Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

    Report Post
    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 103
    1. #1
      Maseto's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 180
      Rep Power : 605
      Likes Received
      90
      Likes Given
      3

      Default Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Kitendo cha kumtaka Waziri Mkuu Pinda ajiuzulu, Mhe. Lissu hakutenda haki. Pinda mara alipoteuliwa tu kuwa waziri Mkuu alijitambulisha kuwa ni mtoto wa mkulima.

      Kusema hivyo haimaanishi kuwa yeye ni mkulima. Na wote tunajua jinsi watoto wa wakulima wasivyopenda kilimo. Kwa hiyo kumtaka mtoto wa mkulima arudi kulima, aache ulaji alionao sasa, ni sawa na kumwambia ajiue.

      Lisu alimtaka PM ajiuzulu wadhifa huo kwa kushindwa kutatua suala la mgomo wa madaktari wakati wa maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu,leo asubuhi.Katika hatua ya kustaabisha,Pinda amekiri kuwa amefanya kila awezalo na ameshindwa.Ndipo katika swali la pili la nyongeza,Lisu akirudia wito wake ule ule alioutoa katika swali la msingi,kwa kiingilishi alisema:

      'If you have done everything in your power and failed why don't you resign?'

      Spika akasema swali hilo lisijibiwe kwani limerudiwa.

      Lakini Pinda alisema '...Mhe. Lissu lugha hiyo si nzuri sana... mimi nakuheshimu sana....'

    2. Miaka 50

    3. #21
      Elizabeth Dominic's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 7th December 2007
      Posts : 2,730
      Rep Power : 5462
      Likes Received
      1959
      Likes Given
      2652

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Quote By MALUNGU
      mfano kulia bungeni 2009, "liwalo na liwe" jana na madudu kibao ambayo anakosa maamuzi.
      The list is endless kusema kweli...............huyu yuko kwenye top of the list ya watu wanaotakiwa waondoke kabisa kwenye uongozi halafu i hate his pretentiousness
      BE RESPECTED............DEMAND RESPECT

    4. #22
      Zinjathropus's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2010
      Posts : 501
      Rep Power : 537
      Likes Received
      149
      Likes Given
      40

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Quote By FJM
      Kwa watu wanaoelewa na kukubali utawala wa demokrasia/vyama vingi, basi watakubaliana na kauli ya Lissu 100%. Alichosema na namna alivyosema Lissu ndivyo inavyotakiwa. Mh Pinda anafanya 'zilipendwa' akisaidiwa na Spika, lakini gharama za huu muziki wa zilipendwa zitalipwa na CCM.

      Kwa kiongozi yoyote ambaye anashindwa kufanya yale anayooamini na ambayo wanachi wanamtegemea kwa sababu zozote zile (iwe mfumo, ugonjwa, whatever) basi kiongozi huyo anatakiwa ajiuzulu. Kuendelea kukalia kiti ni sawa na kugeuka jiwe. Katika hali ya sasa Pinda hawezi kusema ameshindwa kutatua mgogoro wa madaktari halafu akaendelea na kazi zake kama Waziri mkuu. Haiwezekani. Ama unaondoa vizingiti (mfumo mbaya) au vizingiti vinakuondoa. Lakini vyote viwili haviwezi kubaki halafu tukasema tuna uongozi bora. Tuna shida sana na mentality ya zilipendwa.
      Kaka hiyo point lakini tusiache na kuangalia upande wa pili point yako kuu kuhusu suala la utawala wa demokrasia na siasa za vyama. Ambapo utawala uliopo unaposhindwa kutatua matatizo ya jamii inaweza ondolewa vilevile kwa namna hilehile iliyo ifikisha hapo.

      Kwa maana hiyo madaktari pia walikuwa na option ya kusema uchaguzi ujao CCM isipojirekebisha watachagua chama mbadala kitakachojali maslahi yao, lakini suala la kusema adui ni Pinda pekee ni la kipuuzi. Yeye ni mtekelezaji lakini si mpanga bajeti za serikali, akisema kajitahidi kashindwa ni kwamba hana tena huwezo wa kuwashawishi wanao toa hizo hela hili hayo mahitaji yakamilishwe sasa why him always?

      Serikali ndio inayopanga priorities za matumizi ikiongozwa na sera za chama tawala, kama CCM ni wezi na hawajali makazi na mazingira ya kazi ya madaktari si kosa la mgonjwa kupewa adhabu. Ni madktari kutafuta mbinu zao especially pressuring hili kuijuza jamii ubovu wa makazi na matibabu unatokana na vyanzo vipi hili watu wajue wanapoichagua CCM wajue kabisa kulala chini ni mtindo mmoja na kutopata huduma sahihi is a norm.

      Serikali inamajukumu mengi na mahitaji mengi na makundi mengi ya kuyaridhisha katika bajeti hiyo hiyo uchwara ni vigumu kuliridhisha kila kundi katika jamii hila so far serikali yetu imejikita katika kujiridhia wao tu. lakini si kosa la mgonjwa kwenye jamii yeye si mpangaji kabisa wa matumizi na pengine hata hajui haki zake nchini.

      Madkatari kama wasomi wana jukumu la kutoa pressure zao kupitia maandishi magazetini au audio media's kuujulisha umma katika harakati za kuitoa serikali mbovu kama wanaiona hivyo. Lakini kwa kuwa adhibu wagonjwa au kumtaja Pinda kila saa ni weak arguments na kutuachia maswali mengi sana kuhusu uwezo wao wa kufikiri madkatari wetu; au labda hawa amini kama CCM inaweza tolewa madarakani ndio maana inawaadhibu wasio stahili kupitia adhabu kwa wasio husika, now that is not thinking outside the democracy of multi parties.
      Last edited by Zinjathropus; 28th June 2012 at 14:43.

    5. #23
      tatanyengo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th March 2011
      Posts : 931
      Rep Power : 598
      Likes Received
      219
      Likes Given
      186

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Lugha laini do nini?
      Quote By Ileje
      Pamoja na ukweli huo wa kumtaka Pinda ajiuzuru kwa kushindwa kutatua tatizo la madaktari lakini ukweli utabaki kuwa Lisu aliuliza swali la nyongeza kwa sauti (Tone) ya kejeli na hivyo kumfanya Pinda kukasirika!

      Ni maoni yangu kuwaasa wabunge na hasa wa upinzani watumie lugha ya heshima na laini wanapouliza maswali magumu au kutoa hoja ngumu kwa serikali!
      'Our Problems can be solved,our challenges can be met'- Obama

    6. #24
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      tangu jana jioni pinda akili yake haijakaa sawa....kuna kitu kinalia ndani ya nafsi yake chenye kuashiria dhulma kwa watanznaia
      I'm Naturaly Evasive..

    7. #25
      Mundu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2008
      Posts : 1,680
      Rep Power : 879
      Likes Received
      228
      Likes Given
      22

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Hakuna kauli yanye heshima katika mambo ya dharula... Pinda na Bi Mkora walipaswa kujua hivyo siku nyingi. Watanzania maskini wanaugulia bila kujua hatima yao. Afu anakuja mtu kama Pinda (Prime Minister) anasema; 1st: "Litakalotokea na litokee, liwalo na liwe" 2nd: "Nimejitahidi kadri nilivyoweza, lakini nimeshindwa". sasa hapo mlitaka Tundu ampigie magoti na kumwambia "JARIBU TENA BABA"? Maisha ya watu wa Tanzania siyo ya kuyachezea bahati nasibu...

      kama PM ameshindwa kutatua mgogoro wa madaktari basi na aje na solution ili maisha ya wananchi hawa wanyonge yasiendelee kupukutika kama majani ya kiangazi...na Asipokuwa na solution, basi na aondoke, ajiuzuru...kazi imemshinda!!

      Keep it up Lissu...
      Mswahili jambo la kipumbavu likisemwa kizungu, anaona sawasawa kabisa!! J.K.Nyerere

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      Sikonge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2008
      Location : Sikonge, Tabora
      Posts : 7,847
      Rep Power : 2330
      Likes Received
      2855
      Likes Given
      5501

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Lisu siyo SHOGA kuongea na Mwanaume mwingine kwa SAUTI LAINI.

      Hiyo ya kuongea na PM kwa sauti laini ni kazi ya Mamaa Tunu Pinda.


      Quote By Ileje
      Pamoja na ukweli huo wa kumtaka Pinda ajiuzuru kwa kushindwa kutatua tatizo la madaktari lakini ukweli utabaki kuwa Lisu aliuliza swali la nyongeza kwa sauti (Tone) ya kejeli na hivyo kumfanya Pinda kukasirika!

      Ni maoni yangu kuwaasa wabunge na hasa wa upinzani watumie lugha ya heshima na laini wanapouliza maswali magumu au kutoa hoja ngumu kwa serikali!
      Kigogo likes this.
      Nguruwe pita leo sina Mkuki(By Malila wa JF).

    10. #27
      bullet's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2009
      Location : East London
      Posts : 365
      Rep Power : 563
      Likes Received
      116
      Likes Given
      129

      Default

      Quote By MTK
      'If you have done everything in your power and failed why dont you resign?" the statement is clear full stop.
      True indeed,
      Why does'nt Hon Pinda learn from Boniphace Mkwasa who resigned recently on seeing his skills and efforts to help Twiga Stars ended fruitless!!?

    11. #28
      Keen's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th September 2007
      Posts : 414
      Rep Power : 677
      Likes Received
      97
      Likes Given
      125

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Quote By Maseto
      Kitendo cha kumtaka Waziri Mkuu Pinda ajiuzulu, Mhe.Lisu hakutenda haki.Pinda mara alipoteuliwa tu kuwa waziri Mkuu alijitambulisha kuwa ni mtoto wa mkulima.Kusema hivyo haimaanishi kuwa yeye ni mkulima.Na wote tunajua jinsi watoto wa wakulima wasivyopenda kilimo.Kwa hiyo kumtaka mtoto wa mkulima arudi kulima,aache ulaji alionao sasa,ni sawa na kumwambia ajiue.
      Lisu alimtaka PM ajiuzulu wadhifa huo kwa kushindwa kutatua suala la mgomo wa madaktari wakati wa maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu,leo asubuhi.Katika hatua ya kustaabisha,Pinda amekiri kuwa amefanya kila awezalo na ameshindwa.Ndipo katika swali la pili la nyongeza,Lisu akirudia wito wake ule ule alioutoa katika swali la msingi,kwa kiingilishi alisema : 'If you have done everything in your power and failed why dont you resign?'.Spika akasema swali hilo lisijibiwe kwani limerudiwa.Lakini Pinda alisema '...Mhe.Lisu lugha hiyo si nzuri sana.....mimi nakuheshimu sana....'
      "Every object continues in its state of rest, or of uniform motion in a straight line, unless compelled to change that state by external forces acted upon it" Newton's first law of motion. Katika hali ya kawaida na hasa siasa za kiafrica, Mzee Pinda hawezi kujiuzuru bila kuwepo na misuko suko kama hiyo ya Mh. Lissu-"External Force" Kumbuka bila kelele za wabunge kuna waheshimiwa mawaziri waliokuwa wanatuhumiwa kutumia ofisi vibaya walikuwa wameapa kutojiuzuru, lakini kwa sababu kulikuwa na "external force" ilimlazimu H.E. Hon. Kikwete kuwatema!! Go ahead Lissu. Tanzania bila PM Pinda inawezekana.

    12. #29
      bensonlifua92's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th December 2010
      Posts : 82
      Rep Power : 444
      Likes Received
      32
      Likes Given
      32

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Quote By MTK
      'If you have done everything in your power and failed why dont you resign?" the statement is clear full stop.

      PM alihamaki bure, hii ilitokana na statement yake kuwa amefanya kila aliloweza na bado mgomo upo sasa atafanya nini zadi ili mgomo usiwepo? Lisu yuko sawa, hapo suala la kuheshimiana au kuto heshimiana halina uhusiano na swali. Alitakiwa kusema siwezi ku-resign sasa labda tunajaribu hatua za pamoja mfano labda na rais, au...... sasa kigumu hapo ni nini....

      Au maneno yale ya "LIWALO na LIWE" ndo yanampa shida PM maana huenda hakutarajia kama yangekutana na tukio hili la Dr. Ulimboka kutekwa na kuteswa/au kukusudiwa kuuawa, sasa kiasi ni kama yanamuhukumu hivi au wana JF mnalionaje hilo....

    13. #30
      watu8's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th February 2010
      Location : Juu ya Tukutuku
      Posts : 14,979
      Rep Power : 31268
      Likes Received
      7412
      Likes Given
      7402

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Quote By Maseto
      Kitendo cha kumtaka Waziri Mkuu Pinda ajiuzulu, Mhe.Lisu hakutenda haki.Pinda mara alipoteuliwa tu kuwa waziri Mkuu alijitambulisha kuwa ni mtoto wa mkulima.Kusema hivyo haimaanishi kuwa yeye ni mkulima.Na wote tunajua jinsi watoto wa wakulima wasivyopenda kilimo.Kwa hiyo kumtaka mtoto wa mkulima arudi kulima,aache ulaji alionao sasa,ni sawa na kumwambia ajiue.
      Lisu alimtaka PM ajiuzulu wadhifa huo kwa kushindwa kutatua suala la mgomo wa madaktari wakati wa maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu,leo asubuhi.Katika hatua ya kustaabisha,Pinda amekiri kuwa amefanya kila awezalo na ameshindwa.Ndipo katika swali la pili la nyongeza,Lisu akirudia wito wake ule ule alioutoa katika swali la msingi,kwa kiingilishi alisema : 'If you have done everything in your power and failed why dont you resign?'.Spika akasema swali hilo lisijibiwe kwani limerudiwa.Lakini Pinda alisema '...Mhe.Lisu lugha hiyo si nzuri sana.....mimi nakuheshimu sana....'
      ...kumtaka mtoto wa mkulima arudi kulima,aache ulaji alionao sasa,ni sawa na kumwambia ajiue...

      Ulichoandika hapa si sawa kwani umeshindwa kujenga hoja. Suala la uwajibikaji wa kimadaraka matokeo yake sio kifo. Hivyo hakuna ulinganifu mkuu.

      Lisu alimtaka PM ajiuzulu wadhifa huo kwa kushindwa kutatua suala la mgomo wa madaktari...

      Sidhani kama hicho ndicho Tundu Lissu alichomaanisha, ila majibu ya mheshimiwa Waziri Mkuu ndio hasa yaliyopelekea ndugu Lissu amshinikize Waziri Mkuu ajiuzulu. Kitendo cha Waziri Mkuu kukiri kuwa, " nimefanya kila niwezalo na nimeshindwa", huu ni udhaifu kimadaraka. Maana ya kauli hii ni marudio ya ile kauli yake tata ya "liwalo na liwe", ila tu wakati huu imetolewa kwa lugha laini.

      Katika hatua ya kustaabisha...

      Mwisho, sasa ndugu mleta mada hii kama umestaajabishwa na kauli ya Pinda, mbona kichwa cha habari hakioneshi hivyo?
      "Ingawa tunatumia AVATARS na USERNAMES ambazo ni FAKE, bado haibadilishi uhalisia wa MIOYO YETU"



    14. #31
      Uwezo Tunao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 6,867
      Rep Power : 2288
      Likes Received
      1131
      Likes Given
      1478

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Kwa mtaji wa 'LIWALO NA LIWE' na kweli likawa kwa Dr Ulimboka, Mh Pinda hahitaji kusubiri zaidi kusukumwa nje ya ofisi pamoja na aliyemtuma!!!!!!!!!!!!!

    15. #32
      Kiraka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st February 2010
      Location : ILOGANZALA
      Posts : 1,352
      Rep Power : 742
      Likes Received
      258
      Likes Given
      438

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      [QUOTE=Ileje;4137825]Pamoja na ukweli huo wa kumtaka Pinda ajiuzuru kwa kushindwa kutatua tatizo la madaktari lakini ukweli utabaki kuwa Lisu aliuliza swali la nyongeza kwa sauti (Tone) ya kejeli na hivyo kumfanya Pinda kukasirika!

      Ni maoni yangu kuwaasa wabunge na hasa wa upinzani watumie lugha ya heshima na laini wanapouliza maswali magumu au kutoa hoja ngumu kwa serikali![/QUOTE]

      Tumefika hapa kwa ajili ya kudanganyana na kubebana huku, jitu ni mbwa mwitu wewe unaliita mbuzi!!!!
      Form is temporary, Class is permanent...

    16. #33
      Jabulani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th March 2009
      Location : Kituo cha Polisi Jamii
      Posts : 2,972
      Rep Power : 1369
      Likes Received
      820
      Likes Given
      254

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Lakini kuna kweli fulani hapo. If you have done everything in your power and failed why dont you resign?
      Kamanda wa Polisi Jamii - Kanda Maalumu

    17. #34
      bensonlifua92's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th December 2010
      Posts : 82
      Rep Power : 444
      Likes Received
      32
      Likes Given
      32

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Quote By Ileje
      Pamoja na ukweli huo wa kumtaka Pinda ajiuzuru kwa kushindwa kutatua tatizo la madaktari lakini ukweli utabaki kuwa Lisu aliuliza swali la nyongeza kwa sauti (Tone) ya kejeli na hivyo kumfanya Pinda kukasirika!

      Ni maoni yangu kuwaasa wabunge na hasa wa upinzani watumie lugha ya heshima na laini wanapouliza maswali magumu au kutoa hoja ngumu kwa serikali!
      Pamoja na kuwa nimekupa like, but ngoja pia tuweke clear

      Maandiko yanasema hivi....Anaye STAHILI heshima apewe heshima. Hapo neno "stahili" ni muhimu sana. Mtu kama unafanya mambo yenye manufaa kwa wananchi kweli unastahili kujibiwa kwa heshima au kuulizwa swali kwa heshima (tone ya sauti) ila saa nyingine tunasababisha watu wengine wasikie vibaya kwa matendo yetu kuwa hayana faida kwa taifa na ndo maana wengine wanafikia hii hatua ya hizo tone za sauti ambazo wewe umesemea

      Hata hivyo assessment yako kuwa lisu alikejeli ktk swali lake la nyongeza kwa kusikiliza tone ya sauti ya lisu is somehow so subjective and may be unrealistic, how do you know moyo wa lisu kuwa alipotoa hiyo sauti (tone) alimaanisha kumkejeli PM.., yah ni maoni yangu tuu...
      Mr Rocky likes this.

    18. #35
      Etairo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th January 2012
      Posts : 234
      Rep Power : 416
      Likes Received
      42
      Likes Given
      104

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Bravo FJM. huo ndo ukweli-uwezi ukashindwa kumaliza tatizo kwa kusema nikejaribu nimeshindwa -that's not a solution, we want solution and not ezcuse. Tangu awali Bw. Pinda alionesha tabia ya kutaka kuonewa huruma kwa kisingizio cha mtoto wa mkulima. Kiongozi mkubwa kama yeye lazima awe na detarmination and conclusive decision. Asitegemee kuonewa huruma
      Spika na naibu wako =please-msiwafunge kwa namna moja au nyingine wapinzani wa ndani ya ccm na wale wa cdm kusema ukweli -wananchi wanaona na kusikia-enzi za kufumbia masuala kwa msingi wa wenzetu umepitwa na wakati.
      Nimabie Mh. spika-bunge lako lina mpango gani wa kuwaelemisha wabunge kuhusu kuwa wakweli? Ni vipi mbuge aunge mkono kwa asilimia 300 ilihali anachambua hotuba kwa upande wa kushindwa kutekelezwa? Huoni kuwa mnawafanya wanachi mbumbumbu?
      Tumechoka please-spika weka utaratibu, kwa aayeunga mkono bajeti basi asiwe na malalamiko dhidi ya wizara na bajeti husika, la wabunge wawe wazi -wapinge na hata kutaka maelezo bora ya kwa nini bajeti iliyopita ikiwa na mipango ya utekelezaji wa miradi katika majimbo fulani haikutekelezwa?

    19. #36
      KOMBAJR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th November 2011
      Posts : 3,853
      Rep Power : 5948
      Likes Received
      798
      Likes Given
      227

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Hawa dawa yao kuwaambiwa ukweli hakuna kupaka mafuta..........
      Face Reality As it Is, Not As it Was or As You Wish It To Be.

    20. #37
      Bobuk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 2,056
      Rep Power : 920
      Likes Received
      829
      Likes Given
      0

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Pinda sio mtoto wa mkulima ni Mtoto wa Al shabaab ndiyo maana amemtumnia magaidi wenzeka Dr. Ulimboka! Eti liwalo na liwe. Al Shabaab utawajua tu kwa matendo yao, Pinda ni mmoja wao.

    21. #38
      Mzalendo80's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2010
      Location : Magogoni, Tanganyika
      Posts : 2,270
      Rep Power : 958
      Likes Received
      815
      Likes Given
      1589

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      You want respect Pinda Bin Dhaifu? You will have to earn it.
      The CCM is a crime syndicate, Most members and MPs of CCM are corrupt. No conceince, No brains no nothing, just bunches of criminal and theft. Corruption cost mlalahoi in de street.

    22. #39
      Etairo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th January 2012
      Posts : 234
      Rep Power : 416
      Likes Received
      42
      Likes Given
      104

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Kiraka bwana-lugha ya stara inaenda kwa wenye sitara siyo kwa wahuni? Mbona tunaona lugha ya kejeli kwa wapinzani tu lkn inanenwa na wa ccm inakuwa lugha ya wastararbu? nani aliinua mdomo kusema Mwiguru anachangia kwa lugh aya kejeli kwa wapinzania? Au kejeli ni kwa pinda tu. afanye kazi -asitake huruma kwa wapinzani-siyo wa kuunga mkono kokote kule ulimwenguni -bali ni kazi ya watawala kutoa majibu ya kuonesha kuwa wapinzani wan nongwa -watawala wasitegemee kusifiwa. Na bado......Naunga mkono pinda kuanza mbele -ameshindwa kutendas badal yake anatoa lugha za kutia kichefuchefu-LIWALO NA LIWE -LIPI HILO?
      Kizotaka likes this.

    23. #40
      Etairo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th January 2012
      Posts : 234
      Rep Power : 416
      Likes Received
      42
      Likes Given
      104

      Default re: Tundu Lissu hukumtendea haki Pinda kumtaka ajiuzulu

      Tundu as far as i know you since schooling at galanos SS -tanga I am always with confidence into you, keep it -this nation wants people -courageus enough to push things ahead with fear.

    24. Study Abroad
    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...