Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

    Report Post
    Page 2 of 8 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 155
    1. #1
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By NYENJENKURU View Post
      Unakumbuka alipotolewa high table Nkrumah hadi akupoteza kiatu, jamaa alikuwa mkorofi sana, watu wanamvuta aondoke yeye akashikilia meza kidogo aanguke nayo kwenye stage, i think it was 1991 or 92 kama sikosei.
      Quote By NYENJENKURU View Post
      Yaani kuna vijana walioshiriki kumshusha huyo jamaa na kule FOE kaanza kumuita MUTUNGILAHELA aka Mnyamrenge..Siku hizi wengi ni Ma senior Engineers ukiwakumbusha wancheka sanaaaaa...kama John Peter...JP nk

      Thread hii inatofautiana na ile nyingine ya kuuliza kuhusu aliko Benedict Mutungirehi, aliyekuwa mbunge na sasa hatujui yuko wapi.

      {Mutungirehi; mwanasiasa mahiri kazimikia wapi?}

      Nimeamua kuweka thread mpya ili wengi wajue chanzo cha matukio yale kwa faida ya historia.

      Unajua hata wengi hawafahamu relation ya vijana wale wa Engineering (FOE) na kundi lililomtoa Mutungirehi pale stejini. Haya ni makundi mawili tofauti yaliyounganishwa na ile nia ya kumuondoa Mutungirehi.

      Sakata ya Mutungirehi ilitokea mwishoni mwa October 1994, lakini ili uielewe vizuri inabidi uanze na matukio ya tangu April 1994 yaani miezi sita nyuma. Mimi nilikuwa namalizia first year pale Engineering na hivyo ninalikumbuka suala hili vizuri sana.

      Kwa nini nianzie nyuma vile? Ni kwa sababu ninataka kuweka hisoria sawa kwani baadhi wanapotosha na wanajifanya siku hizi ni wapiganaji kwelikweli.

      Tuanze sasa maelezo. Mwezi April 1994 nikiwa first Year pale FOE tulikuwa na somo linaitwa Engineering Mathematics ambayo ilikuwa inafundishwa na walimu toka Mathematics depertment. Wakati huo ndiyo amemaliza kufunidha topics ngumu kichizi kama vile divergence, curl na kadhalika.

      Kisha yule lecture akatoa test ambayo ilikuwa ngumu haina mfano kwani mtu unafika mwisho wa time hujafanya swali hata moja. Lecture akatangaza kwamba muda wa paper umeisha. Mimi nilikuwa nachukua Civil Engineering nimekaa karibu na Bwana anaitwa Mziray. Mziray akaanzisha fujo kwa kumshika lecturer asikusanye zile paper.

      Mziray simkumbuki jina lake la kwanza ila najua alimaliza Kibaha High School, May 1993, akaenda JKT Oljoro na akaja UDSM. Pale Kibaha alikuwa PCM na aliondoka na Dv. One Point 5 yaani ABB.

      Kwa watu kama huyu kudhalilishwa kuibuka na zero kwenye Mathematics ilikuwa kejeli lakini ukweli ni kwamba test ilikuwa ni ngumu.

      Fujo ya Mziray zikaungwa mkono na wengi tu. Yule mwalimu akarudi Maths Dept. na huko akashitaki kwa mkuu wake yaani Prof. Masenge kwamba kafanyiwa fujo na vijana wa Engineering.

      Kumbuka ile test ndiyo ilikuwa ya mwisho wa mwaka. Si kama siku hizi nasikia wanasoma kwa semester, wakati ule test ile ilikuwa ya mwisho na kilichobaki ni tutorials chache kusubiri Unversity Exam. Vumilieni hadi mwisho maana hadi hapa hakuna connection yoyote na Mutungirehi.

      Hivyo, Prof. Masenge akato quotion kwamba Mathematics dept haitafundisha tena Engineering students hadi wa-apologise. Engineering tukakataa kuapologise.

      April ikaisha May ikaingia. May ndiyo ilikuwa mwezi wa University Exams. Tukafanya exams zingine lakini binafsi nilishapata dalili za kugoma kufanya Maths Exam. Hili niliambiwa na Marehemu Dr. Nzali ambaye nilienda kumfuata kuhusu ugonjwa wangu maana niliugua karibu niage dunia hivyo nikawa namtaarifu kuhusu unafuu wangu. Akaniambia nisijaribu kugoma.

      Kesho yake ikafika yaani siku ya Mathematics Exam. Tukaingia madarasani lakini walimu hawakuleta mitihani. Wakati huo sheria ya chuo inasema kuwa zikipita nusu saa basi unaweza kutoka nje ya chumba cha mtihani na hakuna mwingine kuingia.

      Nusu saa ikafika, tension ya wanafunzi ikaanza kupanda maana walimu hawakuja na hivyo tutaonekana first year wote hatukufanya paper na hivyo tumeji-ABSCOND.

      Tukakubaliana kuwa tutoke nje tujadili cha kufanya. Sasa hapa ndipo vurugu ya kwanza ilipoanzia. Class representatives wetu ninaowakumbuka walikuwa zaidi ya watatu yaani Lugiko Mpelwa karungubare (Chemical Engineering), Sweke (Civil Engieer), Hussein Kitilinga (Electrical Engineer). Wengine nimewasahau.

      Msiomjua Karungubare ni yule aliyegombea uenyekiti NCCR akapata kura moja na James Mbatia akashinda uenyekiti huo. Karungubare sasa hivi ni mwanachama mzuri tu wa CHADEMA.

      Wakati tumekaa pale chini hawa ma-class reps wakaitwa kujadili kwa Dean of faculty. Kumbe huko kwa Dean tayari Prof Masenge yuko huko na yule lecturer aliyefanyiwa vurugu. Binafsi sijui walifikaje kule.

      Pale chini tumeshajadili na kuamua kwamba sisi hatujagoma kufanya paper ila wao ndiyo wamekataa kuleta mtihani. Basi tukakaa tukiwa hatujui nini kitatokea. Mitihani huanza saa 3 lakini hadi wakati huo tayari ni saa 5 mchana.

      Ikafika mahala kila mmoja akaamua kuchukua uamuzi wake. Wapo walioamua kuondoka na kwenda mabwenini. Wakaulizwa “hivi nyinyi mnaondoka mtihani ukiletwa si mtakuwa mme-DISCO”. Wakajibu “fanyeni mtakavyoamua”!

      Wengine wakaamua kujiandaa na mtihani wa mchana au siku nyingine na hivyo wakabaki madarasani.

      Ilipofika nadhani saa 5:30 kumbe yale mazungumzo ya Prof. Masenge, Clas reps na daen yamemalizika na hivyo Prof. Masenge na timu yake wakaamua kugawa paper ili mtihani uanze. Wakaenda madarasani wakawakuta wale ambao walitulia kujiandaa na subjects zingine. Prof. na wenzake hawakujua kuwa kulikuwa na mtawanyiko wakagawa paper na waliomo wakaanza mtihani.

      Class reps wakaiona hali hii na waka-panic na kuja kwetu ambao tulikuwa nje. Ninayakumbuka vizuri maneno ya Karungubare kwamba “Jamani ingieni madarasani mkafanya paper maana tayari wenzetu wameshaana na zinasubiriwa tu dakika 30 milango ifungwe tusiingie tulioko nje

      Hapa ndipo likaanza sokomoko la mwaka. Binafsi nikataka kuhakikisha maneno ya Karungebare na ma-class reps wenzake. Tukaenda vyumba kadhaa. Kweli bwana wenzetu walikuwa wanafanya paper taratibu. Ingekuwa wote hatufanyi paper kwangu isingekuwa tatizo. Lakini tatizo ni pale baadhi walikuwa wanaifanya.

      Nikapiga kelele na wenzangu kadhaa nikisema “Jamani, tufanye moja kati ya mawili, ama tuwatoe kwa nguvu hawa wanaofanya paper ama tuingie na sisi tufanye”.

      Hakuna aliyejisumbua na huu ushauri wetu kwa sababu tulikuwa kama wanne tu kati ya kundi la watu zaidi ya 220. Nilipoona huu ni upuuzi nikatangaza “ni ujinga kusubiri na hivyo napanda ngazi kwenda kufanya paper nisije nikafukuzwa”. Nikaanza kupanda ngazi. Kumbe huyu Ladislaus Malima kanisikia na kuniona.

      Akanifuata amefura ajabu na kunisukuma akisema “Unajua wewe unacheza na Maisha ya watu, wale walioondoka utawafanya nini, unataka wafukuzwe”. Mimi nikajibu bila kujua kauli yangu imevutia wengi, nikasema “Wamekwenda wapi, si tulikubaliana tusiondoke. Sasa na wewe unasemaje kuhusu wanaofanya mtihani na hujawazuia”. Malima nikamzidi hoja na tension ikawa inazidi.

      Kumbe hata kundini mmojammoja akawa anachomoka na kwenda kufanya mtihani. Mimi pia nikapata nafasi nikaenda kufanya mtihani. Kumbe mtihani wenyewe ulikuwa mrahisi maana ndani ya dakika 30 nikawa nimeshanya maswali ambayo nimeshavuka passmark yaani 40%.

      Kumbe wakati tunafanya, kule nje dakika 30 zikawa zimeshapita na wakakubaliana kwamba waingie kwa nguvu kwenye vyumba vya mitihani, huko watatukuta sisi ambao kuanzia dakika hiyo tukaitwa TRAITORS, lakini wakubaliana wasitudhuru bali waichanechane mitihani ile ili ushahidi ukosekane unaoonyesha kuwa tulifanya paper na wao hawakufanya.

      Wakafanya hivyo. Lakini hawakujua wlaichokosea. Nilisema mwanzoni mtu kama mimi nilishajua tangu jana yake kuwa kungekuwa na harufu ya mgomo. Hivyo mtu ulikuwa ukiingia tu kwenye chumba cha mtihani kitu cha kwanza ilikuwa ni kuandikisha jina lako na signature. Hivyo fujo ilipoanza wale walikimbilia mitihani hawakujua kama huo ni ushahidi mwingine.

      Masenge na wenzake walichofanya wakachukua majina yote wakatoa photocopy ya majina ya wote tuliosaini, wakaacha copy kwa Dean of Engineering na original akaondoka nayo Prof. Masenge mwenyewe.

      Wakati Pro. Masenge anapanda kuondoka FOE grounds, mmoja wale wanafunzi akapata wao kwamba ushahidi wa list ya waliosaini hawana na anayo Masenge. Hivyo, akiondoka nayo wamekwisha. Wakaondoka kundi lote wakamzingira Prof. Masenge, wakamnyang’anya ile list ya majina na wakichanachana mbele yake.

      Terrible mistake hawakujua kuwa tayari kopi ipo kule kwa Dean. Hapa ndipo hawa wanafunzi 211 walipokosea na sijui kama walikuja kuligundua hili.

      Baada ya siku mbili, ikatangazwa list ya watu 72 na 211. 72 walikuwa ni sisi ambao tulifanya mtihani na tulitakiwa kuendelea kuwepo chuoni. Na wale 211 ni wale waliofanya fujo zile wakatakiwa kuondoka chuoni kwani walifukuzwa.

      Ndipo yakazuka majina mawili maarufu yaani G211 na TRAITORS. G211 walijiita hivyo kwa sababu mwaka mmoja nyuma bungeni kulikuwa na kundi la G55 la wabunge waliotaka hoja ya serikali ya Tanganyika iliyozimwa na Nyerere.

      Mimi kama na wenzangu 72 tukaendelea na Maisha ya Chuo. Wale G211 wakafungua kesi Mahakamani. Kundi la G211 lilikuwa na watu wengi sana. Nimeshamtaja Karungubare (CHADEMA), Sweke, Kitilinga ambaye sijui yuko wapi lakini mara ya mwisho alikuwa OTIS kampuni inayoshughulika na lifts za majengo.

      Wengine ni Phenihas Magesa ambaye nadhani ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Mwanza na mwaka 2009 aligombea ubunge jimbo la Busanda akashindwa na Lorencia Bukwimba wa CCM. Phenihas alikuwa kinara mzuri

      Kesi ya hawa ilendelea hadi nadhani mwishoni mwa September 1994 na wakashinda na wakarudishwa Chuoni. Wakaja huku tunaanza second year na wako very enthusiastic kukishinda Chuo. Hakika walitamba. Wakanunu T-Shirt zimeandikwa G211 kama ambavyo sasa zimeenea zilizoandikwa DHAIFU. Kurudi kwao ilikuwa fahari kwao na huzuni kwetu. Si huzuni kuwa tulipenda, bali walikuwa ni kero kila tulipopita.

      Tukakaa tumenuaniana yaani TRAITORS na G211. Faculty of Engineering au FOE second year tukawa katika makundi hayo mawili. Ninakumbuka siku moja nimeenda kusoma prep darasa moja wakaja wakanifukuza kwa sababu TRAITORS tulipigwa marufuku hakuna ku-study kule FOE.

      Hali ikadumu hivyo kwa nusu mwezi. Ndipo likaja sakata la Mutungirehi. Maadui wa Mutungirehi wakaona kundi pekee lenye uamsho na zuri kulitumia ni hili la G211.

      Kuanzia hapa wengi mnajua yaliyotokea. Mutungirehi akavurumishwa stejini kama thread moja inavyosimuliwa humu. Lakini players wakuu walikuwa ni hawa G211 ingawa wanachuo wengi walidhani ni vijana wote wa engineering. Si kweli, sisi tulioitwa TRAITORS hatukufurahia vurugu kwa Mutungirehi. Kilichofuata ni kufungwa Chuo kwa mgomo uliosababishwa na fujo hizi.

      Tukiwa huko nyumbani tukaletewa barua zenye neon liitwalo INTIMIDATION. Mimi ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kukutana na neno hili na ikabidi nifungue dictionary kulielewa.

      Sitaki kutaja nilipokea barua nikiwa mkoa gani. Lakini G211 nao walikuwa wamejipanga posta zote za miji mikubwa. Wakiona mwanachuo kaenda kupokea barua basi wanakuja na kufanya kavurugu kadogo ili wajue ulichoandikiwa. Walikuwa wameji-organise kama usalama wa taifa.

      Mimi nikaenda posta. Natoka kuchukua barua nikazungukwa na vijana wanne, wote ni katika kundi la G211. Wakata kujua barua niliyopokea. Kwa sababu nilikuwa mkoani na hatuko chuoni na mimi nikapata kiburi sikutaka kuwaonyesha nikawapuuza na kuwatishia kuwaitia polisi wakaachana na mimi.

      Nyumbani nikafanya masharti ya barua ile, kwamba kama nilitishiwa (intimidation) basi ni nani au kikundi gani kilitutishia. Mimi nikaona Mungu akupe nini maana ule mnyanyaso wa kuitwa TRAITORS tangu May 1994 hadi October 1994 nilishauchoka nikataja waziwazi kuwepo kwa kundi la G211 na jinsi walivyokuwa wakitunyanyasa kutufukuza hata madarasani kujisomea usiku (prep).

      Lecturer mmoja alinipa live kwamba barua yangu walii-discus at length.

      Mwanzaoni mwa December 1994 tukaitwa kurudi Chuoni, lakini Mutungirehi akiwa bado President of DARUSO. Effect ni kwamba wanafunzi zaidi ya 200 walisimiamishwa mwaka mzima wengi wao wakiwa ni wale G211.

      Ikaitishwa referendum kuchagua kuendelea na Mutungirehi regime au la na wengi wakachagua kuwa asiendelee na ukaitishwa uchaguzi mwingine.

      Siku moja nimekutana na Lugiko Mpelwa Karungubare akiwa CHADEMA, nikamkumbusha ule woga wake hadi akatuita tuingine madarasani akakataa kabisa kukumbuka.

      Ladislaus Malima aliyekuwa jasiri kunisukuma nisiingie kwenye mtihani mmeeleza kwenye thread nyingine kwamba alipopigwa mkwara kwenye mgomo wa Mutungirehi akanywea na wale wenzake G211 naye wakamuita TRAITOR.

      Haya ndiyo ninayoyakumbuka kuhusiana na sakata lile la wanafunzi wa Engineering { G211} na Benedict Mutungirehi. Samahani kwa Makala ndefu lakini imenibidi niyaseme haya.
      JokaKuu, fide1975, Nyunyu and 10 others like this.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    2. #21
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By muonamambo View Post
      Ndugu Subirijibu.... Nimesikitishwa sana na ujasiri wa kutetea uwoga wako na utraitor wako... mimi ni miongoni mwa G211 na ni mmoja wa viongozi tuliongoza kundi la G211 NA KUSHINDA KESI DHIDI YA CHUO... Naikumbuka sana historia hii na haitakuja kutoka kichwani pangu.... sina haja ya kurudia historia nzima hila napenda kukufahamisha haya machache kwa faida ya wana Jf na kuweka kumbukumbu sahihi..

      Tuna kila sababu ya kuwaita nyinyi matraitor kwa sababu .... sheria za chuo zilieleza wazi kwamba mtihani ukichelewa au mwanachuo akichelewa kufika kwenye chumba cha mtihani kwa zaidi ya dk 30 hataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha mtihani na vilevile mtihani ukichelewa kwa dk 30 ... wanafunzi wanaweza kutoka kwenye chumba cha mtihani unless kuna taarifa za kuchelewa kwa mtihani... Tukio lilivyotokea ni kwamba mtihani ulichelewa zaidi ya masaa 2 na bila taarifa YOYOTE.
      Muonamambo,
      Hapa ndipo hata anayesoma thread hii anapoona mlikosea. Ukiichukulia kama unavyoileta unaweza kudhani ni kweli mtihani ulichelewa na hakukuwa na taarifa yoyote.

      Ni kweli mtihani ulichelewa. Lakini je ni kweli hukuwa na taarifa yoyote? Kama hukuwa na taarifa yoyote ulikuwa unafanya nini eneo la FOE tena mmekaa kundi kubwa mnaongelea tukio hilo?

      Usidanganye watu hapa. Nimesema na haujakanusha ni kwamba mzozo huo ulianza mwezi April na mliujua. Taarifa mlishaambiwa kwamba Mathematics Department haita-liaise na Engineering first year hadi wa-apology. Hukupata taarifa hii?

      OK, siku ya mtihani, tulikusanyika pale nje na tukakubaliana tusiondoke hadi tujue Class Reps wamekubaliana nini na Lecturers. Ulitaka taarifa gani wakati viongozi wako wako mazungumzoni na hujapata feedback.

      Halafu unasema kuwa ni u-traitor nione aibu. Nitaonaje aibu kutetea history ambayo mmeipotosha kwa miaka mingi.

      Tatizo lenu ni kwamba hata kwenye mikutano hamkutaka wenzenu tutoe hoja mkawa mnatumia ubabe na kuzomea mkipewa vipande.

      Unakumbuka bwana mmoja alieleza walimu walivyowakuta darasani mkamzomea na kumuita "WA NDANI WA NDANI WA NJE WA NJE".

      Lete hoja tusahishe history.

      Quote By muonamambo View Post
      SOTE tulikubaliana ya kwamba tusiendelee na mtihani hule na kwa vile wengine walikuwa na mitihani inayofuata muda wa mchana... sasa matraitor wachache kama wewe mliendelea kufanya mtihani hata baada ya kuletwa masaa ma 3 baadaye..
      Uongo ambao unapimwa kwa kitu kidogo tu. Kama wote tulikubaliana, iweje wale Class reps wakae kule ofisini waki-discuss jambo lile. Unataka kutuambia wakati Sweke, Karungubare na Kitilinga mlishawapindua mkaweka resolution yenu nyingine kabisa.

      Na kama mlishakubaliana si mngeondoka mlikuwa mnasubiri nini maeneo yale huku mitihani mingine ikiwasubiri jioni. Uongo mtupu.

      Quote By muonamambo View Post
      Hata baada ya kuendelea na mtihani, tuliokuwa nje tuliwasihi mtoke ili tuwe na msimamo wa pamoja nanyi mliweka masilahi yenu mbele kama mafisadi na kusahau masilahi ya wengi..

      Ona unavyojichanganya katika jambo hili. Sasa kama sisi tulikuwa ndani ya exam room na nyinyi mlikuwa nje, mlitusihi kwa mawasiliano gani. Kwamba mlikuwa mnakuja darasani mnatutangazia halafu sisi tunakataa?

      Huu ni uongo ambao kila anayejua logistics za mtihani ataung'amua. Ukiingia kwenye exam room mtu wa kwanza kukutana naye ni msimamizi au invigilator. Sasa mliwezaje kumvuka invigilator aache kusimamia exam awape muda mtangaze azama yenu kututaka tuache mtihani kisha akawaruhusu mtoke ili sisi ama tukubali ama tuache.

      Ni uogo ambao hauwezekani. Kilichotokea inawezekana kweli mlikuwa mnatuma watu kuja kututoa. Lakin badala yake watu hao wakifika mlangoni wanaona kila mtu amejipinda kwenye pen wanaajiunga pia kuwa na sisi. Na bahati yenu sheria ilikuwa ni nusu saa lakini ingekuwa zaidi basi wengi tu wangechomoka huko kwenu wakaja kufanya paper maana tatizo la wengi walidhani kutokana na mzozo basi Mathematics wametukomoa ili tufeli lakini mtihani ule kumbe ulikuwa rahisi na kila mtu angefaulu.

      Quote By muonamambo View Post
      Napenda kuwapongeza tena wana G211 kwa moyo wa kizalendo na wa kijasiri wa kuungana pamoja dhidi ya udhalimu wa chuo/serikali na kushinda ... nawatakia kila la heri kwenye shughuli zenu na mungu akipenda aweze kutuunganisha tena ili tushinde vita dhidi ya ufisadi kwani naamini bado mnaendeleza mapambano huko mliko
      Hapa ndipo mlipopotoka. Nimeeleza kirefu hadi inachosha lakini lengo langu ieleweka kuwa mzozo haukuwa na sura yoyote ya kisiasa au hata kiutawala.

      Mbona hata siku moja hamkutaka tuujulishe umma kwamba chanzo cha mzozo ni ile test ngumu ya vector calculus yenye curl na divergence. It was a pure academical matter and never administrative or political.
      JokaKuu likes this.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    3. #22
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By mambomengi View Post
      Muonamambo ni kweli ndio maana mlishinda kesi kirahisi.
      Halafu pia sijapenda huyu bwana aka traitor anasema wazi majina ya watu huku lake lipo kapuni, mods huyu traitor anastahili ban walau ya siku 3, kwa kuwa bado analeta utraitor.
      All in all, well said Muonamambo.
      Niliowataja wote walikuwa public figure. Mfano kama ulikuwa kiongozi pale utaachaje kukwepwa kujulikana. Nimemtaja Phenihas Magesa, je hakuwepo kama mshiriki kwenye kesi mliyofungua.

      Nimemtaja Hussein Kitilinga, Sweke, na Lugiko Karungubare kama viongozi yaani class representative wakati ule, kuna tatizo gani katika hilo.

      Nimemtaja Godwin Ngwilimi ambaye ni mwanasheria sasa pale TANESCO, je hakuwa pale pembeni ya Mutungirehi katika varangati ile.

      Ukiwa kiongozi hata ukiranja wa darasa moja huko primary school basi history itaandikwa hivyohivyo na watakaoipenda wataisoma hivyohivyo.

      Kwanza mjiulize kwa nini nimeanzisha thread hii. Ni kwa sababu kuna thread nyingine inaelezea kwa juu sana kuhusu hili nikaona tuumwage ukweli kamili. Thread imetaja G211 na Mutungirehi.

      Mbona Mutungirehi mmemtaja na nyinyi hamjitaji. Si kwamba mnaonyesha ule ubabe wenu wa FOE ambao nilidhani maisha yameubadilisha kumbe bado mko vilevile.

      Tunatakiwa tuweke sawa historia. Binafsi sikupenda lilivyopotoshwa wakati uhalisi ninaujua.

      Mbona nyinyi mmetuita TRAITORS kwa miaka. Tunachofanya sasa ni kuonyesha kwamba hakukuwa na kitu kilichosababisha tuitane traitor au shujaa.

      Tunapigana kuondoa ufisadi. Hebu waangalie pale Bungeni akina John Mnyika, Zitto, Wenje, Halima Mdee na wenzao. Je wanatumia njia za kibabe? Huwezi kutumia ubabe kwa mtu mwenye dola na silaha zote?

      Wanatumia akili zao na kanui hadi Anne Makinda hana hamu nao tena.
      Last edited by SubiriJibu; 30th June 2012 at 18:55.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    4. #23
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,543
      Rep Power : 6185
      Likes Received
      3103
      Likes Given
      1025

      Default

      Quote By TUMBIRI View Post
      Kimbunga njoo mjadiliane na Classmates wenzako. Sisi UDSM tulipita enzi za kina Mtatiro na Mwita Mwikwabe. Hatuna cha kuchangia hapa.
      Mkuu TUMBIRI jamaa kasema maneno ya kweli kabisa kabisa. Unajua kuna kitu kingine kilikuwa kule FOE, mtihani ukionekana mgumu tu basi linaanzishwa kunji la kufa mtu ili watu wakajiandae upya! Sweke alikuja kuwa presidaa wa Daruso baada ya Lenganasa aliyechikua mikoba ya Mutungihela. Story hiyo imenimumbusha mbali sana; akina Eng. Peter, Malima (huyu kwa sasa anaongoza kitengo kimoja huko serikalini). Mtoa mada safi sana kwa kuweka kumbukumbu sawa.
      GP, SubiriJibu and Maundumula like this.

    5. #24
      muonamambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd September 2010
      Posts : 568
      Rep Power : 559
      Likes Received
      179
      Likes Given
      946

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By SubiriJibu ;Hapa ndipo hata anayesoma thread hii anapoona mlikosea. Ukiichukulia kama unavyoileta unaweza kudhani ni kweli mtihani ulichelewa na hakukuwa na taarifa yoyote.

      Ni kweli mtihani ulichelewa. Lakini je ni kweli hukuwa na taarifa yoyote? Kama hukuwa na taarifa yoyote ulikuwa unafanya nini eneo la FOE tena mmekaa kundi kubwa mnaongelea tukio hilo?

      Usidanganye watu hapa. Nimesema na haujakanusha ni kwamba mzozo huo ulianza mwezi April na mliujua. Taarifa mlishaambiwa kwamba Mathematics Department haita-liaise na Engineering first year hadi wa-apology. Hukupata taarifa hii?

      OK, siku ya mtihani, tulikusanyika pale nje na tukakubaliana tusiondoke hadi tujue Class Reps wamekubaliana nini na Lecturers. Ulitaka taarifa gani wakati viongozi wako wako mazungumzoni na hujapata feedback.

      Halafu unasema kuwa ni u-traitor nione aibu. Nitaonaje aibu kutetea history ambayo mmeipotosha kwa miaka mingi.

      Tatizo lenu ni kwamba hata kwenye mikutano hamkutaka wenzenu tutoe hoja mkawa mnatumia ubabe na kuzomea mkipewa vipande.

      Unakumbuka bwana mmoja alieleza walimu walivyowakuta darasani mkamzomea na kumuita "[B
      WA NDANI WA NDANI WA NJE WA NJE[/B]".

      Lete hoja tusahishe history.

      Uongo ambao unapimwa kwa kitu kidogo tu. Kama wote tulikubaliana, iweje wale Class reps wakae kule ofisini waki-discuss jambo lile. Unataka kutuambia wakati Sweke, Karungubare na Kitilinga mlishawapindua mkaweka resolution yenu nyingine kabisa.

      Na kama mlishakubaliana si mngeondoka mlikuwa mnasubiri nini maeneo yale huku mitihani mingine ikiwasubiri jioni. Uongo mtupu.

      Ona unavyojichanganya katika jambo hili. Sasa kama sisi tulikuwa ndani ya exam room na nyinyi mlikuwa nje, mlitusihi kwa mawasiliano gani. Kwamba mlikuwa mnakuja darasani mnatutangazia halafu sisi tunakataa?

      Huu ni uongo ambao kila anayejua logistics za mtihani ataung'amua. Ukiingia kwenye exam room mtu wa kwanza kukutana naye ni msimamizi au invigilator. Sasa mliwezaje kumvuka invigilator aache kusimamia exam awape muda mtangaze azama yenu kututaka tuache mtihani kisha akawaruhusu mtoke ili sisi ama tukubali ama tuache.

      Ni uogo ambao hauwezekani. Kilichotokea inawezekana kweli mlikuwa mnatuma watu kuja kututoa. Lakin badala yake watu hao wakifika mlangoni wanaona kila mtu amejipinda kwenye pen wanaajiunga pia kuwa na sisi. Na bahati yenu sheria ilikuwa ni nusu saa lakini ingekuwa zaidi basi wengi tu wangechomoka huko kwenu wakaja kufanya paper maana tatizo la wengi walidhani kutokana na mzozo basi Mathematics wametukomoa ili tufeli lakini mtihani ule kumbe ulikuwa rahisi na kila mtu angefaulu.

      Hapa ndipo mlipopotoka. Nimeeleza kirefu hadi inachosha lakini lengo langu ieleweka kuwa mzozo haukuwa na sura yoyote ya kisiasa au hata kiutawala.

      Mbona hata siku moja hamkutaka tuujulishe umma kwamba chanzo cha mzozo ni ile test ngumu ya vector calculus yenye curl na divergence. It was a pure academical matter and never administrative or political.
      subirijibu:

      1. Acha kupotosha watu sheria za chuo ziko wazi kwamba mtihani ukichelewa zaidi ya dk 30 bila taarifa maalum basi mwanachuo anaruhusiwa kutoka kwenye chumba cha mtihani. mtihani wa engineering mathematics ulichelewa zaidi ya masaa 2 na taarifa pia zilichelewa zaidi ya dk 30....
      2. Kitendo cha watu kubakia FOE hakina uhusiano na taarifa ya mtihani kuchelewa ... ni kweli class reps walikuwa na discusion na uongozi kuhusu kanuni na nini kifanyike baada ya mtihani kuchelewa bila taarifa... uongozi wa chuo uliamua kuficha udhaifu wao na kuamuru mtihani ukafanywe na hata watu wachache waliopo baada ya masaa 3 nje ya muda wa kawaida wa kuanza mtihani... kuwepo kwa wanachuo FOE kuansababu nyingi kwanza ni chuo chao pili bado wengine tulikuwa tunajiandaa na mitihani mingine... sasa ulitaka tukajiandaye wapi?...
      3. habari ya mzozo wa APRIL wewe ndio unaijua na kamwe huwezi kuhihusisha na mtiani wa UE Kwani mtihani unakuja kutokana na syslbus iliyofundishwa .... hivyo ni upotoshaji mkubwa kuhusisha issue ya nyuma na mtihani wa sasa
      4. kama kweli mlikuwa mnathamini walio wengi ambao ni 211 kati yenu 72 .. basi mngetoka nje na kuungana na wenzenu lakini narudia kusema mliweka masilahi yenu mbele na kusahau kuwa mligawanywa ili mtawalike kirahisi na uzembe wa uongoozi wa chuo...
      5. napata mashaka na utetezi wako kwamba kwa nini tuliendelea kukaa FOE nimeshakwambia vilevile hatukuwa na sababu ya kuondoka kwani hapo palikuwa ni chuoni petu, pili watu tulikuwa tuanajiandaa na mtihani mingine...
      6. Suala la class reps kuzungumza na uongozi haliondoi uhalali wa hoja kwamba uongozi ulichemsha na kama sheria inavyosema kwamba mtihani ulitakiwa kuhahirishwa kutokana na kuchelewa bila taarifa yoyote... kama ilivyokuwa kwamba yoyote aliyechelewa kuingia kwenye chumba cha mtihani alikatazwa kufanya hivyo...
      7. mazungumzo ya class reps na uongozi yalikuwa ni ya lazima kwani tatizo lilishatokea na safari hii lilifanya na chuo... hivyo walitaka kujua outcomes yake..lakini haki yetu ilikuwa palepale na ndio maana tukashinda MAHAKAMANI
      8. nakupa tu ushauri wa bure kubali kiiungwana kwamba ulichemsha kwa kuwa traitor na hiyo haikupunguzii mwili wako bali inakuweka katika jamii ya watu wasioaminika kwa manufaa ya wengi...

    6. #25
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By JokaKuu View Post
      ..waliokosea ni viongozi/wawakilishi waliokubali mtihani uanze baada ya kuchelewa masaa 3++.

      ..pia lazima tukubali kwamba kuna mahusiano mabaya kati ya waalimu na wanafunzi hapo UDSM.

      ..hali ya kuogopana, kutishana, kuwindana, kupigana, haifai ktk mazingira ya kisomi.
      Nakubaliana na wewe mkuu,

      Ila kama hukuwepo labda nirudie jambo moja kulieleza. Nimeeleza kwamba unajua hawa mabwana wanaojiita G211 walitaka ionekane kaan kwamba tatizo lilianza siku ileile ya mtihani. Ingekuwa hivyo kusingetokea yale yote kwani sheria ilikuwa ni wazi kabisa kwamba dakika 30 unaweza kuondoka.

      Labda nirudie narration kwamba siku hizi nasikia wamenaisha semester system ambapo University Exam unafanya ndani ya semester moja mnamalizana na somo hilo.

      Siku zile haikuwa hivyo. Somo kama Engineering Maths au lolote mlikuwa mnalisoma ndani ya terms tatu. Kila term mnasoma kama 10 weeks kisha mnafanya test halafu mnafunga Chuo kwa wiki mbili, first term inaisha. Term ya pili inakuwa hivyohivyo.

      Third term ilikuwa tofauti kidogo. Ni kwamba baada ya kufanya test hatukufunga bali tulikuwa tunakaa wiki mbili tunajiandaa kwa General Unversity Examination. Yaani exam inafanywa mara moja tu kwa mwaka kwa somo lolote.

      Zile test tatu zilichukuliwa kama coursework for 50% weight.

      Tatizo lililojitokeza hapa ni ile third term test ya Mathematics. Ndipo ikawa ngumu na fujo ikafanyika na Maths Dept wakatoa written warning kuwa hawatafundisha au kutoa exams kwa Engineering first year.

      Hiyo ni April 1994 wakati University Exam tulitakiwa kufanya May 1994. Hivyo kulikuwa na gap ya more than two weeks mzozo ukijulikana upo.

      Halafu hawa wanadanganya umma ili ionekane kana kwamba lilikuwa tatizo la siku ileile ya kufanya mtihani yaani May 1994. Na kwa kweli walifanikiwa sana kupata waumini wengi wa kuamini propoganda yao tena kwa miaka mingi na hadi leo bado hawaoni aibu kujiita mashujaa.

      Mimi hata ningekuwa upande wao wa G211 bado ningeona aibu kwa sababu siwezi kuficha ukweli ule miaka mingi ila kuona aibu wakati nikijua kuna wengi tu wanaujua.
      Last edited by SubiriJibu; 30th June 2012 at 19:16.
      JokaKuu likes this.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    7. #26
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,543
      Rep Power : 6185
      Likes Received
      3103
      Likes Given
      1025

      Default

      Quote By SHIMBONONI View Post
      Mkuu SubiriJibu,

      Umenikumbusha miaka ile ya Dhahabu UDSM! Mutungirehi alichaguliwa kwa Kishindo kuwa Rais wa DARUSO late 1993 na kuwa TRAITOR wa Magamba baada ya kupta safari ya Uholanzi au Hungary mwenye kumbukumbu sahihi atasaidia.

      Siku ile aliposhushwa High table kuna kijana mmoja alisimama akasema " you were elected democratically ....now you are also rejected democratically " Nakumbuka kijana huyo then aliitwa NIPASHE. Najua Wakuu wengine kama Eliakim Maswi na Sylvester Sweke watakumbuka vema tukio hili. Sijui wamo humu au wanapita hapa?
      Mkuu umenikumbusha juu ya NIPASHE. Huyu alikuwa Faculty of Education aliitwa nipashe kwa kuwa alikuwa na masikio makubwa kama kikatuni kimoja cha nipashe kilichokuwa kinatoka kwenye gazeti moja. Nilikutana naye akiwa ni mwalimu tukaliga mvinyo tukikumbuka hiyo hadithi. Sweke nilikutana naye akiwa ni mhandisi kwenye kampuni moja ya ushauri (consultancy). Enzi hizo bwana sijui kama bado zipo; rejected democratically!

    8. #27
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,915
      Rep Power : 2990
      Likes Received
      2548
      Likes Given
      3634

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By SubiriJibu View Post
      Niliowataja wote walikuwa public figure. Mfano kama ulikuwa kiongozi pale utaachaje kukwepwa kujulikana. Nimemtaja Phenihas Magesa, je hakuwepo kama mshiriki kwenye kesi mliyofungua.

      Nimemtaja Hussein Kitilinga, Sweke, na Lugiko Karungubare kama viongozi yaani class representative wakati ule, kuna tatizo gani katika hilo.

      Nimemtaja Godwin Ngwilimi ambaye ni mwanasheria sasa pale TANESCO, je hakuwa pale pembeni ya Mutungirehi katika varangati ile.

      Ukiwa kiongozi hata ukiranja wa darasa moja huko primary school basi history itaandikwa hivyohivyo na watakaoipenda wataisoma hivyohivyo.

      Kwanza mjiulize kwa nini nimeanzisha thread hii. Ni kwa sababu kuna thread nyingine inaelezea kwa juu sana kuhusu hili nikaona tuumwage ukweli kamili. Thread imetaja G211 na Mutungirehi.

      Mbona Mutungirehi mmemtaja na nyinyi hamjitaji. Si kwamba mnaonyesha ule ubabe wenu wa FOE ambao nilidhani maisha yameubadilisha kumbe bado mko vilevile.

      Tunatakiwa tuweke sawa historia. Binafsi sikupenda lilivyopotoshwa wakati uhalisi ninaujua.

      Mbona nyinyi mmetuita TRAITORS kwa miaka. Tunachofanya sasa ni kuonyesha kwamba hakukuwa na kitu kilichosababisha tuitane traitor au shujaa.

      Tunapigana kuondoa ufisadi. Hebu waangalie pale Bungeni akina John Mnyika, Zitto, Wenje, Halima Mdee na wenzao. Je wanatumia njia za kibabe? Huwezi kutumia ubabe kwa mtu mwenye dola na silaha zote?

      Wanatumia akili zao na kanui hadi Anne Makinda hana hamu nao tena.
      SubiriJibu,

      ..tatizo hapo ni watu wazima kama Prof.Masenge kushindwa kutumia busara.

      ..mkutano wa wahadhiri na wawakilishi wa wanafunzi ulipaswa kupanga tarehe mpya ya mtihani.

      ..mimi nadhani muweke pembeni hii habari ya "traitors" na "G211" halafu mjiulize kama wahadhiri really acted like guardians and grown ups ktk kulazimisha mtihani ufanyike ukiwa umechelewa 3++ hrs.

      ..hapo inaonesha kabisa kwamba wahadhiri walikuwa na nia mbaya kwa kutaka kuwakosesha baadhi ya wanafunzi nafasi ya kufanya mtihani.

      ..UDSM wanakuja wanafunzi toka background mbalimbali na mashinikizo kibao ktk maisha yao. sasa wahadhiri na watawala wanatumia hali ya wanafunzi kuwalazimisha kutimiza matakwa yao.

    9. #28
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,915
      Rep Power : 2990
      Likes Received
      2548
      Likes Given
      3634

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By SubiriJibu View Post
      Nakubaliana na wewe mkuu,

      Ila kama hukuwepo labda nirudie jambo moja kulieleza. Nimeeleza kwamba unajua hawa mabwana wanaojiita G211 walitaka ionekane kaan kwamba tatizo lilianza siku ileile ya mtihani. Ingekuwa hivyo kusingetokea yale yote kwani sheria ilikuwa ni wazi kabisa kwamba dakika 30 unaweza kuondoka.

      Labda nirudie narration kwamba siku hizi nasikia wamenaisha semester system ambapo University Exam unafanya ndani ya semester moja mnamalizana na somo hilo.

      Siku zile haikuwa hivyo. Somo kama Engineering Maths au lolote mlikuwa mnalisoma ndani ya terms tatu. Kila term mnasoma kama 10 weeks kisha mnafanya test halafu mnafunga Chuo kwa wiki mbili, first term inaisha. Term ya pili inakuwa hivyohivyo.

      Third term ilikuwa tofauti kidogo. Ni kwamba baada ya kufanya test hatukufunga bali tulikuwa tunakaa wiki mbili tunajiandaa kwa General Unversity Examination. Yaani exam inafanywa mara moja tu kwa mwaka kwa somo lolote.

      Zile test tatu zilichukuliwa kama coursework for 50% weight.

      Tatizo lililojitokez hapa ni ile third term test ya Mathematics. Ndipo ikawa ngumu na fujo ikafanyika na Maths Dept wakatoa written warning kuwa hawatafundisha au kutoa exams kwa Engineering first year.

      Hiyo ni April 1994 wakati University Exam tulitakiwa kufanya May 1994. Hivyo kulikuwa na gap ya more than two weeks mzozo ukijulikana upo.

      Halagu hawa wanadanganya umma ili ionekane kana kwamba lilikuwa tatizo la siku ileile ya kufanya mtihani. Na kwa kweli walifanikiwa sana kupata waumini wengi wa kuamini propoganda yao tena kwa miaka mingi hadileo bado hawaoni aibu kujiita mashujaa.

      Mimi hata ningekuwa upande wao wa G211 bado ningeona aibu maana siwezi kuficha ukweli huo miaka mingi ila kuona aibu wakati nikijua kuna wengi tu wanaujua.

      SubiriJibu,

      ..I hear u loud and clear.

      ..naona matatizo kila mahali kuanzia na huo mtihani ambao hakuna mwanafunzi alikuwa na uwezo wa kuufanya.

      ..mtihani ungekuwa umetungwa na mhadhiri tofauti na yule aliyefundisha basi hali iliyotokea ingeeleweka.

      ..kama umesoma nje ya Tanzania ktk level ya chuo kikuu, utakuwa shahidi kwamba hakuna mambo kama hayo ktk nchi za wenzetu.

      ..kwenye nchi za wenzetu lecturers r FIRM but FAIR. unakuta mhadhiri anatunga mtihani ambao unaweza kuchekecha A students, B students, etc etc.
      Maundumula likes this.

    10. #29
      Kasimba G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 19th January 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 918
      Rep Power : 610
      Likes Received
      277
      Likes Given
      265

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Mimi nilikuwa g211, nilikuwa ndani lakini kwa kuona uchungu wa wenzangu nikatoka nje, nikawasihi wengine watoke mmmh!

    11. #30
      Kasimba G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 19th January 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 918
      Rep Power : 610
      Likes Received
      277
      Likes Given
      265

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Tatizo lilikuwa ni kukosa ujasiri na woga, wangetoka darasani wote tatizo lisingekuwepo, kosa lilkuwa la math dept!
      JokaKuu likes this.

    12. #31
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Mkubwa Muonamambo,

      Kwanza habari ya miaka mingi, maana controversty ya thread isitufanye tukasahau kwamba sisi ni classmates. Naamini uliko maisha yanaenda na mimi nasukuma gurudumu la maisha.

      Kuna mmoja kwenye ile thread amesema waliomvua tai Mutungirehi weng sasa ni senior engineers. Ni kweli mimi ni Senior Engineer mahala fulani japo wengine nasikia mlishabadili fani.

      Tuje kwenye last post yako. Kadiri post zinavyotiririka kuna kila dalili za kukubaliana na nilichosema na kilichofichwa kwa miaka mingi. Naanza kujibu point moja hadi nyingine kama ifuatavyo:

      Quote By muonamambo View Post
      Kitendo cha watu kubakia FOE hakina uhusiano na taarifa ya mtihani kuchelewa ... ni kweli class reps walikuwa na discusion na uongozi kuhusu kanuni na nini kifanyike baada ya mtihani kuchelewa bila taarifa... uongozi wa chuo uliamua kuficha udhaifu wao na kuamuru mtihani ukafanywe na hata watu wachache waliopo baada ya masaa 3 nje ya muda wa kawaida wa kuanza mtihani... kuwepo kwa wanachuo FOE kuna sababu nyingi kwanza ni chuo chao pili bado wengine tulikuwa tunajiandaa na mitihani mingine... sasa ulitaka tukajiandaye wapi?...
      Nashukuru kukubali kwamba class rep walikuwa wanajadili hilo. Hivyo sijakanushwa nimethibitisha ninasema ukweli. Lakini class reps outcome ndiyo ilikuwa resolution yetu hata kama tatizo lisingeanzia April. Kama ni kweli baadhi mlikuwa na msimamo bila kujali matokeo ya majadiliano ya class reps na Chuo, basi ni wazi tayari huo ni mgawanyiko tosha kwamba humuhumo mliojiita G211 mliona umuhimu ni sovereignity yenu na wengine walsha-surrender sovereignity kwa class reps.

      Unasema kuwa mlibaki FOE kujiandaa na mitihani mingine. Huu ni uongo mkubwa unaoweza kusadikiwa na asiyejua mazingira ya pale siku ile.

      Kumbuka kwamba University Exam ilikuwa inafanyika kipindi kimoja kwa Chuo kizima. Madarasa yalikuwa hayatoshi kiasi kwamba tuliowatania kwa jina la Mangwini walikuwa inawabidi kuja kufanyia exams kule kwetu FOE.

      Hivyo hakukuwa na darasa lililokuwa wazi zaidi ya yale ambayo tulikuwa tufanyie exam na ambayo nyinyi na hata mimi mwanzoni tulishatoka.

      Kwa ujumla mlikuwa revolution Square ndogo ya kule FOE nikiruhusiwa kuiita hivyo. Yaani kilie kilichozoeleka kufanyika kule Revolution Square pale Cafeteria ndicho kilikuwa kinaendelea.

      Hakukuwa na mjadala wa masomo kujadili next subjects wakati hakuna aliyekuwa anajua whata next hasa kwa waliokuwa nje kama mimi na wewe.

      Wale waliobaki ndani ndiyo ninasema wangeweza kusema walikwua wana-study for next exam.

      Lakini nikukumbushe tena ni kwamba hakukuwa na makubaliano kuwa tutoke chumba cha mtihani kama mtihani utachelewa. Ndiyo maana wengine walibaki hadi Prof. Masenge alipowakuta.

      Quote By muonamambo View Post
      habari ya mzozo wa APRIL wewe ndio unaijua na kamwe huwezi kuhihusisha na mtiani wa UE Kwani mtihani unakuja kutokana na syslbus iliyofundishwa .... hivyo ni upotoshaji mkubwa kuhusisha issue ya nyuma na mtihani wa sasa

      Kwa hiyo mnataka watu waamini ilikuwa ni suala la uchelewshaji wa siku ile!! Ndiyo maana ninasema ile INTIMIDATION yenu ilifanikiwa sana watu wawe na woga wa kusimulia chanzo halisi cha suala lile. Nimesema baada ya vurugu ile Mathematics Department ikaandika kwa management ya FOE kwamba haitafundisha au kutoa Exam hadi students tu-apologise kwa kitendo cha kumfanyia fujo yule Mwalimu.

      Kama hulijui hili basi pole sana labda ulikaa chumba kingine alichosimamia tutorial assistant mwingine.

      Quote By muonamambo View Post
      kama kweli mlikuwa mnathamini walio wengi ambao ni 211 kati yenu 72 .. basi mngetoka nje na kuungana na wenzenu lakini narudia kusema mliweka masilahi yenu mbele na kusahau kuwa mligawanywa ili mtawalike kirahisi na uzembe wa uongoozi wa chuo
      Kwanza hata kabla haijatangazwa hakuna aliyejua nyinyi wangapi na sisi tulikuwa wangapi. Wote tulishtukia list kwenye notice board na idadi magazetini.

      Hakuna aliyekuwa na muda kujua wengi wako wapi na hii inaweza kuwa ilipelekea hilo. Kwa nini nasema hivi? In fact mtihani tulikuwa tunagawanywa kwenye vyumba zaidi hata ya vinane na kila chumba kikiwa na watu labda 30, 20 au 40.

      Hivyo mtu ulikuwa ukienda unaangalia chumba chako tu na ikibidi hujui mwingine chumba chake ni kipi maana hakuna aliyejitayarisha kujua list ya vyumba vyote kwa kujiandaa na hilo.

      Hivyo, iwapo ulisikia kwamba kuna watu wanafanya paper basi ulikimbilia kwenye chumba chako kuhakikisha. Na kibaya kwa mgawanyo wa vyumba hasa vile vya wazi ilionekana kabisa wanaofanya ni wengi.

      Kibaya kingine ni kwamba class reps walipita kwanza vyumbani na kuona watu wanafanya paper. Waliomo ndani wakaona wazi kuwa Prof. Masenge kaleta mitihani mbele ya class reps. Sasa hapa utakataaje kufanya wakati kuna baraka zote za viongozi wako yaani wawakilishi wako katik hali ambayo hamkuwa na makubaliano yoyote ya kuukataa mtihani ukiletwa.

      Quote By muonamambo View Post
      nakupa tu ushauri wa bure kubali kiiungwana kwamba ulichemsha kwa kuwa traitor na hiyo haikupunguzii mwili wako bali inakuweka katika jamii ya watu wasioaminika kwa manufaa ya wengi
      Ona mpaka leo mko vilevile na ubabe wenu, tena uko mmoja na hunijui ID yangu na mimi sikujui ni nani naongea naye. Hebu angalia tungekuwa tuko Chuoni na wenzako wengi ingekuwaje. Lete ushawishi tuweke history sawa.

      Kuhusu kushinda kesi yenu mahakamani ni kwamba mlijikita na matukio ya siku ya mtihani na lile la ugomvi wa nyuma halikuwahusu.

      Ni kweli kuna ukweli kidogo hapa. Si wote waliomvamia yule lecturer baada ya ile test ngumu. Ungeniambia uzembe wa chuo kutowa-identify waliomfanyia vurugu lecture nimgekusikiliza kidogo.

      Mbona sasa hamkutumia mahakama hiyohiyo kufungua kesi mlipojikita kwa wingi kumtimua benedict Mutungirehi kwa kumvuta tai na kumwangusha kana kwamba Nkrumah Hall imegeuka uwanja wa masumbwi, kisha asilimia kubwa ya G211 mkasimamishwa kwa mwaka mzima!!!
      Last edited by SubiriJibu; 30th June 2012 at 20:12.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    13. #32
      Kiraka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st February 2010
      Location : ILOGANZALA
      Posts : 1,352
      Rep Power : 747
      Likes Received
      258
      Likes Given
      438

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Umenikumbusha mbali sana!!
      FoE was a place to be!! Traitors hawakupewa nafasi... na kweli Ma traitor mlikoma!!!
      SubiriJibu likes this.
      Form is temporary, Class is permanent...

    14. #33
      platozoom's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 4,086
      Rep Power : 8295
      Likes Received
      2774
      Likes Given
      3794

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Mjadala huu na ule wa Mtungirehi umanifaidisha sana japo enzi hizo nilikuwa shule ya msingi Kimbunga nilikuwa namuhisi kama age mate wangu lakini kumbe.........
      "Education is something that remain in your head after forgeting what you learn at school"

    15. #34
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By JokaKuu View Post
      SubiriJibu,

      ..tatizo hapo ni watu wazima kama Prof.Masenge kushindwa kutumia busara.

      ..mkutano wa wahadhiri na wawakilishi wa wanafunzi ulipaswa kupanga tarehe mpya ya mtihani.

      ..mimi nadhani muweke pembeni hii habari ya "traitors" na "G211" halafu mjiulize kama wahadhiri really acted like guardians and grown ups ktk kulazimisha mtihani ufanyike ukiwa umechelewa 3++ hrs.

      ..hapo inaonesha kabisa kwamba wahadhiri walikuwa na nia mbaya kwa kutaka kuwakosesha baadhi ya wanafunzi nafasi ya kufanya mtihani.

      ..UDSM wanakuja wanafunzi toka background mbalimbali na mashinikizo kibao ktk maisha yao. sasa wahadhiri na watawala wanatumia hali ya wanafunzi kuwalazimisha kutimiza matakwa yao.
      Mkuu, heshima yako mbele.

      Mkuu kuna jambo moja wanalopotosha hawa wenzetu. Nijichukulie mimi kwa mfano. Ukisoma nilichoeleza movement zangu zinaonyesha kwamba kwanza nilikaa darasani kisha nikatoka nje ili kujua wengine wote wameamua nini.

      Hata katika hili hakuna aliyekuja kutu-organise tutoke nje kisha tufanye nini. Ulikuwa uamuzi binafsi.

      Hebu angalia sababu zao hata leo wanavyosema. Wanasema 30 minutes zinakupa haki ya kutoka nje ya mtihani na kwenda kwenye shughuli zako.

      Ni kweli kwamba wengine wana speed kiasi kwamba ikifika 30 minutes wanatoka na wanaenda kwenye Hall of residence au Library.

      Je, tujiulize iweje tabia ibadilike siku ileile tu kwamba kwa nini tusiondoke wote baada ya kukosekana mtihani.

      OK,

      Tuone sasa rection baada ya kujua kwamba mtihani umeanza. Hapa ndipo vurugu kubwa zilianza.

      Wazo la kwanza ilikuwa JE WENZETU WALIOONDOKA ITAKUWAJE?

      Hivyo, concern ya kwanza kabisa haikuwa TUSIFANYE PAPER KWA SABABU IMECHELEWA. Cincern ilikuwa ni wale walioondoka watakuwa wame-DISCO.

      Kwa ujumla hii concern ndiyo iliyonifanya nianze kufikiri kurudi kwenye mtihani. Kwamba iweje tuwahurumie watu ambao kwanza tuliwasihi wasiondoke hadi tufikie muafaka watakaotulelea viongozi wetu, lakini wao kwa ujeuri wakaondoka na kauli kwamba LIWALO NA LIWE MTIHANI UKIJA MTACHAGUA KUFANYA AU KUACHA.

      Kumbe hata hawa walioondoka, walijua kuwa inawezekana paper ikaja na kukawa na option ya kufanya.

      Kingie ni kwamba G211 walichelewa sana option ya kuwatoa wengine darasani. Nimesema mimi nilikaa hadi dakika 2O nje, nikatoa option hiyo wakanipuuza wakaendelea kubwabwaja pale nje hakuna resolution yoyote.

      Nikaona upuuzi nikaingia kwenye mtihani. Ona sasa delay yao. Nimeingia nikafanya hadi maswali matatu yaani kama dakika 40 hivi ndipo wakaja wamegawana makundi kuingia vyumbani kuwanyang'anya watu mitihani.

      Sasa kama walikuwa na haki ambayo waliishinda kweli mahakamani ni haki gani iliwaambia kwamba waje watutimue kwenye exam rooms na kuchanchana mtihiani yetu.

      Ona hata baada ya kututoa kwenye exam rooms unajua ilikuwa vigumu kumu-identify ni nani TRAITOR na nani G211. Kwa sababu hakukuwa na block moja iliyokaa na kujitambua kwamba hawa walikubali resolution na wale walikataa.

      Identification ilikuja kujulikana rasmi baada ya kutangazwa magazetini na kwenye notice board. Tena kuna wawili watatu hawakujulikana kama walifanya wakakumbwa na dhoruba wakawa ndani ya G211.

      Binafsi siwezi kuacha kutupa lawama kwa wale walioondoka wakisema LIWALO NA LIWE MTIHANI UKIJA TUJICHAGULIE UAMUZI.

      Maana hawa ndiyo ilikuwa concern ya kwanza. Vilivyobaki vyote vilikuwa ni visingizio ambayo ni rahisi kumshawishi ambaye hakuwepo kwenye tukio.
      JokaKuu likes this.

    16. #35
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By Kiraka View Post
      Umenikumbusha mbali sana!!
      FoE was a place to be!! Traitors hawakupewa nafasi... na kweli Ma traitor mlikoma!!!
      Mkuu,

      Umenisaidia kusema point moja. Ndiyo maana zile barua tulizopewa kusema kama tulikuwa INTIMIDATED tutaje watu mimi sikusita hata chembe.

      haya ninayoyaeleza humu niliandika vilevile. Mmekataza humu kutaja watu. Na kweli humu nimetaja pubclic figure of that time and place. lakini kwenye barua ile nilitaja list ya wengi tu, kwa sababu sina huruma na mtu muonevu na hasa anayenionea bila sababu ya msigi eti tu kwa sababu wako genge la wengi.

      Unasema tulikoma. Lakini hukusema kwa muda gani. Mliposimamiswa nyinyi G211 mkaenda mahakamani sisi tukafunga chuo tukaenda Practical training (PT), nyinyi mkasota na kesi iliyodumu hadi late Sepetember yaani miezi zaidi ya mitatu.

      Hivyo hapo sisi hatukukomeshwa nyinyi ndiyo mlisota na ikabidi mkae D'Salaam kipindi chote wakati Chuo kimefungwa na tuko PT na kisha likizo nyumbani.

      Mliporudi yaani early October kweli mkatutishatisha sana kwa intimidations nyingi. Mkakosea mkatumika na watani zenu mangwini kumtimua Benedict Mutungirehi. Mkatumika kama wasukuma wa kanda ya ziwa kwa wingi wao wanavyotumika kuipa CCM kura halafu sasa wanapandishiwa bei ya pamba.

      Mkafanikiwa kumvuruga Mutungirehi yaani late October. Lakini Early November 1994 tukarudishwa nyumbani na sisi baada ya mwezi tukaitwa nyinyi mkasota home mwaka mzima kama adhabu.

      Tulivyorudi G211 walichoma moto T-Shirt zao hawakutaka tena lisikike tena neno hilo. Neno TRAITOR likafa kama kifo cha mende.

      Wanaosoma thread hii wanaujua ukweli huu wote na hawanijui lakini wakiniona watashangaa kama kweli ningeweza kusema haya.

      Ni kweli sitaji majina zaidi maana wapo G211 wengine sasa ni wakuu wa TAKUKURU tena kama watatu ninaowafahamu. Mmoja ni yule ambaye aliwahi kugombana na Polisi alipowaambia kuwa Polisi ndiyo wanaongoza kwa kuomba rushwa na hivyo mapambani ya rushwa yanakuwa magumu.

      Ilimpa tatizo kauli hii.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    17. #36
      Ndukidi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Posts : 374
      Rep Power : 579
      Likes Received
      141
      Likes Given
      352

      Tatizo ni kuwa wewe maisha yako yote hii label ya UTRAITOR haitokutoka, ndio maana mpaka leo bado inakuandama!

    18. #37
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By Ndukidi View Post
      Tatizo ni kuwa wewe maisha yako yote hii label ya UTRAITOR haitokutoka, ndio maana mpaka leo bado inakuandama!

      Nyinyi ma-engineer wenzangu ndiyo ile character yenu bado mnayo hata kimaisha ya leo. Wenzenu kama Zitto, Tundu Lissu. Slaa, Halima Mdee, Wenje wanajua kujenga hoja kiasi kwamba usipokubaliana nao tuna haki ya kukuita TRAITOR.

      Nyinyi hilo mmegoma kabisa kujifunza.

      Mmegoma hata kufungua dictionary ili kujua ina-define vipi neno TRAITOR. Na kama English bado ni ngumu kwenu hadi leo basi angalieni kamusi inasemaje kuhus neno MSALITI.

      Nyinyi kwenu jambo mnalolitaka kwa musuli kama wabeba vyuma mnataka kila mmoja alifuate. Akilikataa mnamwita TRAITOR.

      Basi walau hata hayo mambo yawepo. Hili la G211 na la Mutungirehi halikuwahi kufika katika level ya unanimous decision bado mnaliita ni u-TRAITOR hadi leo.

      Jengeni hoja na maamuzi yawe ya vikundi mtakubaliwa kama yana ushawishi.

      Ugonjwa huu sitanii unawakumba sana maengineer wenzangu. Maofisini wakitaka jambo lao wanataka kama vile unamwita mkeo bila kujenga hoja yenye ushawishi. Msiwashangae walianza hivyohivyo tangu tukiwa chuoni.

      Badala ya kujichanganya na wenzao kuongeza communication skills wao wanawaita wenzao MANGWINI.

      Ona hata hapa sioni ushawishi wowote. Kubalini udhaifu. Mimi niliukubali udhaifu huo nikajizoeza sasa hivi najenga hoja vizuri tu. Si unaona mwenyew thread hii.
      Last edited by SubiriJibu; 30th June 2012 at 23:29.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    19. #38
      muonamambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd September 2010
      Posts : 568
      Rep Power : 559
      Likes Received
      179
      Likes Given
      946

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Ndugu yangu subirijibu heshima Kwako ....

      Kwanza napenda kukushauri Kuwa kukubali kosa nao ni uungwana
      • Fact ni kwamba mtihani ulicheleweshwa zaidi ya Masaa 3 bila taarifa
      • fact ni kwamba math dept na uongozi wa chuo walichemsha kulazimisha mtihani ufanyike licha ya kuchelewesha
      • fact ni kwamba ilikuwa ni haki ya g211 pamoja na wewe kususia mtihani baada ya mtihani kuchelewa
      • fact ni kwamba kwa kukubali kufanya mtihani ulionyesha woga wa kupita kiasi na usaliti kwa wenzako walitaka haki itendeke. Kama mwanafunzi anaadhibiwa kwa kuchelewa Dk 30 na mtihani ukichelewa je nani aadhibiwe

      • Samahani natumia simu hivyo Siwezi kuandika zaidi. Pole kwa Dow la Kuwa traitor.

    20. #39
      Albedo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th February 2008
      Posts : 5,032
      Rep Power : 1588
      Likes Received
      1113
      Likes Given
      561

      Default Re: Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Subirijibu acha ku expose Uoga wako. Hivi hata mkeo akisoma hapa si atakudharau sana. FOE SPIRIT Forever

    21. #40
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 772
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

      Quote By muonamambo View Post
      act ni kwamba math dept na uongozi wa chuo walichemsha kulazimisha mtihani ufanyike licha ya kuchelewesha
      Kama walilazimisha, walikuwa na uwezo gani kuilazimisha management ya FOE na management ya wanafunzi. Hii kulazimisha ni hypothesis yako
      Hukuwepo kwenye yale mazungumzo na class reps kwa hiyo huwezi kusema walilazimisha kana kwamba hakukuwa na demands toka pande zote.

      Quote By muonamambo View Post
      fact ni kwamba ilikuwa ni haki ya G211 pamoja na wewe kususia mtihani baada ya mtihani kuchelewa
      Sheria iliyotulinda ni kwamba mtihani ukianza ndipo sheria ya dakika 30 inatumika. Kabla ya kuanza hakukuwa na na sheria iliyosema tuitumie iwe kama haki yetu tutokomee. Ndiyo maana na wewe hukutokomea ulibaki unasubiri kwa hamu majibu ya class reps watakachokubaliana na akina Prof. Masenge wa Maths na Dean of Engineering.

      Quote By muonamambo View Post
      fact ni kwamba kwa kukubali kufanya mtihani ulionyesha woga wa kupita kiasi na usaliti kwa wenzako walitaka haki itendeke
      Hadi dakika tunafanya mtihani hakukuwa na madai ya aina yoyote ktuoka kwangu wala kwako. Na kama ni madai ya siku hiyo basi haki yetu ilikuwa ni mtihani na tungedai kwa nini hatuletewei mtihani wakati tumeshajiandaa. Hivyo hamkuwahi kuwa na madai ya kutofanyika mtihani.

      Nitaongea sana kwa sababu hili mlilipotosha sana

      Quote By muonamambo View Post
      Kama mwanafunzi anaadhibiwa kwa kuchelewa Dk 30 na mtihani ukichelewa je nani aadhibiwe
      Narudia kama nilivyosema hapo juu. Ndiyo maana tulikaa kusubiri itokee nini. Kumbe unajua kuw amaswali kama hayo lazima yalete ambiguity na lazima tuwe na resolution kwa sababu hayakuwa define.

      Ndiyo maana hata reslotuion mliyochukua bado ilikuwa ya kitoto. Kama kosa lilikuwa ni Maths Dept mbona hamkuli-address moja kwa moja kwa kumzuia Masenge asiendelee kusimamia mitihani badala yake mkadhani solution ni sisi wote tuonekane kama hatukufanya paper kwa kuzichana.

      Kuna tofauti gani kama mlikuwa na haki mtihani uendelee na nyinyi mkaitafuta haki yenu mahakamani kwa sababu hizihzi mnazozisema humu.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    Page 2 of 8 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...