Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

    Report Post
    Page 7 of 8 FirstFirst ... 5678 LastLast
    Results 121 to 140 of 155
    1. #1
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By NYENJENKURU View Post
      Unakumbuka alipotolewa high table Nkrumah hadi akupoteza kiatu, jamaa alikuwa mkorofi sana, watu wanamvuta aondoke yeye akashikilia meza kidogo aanguke nayo kwenye stage, i think it was 1991 or 92 kama sikosei.
      Quote By NYENJENKURU View Post
      Yaani kuna vijana walioshiriki kumshusha huyo jamaa na kule FOE kaanza kumuita MUTUNGILAHELA aka Mnyamrenge..Siku hizi wengi ni Ma senior Engineers ukiwakumbusha wancheka sanaaaaa...kama John Peter...JP nk

      Thread hii inatofautiana na ile nyingine ya kuuliza kuhusu aliko Benedict Mutungirehi, aliyekuwa mbunge na sasa hatujui yuko wapi.

      {Mutungirehi; mwanasiasa mahiri kazimikia wapi?}

      Nimeamua kuweka thread mpya ili wengi wajue chanzo cha matukio yale kwa faida ya historia.

      Unajua hata wengi hawafahamu relation ya vijana wale wa Engineering (FOE) na kundi lililomtoa Mutungirehi pale stejini. Haya ni makundi mawili tofauti yaliyounganishwa na ile nia ya kumuondoa Mutungirehi.

      Sakata ya Mutungirehi ilitokea mwishoni mwa October 1994, lakini ili uielewe vizuri inabidi uanze na matukio ya tangu April 1994 yaani miezi sita nyuma. Mimi nilikuwa namalizia first year pale Engineering na hivyo ninalikumbuka suala hili vizuri sana.

      Kwa nini nianzie nyuma vile? Ni kwa sababu ninataka kuweka hisoria sawa kwani baadhi wanapotosha na wanajifanya siku hizi ni wapiganaji kwelikweli.

      Tuanze sasa maelezo. Mwezi April 1994 nikiwa first Year pale FOE tulikuwa na somo linaitwa Engineering Mathematics ambayo ilikuwa inafundishwa na walimu toka Mathematics depertment. Wakati huo ndiyo amemaliza kufunidha topics ngumu kichizi kama vile divergence, curl na kadhalika.

      Kisha yule lecture akatoa test ambayo ilikuwa ngumu haina mfano kwani mtu unafika mwisho wa time hujafanya swali hata moja. Lecture akatangaza kwamba muda wa paper umeisha. Mimi nilikuwa nachukua Civil Engineering nimekaa karibu na Bwana anaitwa Mziray. Mziray akaanzisha fujo kwa kumshika lecturer asikusanye zile paper.

      Mziray simkumbuki jina lake la kwanza ila najua alimaliza Kibaha High School, May 1993, akaenda JKT Oljoro na akaja UDSM. Pale Kibaha alikuwa PCM na aliondoka na Dv. One Point 5 yaani ABB.

      Kwa watu kama huyu kudhalilishwa kuibuka na zero kwenye Mathematics ilikuwa kejeli lakini ukweli ni kwamba test ilikuwa ni ngumu.

      Fujo ya Mziray zikaungwa mkono na wengi tu. Yule mwalimu akarudi Maths Dept. na huko akashitaki kwa mkuu wake yaani Prof. Masenge kwamba kafanyiwa fujo na vijana wa Engineering.

      Kumbuka ile test ndiyo ilikuwa ya mwisho wa mwaka. Si kama siku hizi nasikia wanasoma kwa semester, wakati ule test ile ilikuwa ya mwisho na kilichobaki ni tutorials chache kusubiri Unversity Exam. Vumilieni hadi mwisho maana hadi hapa hakuna connection yoyote na Mutungirehi.

      Hivyo, Prof. Masenge akato quotion kwamba Mathematics dept haitafundisha tena Engineering students hadi wa-apologise. Engineering tukakataa kuapologise.

      April ikaisha May ikaingia. May ndiyo ilikuwa mwezi wa University Exams. Tukafanya exams zingine lakini binafsi nilishapata dalili za kugoma kufanya Maths Exam. Hili niliambiwa na Marehemu Dr. Nzali ambaye nilienda kumfuata kuhusu ugonjwa wangu maana niliugua karibu niage dunia hivyo nikawa namtaarifu kuhusu unafuu wangu. Akaniambia nisijaribu kugoma.

      Kesho yake ikafika yaani siku ya Mathematics Exam. Tukaingia madarasani lakini walimu hawakuleta mitihani. Wakati huo sheria ya chuo inasema kuwa zikipita nusu saa basi unaweza kutoka nje ya chumba cha mtihani na hakuna mwingine kuingia.

      Nusu saa ikafika, tension ya wanafunzi ikaanza kupanda maana walimu hawakuja na hivyo tutaonekana first year wote hatukufanya paper na hivyo tumeji-ABSCOND.

      Tukakubaliana kuwa tutoke nje tujadili cha kufanya. Sasa hapa ndipo vurugu ya kwanza ilipoanzia. Class representatives wetu ninaowakumbuka walikuwa zaidi ya watatu yaani Lugiko Mpelwa karungubare (Chemical Engineering), Sweke (Civil Engieer), Hussein Kitilinga (Electrical Engineer). Wengine nimewasahau.

      Msiomjua Karungubare ni yule aliyegombea uenyekiti NCCR akapata kura moja na James Mbatia akashinda uenyekiti huo. Karungubare sasa hivi ni mwanachama mzuri tu wa CHADEMA.

      Wakati tumekaa pale chini hawa ma-class reps wakaitwa kujadili kwa Dean of faculty. Kumbe huko kwa Dean tayari Prof Masenge yuko huko na yule lecturer aliyefanyiwa vurugu. Binafsi sijui walifikaje kule.

      Pale chini tumeshajadili na kuamua kwamba sisi hatujagoma kufanya paper ila wao ndiyo wamekataa kuleta mtihani. Basi tukakaa tukiwa hatujui nini kitatokea. Mitihani huanza saa 3 lakini hadi wakati huo tayari ni saa 5 mchana.

      Ikafika mahala kila mmoja akaamua kuchukua uamuzi wake. Wapo walioamua kuondoka na kwenda mabwenini. Wakaulizwa “hivi nyinyi mnaondoka mtihani ukiletwa si mtakuwa mme-DISCO”. Wakajibu “fanyeni mtakavyoamua”!

      Wengine wakaamua kujiandaa na mtihani wa mchana au siku nyingine na hivyo wakabaki madarasani.

      Ilipofika nadhani saa 5:30 kumbe yale mazungumzo ya Prof. Masenge, Clas reps na daen yamemalizika na hivyo Prof. Masenge na timu yake wakaamua kugawa paper ili mtihani uanze. Wakaenda madarasani wakawakuta wale ambao walitulia kujiandaa na subjects zingine. Prof. na wenzake hawakujua kuwa kulikuwa na mtawanyiko wakagawa paper na waliomo wakaanza mtihani.

      Class reps wakaiona hali hii na waka-panic na kuja kwetu ambao tulikuwa nje. Ninayakumbuka vizuri maneno ya Karungubare kwamba “Jamani ingieni madarasani mkafanya paper maana tayari wenzetu wameshaana na zinasubiriwa tu dakika 30 milango ifungwe tusiingie tulioko nje

      Hapa ndipo likaanza sokomoko la mwaka. Binafsi nikataka kuhakikisha maneno ya Karungebare na ma-class reps wenzake. Tukaenda vyumba kadhaa. Kweli bwana wenzetu walikuwa wanafanya paper taratibu. Ingekuwa wote hatufanyi paper kwangu isingekuwa tatizo. Lakini tatizo ni pale baadhi walikuwa wanaifanya.

      Nikapiga kelele na wenzangu kadhaa nikisema “Jamani, tufanye moja kati ya mawili, ama tuwatoe kwa nguvu hawa wanaofanya paper ama tuingie na sisi tufanye”.

      Hakuna aliyejisumbua na huu ushauri wetu kwa sababu tulikuwa kama wanne tu kati ya kundi la watu zaidi ya 220. Nilipoona huu ni upuuzi nikatangaza “ni ujinga kusubiri na hivyo napanda ngazi kwenda kufanya paper nisije nikafukuzwa”. Nikaanza kupanda ngazi. Kumbe huyu Ladislaus Malima kanisikia na kuniona.

      Akanifuata amefura ajabu na kunisukuma akisema “Unajua wewe unacheza na Maisha ya watu, wale walioondoka utawafanya nini, unataka wafukuzwe”. Mimi nikajibu bila kujua kauli yangu imevutia wengi, nikasema “Wamekwenda wapi, si tulikubaliana tusiondoke. Sasa na wewe unasemaje kuhusu wanaofanya mtihani na hujawazuia”. Malima nikamzidi hoja na tension ikawa inazidi.

      Kumbe hata kundini mmojammoja akawa anachomoka na kwenda kufanya mtihani. Mimi pia nikapata nafasi nikaenda kufanya mtihani. Kumbe mtihani wenyewe ulikuwa mrahisi maana ndani ya dakika 30 nikawa nimeshanya maswali ambayo nimeshavuka passmark yaani 40%.

      Kumbe wakati tunafanya, kule nje dakika 30 zikawa zimeshapita na wakakubaliana kwamba waingie kwa nguvu kwenye vyumba vya mitihani, huko watatukuta sisi ambao kuanzia dakika hiyo tukaitwa TRAITORS, lakini wakubaliana wasitudhuru bali waichanechane mitihani ile ili ushahidi ukosekane unaoonyesha kuwa tulifanya paper na wao hawakufanya.

      Wakafanya hivyo. Lakini hawakujua wlaichokosea. Nilisema mwanzoni mtu kama mimi nilishajua tangu jana yake kuwa kungekuwa na harufu ya mgomo. Hivyo mtu ulikuwa ukiingia tu kwenye chumba cha mtihani kitu cha kwanza ilikuwa ni kuandikisha jina lako na signature. Hivyo fujo ilipoanza wale walikimbilia mitihani hawakujua kama huo ni ushahidi mwingine.

      Masenge na wenzake walichofanya wakachukua majina yote wakatoa photocopy ya majina ya wote tuliosaini, wakaacha copy kwa Dean of Engineering na original akaondoka nayo Prof. Masenge mwenyewe.

      Wakati Pro. Masenge anapanda kuondoka FOE grounds, mmoja wale wanafunzi akapata wao kwamba ushahidi wa list ya waliosaini hawana na anayo Masenge. Hivyo, akiondoka nayo wamekwisha. Wakaondoka kundi lote wakamzingira Prof. Masenge, wakamnyang’anya ile list ya majina na wakichanachana mbele yake.

      Terrible mistake hawakujua kuwa tayari kopi ipo kule kwa Dean. Hapa ndipo hawa wanafunzi 211 walipokosea na sijui kama walikuja kuligundua hili.

      Baada ya siku mbili, ikatangazwa list ya watu 72 na 211. 72 walikuwa ni sisi ambao tulifanya mtihani na tulitakiwa kuendelea kuwepo chuoni. Na wale 211 ni wale waliofanya fujo zile wakatakiwa kuondoka chuoni kwani walifukuzwa.

      Ndipo yakazuka majina mawili maarufu yaani G211 na TRAITORS. G211 walijiita hivyo kwa sababu mwaka mmoja nyuma bungeni kulikuwa na kundi la G55 la wabunge waliotaka hoja ya serikali ya Tanganyika iliyozimwa na Nyerere.

      Mimi kama na wenzangu 72 tukaendelea na Maisha ya Chuo. Wale G211 wakafungua kesi Mahakamani. Kundi la G211 lilikuwa na watu wengi sana. Nimeshamtaja Karungubare (CHADEMA), Sweke, Kitilinga ambaye sijui yuko wapi lakini mara ya mwisho alikuwa OTIS kampuni inayoshughulika na lifts za majengo.

      Wengine ni Phenihas Magesa ambaye nadhani ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Mwanza na mwaka 2009 aligombea ubunge jimbo la Busanda akashindwa na Lorencia Bukwimba wa CCM. Phenihas alikuwa kinara mzuri

      Kesi ya hawa ilendelea hadi nadhani mwishoni mwa September 1994 na wakashinda na wakarudishwa Chuoni. Wakaja huku tunaanza second year na wako very enthusiastic kukishinda Chuo. Hakika walitamba. Wakanunu T-Shirt zimeandikwa G211 kama ambavyo sasa zimeenea zilizoandikwa DHAIFU. Kurudi kwao ilikuwa fahari kwao na huzuni kwetu. Si huzuni kuwa tulipenda, bali walikuwa ni kero kila tulipopita.

      Tukakaa tumenuaniana yaani TRAITORS na G211. Faculty of Engineering au FOE second year tukawa katika makundi hayo mawili. Ninakumbuka siku moja nimeenda kusoma prep darasa moja wakaja wakanifukuza kwa sababu TRAITORS tulipigwa marufuku hakuna ku-study kule FOE.

      Hali ikadumu hivyo kwa nusu mwezi. Ndipo likaja sakata la Mutungirehi. Maadui wa Mutungirehi wakaona kundi pekee lenye uamsho na zuri kulitumia ni hili la G211.

      Kuanzia hapa wengi mnajua yaliyotokea. Mutungirehi akavurumishwa stejini kama thread moja inavyosimuliwa humu. Lakini players wakuu walikuwa ni hawa G211 ingawa wanachuo wengi walidhani ni vijana wote wa engineering. Si kweli, sisi tulioitwa TRAITORS hatukufurahia vurugu kwa Mutungirehi. Kilichofuata ni kufungwa Chuo kwa mgomo uliosababishwa na fujo hizi.

      Tukiwa huko nyumbani tukaletewa barua zenye neon liitwalo INTIMIDATION. Mimi ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kukutana na neno hili na ikabidi nifungue dictionary kulielewa.

      Sitaki kutaja nilipokea barua nikiwa mkoa gani. Lakini G211 nao walikuwa wamejipanga posta zote za miji mikubwa. Wakiona mwanachuo kaenda kupokea barua basi wanakuja na kufanya kavurugu kadogo ili wajue ulichoandikiwa. Walikuwa wameji-organise kama usalama wa taifa.

      Mimi nikaenda posta. Natoka kuchukua barua nikazungukwa na vijana wanne, wote ni katika kundi la G211. Wakata kujua barua niliyopokea. Kwa sababu nilikuwa mkoani na hatuko chuoni na mimi nikapata kiburi sikutaka kuwaonyesha nikawapuuza na kuwatishia kuwaitia polisi wakaachana na mimi.

      Nyumbani nikafanya masharti ya barua ile, kwamba kama nilitishiwa (intimidation) basi ni nani au kikundi gani kilitutishia. Mimi nikaona Mungu akupe nini maana ule mnyanyaso wa kuitwa TRAITORS tangu May 1994 hadi October 1994 nilishauchoka nikataja waziwazi kuwepo kwa kundi la G211 na jinsi walivyokuwa wakitunyanyasa kutufukuza hata madarasani kujisomea usiku (prep).

      Lecturer mmoja alinipa live kwamba barua yangu walii-discus at length.

      Mwanzaoni mwa December 1994 tukaitwa kurudi Chuoni, lakini Mutungirehi akiwa bado President of DARUSO. Effect ni kwamba wanafunzi zaidi ya 200 walisimiamishwa mwaka mzima wengi wao wakiwa ni wale G211.

      Ikaitishwa referendum kuchagua kuendelea na Mutungirehi regime au la na wengi wakachagua kuwa asiendelee na ukaitishwa uchaguzi mwingine.

      Siku moja nimekutana na Lugiko Mpelwa Karungubare akiwa CHADEMA, nikamkumbusha ule woga wake hadi akatuita tuingine madarasani akakataa kabisa kukumbuka.

      Ladislaus Malima aliyekuwa jasiri kunisukuma nisiingie kwenye mtihani mmeeleza kwenye thread nyingine kwamba alipopigwa mkwara kwenye mgomo wa Mutungirehi akanywea na wale wenzake G211 naye wakamuita TRAITOR.

      Haya ndiyo ninayoyakumbuka kuhusiana na sakata lile la wanafunzi wa Engineering { G211} na Benedict Mutungirehi. Samahani kwa Makala ndefu lakini imenibidi niyaseme haya.
      JokaKuu, fide1975, Nyunyu and 10 others like this.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    2. #121
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By Kichuguu View Post
      Mimi nili-graduate FoE mwaka 1987
      Msalimie Dr. Peter Chitamu. Nasikia ameshakuwa Proffessor. Chronology yake ya ku-graduate na kukaa FOE muda mfupi, na time ya kupata PhD ina tofauti ndogo mno na yako.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    3. #122
      Kichuguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2006
      Location : Popote Porini
      Posts : 6,857
      Rep Power : 3280
      Likes Received
      1342
      Likes Given
      930

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By SubiriJibu View Post
      Msalimie Dr. Peter Chitamu. Nasikia ameshakuwa Proffessor. Chronology yake ya ku-graduate na kukaa FOE muda mfupi, na time ya kupata PhD ina tofauti ndogo mno na yako.
      Nitamsalimia nikikutana naye; kuna watu wengi sana sijakutana nao tangu mwezi january mwaka 1996 nilipoondoka dar es salaam. Nimefika dar mara kadhaa lakini mara zote nimekuwa nashughulikia mambo ya kifamilia tu; ni mara moja tu nilipata na muda wa kutembelea main campus. Halafu effort yako ya kujaribu kutafuta watu wa kuchukia zaidi ni mbaya sana kwa sababu hujui ni nani kati ya hao unaotaka kuwachukia utakuja hitaji msaada wake. G123457XYZ kwa sasa ni adui zako, lakini you never know what is in the cooking; kuwa makini sana na watu katika umri wako wa leo. Wewe siyo mtoto wa shule tena.

      Somo kubwa kwako: ukifanya kosa, lisahau ili upate mda wa kuendelee na mambo mengine ya maana kwa sababu hata ukijaribu kusahihisha kosa hilo inakuwa ni too late; ni kama kujaribu kurudisha fuse kwenye bomu ambalo tayari limeshaaza process ya kulipuka. Usingeadika hadithi yako hiyo hapo juu, mimi nisingejua kuwa kweli kulikuwa na wanafunzi waliosaliti wenzao. Muda wote nilijua kuwa ni student politics zilizosababisha wanafunzi kutoelewana, lakini sasa najua kuwa kulikuwa na kudi la wanafunzi waliokuwa na philosophy ya ".....nuimekuja na begi langu peke yangu, usiniambie lolote...." Ubinafsi.

      BTW: Nitechelewa kujibu post zako utakazoelekeza kwangu kwa muda wa kama masaa manne, kwa vile nia shughuli nyingine. Ila ukielekeza lolote kwangu, nitalijibu.
      Ibambasi likes this.
      Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

    4. #123
      Kingcobra's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th January 2011
      Posts : 713
      Rep Power : 567
      Likes Received
      129
      Likes Given
      14

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Kufuatilia haya masentensi marefumarefu inahitaji uwe umetulia sana. Nitasoma Jpili.

    5. #124
      Suzie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th May 2010
      Posts : 1,097
      Rep Power : 0
      Likes Received
      342
      Likes Given
      309

      Default

      Quote By Kichuguu View Post
      Nitamsalimia nikikutana naye; kuna watu wengi sana sijakutana nao tangu mwezi january mwaka 1996 nilipoondoka dar es salaam. Nimefika dar mara kadhaa lakini mara zote nimekuwa nashughulikia mambo ya kifamilia tu; ni mara moja tu nilipata na muda wa kutembelea main campus. Halafu effort yako ya kujaribu kutafuta watu wa kuchukia zaidi ni mbaya sana kwa sababu hujui ni nani kati ya hao unaotaka kuwachukia utakuja hitaji msaada wake. G123457XYZ kwa sasa ni adui zako, lakini you never know what is in the cooking; kuwa makini sana na watu katika umri wako wa leo. Wewe siyo mtoto wa shule tena.

      Somo kubwa kwako: ukifanya kosa, lisahau ili upate mda wa kuendelee na mambo mengine ya maana kwa sababu hata ukijaribu kusahihisha kosa hilo inakuwa ni too late; ni kama kujaribu kurudisha fuse kwenye bomu ambalo tayari limeshaaza process ya kulipuka. Usingeadika hadithi yako hiyo hapo juu, mimi nisingejua kuwa kweli kulikuwa na wanafunzi waliosaliti wenzao. Muda wote nilijua kuwa ni student politics zilizosababisha wanafunzi kutoelewana, lakini sasa najua kuwa kulikuwa na kudi la wanafunzi waliokuwa na philosophy ya ".....nuimekuja na begi langu peke yangu, usiniambie lolote...." Ubinafsi.

      BTW: Nitechelewa kujibu post zako utakazoelekeza kwangu kwa muda wa kama masaa manne, kwa vile nia shughuli nyingine. Ila ukielekeza lolote kwangu, nitalijibu.
      Hii inaonekana imejibiwa na mtu mwenye upeo wa juu na aliyetulia. Subirijibu kama hujaridhika nitakuwa na wasiwasi na hivyo vyeti vyako vyenye maksi za kudesa
      Ibambasi and Ndukidi like this.

    6. #125
      KipimaPembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th August 2007
      Posts : 785
      Rep Power : 768
      Likes Received
      347
      Likes Given
      131

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      SubiriJibu,

      Inaonekana ume-reserve bitterness sana kwa kitendo cha kuitwa TRAITOR na kufukuzwa darasani enzi hizo. Lakini inaonekana wakati huo ulishindwa kabisa kupambana na hali hiyo, pamoja na kuwachomea wenzio utambi kwa utawala bado walikunyanyapaa na unyanyapaa huo unaonekana kuendelea kukutesa hadi leo; kwani hao jamaa waliokunyanyapaa inaonekana waliendelea kupeta katika maisha; kitu ambacho hukukitarajia.

      Kabla ya kuendelea kulalama humu ndani, jaribu kumpa mtu mwingine akusomee hii thread mwanzo hadi mwisho, bila shaka atakushauri kuachana na thread hii. Hayo mambo yalipita muda mrefu, lakini inaelekea JOHO LA U-TRAITOR ulilojivisha enzi hizo bado umelivaa na pengine mambo si mambo! Jitahidi kusamehe na kusahau, utapona na kuendelea na maisaha yako.
      Ibambasi likes this.

    7. #126
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By KipimaPembe View Post

      Ukiitwa TRAITOR na HOOLIGAN ambaye amedhihirisha HOOLIGANISM yake kwa kutwanga wenzake mkong'oto, kutupia wenzake viti na kufukuza wenzake madarasani na hata mwaka 1996 kuwafuata wasichana kule Hall 3 kuwafanyia fujo ya kuwalazimisha waje Nkrumah kusikiliza Baraza kana kwamba anasukuma kundi la mbuzi, basi huna haja kujali maana huyo amefika mwisho wa upeo wake wa kufikiri.
      Last edited by SubiriJibu; 5th July 2012 at 11:41.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    8. #127
      Idimi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2007
      Location : Ikwiriri
      Posts : 4,816
      Rep Power : 13657
      Likes Received
      934
      Likes Given
      345

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By SHIMBONONI View Post
      Mkuu SubiriJibu,

      Umenikumbusha miaka ile ya Dhahabu UDSM! Mutungirehi alichaguliwa kwa Kishindo kuwa Rais wa DARUSO late 1993 na kuwa TRAITOR wa Magamba baada ya kupta safari ya Uholanzi au Hungary mwenye kumbukumbu sahihi atasaidia.

      Siku ile aliposhushwa High table kuna kijana mmoja alisimama akasema " you were elected democratically ....now you are also rejected democratically " Nakumbuka kijana huyo then aliitwa NIPASHE. Najua Wakuu wengine kama Eliakim Maswi na Sylvester Sweke watakumbuka vema tukio hili. Sijui wamo humu au wanapita hapa?
      Duh Stori ndefu na ya kusisimua kwelikweli.
      Huyo jamaa kwenye wino mwekundu kwa sasa ni Katibu Mkuu (PS) wa Wizara ya Nishati na Madini. Alihamishiwa hapo baada ya kuondolewa David Kitundu Jairo, kaliyeondolewa kwa kashfa ya kuwahonga wabunge. Maswi katokea Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi
      SubiriJibu likes this.
      A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man!
      [email protected]

    9. #128
      mechard Rwizile's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 90
      Rep Power : 409
      Likes Received
      52
      Likes Given
      21

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Subirinijibu, nakushukuru sana kwa kutoa maelezo marefu yakiwa na maana ya kutuonyesha sisi ambao hatuja bahatika kuwa UDSM katika maisha yetu yote na hata wale ambao walipitia kabla na baada yenu.

      Nakushukuru kwa maana maelezo yako yote yalikuwa na lengo moja " Ukweli kumhusu Benedicto Mutungirehi". Shukrani hizi zitakuwa na maana kama kweli wewe sio Benedicto Mtungirehi kwa maana umemtoa hatiani angalau kwa viwango vyako na badhi ya watu wengine.

      Lengo halikuwa kutetea kufanya au kutofanya mtihani wa hesabu, ila kuonyesha chimbuko lililomtoa Benedicto madarakani kutokana na hukumu isiyokuwa ya haki.

      Kushinda kesi au kushindwa kesi hakumtii hatiani asiyekuwa na hatia wala kinyume chake, kwa kuwa yapo mambo mengi yanachagia kushinda au kushindwa kesi. Mimi ningekuwa hakimu wa kesi hiyo nisingewatia hatiani kwa kuzingatia kuwa dhumuni la hatia halikuwa na manufaa kwa Watanzania.

      Mchangiaji mmoja amesema ubabe wa Ma-lecutrers na watawala walio wengi wa nchi hii, wote ni mashahidi kuwa sio mara zote unakuwa na maana yeyote na mara nyingi ni majingambo na wakati mwingine kuandaa mazingira ya kujinufaisha. Aibu kwao.

      Kwa maana hii na kwa kuwa hatujabahatika kusikia kauli ya Mutungirehi asiwepo mtu wa kumuhukumu kwa kuwa Msaliti/traitor au la.
      SubiriJibu likes this.

    10. #129
      ntogwisangu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th November 2011
      Posts : 436
      Rep Power : 469
      Likes Received
      115
      Likes Given
      29

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By SubiriJibu View Post
      Wapo ambao wameandika vitabu kuhusu maisha ya Chuoni pale. Kuna dada anaitwa Hoyce Temu aliandika kitabu aliandika sana kuhusu harrassment za UDSM.

      Yeye alimaliza Zanaki High School na akafaulu kwenda UDSM. Wakati anasubiri kuingia pale akaamua kujaribisha mashindano ya Urembo yaani Miss Tanzania kwa kanda ya D'Salaam.

      Ajabau akashinda akawa Miss Dar na hatimaye akawa Miss Tanzania wa mwaka huo yaani 1999. Mwaka huohuo akaingia UDSM yaani sisi tuliomaliza 1997 tukiwa tumeshatoka.

      Hoyce Temu aliandika mengi tu ambayo tuliosma pale tunakubaliana. Aliandika hata jinsi alivyofukuzw apale Chuoni.

      Mkitaka tuandika hili la G211 basi mkubali msiltete ule ubabe wa wenzako ambao naona humu bado wanao. Wakubali tugawane page. Nusu ya kitabu waandike kuhusu upande wao na sisi nusu inayobaki tuandike yetu.

      Kwa taarifa yako mimi ninacho kitabu cha Mzee Punch ambacho kinasimulia lile kunji (mgomo) la mwaka 1990. Hapo kinaelezea kuhusu maisha ya UDSM yote na lile kunji. Mkikitaka wadau niwamwagie kama tulivyomwaga cha Nyerere humu yaani {Uongozi wetu na hatima ya Tanzania}.

      Wasalaam
      Japo nami ckuwa mlimani,ila kwa kipindi kile changu kampasi ya muhimbili ilijulikana vile vile ni sehemu ya UDSM.nimefurahi sana kupata simulizi hizi ambazo nilikuwa nazijua juu juu!!!!please tupe kitabu cha mzee Punch!!!!
      SubiriJibu likes this.

    11. #130
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Mkuu Mechard,

      Nashukuru kwa maelezo na conclusion yako. Naamini tunafanana ila kwa sababu mimi nilikuweko UDSM toka 1994 hadi 1997 niliona kuna haja ya kuelewsha mambo kadhaa.

      Nikukumbushe kwamba mimi si Mutungirehi maana hata hawa G211 kulingana na maelezo wanajua kabisa maelezo haya yanatolewa na mtu aliyeujua hasa undani wa FOE na wala si Mutungirehi. Labda nirekebishe kidogo statements mbili tatu za kwako kwa clarification.

      Quote By mechard Rwizile View Post
      kama kweli wewe sio Benedicto Mtungirehi kwa maana umemtoa hatiani angalau kwa viwango vyako
      Ukisoma vizuri post zangu zote utaona kuwa Benedict Mutungirehi tulimuondoa kwa njia ya kistaarabu kwa kumpigia vote of no confidence. Narudia ni kwamba uwezo wetu ulikuwa ni kutokuwa na imani naye kwani si sisi wala hao wanaojiita G211 wangeweza kuthibitisha tuhuma dhidi yake, na hawajwahi kuthibitisha.

      Tukapiga kura akaondoka na akaja Lenganasa. Na kura hizi tulipiga huku karibu zaidi ya watu 300 wamesimamishwa wako nyumbani na wengi wao wakiwa hawa G211.

      Ni wazi kuwa kama tungekutana Chuo kizima pale Rev Square tuakajadiliana agenda ya kumuondoa basi yale matokeo ya ile referendum ni ushahidi tosha kabisa agenda hiyo ingepita na sia ajabu tungeingia wote Nkrumah tukiwa na sauti moja kwamba pamoja na agenda zote kuna agenda ya kumpigia vote of no confidence.

      Hivyo, sijamsafisha Mutungirehi na hata hawa G211 hawanilaumu humu kwa hilo, ila pia siko tayari kujiunga na kundi la wanaosifia kitendo cha Mutungirehi kufanyiwa ubondia kwa kuvutwa tai, kuangushwa, kutwangwa ngumi na kutupiwa viti hadi akapelekwa hospitali na kiatu kimoja kwani kingine kilipotea.

      Quote By mechard Rwizile View Post
      Lengo halikuwa kutetea kufanya au kutofanya mtihani wa hesabu, ila kuonyesha chimbuko lililomtoa Benedicto madarakani kutokana na hukumu isiyokuwa ya haki
      Kama nillivyoeleza hapo juu, nakiri kwamba hooliganism aliyofanyiwa pale Nkrumah siwezi kuiita vingine na wala siwezi kuiita kuwa ni hukumu isiyo ya haki. Ile ni mob justice ambayo inaweza kushabikiwa na mtu ambaye inabidi uchunguze uwezo wake wa kufikiri ukoje.

      Hukumu ambayo hata yeye Mutungirehi hawezi kuikana ni ile referendum tuliyopiga tukamuondoa kwa sanduku la kura yaani vote of no confidence.

      Hii referendum tunaweza kusema wanachuo wote tulimfariji kwa uhuni aliofanyiwa pale Nkrumah Hall lakini tukasema sisi “sisi hatukuondoi kwa mateke na magumi au mieleka kama wale mabwana, bali tunakuondoa kistaarabu kwa kura” . Na tukamuondoa na akaondoka.

      Mutungirehi hajawahi kulalamika magazetini kuhusu ile kura tuliyomuondoa, ila aliwahi kulalamika kuhusu ule uhuni waliofanyiwa pale Nkrumah Hall ambao inahitaji akili ya ajabu kuutetea.

      Quote By mechard Rwizile View Post
      Kwa maana hii na kwa kuwa hatujabahatika kusikia kauli ya Mutungirehi asiwepo mtu wa kumuhukumu kwa kuwa Msaliti/traitor au la
      Tangu 2006 hadi hivi majuzi gazeti la RAI halina mvuto sana. Lakini ukipata nafasi pitia matoleo ya gazeti hilo mwaka 2003 hadi 2005 ni lazima utakuta kauli ya Mutungirehi kuhusu yaliyotokea pale Nkrumah Hall.

      Mimi nilisoma interview yote aliyohojiwa na mwandishi na kumbuka kipindi hicho alikuwa ni mbunge. Nilikuwa interested kuona atalielezaje tukio lile la October 1994 pale Nkrumah.

      Yeye anasema walipania kumuua. Sasa hili sina uhakika nalo. Na anasema kwamba baada ya kuanguka aliamua kurusharusha miguu na ndipo wavamizi wake wakaamua kukimbia wakidhani anakata roho. Sijui ni kweli au la lakini ni kweli alirusharusha miguu.

      Suala la TRAITOR na G211, Mutungirehi hawezi kulisimulia sana maana lilihusu first year wa Engineering na yeye atakuwa ni msimuliwaji tu. Ukweli ni kwamba hata second year, third year na fourth year Engineering wengi walikuwa wasimuliwaji maana lilitokea wakati tuko kwenye mitihani na hakukuwa na event iliyolead mikusanyika mingi.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    12. #131
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By ntogwisangu View Post
      Japo nami ckuwa mlimani,ila kwa kipindi kile changu kampasi ya muhimbili ilijulikana vile vile ni sehemu ya UDSM.nimefurahi sana kupata simulizi hizi ambazo nilikuwa nazijua juu juu!!!!please tupe kitabu cha mzee Punch!!!!
      Naomba wote wanaoniomba kitabu cha mzee PUNCH wani-PM kwenye messag box yangu humuhumu JF maana tunajaza page bure wakati tumeshaanzia thread mpya kwa ajili ya hicho. Hii hapa:

      {http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...ka-1990-a.html}
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    13. #132
      lukatony's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th March 2011
      Posts : 158
      Rep Power : 448
      Likes Received
      34
      Likes Given
      4

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By kadoda11 View Post
      mimi wa kizazi hiki cha digital ingawa sijapitia chuo kukuu cha UDSM mpaka sasa naweza kujivunia mafanikio mawili matatu ya elimu yangu.haya nyie ma-G211 na ma-TRAITORS wa UDSM ya 1994 mnajivunia nini?i mean is there any positive impact alongside to what you have narrated before us?
      Mafanikio gani wewe?umebebwa na ufisadi wa baba yako!!!!!!muwe na heshima watu wakizungumzia mapigano ya elimu za kweli kulikokuwa hakuna kubebana!!!!ungezaliwa na kusoma kipindi hicho na baba asingekuwa fisadi tena kijijini Ishishang'oro-Sengerema ungekuwa wapi wewe?
      SubiriJibu likes this.

    14. #133
      Lugeye's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th April 2011
      Posts : 305
      Rep Power : 475
      Likes Received
      40
      Likes Given
      43

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      mm cjui ntafika huko ndo kwana najkongoja na elimu yangu yakuunga unga
      Ibambasi likes this.

    15. #134
      Kakalende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2006
      Posts : 2,940
      Rep Power : 1238
      Likes Received
      391
      Likes Given
      388

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Nakumbuka wakati wa sakata lile la mtihani wa Maths, traitor mmoja aliandika barua ya kujitetea kwa Faculty Dean na baada ya G211 kushinda kwasi ile barua ikabandikwa notice board pale Foe, jamaa alikosa amani sana kwa miaka 3 iliyofuata hadi kumaliza chuo. Sishangai baada ya miaka 18 akina SubiriJibu wanakuja hapa kutetea usaliti wao.
      Ibambasi and SubiriJibu like this.
      Volunteers are not paid -- not because they are worthless, but because they're priceless!

    16. #135
      muonamambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd September 2010
      Posts : 568
      Rep Power : 559
      Likes Received
      179
      Likes Given
      946

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By Kakalende View Post
      Nakumbuka wakati wa sakata lile la mtihani wa Maths, traitor mmoja aliandika barua ya kujitetea kwa Faculty Dean na baada ya G211 kushinda kwasi ile barua ikabandikwa notice board pale Foe, jamaa alikosa amani sana kwa miaka 3 iliyofuata hadi kumaliza chuo. Sishangai baada ya miaka 18 akina SubiriJibu wanakuja hapa kutetea usaliti wao.
      Bila Shaka barua hiyo ilikuwa ya Subiri jibu.. Dhambi hii haiwezi kumtoka.ni sawa na kula Nyama ya mtu
      SubiriJibu and Nyamnyam like this.

    17. #136
      mechard Rwizile's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 90
      Rep Power : 409
      Likes Received
      52
      Likes Given
      21

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By SubiriJibu View Post
      Mkuu Mechard,

      Nashukuru kwa maelezo na conclusion yako. Naamini tunafanana ila kwa sababu mimi nilikuweko UDSM toka 1994 hadi 1997 niliona kuna haja ya kuelewsha mambo kadhaa.

      Nikukumbushe kwamba mimi si Mutungirehi maana hata hawa G211 kulingana na maelezo wanajua kabisa maelezo haya yanatolewa na mtu aliyeujua hasa undani wa FOE na wala si Mutungirehi. Labda nirekebishe kidogo statements mbili tatu za kwako kwa clarification.

      Ukisoma vizuri post zangu zote utaona kuwa Benedict Mutungirehi tulimuondoa kwa njia ya kistaarabu kwa kumpigia vote of no confidence. Narudia ni kwamba uwezo wetu ulikuwa ni kutokuwa na imani naye kwani si sisi wala hao wanaojiita G211 wangeweza kuthibitisha tuhuma dhidi yake, na hawajwahi kuthibitisha.

      Tukapiga kura akaondoka na akaja Lenganasa. Na kura hizi tulipiga huku karibu zaidi ya watu 300 wamesimamishwa wako nyumbani na wengi wao wakiwa hawa G211.

      Ni wazi kuwa kama tungekutana Chuo kizima pale Rev Square tuakajadiliana agenda ya kumuondoa basi yale matokeo ya ile referendum ni ushahidi tosha kabisa agenda hiyo ingepita na sia ajabu tungeingia wote Nkrumah tukiwa na sauti moja kwamba pamoja na agenda zote kuna agenda ya kumpigia vote of no confidence.

      Hivyo, sijamsafisha Mutungirehi na hata hawa G211 hawanilaumu humu kwa hilo, ila pia siko tayari kujiunga na kundi la wanaosifia kitendo cha Mutungirehi kufanyiwa ubondia kwa kuvutwa tai, kuangushwa, kutwangwa ngumi na kutupiwa viti hadi akapelekwa hospitali na kiatu kimoja kwani kingine kilipotea.

      Kama nillivyoeleza hapo juu, nakiri kwamba hooliganism aliyofanyiwa pale Nkrumah siwezi kuiita vingine na wala siwezi kuiita kuwa ni hukumu isiyo ya haki. Ile ni mob justice ambayo inaweza kushabikiwa na mtu ambaye inabidi uchunguze uwezo wake wa kufikiri ukoje.

      Hukumu ambayo hata yeye Mutungirehi hawezi kuikana ni ile referendum tuliyopiga tukamuondoa kwa sanduku la kura yaani vote of no confidence.

      Hii referendum tunaweza kusema wanachuo wote tulimfariji kwa uhuni aliofanyiwa pale Nkrumah Hall lakini tukasema sisi “sisi hatukuondoi kwa mateke na magumi au mieleka kama wale mabwana, bali tunakuondoa kistaarabu kwa kura” . Na tukamuondoa na akaondoka.

      Mutungirehi hajawahi kulalamika magazetini kuhusu ile kura tuliyomuondoa, ila aliwahi kulalamika kuhusu ule uhuni waliofanyiwa pale Nkrumah Hall ambao inahitaji akili ya ajabu kuutetea.

      Tangu 2006 hadi hivi majuzi gazeti la RAI halina mvuto sana. Lakini ukipata nafasi pitia matoleo ya gazeti hilo mwaka 2003 hadi 2005 ni lazima utakuta kauli ya Mutungirehi kuhusu yaliyotokea pale Nkrumah Hall.

      Mimi nilisoma interview yote aliyohojiwa na mwandishi na kumbuka kipindi hicho alikuwa ni mbunge. Nilikuwa interested kuona atalielezaje tukio lile la October 1994 pale Nkrumah.

      Yeye anasema walipania kumuua. Sasa hili sina uhakika nalo. Na anasema kwamba baada ya kuanguka aliamua kurusharusha miguu na ndipo wavamizi wake wakaamua kukimbia wakidhani anakata roho. Sijui ni kweli au la lakini ni kweli alirusharusha miguu.

      Suala la TRAITOR na G211, Mutungirehi hawezi kulisimulia sana maana lilihusu first year wa Engineering na yeye atakuwa ni msimuliwaji tu. Ukweli ni kwamba hata second year, third year na fourth year Engineering wengi walikuwa wasimuliwaji maana lilitokea wakati tuko kwenye mitihani na hakukuwa na event iliyolead mikusanyika mingi.
      Subirijibu, maelezo yako yamekuwa ya kuvutia na yana mtiririko ambao hauwezi ukawa wa kulazimisha yaani kujitetea. Ni maelezo yanayoongozwa na dhati ya ndani kabisa vinginevyo ujasiri huu ungekuwa na kikomo. Maana umeandika sio haba.

      Maelezo yako na uchungu uliokuwa nao ni dhahiri ulikandamizwa kwa kutotendewa haki, na haukuwepo uwanja wa kutoa maelezo kama ulivyofanikiwa kufanya. Umekuwa na bahati umeutumia uwanja huu vizuri na imeonyesha wahusika wengi wamepata upande wa pili wa shilingi bila kujali wamekuliana na wewe. Wasiokubaliana nawe usiwajali labda watakubali kesho au hata siku chache kabla ya kufa kwao lakini ujumbe umefikishwa, hii ni bahati sana.

      Funzo nililolipata ni kwamba Watanzania walio wengi wamekuwa katika mazingira kama yako, wamekamdamizwa na marafiki zao wenye nguvu, wafanyakazi wengi wameumizwa na wafayakazi wenzio wenye madaraka na ushawishi mkubwa. Kwenye vyama vya siasa mambo ni kama hayo, kwenye makanisa yetu hali sio tofauti. Unaweza kugundua siri ya watu kuwa na hasira na chuki. Mkandamizo wa hivi ndio unaoleta vurugu katika nchi na katika taasisi mbali mbali.

      Tujitahidi kujifunza kusikiliza,kusema kwa kiasi, tuepuke ukandamizaji kwa maana sio rahisi kujua mwenzio atumizwa kwa kiasi gani. Kusema ukweli wakati wote na tuepuke kila aina ya udharirishaji uwe wa kijinsia,kikabila na kidini. Maana maeneo haya yanaigusa nafsi ya mtu na maumivu yake ni makali sana.

      Jamii forum pamekuwa mahali pakusemea ukweli, kutolea malalamiko na mawasiliano kutoka upande moja kwenda upande mwingine. Udumu jamii forum.
      SubiriJibu likes this.

    18. #137
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By Kakalende View Post
      Nakumbuka wakati wa sakata lile la mtihani wa Maths, traitor mmoja aliandika barua ya kujitetea kwa Faculty Dean na baada ya G211 kushinda kwasi ile barua ikabandikwa notice board pale Foe, jamaa alikosa amani sana kwa miaka 3 iliyofuata hadi kumaliza chuo. Sishangai baada ya miaka 18 akina SubiriJibu wanakuja hapa kutetea usaliti wao.
      Bwana Kakalende,

      Ndiyo maana nimesema sana na narudia, inabidi mjipange mnapokuja humu JF. Maana huku mtaani na humu JF watu wanaangalia ubora wa kufikisha hoja. Sasa ngoja nikukumbushe kuhusu tukio hilo la huyo aliyebandikwa hapo ubaoni FOE.

      Kwanza kabisa, huyo jamaa alikuwa ni G211 mwenzenu hakuwa upande wetu mliotuita TRAITOR.

      Nakumbuka kuna mwenzetu mmoja rafiki yangu, mlipoanza kutuita sisi TRAITOR mwenzetu yule akawapa live kwamba nyinyi mnaojiita G211 ndiko mtazaa ma-TRAITOR wengi mtakapoanza kusalitiana.

      Huyu rafiki yangu nikamuuliza kwa nini alipata ujasiri wa kuwaambia vile? Akasema kwamba yeye aliongea na G211 wengi na akagundua kwamba wengi tu walikuwa na nia ya kuingia kufanya ule mtihani lakini waliogopa macho ya watu na waliogopa consequence kama hizi za kuitwa TRAITOR.

      Hivyo, kisa hicho cha jamaa kuandika barua ya kuomba radhi wala hakikutushangaza. Unajua kesi ilikuwa imewakalia kiasi kwamba haikujulikana kama mtashinda na kurudishwa chuoni au la.

      Hivyo, yule jamaa kwa kujua ugumu huo wa kesi akaandika barua kuomba msamaha na akaeleza kwamba alilazimishwa kutoingia kwenye chumba cha mtihani si kwa mapenzi yake bali alikuwa INTIMIDATED. Bahati mbaya wakati ule hata photocopy zilikuwa nadra lakini ingekuwa ni sasa tungepiga picha barua ile na kuimwaga humu JF.

      Ndipo hapo tungethibitisha kwamba kumbe hata hukohuko kundini kwenu mlikojiita G211 wengi waliwaogopa nyinyi na si kwa matakwa yao.

      Huyu jamaa ni kweli hata mimi ningeweza kumuita TRAITOR kwa maana halisi ya TRAITOR. Kwani alikuwa kinara sana wa kutuita sisi TRAITOR na kujikweza kuwa yeye ni G211.

      Na kwa kweli alikuwa anatuudhi na nyinyi G211 mlimuona kama kiongozi mzuri wa mapambano yenu. Nakumbuka jamaa alikuwa mhaya. Na kama isingekuwa barua yake ku-leak basi hakika yule jamaa siku moja mngempa uongozi ama wa FOE au hata wa DARUSO. Mimi huwa ninalifikiri tendo lile lilikuwa ni kum-block move yoyote asiwe kiongozi baadaye maana wapo walioiona hiyo move kama ambavyo sasa hivi zinavyo-leak barua za maofisini kwenye magazeti au mitandaoni.

      Hivyo, huyu ndiye alikuwa TRAITOR halisi maana mligoma naye kufanya mtihani, hakufanya kama sisi mkadhani mko naye. Lakini kumbe alivyoona mwisho wa kesi unaweza usiwe mzuri akawageuka na kuwasaliti kwa kuomba msamaha tena kwa baru na akaeleza kuwa alitishiwa.

      Hiyo ni dalili kwamba mngeshindwa kesi ile na kufanya msiwe wanachuo basi ma-TRAITOR wengi kama huyu wangejitokeza wenyewe kutoka humohumo mlikojiita G211.

      Bwana Kakalende,

      Asante sana kunikumbusha tukio la huyu bwana maana nilikuwa nimejisahau kabisa kulitaja. na ninashukuru mmelitaja wenyewe G211.
      Last edited by SubiriJibu; 5th July 2012 at 15:47.
      Ibambasi likes this.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    19. #138
      Nsabhi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd February 2011
      Posts : 669
      Rep Power : 554
      Likes Received
      75
      Likes Given
      135

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Ni hadithi ndefu na inavutiakuisoma lakini ulilenga kueleza nini hasa? Maana ni kama unatusimuliatu. What is the motive behind this?
      Quote By SubiriJibu View Post
      Thread hii inatofautiana na ile nyingine ya kuuliza kuhusu aliko Benedict Mutungirehi, aliyekuwa mbunge na sasa hatujui yuko wapi.

      {Mutungirehi; mwanasiasa mahiri kazimikia wapi?}

      Nimeamua kuweka thread mpya ili wengi wajue chanzo cha matukio yale kwa faida ya historia.

      Unajua hata wengi hawafahamu relation ya vijana wale wa Engineering (FOE) na kundi lililomtoa Mutungirehi pale stejini. Haya ni makundi mawili tofauti yaliyounganishwa na ile nia ya kumuondoa Mutungirehi.

      Sakata ya Mutungirehi ilitokea mwishoni mwa October 1994, lakini ili uielewe vizuri inabidi uanze na matukio ya tangu April 1994 yaani miezi sita nyuma. Mimi nilikuwa namalizia first year pale Engineering na hivyo ninalikumbuka suala hili vizuri sana.

      Kwa nini nianzie nyuma vile? Ni kwa sababu ninataka kuweka hisoria sawa kwani baadhi wanapotosha na wanajifanya siku hizi ni wapiganaji kwelikweli.

      Tuanze sasa maelezo. Mwezi April 1994 nikiwa first Year pale FOE tulikuwa na somo linaitwa Engineering Mathematics ambayo ilikuwa inafundishwa na walimu toka Mathematics depertment. Wakati huo ndiyo amemaliza kufunidha topics ngumu kichizi kama vile divergence, curl na kadhalika.

      Kisha yule lecture akatoa test ambayo ilikuwa ngumu haina mfano kwani mtu unafika mwisho wa time hujafanya swali hata moja. Lecture akatangaza kwamba muda wa paper umeisha. Mimi nilikuwa nachukua Civil Engineering nimekaa karibu na Bwana anaitwa Mziray. Mziray akaanzisha fujo kwa kumshika lecturer asikusanye zile paper.

      Mziray simkumbuki jina lake la kwanza ila najua alimaliza Kibaha High School, May 1993, akaenda JKT Oljoro na akaja UDSM. Pale Kibaha alikuwa PCM na aliondoka na Dv. One Point 5 yaani ABB.

      Kwa watu kama huyu kudhalilishwa kuibuka na zero kwenye Mathematics ilikuwa kejeli lakini ukweli ni kwamba test ilikuwa ni ngumu.

      Fujo ya Mziray zikaungwa mkono na wengi tu. Yule mwalimu akarudi Maths Dept. na huko akashitaki kwa mkuu wake yaani Prof. Masenge kwamba kafanyiwa fujo na vijana wa Engineering.

      Kumbuka ile test ndiyo ilikuwa ya mwisho wa mwaka. Si kama siku hizi nasikia wanasoma kwa semester, wakati ule test ile ilikuwa ya mwisho na kilichobaki ni tutorials chache kusubiri Unversity Exam. Vumilieni hadi mwisho maana hadi hapa hakuna connection yoyote na Mutungirehi.

      Hivyo, Prof. Masenge akato quotion kwamba Mathematics dept haitafundisha tena Engineering students hadi wa-apologise. Engineering tukakataa kuapologise.

      April ikaisha May ikaingia. May ndiyo ilikuwa mwezi wa University Exams. Tukafanya exams zingine lakini binafsi nilishapata dalili za kugoma kufanya Maths Exam. Hili niliambiwa na Marehemu Dr. Nzali ambaye nilienda kumfuata kuhusu ugonjwa wangu maana niliugua karibu niage dunia hivyo nikawa namtaarifu kuhusu unafuu wangu. Akaniambia nisijaribu kugoma.

      Kesho yake ikafika yaani siku ya Mathematics Exam. Tukaingia madarasani lakini walimu hawakuleta mitihani. Wakati huo sheria ya chuo inasema kuwa zikipita nusu saa basi unaweza kutoka nje ya chumba cha mtihani na hakuna mwingine kuingia.

      Nusu saa ikafika, tension ya wanafunzi ikaanza kupanda maana walimu hawakuja na hivyo tutaonekana first year wote hatukufanya paper na hivyo tumeji-ABSCOND.

      Tukakubaliana kuwa tutoke nje tujadili cha kufanya. Sasa hapa ndipo vurugu ya kwanza ilipoanzia. Class representatives wetu ninaowakumbuka walikuwa zaidi ya watatu yaani Lugiko Mpelwa karungubare (Chemical Engineering), Sweke (Civil Engieer), Hussein Kitilinga (Electrical Engineer). Wengine nimewasahau.

      Msiomjua Karungubare ni yule aliyegombea uenyekiti NCCR akapata kura moja na James Mbatia akashinda uenyekiti huo. Karungubare sasa hivi ni mwanachama mzuri tu wa CHADEMA.

      Wakati tumekaa pale chini hawa ma-class reps wakaitwa kujadili kwa Dean of faculty. Kumbe huko kwa Dean tayari Prof Masenge yuko huko na yule lecturer aliyefanyiwa vurugu. Binafsi sijui walifikaje kule.

      Pale chini tumeshajadili na kuamua kwamba sisi hatujagoma kufanya paper ila wao ndiyo wamekataa kuleta mtihani. Basi tukakaa tukiwa hatujui nini kitatokea. Mitihani huanza saa 3 lakini hadi wakati huo tayari ni saa 5 mchana.

      Ikafika mahala kila mmoja akaamua kuchukua uamuzi wake. Wapo walioamua kuondoka na kwenda mabwenini. Wakaulizwa “hivi nyinyi mnaondoka mtihani ukiletwa si mtakuwa mme-DISCO”. Wakajibu “fanyeni mtakavyoamua”!

      Wengine wakaamua kujiandaa na mtihani wa mchana au siku nyingine na hivyo wakabaki madarasani.

      Ilipofika nadhani saa 5:30 kumbe yale mazungumzo ya Prof. Masenge, Clas reps na daen yamemalizika na hivyo Prof. Masenge na timu yake wakaamua kugawa paper ili mtihani uanze. Wakaenda madarasani wakawakuta wale ambao walitulia kujiandaa na subjects zingine. Prof. na wenzake hawakujua kuwa kulikuwa na mtawanyiko wakagawa paper na waliomo wakaanza mtihani.

      Class reps wakaiona hali hii na waka-panic na kuja kwetu ambao tulikuwa nje. Ninayakumbuka vizuri maneno ya Karungubare kwamba “Jamani ingieni madarasani mkafanya paper maana tayari wenzetu wameshaana na zinasubiriwa tu dakika 30 milango ifungwe tusiingie tulioko nje

      Hapa ndipo likaanza sokomoko la mwaka. Binafsi nikataka kuhakikisha maneno ya Karungebare na ma-class reps wenzake. Tukaenda vyumba kadhaa. Kweli bwana wenzetu walikuwa wanafanya paper taratibu. Ingekuwa wote hatufanyi paper kwangu isingekuwa tatizo. Lakini tatizo ni pale baadhi walikuwa wanaifanya.

      Nikapiga kelele na wenzangu kadhaa nikisema “Jamani, tufanye moja kati ya mawili, ama tuwatoe kwa nguvu hawa wanaofanya paper ama tuingie na sisi tufanye”.

      Hakuna aliyejisumbua na huu ushauri wetu kwa sababu tulikuwa kama wanne tu kati ya kundi la watu zaidi ya 220. Nilipoona huu ni upuuzi nikatangaza “ni ujinga kusubiri na hivyo napanda ngazi kwenda kufanya paper nisije nikafukuzwa”. Nikaanza kupanda ngazi. Kumbe huyu Ladislaus Malima kanisikia na kuniona.

      Akanifuata amefura ajabu na kunisukuma akisema “Unajua wewe unacheza na Maisha ya watu, wale walioondoka utawafanya nini, unataka wafukuzwe”. Mimi nikajibu bila kujua kauli yangu imevutia wengi, nikasema “Wamekwenda wapi, si tulikubaliana tusiondoke. Sasa na wewe unasemaje kuhusu wanaofanya mtihani na hujawazuia”. Malima nikamzidi hoja na tension ikawa inazidi.

      Kumbe hata kundini mmojammoja akawa anachomoka na kwenda kufanya mtihani. Mimi pia nikapata nafasi nikaenda kufanya mtihani. Kumbe mtihani wenyewe ulikuwa mrahisi maana ndani ya dakika 30 nikawa nimeshanya maswali ambayo nimeshavuka passmark yaani 40%.

      Kumbe wakati tunafanya, kule nje dakika 30 zikawa zimeshapita na wakakubaliana kwamba waingie kwa nguvu kwenye vyumba vya mitihani, huko watatukuta sisi ambao kuanzia dakika hiyo tukaitwa TRAITORS, lakini wakubaliana wasitudhuru bali waichanechane mitihani ile ili ushahidi ukosekane unaoonyesha kuwa tulifanya paper na wao hawakufanya.

      Wakafanya hivyo. Lakini hawakujua wlaichokosea. Nilisema mwanzoni mtu kama mimi nilishajua tangu jana yake kuwa kungekuwa na harufu ya mgomo. Hivyo mtu ulikuwa ukiingia tu kwenye chumba cha mtihani kitu cha kwanza ilikuwa ni kuandikisha jina lako na signature. Hivyo fujo ilipoanza wale walikimbilia mitihani hawakujua kama huo ni ushahidi mwingine.

      Masenge na wenzake walichofanya wakachukua majina yote wakatoa photocopy ya majina ya wote tuliosaini, wakaacha copy kwa Dean of Engineering na original akaondoka nayo Prof. Masenge mwenyewe.

      Wakati Pro. Masenge anapanda kuondoka FOE grounds, mmoja wale wanafunzi akapata wao kwamba ushahidi wa list ya waliosaini hawana na anayo Masenge. Hivyo, akiondoka nayo wamekwisha. Wakaondoka kundi lote wakamzingira Prof. Masenge, wakamnyang’anya ile list ya majina na wakichanachana mbele yake.

      Terrible mistake hawakujua kuwa tayari kopi ipo kule kwa Dean. Hapa ndipo hawa wanafunzi 211 walipokosea na sijui kama walikuja kuligundua hili.

      Baada ya siku mbili, ikatangazwa list ya watu 72 na 211. 72 walikuwa ni sisi ambao tulifanya mtihani na tulitakiwa kuendelea kuwepo chuoni. Na wale 211 ni wale waliofanya fujo zile wakatakiwa kuondoka chuoni kwani walifukuzwa.

      Ndipo yakazuka majina mawili maarufu yaani G211 na TRAITORS. G211 walijiita hivyo kwa sababu mwaka mmoja nyuma bungeni kulikuwa na kundi la G55 la wabunge waliotaka hoja ya serikali ya Tanganyika iliyozimwa na Nyerere.

      Mimi kama na wenzangu 72 tukaendelea na Maisha ya Chuo. Wale G211 wakafungua kesi Mahakamani. Kundi la G211 lilikuwa na watu wengi sana. Nimeshamtaja Karungubare (CHADEMA), Sweke, Kitilinga ambaye sijui yuko wapi lakini mara ya mwisho alikuwa OTIS kampuni inayoshughulika na lifts za majengo.

      Wengine ni Phenihas Magesa ambaye nadhani ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Mwanza na mwaka 2009 aligombea ubunge jimbo la Busanda akashindwa na Lorencia Bukwimba wa CCM. Phenihas alikuwa kinara mzuri

      Kesi ya hawa ilendelea hadi nadhani mwishoni mwa September 1994 na wakashinda na wakarudishwa Chuoni. Wakaja huku tunaanza second year na wako very enthusiastic kukishinda Chuo. Hakika walitamba. Wakanunu T-Shirt zimeandikwa G211 kama ambavyo sasa zimeenea zilizoandikwa DHAIFU. Kurudi kwao ilikuwa fahari kwao na huzuni kwetu. Si huzuni kuwa tulipenda, bali walikuwa ni kero kila tulipopita.

      Tukakaa tumenuaniana yaani TRAITORS na G211. Faculty of Engineering au FOE second year tukawa katika makundi hayo mawili. Ninakumbuka siku moja nimeenda kusoma prep darasa moja wakaja wakanifukuza kwa sababu TRAITORS tulipigwa marufuku hakuna ku-study kule FOE.

      Hali ikadumu hivyo kwa nusu mwezi. Ndipo likaja sakata la Mutungirehi. Maadui wa Mutungirehi wakaona kundi pekee lenye uamsho na zuri kulitumia ni hili la G211.

      Kuanzia hapa wengi mnajua yaliyotokea. Mutungirehi akavurumishwa stejini kama thread moja inavyosimuliwa humu. Lakini players wakuu walikuwa ni hawa G211 ingawa wanachuo wengi walidhani ni vijana wote wa engineering. Si kweli, sisi tulioitwa TRAITORS hatukufurahia vurugu kwa Mutungirehi. Kilichofuata ni kufungwa Chuo kwa mgomo uliosababishwa na fujo hizi.

      Tukiwa huko nyumbani tukaletewa barua zenye neon liitwalo INTIMIDATION. Mimi ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kukutana na neno hili na ikabidi nifungue dictionary kulielewa.

      Sitaki kutaja nilipokea barua nikiwa mkoa gani. Lakini G211 nao walikuwa wamejipanga posta zote za miji mikubwa. Wakiona mwanachuo kaenda kupokea barua basi wanakuja na kufanya kavurugu kadogo ili wajue ulichoandikiwa. Walikuwa wameji-organise kama usalama wa taifa.

      Mimi nikaenda posta. Natoka kuchukua barua nikazungukwa na vijana wanne, wote ni katika kundi la G211. Wakata kujua barua niliyopokea. Kwa sababu nilikuwa mkoani na hatuko chuoni na mimi nikapata kiburi sikutaka kuwaonyesha nikawapuuza na kuwatishia kuwaitia polisi wakaachana na mimi.

      Nyumbani nikafanya masharti ya barua ile, kwamba kama nilitishiwa (intimidation) basi ni nani au kikundi gani kilitutishia. Mimi nikaona Mungu akupe nini maana ule mnyanyaso wa kuitwa TRAITORS tangu May 1994 hadi October 1994 nilishauchoka nikataja waziwazi kuwepo kwa kundi la G211 na jinsi walivyokuwa wakitunyanyasa kutufukuza hata madarasani kujisomea usiku (prep).

      Lecturer mmoja alinipa live kwamba barua yangu walii-discus at length.

      Mwanzaoni mwa December 1994 tukaitwa kurudi Chuoni, lakini Mutungirehi akiwa bado President of DARUSO. Effect ni kwamba wanafunzi zaidi ya 200 walisimiamishwa mwaka mzima wengi wao wakiwa ni wale G211.

      Ikaitishwa referendum kuchagua kuendelea na Mutungirehi regime au la na wengi wakachagua kuwa asiendelee na ukaitishwa uchaguzi mwingine.

      Siku moja nimekutana na Lugiko Mpelwa Karungubare akiwa CHADEMA, nikamkumbusha ule woga wake hadi akatuita tuingine madarasani akakataa kabisa kukumbuka.

      Ladislaus Malima aliyekuwa jasiri kunisukuma nisiingie kwenye mtihani mmeeleza kwenye thread nyingine kwamba alipopigwa mkwara kwenye mgomo wa Mutungirehi akanywea na wale wenzake G211 naye wakamuita TRAITOR.

      Haya ndiyo ninayoyakumbuka kuhusiana na sakata lile la wanafunzi wa Engineering { G211} na Benedict Mutungirehi. Samahani kwa Makala ndefu lakini imenibidi niyaseme haya.

    20. #139
      Ibambasi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th July 2007
      Location : Iponyamakalai - Isungang'holo
      Posts : 752
      Rep Power : 763
      Likes Received
      128
      Likes Given
      823

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Sweke ni Msukuma mmoja nakumbuka kwao ni Sengerema, Mwanza. Kwa sasa ana kampuni yake ya ujenzi na nadhani bado anaishi Sinza. Jamaa ni mbishi kweli kweli.

      SubiriJibu umenikumbusha baadhi ya watu ambao ukiwaona kwa sasa na siku zao za uanafunzi unabaki kucheka tu.

    21. #140
      Peele's Avatar
      Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Posts : 13
      Rep Power : 353
      Likes Received
      5
      Likes Given
      3

      Default

      Sweke was a great leader. Allisimama katika kile alichokiamini.sijamuona siku nyingi lakini naambiwa aliweka rekodi ya kuwa consulting engineer miaka Sita tu baada ya ku graduate. Sina hakika huwa anapita huku JF.
      Subirijibu anahitaji uponyaji wa nafsi. Sote binadamu tuna mwili, roho na nafsi. Uponyaji wa nafsi ni mgumu na muhimu kuliko ule wa mwili na Roho. Tuendelee kumuombea.

    Page 7 of 8 FirstFirst ... 5678 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...