Nafungua TV namkuta waziri mkuu tayari kwa maswali na majibu papo kwa papo.Mtoto wa mkulima anatabasamu, ingawa si tabasamu la kupendeza kwani limejaa kejeli ni mizaha. Anapewa maswali na wapinzani anakuja na majibu duni,ila analazimisha yakubalike na spika anambeba, PM anahisi noma analazimisha jibu .Mama akiwa anatoa maelezo yake.
maelezo ya mama nayo yanaonyesha hajaelewa swali.
PM anapewa mwanaccm ambaye anaanza kwa uongo, anaelezea mambo ya kufikirika au hata mambo ya mitaani (tena mitaa ya CCM ndio ina watu wa kuamini au kuongea uongo wa kukusudia), PM naye anajibu kwa staili ya kuongezea uchochezi.K
isha CCM Wanapongezana,
Muda si mrefu anasimama tena mpinzani CCM B/C/Orijino. wanajitahidi kuwa katikati kwa kuwashambulia wapinzani rasmi halafu wanarekebisha kwa kuwasifu CCM orijino.
PM hajakaa sawa zimwi linamrudia ,mwendelezo wa maswali ambao hajaweza kuyajibu,mama anahisi kuwa inakuwa mbaya, anarukia kuokoa jahazi, kabla hajamaliza , PM anahisi hatari anakimbilia kujibu, anajibu kichovu km anaomba ushawishi wa huruma,
raia nje ya bunge wanachoka, wabunge wa rasmi wa upinzani wanajua bado hajajibu , wanongeza dozi.
Mchezo mzima wabunge wa CCM orijino hawauluewi kama jinsi viongozi wao wasivyo elewa. wanasimama tena wabunge wa ccm-orijino wanaongea kitu kilichotolewa maelekezo muda mfupi, huku wakianza kwa uchochezi na vitisho kwa raia kuhusu wapinzani rasmi.
Ghafla akili inaniamka kuwa CCM wana hofu, wanaogopa uchaguzi kwa vile hakuna hela, wanogopa uchaguzi kwa vile majimbo yao tayari wanasema hayana amani, kwani walitishiwa na wakatishika sasa wapo tayari kwa vita na kupoteza amani kabisa. Najiuliza lini wameacha tishia wenyewe kuwa wasijipitishe majimbo ya wenzao, na sasa wanataka wapiga mkwara wapinzani.....
Kabla sijamaliza tafakari kauli za woga, kukata tamaa kwa wabunge wa ccm, ugumu wa kubalance kati ya kuokoa chama au kujiokoa, anasimama jamaa wa Upinzani rasmi anauliza swali hata mimi nilipenda kuliuliza kwa PM...majibu yake yote,project zake zote zimekwama.
Na leo mshirika wake ambaye kamshinda ktk dialogue "presidaa wa Madaktari" katekwa kipuuzi, kateswa kinyama, na kapona kibahati ....PM anakuja na majibu ambayo hata wanywa gongo mitaani hawana mashaka wananyooshea vidole serikali, wanashangaa makomandoo wetu ndicho walichoweza achieve? Wanashangaa kuwa cream yote ya ccm haina chocote smart and dissent for a day?
MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KAMBANA PM MARA MBILI AJIUzulu.PM kusaidiana na mama wakajibu kikorofi na kwa aibu.Ila ukweli ni kuwa msemaji alianza kwa hilo PM akajibu bila kujua si mara ya kwanza maswali ya upinzani huwa yanamtega kwa swali lifuatalo.Akithibtisha kuwa ameshindwa kisha akaambiwa wazi kuwa ajitoe tuu.PM na mama wakaamua kwenda kama mob.
Ki ukweli ni kwamba kila raia yupo sympathetic kwa Ulimboka, kila mtu hanunui idea kuwa kuna watu wanachanga hela kuwahonga madaktari, watu hawanunui habari kuwa amani itatoweka kama hakuna CCM kwani kila siku, nahata bungeni msemaji wa upinzani alihusisha ccm na mauaji na hawakuweza toa majibu.
CCM wamejiloga na propaganda zao wenyewe, ccm wamezidisha hofu kuhusu CHADEMA NA HATIMA YAO kiasi cha kushindwa fanya chochote ktk mpangilio safi.
CCM wamekuwa wapinzani ktk utawala wao.Hawafanyi tena hata mambo wayawezayo vyema kwa ufanisi.
Raia wanateseka? (BILA SHAKA RAIA WANATESWA NA CCM), raia wanalia, wao wanalia (CCM WANAJILIZA).Wanaleta hofu, hawajui kuwa raia wakipata hofu sana baadaye huiondoa, na wanaweza iondoa vibaya.
Nashauri PM ajipange, na ule unyago wa wabunge aufanyao kabla ya bunge ili kuikabili CDM aachane nao , awape wabunge uhuru watumie fikra, waongee mambo ya watanzania, na yanayowashinda wasisingizie mtu wala kutengeneza sifa mbaya kuhusu CDM km za igunga.Kwa raia siku hizi hawaiamini CCM siku hizi kuliko chochote.PM asifanye mzaha na maswali ya CDM kwani ktk bunge hili hakuna swali PM kaweza jibu.
Na dharau zake zimemponza kwani akijibu la kwanza kwa kebehi la pili linakuwa gumu zaidi.
Follow Us Here