Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

    Report Post
    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast
    Results 21 to 40 of 49
    1. #1
      Tumaini Makene's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2012
      Posts : 1,062
      Rep Power : 8907
      Likes Received
      2231
      Likes Given
      768

      Default CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
      TAMKO LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU TUKIO LA KUTEKWA KWA DKT. ULIMBOKA NA MGOMO WA MADAKTARI

      Ndugu wanahabari kwanza asanteni kwa kuitikia mwito wetu leo na kwa ushirikiano mnaotoa kwa Watanzania katika majukumu yenu ya kila siku katika kuitumikia jamii. Kuna masuala mawili tungependa kuzungumza mbele yenu leo;

      Kwanza; kwa namna ya pekee, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kutekwa, kuteswa na kuumizwa vibaya kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini Dkt. Steven Ulimboka jijini Dar es salaam.
      Tukio hili limetukumbusha mambo mengi ambayo yamekifanya chama chetu kitafakari kwa kina suala zima la mgomo wa madaktari unaoendelea nchini. Kama tulivyowahi kusema mara kadhaa kuwa ni bahati mbaya sana kuwa madaktari wetu ambao kwa hakika ni wachache sana, wanalazimika kutumia haki yao ya kugoma katika kudai maboresho ya msingi kwenye sekta ya afya, jambo ambalo linagharamu maisha ya watu hususani wa kawaida (walalahoi) ambao matibabu yao hutegemea hospitali za umma.

      CHADEMA inaamini kuwa moja ya majukumu ya msingi ya serikali yoyote makini ni wajibu wa kulinda haki, mali na usalama wa kila raia na pia kuhakikisha kuwa huduma muhimu za jamii zinapatikana wakati wote kwa nchi nzima.
      Tukio la kutekwa nyara kwa kiongozi wa madaktari, Dkt. Ulimboka, si suala dogo wala la mzaha na haliwezi kuisha kwa MALALAMIKO tu, ya sisi wapinzani, wanaharakati na serikali yenyewe. Hapa ni lazima watu wenye wajibu wa kuhakikisha usalama huo wa raia wawajibike, hasa katika kutuambia ukweli wa nani aliyehusika na UGAIDI huu afahamike na hatua zichukuliwe dhidi yake.

      Tukio hili linatukumbusha njama mbalimbali ambazo zimekuwa zinafanywa na serikali dhalimu katika maeneo mengine duniani dhidi ya wapigania haki au wale wote wanaotoa mawazo mbadala dhidi ya watawala.
      Lakini pia katika nchi yetu hii leo, yapo mauaji ambayo yana kila harufu ya serikali, vyombo vyake na chama tawala kuhusika. Mfano mauaji ya kijanaMbwana Masoud, aliyeuawa huko Igunga mwaka Oktoba 2011, baada ya kutekwa na kuteswa.

      Mfano mwingine ni mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA Kata ya Usa River,Msafiri Mbwambo, huko Arumeru Aprili 2012, viongozi na wanaharakati kubambikiwa mashtaka ya uongo sehemu mbalimbli nchini, kuzingirwa kwaWabunge wa CHADEMA huko Mwanza, kisha wakapigwa na kuumizwa vibaya,wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, hususan viongozi wao, kunyimwa haki zao za kusomeshwa na kufunguliwa mashtaka yasiyo na msingi kwa sababu ya misimamo yao katika kudai haki, n.k.

      Lakini pia tukio hili linakumbushia matukio ya namna hii ambayo yamehusishwa na vyombo vya dola pamoja na CCM wakati wa chaguzi ndogo katika maeneo mbalimbali mathalani huko Kiteto, Biharamulo na Busanda ambako mpaka leo pamoja na kuwepo kwa viashiria vyote kuwa serikali, kwa maana ya dola ilihusika katika matukio ya namna hii ili kukisaidia CCM kushinda uchaguzi, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa zaidi ya polisi kukalia majalada hayo mpaka leo.

      Yote hayo hapo juu yanaimarisha msimamo wetu kuwa ni LAZIMA serikali iwe na jibu la kutekwa, kuteswa na kuumizwa vibaya kwa Dr. Ulimboka.

      Na katika hili CHADEMA tunaweka msimamo kuwa serikali haiwezi kuaminika katika kufanya uchunguzi, wala Jeshi la Polisi pia haliwezi kuwa na uhalali wa kufanya hiyo kazi. Mpaka sasa kwa mazingira yaliyopo, serikali ni mtuhumiwa katika tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa sana kwa Dkt. Ulimboka. Ni kanuni ya msingi sana katika dhana ya uongozi bora, kuwa mtuhumiwa hawezi kujichunguza mwenyewe.

      Wakati ambapo Watanzania wote tunaoitakia heri nchi yetu, tukiendelea kumwombea Dkt. Ulimboka katika wakati mgumu wa maumivu makali aliyonayo apone haraka, CHADEMA kinaitaka serikali kutohusika kwa namna yoyote katika uchunguzi wa tukio la Dkt. Ulimboka.

      Ili waliohusika wapatikane na kuwajibishwa, tunataka iundwe tume huru, itakayojumuisha watu wanaoaminika kutoka kada mbalimbali, ili ufanyike uchunguzi huru juu ya suala hili ambalo ni dhahiri limeibua taharuki nyingine katikati ya taharuki kubwa ya mgomo wa madaktari ambao unazidi kushika kasi kwa sababu ya serikali kutowajibika ipasavyo kwa wananchi walioiweka madarakani. Kuundwa kwa tume huru kuchunguza matukio au vifo tata kila inapotokea, imekuwa ni rai yetu mara kwa mara ili serikali ioneshe uongozi bora kwa vitendo.

      Mbali ya kuwa suala hili linahusu maisha ya binadamu ambayo hayana thamani ya kitu kingine chochote, bado pia ni kitendo kinachozima demokrasia na kuhatarishaamani ya taifa.

      Kuhusu mgomo wa madaktari

      Ndugu wanahabari suala la pili; lazima sasa mgomo huu wa madaktari unaoendelea umalizike kwa wananchi ambao ndio wanaoathirika, kuingilia kati iliserikali imalize mvutano na madaktari.
      CHADEMA kinaona suala hili kuwa zaidi ya “siasa”. Ni suala linalohusu maisha ya watu. Tunatoa mwito kwa watu wote wenye mapenzi mema kuungana katika kushinikiza mgomo wa madaktari kupatiwa suluhisho la kudumu ili kunusuru maisha ya Watanzania, hasa wasiokuwa na uwezo wa kutibiwa nje ya nchi kama viongozi wao. Dawa ya mgomo huu iko ndani ya uwezo wa serikali; isipokuwa tuhaina nia ya kweli na dhati kutatua tatizo hili kwa manufaa ya wananchi. Kwa kuwa serikali ni ya wananchi na serikali inawajibika kwa wananchi katika masuala yote, ikiwemo kuhakikisha huduma za jamii zinapatikana, ni lazima sasa wenye nchi hawa waoneshe msimamo wao katika suala hili. Tunawaomba Watanzania kusimama kuiwajibisha, ikiwa Serikali ya Rais Kikwete chini ya CCM, itaendelea kupuuza na kufanya mzaha katika suala hili linalohatarisha amani na utulivu wa taifa.

      Kama Serikali ya Rais Kikwete itaendelea kupuuza, hata baada ya msimamo wa wananchi wa kuitaka iwajibike kutatua tatizo hili, basi serikali hii itakuwa imeongeza idadi ya viashiria vinavyoikosesha uhalali wa kuongoza.

      Ndugu wanahabari, kwa kipekee kabisa tunawasihi Watanzania ambao ndiyo waathirika wakubwa wa mvutano kati ya serikali na madaktari, uliosababisha mgomo unaoendelea, wamtake Rais Jakaya Mrisho Kikwete amalize mgomo huumara moja kuzuia madhara makubwa kwa maisha ya binadamu.

      Tunasema hivyo kwa sababu, katika mgomo wa awali, Januari/Februari, baada ya wasaidizi wake, akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda kushindwa kuutatua, suala hili lilifika kwa Rais Kikwete, ambaye alikutana, kujadiliana na kufikia mwafaka na madaktari.
      Baada ya hapo aliwatangazia Watanzania wote kupitia ‘wazee wa Dar es Salaam’, kuwa mgomo umekwisha. Rais Kikwete aliahidi pia kuwa hakutakuwa na mgomo wa madaktari tena. Sasa tunamtaka Rais Kikwete atoke hadharani tena awaambie Watanzania vitu gani alikubaliana na madaktari, ametekeleza yapi na mangapi ambayo hayajatekelezwa mpaka sasa, kiasi madaktari wameamua kugoma tena,huku wananchi wakiumia. Serikali haiwezi kukwepa kuwajibika kwa madhara yoyote yanayotokea kwa maisha ya binadamu, kutokana na mgomo wa madaktari.

      Tunasisitiza huu ni wajibu wa Rais Kikwete kwa Watanzania, kwa sababu wanajua suala hili lilishafika kwake. Kinyume na hapo Watanzania wataendelea kujua wanaye rais wa namna gani katika kusimamia masuala ya msingi yanayoamua hatma yao, mtu mmoja mmoja na kama taifa.

      Kwa sababu Mhimili wa Bunge ambao ndiyo mwakilishi wa wananchi, ulipaswa kuwa tegemeo na kimbilio katika kuokoa maisha ya watu, umeonekana kuwa na meno ya plastiki na kushindwa kuwaokoa Watanzania, tunatumia fursa hiikuwataka Watanzania wote watimize wajibu wao wa kuitaka serikali na Rais Kikwete kumaliza mgomo huu.

      Ndugu wanahabari mwisho tunasema kuwa Serikali isiyoweza kuwahakikishia wananchi wake usalama na upatikanaji wa huduma zingine muhimu za jamii, mathalani; afya, elimu, maji, umeme n.k, ni serikali inayopoteza uhalali wa kuongoza.

      Imetolewa leo Juni 28, 2012 Dar es Salaam na;
      Singo K. Benson
      Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo-CHADEMA
      Kny. Katibu Mkuu

      Sangarara and kitero like this.

    2. RukaaJuu Final

    3. #21
      Baba V's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2010
      Location : Buguruni Mnyamani
      Posts : 10,872
      Rep Power : 30216
      Likes Received
      4699
      Likes Given
      3477

      Default re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      Maovu yote hayo wanayafanya "wenyewe" afu wanazuga kuunda tume,mxsnzlxptug zao!

    4. #22
      Kobello's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th February 2011
      Posts : 2,950
      Rep Power : 1660
      Likes Received
      1107
      Likes Given
      191

      Default re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      Quote By asigwa
      hivi yule mtalii aliyeuwawa mbugani aliundiwa tume?? imechukua muda gani kuwakamata wahalifu???
      Mzungu ni mtu muhimu duniani. Sisi waswahili tupo tupo tu.
      Samahani, ila habari ndiyo hiyo.
      MANI likes this.
      Keeping quiet is a war crime.

    5. #23
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,480
      Rep Power : 19785
      Likes Received
      4300
      Likes Given
      1248

      Default re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      Hatuwezi kuunda tume ya kuichunguza serikali ya ccm, tunataka tume huru.

    6. #24
      Pendael laizer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2012
      Posts : 945
      Rep Power : 560
      Likes Received
      90
      Likes Given
      5

      Default re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      Ufsadi mwingine wanataka kutuletea hawa manake wamezoea sana kila tukio tume na hakuna hata tume moja ambaye ilishawai kuleta habari au bado zinachunguzaga?shame on ccm.

    7. #25
      sesy nzenga's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th June 2012
      Posts : 118
      Rep Power : 372
      Likes Received
      11
      Likes Given
      94

      Default re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      serikali dhaifu hatutaki tume ...mnataka kujitafuti ulaji au mnataka kuwalipa waliohusika na tukio kwa kutumia tume hizo hera za kulipa tume bora mboreshe hospitali

    8. Miaka 50

    9. #26
      Crashwise's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2007
      Location : Safarini
      Posts : 13,122
      Rep Power : 14288
      Likes Received
      4013
      Likes Given
      3271

      Default

      Quote By Mchaka Mchakani
      utasikia UCHUNGUZI UNAENDELEA MPAKA TUNASAHAU!
      kwa kizazi hiki hatusahau ng'oo...

    10. #27
      Lambardi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th February 2008
      Location : KITAANI ZAIDI
      Posts : 4,523
      Rep Power : 1797
      Likes Received
      654
      Likes Given
      0

      Default re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      Hatutaki tume ya kinafiki!!wajiundie wenyewe kuwa serikali imewashinda wamtoe alie dhaifu mambo yaende!mnakimbilia ikilu uwezo wenu mdogo mnaona sasa???chama kibadili utaratibu ..sio watu wakimbilie kuchukua form hapana......chama kichague candidate wa 3 wapigiwe kura hata bila kujinadi apatikane mmoja makini!!itapunguza vilaza kuongoza nchi kwa kura za kununua wajumbe!napata hasira sana!iko wazi usalama wa taifa wamehusika moja kwa moja hata kudanganya hawawezi aibu sana usalama wa taifa wa sikuhizi nao wamechoka maana wanaishia kuwa masikini watu wa muda mfupi wananeeemeka!!haina maana!!jeshi lipo kwlei linajua wajibu wake kwa dhaifu na legelege??

    11. #28
      Leodgard's Avatar
      Member Array
      Join Date : 22nd June 2012
      Posts : 33
      Rep Power : 354
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Hizi tume ni kwaajili ya kuendelea kuwapa maumivu watanzania wagonjwa!! Hazina tija!!! Bora iundwe tume huru tena ya kimataifa inaweza kuja NA jibu positive!! NA sio hao hao wauwaji!!!

    12. #29
      Shine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2011
      Posts : 9,185
      Rep Power : 2429
      Likes Received
      944
      Likes Given
      377

      Default

      Quote By FJM
      Tukio la kuuwawa kwa mtalii Serengeti mbona limefanyika bila tume? Kwa maana hiyo wananchi wachukulie kwamba Jeshi la polisi Tanzania lina ujuzi wa kufuatalia mauaji ya wazungu peke yake?
      Teh teh swali zuri sana natamani ungekuwa mwakilishi pale bungeni ukauliza hili swali tusikie magamba watakavyo haha!

    13. #30
      Shine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2011
      Posts : 9,185
      Rep Power : 2429
      Likes Received
      944
      Likes Given
      377

      Default Re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      Sidhani kama kuna mtanzania yoyote anaekubaliana na suala la tume!

    14. #31
      Bangoo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2011
      Posts : 2,270
      Rep Power : 835
      Likes Received
      370
      Likes Given
      0

      Default Re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      ccm inauwa watu?

    15. #32
      Pastor Achachanda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2012
      Posts : 280
      Rep Power : 411
      Likes Received
      9
      Likes Given
      3

      Default Re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      Mungu wetu unayeona machozi ya watanzania wote nakuomba utusaidie katika maumivu haya mazito ukamate hawa wahalifu.AMEN.

    16. #33
      Ally Kanah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2011
      Posts : 780
      Rep Power : 559
      Likes Received
      37
      Likes Given
      35

      Default

      Quote By Tumaini Makene
      TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
      TAMKO LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU TUKIO LA KUTEKWA KWA DKT. ULIMBOKA NA MGOMO WA MADAKTARI

      Ndugu wanahabari kwanza asanteni kwa kuitikia mwito wetu leo na kwa ushirikiano mnaotoa kwa Watanzania katika majukumu yenu ya kila siku katika kuitumikia jamii. Kuna masuala mawili tungependa kuzungumza mbele yenu leo;

      Kwanza; kwa namna ya pekee, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kutekwa, kuteswa na kuumizwa vibaya kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini Dkt. Steven Ulimboka jijini Dar es salaam.
      Tukio hili limetukumbusha mambo mengi ambayo yamekifanya chama chetu kitafakari kwa kina suala zima la mgomo wa madaktari unaoendelea nchini. Kama tulivyowahi kusema mara kadhaa kuwa ni bahati mbaya sana kuwa madaktari wetu ambao kwa hakika ni wachache sana, wanalazimika kutumia haki yao ya kugoma katika kudai maboresho ya msingi kwenye sekta ya afya, jambo ambalo linagharamu maisha ya watu hususani wa kawaida (walalahoi) ambao matibabu yao hutegemea hospitali za umma.

      CHADEMA inaamini kuwa moja ya majukumu ya msingi ya serikali yoyote makini ni wajibu wa kulinda haki, mali na usalama wa kila raia na pia kuhakikisha kuwa huduma muhimu za jamii zinapatikana wakati wote kwa nchi nzima.
      Tukio la kutekwa nyara kwa kiongozi wa madaktari, Dkt. Ulimboka, si suala dogo wala la mzaha na haliwezi kuisha kwa MALALAMIKO tu, ya sisi wapinzani, wanaharakati na serikali yenyewe. Hapa ni lazima watu wenye wajibu wa kuhakikisha usalama huo wa raia wawajibike, hasa katika kutuambia ukweli wa nani aliyehusika na UGAIDI huu afahamike na hatua zichukuliwe dhidi yake.

      Tukio hili linatukumbusha njama mbalimbali ambazo zimekuwa zinafanywa na serikali dhalimu katika maeneo mengine duniani dhidi ya wapigania haki au wale wote wanaotoa mawazo mbadala dhidi ya watawala.
      Lakini pia katika nchi yetu hii leo, yapo mauaji ambayo yana kila harufu ya serikali, vyombo vyake na chama tawala kuhusika. Mfano mauaji ya kijanaMbwana Masoud, aliyeuawa huko Igunga mwaka Oktoba 2011, baada ya kutekwa na kuteswa.

      Mfano mwingine ni mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA Kata ya Usa River,Msafiri Mbwambo, huko Arumeru Aprili 2012, viongozi na wanaharakati kubambikiwa mashtaka ya uongo sehemu mbalimbli nchini, kuzingirwa kwaWabunge wa CHADEMA huko Mwanza, kisha wakapigwa na kuumizwa vibaya,wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, hususan viongozi wao, kunyimwa haki zao za kusomeshwa na kufunguliwa mashtaka yasiyo na msingi kwa sababu ya misimamo yao katika kudai haki, n.k.

      Lakini pia tukio hili linakumbushia matukio ya namna hii ambayo yamehusishwa na vyombo vya dola pamoja na CCM wakati wa chaguzi ndogo katika maeneo mbalimbali mathalani huko Kiteto, Biharamulo na Busanda ambako mpaka leo pamoja na kuwepo kwa viashiria vyote kuwa serikali, kwa maana ya dola ilihusika katika matukio ya namna hii ili kukisaidia CCM kushinda uchaguzi, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa zaidi ya polisi kukalia majalada hayo mpaka leo.

      Yote hayo hapo juu yanaimarisha msimamo wetu kuwa ni LAZIMA serikali iwe na jibu la kutekwa, kuteswa na kuumizwa vibaya kwa Dr. Ulimboka.

      Na katika hili CHADEMA tunaweka msimamo kuwa serikali haiwezi kuaminika katika kufanya uchunguzi, wala Jeshi la Polisi pia haliwezi kuwa na uhalali wa kufanya hiyo kazi. Mpaka sasa kwa mazingira yaliyopo, serikali ni mtuhumiwa katika tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa sana kwa Dkt. Ulimboka. Ni kanuni ya msingi sana katika dhana ya uongozi bora, kuwa mtuhumiwa hawezi kujichunguza mwenyewe.

      Wakati ambapo Watanzania wote tunaoitakia heri nchi yetu, tukiendelea kumwombea Dkt. Ulimboka katika wakati mgumu wa maumivu makali aliyonayo apone haraka, CHADEMA kinaitaka serikali kutohusika kwa namna yoyote katika uchunguzi wa tukio la Dkt. Ulimboka.

      Ili waliohusika wapatikane na kuwajibishwa, tunataka iundwe tume huru, itakayojumuisha watu wanaoaminika kutoka kada mbalimbali, ili ufanyike uchunguzi huru juu ya suala hili ambalo ni dhahiri limeibua taharuki nyingine katikati ya taharuki kubwa ya mgomo wa madaktari ambao unazidi kushika kasi kwa sababu ya serikali kutowajibika ipasavyo kwa wananchi walioiweka madarakani. Kuundwa kwa tume huru kuchunguza matukio au vifo tata kila inapotokea, imekuwa ni rai yetu mara kwa mara ili serikali ioneshe uongozi bora kwa vitendo.

      Mbali ya kuwa suala hili linahusu maisha ya binadamu ambayo hayana thamani ya kitu kingine chochote, bado pia ni kitendo kinachozima demokrasia na kuhatarishaamani ya taifa.

      Kuhusu mgomo wa madaktari

      Ndugu wanahabari suala la pili; lazima sasa mgomo huu wa madaktari unaoendelea umalizike kwa wananchi ambao ndio wanaoathirika, kuingilia kati iliserikali imalize mvutano na madaktari.
      CHADEMA kinaona suala hili kuwa zaidi ya “siasa”. Ni suala linalohusu maisha ya watu. Tunatoa mwito kwa watu wote wenye mapenzi mema kuungana katika kushinikiza mgomo wa madaktari kupatiwa suluhisho la kudumu ili kunusuru maisha ya Watanzania, hasa wasiokuwa na uwezo wa kutibiwa nje ya nchi kama viongozi wao. Dawa ya mgomo huu iko ndani ya uwezo wa serikali; isipokuwa tuhaina nia ya kweli na dhati kutatua tatizo hili kwa manufaa ya wananchi. Kwa kuwa serikali ni ya wananchi na serikali inawajibika kwa wananchi katika masuala yote, ikiwemo kuhakikisha huduma za jamii zinapatikana, ni lazima sasa wenye nchi hawa waoneshe msimamo wao katika suala hili. Tunawaomba Watanzania kusimama kuiwajibisha, ikiwa Serikali ya Rais Kikwete chini ya CCM, itaendelea kupuuza na kufanya mzaha katika suala hili linalohatarisha amani na utulivu wa taifa.

      Kama Serikali ya Rais Kikwete itaendelea kupuuza, hata baada ya msimamo wa wananchi wa kuitaka iwajibike kutatua tatizo hili, basi serikali hii itakuwa imeongeza idadi ya viashiria vinavyoikosesha uhalali wa kuongoza.

      Ndugu wanahabari, kwa kipekee kabisa tunawasihi Watanzania ambao ndiyo waathirika wakubwa wa mvutano kati ya serikali na madaktari, uliosababisha mgomo unaoendelea, wamtake Rais Jakaya Mrisho Kikwete amalize mgomo huumara moja kuzuia madhara makubwa kwa maisha ya binadamu.

      Tunasema hivyo kwa sababu, katika mgomo wa awali, Januari/Februari, baada ya wasaidizi wake, akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda kushindwa kuutatua, suala hili lilifika kwa Rais Kikwete, ambaye alikutana, kujadiliana na kufikia mwafaka na madaktari.
      Baada ya hapo aliwatangazia Watanzania wote kupitia ‘wazee wa Dar es Salaam’, kuwa mgomo umekwisha. Rais Kikwete aliahidi pia kuwa hakutakuwa na mgomo wa madaktari tena. Sasa tunamtaka Rais Kikwete atoke hadharani tena awaambie Watanzania vitu gani alikubaliana na madaktari, ametekeleza yapi na mangapi ambayo hayajatekelezwa mpaka sasa, kiasi madaktari wameamua kugoma tena,huku wananchi wakiumia. Serikali haiwezi kukwepa kuwajibika kwa madhara yoyote yanayotokea kwa maisha ya binadamu, kutokana na mgomo wa madaktari.

      Tunasisitiza huu ni wajibu wa Rais Kikwete kwa Watanzania, kwa sababu wanajua suala hili lilishafika kwake. Kinyume na hapo Watanzania wataendelea kujua wanaye rais wa namna gani katika kusimamia masuala ya msingi yanayoamua hatma yao, mtu mmoja mmoja na kama taifa.

      Kwa sababu Mhimili wa Bunge ambao ndiyo mwakilishi wa wananchi, ulipaswa kuwa tegemeo na kimbilio katika kuokoa maisha ya watu, umeonekana kuwa na meno ya plastiki na kushindwa kuwaokoa Watanzania, tunatumia fursa hiikuwataka Watanzania wote watimize wajibu wao wa kuitaka serikali na Rais Kikwete kumaliza mgomo huu.

      Ndugu wanahabari mwisho tunasema kuwa Serikali isiyoweza kuwahakikishia wananchi wake usalama na upatikanaji wa huduma zingine muhimu za jamii, mathalani; afya, elimu, maji, umeme n.k, ni serikali inayopoteza uhalali wa kuongoza.

      Imetolewa leo Juni 28, 2012 Dar es Salaam na;
      Singo K. Benson
      Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo-CHADEMA
      Kny. Katibu Mkuu

      Lazima wapinge wataachaje kupinga wakati wao ndio wamepanga mgomo na wao ndio waliomteka Dk Ulimboka kumpiga na kumtesa kwa manufaa yao ya kisiasa

      Sasa lazma wahofie uchunguzi huru ambao utawabainisha wao

      Ama kweli usilolijua ni sawa na usiku wa giza MAGAMBAGWANDA wakubwa nyie

    17. #34
      kitero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st February 2012
      Location : Kaskazini
      Posts : 516
      Rep Power : 469
      Likes Received
      97
      Likes Given
      48

      Mengi yaliyosemwa ni mazuri sana na naunga hoja mkono mia kwa mia,Ila kingine yale makubaliano yaliyo fikiwa awali kati ya Madaktari na serekali yapelekwe bungeni na yajadiliwe na wabunge serekali iseme imefikia wapi na madaktari waseme yao,hapa tutajua nani mwenye makosa kama nimadaktari wachukuliwe hatua zote kali kama niserekali tujue itawajibika vipi na kama niserekali na imeshindwa iachie wenye uwezo wa kuyatekeleza.
      FJM likes this.

    18. #35
      MANI's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 22nd February 2010
      Location : CHINI YA MBUYU
      Posts : 1,915
      Rep Power : 954
      Likes Received
      569
      Likes Given
      631

      Default Re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      Quote By kobello
      Mzungu ni mtu muhimu duniani. Sisi waswahili tupo tupo tu.
      Samahani, ila habari ndiyo hiyo.
      Kweli inasikitisha yaani mwenyeji hana maana kwake!
      " TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA"

    19. #36
      Mr Rocky's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th October 2007
      Location : Hungumalwa
      Posts : 9,181
      Rep Power : 46188
      Likes Received
      6512
      Likes Given
      5321

      Default Re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      Wakuu acheni kucopy taarifa nzima tunashindwa kufuatilia sisi tunaotumia simu samahani sana wakuu.

    20. #37
      mhalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2011
      Posts : 565
      Rep Power : 600
      Likes Received
      139
      Likes Given
      121

      Default Re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      hatuna imani na tume inayoongozwa na watuhumiwa.

    21. #38
      MKALIKENYA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 714
      Rep Power : 502
      Likes Received
      282
      Likes Given
      409

      Default

      Quote By Ally Kanah
      Lazima wapinge wataachaje kupinga wakati wao ndio wamepanga mgomo na wao ndio waliomteka Dk Ulimboka kumpiga na kumtesa kwa manufaa yao ya kisiasa

      Sasa lazma wahofie uchunguzi huru ambao utawabainisha wao

      Ama kweli usilolijua ni sawa na usiku wa giza MAGAMBAGWANDA wakubwa nyie
      Yani kama uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo mwenye hasara ni mama yako.

    22. #39
      majorbuyoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2012
      Posts : 663
      Rep Power : 2613
      Likes Received
      183
      Likes Given
      238

      Default Re: CHADEMA yapinga kuundwa tume kuchunguza tukio la Dk Ulimboka

      Quote By kanyi
      Tume ya nini? Usalama wa taifa ndio Wana husika kuchoma makanisa na kumpiga na kumuumiza Dr ulimboka
      Acha kuchanganya habari wewee!! tunaongelea habari za Dr. Ulimboka halafu wewe unaleta ishu za Uamsho.

    23. #40
      Ally Kanah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2011
      Posts : 780
      Rep Power : 559
      Likes Received
      37
      Likes Given
      35

      Default

      Quote By MKALIKENYA
      Yani kama uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo mwenye hasara ni mama yako.
      Tikitimaji ni tikiti maji nakusikitia coz hujui kwanini upo hapa Duniani GAMBAGWANDA mkubwa wewe

    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...