeti "yeye hahusiki kabisa na hakuwepo ofisini siku ya tukio" nimejiuliza sasa hiyo ndio siri iliyotobolewa? Media zetu bana zina weledi dhaifu mno katika tasnia ya habari na uandishi huu wa kizushi ndio umemfikisha Joshua Arap Sang wa Kenya THE HAGUE akitakiwa kujibu shtaka la uchochezi na mauaji. Mwanahalisi na wengine mjifunze katika hilo. Ukasuku wenu utawatokea puani siku moja
      Wewe nawe ulikujaje humu JF? Mbona upeo ni kama mdogo mno? Suala la Ulimboka linahitaji uchunguzi, na kila yapatikanapo maendeleo ya kumfikia mhusika/wahusika wakuu, ni sahihi kabisa kuweka taarifa hiyo. Taarifa ya MWANAHALISI ni maendeleo ya uchunguzi. Leo wamefikia kwa Rama, kama kesho watakuwa wamepata habari ya nyongeza kuwa Mkuchika alihusika ni sahihi kuiweka, na keshokutwa wakipata uhakika kuwa Mkuchika alipata maelekezo toka kwa JK, wataweka pia, mwenye akili hatawezi kusema, mbona juzi mlisema mhusika ni Rama, sasa imekuwaje tena mnasema mhusika ni JK.
      kibogo likes this.

    14. #271
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,577
      Rep Power : 16764
      Likes Received
      2481
      Likes Given
      1846

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Hili sakata limeibuka tena?

    15. #272
      Bams's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th October 2010
      Posts : 829
      Rep Power : 601
      Likes Received
      333
      Likes Given
      9

      Default

      Quote By tabu kuishi
      Kwani kakulazimisha kusoma gazeti lake acha soma ya siiiiiiiisiiiiiiiiieeeeeeeeeem uuuuuuuuuuu yenye habari nzuri za kikubwa
      Habari ya Mwanahalisi inaeleweka sana kwa kila anayejua kusoma na mwenye akili. Kama mtu haelewi, hiyo itakuwa nI KUTOKANA Na upeo mdogo wa kusoma na kuelewa wa msomaji.HONGERA SANA KUBENEA KWA TAARIFA ZA KIUCHUNGUZI. Kubenea ni mfano mzuri kwa waandishi wengine wanaopenda kuandika habari za kiuchunguzi. BRAVO KUBENEA.
      kibogo likes this.

    16. #273
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2884
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Yule alotajwa leo na Kubenea?????

    17. #274
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2884
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By tamuchungu
      Kaka Masoud Kipanya ametuchorea katuni juzi kutuambia "Filamu ya Mv Skagit imesitishwa tunarejea kwenye filamu ya Ulimboka". Leo Mwanahalisi limeibuka tena na filamu hiyo, Tanzania Daima nalo linadai SIRI IMETOBOLEWA nimelinunua kutaka kujua ukweli hiyo siri nimeitafuta hadi kwa tochi sijaiona zaidi ya kuambulia maelezo ya OC CID wa Kawe kuwa amekiambia chanzo cha gazeti "yeye hahusiki kabisa na hakuwepo ofisini siku ya tukio" nimejiuliza sasa hiyo ndio siri iliyotobolewa? Media zetu bana zina weledi dhaifu mno katika tasnia ya habari na uandishi huu wa kizushi ndio umemfikisha Joshua Arap Sang wa Kenya THE HAGUE akitakiwa kujibu shtaka la uchochezi na mauaji. Mwanahalisi na wengine mjifunze katika hilo. Ukasuku wenu utawatokea puani siku moja
      tanzania daima maelezo si wameyatoa hapa?????labda kwakua wengine hawajui

    18. #275
      manucho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Posts : 561
      Rep Power : 469
      Likes Received
      79
      Likes Given
      0

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Watawala wamefika ukingoni, kilichobaki ni VITA tu! Kila mtawala ni Rais ndani ya kichwa chake hakuna anayetaka kuambiwa/kushindwa kwa hiyo atakayekosa lazima aharibu kwa mwenzake matokeo yake vita ni vita mura, haikwepeki.

    19. #276
      kibogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Location : MBEYA
      Posts : 1,693
      Rep Power : 695
      Likes Received
      422
      Likes Given
      320

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By tamuchungu
      naamini ilo gazeti limenunuliwa na maadui wa serikali ya awamu ya nne. Ili kuichafu kisha wakidhani uyo alie wanunua atashinda ccm awe rais wa nchi limepoteza dira gazeti hili
      We unatakiwa usome habari yote ya gazeti sio kwa sababu ya umagamba wako unasoma vichwa vya habari tu na kuanza kutoa maneno kama hayo. Hiyo habari ina ukweli ndani yake ili kupinga hilo tunataka huyo aliyetakwa (Rama AKA Abedi na bosi wake Zoka wakanushe sio wewe tamuchungu au kama wewe ndio hao niliowataja kanusha kwa kufuata kila kipengere kinavyojieleza.

    20. #277
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2884
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By Bams
      Wewe nawe ulikujaje humu JF? Mbona upeo ni kama mdogo mno? Suala la Ulimboka linahitaji uchunguzi, na kila yapatikanapo maendeleo ya kumfikia mhusika/wahusika wakuu, ni sahihi kabisa kuweka taarifa hiyo. Taarifa ya MWANAHALISI ni maendeleo ya uchunguzi. Leo wamefikia kwa Rama, kama kesho watakuwa wamepata habari ya nyongeza kuwa Mkuchika alihusika ni sahihi kuiweka, na keshokutwa wakipata uhakika kuwa Mkuchika alipata maelekezo toka kwa JK, wataweka pia, mwenye akili hatawezi kusema, mbona juzi mlisema mhusika ni Rama, sasa imekuwaje tena mnasema mhusika ni JK.
      okay,umeelezea kiufasaha,hata tuloishia kanumba primary

    21. #278
      Ndukidi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Posts : 372
      Rep Power : 575
      Likes Received
      141
      Likes Given
      327

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By Chona
      Ndugu mbona unaonesha kustushwa sana na habari hii? Kiasi kwamba umelazimika kupost tread nyingi bila sababu. Tulia, fanya uchambuzi na wewe umpinge kwa hoja. Jipange na ukosoe pale unapodhani kapotosha. Kwa porojo hizi huwezi kueleweka!! Au nawe unahusika?
      Inaonekana tamuchungu imekuwa chungu tu, hawezi kumeza, si unajua ukiguswa!!

    22. #279
      Kiherehere's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 1,074
      Rep Power : 648
      Likes Received
      71
      Likes Given
      132

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By rais wa tano
      Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni 2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma hivi sasa katika Hospitali. Imebainika kwamba utoaji huduma umeathirika kutokana na mgomo wa baadhi ya madaktari unaondelea kwa takriban wiki moja sasa tangu ulipoanza Jumamosi yatarehe 23 Juni 2012.

      Baada ya tathmini hiyo, Bodi ya Wadhamini imeagiza yafuatayo:

      (i) Madaktari waliopo kazini waendelee na kazi kama kawaida;
      (ii) Madaktari waliogoma warejee kazini kutii amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha kazi, kwa mujibu wa Kifungu Na. 76 (1) na (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.
      (iii) Madaktari waliopo likizo warejee kazini mara moja. Utaratibu wa kufidia likizo na nauli zao umeandaliwa.
      (iv) Uongozi wa Hospitali uwachukulie hatua za kinidhamu wafanyakazi wote watakaoendelea kutokuhudhuria kazini na kufanya kazi bila sababu za msingi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za kazi;
      (v) Uongozi wa Hospitali ufute mara moja ‘rotations’ za Madaktari waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo (interns); na
      (vi) Uongozi wa Hospitali uwapange (re-deploy) Madaktari na Madaktari Bingwa waliopo kwenye maeneo yaliyoathirika wakati huu wa mgomo.

      Aidha, Bodi ya Wadhamini inawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote ambao wameendelea kuwahudumia wagonjwa wetu na wananchi kwa ujumla. Vilevile, Bodi ya Wadhamini inawasihi madaktari na wafanyakazi wote wawe na subira na waheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo pamoja na maadili ya taaluma zao.

      _________________
      Dkt. Gabriel Upunda
      KAIMU MWENYEKITI
      BODI YA WADHAMINI
      waheshimu sheria??? nyie mnaziheshimu??
      CONFIDENCE IS WHAT AM LOOKING FOR.... NOT HAPPINESS

    23. #280
      kibogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Location : MBEYA
      Posts : 1,693
      Rep Power : 695
      Likes Received
      422
      Likes Given
      320

      Default Re: UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

      Quote By Katavi
      Hili sakata limeibuka tena?
      Kwani lilikuwa limekwisha? tulikuwa kwenye maombolezo, halitaisha hadi pale wahusika watakapokuwa wamehukumiwa kama sio na Mahakama basi Mungu atatusaidia kutoa hukumu kwani malipo Duniani (Hitler, Idd Amini, Bokasa na wengineo wengi tu wakowapi?)

    Page 14 of 17 FirstFirst ... 41213141516 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...