Mkandara
Hii ndio kitu nisichokubaliana nacho kabisa!.. Sasa hawa madaktari wanapogoma ndio kusema Dr.Ulimboka kapigwa na wananchi kiasi kwamba wao ndio wachukue adhabu hii?
Halafu wanaombwa wananchi wale wale waliadhibiwa kuchangia tiba ya Ulimboka wakati wengine tuna wagonjwa wanaotaka huduma tu wapone lakini wanatufia mkononi kwa sababu ya mgomo huu..Nawaomba Madaktari iadhibuni serikali na sii wananchi walipa kodi ambao hawana makosa kabisa.
TUCTA wametoa kauli na wito kwamba swala hili litafikishwa ktk vyombo vya kimataifa, na hatuelewi mazungumzo baina ya serikali na shirikisho la madaktari limeenda vipi au wamekwama wapi..
Tunaona migomo hadi Bugando na Hospital za makanisa halafu tukisema mfumo mbaya na wapi penye mapungufu watu wanakuja juu kutetea kanisa ilihali vyombo hivi havifanyi kazi inavyohitajika.
Kazi kusubiri fedha za donors na misamaha wajirushe kwa sifa ya huduma ambayo haitusaidii wananchi ktk kupunguza gharama za Afya na sasa ndio hatutibiwi kabisaa wakati kodi zetu wanakula.
Kinachofanywa na madaktari hakina tofauti na UAMSHO, wao wanaona kila haki ya kuchoma makanisa au kugoma lakini wanashindwa kuidhibu serikali yenyewe. Kesho ukisikia Sheikh mkubwa wa UAMSHO kafanyiziwa, utawasikia Wazanzibar na Waislaam wakilaani Wakristu na serikali lakini hawapimi kitendo cha kuchoma makanisa yasiyohusika na mgogoro ndio unafiki ulipoanzia. Vitendo vyetu sisi wenyewe ktk kuwaadhibu wananchi ndivyo vinavyozidi kutugawa.
Sioni sababu ya madaktari kugoma pasipo kuwashirikisha wananchi, kulifanya swala hili ni lao wao wenyewe kwa kuwasulubu wananchi ii kuikomoa serikali.. Watu wanakufa jamani, muwe na huruma japo kidogo wakati tunaitafuta suluhu.
TUCTA wamesema watalipeleka swala hili ktk vyombo vya kimataifa, muda wote kwa nini wasihusishwe mapema tukatafuta suluhu badala ya kuwaadhibu wananchi?..
Follow Us Here