Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

    Report Post
    Page 11 of 12 FirstFirst ... 9101112 LastLast
    Results 201 to 220 of 227
    1. #1
      Chal's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th October 2010
      Posts : 113
      Rep Power : 459
      Likes Received
      45
      Likes Given
      4

      Default Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Kwa maneno uake Dr ULIMBOKA ametoa kauli ya kishujaa na kutia shime na hamasa katika mapambano yanayoendelea ya kudai haki katika kuboresha huduma za afya na maslahi ya madaktari

      "Naelekea nje ya nchi kwa matibabu, nawasihi madaktari wenzangu wanaobaki waendelee ma mapambano ya kudai haki ambayo kimsingi bado haijapatikana, nawaomba damu yangu iliyomwagika ikawe chachu na hamasa katika harakati hizi za kudai haki, asanteni sana"

      Source: ITV HABARI
      BAK, alex50, Tuandamane and 15 others like this.

    2. FemaTV & Radio

    3. #201
      namshitu kazeni's Avatar
      Member Array
      Join Date : 31st January 2012
      Posts : 18
      Rep Power : 372
      Likes Received
      0
      Likes Given
      30

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      poignant!

    4. #202
      namshitu kazeni's Avatar
      Member Array
      Join Date : 31st January 2012
      Posts : 18
      Rep Power : 372
      Likes Received
      0
      Likes Given
      30

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      vifaa tiba, jifunze kiswahili na usiwe na jazba! ndio mambo yanayozungumzwa vitendea kazi vya watumishi wa afya vi wapi? magonjwa ya TB, HIV na Hepatitis yanakabiliwaje wodini, kulala chini kunashughulikiwaje, watendaji wako wa kutosha. TAFAKARI

    5. #203
      namshitu kazeni's Avatar
      Member Array
      Join Date : 31st January 2012
      Posts : 18
      Rep Power : 372
      Likes Received
      0
      Likes Given
      30

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      The health providers at all levels need better support to work in a patient and provider friendly environment, their personal benefits are secondary. It is true Tanzania is vast all can not be done unilaterally at the same one time but can we not have an action plan that covers zones and make sure the zone is up to scratch before we move on to the next. A mutually agreed upon time line was what I expected of the mutual meetings that seem to have broken

    6. #204
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Quote By reformer
      Zile hadithi zako zote mbili nimezipitia nikazijibu..my last question was; when and how many successful heart surgery have been done in ZT. Support your information with a reliable reference. Unajifanya hujaona?
      Ndugu yangu uko nje ya ulimwengu huu, soma:

      East and Central African Journal of Surgery, Vol. 15, No. 1, Mar-Apr, 2010, pp. 111-118
      Cardiac Surgery: One Year Experience of Cardiac Surgery at Muhimbili National Hospital, Dar es Salaam, Tanzania

      Results: A total of 105 cases of cardiac surgery were done 21% were male and 79% were females. Mean age was 19.4±12.3. The majority of cases were due to Rheumatic heart diseases (47.6%), congenital heart disease (35.2%), myxomatous valvular degeneration (16.2%) and pericardial disease 1%. Mitral valve disease was the commonest cause of cardiac disease (58.1%). Prolonged duration of aortic cross-clamp and total operation time were associated with prolonged intensive care stay and poor patients’ outcome respectively (p<0.05). While, ventricular dysfunction and total cardiopulmonary bypass time were not. The overall mortality rate was 13.3%. Majority of all death (64.3%) followed mitral valve repair.

      Source: Bioline International Official Site (site up-dated regularly)
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    7. #205
      Leornado's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th November 2010
      Location : Papua New Guinea
      Posts : 1,382
      Rep Power : 716
      Likes Received
      106
      Likes Given
      134

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Quote By Micro E coli
      We mwali acha kumdhalilisha DR Uli kwa maneno yako machafu ambayo huja ya dhibitisha njoo na fact hapo sio unalopoka lopoka vitendo vya kudhalilisha watu humu.
      hujatiwa vidole cku mingi nini? Sina haja ya kubishana na zumbu kama wewe huu mda unaotumia kujibishana na mie ungeshampikia mumeo saa nyingi...

    8. Miaka 50

    9. #206
      webondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Location : Chini ya mwembe
      Posts : 1,167
      Rep Power : 589
      Likes Received
      178
      Likes Given
      381

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Quote By TEGEMEA
      Vifaa hakuna wataalam watafanyeje kazi?Tanzania elimu ya sayansi iko chini sana.
      Hivi vifaa vimekosekana mwaka huu!!! It's well known kuwa vitendea kazi viko duni na mazingira pia hayajaboreshwa lakini sio sababu kubwa ya mgomo, doctors demand yao kubwa ni pesa ambazo kima cha chini ni 7.8 Milioni kwa mwezi. Ishu ya vitendea kazi na mazingira duni ni supportive measure kwao ili waonekane kwa wananchi kuwa madai yote ni ya msingi, nazidi kusikitika vifo vya watanzania vinavyoendelea kutokea.

    10. #207
      thereitis's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Location : Arusha
      Posts : 237
      Rep Power : 480
      Likes Received
      24
      Likes Given
      60

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Quote By zomba
      Mkikosa hoja mnaanza viroja. Kikwete kawaziba midomo.
      Kwa akili zako za kifisadi ni kweli kikwete kawaziba midomo. Tunajua wewe na hao watoto wa vigogo hamna shida kwa sababu mnatibiwa nje ya nchi. Zama za leo CCM yako haiwezi kudanganya watanzania. Wanatambua kuwa hakuna dawa ktk hospitali za umma kwa sababu ya udhaifu wa Chama chenu. Mnachoweza kufanya ni kutumia dola kunyamazisha wananchi wanapohoji serikali kushindwa kuwahudumia baada ya kukusanya kodi zao. Afadhali mkoloni kuliko Utawala wa CCM. Mkoloni alinyanyasa wananchi lakini alitoa huduma bora za afya.
      "Our party CCM, eventually became complacent, bureaucratic and corrupt. We had to change" Nyerere

    11. #208
      kijanaa's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 9th April 2010
      Posts : 3
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      1

      Post Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Ni kweli leo damu yake inaweza kutharauliwa na kuonekana kuwa imemwagika bure lakini ipo siku itasema kutoka katka aridhi kama ya Abel alie uliwa na kaka yake Kaini

    12. #209
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Quote By thereitis
      Kwa akili zako za kifisadi ni kweli kikwete kawaziba midomo. Tunajua wewe na hao watoto wa vigogo hamna shida kwa sababu mnatibiwa nje ya nchi. Zama za leo CCM yako haiwezi kudanganya watanzania. Wanatambua kuwa hakuna dawa ktk hospitali za umma kwa sababu ya udhaifu wa Chama chenu. Mnachoweza kufanya ni kutumia dola kunyamazisha wananchi wanapohoji serikali kushindwa kuwahudumia baada ya kukusanya kodi zao. Afadhali mkoloni kuliko Utawala wa CCM. Mkoloni alinyanyasa wananchi lakini alitoa huduma bora za afya.
      Hata Ulimboka anatibiwa nje ya nchi. Zitto umesahau? Mbowe unajuwa kaanza kwenda checkups UK mwaka gani?

      Ukiisoma hotuba ya Jakaya Mrisho Kikwete kwa umakini na vizuri, utaelewa kuwa ni haohao madaktari wanaogoma ndio wanatoa vibali vya watu kutibiwa nje. Soma vizuri.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    13. #210
      haki na usawa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 152
      Rep Power : 395
      Likes Received
      20
      Likes Given
      0

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Hivi kwanini watu wanaongelea mishahara tu ya madaktari? je madaktari hawakuorodhesha mahitaji ya vifaa? Mbona waziri mkuu hakusema miongoni mwa mambo ambayo serikali imeyatekeleza? mbona vifaa haikusema?Naomba muelewe kuwa kama ni mwandishi wa habari unategemea ukuu wa wilaya kwa hisani fuata yanayosemwa na serikali lakini kama unataka kutumia akili yako kwa manufaa ya wote sema kweli daima japo ukweli huo unaweza ukasababisha madhara kwako kwani ukweli utabaki milele na uongo hupotea na hutakumbukwa kwa uongo wako. Naomba semeni kweli mmesoma na ndiyo maana unaweza kuandika usilambe miguu ya watawala ukadhani siku zote utaishi nao kumbuka kwa Mola wako anahitaji HAKI na si uongo
      "NAOMBA MSIPENDE KUJIPENDEKEZA KWA WATAWALA KAMA WANGEFANYA HIVYO WALIOTUTANGULIA LEO HII TUSINGEKUWA HURU/TUSINGEPATA UHURU" VIBARAKA WASIOJIAMINI WAPO MAANA NA WAPO HASA WANAUME WASIOJIAMINI KULIKO WANAWAKE- MWANAMKE ANAWEZA KUWA IMARA KULIKO MWANAUME KATIKA KUSEMA UKWELI LAKINI MUNGU ALIMPA MAMLAKA MWANAMME NI VEMA KUTUMIA HEKIMA YAKO VIZURI KESHO (KABURINI/SIKU YA HUKUMU) UTAULIZWA NA MOLA WAKO KWA NEEMA ALIZOKUPA"

    14. #211
      Gilly's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th August 2009
      Posts : 68
      Rep Power : 511
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Gaudays
      Ziada ya kipato kukipata kupitia roho za watu huu ni ufreemasons,najiuliza kama mlikuwa hivyo mmefuata nini huko afya,iko wapi kujitolea kwenu kwa ajili ya afya zetu,politcs in profesionals is more harmful than expired medics,
      lol drs
      Kelele zote na matatizo yote ni tisa, kumi ni mfumo mbaya uliopo: wanasema siasa ni uporaji na mgawanyo wa madaraka katika nchi na uchumi ni uporaji na mgawanyo wa rasilmali katika nchi. Katika mfumo wa kibepari ambao sisi tuna ufuata, wanasiasa (waporaji wa madaraka) KAZI YAO NI KUWADHIBITI NA KUWALINDA wanaopora uchumi (au WAWEKEZAJI) wasituibie na wala wasiibiwe kwa kuwatoza kodi na kusimamia mgawanyo halali wa mapato.

      Short of that - hao watu hawatufai kabisa na Nyerere alishawaambia siku nyingi! "Good governance" gani ya kusimamia mikataba feki na sheria kandamizi zinazokataza wawekezaji wasilipe kodi? Eti kuwavutia wawekezaji?

      Kwani wanasema hawataki? Kama hawataki si waache tu tutafute wanaotaka? Tatizo jingine ni kwamba mwanasiasa HARUSIWI kuwa muwekezaji! Atashindwa kujidhibiti na kuwadhibiti wengine. Ataanguka vibaya katika vyote na anaweza kuhukumiwa na umma kwa usaliti kwa vile wana kula kiapo kuilinda Katiba.

      Hayo ndiyo matatizo wanayoyapata wanasiasa wetu kwa sasa. Wana "interests" za kiuchumi na hawawezi kusimamia uchumi wa nchi (uporaji na mgawanyo wa rasilmali za nchi) kwa faida ya nchi na kupelekea hata "almost" kuifutilia mbali Sekta ya Afya nchini.

      Tunaowategemea kuiendesha Sekta hiyo ni maDr ambao sasa wamegoma na wanafukuzwa ovyo haraka haraka. Na kama mgogoro huu utapelekeshwa kwa jazba na visasi kama ilivyo sasa Sekta ya Afya (na Wizara) yenyewe itabidi ikabidhiwe kwa wageni (mamluki) watuendeshee.

      Mimi sijui kama Katiba ya nchi inaruhusu. Kwani Serikali haijiulizi kwamba mchezo wanaofanya wao na maDr wao ni mauti kwetu? Kutuambia sisi tunaougua kwamba ni maDr ndiyo katili na wabinafsi Serikali haina fedha inatufaa nini sisi?

      Wakati tunaambiwa kuna fedha nyingi tu zimeibwa kifisadi na kujadiliwa Bungeni na wahusika wameachwa hivihivi? Mbona mnatuchanganya? Mnadhani tunasahau?

    15. BAK
      #212
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,597
      Rep Power : 44964
      Likes Received
      8345
      Likes Given
      8330

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Ulimboka apelekwa nje kutibiwa
      Sunday, 01 July 2012 08:12
      FEDHA ZA MATIBABU ZAPATIKANA,MADAKTARI WAKATAA MSAADA WA SERIKALI
      Geofrey Nyang’oro
      Mwananchi

      MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka amesafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.Kusafirishwa kwake kunafuatia hatua ya jopo la madaktari waliokuwa wakimhudumia, kueleza mabadiliko ya hali ya afya yake, yaliyosababisha figo kushindwa kufanya kazi, hali iliyolazimu pamoja na matibabu mengine, kwenda kusafishwa damu.

      Ingawa madaktari hao wamekataa kuweka wazi nchi anayopelekwa, kuna taarifa kwamba huenda amesafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini.

      Katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) jana makundi mbalimbali ya watu yalifurika wakiwamo wanaharakati na ndugu wa Dk Ulimboka, waliofika kwa lengo la kumsindikiza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

      Watu hao waliofika hospitalini hapo kuanzia asubuhi, waliendelea kubaki eneo hilo hadi saa 6:45 mchana msafara ulipoanza.

      Dk Ulimboka alisafirishwa kwa gari la kubebea wagonjwa la kampuni ya AAR. Alipofika uwanjani, alisafirishwa kwa ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini, akisindikizwa na watu watatu.

      Usiri safari ya Dk Ulimboka

      Mapema jana asubuhi, taarifa za kusafirishwa kwake zilizagaa, lakini hapakuwa na mtu wa kuthibitisha safari hiyo na namna atakavyosafiri.

      Katika safari hiyo, Dk Ulimboka amesindikizwa na Dk Pascal Lugajo, kaka yake, Dk Hobakile Ulimboka na mke wake, Dk Judith Mzovela.

      Madaktari watoa tamko

      Baada ya Ulimboka kusafirishwa, madaktari walilaani kitendo cha kutekwa na kupigwa mwenzao na kuitaka Serikali itoe tamko juu ya usalama wao.

      Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Edwan Chitage aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo na vitisho vya kufukuzwa kazi wanataaluma hao kunakofanywa na Serikali, kumezua hofu kwa madaktari wote nchini.

      “Tunaamini Serikali inawajibika kwa watu wake, kwa hali ilivyo sasa madaktari wapo kwenye hofu kubwa, tunataka itoe tamko juu ya usalama wa madaktari,” alisema Dk Chitage.

      Akizungumzia hali ya Dk Ulimboka, alisema imekuwa ikibadilika mara kwa mara hali ambayo imesababisha kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi .

      Chitage alisema kama Serikali ingekuwa na nia ya kuboresha huduma hospitalini hapo ingeweza kununua mashine ya CT Scan ambayo alisema bei yake ni sawa na Toyota ‘Shangingi’ moja.

      Kwa upande wao wanaharakati wa haki za binadamu, jana walifika Uwanja wa Ndege wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti wakilaani kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka.

      Dk Chitega alisema hadi kufikia jana, walikuwa wamepata fedha zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya matibabu yake. Juzi madaktari hao walisema wanahitaji Dola za Marekani 40,000 (Sh63.2 milioni) ili kumtibu mwenzao nje ya nchi.


      Serikali na tiba ya Ulimboka


      Wakati mgomo wa madaktari ukiingia siku ya nane leo, Serikali imesema ilikuwa tayari kugharimia matibabu ya Dk Ulimboka.

      Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja jana alisema Serikali ilikuwa tayari kugharimia matibabu ya daktari huyo.

      Mwamaja aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa ni haki ya mgonjwa anayepewa rufani ya kutibiwa nje, kugharimiwa na Serikali, lakini
      msaada huo wa Serikali ulikataliwa na madaktari hao na kuitaka ikae mbali na matibabu ya kiongozi wao.

      “Sisi tulishaanza maandalizi ya kugharimia matibabu yake, lakini madaktari wenyewe walikataa msaada wa Serikali,” alisema Mwamwaja.

      Hali yazidi kuwa tete

      Kutokana na mgomo huo, uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi, umewatimua zaidi ya madaktari 80 walioko kwenye mafunzo kwa vitendo.

      Hadi kufikia juzi, madaktari 146 walikuwa wamefukuzwa kutokana na mgomo huo katika hospitali za Bugando na Sekou Toure mkoani Mwanza na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na ile ya Mkoa wa Dodoma.

      Mbeya

      Habari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya zinadai kwamba, baada ya uongozi wa hospitali hiyo kulazimika kuomba madaktari wengine kutoka hospitali za jijini Mbeya ili kuongeza nguvu, madaktari hao nao wameonekana kutoridhishwa na ombi hilo.

      Habari hizo zinasema kwamba, licha ya madaktari hao kupatikana na kwenda hospitalini hapo, walisikika wakilalamika kwamba wao hawapo tayari kufanya kazi sehemu yenye mgogoro na kwamba wao hawawezi kufanywa kama chambo kwa kuhofia usalama wao.

      Akizungumza kwa njia ya simu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk Eliuter Samky alikiri kuzidiwa na kusuasua kwa utoaji huduma kwa wagonjwa ambapo alisema kuwa hadi sasa huduma zinazotolewa ni zile za dharura pekee na zile za kawaida wagonjwa wanaambiwa waende Hospitali ya Mkoa.

      Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk Seif Mhina, alisema kwa sasa hali inaendelea vizuri kutokana na kujipanga vyema kukabiliana nayo, licha ya kuwa bado kuna tatizo la upungufu wa vitanda hivyo kusababisha wagonjwa kulala chini.

      Tanga

      Baadhi ya wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo, wameitaka Serikali kukaa pamoja na madaktari ili kumaliza tatizo hilo.

      Wamesema hali iliyofikia sasa ni mbaya hivyo ni busara pande hizo mbili kukaa meza moja kutatua mgogoro huo bila kujali nani kati yao amesababisha.

      Sakina Abdallah ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi ya Gallanis, alisema amesikitishwa na baadhi ya wanasiasa wanaoshabikia kutekwa Dk Ulimboka.

      “Binafsi hali inayoendelea ya mgomo wa madaktari inanihuzunisha sana kwani tunaoumia ni sisi wananchi tunaotibiwa katika hospitali hizi,” alisema Sakina.


      Godfrey Jambia ambaye ni majeruhi aliyelazwa katika hospitali hiyo, alisema Serikali inatakiwa kutatua madai ya madaktari hao ili kuwanusuru raia wasio na hatia.


      NCCR yaivaa Serikali

      Chama cha NCCR-Mageuzi kimesema Serikali ina maswali ya kujibu kutokana na kushindwa kutatua mgomo wa madaktari nchi nzima.

      Chama hicho kimesema Serikali haitakiwi kutumia nguvu ya dola kumaliza mgomo na kuitaka ifute kesi iliyofunguliwa mahakamani ili kukaa meza ya majadiliano na madaktari hao kwa kuwa raia wasio na hatia, wanapoteza maisha kwa kukosa matibabu.

      Akizungumza wakati akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama, James Mbatia, alisema hata kama suala hilo limefika mahakamani, bado linazungumzika kwa kuwa afya za Watanzania zinawahusu wote.

      “Hivi Serikali inashindwa kuliondoa jambo hilo mahakamani na kukaa meza moja na madaktari kumaliza tatizo hili..., katika hili lazima tuseme, yaani watu wanakufa tukae kimya, haiwezekani hata kidogo,” alisema Mbatia na kuongeza:

      “Ubabe hauwezi kuingizwa katika uhai wa Watanzania, kama majadiliano ya awali hayakufanikiwa basi wawekwe watu makini watakaosimamia majadiliano haya, hata wabunge wanaweza kusimamia suala hili, mgomo huu hauna itikadi za vyama unawahusu wananchi wote.”


      Habari Hii imeandaliwa na Fidelis Butahe, Claud Mshana, Dar, Burhani Yakub,Tanga na Godfrey Kahango, Mbeya
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    16. #213
      Micro E coli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2011
      Posts : 552
      Rep Power : 492
      Likes Received
      103
      Likes Given
      88

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Quote By zomba
      katika madai 12 ya madaktari lipi la madawa? Ukilionesha na wewe umelitaja hapa, ntajuwa kweli huna mtindio wa ubongo. Ukishindwa kulionesha, nikuiteje? Mnafik?
      nini maana ya kuboresha mazingira ya kazi unataka kila kitu utafuniwe tapeli wewe.

    17. #214
      samora10's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st July 2010
      Location : Kwa-Gude
      Posts : 3,252
      Rep Power : 1103
      Likes Received
      729
      Likes Given
      1163

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Quote By webondo
      Wapo watanzania wengi hadi muda huu wanakufa kwa kukosa huduma mahospitalini.
      We habari hizo umezitoa wapi? Serikali imesema hali ni shwari
      ''Mipango na Mikakati imekamilika na sasa tuko kwenye mchakato wa mazungumzo na wafadhili"- M Pinda

    18. #215
      Borakufa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th May 2011
      Location : Tohell
      Posts : 1,155
      Rep Power : 640
      Likes Received
      259
      Likes Given
      207

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Quote By Hans Roger Dibagula
      What about damu ya wagonjwa waliokufa kutokana na mgomo?
      Huu ni ubongo usiotaka kuangalia kiini cha tatizo bali madhara yake! Bange la mavi hili!


    19. #216
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Quote By Micro E coli
      nini maana ya kuboresha mazingira ya kazi unataka kila kitu utafuniwe tapeli wewe.
      12-1= 11. Haya tuambie hayo kumi na moja yaliyobaki ni yepi? halafu utajuwa tapeli ni nani.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    20. #217
      spiritual-thinker's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th March 2012
      Posts : 45
      Rep Power : 369
      Likes Received
      8
      Likes Given
      4

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Quote By Butola
      ...Ulimboka anaweza akawa Mpiganaji lakini katika hili kwa sababu anachopigania hakina sifa ya kumpa "ushujaa" kwa sababu amesimama upande wa "maslahi"tofauti na upande wa wananchi maskini wanaokufa sasa kwa kukosa matibabu waliokuwa wanayapata kwa sababu madaktari hawapo kazini....

      ....Kama angewakumbuka wananchi hawa japo kidogo basi angeungana nao hospitalini bila kupata huduma za Madaktari ili ayasikie machungu wanayoyapata,ila kwa kuwa hayupo tayari kuyaonja machungu hayo kwa sababu hayajali na anajali zaidi uahi wake,amsehindwa kuungana nao naye kukimbilia nje kwenye huduma nzuri zaidi,wananchi hawa maskini hawana pa kukimbia,huua ni Usaliti....

      ...Ndugu yangu,uhai haununuliwi,hawa wananchi maskini uhai wao hautarudi, machungu watakayoyapata ndugu zao wa karibu hayaelezeki,kushiriki kufanya hicho hakuweza kukufanya kuwa Shujaa bali kunakufanya kuwa Msaliti na Muuaji....
      Ndugu yangu umeongea mambo ya msingi sana ambayo baaadhi ya wanajamvi humu hawayaoni kabisa kiasi kwamba nachelea kuwaita great thinkers, kimsingi wanastahili kuitwa mashabiki.

      Maisha ya watu wanaokufa kamwe hayawezi kuwa ndio gharama ya madai ya maslahi ya madaktari. Najua serikali yetu ni dhaifu na imeshidwa kuboresha maisha ya watanzania wote (si madaktari pekee) lakini mtindo walioamua kutumia madaktari ni wa kuumiza wananchi ambao wanaodai wanawatetea.

      Hata Ulimboka ambaye leo petty thinkers wanamwita shujaa, baada ya kusomeshwa kwa jasho la walalahoi hakukumbuka kuwatumikia hata kidogo badala yake akaenda kwenye shughuli zenye maslahi mazuri kwake.Leo anasema anatetea wananchi, uzalendo huu kaanza lini??Huu hauwezi kuwa ushujaa, huu ni u binafsi tu.

      Siungi mkono mgomo wa madaktari wala serikali ya magamba
      Butola likes this.

    21. #218
      webondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Location : Chini ya mwembe
      Posts : 1,167
      Rep Power : 589
      Likes Received
      178
      Likes Given
      381

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Quote By samora10
      We habari hizo umezitoa wapi? Serikali imesema hali ni shwari
      Fuatilia utajua.

    22. #219
      meningitis's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2010
      Location : sewahaji
      Posts : 2,918
      Rep Power : 3207
      Likes Received
      1014
      Likes Given
      149

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      walichokiona serikali ni posho ya kuchunguza maiti tu na sio ununuzi wa ct scanner.hovyo sana!

    23. #220
      Pops's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 27th June 2012
      Posts : 1
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      3

      Default Re: Dr. Ulimboka: Damu yangu iliyomwagika ikawe chachu

      Haki itapatikana tu dr Uli tunakutakia kila la heri na kwa Imani yetu ushapona

    Page 11 of 12 FirstFirst ... 9101112 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...