Thread hii inatofautiana na ile nyingine ya kuuliza kuhusu aliko Benedict Mutungirehi, aliyekuwa mbunge na sasa hatujui yuko wapi.
{http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...ia-wapi-3.html}
Nimeamua kuweka thread mpya ili wengi wajue chanzo cha matukio yale kwa faida ya historia.
Unajua hata wengi hawafahamu relation ya vijana wale wa Engineering (FOE) na kundi lililomtoa Mutungirehi pale stejini. Haya ni makundi mawili tofauti yaliyounganishwa na ile nia ya kumuondoa Mutungirehi.
Sakata ya Mutungirehi ilitokea mwishoni mwa October 1994, lakini ili uielewe vizuri inabidi uanze na matukio ya tangu April 1994 yaani miezi sita nyuma. Mimi nilikuwa namalizia first year pale Engineering na hivyo ninalikumbuka suala hili vizuri sana.
Kwa nini nianzie nyuma vile? Ni kwa sababu ninataka kuweka hisoria sawa kwani baadhi wanapotosha na wanajifanya siku hizi ni wapiganaji kwelikweli.
Tuanze sasa maelezo. Mwezi April 1994 nikiwa first Year pale FOE tulikuwa na somo linaitwa Engineering Mathematics ambayo ilikuwa inafundishwa na walimu toka Mathematics depertment. Wakati huo ndiyo amemaliza kufunidha topics ngumu kichizi kama vile divergence, curl na kadhalika.
Kisha yule lecture akatoa test ambayo ilikuwa ngumu haina mfano kwani mtu unafika mwisho wa time hujafanya swali hata moja. Lecture akatangaza kwamba muda wa paper umeisha. Mimi nilikuwa nachukua Civil Engineering nimekaa karibu na Bwana anaitwa Mziray. Mziray akaanzisha fujo kwa kumshika lecturer asikusanye zile paper.
Mziray simkumbuki jina lake la kwanza ila najua alimaliza Kibaha High School, May 1993, akaenda JKT Oljoro na akaja UDSM. Pale Kibaha alikuwa PCM na aliondoka na Dv. One Point 5 yaani ABB.
Kwa watu kama huyu kudhalilishwa kuibuka na zero kwenye Mathematics ilikuwa kejeli lakini ukweli ni kwamba test ilikuwa ni ngumu.
Fujo ya Mziray zikaungwa mkono na wengi tu. Yule mwalimu akarudi Maths Dept. na huko akashitaki kwa mkuu wake yaani Prof. Masenge kwamba kafanyiwa fujo na vijana wa Engineering.
Kumbuka ile test ndiyo ilikuwa ya mwisho wa mwaka. Si kama siku hizi nasikia wanasoma kwa semester, wakati ule test ile ilikuwa ya mwisho na kilichobaki ni tutorials chache kusubiri Unversity Exam. Vumilieni hadi mwisho maana hadi hapa hakuna connection yoyote na Mutungirehi.
Hivyo, Prof. Masenge akato quotion kwamba Mathematics dept haitafundisha tena Engineering students hadi wa-apologise. Engineering tukakataa kuapologise.
April ikaisha May ikaingia. May ndiyo ilikuwa mwezi wa University Exams. Tukafanya exams zingine lakini binafsi nilishapata dalili za kugoma kufanya Maths Exam. Hili niliambiwa na Marehemu Dr. Nzali ambaye nilienda kumfuata kuhusu ugonjwa wangu maana niliugua karibu niage dunia hivyo nikawa namtaarifu kuhusu unafuu wangu. Akaniambia nisijaribu kugoma.
Kesho yake ikafika yaani siku ya Mathematics Exam. Tukaingia madarasani lakini walimu hawakuleta mitihani. Wakati huo sheria ya chuo inasema kuwa zikipita nusu saa basi unaweza kutoka nje ya chumba cha mtihani na hakuna mwingine kuingia.
Nusu saa ikafika, tension ya wanafunzi ikaanza kupanda maana walimu hawakuja na hivyo tutaonekana first year wote hatukufanya paper na hivyo tumeji-ABSCOND.
Tukakubaliana kuwa tutoke nje tujadili cha kufanya. Sasa hapa ndipo vurugu ya kwanza ilipoanzia. Class representatives wetu ninaowakumbuka walikuwa zaidi ya watatu yaani Lugiko Mpelwa karungubare (Chemical Engineering), Sweke (Civil Engieer), Hussein Kitilinga (Electrical Engineer). Wengine nimewasahau.
Msiomjua Karungubare ni yule aliyegombea uenyekiti NCCR akapata kura moja na James Mbatia akashinda uenyekiti huo. Karungubare sasa hivi ni mwanachama mzuri tu wa CHADEMA.
Wakati tumekaa pale chini hawa ma-class reps wakaitwa kujadili kwa Dean of faculty. Kumbe huko kwa Dean tayari Prof Masenge yuko huko na yule lecturer aliyefanyiwa vurugu. Binafsi sijui walifikaje kule.
Pale chini tumeshajadili na kuamua kwamba sisi hatujagoma kufanya paper ila wao ndiyo wamekataa kuleta mtihani. Basi tukakaa tukiwa hatujui nini kitatokea. Mitihani huanza saa 3 lakini hadi wakati huo tayari ni saa 5 mchana.
Ikafika mahala kila mmoja akaamua kuchukua uamuzi wake. Wapo walioamua kuondoka na kwenda mabwenini. Wakaulizwa “hivi nyinyi mnaondoka mtihani ukiletwa si mtakuwa mme-DISCO”. Wakajibu “fanyeni mtakavyoamua”!
Wengine wakaamua kujiandaa na mtihani wa mchana au siku nyingine na hivyo wakabaki madarasani.
Ilipofika nadhani saa 5:30 kumbe yale mazungumzo ya Prof. Masenge, Clas reps na daen yamemalizika na hivyo Prof. Masenge na timu yake wakaamua kugawa paper ili mtihani uanze. Wakaenda madarasani wakawakuta wale ambao walitulia kujiandaa na subjects zingine. Prof. na wenzake hawakujua kuwa kulikuwa na mtawanyiko wakagawa paper na waliomo wakaanza mtihani.
Class reps wakaiona hali hii na waka-panic na kuja kwetu ambao tulikuwa nje. Ninayakumbuka vizuri maneno ya Karungubare kwamba “Jamani ingieni madarasani mkafanya paper maana tayari wenzetu wameshaana na zinasubiriwa tu dakika 30 milango ifungwe tusiingie tulioko nje”
Hapa ndipo likaanza sokomoko la mwaka. Binafsi nikataka kuhakikisha maneno ya Karungebare na ma-class reps wenzake. Tukaenda vyumba kadhaa. Kweli bwana wenzetu walikuwa wanafanya paper taratibu. Ingekuwa wote hatufanyi paper kwangu isingekuwa tatizo. Lakini tatizo ni pale baadhi walikuwa wanaifanya.
Nikapiga kelele na wenzangu kadhaa nikisema “Jamani, tufanye moja kati ya mawili, ama tuwatoe kwa nguvu hawa wanaofanya paper ama tuingie na sisi tufanye”.
Hakuna aliyejisumbua na huu ushauri wetu kwa sababu tulikuwa kama wanne tu kati ya kundi la watu zaidi ya 220. Nilipoona huu ni upuuzi nikatangaza “ni ujinga kusubiri na hivyo napanda ngazi kwenda kufanya paper nisije nikafukuzwa”. Nikaanza kupanda ngazi. Kumbe huyu Ladislaus Malima kanisikia na kuniona.
Akanifuata amefura ajabu na kunisukuma akisema “Unajua wewe unacheza na Maisha ya watu, wale walioondoka utawafanya nini, unataka wafukuzwe”. Mimi nikajibu bila kujua kauli yangu imevutia wengi, nikasema “Wamekwenda wapi, si tulikubaliana tusiondoke. Sasa na wewe unasemaje kuhusu wanaofanya mtihani na hujawazuia”. Malima nikamzidi hoja na tension ikawa inazidi.
Kumbe hata kundini mmojammoja akawa anachomoka na kwenda kufanya mtihani. Mimi pia nikapata nafasi nikaenda kufanya mtihani. Kumbe mtihani wenyewe ulikuwa mrahisi maana ndani ya dakika 30 nikawa nimeshanya maswali ambayo nimeshavuka passmark yaani 40%.
Kumbe wakati tunafanya, kule nje dakika 30 zikawa zimeshapita na wakakubaliana kwamba waingie kwa nguvu kwenye vyumba vya mitihani, huko watatukuta sisi ambao kuanzia dakika hiyo tukaitwa TRAITORS, lakini wakubaliana wasitudhuru bali waichanechane mitihani ile ili ushahidi ukosekane unaoonyesha kuwa tulifanya paper na wao hawakufanya.
Wakafanya hivyo. Lakini hawakujua wlaichokosea. Nilisema mwanzoni mtu kama mimi nilishajua tangu jana yake kuwa kungekuwa na harufu ya mgomo. Hivyo mtu ulikuwa ukiingia tu kwenye chumba cha mtihani kitu cha kwanza ilikuwa ni kuandikisha jina lako na signature. Hivyo fujo ilipoanza wale walikimbilia mitihani hawakujua kama huo ni ushahidi mwingine.
Masenge na wenzake walichofanya wakachukua majina yote wakatoa photocopy ya majina ya wote tuliosaini, wakaacha copy kwa Dean of Engineering na original akaondoka nayo Prof. Masenge mwenyewe.
Wakati Pro. Masenge anapanda kuondoka FOE grounds, mmoja wale wanafunzi akapata wao kwamba ushahidi wa list ya waliosaini hawana na anayo Masenge. Hivyo, akiondoka nayo wamekwisha. Wakaondoka kundi lote wakamzingira Prof. Masenge, wakamnyang’anya ile list ya majina na wakichanachana mbele yake.
Terrible mistake hawakujua kuwa tayari kopi ipo kule kwa Dean. Hapa ndipo hawa wanafunzi 211 walipokosea na sijui kama walikuja kuligundua hili.
Baada ya siku mbili, ikatangazwa list ya watu 72 na 211. 72 walikuwa ni sisi ambao tulifanya mtihani na tulitakiwa kuendelea kuwepo chuoni. Na wale 211 ni wale waliofanya fujo zile wakatakiwa kuondoka chuoni kwani walifukuzwa.
Ndipo yakazuka majina mawili maarufu yaani G211 na TRAITORS. G211 walijiita hivyo kwa sababu mwaka mmoja nyuma bungeni kulikuwa na kundi la G55 la wabunge waliotaka hoja ya serikali ya Tanganyika iliyozimwa na Nyerere.
Mimi kama na wenzangu 72 tukaendelea na Maisha ya Chuo. Wale G211 wakafungua kesi Mahakamani. Kundi la G211 lilikuwa na watu wengi sana. Nimeshamtaja Karungubare (CHADEMA), Sweke, Kitilinga ambaye sijui yuko wapi lakini mara ya mwisho alikuwa OTIS kampuni inayoshughulika na lifts za majengo.
Wengine ni Phenihas Magesa ambaye nadhani ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Mwanza na mwaka 2009 aligombea ubunge jimbo la Busanda akashindwa na Lorencia Bukwimba wa CCM. Phenihas alikuwa kinara mzuri
Kesi ya hawa ilendelea hadi nadhani mwishoni mwa September 1994 na wakashinda na wakarudishwa Chuoni. Wakaja huku tunaanza second year na wako very enthusiastic kukishinda Chuo. Hakika walitamba. Wakanunu T-Shirt zimeandikwa G211 kama ambavyo sasa zimeenea zilizoandikwa DHAIFU. Kurudi kwao ilikuwa fahari kwao na huzuni kwetu. Si huzuni kuwa tulipenda, bali walikuwa ni kero kila tulipopita.
Tukakaa tumenuaniana yaani TRAITORS na G211. Faculty of Engineering au FOE second year tukawa katika makundi hayo mawili. Ninakumbuka siku moja nimeenda kusoma prep darasa moja wakaja wakanifukuza kwa sababu TRAITORS tulipigwa marufuku hakuna ku-study kule FOE.
Hali ikadumu hivyo kwa nusu mwezi. Ndipo likaja sakata la Mutungirehi. Maadui wa Mutungirehi wakaona kundi pekee lenye uamsho na zuri kulitumia ni hili la G211.
Kuanzia hapa wengi mnajua yaliyotokea. Mutungirehi akavurumishwa stejini kama thread moja inavyosimuliwa humu. Lakini players wakuu walikuwa ni hawa G211 ingawa wanachuo wengi walidhani ni vijana wote wa engineering. Si kweli, sisi tulioitwa TRAITORS hatukufurahia vurugu kwa Mutungirehi. Kilichofuata ni kufungwa Chuo kwa mgomo uliosababishwa na fujo hizi.
Tukiwa huko nyumbani tukaletewa barua zenye neon liitwalo INTIMIDATION. Mimi ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kukutana na neno hili na ikabidi nifungue dictionary kulielewa.
Sitaki kutaja nilipokea barua nikiwa mkoa gani. Lakini G211 nao walikuwa wamejipanga posta zote za miji mikubwa. Wakiona mwanachuo kaenda kupokea barua basi wanakuja na kufanya kavurugu kadogo ili wajue ulichoandikiwa. Walikuwa wameji-organise kama usalama wa taifa.
Mimi nikaenda posta. Natoka kuchukua barua nikazungukwa na vijana wanne, wote ni katika kundi la G211. Wakata kujua barua niliyopokea. Kwa sababu nilikuwa mkoani na hatuko chuoni na mimi nikapata kiburi sikutaka kuwaonyesha nikawapuuza na kuwatishia kuwaitia polisi wakaachana na mimi.
Nyumbani nikafanya masharti ya barua ile, kwamba kama nilitishiwa (intimidation) basi ni nani au kikundi gani kilitutishia. Mimi nikaona Mungu akupe nini maana ule mnyanyaso wa kuitwa TRAITORS tangu May 1994 hadi October 1994 nilishauchoka nikataja waziwazi kuwepo kwa kundi la G211 na jinsi walivyokuwa wakitunyanyasa kutufukuza hata madarasani kujisomea usiku (prep).
Lecturer mmoja alinipa live kwamba barua yangu walii-discus at length.
Mwanzaoni mwa December 1994 tukaitwa kurudi Chuoni, lakini Mutungirehi akiwa bado President of DARUSO. Effect ni kwamba wanafunzi zaidi ya 200 walisimiamishwa mwaka mzima wengi wao wakiwa ni wale G211.
Ikaitishwa referendum kuchagua kuendelea na Mutungirehi regime au la na wengi wakachagua kuwa asiendelee na ukaitishwa uchaguzi mwingine.
Siku moja nimekutana na Lugiko Mpelwa Karungubare akiwa CHADEMA, nikamkumbusha ule woga wake hadi akatuita tuingine madarasani akakataa kabisa kukumbuka.
Ladislaus Malima aliyekuwa jasiri kunisukuma nisiingie kwenye mtihani mmeeleza kwenye thread nyingine kwamba alipopigwa mkwara kwenye mgomo wa Mutungirehi akanywea na wale wenzake G211 naye wakamuita TRAITOR.
Haya ndiyo ninayoyakumbuka kuhusiana na sakata lile la wanafunzi wa Engineering { G211} na Benedict Mutungirehi. Samahani kwa Makala ndefu lakini imenibidi niyaseme haya.

Reply With Quote


Follow Us Here