Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

    Report Post
    Page 23 of 40 FirstFirst ... 13212223242533 ... LastLast
    Results 441 to 460 of 791
    1. #1
      Fred Katulanda's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st April 2011
      Location : Mwanza, Tanzania
      Posts : 209
      Rep Power : 461
      Likes Received
      213
      Likes Given
      67

      Default Kilichomtokea Dk. Ulimboka ni hiki hapa...

      "Ndugu zangu,

      Najaribu kutuliza mawazo ili angalau niweze kuwapa kidogo tulipofikia na tunakoelekea juu ya suala hili. Kwa kweli haivumiliki ukimwona ulimboka kwa jinsi alivyotendewa na hali aliyonayo; kwa wale wanaojua hali za kitabibu, "this is a very unstable condition that demands permanent watch 24/7".

      Kwa taarifa tulizokusanya, ulimboka na mwenzake waliitwa na Afisa mmoja (Jina linahifadhiwa) ili kuzungumza mambo (fulani) na wakiwa wanaendelea na mazungumzo bila kuwa na mwelekeo wa muafaka, jamaa akawasiliana na watu (fulani) kwa simu. Ghafla wakajitokeza "ASKARI" wakawataka yule (Afisa) na Dr (aliyeongozana na Ulimboka) waendelee na shughuli zao na kuwambia "Tunamtaka huyu". Wakatumia nguvu, wakamburuta na kumtia kwenye gari jeusi na kuondoka naye wakidai wanampeleka Polisi.

      Huku wakiwa wanamtesa, walimlazimisha mambo kadhaa (kwa sasa tusiyataje) wakaenda naye asikokujua, wakampiga sana kwa ngumi, mateke na magongo na wakati mwengine wakitumia Bunduki zao. Wakiwa wanampiga pia walikuwa wakisema kuwa amewatesa/wasumbua sana na kuwa anajifanya mjanja mbele ya (Srk) na hivyo wanamalizana naye; akapoteza fahamu...

      Wakamtupa eneo la mapori huko Tegeta hadi alipookotwa na wananchi asubuhi na kukabidhiwa mikononi mwa Wanaharakati waliompeleka Hospitali Muhimbili.

      Wakati akipokelewa MOI tayari baadhi ya wanaharakati walishafika eneo lile, kumbe kati ya walimpokea alikuwamo kijana anayesadikiwa kuwa ni "Askari". Huyu aligundulika baada ya mda mfupi akiwa amejificha chooni akiwasiliana kwa simu na watu aliokuwa akiwaambia " Hajafa. Bado anahema.... na maneno mengine yaliyoashiria kuwa waliofanya 'kazi' ile hawakukamilisha 'maagizo'. Vijana wakamfundisha adabu kwa hasira na kumkuta akiwa na Redio Call, ambayo baada ya muda mfupi Polisi FFU walifika na gari na vifaa vya vurugu wakiisaka ile Radio.

      Nashindwa kuendelea....."
      NB: Haya ni maelezo ya mwanaharakati Albanie Marcossy wa LHRC
      Quote By Mupirocin
      Katika taarifa ya habari mtu aliyekuwa akimtafuta mfululizo kwa siku tatu ni mtu wa Ikulu aitwaye kwa jina moja David na baadaye aliondoka kumfuata huyu David na baadaye akatekwa infront of him. Kwa mwenye akili anajua tu hii ni plan from somewhere
      Quote By Azimio Jipya
      Mbona hili wala sio siri tena ... Jamaa alimpigia simu wakamalize maongezi LEADERS CLUB!!! Ulimboka akaondoka na Rafiki yake mmoja! Wakati wanongea na huyo Jamaa hakueelwana ...

      Jamaa akapiga simu kwa hao wanjeshi walikuja kumburuza na kumchukua ... wakamuacha Rafiki wa ulimboka na huyo jamaa mwingine kwa kusema hatuwahitaji nyie tunamuhitaji Dr Ulimboka ....!

      Rafiki wa Ulimboka ... Akapiga simu kwa waaharakati wa Haki za Binadamu ..Hellen Kijo Bisimba at al .. na usiku huo wakaanza kumtafuta na kuripoti vituoa mbalimbali vya Polisi ...lakini Kila kituo wakidai ... hamjui huyo mtu .... labda waje asubuni .... na subuhi? Wapata habari toka kituo cha polisi tegata .... kaokotwa mtu ....blabalahhhh!!

      Source. Hellen Kijo Bisimba!!
      Lyimo, BAK, Ibambasi and 63 others like this.

    2. #441
      Polisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2010
      Posts : 1,569
      Rep Power : 748
      Likes Received
      380
      Likes Given
      237

      Default Re: Pande mbili muhimu za kutizamwa kuhusu suala la kutekwa Dk Ulimboka

      Inawezekana kabisa maadui wa Dr. Uli wakajificha katika mgongo wa serikali ambaye pia ni adui wa madaktari wote. Lakini nikuulize swali moja, mkikosana na jirani yako na akakuambua kuwa 'leo utanitambua'. Jioni ukamwona katika kituo cha mafuta akinunua petroli wakati hana gari wala pikipiki na usiku huo nyumba yako ikaungua kwa moto. Neno liwalo na liwe likitumiwa na kiongozi mkubwa lina tafsiri nyingi mno ambazo zote zinakubalika na anaelewa kabisa uamuzi wowote utakaochukuliwa utakuwa na madhara aidha kwa serikali au kwa wananchi

    3. #442
      Remmy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th June 2009
      Location : home
      Posts : 4,388
      Rep Power : 7780
      Likes Received
      1560
      Likes Given
      1825

      Default Re: Pande mbili muhimu za kutizamwa kuhusu suala la kutekwa Dk Ulimboka

      Hatupo pamoja nawe kwa hili. Wala sikubaliani nawe.

    4. #443
      Expedito Mduda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd September 2009
      Posts : 269
      Rep Power : 548
      Likes Received
      32
      Likes Given
      33

      Default Re: Pande mbili muhimu za kutizamwa kuhusu suala la kutekwa Dk Ulimboka

      Ni sahihi. Nafikiri tusi-focus sehemu moja. Tupepese macho yetu kote kote. Bahati mbaya tu ni kuwa hatuna uhakika na uchunguzi utakaofanywa na hao watakaofanya
      Mtanzania1 likes this.

    5. #444
      Jumakidogo's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 16th July 2009
      Location : DOM & DAR
      Posts : 1,868
      Rep Power : 1180
      Likes Received
      390
      Likes Given
      42

      Default

      Quote By Remmy
      Hatupo pamoja nawe kwa hili. Wala sikubaliani nawe.
      Sawa! Lakini chochote kati ya haya chaweza kuwa. Sisimamii mguu moja kwa sababu ya chuki yangu dhidi ya serikali. Naweza kumpoteza muhusika halisi wa tukio kwa sababu ya ushabiki wa kisiasa.

    6. #445
      Jumakidogo's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 16th July 2009
      Location : DOM & DAR
      Posts : 1,868
      Rep Power : 1180
      Likes Received
      390
      Likes Given
      42

      Default

      Quote By Polisi
      Inawezekana kabisa maadui wa Dr. Uli wakajificha katika mgongo wa serikali ambaye pia ni adui wa madaktari wote. Lakini nikuulize swali moja, mkikosana na jirani yako na akakuambua kuwa 'leo utanitambua'. Jioni ukamwona katika kituo cha mafuta akinunua petroli wakati hana gari wala pikipiki na usiku huo nyumba yako ikaungua kwa moto. Neno liwalo na liwe likitumiwa na kiongozi mkubwa lina tafsiri nyingi mno ambazo zote zinakubalika na anaelewa kabisa uamuzi wowote utakaochukuliwa utakuwa na madhara aidha kwa serikali au kwa wananchi
      Maneno yako ni sawa mkuu. Ndiyo maana nikasema jambo litizamwe kwa pande zote mbili ili kuziba uwezekano wa mianya inayoweza kumfanya muhusika mkuu akasevu kisanga. Nautizama upande wa pili pia kwa sababu njama yenyewe na utekelezaje wake haijakaa ki serikali serikali, imefanywa ki huni huni hivi.
      Polisi likes this.

    7. #446
      Abraham's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 9th October 2008
      Posts : 110
      Rep Power : 567
      Likes Received
      6
      Likes Given
      45

      Default Re: Pande mbili muhimu za kutizamwa kuhusu suala la kutekwa Dk Ulimboka

      Quote By Uwezo Tunao
      Nonsense of the first order!!!!!!!!!!!!!!!!!
      Of course..ikumbukwe kuwa kama "polisi njaa" wangetumika then kusingekuwa na coordination na uongozi wa polisi...Mfano alipopolekwa kituo cha polisi bunju Dr Uli hakupewa msaada wowote na kituo ilhali wakijua alikuwa amedhurika vibaya - hii inamaanisha tayari walikuwa na mwongozo kutoka juu kuwa wasihangaike kumpeleka hospitali. Pili, ukiangalia uongozi wa juu wa polisi na wizara ya mambo ya ndani inatetea huku wakijichanganya - hii inamaanisha uhusika wao hauna mashaka hata kidogo. Tatu, Polisi aliyepewa kibano pale Moi alisikika akiongea na Radiocall kuwa " Ulimboka kafikishwa MOI lakini bado yuko hai.....ikimaanisha kuna mpango uliokuwepo ambao walidhani angekuwa keshafariki hadi kufikia muda huo. kwa hiyo ni kuwa alikuwa anauarifu utawala kuwa jamaa bado hajafa. Yaani inasikitisha ila at the same time inaonesha jinsi ambavyo serikali ya tz haina akili hata kidogo na hasa baada ya JK aka (raisi mdhaifu) alipojipeleka hospitali kama kawaida yake na yale maneno yake ya kukariri" Serikali inampa pole dokta na tunamtakia kupona haraka na naomba madaktari wawe na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu" alafu huyoooo anasafiri leo nje ya nchi asikilizie soo kwa njia ya simu. Shame shame shame on the weak presida mwiba kura
      "Don't argue with a fool , as people might not notice the difference!"

    8. #447
      hoyce's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th October 2010
      Posts : 492
      Rep Power : 537
      Likes Received
      107
      Likes Given
      1

      Default Re: Pande mbili muhimu za kutizamwa kuhusu suala la kutekwa Dk Ulimboka

      Tunajua kuwa huu ndo upotoshaji mlioupanga kupindisha unyama huu. Mtajilaumu sana kwa kuwatuma wachakachuaji wa mafunzo kutekeleza mpango huu

    9. #448
      Jumakidogo's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 16th July 2009
      Location : DOM & DAR
      Posts : 1,868
      Rep Power : 1180
      Likes Received
      390
      Likes Given
      42

      Default

      Quote By Abraham
      Of course..ikumbukwe kuwa kama "polisi njaa" wangetumika then kusingekuwa na coordination na uongozi wa polisi...Mfano alipopolekwa kituo cha polisi bunju Dr Uli hakupewa msaada wowote na kituo ilhali wakijua alikuwa amedhurika vibaya - hii inamaanisha tayari walikuwa na mwongozo kutoka juu kuwa wasihangaike kumpeleka hospitali. Pili, ukiangalia uongozi wa juu wa polisi na wizara ya mambo ya ndani inatetea huku wakijichanganya - hii inamaanisha uhusika wao hauna mashaka hata kidogo. Tatu, Polisi aliyepewa kibano pale Moi alisikika akiongea na Radiocall kuwa " Ulimboka kafikishwa MOI lakini bado yuko hai.....ikimaanisha kuna mpango uliokuwepo ambao walidhani angekuwa keshafariki hadi kufikia muda huo. kwa hiyo ni kuwa alikuwa anauarifu utawala kuwa jamaa bado hajafa. Yaani inasikitisha ila at the same time inaonesha jinsi ambavyo serikali ya tz haina akili hata kidogo na hasa baada ya JK aka (raisi mdhaifu) alipojipeleka hospitali kama kawaida yake na yale maneno yake ya kukariri" Serikali inampa pole dokta na tunamtakia kupona haraka na naomba madaktari wawe na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu" alafu huyoooo anasafiri leo nje ya nchi asikilizie soo kwa njia ya simu. Shame shame shame on the weak presida mwiba kura
      Siku zote polisi kuna uzembe na dharau fulani. Vituoni huwa hakuna hata karatasi. Hata babu yako angepelekwa pale polisi Bunju akiwa katika hali kama ya dk Ulimboka hakuna chochote cha maana ambacho kingefanyika. Naomba nishangae kidogo, hivi serikali haijui kuwa kuna mamia ya madaktari wagomaji na si Ulimboka pekee? Je, haijui kama kwa kumuua Ulimboka huyu angeweza kuibuka Ulimboka mwingine matata zaidi?
      KISUKALI likes this.

    10. #449
      MTENGETI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th January 2012
      Posts : 538
      Rep Power : 527
      Likes Received
      199
      Likes Given
      40

      Default Mpango dhaifu,mkakati dhaifu na utekelezaji wa kizembe!

      nimefuatalia na kusikiliza hili suala la Dr. Ulimboka kwa makini sana. Tunapoleekea Watanzania ni kubaya mno ukiangalia matatizo ya nchi kama madagasca, Tunisia, Libya na Hata Syria ni vitu kama hivi kuanza na mtu mmoja kama ilivyo kwa Dr. Ulimboka.

      Si ajabu kuanzia leo ukaiona jumuia ya Madaktari wakiingia mtaani kutaka kuiwajibisha serikali na watu wengine wakaungana nao. Mkakati waliofanya hawa jamaa waliomteka Ulimboka ni Dhaifu na wa kijinga sana.

      Ukanushaji uliotolewa na Serikali pia ni dhaifu na hatutufanyi tuamini kuwa serikali haiusiki na kadhia hii. Pia yule Mpolisi aliedundwa kule AAR ni sehemu ya kuonyesha udhaifu kwa jeshi letu la Polisi. kwa Hili naomba tuwaunge madaktari Mkono kwa hali na mali ili kukomesha udhaifu huu wa serikali badala ya kutatua matatizo ya msingi inaongeza moto kwenye matatizo yanayotusibu.

      Nilishuhudia live pale KCMC jana Madakatari wakiwatimua wenzao mawodini jana mara tu baada ya kupata taarifa za Dr Ulimboka kutekwa. Ukiangalia ule utesaji uliofanywa kwa Dr. Ulimboka unafanana kabisa na utesaji mwingine wanaofanyiwa majambazi,wanaobambikiwa kesi kulazimishwa kukiri na Polisi wetu wa vitengo maalumu. Huku kutoana kucha , kubanwa korodani ni kazi ya Tiss na Polisi.

      MPANGO DAHIFU HUO NAOMBA KUWASILISHA
      Mr. Teacher likes this.
      CCM. - CHAMA CHA MACHUMA ULETE

    11. #450
      Azipa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th March 2012
      Posts : 933
      Rep Power : 552
      Likes Received
      226
      Likes Given
      1

      Default Re: Pande mbili muhimu za kutizamwa kuhusu suala la kutekwa Dk Ulimboka

      Nijuavyo mimi katika hali ile regardless who it was Kituo cha Tegeta as a matter of procedure walitakiwa wampeleke hospitali. Cha kushangaza tunaona Mwanaharakati wa haki za binadamu ndo aliyekwenda kumpeleka hospitali

      Pia kuhusika kwa mtu toka ikulu

      Pia state propaganda machinery TV ya taifa haikucover hiyo story

      Pia kauli ya Pinda before and after the incident
      franksarry and Ulimakafu like this.

    12. #451
      Profesa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : Anywhere in Africa
      Posts : 556
      Rep Power : 763
      Likes Received
      237
      Likes Given
      365

      Default Swala la Ulimboka: Srikali kweli inahusika? Sidhani! Pinda na JK kuweni makini

      Kwa staili ya uongozi wa JK, yeye binafsi sidhani kama anahusika, kwa kuwa watendajhi wake hukosa busara mara nyingi sana na kwa kuwa hana tabia ya kumlinda mtu, au kumpa mtu maelekezo ya nini cha kufanya, mpaka ashindwe ndio anaingilia kati (rejea swala la katiba, rejea mgomo uliopita vongozi wa kada mbalimbali waliropokwa wee mwinsho wakaumbulia na maamuzi na msimamo tofauti) Kuna Maswali muhimu ya kujiuliza ambayo yanasaidia kutafakari:

      1. Je, haiwezekani ikawa ni chombo fulani cha dola au taasisi ya serikali (au kiongozi wake) kimeona kitengo chake kinadhalilishwa kwa kushindwa kuzuia vuguvugu hili na wanaona wajichukulie hatu wanazo ona wao ili kulinda kitengo na nafasi walizonazo? Hasa hasa ukizingatia watu wanavyopoteza kazi serikalini kwa kushindwa kusimamia maeneo yao ya kazi (yani hakuna garantee ya post uliyonayo). wako tayari hata kumshauri waziri mkuu vibaya kama walivyofanya kipindi kilichopita.

      2. je kutokana na kuongezeka kwa uadui wa kisiasa (wa ndani au/na nje ya CCM), haiwezekani ikawa madui wametake advantage ya situation ku-set more fire? Na kuhakikisha wanafanya kitu ambacho kitaimarisha mgomo na kuifanya serikali ionekane dhaifu na inatumia mbinu chafu? Na hivyo kupelekea watu wa rika la kati (midle class) ambao ndio chachu hasa ya mapinduzi, ingawa sasa hawashiriki kikamilifu katika siasa kwani wako busy na uzalishaji mali.

      3. Je watakuwa ni baadhi ya wale waliothiriwa kwa njia moja au nyingine na migomo hii?

      Je hawadhani JK angependa busara itumike zaidi kuliko nguvu na maneno ya kejeli? Au kutaka kuonyesha mabavu kwa watu ambao serikali hii ni yao na si yenu nyinyi mlioko madarakani ambao ni dhamana tu mmepewa na haohao wanaolalamika?
      Ndahani likes this.

    13. #452
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,651
      Rep Power : 4020
      Likes Received
      2942
      Likes Given
      5067

      Default Re: Swala la Ulimboka: Srikali kweli inahusika? Sidhani! Pinda na JK kuweni makini

      Quote By Profesa

      Kwa vyovyote vile ilivyo, aliyeshika dola ndio ana wajibu wa kulinda mali na maisha ya wananchi wake. Ikishindikana kufanya huvyo lawama anabeba nani?
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    14. #453
      Jumakidogo's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 16th July 2009
      Location : DOM & DAR
      Posts : 1,868
      Rep Power : 1180
      Likes Received
      390
      Likes Given
      42

      Default

      Quote By hoyce
      Tunajua kuwa huu ndo upotoshaji mlioupanga kupindisha unyama huu. Mtajilaumu sana kwa kuwatuma wachakachuaji wa mafunzo kutekeleza mpango huu
      Ni matumaini yangu kuwa unajua kusoma vizuri. Upotoshaji uko wapi hapo? Nimejaribu kuweka uwezekano wa yote mawili kuwa moja wapo huenda likawa sahihi. Ndugu yangu, itikadi na imani ya kisiasa ikizidi katika akili ya mtu anakuwa mjinga au mpumbavu. Na mjinga siku zote huamini kila neno.
      Profesa likes this.

    15. #454
      Anselm's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2010
      Location : Dar-es-salaam
      Posts : 1,476
      Rep Power : 731
      Likes Received
      183
      Likes Given
      138

      Default Re: Pande mbili muhimu za kutizamwa kuhusu suala la kutekwa Dk Ulimboka

      Quote By Jumakidogo
      Awali ya yote yatupasa kumpa pole na kumuombea apone haraka dakatari wetu huyu bwana Ulimboka na walaaniwe kwa nguvu zote wale wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine.

      Wengi wetu kwa asilimia kubwa tumekuwa na imani kuwa, utekelezaji wa jambo hilo ni njama au mkakati wa serikali kupunguza kasi ya harakati za madaktari katika kudai haki zao.

      Tunapoihusisha moja kwa moja serikali kwa upande mmoja wa mbele, hebu tugeuke nyuma na kuangalia upande wa pili.

      Bila shaka Dk Ulimboka alikuwa na maadui wa hatari wenye chuki binafsi naye hasa kipindi cha vugu vugu hili la migomo ya madaktari. Kuna watu waliopoteza madaraka yao matamu kutokana na kadhia hii, upo uwezekano wa kupanga njama za kulipiza kisasi.

      Kutumika polisi si kitu mbele ya pesa. Ukiwa na fungu la kutosha ukitaka kuwatumia polisi njaa kwa ajili ya uhalifu unawatumia bila shida. Ikiwa wapo ambao hufanya ujambazi na kupora mali za watu, itakuwa hawa wa kukodiwa! Tugawanye fikra na mitazamo yetu, wakati tunaitupia jicho la mashaka serikali.

      Tuangalie na upande wa pili, wale waliomwaga unga kutokana na harakati hizi tunawachukuliaje? Hapa mhalifu halisi anaweza kujificha chini ya kivuli cha serikali.

      Mwisho napenda niwapongeza madaktari wote waliotoa kichapo kwa mtu anayedhaniwa kuwa alikuwa mmoja wa wateka nyara.

      Mungu msaidie Dk Ulimboka apone haraka ili aendelee na harakati zake.
      Habari nzima ni point kasoro hapo kwenye red,kuhukumu kwa kudhania siyo sahihi kwahiyo hukupaswa kuwapongeza...ni maoni yangu tu.

    16. #455
      Profesa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : Anywhere in Africa
      Posts : 556
      Rep Power : 763
      Likes Received
      237
      Likes Given
      365

      Default Re: Swala la Ulimboka: Srikali kweli inahusika? Sidhani! Pinda na JK kuweni makini

      Quote By Ndahani
      Kwa vyovyote vile ilivyo, aliyeshika dola ndio ana wajibu wa kulinda mali na maisha ya wananchi wake. Ikishindikana kufanya huvyo lawama anabeba nani?
      Ndahani, hawsaaaa, ila kwa mchezo ninaouona, kunauwezekano watu wakaingia kwenye mtego sijui ni akina nani hasa watakaonasa, JK na Pinda wakienda vibaya imekula kwao, lazima swala la Uwajibikaji litawakumba... Sina uhakika kama Mh Pinda alivyoongea jana kwanye Bunge, kama tayari alikuwa ameshapata inteligence briefing ya kutosha ikihusisha swala la Ulimboka?? Na kama alikuwa anajua, ile kauli ni mafuta kwenye moto. Nawasihi wtumie na waonyeshe busara na hekima ya hali ya juu ndiyo silaha pekeee yakutatua matatizo yaliyopo sasa, haijalishi chanzo

    17. #456
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,651
      Rep Power : 4020
      Likes Received
      2942
      Likes Given
      5067

      Default Re: Swala la Ulimboka: Srikali kweli inahusika? Sidhani! Pinda na JK kuweni makini

      Quote By Profesa
      Hawsaaaa, ila kwa mchezo ninaouona, kunauwezekano watu wakaingia kwenye mtego sijui ni akina nani hasa watakaonasa, JK na Pinda wakienda vibaya imekula kwao, lazima swala la Uwajibikaji litawakumba... Sina uhakika kama Mh Pinda alivyoongea jana kwanye Bunge, kama tayari alikuwa ameshapata inteligence briefing ya kutosha ikihusisha swala la Ulimboka?? Na kama alikuwa anajua, ile kauli ni mafuta kwenye moto. Nawasihi wtumie na waonyeshe busara na hekima ya hali ya juu ndiyo silaha pekeee yakutatua matatizo yaliyopo sasa, haijalishi chanzo
      Kwa mtazamo huo basi, washukiwa wa kwanza unafikiri ni kina nani? Kinachoniumiza ni kushindwa kwa serikali kumaliza matatizo ya madaktari kwa diplomasia.Badala yake kufanya kitendo kama hicho baada ya kutishiana nani ndiye mshukiwa mkuu?
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    18. #457
      Jumakidogo's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 16th July 2009
      Location : DOM & DAR
      Posts : 1,868
      Rep Power : 1180
      Likes Received
      390
      Likes Given
      42

      Default

      Quote By Azipa
      Nijuavyo mimi katika hali ile regardless who it was Kituo cha Tegeta as a matter of procedure walitakiwa wampeleke hospitali. Cha kushangaza tunaona Mwanaharakati wa haki za binadamu ndo aliyekwenda kumpeleka hospitali

      Pia kuhusika kwa mtu toka ikulu

      Pia state propaganda machinery TV ya taifa haikucover hiyo story

      Pia kauli ya Pinda before and after the incident
      Naomba kujifunza kupitia kwako. Inamaana unaamini kwa % 100 kuwa serikali imeshindwa kumkamata dk Ulimboka na kumpeleka katika vyombo husika ikaamua kumuua? Je serikali inaamini kuwa njia pekee ya kukomesha mgomo ni kumuua dk Ulimboka wakati ikijua kuna mamia ya madaktari nyuma yake? Tujiulize kwa pande zote mkuu.

    19. #458
      Matola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2010
      Posts : 12,856
      Rep Power : 19823
      Likes Received
      5643
      Likes Given
      3875

      Default Re: Swala la Ulimboka: Srikali kweli inahusika? Sidhani! Pinda na JK kuweni makini

      Ukiona hakuna tamko lolote la CCM wala Bakwata kulaani unyama huu, wala huwezi kuangaika kujuwa kwamba hii ni "Inside Job".
      Division four point 29 = Masters Mzumbe University. Nape Nnauye is my role model.

    20. #459
      kichomiz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 4,122
      Rep Power : 1250
      Likes Received
      669
      Likes Given
      80

      Default

      Quote By Madela Wa- Madilu
      Kabla hatujaja huku Ughaibuni tulisha fanya kazi ndani ya serikali na mashirika yake.
      Hatujazaliwa jana we know very well how CCM government operates.

      Ili uwe mtendaji bora wa serikali ya CCM ni lazima uwe Schizophrenia, hawa ni watu ambao brain yao haina sense ya emotion. Hawa ni watu ambao wanaweza kula hata ndani ya choo cha City kwa sababu halufu ya mavi haiwasumbui.
      Hawa ni watu wanao weza kuua mtu kwa kumwonea wivu kavaa shati jipya.
      Hawa ni watu tangu enzi za form one ni kulilia umonita darasani na ukiranja ili kila siku wafaidi kuona mtu akilamba viboko kwa unaa wao.
      Hawa ni watu ambao mkifanya biashara ya ubia na kupata faida millioni moja utakuwa na bahati sana akikupa 100,000 katika millioni.
      Serikali dharimu siku zote hupenda kuajiri watu kama hawa katika kazi ambazo huhitaji aina fulani ya unyama.

      Uchunguzi hapa Marekani umeonyesha Scizophrenic wengi wanafanya kazi Wall Street na wengi ni Ma CEO wa makapuni yanayopata faida kwa kufanya kila unyama hapa duniani.

      Kifupi ni kwamba serikali ya CCM inaongozwa na wagonjwa wa akili.
      Ukiwasikia kwenye mazungumzo yao ya faragha utashangaa. Hawana ubinadamu hata unyama hawana wana Uibilisi tu.

      Unajua hata Fisi hawezi kupanga njama ya kumla Fisi mwenza lakini ukiwa ndani ya serikali ya CCM mazungumzo ya kuua watu wanaowavurugia mlo wao haramu ni ya kawaida tu.
      Ndiyo maana watumishi wengi wa serikali ya CCM wakisha staafu hali yao huanza kuwa duni ndani ya masaa 24 tu ni wagonjwa wa akili bila kufanya unyama maisha yao hayaendi.

      Hili changa la macho la kujifanya eti kuna watu wenye hasira ni upuuzi wenye utepetevu wa akili na nia mahususi ya kulinda maovu ya serikali ya CCM. Ushawishi huu duni hauna uhusiano na kitu mna ita Looking Ouside the Box. Msemo umetumiwa kimaharamia na si mahali pake.

      Dozi ya ujinga ambayo Ideology ya CCM imewabugiza watanzania ilikuwa kubwa sana, Mungu bariki mwananchi mmoja mmoja anaamka na kutambua uovu wa serikali hii dharimu. Uongo wa karne ya 20 hauwezi fua dafu karne ya 21. Uongo mahali pake ni kwenye mikutani ya NEC kwa akina Mamvi Richmonduli.
      Mkuu umeongea ukweli mtupu,
      kuna vibaraka wanajaribu kupotosha watu kwa kuitetea serikali uaji ya wanyonge,
      sasa kila mtu anaenda anaelewa kwamba serikali yetu ni adui yetu.
      Madela Wa- Madilu likes this.

    21. #460
      jembe mwanaharakati's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st June 2012
      Posts : 27
      Rep Power : 357
      Likes Received
      6
      Likes Given
      2

      Default Re: Mpango dhaifu,mkakati dhaifu na utekelezaji wa kizembe!

      Hoja imepita ndugu mbunge

    Page 23 of 40 FirstFirst ... 13212223242533 ... LastLast

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...