Kwa niaba ya Chama changu makini CCM naomba kuwataka radhi Wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano mliokesha usku kucha kusubiri hotuba ya Mpendwa Rais wetu Mh Jakaya bila mafanikio hivyo naomba mtusamehe kwa uzembe uliofanywa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kwa kutokutoa Tangazo la Mh Kuhairisha kuhutubia Taifa siku ya tararehe 30/06/2012.
Kwa sisi wananchi na wapenzi makini wa Chama cha mapinduzi tunaona kuna uzembe wa hali ya juu uliofanywa na wasaidizi wa Rais na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kutokana na sakata hili ambalo hadi kufikia sasa bado wahajatoa kauli kwa vyombo vya habari ya kuhairishwa kwa hotuba ya Rais.
Kutokana na Rais kushindwa kuhutubia Taifa hapo jana baada ya Taarifa kuwa zimetolewa na Vyombo vya habari Wananchi wapo katika taharuki kubwa kwani hawajui kitu kinachoendelea na kitu kilichompata Rais Wetu hadi kufikia kushindwa kuhutubia Taifa.
Kwasasa Tunaitaka Kurugenzi ya Mawasilino Ikulu kuwajibika kwa kuupotosha Umma juu ya jambo hili nyeti kwa Taifa na aidha tunawataka kutoa tamko kwa vyombo vya habari na kuwaomba radhi wananchi wote waliokesha ucku kucha kusubiri hotuba ya Mpendwa wao Rais na kupelekea wengine kushindwa kwenda kwenye Ibada siku leo.

Reply With Quote

Follow Us Here