Nia yangu sio kutukana ila jamani mimi maongezi yamenichosha, tunaingia humu tunachonga weee, tunaongea weee, tunaandika wee, labda nikubali kuwa hii ni namna ya kupunguza hasira zetu tu. Tuliwachagua wabunge wetu watuwakilishe na kutuhabarisha mambo yote yanayotendeka serikalini. Kwa kweli naomba niseme kwamba, especially wabunge wa upinzani wamejitahidi sana ktk kutuhabarisha na kutujulisha mapungufu na Madhaifu ya serikali yetu. Kuanzia EPA, Richmond, Kiwira, Rada, Ngege ya Rais,fedha za Uswiss, etc, etc.
Tunaona yaliyotokea kwa Mwakyembe, na sasa Ulimboka na wengine ambao kwa namna moja au nyingine wameadhibiwa katika kujaribu kutetea maslahi ya wananchi. Wengine hata walifikia kuhoji kwa nini aliukubali Uwaziri, na wengine kusema kwamba Mwakyembe kaufyata hivi mlitaka afanye nini?? Sisi kama watanzania tumempa support gani? hata ningekuwa mimi ningeufyata manake wale unaofanya jitihada ya kuwatetea hawaonyeshi hata nguvu angalau nusu ya kukuunga mkono kwenye harakati hizi.
Tumuangalie Ulimboka, kapigwa karibu ya kuuawa, tusubiri tuone sisi kama watanzania tutafanya nini angalau kuunga mkono ujasiri wake wa kutetea maslahi ya wenzake. Sirikali inasema madaktari watafute njia nyingine ya kudai madai yao na sio mgomo, hiyo sirikali imeona njia ya kumuadhibu Ulimboka ni sahihi? Anyway tuyaache hayo.
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kuanzia sasa tusiwalaumu wabunge wetu kwa lolote lile tena hapa naongelea pia baadhi ya wabunge wa CCM ambao wameonyesha kuipinga sirikali wazi wazi. Hawa watu wameishafanya ya kutosha kutuhabarisha mabovu ya sirikali yetu, wizi, mikataba mibovu, ubinafsishaji kwa maslahi binafsi, n.k. Sisi kama Watanzania tunawapa support gani?? Jamani kama hatufahamu sisi ndio wamiliki halali wa nchi hii, tuna sauti kubwa na yenye nguvu sana kama tutaamua leo hii kwamba huu upuuzi wa viongozi wetu basi. Tafakari Chukua Hatua!

Reply With Quote


Follow Us Here