Madaktari wafukuzwa Mbeya, Bugando na Dodoma... Mwananyamala walazimishwa kusaini...
Taarifa ambazo zimethibitishwa zinatabanaisha kuwa madaktari walio katika uzoefu kazini, INTERN doctors wameanza kufukuzwa katika hospitali mbalimbali ambapo katika hospitali ya DODOMA madaktari 11 kati ya 33 wamefukuzwa na madaktari wote 70 waliokuwepo hospitali ya rufaa mbeya chini ya ulinzi mkali wa polisi wameambiwa waondoke kufikia saa 11 jioni ya leo wakati huo huo mkurugenzi wa hospitali ya BUGANDO amewafukuza madaktari wote 44 na kuwataka warudi wizarani wakati madaktari waliosajiriwa wameamuriwa kufika kesho wawe kazini au la wanafukuzwa.
Wakati huo huo madaktari wakazi waliitwa na senate ya BUGANDO na kulazimishwa kurudi kazini lakini walikataa mbele ya senate hiyo hivyo wakaambiwa watafutiwa udahili wao na wote kwa pamoja wakapiga makofi wakisema wako tayari kwa hilo.
Habari zaidi zinazidi kupasha kuwa hospitali ya Mwananyamala wameletewa fomu za kujaza kama wako tayari kuendelea na kazi au la,ila madaktari wamesimamia msimamo wao huo kuwa mgomo uko pale pale.
Katika hatua nyingine CHUO CHA TIBA BUGANDO NA KILE CHA MUHIMBILI VIKO MBIONI KUFUNGWA kutoka na walimu wao ambao ni madaktari kugoma na mazingira kutokuwa rafiki kwa kujifunzia.
Wakati hayo yakiendelea taarifa zinasema hsopitali ya Tanga BOMBO imeingia rasmi kwenye mgomo na ile ya MOUNT MERU
Habari zaidi madaktari wanajiandaa kwa mass resignation muda wowote
Re: Madaktari wafukuzwa Mbeya, Bugando na Dodoma... Mwananyamala walazimishwa kusaini...
By BAK
Nani amekwambia kuna watu tunasheherekea mgomo wa madaktari? Madaktari wanaomba kulipwa mishahara ambayo inaendana na taaluma yao ili waweze kukidhi gharama za maisha na pia kupewa vitendea kazi na kuboresha hospitali zetu ambazo zote ziko katika hali ya kutisha...Iweje Mbunge ambaye hajaenda shule apate mshahara mkubwa kuliko daktari aliyesota vyuoni miaka chungu nzima ili kuhitimu katika taaluma yake?
Hakuna hata Mtanzania mmoja anayesherehekea mgomo wa madaktari bali tunawaunga mkono kwa vile tunayaona madai yao yote yana umuhimu mkubwa katika kuboresha sekta ya afya nchi.
Mkuu umenifanya nitie neno hapa!
Huyo mtu uliyemjibu anawakilisha fikra halisi za mtanzania wa kawaida....
Mkuu wangu BAK, jamii hii inaundwa na aina ya watu wenye fikra dhoofu, zilizojaa uoga na unyonge wa hali ya juu.
Sijui Mungu alitumia sample ya udongo wa wapi kuumba watu wa namna kama yetu watanganyika (Ndio wazenji nimewatoa wao hawapo kama sisi).....
Tumekuwa watu wa kuamini kuwa sisi hadhi yetu ni "kidogo" , sisi ni "masikini" na mambo mengine mbona "kama kawaida tu"...
Mtu akifuatilia malalamiko tuyowalalamikia Madr leo hii anaweza kudhani kuwa hii nchi tatizo kuu letu kwa sasa ni madr tu ila vitu vingine kwenye sekta hii viko safi...
Tupate mwanga wa kuona mambo katika picha kubwa watz wenzangu ;
hatustahili kulala zaidi ya mtu mmoja kwenye kitanda kimoja hospitali
Xrays na mitambo mingine yote ya kiutendaji ifanye kazi kwa wakati wote
Madawa yote stahiki yapatikane kwa wakati tena kwenye eneo husika
Sehemu yoyote yenye kutolewa huduma ya afya lazima pawe na hadhi na paheshimiwe
nk.... nk......nk
Kama japo kwa udogo tu watz tungekuwa tunaamini katika hayo niliyoyataja hapo basi naamini hamna mtu ambaye angewaona madr ni watu wa ajabu katika madai yao na naamini kuwa watz wote tungewaunga mkono tena kwa msukumo mkubwa sababu tungeona haki yetu kubwa kwenye madai yao ......
Ila kwa bahati mbaya sana jamii yetu iliyo athirika na utapiamlo wa fikra kwa kubemendwa na utawala wa kichovu wa ccm, haoni mambo katika ngazi hiyo jamii nzima inaamini saiv adui namba moja ni Madr sababu wamezuia aina yao ya maisha ya "kama kawaida"..... Madr wapo kwenye mchakato wa kukata laana ya unyonge na maisha ya kudharirika ambayo yamejishikanisha na maisha ya kila siku ya Mtz...
Wito kwa waandishi wa habari, wabunge na idara nyingine za fikra za taifa hili si sahihi kuendelea kulisha sumu umma kuwa eti madr wanapigania maslahi yao tuu..
Pia kwa watz wenzangu tuache kuamini kuwa tunastahili kitu cha chini na cha hovyo... hapana... sisi ni wa thamani kama walivyo wazungu au wahindi au wachina na tunastahili huduma bora kama watu wa mataifa mengine, tukijidharau hakuna anayeweza kutuheshimu!
Re: Madaktari wafukuzwa mbeya,bugando na dodoma......mwananyamala walazimishwa kusaini,vyuo vya udak
By Kapeleka
Kufukuzwa madaktari siyo dawa, ila ni funzo. Hakuna haja ya wao kuendelea kuitwa watumishi wa umma wakati hawautumikii umma. 'Fukuza woooteee, kuanza upya si ujinga' Mjomba aliimba. Sifurahii kupigwa Dr. Ulimboka, ila ni funzo kwao na njia ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa mgomo wao. Madaktari hawapaswi kutumia wagonjwa kama kiboko cha kuichapia serikali kwa madai yao hata kama yanamsingi kiasi gani. Sasa je, wamegoma kumuudumia Dr. Ulimboka alipopata matatizo yanayowapata watanzania wengi.
Nakubaliana na unamuzi wa madakatari kufukuzwa wote wanaogoma, na hata wakitaka kujuizuru wote sawa. Serikali ijipange hata kwa gharama kubwa kuwaleta madaktari kutoka majeshi ya nchi marafiki na mashirika km red cross kusaidia wakati suluhu ikitafutwa ya kudumu.
Wewe unaongea FYONGO tuu wala hujui unalosema, kwanza sio wananchi waliofanya hayo ili kuonyesha hisia zao na pili kama unadhani madaktari wotee wakifutwa kazi na serekali kuanza moja kwa gharama yoyote unakosea mazima, mpaka sasa haya matatizo ni sababu serekali inashindwa kugharamia hao madaktari na miundombinu bora za huduma ya afya, sasa watawezaje kujipanga kwa gharama kubwa kuanza moja? acha kuwachukulia madaktari kama wako katika fani ya kitumwa, ile ni ajira kama ajira zingine wao sio malaika.
Re: Madaktari wafukuzwa Mbeya, Bugando na Dodoma... Mwananyamala walazimishwa kusaini...
Kwa nchi maskini kama Tanzania nadhani mgomo huu utakuwa kipimo cha mambo mengi sana na hakika mwisho wake ndio utatupa majibu. Binafsi yangu sintaunga mkono mgomo wa Madaktari ikiwa swala zima linatanguliwa na ongezeko la mishahara yao. Kama kweli sababu nyinginezo ni vyombo vya kutendea kazi, mazingira ya kazi na kadhalika, ilikuwaje walikubali kurudi kazini ambako hakuna vyombo vya kutendea kazi wala mazingira bora kwa afya zao na waginjwa?. Hivi kweli mtu unaweza vaa koti lako la udaktari ukijua fika kwamba mgonjwa unayemtibu hatapona kwa sababu hakuna vifaa, na unayaweka maisha yako hatarini lakini upo radhi kupokea mshahara wako kwa mwezi Ukisubiri JK ataongeza mishahara na kuleta vifaa baadaye!
Madaktari mtanichukia sana na wala maneno yangu hayampendezi mtu, isipokuwa nashindwa kabisa kuunganisha dots za mgomo huu na ule wa mwanzo kiasi kwamba walitaka kwanza mawaziri wajiuzuru ndipo mazungumzo yafuatie pamoja na kwamba tuliwaonya hapa kijiweni ya kwamba hili ni swala la kimfumo kuondoka kwa waziri na naibu wake hakuwezi badilisha kitu. Wao ni wafanyakazi waliochaguliwa na rais na wanafuata maagizo na mpango wa serikali ktk kutoa fedha za hutuma hiyo.
Lakini maajabu mkatuona majuha mkaenda Ikulu mkanywa juice na JK mkatoka huko na furaha tele baada ya sisi weniungine potozewa na ndugu na jamaa zetu kwa kile mlichodai ni haki yenu na sijasikia haki ya Wananchi japokuwa vipengele vyenu vinatujumuisha sote. Nasikitika sana kuona hali hii imefikia hapa lakini binafsi yangu nilijua tutafikia hapa. Na kwa bahati mbaya sana watu wamepoteza maisha wengine (kina Ulimboka) ndio mahtuti kwa jambo ambalo lingeweza kabisa kutatuliwa kisiasa zaidi kama vyama vya Upinzani vingehusishwa ktk kujua na kuhoji matumizi ya fedha ktk wizara hii ya Afya na Elimu.
Re: Madaktari wafukuzwa Mbeya, Bugando na Dodoma... Mwananyamala walazimishwa kusaini...
Siungi mkono kabisa ubabe unaoonyeshwa na serikali yetu, mbona madaktari wanasema wakae meza moja na serikali wamalize haya mambo shida iko wapi? Kinachofanywa na madaktari ni kuonyesha taswira nzima mahali jamii ya kitanzania ilipofika, Serikali wangetakiwa kutumia busara tu kulimaliza hili, lakini kwahiyi ya kuwatishia kufukuza, sijui.
Ikumbukwe Dr. wa Tanzania kwa haya maslahi wanayopata, tukifukuza wote hatuna uwezo wa kuajiri Dr. toka nchi nyingine, kwahiyo ni vema busara za serikali zikatumika, likiendelea hili kama juma zima wananchi wakitaharuki tu kwisha kazi
Kufukuzwa madaktari siyo dawa, ila ni funzo. Hakuna haja ya wao kuendelea kuitwa watumishi wa umma wakati hawautumikii umma. 'Fukuza woooteee, kuanza upya si ujinga' Mjomba aliimba. Sifurahii kupigwa Dr. Ulimboka, ila ni funzo kwao na njia ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa mgomo wao. Madaktari hawapaswi kutumia wagonjwa kama kiboko cha kuichapia serikali kwa madai yao hata kama yanamsingi kiasi gani. Sasa je, wamegoma kumuudumia Dr. Ulimboka alipopata matatizo yanayowapata watanzania wengi.
Nakubaliana na unamuzi wa madakatari kufukuzwa wote wanaogoma, na hata wakitaka kujuizuru wote sawa. Serikali ijipange hata kwa gharama kubwa kuwaleta madaktari kutoka majeshi ya nchi marafiki na mashirika km red cross kusaidia wakati suluhu ikitafutwa ya kudumu.
Re: Madaktari wafukuzwa Mbeya, Bugando na Dodoma... Mwananyamala walazimishwa kusaini...
Tatizo la tanzania hatuna viongozi bali tuna watawala. Hili ni tatizo lakuua professional leadership colleges kama mzumbe na kivukoni. Watawala wetu hawana knowledge, skill and aptitude katika leadership. na matokeo yake ndio haya. Irational scheme of services, poor management and distribution of national cake. Sasa moto wayaka, hii ni laana ya kutokusikiliza wazee. CCM inakwenda kufutika kabisa.
Re: Madaktari wafukuzwa Mbeya, Bugando na Dodoma... Mwananyamala walazimishwa kusaini...
it's getting more interesting now...ifike kipindi wanasiasa waheshimu taaluma za wenzao...
watu wamehenyeka miaka 6 hadi 7 kuwa tu MD, bado wale wanaobobea....
mwisho wa siku serikali isiyo sikivu inaishia kuwanyanyasa...
wengi tunaopinga mgomo huu ni kwa vile mnatambua umuhimu wa madaktari...
kwa kuwa mnatambua, ni vyema mngeungana nao kila mmoja katika kada yake....
kufanikisha azma ya kuutokomeza ubeberu wa serikali yetu...
naomba hili vuguvugu liendelee na kwa wenye vituo vya mafuta(yale mashangingi yao tuone kama yatatumia maji), madereva mabasi ya mikoani, makampuni ya simu(zimeni mitambo tuone kama watawasiliana)...
"Njia ya ukombozi ni ngumu, inawapasa wenye nia thabiti!"
"Ingawa tunatumia AVATARS na USERNAMES ambazo ni FAKE, bado haibadilishi uhalisia wa MIOYO YETU"
BODI ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari 72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya mkataba.
Imeelezwa kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo la 2009 kifungu namba F.16-F17 na F. 27.
"Hivyo kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu,"alisema Sigara.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe 23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi 19(Intern doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.
Alisema, kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns doctor 54 na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012 ambapo tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.
Sigara, aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.
Alisema, baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali ili waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka kanuni za kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi
"Iwapo madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo tarehe 28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,"alisema.
Aidha, alisema kuwa kwa ujumala madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.
Follow Us Here