Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

    Report Post
    Page 3 of 6 FirstFirst 12345 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 105
    1. #1
      Jackbauer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : CTU
      Posts : 4,873
      Rep Power : 1690
      Likes Received
      1348
      Likes Given
      277

      Default Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA

      YAH: TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 28.06.2012

      Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo.

      Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu.

      Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati.

      Madaktari tumechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka ,

      Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja

      Tumechoka kuona msongamano mkubwa kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji.

      Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma.


      Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya vitisho tunavyoendelea kuvipata.

      Rai kwa Madaktari; Madaktari wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu, tunashukuru madaktari wote kwa ushirikiano na kuendelea na mshikamano.

      MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!

      Imetolewa na
      Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.

      huu ni ujumbe kutoka kwa Dr ulimboka stephen kutoka ICU!!!!
      Attachment 57669
      Last edited by Jackbauer; 28th June 2012 at 23:25.
      You may succeed in silencing me but that silence comes at a price-Alex litvinenko

    2. Miaka 50

    3. #41
      bensonlifua92's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th December 2010
      Posts : 82
      Rep Power : 444
      Likes Received
      32
      Likes Given
      32

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      Quote By KIBE
      wazushi tu nyinyi ..nyinyi mnadai fedha sasa mnakuja na uboreshaji wa afya .tumewachoka sasa msifikiri sisi wananchi tuko pamoja nanyi wauaji wakubwa ambao mumeweka fedha mbele... tumewachoka kama mmeshindwa kufanya kazi serikali nende mkaazishe zahanati zenu..... hongera serikali asiyetaka kazi fukuzeni tu tujue moja hatuna hawa binadamu wapenda fedha badala ya utu kwanza. mana madai yenu ya msingi mumetekelezewa lakini bado tu sijui mnawatakia nini watz... mengine mumeambiwa yatatekelezwa huko mbeleni kama uwezo ukiwepo lakini bado tu..ni haki kusema anajambo lenu nyuma
      Kwani kudai fedha ni vibaya kama ndo madoctor na hata wasomi wengine ambao hawalipwi vizuri walisotea madarasani kwa kwenda shule, lengo si ni mtu awe na maisha bora.

      Kama pesa hazina maana Mbona nyie pamoja na kuwa mnajilipa vizuri lakini bado tu mnafanya ufisadi wa nguvu kwa kwenda mbele na hata mnafikia fedha zingine mnazificha nje ya nchi yetu.

      Hivi nyie mmewahi jiuliza kuwa hizo fedha mnazoenda ficha huko nje mtazila lini maana ni mabillioni ya pesa mnaweka kwenye mabenki ya hao wazungu yaani mnazidi kuwapelekea mitaji zaidi ya biashara za mabenki yao, au nyie mnadhani zinakaa tu kuwangojea nyie.... eeeh kweli hamjaelimika bado....hizo pesa hata nyie hamtazifaidi maana hivi punde tu mtaaga dunia kwa pressure....

    4. #42
      Africa_Spring's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th June 2012
      Posts : 421
      Rep Power : 402
      Likes Received
      106
      Likes Given
      64

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      Quote By hengo
      Mbona katika madai ya madaktari kinacho tamkwa sana ni posho mbalimbali na mishahara?Kama kweli wanaumia kuon watanzania wakisongamana hospitalini mbona sasa wana waacha wana kufa bila kuonyesha jitihada za kuokoa maisha wagonjwa hao?Hu ni uzalendo au ubinafsi mbele?
      PENGO tatizolako huelwi wanachokisema,,,,,wamevumilia wamechoka...sasa wewe unataka waendelee kutibu mpaka lini wakati hali nimbaya..

    5. #43
      NG'OMBE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th March 2011
      Posts : 290
      Rep Power : 437
      Likes Received
      60
      Likes Given
      125

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      Wewe KIBE nenda kwa aliyekutuma kamwambie watanzania wa sasa wanaelewa. ni hospitali ipi ya serikali ina huduma bora hapa nchini? na kwanini viongozi hawatibiwi hapa. Eti unasema watanzania tumewachoka, umewachoka wewe na mkeo mlio na akili ya kuku.

    6. #44
      Dawa ya Mjinga's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 12th June 2009
      Location : Magubike
      Posts : 160
      Rep Power : 538
      Likes Received
      34
      Likes Given
      76

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      Quote By NG'OMBE
      Wewe KIBE nenda kwa aliyekutuma kamwambie watanzania wa sasa wanaelewa. ni hospitali ipi ya serikali ina huduma bora hapa nchini? na kwanini viongozi hawatibiwi hapa. Eti unasema watanzania tumewachoka, umewachoka wewe na mkeo mlio na akili ya kuku.

      Inaelekea huyo KIBE hayawahi kuugua wala kuuguliwa hivi karibuni. Tumuombee Mungu ampe walau kamaleria sugu hivi au taifodi kali na aende akapate huduma ajionee. Wenye taaluma yao wanapokueleza kuwa hali ni mbaya wewe kilaza ni nani kuwabishia?
      Vilevile kama umewachoka madaktari jaribu waganga wa kienyeji. Tena kama wewe umande wa udaktari ulikushinda basi mwanao mpeleke akasomee. Si fani rahisi tu kama zingine? Aende huko usikie muziki wake! Mzigo wa mwenzako kweli ni furushi la sufi, mwepesi. Beba wewe uone! Kwa fedha hizo wanazipewa sasa kuna madaktari kadhaa wamepoteza maisha kwa kuambikizwa magonjwa hatari kutokana na ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi na familia zao zinateseka sana na hali ngumu hii ya maisha. Wakipata nyongeza walau wanaweza kujiwekea viakiba au bima kwa manufaa ya familia zao. Hawafanyi kazi ya kujitolea maana hata kujitoa kwao mhanga kuna kikomo! Nani kama daktari? Wamekoholewa na wenye TB bila maski, wengine wakagusa damu, na uchafu mwingine bila glovuz, wakajidunga kwa bahati mbaya na sindano zenye vimelea. Tumepoteza wengi kwa hali hii. Imetosha!
      Hali za wagonjwa hospitalini kumbe wewe huzijui, unaishi wapi au ni mmojawao wa wanatibiwa India. Walisema waswahili kuwa mweye shibe hamju mwenye njaa. Jambo ambalo hawajawahi kulisema ni kuhusu mwenye njaa. Je, mwenye njaa naye hamjui mwenye shibe? Usijidanganye rafiki!

    7. #45
      Sigma's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 26th February 2011
      Location : The 2nd House on the Left
      Posts : 4,258
      Rep Power : 0
      Likes Received
      914
      Likes Given
      613

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      Quote By Bitende
      mwanzoni kilichokuwa kinasikika sana kwenye madai ya migomo yao ilikuwa ni mishahara kupanda na allawances sasa hv mambo yamekuwa magum mumeanza kuhusisha na matatizo ya wananchi ili mpate saport hamna lolote msemo wa mhe.pinda acha liwalo na liwe
      tangu mwanzo hayo yalokuwamo katika madai manane.
      hakuna dai jipya

    8. FemaTV & Radio

    9. #46
      Sigma's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 26th February 2011
      Location : The 2nd House on the Left
      Posts : 4,258
      Rep Power : 0
      Likes Received
      914
      Likes Given
      613

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      Still the government is busy to accomplish the "unfinished business, i.e. eliminate Ulimboka"
      Madaktari japo hawajasomea intellijesia washipiku tayari serikali kwa kila wanachopanga.

    10. GIB
      #47
      GIB's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2012
      Posts : 301
      Rep Power : 424
      Likes Received
      81
      Likes Given
      123

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      Quote By KIBE
      wazushi tu nyinyi ..nyinyi mnadai fedha sasa mnakuja na uboreshaji wa afya .tumewachoka sasa msifikiri sisi wananchi tuko pamoja nanyi wauaji wakubwa ambao mumeweka fedha mbele... tumewachoka kama mmeshindwa kufanya kazi serikali nende mkaazishe zahanati zenu..... hongera serikali asiyetaka kazi fukuzeni tu tujue moja hatuna hawa binadamu wapenda fedha badala ya utu kwanza. mana madai yenu ya msingi mumetekelezewa lakini bado tu sijui mnawatakia nini watz... mengine mumeambiwa yatatekelezwa huko mbeleni kama uwezo ukiwepo lakini bado tu..ni haki kusema anajambo lenu nyuma
      you man it my sincerely hope your ----------******f&&&&88..u
      Muswada unaendeleza kivuli kirefu cha Urais wa Kifalme katika mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya. Tundu Antiphas Mughwai Lissu (MB) 2012


    11. #48
      IHANDA's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th June 2012
      Location : GOLANI
      Posts : 26
      Rep Power : 352
      Likes Received
      5
      Likes Given
      2

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      jamani hii tanzania nahisi inakoelekea ni kubaya sana tusipokuwa makini tutakuja kujuta

    12. #49
      Gang Chomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th February 2008
      Location : hell
      Posts : 5,027
      Rep Power : 1721
      Likes Received
      967
      Likes Given
      0

      Default

      hapo chini hayo ndio madai makuu ya madaktari...
      Sasa nionyeshe sehemu waliozungumzia posho au mishahara yao kama wewe unavyokurupuka bila kuchamba na kuleta ushambenga wako hapa...


      Quote By KIBE
      wazushi tu nyinyi ..nyinyi mnadai fedha sasa mnakuja na uboreshaji wa afya .tumewachoka sasa msifikiri sisi wananchi tuko pamoja nanyi wauaji wakubwa ambao mumeweka fedha mbele... tumewachoka kama mmeshindwa kufanya kazi serikali nende mkaazishe zahanati zenu..... hongera serikali asiyetaka kazi fukuzeni tu tujue moja hatuna hawa binadamu wapenda fedha badala ya utu kwanza. mana madai yenu ya msingi mumetekelezewa lakini bado tu sijui mnawatakia nini watz... mengine mumeambiwa yatatekelezwa huko mbeleni kama uwezo ukiwepo lakini bado tu..ni haki kusema anajambo lenu nyuma

      Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia
      nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu
      isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za
      msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo
      ya dhati.

      Madaktari tumechoka kuona huduma za
      afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi
      mwaka , Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini
      na watoto wakilala wanne katika kitanda
      kimoja Tumechoka kuona msongamano mkubwa
      kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku
      kukiwa hakuna mpango wowote wa
      uboreshaji.

      Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa
      dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya
      wakifanya kazi katika mazingira magumu
      yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya
      taaluma.

      Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea
      kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya
      vitisho tunavyoendelea kuvipata.

    13. #50
      Henry Philip's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 29th July 2008
      Posts : 109
      Rep Power : 572
      Likes Received
      31
      Likes Given
      15

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      Quote By KIBE
      wazushi tu nyinyi ..nyinyi mnadai fedha sasa mnakuja na uboreshaji wa afya .tumewachoka sasa msifikiri sisi wananchi tuko pamoja nanyi wauaji wakubwa ambao mumeweka fedha mbele... tumewachoka kama mmeshindwa kufanya kazi serikali nende mkaazishe zahanati zenu..... hongera serikali asiyetaka kazi fukuzeni tu tujue moja hatuna hawa binadamu wapenda fedha badala ya utu kwanza. mana madai yenu ya msingi mumetekelezewa lakini bado tu sijui mnawatakia nini watz... mengine mumeambiwa yatatekelezwa huko mbeleni kama uwezo ukiwepo lakini bado tu..ni haki kusema anajambo lenu nyuma
      Naomba nianze na mfano wa mwalimu: Mwalimu ktk kipindi chake, kuna wakati alikuwa akihutubia umma, na ktk hotuba ile alitoa mfano mmoja ambao ni hai sana hata leo ambao wewe unayesema madaktari ni wahuni, basi wewe ndiye muhuni namba moja ambaye umepumbazwa na madawa ya kulevya pengine na vijisenti unavyopata toka kwa mfugaji wako kwani wewe ni mbwa tena la kufugwa afadhali ya koko anayejua kujitafutia na anafahamu pa kwenda wakati wa hatari. Mwalimu alisema hivi: Mbwa koko alikuwa anapitapita mtaani kujitafutia riziki, na ktk pitapita, akamwona mbwa mwenzake ndani ya fensi ya mtu tajiri, mbwa koko akajisemea dah! mwenzangu anafaidi kweli yaani haangaiki kutafuta kama mimi, yeye kila kitu analetewa tu. Na yule mbwa wa kufugwa ndani alipomwona Mbwa koko nje ya fence akajisemea, duh; mwenzangu anafaidi, ona alivyo huru, anaenda anapotaka na kujitafutia anachohitaji kuliko mimi ambaye mara nyingi naletewa nisichokitaka, natamani ningekuwa yeye. Basi ktk kutamaniana wakasogeleana na kuanza kusalimiana na kuzungumza. Yule mbwa koko akamwambia mwenziwe, ndugu yangu inaonekana huko uliko ni kuzuri ona ulivyonawiri sio kama mimi jua lanichoma mchana kutwa na kunyeshewa pia. Yule mwenziwe akajibu, dah mwenzangu wewe hujui tu, nayatamani sana maisha yako kwani huku niliko nafungiwa tu na kufunguliwa muda wautakao,napewa chakula nisichotaka na kwa muda wautakao, na sikuwahi kupewa hata muda wa kukatiza nje ya geti yaani maisha yangu yote ni ndani tu, yaani una raha sana na natamani sana nitoke huku ndani...Mwisho.


      Kwa story hiyo fupi ya mwalimu ni wazi kuwa wewe ni mbwa wa kufugwa na kwa sababu ushazoea kupewa kila kitu, wala hujui kuhangaika maana yake nini ndio maana unatapika makombo ya wakufugao...NJOO MATAANI TUUNGUE JUA NA KUNYESHEWA MVUA PAMOJA ALAFU UONE KAMA UTAONGEA UTUMBO NA MATAPISHI HAYO...PUMBAVU KABISA...INFACT, YOU ARE FULL OF SHIT EVERYWHERE. UNAWEZA UKAONEKANA UMENAWIRI NA MWILI UNA AFYA LAKINI AKILI YOTE WAMECHUKUA, KAMA ILIVYOKUWA SERA YA WAKOLONI ENZI ZILE "TAKE THE MIND, KEEP THE BODY" WEWE UKO UTUMWANI NA HAUJITAMBUI KUWA AKILI YOTE WAMECHUKUWA NA WAMEKUACHIA HILO FUVU TU, NDANI KUNA MGANDO MIDHILI YA MAZIWA YALOGANDA YALIYOHARIBIKA NA HAYAFAI KULIWA, NDIO WEWE HAPO, TOKA UTUMWANI WEWEEE

    14. #51
      mamabaraka's Avatar
      Member Array
      Join Date : 18th October 2011
      Posts : 81
      Rep Power : 399
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      wavivu wa kufikir ndio wanaoshabikia mgomo wa madactari, binafsi siwaungi mkono hasa hao wa muhimbili baadhi yao ni wauwaji wakubwa wapo kipesa zaidi, sitosahu siku moja nilipoenda kujifungua muhimbili mwaka 2010 mwezi february. Nikiwa nagugumia maumivu docta mmoja jina ninalo akaanza kunitukana eti kwa nini nilienda usiku hospitali na kunitaka nimpe hela ya tax, nikamwambia asubiri. Nilitukana sana na kuandikiwa nijifungue kwa kisu bila kujua sababu nilipelewa thieter huku nalia. Baada ya hapo nikaanza kudaiwa hela ya tax na kwa kuwa sikuwa na pesa kwa wakati ule nilimpa elfu kumi, wee alinitukana nilishamsamehe ila sitomsahau maishani mwangu. Naomba tu madaktari na serikali mmalize migogoro na kutuhudumia bila migomo weken uzalendo mbele.

    15. #52
      gfsonwin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 12th April 2012
      Posts : 10,674
      Rep Power : 21309
      Likes Received
      10032
      Likes Given
      13933

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      work, the emancipator............
      "thought takes man out of servitude into freedom"
      'daima tudumu katika upendo'

    16. #53
      Puppy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th October 2011
      Posts : 1,474
      Rep Power : 679
      Likes Received
      360
      Likes Given
      53

      Default

      Quote By majorbanks
      Kamanda Msangi aliyemkamata na kumtesa Dr Ulimboka yupo katika jopo la kuchunguza nini kilimtokea Dr Ulimboka. Alipofika kumuhoji Dr Ulimboka alimwambia 'Nirudishie simu na waleti yangu'. Kamanda Msangi taratibu akatoka wodini kichwa chini.

      Duh noma hivo

    17. #54
      Ciril's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2011
      Posts : 1,971
      Rep Power : 879
      Likes Received
      243
      Likes Given
      19

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      Serikali dhaifu lazima itende mambo ya kidhaifu dhaifu yanayotokana na mawazo dhaifu.
      MWISHO WA UBAYA NI AIBU.

    18. #55
      watu8's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th February 2010
      Location : Juu ya Tukutuku
      Posts : 14,991
      Rep Power : 31271
      Likes Received
      7418
      Likes Given
      7411

      Default

      Quote By KIBE
      Wazushi tu nyinyi ..nyinyi mnadai fedha sasa mnakuja na uboreshaji wa afya .tumewachoka sasa msifikiri sisi wananchi tuko pamoja nanyi wauaji wakubwa ambao mumeweka fedha mbele... tumewachoka kama mmeshindwa kufanya kazi serikali nende mkaazishe zahanati zenu..... hongera serikali asiyetaka kazi fukuzeni tu tujue moja hatuna hawa binadamu wapenda fedha badala ya utu kwanza. mana madai yenu ya msingi mumetekelezewa lakini bado tu sijui mnawatakia nini watz... mengine mumeambiwa yatatekelezwa huko mbeleni kama uwezo ukiwepo lakini bado tu..ni haki kusema anajambo lenu nyuma
      mkuu jaribu tu kufikiria, kama kweli madai ya madaktari ni madai binafsi, kwa nini serikali haitamki chochote!

    19. #56
      Filipo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Location : Kiding'a
      Posts : 6,349
      Rep Power : 18614
      Likes Received
      3508
      Likes Given
      1612

      Default

      Quote By nndondo
      David Abeid bado anaishi? inakuaje kama kweli kuna peoples power how long shall they kiil our prophets while we stand aside and look? hivi tunaakili sisi, lazima wanza kudondoshwa mmoja baada ya mwingine kuanzia leo,
      That man hatakiwi kufa kwa sasa. Tunamhitaji sana kwenye uchunguzi. Ninauhakika kuna mahali "akiguswa vizuri" atasema yote!

    20. #57
      Sunshow's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th November 2011
      Posts : 689
      Rep Power : 517
      Likes Received
      95
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By NG'OMBE
      Wewe KIBE nenda kwa aliyekutuma kamwambie watanzania wa sasa wanaelewa. ni hospitali ipi ya serikali ina huduma bora hapa nchini? na kwanini viongozi hawatibiwi hapa. Eti unasema watanzania tumewachoka, umewachoka wewe na mkeo mlio na akili ya kuku.
      Ng'ombe kuwa mpole kidogo hakuna kitu kama eti madakt wanapata huruma kwa dawa kukosekana na wagonjwa kulala chini zaidi ya maslahi binafsi. Wajue wapo wanataaluma nyingine na mshahara kidogo zaidi ya wao lakini wanafanya kazi wasidhani wao ndiyo wasomi pekee. Ni vizuri kwa msomi mstaarabu kuliko kuharibu ufanisi wa mwajiri wako ni bora kujiengua mwenyewe na kutafuta maslahi ya juu sehemu nyingine.

    21. #58
      yutong's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th April 2011
      Posts : 1,345
      Rep Power : 683
      Likes Received
      239
      Likes Given
      96

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      Quote By HP1
      Freedom is coming soon and very soon
      Freedom is coming tomorrow "SARAFINA"
      Sign of Victory - R. Kelly

    22. #59
      Filipo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Location : Kiding'a
      Posts : 6,349
      Rep Power : 18614
      Likes Received
      3508
      Likes Given
      1612

      Default

      Quote By majorbanks
      Kamanda Msangi aliyemkamata na kumtesa Dr Ulimboka yupo katika jopo la kuchunguza nini kilimtokea Dr Ulimboka. Alipofika kumuhoji Dr Ulimboka alimwambia 'Nirudishie simu na waleti yangu'. Kamanda Msangi taratibu akatoka wodini kichwa chini.
      Hapo ndipo unagundua jinsi jeshi la polisi lilivyojaa vibaka. Kuanzia makoplo hadi maofisa!

    23. 654
      #60
      654's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st February 2012
      Posts : 132
      Rep Power : 394
      Likes Received
      32
      Likes Given
      16

      Default Re: Tamko fupi la Jumuiya ya Madaktari - Juni 28, 2012

      Quote By FIDIVIN
      TZ naona kila mtu amekuwa msanii na mwanasiasa, hili tamko la madaktari wanajifanya wanagoma kutetea wagonjwa wakati kikubwa wanadai pesa.
      Madaktari hawa hawa ndo wamesababisha vifo au ulemavu wa kudumu kwa mamia ya waTZ kwa uzembe wao au kutojali kwao harafu leo wanaleta picha kuonyesha wako na wananchi, wengine ndo wezi wa dawa hospitalini.
      Hii ni mchemko tu, ngojeni ndo mtajua madai yenu na jeuri yenu si chochote.
      Mkuu tupatie data za haya unayoyasema ili nao wasulubiwe, itakuwa bora ukitaja majina ya wagonjwa na mahali hizo dhambi baya zilifanywa, kama hii haitakuwa kukuuliza sana, itakuwa bora kama hauna data ambazo ni verified u withdraw comment yako na kuomba radhi wanajamvi. Asante kwa ushirikiano wako

    Page 3 of 6 FirstFirst 12345 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...