Spika Makinda aache mara moja kulaghai Bunge na Watz kwa ujumla -- kwani wengi tuna uelewa wa mambo kuliko yeye -- hata hizi Kanuni za Bunge anazodai anazisimamia pia tunazifahamu. Anavungavunga tu katika kutoa tafsiri.
Naomba kumuuliza Spika Makinda hivi: Atueleze bila ya kumung'unya maneno lini suala la kupigwa kwa Dr Ulimboka lilifikishwa mahakamani?
Kinachofahamika ni kwamba kesi iliyo mahakamani ni ombi la Mwanasheria Mkuu wa serikali dhidi ya Chama cha Madaktari (MAT) kutaka mgomo wa madaktari utangazwe kuwa batili -- ombi ambalo Mahakama ilikubalia mara moja.
sasa Spika Makinda anapowakatalia Wabunge kuzungumzia suala la kupigwa Dr Ulimboka kwa kusema liko mahakamani -- atuambie ni mahakama ipi, na ni kesi namba ngapi. Labda wengi hatujui.
Mimi naona Spika huyu ni janga la kitaifa -- naona anachangia kwa kasi kulitumbukiza taifa katika farakano.

Reply With Quote



Follow Us Here