Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

    Report Post
    Page 3 of 6 FirstFirst 12345 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 104
    1. #1
      Felixonfellix's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th February 2010
      Posts : 1,673
      Rep Power : 804
      Likes Received
      165
      Likes Given
      95

      Default Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Waheshimiwa Wananchi wenzangu,

      Amani iwe kwenu,

      Kwa kipindi cha wiki nzima kumekuwepo na mjadala mkali bungeni, kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na katika taifa kwa ujumla juu ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/13 sanjari na yaliyojiri kutokana na kauli niliyotoa bungeni juu ya udhaifu wa Rais katika usimamizi wa maandalizi na utekelezaji wa bajeti pamoja na mipango muhimu ya maendeleo. Ukweli ni uhuru!.

      Aidha, kupitishwa kwa Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka wa Fedha 2012/2013 na Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2012/2013 bila marekebisho yoyote ya msingi pamoja na michango mingi ya wabunge ya kukosoa kumedhihirisha kile nilicho tahadharisha tangu awali kwamba; kwa kuwa udhaifu wa kikatiba umetoa nguvu kubwa kwa Rais juu ya bajeti na uendeshaji wa nchi, udhaifu wa Rais una athiri maisha ya wananchi. Ukweli ni Uhuru!.

      Katika mazingira haya, udhaifu wa rais na uzembe wa bunge unapandikiza migogoro kati ya wananchi na serikali kutokana ufisadi na masuala ya maendeleo kutopewa kipaumbele cha kutosha zaidi ya matumizi ya kawaida lakini pia inachochea pia migomo baridi ya watumishi wa umma hususun madaktari, walimu na askari kutokana pia na madai yao ya muda mrefu kutokuzingatiwa kwenye bajeti. Ukweli ni Uhuru!.

      Kadhalika udhaifu wa kanuni za Kudumu za Bunge umefanya wabunge kuwekewa mipaka kwa mujibu wa kanuni 97 (2) ya kuchangia mjadala kuhusu hotuba ya bajeti kwa kuchangia tu mambo ya ujumla yanayohusiana na hali ya uchumi wa nchi na kwamba mbunge yoyote haruhusiwi kupendekeza mabadiliko katika makadirio ya mapato na matumizi ya serikali. Ukweli ni Uhuru!.

      Pia, katiba imempa mamlaka makubwa Rais juu ya Bunge kwa kuwa Bunge likikataa bajeti ya serikali kwa mujibu wa Ibara ya 90 (2) (b) moja kwa moja Rais analivunja bunge suala ambalo huwapa hofu wabunge wengi hususani wa chama kinachotawala na kuwafanya wapige kura ya NDIO hata kama waliikosoa bajeti husika. Hivyo, udhaifu wa bunge unachangiwa na ukweli kwamba katiba imeweka nguvu kubwa kwa Rais katika kuvunja bunge linapokataa bajeti wakati huo huo kanuni zimekataza wabunge kupendekeza mabadiliko katika bajeti; kwa hivyo wabunge hawana uwezo wa kubadilisha na wakati huo huo wakikataa bunge linavunjwa, katika mazingira haya udhaifu wa Rais wa kushindwa kutumia nguvu hizo za kikatiba una madhara makubwa sana kwa nchi na maisha ya wananchi. Ukweli ni Uhuru!.

      Kwa mantiki hiyo, katika mchakato wa katiba mpya ni muhimu kwa wananchi kutoa maoni ya kuwezesha ukuu na uhuru wa bunge katika kuisimamia serikali kwenye mchakato wa bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi. Wakati katiba mpya ikisubiriwa, ni muhimu kwa marekebisho ya haraka kufanyika katika kanuni za kudumu za bunge hususani sehemu ya tisa inayohusu utaratibu wa kutunga sheria kuhusu mambo ya fedha kuanzia kanuni ya 94 mpaka kanuni ya 107 ili kuongeza nguvu za bunge katika kuishauri na kuisimamia serikali kwa mujibu wa madaraka ya bunge ya ibara ya 63 (2) na (3) ya katiba ya sasa. Katika muktadha huo, nimeanza kufanya uchambuzi ili kuwasilisha bungeni mapendekezo ya mabadiliko ya kanuni. Ukweli ni Uhuru!.

      Hata hivyo, hata kwa kanuni zilizopo sasa udhaifu wa bunge unaongezeka kutokana na maamuzi ya kizembe mathalani ya kutozingatia matakwa ya kanuni za bunge, mfano Kanuni ya 94 inalitaka bunge ili kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika ibara ya 63 (3) (c) ya Katiba kwa kukaa kama kamati ya mipango katika mkutano wake wa mwezi Februari ili kujadili na kushauri kuhusu mapendezo ya mpango wa taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali kwa mwaka wa fedha unaofuata, kanuni ambayo toka niingie bungeni haijawahi kutekelezwa kwa wakati hata mara moja pamoja na kuwakumbusha wanaohusika kusimamia kanuni. Ukweli ni Uhuru!.

      Mwaka huu udhaifu umekuwa mkubwa zaidi kwa Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/2013 sanjari na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2012/2013 tarehe 18 Juni 2012 na kupitishwa siku moja tarehe 22 Juni 2012 hali ambayo imechangia katika kufanya bajeti ya nchi isizingatie kwa ukamilfu mpango wa taifa wa miaka mitano. Ukweli ni Uhuru!.

      Nashukuru kwamba Spika wa Bunge Anna Makinda amekiri bungeni tarehe 20 Juni 2012 kwamba kulikuwa na udhaifu wa miaka mingi wa kutozingatia kanuni ya 106 ambayo inalitaka bunge kujadili muswada wa sheria ya fedha mwishoni baada ya bunge kukamilisha kazi ya kupitisha muswada wa fedha za matumizi ili kuiwezesha serikali kuongeza vyanzo vya mapato kama wabunge tulivyopendekeza mwaka 2011 na pendekezo hilo kurudiwa tena na kamati ya fedha na uchumi tarehe 18 Juni 2012. Ukweli ni Uhuru!.

      Izingatiwe kuwa iwapo sheria ya fedha ingepitishwa tarehe 22 Juni 2012 kama ilivyokuwa imepangwa awali athari zake zingekuwa kubwa kwa kuwa udhaifu wa kikatiba umetoa nguvu kubwa kwa Rais juu ya utaratibu wa kutunga sheria kuhusu mambo ya fedha kwa mujibu wa ibara ya 99 (1) kwa kuweka masharti kwamba bunge halitashughulikia sehemu kubwa ya masuala ya fedha isipokuwa kama Rais amependekeza kwamba jambo hilo lishughulikiwe na bunge na pendekezo hilo la Rais liwe limewasilishwa kwenye bunge na waziri. Hivyo, michango na mapendekezo ya wabunge bila Rais mwenyewe kupendekeza isingeliwezesha bunge kufanya mabadiliko ya kupanua wigo wa mapato kwa kuwa kwa kuwa mujibu wa ibara 99 (2) (a) (i) udhaifu wa bunge ni pamoja na kukatazwa kutoza kodi au kuongeza kodi. Ukweli ni Uhuru!.

      Hivyo, Kamati ya Fedha na Uchumi itumie vizuri mwanya wa ibara ya 99 (3) kurejea maoni yake, ya kambi rasmi ya upinzani bungeni na michango ya wabunge ya mkutano wanne wa Bunge mwaka 2011 na Mkutano wa nane wa Bunge mwaka 2012 na kufanya marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha kwa kumshauri Waziri. Ukweli ni Uhuru!.

      Aidha, ili kuondoa udhaifu uliopo Rais Kikwete mwenyewe asome kumbukumbu rasmi za bunge (Hansard) za tarehe 18 Juni mpaka 22 Juni 2012 na kuliongoza baraza la mawaziri kumwezesha Waziri wa Fedha ya 86 (10) kuwasilisha muswada wa sheria uliochapishwa upya ukiwa na marekebisho au mabadiliko yanayopaswa kufanyika yenye kulenga kupunguza kodi katika bidhaa zenye kuchangia mfumuko wa bei na kupanua wigo wa mapato kwa kuongeza kodi kwenye vyanzo mbadala tulivyovieleza bungeni. Ukweli ni Uhuru!.

      Izingatiwe kuwa nilipotolewa bungeni tarehe 19 Juni 2012 nilieleza kwa ufupi nilichosema bungeni na nilichotarajia kusema na kuahidi kwamba nitatoa tamko kamili baadaye; baada ya kujipa muda wa kutafakari nimefikia uamuzi wa kutoa tamko husika wakati bunge litakapoelekea kujadili utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012 na makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2012/2013; ambapo pamoja na masuala mengine nitaeleza hatua ambazo Rais anapaswa kuchukua kuwezesha ahadi alizotoa kwa watanzania kuweza kutekelezwa na serikali. Ukweli ni Uhuru!.

      Kwa sasa niwashukuru wananchi wa Ubungo, wakazi wa mkoa wa Dar es salaam na watanzania kwa ujumla walionielewa na kuniunga mkono kupitia maoni yao kwenye mitandao ya kijamii, simu za mkononi na katika vyombo vya habari. Nawashukuru pia viongozi wa dini, chama na asasi mbalimbali nje na ndani ya serikali walionipa moyo wa kuendelea kusimamia ukweli na kuacha unafiki ili kusimamia uwajibikaji wa viongozi kwa maendeleo ya taifa. Ukweli ni Uhuru!.

      Nashukuru pia kwa mchango wa walinipinga na kunikosoa kutokana na kauli niliyotoa juu ya udhaifu wa Rais Kikwete, wapo walioeleza kuwa ilitokana na jazba na wengine wameeleza kuwa ningetumia lugha ya diplomasia kufikisha ujumbe ili kutodhalilisha taasisi ya urais na kwa kuzingatia utamaduni wetu wa heshima kwa wakubwa na wapo wachache waliosema kwamba ni matusi kutamka ‘udhaifu wa Rais’. Ukweli ni Uhuru!.

      Wakati mjadala huu ukiendelea ni rai yangu kwamba rejea ifanyike katika mchango wangu wa tarehe 5 Julai 2011 wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Rais kwa mwaka 2011/2012 na rejea kamili pia ifanyike kwenye mchango wangu wa tarehe 19 Juni 201; na ieleweke kwamba naheshimu taasisi ya urais na umri, naamini katika matumizi ya lugha ya kidiplomasia, hata hivyo nilitafakari na kuamua kuusema ukweli kwa lugha ya moja kwa moja ili ujumbe ufike kwa mamlaka zote zinazohusika na wauchukulie kwa uzito tofauti ilivyokuwa mwaka mmoja uliopita. Ukweli ni uhuru!.

      Niliamini, naamini na nitaendelea kuamini kwamba kutamka neno ‘udhaifu wa Rais’ sio kumtukana Rais na wala sio kulitumia jina la Rais kwa dhihaka; hata hivyo kwa kuwa pamekuwepo na mwelekeo wa propaganda za kudai kuwa kauli hiyo ni matusi na kwa kuwa chanzo cha propaganda hizo ni udhaifu uliofanywa na Naibu Spika Job Ndugai bungeni wa kunihukumu kwa kutumia kanuni tofauti na tuhuma iliyotolewa; nakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi wake ili kuwe na mjadala mpana wa kibunge utakaowezesha kumbukumbu sahihi kuwekwa. Ukweli ni uhuru!.

      Katiba ya Nchi ambayo niliapishwa kuilinda pamoja na ubovu wake inatamka katika Ibara ya 63 (2) kwamba “Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba”. Toka nichaguliwe kuwa mbunge mwaka 2010 kwa nyakati na maeneo mbalimbali viongozi wa vyama, dini, asasi za kiraia, vyombo vya habari na wananchi wa kawaida wakilalamika kuhusu udhaifu wa Rais na kutaka atumie nguvu na mamlaka yake ya kikatiba kuiongoza kwa uthabiti serikali kushughulikia masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yanayolikabili taifa; niliamua kuendelea kusema bungeni kwa mara nyingine ikiwa ni sehemu ya kutimiza wajibu wa kibunge wa kuwakilisha wananchi na kuisimamia serikali. Ukweli ni Uhuru!.

      Tarehe 19 Juni 2012 nilieleza bungeni kabla ya kutolewa sababu za kuikataa bajeti na tarehe 22 Juni 2012 nilipiga kura ya hapana ya kuikataa bajeti kwa kutokuweka misingi thabiti ya kutimiza ahadi ya Rais Kikwete na CCM ya maisha bora kwa kila mtanzania na badala yake kuongeza ugumu wa maisha kutokana na kushindwa kukabiliana na matatizo ya mfumuko wa bei. Aidha, kiwango cha fedha kwa ajili ya miradi ya barabara na maji kwa upande wa jiji la Dar es salaam ikiwemo jimbo la Ubungo ni kidogo tofauti na kile kilichotajwa na Rais Kikwete na kuingizwa kwenye jedwali la Mpango wa Taifa wa miaka mitano kwa upande wa miradi ya maendeleo iliyopaswa kutengewa fedha katika bajeti ya 2012/2013. Ukweli ni Uhuru!.

      Pamoja na utetezi uliotolewa na Serikali juu ya mgongano kati ya tafsiri kati ya kiingereza na Kiswahili, ukweli utaendelea kubaki kuwa tuliamua kuikataa bajeti kwa kuwa ilishindwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao uliwasilishwa na Rais Kikwete na ukapitishwa kwa azimio la bunge ambao ulipaswa kuiongoza serikali kuweka mkazo katika kuendeleza nchi kwa kutumia fedha za ndani kwa kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwenye miradi ya maendeleo kama zilivyokokotolewa katika mpango husika. Ukweli ni Uhuru!.

      Naamini Rais Kikwete anayofursa ya kurekebisha udhaifu huo kwa kuongeza nguvu zake katika muswada wa sheria ya fedha kupanua wigo wa mapato na hatimaye kumwezesha Waziri wa Fedha kuwasilisha bungeni kwa mujibu wa kanuni ya 107 mapendekezo ya matumizi ya nyongeza ya fedha za serikali yenye kulenga kuongeza kiwango cha fedha za maendeleo. Kwa upande wa Jimbo la Ubungo na Jiji la Dar es salaam, serikali kwenye bajeti ya nyongeza inayopaswa kuwasilishwa iongeze fedha za miradi ya Maji kwa upande wa Ruvu Juu ikiwemo kutenga fedha za kutosha za ujenzi wa Bwawa la Kidunda, kwa upande wa Barabara iongeze fedha za ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara za pembezoni za mchujo na za mzunguko za kupunguza msongamano wa magari, na fidia ya ardhi kwa wananchi wa Kata ya Kwembe wanaopaswa kuhama kupisha ujenzi wa Chuo Kikuu Muhimbili (MUHAS) Eneo la Mloganzila. Ukweli ni Uhuru!.

      Kwa Wasemaji wa CCM waliodai kwamba nimetoa lugha ya matusi dhidi ya Rais na mwenyekiti wa chama chao wasome Kitabu cha Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania cha mmoja wa waasisi wa TANU na CCM Mwalimu Julius Nyerere ambapo wakati huo taifa likiwa katika mtanziko alimueleza Rais wa wakati huo kuwa ni ‘kiongozi dhaifu’ katika ukurasa wa 50 na kuendelea kusema katika Ukurasa wa 51 na namnukuu “Kwa sababu ya minong’ono-nong’ono ya watu wasiiona mbali kuhusu Rais, na kubabaishwa anakobabaishwa na washauri wake wakuu, nililazimika kuiambia wazi wazi Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kwamba najiona kuwa ninao wajibu wa kumsaidia Rais amalize kipindi chake salama” . Ukweli ni Uhuru!

      Naamini Mwalimu Nyerere hakumtukana Rais Mwinyi, kwa hiyo kunituhumu nimetukana ni kumtuhumu pia Marehemu Baba wa Taifa; narudia tena kusisitiza kuwa udhaifu uliojitokeza ni kutokana na Rais kutokutumia kwa uthabiti nguvu na mamlaka yake kwa mujibu wa katiba ibara za 33, 34, 35, 36, 37, 38 na 99 juu ya utendaji wa serikali na utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo. Ukweli ni Uhuru!.

      Nimalize kwa kunukuu kitabu kingine cha Mwalimu Nyerere cha miaka ya mwanzoni mwa 1960 cha TUJISAHIHISHE, “ Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua kuwa hana makosa. Na msingi wa woga ni ubinafsi. Pengine huwa tunaogopa sisi wenyewe kulaumiwa au kupata hasara fulani. Pengine twaweza kuwa hatuna cheo chochote ambacho tunaogopa kupoteza; pengine huwa hatuna wala tamaa yoyote ya kupata cheo fulani. Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi wote tunayo tamaa hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza ukamfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni ubinafsi mbaya sana.", mwisho wa kunukuu: Ukweli ni uhuru.

      Wenu katika utumishi wa umma,

      John Mnyika
      22 Juni 2012
      Bungeni-Dodoma
      JokaKuu, 911, Kiresua and 14 others like this.
      Tushirikiane Tutafika Tuendako

    2. Miaka 50

    3. #41
      Maasai_'s Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th June 2012
      Posts : 17
      Rep Power : 351
      Likes Received
      2
      Likes Given
      6

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      nimeamini Mbunge mmoja wa Chadema skills zake ni sawa na wabunge 10 wa CCM
      Tumaini Makene likes this.

    4. #42
      Kasimba G's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 852
      Rep Power : 592
      Likes Received
      252
      Likes Given
      265

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      John, copernicus alisimamia ukweli dunia nzima ilipotoka! Simamia haki daima, usitishwe mwisho wa siku utakuwa mshindi!

    5. #43
      sanjo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th October 2010
      Posts : 861
      Rep Power : 606
      Likes Received
      219
      Likes Given
      33

      Default

      Quote By admiral elect
      safi mnyika huo ndio msimamo wangu pia kuwa sisi watanzania tumekuwa waoga na hivyo wanafiki na ndo maana tumefika hapa kwa kisingizio cha mfumo wetu ni mbaya na dhaifu wakati sisi wenye mfumo hatukubali kuwa ndio wabaya na wadhaifu nambari wani. mimi binafsi najilaumu na kwa kutofanya jambo la kubadilisha hali hii maana itakuwa aibu kwa watoto na wajukuu zetu.mimi nachukia unafiki sana.wakati nikisoma sekondari(O- level) mama yetu alifariki na baba akaoa mwanamke mwingine baada ya muda wa chini ya mwaka 1,nilimwambia wazi bila kumumunya maneno kuwa amefanya haraka sana na zaidi mwanamke aliyemuoa haikuwa chaguo sahihi nikagombezwa sana na ikafikia hatua ya kuitwa kwenye kikao cha wanafamilia nakutakiwa kuomba radhi kwa kuingilia mambo ya mzazi wangu,lakini nikasimamia ukweli kwa gharama ya kunyimwa ada,baadaya miaka mitatu my father admitted that i was dame right!UNAFIKI NA UOGA NDIO CHANZO CHA MATATIZO YETU WATANZANIA! mnyika hongera na kandamizia hapo hapo no matter what !
      Woga ni tabia ya watu waliokata tamaa na wachoyo. Tujenge tabia ya kusema hapana kwenye kitu ambacho tunaamini ni cha kweli. Mnyika umefanya jambo la maana kusimamia ukweli.
      Tumaini Makene likes this.

    6. #44
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2884
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Zama za WARAKA NA MATAMKO,,,,,,
      HAYA
      UKWELI NI UHURU

    7. #45
      Mlengo wa Kati's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th February 2011
      Posts : 1,297
      Rep Power : 0
      Likes Received
      188
      Likes Given
      11

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      duh nimepitia waraka wote hakuna hata kero za jimbo la ubungo hakuna kwenye waraka mrefu wa ngojera ya ukweli uhuru! ngonjera ngonjera ngonjera! wana ubungo mme-vulugwa mchana kweupe!

    8. FemaTV & Radio

    9. #46
      mgashi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 226
      Rep Power : 404
      Likes Received
      61
      Likes Given
      3

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Ukweli ni uhuru safi sana kamanda na huo ndo ukweli wenyewe tofauti na hivyo ni uongo na ndo magamba wanachopenda kusikia.

    10. #47
      Mlengo wa Kati's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th February 2011
      Posts : 1,297
      Rep Power : 0
      Likes Received
      188
      Likes Given
      11

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      ubungo imekula kwenu! ngonjera hizi hadi lini!

    11. #48
      wahabisaidi's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 14th December 2011
      Posts : 2
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      1

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Tiririkaaaaa kiongozi

    12. #49
      Leonard Robert's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2011
      Posts : 4,247
      Rep Power : 1262
      Likes Received
      522
      Likes Given
      175

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Asanteh sana kaka yangu Mnyika,sisi wadogo zako tuko nyuma yako..
      Kikwete ni Dhaifu..
      Tumaini Makene likes this.

    13. #50
      MpendaTz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th May 2009
      Posts : 1,073
      Rep Power : 724
      Likes Received
      146
      Likes Given
      537

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Quote By zomba
      Mnyika nilikwambia humuwezi Kikwete, shauri lako, wewe endelea tu.
      Mkuu ningependa sana kufahamu nini haswa unalowaza, nini unalotaka tulifahamu hapa? Je unavyotoa ni vitisho kwamba wewe ndiye mtekelezaji wa majibu au visasi, ni mtetezi au unajaribu kututhibitshia kuwa Raisi si dhaifu na kwamba anaonewa ? Hebu jaribu kutupatia mwelkeo wa mawazo yako kwa undani zaidi. Wakati mwingine inakaa kama unamfahamu sana Kikwete uwezo wake wa kutenda. Ingekuwa uzalendo mwema kuyajadili mambo kwa uwazi zaidi kama kweli unalipenda Taifa lako.
      Ila nikuhakikishie tu kuwa wengi humu tunamuelewa Mh. Mnyika kama "a True Patriot of this Nation".
      Please come out clean!
      Tumaini Makene likes this.

    14. #51
      majebere's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 2,206
      Rep Power : 0
      Likes Received
      322
      Likes Given
      111

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Endeleeni kupindisha maneno lakini ukwel uko pale pale, mbunge wenu anajitetea na mnakaa kumsifia.

    15. #52
      The Invincible's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2006
      Location : Online
      Posts : 1,945
      Rep Power : 1057
      Likes Received
      169
      Likes Given
      0

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Quote By Mlengo wa Kati
      ubungo imekula kwenu! ngonjera hizi hadi lini!
      Mimi ni mwana Ubungo.

      Big up Mnyika. Ukweli utakuweka huru......Ukweli ni uhuru.
      JokaKuu and Tumaini Makene like this.
      Watanzania mbumbumbu wamemchagua raisi dhaifu ajenge taifa la watu wasiojiamini, 2010/2015 - Tafakari

    16. #53
      MpendaTz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th May 2009
      Posts : 1,073
      Rep Power : 724
      Likes Received
      146
      Likes Given
      537

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Waraka kama huu huwezi kukurupuka tu na kuanza kujibu hovyo hovyo kama vile umesimama kwenye kamba iliyoning'inizwa hewani. Utaangukia kichogo!
      Tumaini Makene likes this.

    17. #54
      Gwalihenzi's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 2,379
      Rep Power : 0
      Likes Received
      615
      Likes Given
      377

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Quote By zomba
      Mnyika nilikwambia humuwezi Kikwete, shauri lako, wewe endelea tu.
      Nidhamu ya unafiki na uoga tu. Unaogopa kumwambia mtawala ukweli kwa kuwa tu mnasali pamoja!
      Tumaini Makene likes this.

    18. #55
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14620
      Likes Received
      2841
      Likes Given
      1961

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Quote By Gwalihenzi
      Nidhamu ya unafiki na uoga tu. Unaogopa kumwambia mtawala ukweli kwa kuwa tu mnasali pamoja!
      Kuna ukweli upi mnaujuwa nyinyi? ukweli "0", kwi kwi kwi teh teh teh, si makosa yenu, mnadanganyana toka Sunday school.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    19. #56
      thereitis's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Location : Arusha
      Posts : 237
      Rep Power : 480
      Likes Received
      24
      Likes Given
      60

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Quote By Mlengo wa Kati
      ubungo imekula kwenu! ngonjera hizi hadi lini!
      Wewe unaona ngonjera kwa sababu ukweli huo unakuumiza. Mlengo wa kati unapaswa kutambua kuwa licha ya kuwajibiga kwa wapiga kura wake, mbunge huwajibika pia kwa taifa lake. Mnyika ni miongoni mwa wabunge wachache wanaojua majukumu yao ipasavyo. Bahati mbaya yupo chini ya uongozi dhaifu wa muhimili mwingine wa dola aka sirikali. Ukweli ni uhuru
      "Our party CCM, eventually became complacent, bureaucratic and corrupt. We had to change" Nyerere

    20. #57
      Gwalihenzi's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 2,379
      Rep Power : 0
      Likes Received
      615
      Likes Given
      377

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Quote By zomba
      Kuna ukweli upi mnaujuwa nyinyi? ukweli "0", kwi kwi kwi teh teh teh, si makosa yenu, mnadanganyana toka Sunday school.
      Utacheka sana, mwisho utagundua kuwa kinachokuchesha ni kukosa ujasiri wa kukubali kuwa unaye mtetea ni raisi dhaifu kupita kiasi.

    21. #58
      Ruppy karenston's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2011
      Posts : 396
      Rep Power : 482
      Likes Received
      69
      Likes Given
      26

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Ukweli ni uhuru,na msema kweli ni kipenzi cha Mungu.Bravo Mnyika,jeykei ni dhaifu sana

    22. #59
      Gagurito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2011
      Location : Gangilonga....
      Posts : 5,263
      Rep Power : 1455
      Likes Received
      693
      Likes Given
      696

      Default Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Mkuu umenena vyema...
      The God who gave us life, gave us liberty at the same time.

    23. #60
      evoddy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2011
      Posts : 250
      Rep Power : 430
      Likes Received
      45
      Likes Given
      8

      Post Re: Waraka no. 1 wa mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”- Mnyika

      Kutetea haki ni gharama hasa pale ukweri unaposemwa kuhusu udhaifu wa wakubwa,
      pambana kijana tupo nyuma yako
      "Tanzania freedom does not stop at political independence we have to cross borders to see what is next"

    Page 3 of 6 FirstFirst 12345 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...