Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Raia wanaposhinikizwa kupisha maendeleo....

    Report Post
    Page 3 of 3 FirstFirst 123
    Results 41 to 43 of 43
    1. #1
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,892
      Rep Power : 12961
      Likes Received
      4572
      Likes Given
      7577

      Default Raia wanaposhinikizwa kupisha maendeleo.............

      Hii ni nchi ya ajabu sana ambayo kila kukicha inakuja na mikakati ya kufukarisha raia wake kwa visingizio vya wapishe maendeleo kama vile raia siyo sehemu ya hayo maendeleo..................... ........ Matokeo yake raia husukumwa nje ya maendeleo kwa maana ya huduma muhimu na kupunjwa fidia ya thamani khalisi ya mtaji aliouwekeza kwenye shughuli zake kama vile nyumba, shamba na maendeleo mengineyo..................... ... La ajabu kabisa huyo mwekezaji anayepishwa huwa halazimishwi na sera/sheria kuwafidia waathirika wake kwa hasara ya kunyimwa kivuno cha matarajio yajayo ya waathirika......athariza kimazingira, uchumi, afya n.k hujitokeza....zikiwemo hasara ya kukosa huduma muhimu ambazo sasa yabidi wazifuate mbali na gharama nyinginezo ambazo sasa zinakuwa zimebinafsishwa kwa huyu mwekezaji....................n a kuwa faida ambayo mwekezaji hata anakuwa hajaipanda..... kwa hiyo huvuna asichopanda wala kustahili.....na mwaathirika huwa amesahaulika kabisa!!!!!!!!!!!!!!!! Ushauri Tunahitaji sera ambazo zitamtambua raia mwathirika kama sehemu ya huo uwekezaji mpya ili aendelee kuvuna na kumpunguzia makali ya kupisha maendeleo......kumtambua apewe hisa naye awe sehemu ya umiliki wa huo uwekezaji na kwahiyo hajapisha maendeleo bali naye amekuwa sehemu ya maendeleo kama kweli yapo! Tusipofanya hivyo kwa kuwapa hisa watu wetu kwenye mitaji ya maendeleo tajwa...ina maana baada ya miaka kama 20 hivi ijayo sehemu kubwa ya raia wetu watakuwa wakimbizi wa kiuchumi ndani ya nchi yao................ Kwa minajili ipi tuaafiki na khali hiyo?
      Last edited by Rutashubanyuma; 26th June 2012 at 10:00.
      Sikonge, Haika, BantuGirl and 11 others like this.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    2. #41
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,892
      Rep Power : 12961
      Likes Received
      4572
      Likes Given
      7577

      Default Re: Raia wanaposhinikizwa kupisha maendeleo....

      nadhani hakuna anaependa kufanyiwa dhulma ,ila tatizo misingi ya kujitetea au kutetea haki zako ,coz vyombo vya sheria vya kutetea sheria za wananchi vyote viko pamoja na serikali na rushwa mbele ,ndio maana watu wanakuwa hawajui nn wafanye ,,kama kuta kuwa na mfumo kama ule wa waengereza kueka citizen advice bureau,, sehemu ya kutetea wananchi na haki zao,maybe ita saidia ,ila isiwe chini ya serikali iwe taasisi binafsi ,ambayo itakuwa na wanasharia walio kuwa wanajali haki za binaadamu
      wahida inabidi tuendelee kujifunza namna ya kuzitambua haki zetu na jinsi ya kuzidai na kuzitetea badala ya kuviamini vya siasa...
      wahida likes this.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    3. #42
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,892
      Rep Power : 12961
      Likes Received
      4572
      Likes Given
      7577

      Default Re: Raia wanaposhinikizwa kupisha maendeleo....

      Hoja zako zimeshikamana vizuri kweli kweli.
      Kama viongozi wanaochaguliwa direct na wananchi ndio wangekuwa wanasimamia maamuzi ya namna hii sidhani kama haya yangekuwa yanatokea, viongozi wanaofanya maamuzi ya kizembe namna hii ni administrative ambao ni wateule wa ama viongozi tuliowachagua sisi wenyewe au wateule wa wateule wa wateule wa wateule wa viongozi tuowachagua wenyewe kwenye mabox ya kura.

      napendekeza kwamba, kwenye mchakato wa uaandaji wa katiba mpya tuhakikishe kwamba ama viongozi wanaoteuliwa na viongozi waliochaguliwa kwa sanduku la kura wasiwe na mamlaka ya kuteua viongozi, na pia tuongeze idadi ya viongozi wa kuchaguliwa kwa sanduku la kura au tuamue maamzi fulani fulani yafanyike baada ya kupigiwa kura badala ya kupigia kura viongozi pekee.
      Sangarara kwa kuanza serikali za mitaa ziongozwe na mameya wa kuchaguliwa.........ma madiwani wawe waajiriw awa tumishi waote wa halmashauri zao badala ya Ikulu kupitia waziri wa serikali za mitaa au Pm kuwanyang'anya majukumu yao ya kudhibiti matumizi na nidhamu ya sehemu walizochaguliwa
      Sangarara likes this.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    4. #43
      Mziba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th February 2010
      Posts : 228
      Rep Power : 521
      Likes Received
      34
      Likes Given
      73

      Default Re: Raia wanaposhinikizwa kupisha maendeleo.............

      Quote By Rutashubanyuma View Post
      Hii ni nchi ya ajabu sana ambayo kila kukicha inakuja na mikakati ya kufukarisha raia wake kwa visingizio vya wapishe maendeleo kama vile raia siyo sehemu ya hayo maendeleo..................... ........ Matokeo yake raia husukumwa nje ya maendeleo kwa maana ya huduma muhimu na kupunjwa fidia ya thamani khalisi ya mtaji aliouwekeza kwenye shughuli zake kama vile nyumba, shamba na maendeleo mengineyo..................... ... La ajabu kabisa huyo mwekezaji anayepishwa huwa halazimishwi na sera/sheria kuwafidia waathirika wake kwa hasara ya kunyimwa kivuno cha matarajio yajayo ya waathirika......athariza kimazingira, uchumi, afya n.k hujitokeza....zikiwemo hasara ya kukosa huduma muhimu ambazo sasa yabidi wazifuate mbali na gharama nyinginezo ambazo sasa zinakuwa zimebinafsishwa kwa huyu mwekezaji....................n a kuwa faida ambayo mwekezaji hata anakuwa hajaipanda..... kwa hiyo huvuna asichopanda wala kustahili.....na mwaathirika huwa amesahaulika kabisa!!!!!!!!!!!!!!!! Ushauri Tunahitaji sera ambazo zitamtambua raia mwathirika kama sehemu ya huo uwekezaji mpya ili aendelee kuvuna na kumpunguzia makali ya kupisha maendeleo......kumtambua apewe hisa naye awe sehemu ya umiliki wa huo uwekezaji na kwahiyo hajapisha maendeleo bali naye amekuwa sehemu ya maendeleo kama kweli yapo! Tusipofanya hivyo kwa kuwapa hisa watu wetu kwenye mitaji ya maendeleo tajwa...ina maana baada ya miaka kama 20 hivi ijayo sehemu kubwa ya raia wetu watakuwa wakimbizi wa kiuchumi ndani ya nchi yao................ Kwa minajili ipi tuaafiki na khali hiyo?
      Hii ni Laana: Mkuu Ruta, kwanza asante kuandika hii posti. Mungu akuzidishie na akubariki. Umejitolea kuandika haya mambo kwa niaba ya wanyonge, na wote waliodhulumiwa au wanaodhulumiwa mali na haki zao. Kumbuka kua watu hawa walijitolea muhanga na kumwaga damu kwa kupigania nchi mwaka 1978 na pia katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa. Leo, wanafikwa na msiba huu. Kweli hujafa hujaumbika. Nani aliejua jua wakati wa Draft (Lazima kuingia Jeshi kwenda mtukula), iko siku nchi hii itawahamisha kwa dhulma? Vipi kama walipoteza watoto zao katika kupigania nchi? Huu mtindo wa kuhamisha watu kihivi ni Laana. Huu ni wakati wa kuwa Patriotic. Na walio hamishwa na wanaohamishwa wote wapewe haki zao. Huu sio ubinaadam.

      Mkuu, wazo la kua na sera za kumtambua raia muathirika ni muafaka sana. Ingekua vema zikatia maanani kua kuna dhulma za aina mbili inapokuja kwenye matumizi ya mali asili. 1. Kuitumia hovyo bila kujali watoto (Taifa la kesho) kwa mfano, mazingira, uchumi wa baadae ambao unatumika sasa hivi, etc . 2. Na Pili ni dhulma ya kutowapa malipo sawa wenye mali yao (wanainchi). kwa mfano mali asili zinauzwa bila utaratibu maalum ambao mfanyakazi wa serikali anaelewana na Muwakilishi wa kampuni wanakutana na kuelewana bei. Hii husababisha hata wawakilishi wa serikali kupunjwa saana tu. (kwa sababu hawajui mali inathamani gani).

    Page 3 of 3 FirstFirst 123

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...