Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

    Report Post
    Results 1 to 11 of 11
    1. #1
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,344
      Rep Power : 692
      Likes Received
      649
      Likes Given
      382

      Default Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

      Ktk maisha kuna msemo malipo ni hapa hapa duniani.Kwa maana ya uovu utakaofanya dhidi ya binadamu mwenzako malipo ni hapa hapa duniani.Nchi ambayo sina haja ya kuitaja kwa sasa inakabiliwa na mfululizo wa matukio ambayo kwa kweli hayaishi na unaweza kujiuliza mbona mambo hayo hayafikii ukomo.Kila kukicha ni matatizo ambayo kwa akili ya kawaida yangeweza kupatiwa ufumbuzi ila bila shaka kutokana na laana ambayo kwa sasa viongozi wanaitumikia bila kujijua wamejikuta wanakosa busara na maarifa ya kuyatatua na badala yake ni kama wanatia pili pili kwenye kidonda.Kinachowasumbua ni hii laana wanayoitumikia kutokana na dhuluma,uonevu,unyanyasaji na ukandamizaji dhidi ya watu wao wenyewe na sasa haya ni matokea ya kilio cha watu hawa ambapo mwenye mamlaka kuliko wote sasa amesika kilio chao na ameshusha laana hii inayowafanya wakose busara na sasa wanajikuta wanashindwa kuongoza na kinachofuata ni wao kuanguka ktk utawala wao.

      Ushahidi wa haya niyasemayo ni wao kukosa busara ya kuyashughulikia na badala yake wanaumbuka kila kukicha.Kwa kifupi mwenye mamlaka kuliko wote kawashushia laana na wanajikiuta wanakosa dira na mwelekeo.Hawa watu unaweza kuwafananishi na wale waliokuwa wanajenga ule mnara maarufu ktk vitabu vitakatifu unaoitwa mnara wa babeli kwa lengo la kumfikia huyu mwenye mamlaka.Aliwashushia laana wakajikuta hawaelewani ktk lugha na hivyo kusambaratika.Sasa hawa jamaa nao kaamua kuwaadhibu kwa staili ile ile ila tofauti ni kuwa kawaacha na lugha yao moja ila alichokifanya ni kuwanyima busara na hekima ya kutatua matatizo na mwisho wa siku watajikuta wanaelemewa na kuanguka.

      Maovu waliyoyafanya kwa watu wao ni mengi mno mfano kuuza maliasili za watu wao,kuwapora ardhi yao,kuwanyanyasha na mengine mengi.Matokea yake sasa ni nchi ile kujikuta ikiachwa na mashimo na uharibifu wa mazingira baada ya wao na washirika wao kupora maliasili za watu wao.

      Hatua waliofikia naifananisha na ule msemo wa kiswahili unaosema siku ya kufa nyani miti yote huteleza.Wamefikia kikomo na sasa wanatapatapa tu kama mfa maji.Laana hii ndio inawafanya watoe kauli za kuwarudi wao wenyewe na kuongeza matatizo na sio kauli tu bali hata matendo yao nayo yanawagharimu kila kukicha.

      Kila kitu kina mwanzo na mwisho.
      Last edited by Salary Slip; 28th June 2012 at 21:54.

    2. RukaaJuu Final

    3. #2
      Paul Katyega's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 139
      Rep Power : 387
      Likes Received
      29
      Likes Given
      23

      Default Re: Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

      Tusubiri tuone nini kitajiri.

    4. #3
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,727
      Rep Power : 910
      Likes Received
      435
      Likes Given
      440

      Default Re: Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

      na bado...mass resignation inakuja,stay tuned

    5. #4
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,344
      Rep Power : 692
      Likes Received
      649
      Likes Given
      382

      Default Re: Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

      Ok,mkuu nimekusikia.

    6. #5
      BJEVI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2011
      Posts : 745
      Rep Power : 572
      Likes Received
      158
      Likes Given
      138

      Default Re: Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

      haya bwana.MUNGU TUNUSURU

    7. Miaka 50

    8. #6
      Nyetk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2012
      Posts : 1,028
      Rep Power : 682
      Likes Received
      574
      Likes Given
      590

      Default Re: Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

      Quote By Salary slip
      Ktk maisha kuna msemo malipo ni hapa hapa duniani. Maana yake ni kwamba uovu utakaofanya dhidi ya binadamu mwenzako malipo ni hapa hapa duniani. Nchi ambayo sina haja ya kuitaja kwa sasa inakabiliwa na mfululizo wa matukio ambayo kwa kweli hayaishi na unaweza kujiuliza mbona mambo hayo hayafikii ukomo. Kila kukicha ni matatizo ambayo kwa akili ya kawaida yangeweza kupatiwa ufumbuzi ila bila shaka kutokana na laana ambayo kwa sasa viongozi wanaitumikia bila kujijua wamejikuta wanakosa busara ya kuyatatua na badala yake ni kama wanatia pili pili kwenye kidonda. Kinachowasumbua ni hii laana wanayoitumikia kutokana na dhuluma, uonevu, unyanyasaji na ukandamizaji dhidi ya watu wao wenyewe na sasa haya ni matokea ya kilio cha watu hawa ambapo mwenye mamlaka kuliko wote sasa amesika kilio chao na ameshusha laana hii inayowafanya wakose busara na sasa wanajikuta wanashindwa kuongoza na kinachofuata ni wao kuanguka ktk utawala wao.

      Ushahidi wa haya niyasemayo ni wao kukosa busara ya kuyashughulikia na badala yake wanaumbuka kila kukicha. Kwa kifupi mwenye mamlaka kuliko wote kawashushia laana na wanajikiuta wanakosa dira na mwelekeo. Hawa watu unaweza kuwafananishi na wale waliokuwa wanajenga ule mnara maarufu ktk vitabu vitakatifu unaoitwa Mnara wa Babeli kwa lengo la kumfikia huyu mwenye mamlaka. Aliwashushia laana wakajikuta hawaelewani ktk lugha na hivyo kusambaratika. Sasa hawa jamaa nao kaamua kuwaadhibu kwa staili ile ile ila tofauti ni kuwa kawaacha na lugha yao moja ila alichokifanya ni kuwanyima busara na hekima ya kutatua matatizo na mwisho wa siku watajikuta wanaelemewa na kuanguka.

      Maovu waliyoyafanya kwa watu wao ni mengi mno mfano kuuza maliasili za watu wao, kuwapora ardhi yao, kuwanyanyasha na mengine mengi. Matokea yake sasa ni nchi ile kujikuta ikiachwa na mashimo na uharibifu wa mazingira baada ya wao na washirika wao kupora maliasili za watu wao.

      Hatua waliofikia naifananisha na ule msemo wa kiswahili unaosema siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Wamefikia kikomo na sasa wanatapatapa tu kama mfa maji. Laana hii ndio inawafanya watoe kauli za kuwarudi wao wenyewe na kuongeza matatizo na sio kauli tu bali hata matendo yao nayo yanawagharimu kila kukicha. Kila kitu kina mwanzo na mwisho.
      Sorry. nilikuwa nakusaidia tu ku-edit ili usomeke.

    9. #7
      Shine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2011
      Posts : 9,185
      Rep Power : 2429
      Likes Received
      945
      Likes Given
      377

      Default

      Quote By BJEVI
      haya bwana.MUNGU TUNUSURU
      Atunusuru sisi na siyo hawa wanyang'anyi wa haki za waTz

    10. #8
      Shine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2011
      Posts : 9,185
      Rep Power : 2429
      Likes Received
      945
      Likes Given
      377

      Default Re: Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

      Mkuu umenena ila na sisi kama waTZ yafaa tujitambue na kujua haki zetu kama sasa huduma za afya hatupati yafaa tutumie njia thabiti ya kuingia barabarani na kuikataa serikali hii iliyoshindwa kuiongoza hii ktk nyanja zote!

    11. #9
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,344
      Rep Power : 692
      Likes Received
      649
      Likes Given
      382

      Default Re: Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

      Sawa mkuu.Nimekusikia.

    12. #10
      Gosbertgoodluck's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd March 2008
      Posts : 2,863
      Rep Power : 1149
      Likes Received
      334
      Likes Given
      4

      Default Re: Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

      Naunga mkono mawazo yako.

    13. #11
      Bangoo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2011
      Posts : 2,271
      Rep Power : 836
      Likes Received
      371
      Likes Given
      0

      Default Re: Nchii hii haiwezi kutulia mpaka laana hii itimie

      Ni kweli kabisa!

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...