Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

    Report Post
    Page 5 of 6 FirstFirst ... 3456 LastLast
    Results 81 to 100 of 112
    1. #1
      OSOKONI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2011
      Posts : 3,632
      Rep Power : 1109
      Likes Received
      999
      Likes Given
      756

      Default Taarifa za Dar, Morogoro, Mwanza, Dodoma kuhusu mgomo wa Madaktari,

      WAKATI kukiwa na mgawanyiko mkubwa kwa madaktari nchini katika kushiriki mgomo ulioitishwa na Chama cha Madaktari nchini (MAT), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Said Meck Sadik amepiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote katika hospitali za Jiji, yenye lengo la kuchochea watumishi wa afya kugoma.

      Akizungumza Dar es Salaam jana, Sadik alisisitiza kuwa Serikali itachukua hatua kali za kisheria kwa watu watakaobainika kushiriki katika kuwashawishi watumishi wa sekta ya afya wakiwemo madaktari na wauguzi kugoma.

      Sadik anaungana na viongozi wengine wa kitaifa na Mahakama Kuu ya Tanzania, kutoa amri ya kusitishwa kwa mgomo huo wa madaktari ambao ulianza jana katika baadhi ya hospitali huku huduma katika hospitali nyingine zikiendelea vizuri kutokana na madaktari na wauguzi katika hospitali hizo kutogoma.

      “Kufuatia tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Kazi, Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.”

      Ilisema taarifa ya Mahakama Kuu kwa vyombo vya habari. Amri hiyo ya Mahakama ilitolewa kufuatia maombi namba 73 ya mwaka 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania.

      Gazeti hili lilipofika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jana asubuhi lilishuhudia madaktari wakiendelea na kazi kitendo kilichoonesha kuwa hawakushiriki katika mgomo.

      Wakati hayo yakiendelea, Serikali imeendelea kuwataka madaktari wote nchini kuendelea na kazi wakati suala la kupatiwa suluhisho likiwa katika chombo cha kisheria Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi.

      Pia imesema itakuwa tayari kutekeleza maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Kazi, kuhusu mapendekezo yatakayotolewa juu ya suala zima la maslahi na haki za madaktari kama maombi yao yalivyowasilishwa.

      Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Selaman Rashid, aliyasema hayo mjini Morogoro jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kuona iwapo madaktari wameamua kutekeleza mgomo wao au la.

      Akiwa hospitalini hapo, Naibu Waziri huyo alishuhudia madaktari kwa kushirikiana na wauguzi wakiendelea kufanya kazi mbalimbali za kuhudumia wagonjwa licha ya Chama cha Madaktari kutoa tamko la kuwataka wagome nchi nzima kuanzia jana.

      Uongozi wa Hospitali ya Rufaa hiyo ukiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa , Dk. Godfrey Mtey , ulimtembeza Naibu Waziri maeneo mbalimbali ikiwemo wodini, maabara na chumba cha kujifungulia na kuzungumza na baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakipatiwa tiba.

      “Nawaomba madaktari wote waendelee na kazi ya kuwahudumia wagonjwa wakati suala lao lipo kwenye chombo cha kisheria ...sote tumekubaliana usuluhishi wa mgogoro huu uamuliwe na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi. Hata hivyo alisema, Serikali imejipanga kuhakikisha inaboresha maslahi ya wafanyakazi wote si kwa ajili ya madaktari pekee ili wapate mishahara kulingana na kazi wanazozifanya.

      Alisema, Serikali inapozungumzia mishahara haizungumzii kwa daktari pekee bali inazungumzia sekta mbalimbali na si kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pekee bali na wizara nyingine za Serikali.

      Aliupongeza Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro kwa watumishi wake wakiwemo madaktari kuendelea na kazi za utoaji wa huduma kwa wagonjwa. Kutoka Dodoma taarifa zinasema kuwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dk Ezekiel Mpuya alisema jana kuwa hali ni shwari katika hospitali hiyo na hakuna mgomo.

      Akizungumza na gazeti hili, Dkt. Mpuya alisema madaktari na wauguzi walikuwa wanaendelea na kazi zao kama kawaida na hakukuwa na mgomo wowote.

      “Hali ni shwari na wale wote wenye zamu wako kazini isipokuwa daktari mmoja aliyeko kwenye mafunzo leo hajaripoti sijui ana tatizo gani, lakini hapa hakuna mgomo,” alisema.

      Hata hivyo hali haikuwa shwari jijini Mwanza kwani madaktari zaidi ya 200 waliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando walianza mgomo rasmi jana baada ya Serikali kushindwa kutoa majibu ya kuridhisha kuhusu madai yao mbalimbali.

      Katika mahojiano na gazeti hili Mwakilishi wa Kamati ya kufuatilia madai ya Madaktari hao waliyapeleka serikalini, Dk Richard Kirita alisema kwamba madaktari wa kada zote katika hospitali hiyo wapo kwenye mgomo isipokuwa baadhi ya madaktari bingwa pamoja na wakuu wa idara.

      Mapema wiki hii, Kamati ndogo ya Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyokuwa ikifuatilia mgogoro dhidi yao na Serikali ilisema haijaridhishwa na majibu yaliyotolewa na Serikali juu ya madai yao na kuonesha nia ya kufanya mgomo wa nchi nzima kuanzia jana.

      “Ni kweli tumeanza mgomo rasmi, madaktari waliokuwa zamu leo (jana) hawajaenda kazini, hata hivyo kwa kuwa leo si siku ya kazi unaweza kudhani hakuna mgomo, lakini njoo Jumatatu ndio utapata picha halisi ya mgomo kwa sababu wagonjwa watakuwa wengi lakini hakutakuwa na huduma,” alisema Dkt. Kirita.

      Hata hivyo alisema kwamba wanaendelea na vikao ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na wenzao wa Dar es Salaam ili kujua ni hatua zipi zaidi wachukue kuhusiana na mgomo wao huo.

      Dkt. Kirita alisema kwamba katika kikao cha madaktari wa Bugando kilichofanyika hivi karibuni kujadili majibu ya Serikali juu ya madai yao na kuhusisha jumla ya madaktari 202 walikubaliana kwa pamoja kuanza mgomo kuanzia jana iwapo madai yao hayatatekelezwa na Serikali.

      Katika mgomo wa kwanza wa madaktari uliofanyika mapema mwaka huu madaktari walikuwa na madai mbalimbali yakiwemo ya kuboreshwa kwa huduma za afya zikiwemo dawa, vitanda na vifaa tiba, mishahara na nyumba za madaktari.

      Baadhi ya watu waliokuwa wamepeleka wagonjwa katika hospitali hiyo jana walionekana wakiwaondoa baada ya kukosa huduma kutoka kwa madaktari ambao baadhi walikuwa kwenye kikao na wengine walionekana katika vikundi vikundi wakipiga soga.

      Kwa upande wao wagonjwa katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Bugando wameiomba Serikali pamoja na madaktari walio kwenye mgomo kumaliza tofauti zao ili madaktari waweze kurejea kazini na kuwapatia huduma.

      Wakizungumza jana katika wodi namba 6 na 8, Yohana Matinde, Abel Joseph, Martha Maduhu na Pendo Saimon walisema kuwa tangu kutangazwa kwa mgomo huo jana, hawajaweza kuonana na madaktari zaidi ya kuhudumiwa na wauguzi kwa kugawiwa vidonge na sindano.

      “Tunawaomba Serikali na madaktari wamalize tofauti zao, maana endapo hali hii ya mgomo ikiendelea tunaoumia ni sisi, na pia ni vyema Serikali ingesikia madai ya madaktari ili waweze kurejea kazini,” alisema Joseph.

      Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa kwa Jiji la Mwanza mgomo huo ulikuwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, tofauti na katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure ambapo madaktari na baadhi ya wauguzi walikuwa wanaendelea na kazi kama kawaida.
      Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

    2. Miaka 50

    3. #81
      Jackbauer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : CTU
      Posts : 4,873
      Rep Power : 1690
      Likes Received
      1348
      Likes Given
      277

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      nasubiri kuona ''usikivu'' wa serikali katika huu mgomo.

    4. #82
      Ninaweza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2010
      Location : bukonda moyo
      Posts : 2,159
      Rep Power : 868
      Likes Received
      315
      Likes Given
      719

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      Jk na selikali yake wanaamini kuwa kwenda mahakamani vitanda vinaongezeka mahospitalini, ct scn inatengemaa, ward zinapanuka, nk, nk,.......

    5. #83
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,181
      Rep Power : 19209
      Likes Received
      8137
      Likes Given
      26606

      Default Mgomo wa madaktari waanza rasmi


      Mgonjwa akihamishwa kutoka Wodi ya Kibasila katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), iliyopo Dar es Salaam jana, ili kupelekwa katika hospitali nyinyine kutokana na tishio la kuwepo kwa mgomo wa madaktari, katika hospitali hiyo na nyingine za serikali sehemu mbali mbali nchini wanaodai stahiki zao mbali mbali, kwa madai ya serikali kushindwa kuzitekeleza. Picha na Emmanuel Herman

      HUDUMA ZA KAWAIDA ZAZOROTA

      Waandishi Wetu, Dar na Mikoani

      MADAKTARI
      nchini wameanza mgomo katika baadhi ya hospitali nchini baada ya Serikali kushindwa kutekeleza madai yao waliyowasilisha katika Kamati ya Majadiliano iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

      Mgomo huo umetangazwa na Jumuiya ya Madaktari nchini huku ikifafanua kwamba kati ya madai kumi waliyotaka yatekelezwe na Serikali, hakuna hata moja lililofanyiwa kazi. Hata hivyo, jana madaktari hao ambao walikaa vikao vya majadiliano na Serikali kwa siku 90 baada ya kusitisha mgomo wao wa pili, wamesema katika madai yao kumi, hakuna hata moja lililotekelezwa na Serikali.

      Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk Stephen Ulimboka jana aliwaeleza waandishi wa habari kwamba ili warejee kazini, Serikali inatakiwa kutekeleza madai yao yote na kusisitiza kwamba dai lao la kwanza ni kuitaka Serikali kuboresha huduma za msingi kwa wagonjwa.


      “Mgomo umeanza leo na hauna kikomo, lengo ni kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yetu, hata zile huduma za dharura nazo kuanzia kesho (leo) zinaweza kusitishwa,” alisema Dk Ulimboka. Wakati Ulimboka akieleza hayo, huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa (Moi) ilikuwa ikitolewa kwa kusuasua huku baadhi ya wafanyakazi wakisisitiza kuwa mgomo huo upo.

      Licha ya wafanyakazi hao kukiri kuwa siku za mwisho wa wiki idadi ya wagonjwa katika hospitali hizo huwa ndogo, lakini walisisitiza kuwapo kwa mgomo huo na kufafanua kuwa kwa mtu mgeni katika eneo hilo si rahisi kutambua hali hiyo. Mwananchi Jumapili lilifika katika hospitali hiyo na kukuta huduma zikitolewa ‘kiaina’ huku baadhi ya wagonjwa wakieleza kwamba zimezorota, sio kama siku zilizopita.

      Tamko la Jumuiya Akieleza kwa kina sababu za mgomo huo, Dk Ulimboka alisema katika madai waliyoyawasilisha, hakuna hata moja lililotekelezwa na kufafanua kwamba Serikali imeongeza dai ambalo wao hawakuliwasilisha. Madai hayo ni pamoja na kupandishwa kwa ongezeko la mishahara, posho ya kuitwa kazini, posho za kufanya kazi katika mazingira magumu, bima ya afya, nyumba za kuishi, kukopeshwa magari kwa ajili ya usafiri, kuboreshwa kwa mazingira ya kufanyia kazi kwa kupeleka vifaa vya kazi, dawa na kuboresha miundombinu.


      “Serikali imesema imerekebisha viwango vinavyotumika kulipa posho ya uchunguzi wa maiti kwa Sh 100,000 kwa uchunguzi wa madaktari na Sh50,000 kwa watumishi wengine, lakini hili halikuwa dai letu!” alisema Dk Ulimboka.

      Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi aliwatahadharisha madaktari hao kuacha mgomo, akieleza kuwa ni batili na ni kinyume cha viapo vyao vya kazi. Dk Mwinyi aliainisha mambo 10 ambayo madaktari walikuwa wamepanga kutekelezewa na kusema kuwa kwa sehemu, yametekelezwa na baadhi ya mambo yaliyobakia wanaweza kuyazungumza.

      Mwanza

      Madaktari zaidi ya 200 waliopo katika Hosptali ya Rufaa ya Bugando jana walianza mgomo rasmi baada ya Serikali kushindwa kutoa majibu ya kuridhisha kuhusu madai yao mbalimbali yaliyosababisha madaktari hao kugoma mapema mwaka huu. Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Mwakilishi wa Kamati ndogo ya kufuatilia madai madaktari hao, Dk Richard Kirita alisema kwamba madaktari wa kada zote katika hospitali hiyo wapo kwenye mgomo isipokuwa baadhi ya madaktari bingwa pamoja na wakuu wa idara.

      “Kwa kuwa leo sio siku ya kazi unaweza kudhani hakuna mgomo, lakini njoo Jumatatu (kesho) ndo utapata picha halisi ya mgomo kwa sababu wagonjwa watakuwa wengi, lakini hakutakuwa na huduma,”alisema
      Moshi

      Hali ya utendaji wa madaktari mkoani Kilimanjaro imeonekana ya kusuasua huku baadhi ya madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC wakisema hawaingii kazini na wengine wakisema bado wanasikilizia.

      Katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi, madaktari waliokuwa zamu walisema kwa leo huwezi kujua aliyeko kwenye mgomo na ambaye hayupo, kwani wengi hawako kazini leo hadi kesho. B

      aadhi ya wagonjwa waliolazwa Hospitali ya KCMC katika wodi ya wanawake, walisema kuwa walitangaziwa kuwa kutakuwa na mgomo wa madaktari na kila mmoja aangalie cha kufanya na kuwa walifika wodini hapo asubuhi na hawakuzungumza na mgonjwa na kutoka.

      Wagonjwa hao wamesema Ijumaa jioni wagonjwa wengi waliruhusiwa kuondoka hata kama hali zao hazijatengemaa ambapo walisema wanahofia afya zao kama madaktari watatekeleza msimamo wao. Mbeya Katika Hospitali ya Rufaa Mbeya madaktari 10 kati ya 80 ndiyo waliokubali jana kuendelea na huduma ya kutibu wagonjwa ambapo wengine wameanza mgomo rasmi.

      Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Dk Eliuter Samky amethibitisha kuwapo na hali ya mgomo na kwamba ana uhakika wa madaktari 10 waliopo zamu kuendelea kazi.

      Awali Mwandishi wa gazeti hili alipofika katika hospitali hiyo hakukuta daktari yeyote na ofisi za utawala zikiwa zimefungwa huku katika eneo la mapokezi likiwa na wagonjwa ambao wamekaa wakisubiria kupata huduma. Katika kitengo cha wazazi Meta wanawake wanaokwenda kupata huduma wamesema wameingiwa na hofu kubwa kwa kukosa huduma hiyo baada ya kuona matangazo yanayosema hakuna mgojwa atakayepatiwa matibabu.

      Wakizungumza hospitalini hapo wanawake hao ambao hawakutaka kuandikwa majina yao, walisema kuwa mbali na kuona tangazo hilo lakini pia waliambiwa na baadhi ya madaktari kuwa ni bora wakaenda sehemu nyingine kwa ajili ya matibabu kwa kile kilichoelezwa kuwa kuwa na wao wapo katika mgomo huo hivyo hakuta kuwa na huduma yeyote kwa mgonjwa.

      Arusha
      Hali ya mgomo wa madaktari katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, haikuonekana jana asubuhi ingawa katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya madaktari na manesi hawakufika wodimi kuwaona wagonjwa kama wananvyofanya siku nyingine.

      Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo,Dk Mlay alipoulizwa na gazeti hili alisema hali hiyo isihusishwe na mgomo uliotangazwa na chama cha madaktari kwa kuwa kimetona na sababu kwamba leo na kesho ni siku za mapumziko .

      Baadhi ya wagonjwa na ndugu wanaowauguza walihojiwa na gazeti hili walionyeshwa kushangazwa na hali ya madaktari na manesi kushindwa kuwatembelea leo katika wodi zao kinyume na siku zote.

      Mganga Mkuu wa hospitali alisema kwamba hospitalini kwake hakuna mgomo wowote wa madaktari kwa kuwa wanafanya kazi kama kawaida na wala hawatambui suala la mgomo wa madaktari uliotangazwa na Chama cha Madaktari nchini(MAT).

      Tanga Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo
      pamoja hospitali nyingine za wilayani jana ziliendelea na huduma ya kutoa matibabu kwa wagonjwa kama kawaida. Katika Hospitali ya Bombo ambayo ni ya Mkoa wa Tanga, Mwandishi wa habari hizi jana alikuta madaktari pamoja na wauguzi waliokuwa zamu wakiendelea na kutoa matibabu kwa wagonjwa waliolazwa pamoja na wale wa kutoka nje.


      Wakizungumza na Mwananchi Jumapili madaktari wa Hospitali ya Bombo walisema wameshindwa kufanya mgomo kwa kuwa hawana taarifa za kuwataka kufanya hivyo bali wamekuwa wakisikia na kusoma kupitia vyombo vya habari.

      Haruna Juma ambaye ni mkazi wa Barabara ya 10 Jijini Tanga, aliwashukuru madaktari wa Hospitali ya Bombo kwa kutogoma kwa kuwa mdogo wake anayesumbuliwa na Apendex alipangiwa kufanyiwa upasuaji jana ambapo waganga walimfanyia kama kawaida.

      Waziri
      Serikali imesema kuwa itaendelea na msimamo wake ilioutoa bungeni mjini Dodoma wa kuwataka madaktari nchini kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wakati ambapo madai yao ya msingi yakiwa yanashughulikiwa.
      Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro jana baada ya kufanya ziara yake katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, alisema kuwa kimsingi yako mambo ambayo katika mazungumzo na madaktari hao walikubaliana lakini pia yako mambo ambayo hawakukubalina.

      Dk Rashid alisema kuwa mambo ambayo walikubalina na madaktari hao yanaendelea kushughulikiwa lakini mambo ambayo walishindwa kukubalina katika baraza la usuluhishi madaktari hao walikimbilia mahakamani ili kutafuta suluhu.

      “Na sisi tunasubiri maamuzi ya mahakama kwa hivyo kitendo cha wao kugoma kinakwenda kinyume na sheria kwa kuwa jambo hilo bado halijapatiwa ufumbuzi na mahakama,” alisisitiza.

      Katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro hakukuwa na dalili zozote za madaktari na wauguzi kugoma, huduma za matibabu kwa wagonjwa zilikuwa zikiendelea kama kawaida huku baadhi ya wauguzi na madaktari wa hospitali hiyo wakidai kutokuwa tayari kuingia katika mgomo huo.

      Amana, Temeke Katika hospitali ya Amana na Temeke za jijini Dar es Salaam wameendelea kutoa huduma kama kawaida, isipokuwa Hospitali ya Mwananyamala ambayo kulikuwa na madaktari na waguzi wachache. Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Meshack Shemwela aliiambia Mwananchi Jumapili jana kwamba huduma ya afya zinaendelea kutolewa kama kawaida na kwamba wanafanya tathmini ilikutambua kama kuna madaktari waliogoma.

      Akizungumzia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick alisema kuanzia jana saa 6 usiku walifanya uchunguzi na kubaini kwamba kuna watu waliokuwa wanapita katika kila hosptali kuhamasisha kufanyika lakini madaktari hawajagoma.

      Imeandaliwa na Rehema Matowo,Moshi, Venance George, Morogoro, Burhani Yakub,Tanga, Brandy Nelson, Godfrey Kahango,Mbeya, Moses Mashalla,Arusha,Sheilla Sezzy,Mwanza Aidan Mhando, Ibrahim Yamola, Geofrey Nyang'oro na Fidelis Butahe,Fidelis Butahe na Geofrey Nyang’oro

      Mgomo wa madaktari waanza rasmi
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    6. #84
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,181
      Rep Power : 19209
      Likes Received
      8137
      Likes Given
      26606

      Default Re: Mgomo wa madaktari waanza rasmi

      AU MUMEGOMA NILIANZISHE!!
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    7. #85
      Petram's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th June 2011
      Posts : 114
      Rep Power : 424
      Likes Received
      19
      Likes Given
      2

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      mwanaume msimamo

    8. FemaTV & Radio

    9. #86
      Allien's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2008
      Posts : 4,159
      Rep Power : 10780
      Likes Received
      1223
      Likes Given
      460

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      Inatakiwa busara ya hali ya juu sana kupita uwezo wa kawaida wa viongozi wa sasa na dhamira ya kweli na dhati kumaliza tatizo hili.

      Basically inafika wakati Madaktari wanakosa the best alternative ya kudai haki zao na mazingira bora ya kazi zaidi ya hii ya kugoma.

      Lakini pia, kutimiza madai ya Madaktari kunahitajika pesa za ziada ambazo, kama serikali iko very very serious na ina dhamira ya kweli hizo pesa zinaweza kupatikana simply kwa kukusanya kodi vizuri, kuziba mianya ya rushwa, kupunguza matumizi na kubuni vyanzo vingine vya fedha na mapato.

      Lakini pia, kutekeleza madai ya madaktari, ni kufungua njia ya sekta nyingine kama Elimu, nk kuanza kudai haki yao na hivyo kusababisha migomo zaidi.

      Ndiyo maana nasema inatakiwa busara ya hali ya juu sana. It is about total change and 100% commitment kumaliza mgomo huu wa Madaktari.

      Na kama kweli Madaktari wamedhamiria as they sound this time, the government will never have any alternative other than bowing down. Wasipo bow down na watu wakafa, what happened last time will happen this time massively: Wanaharakati will join mgomo, Wanafunzi; Raia, nk.

      Wasipokuwa makini, hii pia ni kete muhimu kwa opposition.

      Kama Madakatari wameamua kweli kujitoa muhanga, they just remind me of some of the readings: "Ili wengi wapone, moja lazima afe kwa ajili yao". Literally means, kwa madaktari kujitoa na raia kuathirika au kuwa wahanga ikiwepo vifo, it is only way Serikali ya Kidikteta itasikia na kubadilika (Utawala wa Kidikteta si lazima utumie mabavu, ila kutowapatia raia haki zao ni aina ya Udikteta).

      Siungi Mkono Mgomo maana najua wengi watakufa na kaathirika, lakini kama Serikali imeweka pamba masikioni, Goo . . Gooo Doctors on Strike.

      Rwanda inaheshimiwa sana Duniani sasa kwa better performance because of Genocide. Kama ina maana kupitia mgomo huu, tanzania will change for better, then let it me. It is a bitter pill to swallow, but we will finally get cured.

      Mungu Ibariki Tanzania!

    10. #87
      cedrickngowi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 9th June 2012
      Location : Arusha
      Posts : 119
      Rep Power : 373
      Likes Received
      18
      Likes Given
      23

      Default Mgomo wa madaktari.

      Mwaka wa fedha 2011-2012 serikali imetumia 7 bilion kugharamia matibabu nchi za nje,mainly India. Wakati hospitali zetu kubwa za rufaa yani Muhimbili,Bugando,Kcmc and the likes zote kwa ujumla wake zimepewa 5 bilions only.

      Do you see the difference here, watanzania tufike mahali tuaache kuongea sana, Tunahitaji kuchukua hatua zaidi kushinikiza serikali itatue mgogoro huu, kwani uwezo huu upo.Kama rais anatengewa 3 bilion kwa safari moja ya nje ambayo hatujui ina faida gani kwetu tunashindwaje ku-support our health sector?

    11. #88
      Kwetu Iringa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2011
      Posts : 339
      Rep Power : 466
      Likes Received
      54
      Likes Given
      595

      Default Maendeleo ya mgomo wa ma-dr

      Jamani vp hospitalini kunapatikana huduma za matibabu? Vyombo vya habari naona vimepigwa biti havisemi lolote kuhusu huu mgomo!!


      Je na JF imepigwa biti? Mbona sizioni habari za huu mgomo humu jamvini?

      Au ma-Dr wametii amri ya mahakama??

    12. #89
      Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2006
      Posts : 1,725
      Rep Power : 1022
      Likes Received
      54
      Likes Given
      6

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      Quote By ellyjr8
      UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI TANZANIA.
      MADAI
      1. Kuboresha Huduma za afya hospitalini kwa vifaa vya upimiaji, madawa.
      2. Kuboresha Mazingira Ya kazi (ukarabati wa majengo, uongezaji wa vitanda)
      3. Posho ya muda wa ziada wa kazi (call allowance) 5% kama ilivyo kisheria kwa kada yoyote.
      4. Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu 40% ( MEANING anayefanya kazi SAME, TANDAHIMBA, NYAMPULUKANO nk ni tofauti na akaaye MJINI)
      5. Posho ya makazi 40% au nyumba kama ilivyo kisheria(since DOCTOR IS ENTITLED KUPATA, HII NI KATIKA SHERIA YAO WENYEWE)
      6. Bima ya Afya(Green Card) kwa wafanyakazi wote wa sekta ya Afya.
      7. Kuwaondoa viongozi wa juu wa W/Afya kutokana na ubadhirifu.
      8. Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi 30% au Chanjo(Homa ya ini-hepatitis, HIV/AIDS, TB)...
      Jidanganye,Hakuna linaloshindikana ni kutokuwa na utashi wa viongozi kufanya maamuzi magumu!Wangethubutu wangeweza !
      UKIJUA UNAPOKWENDA NI RAHISI KUFIKA!

    13. #90
      LINCOLINMTZA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th March 2011
      Location : Opposite The JF Web Page
      Posts : 1,361
      Rep Power : 696
      Likes Received
      352
      Likes Given
      216

      Default Re: Taarifa za Dar, Morogoro, Mwanza, Dodoma kuhusu mgomo wa Madaktari,

      Quote By Honolulu
      Iwapo madaktari hawapewi haki zao basi serikali yetu dhaifu iturudishie kikombe cha babu!!

      Mkuu usisahau kuitupia kwenye jukwaa la utani. Kwani hii picha inachekesha kweli kwa jinsi hawa watu walivyokamatilia kikombe cha babu.Viongozi wetu hawa
      Love everybody, trust no body. If you can not convince them, confuse them. If you can not teach them, cheat them.

    14. #91
      Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2006
      Posts : 1,725
      Rep Power : 1022
      Likes Received
      54
      Likes Given
      6

      Default Re: madaktari waanza kufunguka!! sasa kuweka wazi hali halisi za mahospitali yetu

      Quote By mtotowamjini
      mh juzi juzi nilikua muhimbili kumuona mgonjwa aisee hali inatisha mno tatizo ni kwamba hata serikali wakitenga fedha za kuimarisha huduma ya afya hizo pesa zitaliwa hazitafanya chochote...
      Atleast, You have an Idea,Kwa kifupi hakuna madaktari wanaogoma kwasababu wanataka huduma zibwereshwe hapana wanagoma kwasababu ya ulafi wao.

      Ni kwanini madaktari hao hao wanawatoza wagonjwa pesa nje ya utaratibu,ni kwanini hawawajali wagonjwa wanapohitaji msaada sehemu zao za kazi, ni kwanini serikali ikipeleka vifaa wanaviharibu kwa maksudi ili wawaandikie wagonjwa wakafanye vipimo kwenye sehemu ambazo wanafaidika kwa kupata mgao kwa kila mgonjwa wanayempeleka,ni kwanini wanaiba vifaa kwenye hospitali za serikali na kuvipeleka mahospitali binafsi,I will go on and on............................ .,

      Kwa upande wa serikali wanayumba kuchukua maamuzi magumu kwasababu viongozi nao sio wa safi,wamejenga matabaka ya wanaolipwa zaidi ya mara elfu moja ya wengine chini ya kivuli cha uana siasa,Wanaotibiwa india na wanaotibiwa mwananyamala,Hili nalo ni limechangia sana.Ufisadi na wizi umekithiri kila sehemu.

      Fedha zinazotengwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo na shughuli za kijamii zinaishia kwenye makaratasi kwamba hili limefanyika na fedha imetumika kama ilivyokusudiwa.Watanzania wote tubadilike na tunalolisimamia na kuliamini liwe na ukweli ndani yake.

      Tuwajibike na tuogope kutumia fedha za umma kwa manufaa binafsi,waliopewa dhamana ya uongozi wasiwagawe watanzania kwa matabaka kwa kuona tabaka fulani linastahili kutibiwa India na jingine Temeke.

      Au wengine wanastahili kuipwa mara asilimia 1000 zaidi ya wengine,Malipo na marupupu yafuate vigezo kama elimu,uzoefu ,ugumu wa kazi husika na ufanisi kwa mtumishi husika.
      UKIJUA UNAPOKWENDA NI RAHISI KUFIKA!

    15. #92
      Mwanawalwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2012
      Posts : 324
      Rep Power : 416
      Likes Received
      88
      Likes Given
      53

      Default Re: Taarifa za Dar, Morogoro, Mwanza, Dodoma kuhusu mgomo wa Madaktari,

      mweeee

    16. #93
      masatujr1985's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th October 2011
      Location : Anumbeye
      Posts : 414
      Rep Power : 464
      Likes Received
      65
      Likes Given
      25

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      Ningekuwa na uwezo wa ziada (usioonekana) ningeondoa kizazi cha nyoka, mafisadi na makuwadi wa uchumi wa nchi yetu instantly. Nitahakikish one day nami ndugu yangu ama jamaa ama mwanangu anakuwa Daktari ili Kikwete na Mafisadi wenzie watakapougua baada ya kustaafu ama kizazi chake nao waonje machungu ya kuugulia hospitali zetu.
      We learn to be aggressive through learning from the aggressors.

    17. #94
      Communist's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st June 2012
      Location : Ubungo
      Posts : 2,726
      Rep Power : 2266
      Likes Received
      601
      Likes Given
      783

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      Wamegoma, hali ni mbaya, nsipande bodaboda, hamna huduma huko, ohoooooo
      Simple life is healthier than egoism.

    18. #95
      Godlisten Masawe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th July 2011
      Location : Hapa Hapa
      Posts : 607
      Rep Power : 518
      Likes Received
      220
      Likes Given
      2877

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      kamanda ellyjr8 kwani dr mnapokea mshahala kiasi gani? nataka ku compare with rwanda ambao wanapokea 1500USD
      [[MUFC]]

    19. #96
      Talklicious's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 50
      Rep Power : 370
      Likes Received
      6
      Likes Given
      12

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      Quote By Uda
      HATIMAYE madaktari nchini jana walianza mgomo usio na kikomo kwa lengo la kuishinikiza serikali kuwatimizia matihaji yao ikiwamo kuboresha mazingira ya kufanyia kazi pamoja na kuwapandishia mishahara.

      Uamuzi huo wa madaktari unapingana na amri ya Mahakama Kuu Tanzania, Kitengo cha Kazi ambayo juzi ilizuia mgomo huo baada ya kupokea maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).

      Mahakama hiyo ilitoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo shauri la pande zote mbili (Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

      Kwa mujibu wa taarifa ya Mahakama hiyo iliyotolewa juzi jioni na kusambazwa kwenye vyombo vya habari, imewataka MAT na wanachama wake kutoshiriki kwenye mgomo huo.

      Mgomo waanza

      Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es Salaam huduma za dharura zinatarajiwa kusitishwa wakati wowote kuanzia sasa.

      Mgomo huo unaanza wiki mbili baada ya madaktari hao kuitaka serikali itekeleze madai yao la sivyo jana wangeanza mgomo usio na kikomo.

      Tanzania Daima Jumapili, lilitembelea hospitali za Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Muhimbili na zile za mkoa ambazo ni Temeke, Amana na Mwananyamala na kushuhudia kusuasua kwa huduma.

      Vitengo vya dharura katika hospitali hizo viliendelea kupokea wagonjwa huku baadhi ya madaktari wakiweka wazi kuwa kuna uwezekano wa huduma hizo kusimama katika muda wa saa 24 kuanzia jana.

      Muhimbili

      Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wagonjwa walilamikia huduma zilizokuwa zikitolewa huku wengine wakisema wametelekezwa na wauguzi waliokuwa zamu.

      Eneo la mapokezi baadhi ya askari walionekana wakiwaeleza wagonjwa waliofika kuwa huduma zimesimama na kuwasihi waondoke eneo hilo.

      Mgonjwa mmoja ambaye alionekana kuchanganyikiwa alisikika akisema kuwa alimkabidhi nchi Rais Jakaya Kikwete lakini haieleweki kiongozi huyo anakoipeleka.

      “Rais Kikwete nilikukabidhi nchi hii sasa unaipeleka wapi?” alisikika akisema.

      John Kobelo, alisema kuwa tangu juzi kijana wake alitakiwa kufanyiwa upasuaji lakini ilipofika jana aliambiwa ampatie mgonjwa wake chakula kutokana na huduma hiyo kutokuwepo.

      “Kwa kweli hali inasikitisha na kukatisha tamaa, sijui nchi hii tunaelekea wapi maana viongozi wanaamua kwa makusudi kuchezea uhai wa Watanzania,” alisikika baba mmoja akilalamika.

      Tanzania Daima Jumapili ilifika katika wodi ya Sewa Haji na kukutana na mgonjwa ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake lakini alilalamikia kitendo cha madaktari kushindwa kupita zamu kwa siku ya jana huku huduma zikiwa zimezorota.

      Katika wodi ya Kibasila gazeti hili lilikutana na baadhi ya wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao walikuwa wakiangaika kumhamisha mgonjwa wao aliyekuwa akilalamika kwa maumivu makali.

      Gazeti hili halikuishia hapo kwani lililazimika kufika katika Kitengo cha Mifupa (Moi) ambapo ilikutana na Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Jumaa Almasi, ambaye alisema kuwa kwa jana ilikuwa ni vigumu kuzungumzia mgomo huo kutokana na kuwa siku ya mapumziko.

      “Unajua kwa (leo) yaani jana siwezi kuzungumzia mgomo kwa kuwa tuna kliniki mbili za binafsi, labda picha kamili ya kuwepo kwa mgomo tunaweza kuipata kuanzia Jumatatu, kwa vile kuna kliniki zote,” alisema.

      Aidha, Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha, alijikuta akishindwa kutokea katika kikao cha waandishi wa habari alichokiita ofisini kwake.

      Mwananyamala na Temeke

      Hali ilikuwa si shwari kwani baadhi ya wagonjwa walisikika wakisema kuwa hawajapata huduma na baadhi ya wauguzi wanajifanya kutoa huduma baada ya kuona wanahabari.

      Katika Hospitali ya Amana, Tanzania Daima Jumapili ilishuhudia shughuli za matibabu zikiwa zinaendelea ingawa baadhi ya wagonjwa walikuwa wakilalamika kukaa muda mrefu pasipo kupatiwa huduma.

      Mmoja wa watu waliokuwa hospitalini hapo aliyempeleka ndugu yake kupatiwa huduma baada ya kupata ajali aliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa wamekaa katika eneo hilo zaidi ya saa tatu bila mgonjwa wake kupatiwa matibabu.

      “Nipo hapa na huyu afande tumemleta mtu aliyepata ajali maeneo ya Sitakishari lakini hatujahudumiwa mpaka saa hizi sasa sijui ndiyo wanagoma kisirisiri?” alisema mtu huyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

      Katibu wa utawala wa hospitali hiyo, Tunu Mwachale, alisema madaktari waliotakiwa kufika zamu kwa siku ya jana wote walifika na kwamba walikuwa wakiendelea na kazi kama kawaida.

      Dk. Ulimboka anena

      Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, alisema hawajapata taarifa zozote kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, ya kuzuia mgomo huo.

      Alisema mgomo ulioanza jana haukihusishi Chama cha Madaktari nchini (MAT).

      Alisema wao taarifa hizo wamezisikia katika vyombo vya habari hivyo hawajui kama zinawahusu wao au MAT, na kwamba itakuwa ni vigumu kutolea ufafanuzi jambo lisilowahusu.

      Dk. Ulimboka alisema kuwa kimsingi serikali imekuwa ikipotosha dhana nzima ya mgomo huo kwani inaonyesha kuwa suala la posho ndilo linalogomewa na madaktari wakati si kweli.

      “Watu wanadhani tunapigania posho zaidi, hapana tunapigania huduma bora kwa wagonjwa, kwa sababu sifa ya kwanza katika hospitali ya rufaa ni kuhakikisha yale yanayoshindikana katika hospitali nyingine yanawezekana katika hospitali za rufaa,” alisema.

      Alitolea mfano kifaa cha kupimia cha CT- SCAN ambacho kina zaidi ya miezi saba hakifanyi kazi katika Hospitali ya Muhimbili huku ikiwalazimu baadhi ya wagonjwa wanaofika kutakiwa kufanya kipimo hicho katika hospitali nyingine.

      “Wengine hawana uwezo huo, wale wanaobahatika kufika huku wanakuta kifaa hakifanyi kazi, huyu ni mgonjwa bado unamuongezea gharama nyingine, tukiyasema haya wanasema sisi hatuwajali wagonjwa,” alisema Dk. Uliomboka.

      Alisema madai mengine ni pamoja na miundombinu ya hospitali kwa kile alichoeleza haziwiani na idadi ya wagonjwa na kutolea mfano wodi ya watoto katika Hospitali ya Temeke kuwa mazingira ni magumu.

      Alibainisha kuwa kitaaluma ni lazima wawahudumie wagonjwa wakiwa vitandani na inapotokea wagonjwa wakiwa chini inawawia vigumu kuwahudumia, na kwamba hayo ndiyo masuala waliyokuwa wanalalamikia.

      “Kwanini hospitali zetu ziwe sehemu ya mateso kwa wagonjwa badala ya kuwa sehemu ya faraja? Tunaambiwa tuwaandikie dawa wagonjwa, wakienda dirishani hata Panadol hakuna, haya hawataki kuzungumzia, wameamua kupandisha posho ya maiti wakati hata katika madai yetu hatukuwa na dai hilo,” alisema.

      Matabibu asili wanena

      Chama cha Utabibu wa dawa za asili Tanzania (ATME) wamewataka madaktari nchini kutopoteza uhai wa binadamu wenzao kama njia ya kuishinikiza serikali kusikiliza na kuwatekelezea madai yao.

      Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa chama hicho, Simba Abrahaman, alisema kuwa kwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki wagonjwa ya kupata matibabu.

      Abrahaman aliwataka madaktari kukaa meza moja na serikali katika kuweza kutatua malalamiko yao na si kugoma ambapo anayeathirika ni mwananchi kwa kukosa haki hiyo ya huduma za afya.

      Aidha, katika kuhakikisha mgogoro kama huo hautokei tena siku za usoni, alisema ni vema kukaundwa mfuko wa afya ambapo wananchi wataweza kuuchangia, kwa kuwa ukweli ni kwamba wamekuwa wakiitikia kuchangia mambo mbalimbali ikiwamo vyama vya siasa, hivyo halitakuwa zito.

      Hapo kwenye red mie naona sasa hivi kukaa kwa madaktari na serikali irushwe wazi kwenye vituo vya television na radio moderator awe mtu ambaye si mtanzania na hana maslahi na pande yeyote labda itasaidia kufungua macho watanzania. Na by the way hao waganga wanajishaua ili watangaze soko lao kwani inawashinda kitu gani waongee na serikali waingie muhimbili kama wao ni wa muhimu sana na wana utu.....mbona hawatoi dawa zao bure au huduma bure tena wao ni wafanyabiashara na wezi. Heri kugoma ili vizazi na vizazi vifaidi, mbona wanajeshi huwa wanajitolea kwenye vita na wengine mmefaidi, ingekuwa na wao mnawaambia wabaki ili mfe wote kama mnautu nyie mnaojifanya hamuelewi.

    20. #97
      Kwitu Kumpepo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Posts : 65
      Rep Power : 369
      Likes Received
      4
      Likes Given
      27

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      Lakini kumbuka kuwa wakiongezewa malipo madaktari, wananchi wa kawaida hatutanufaiki chochote kwa maslahi yao, na huduma itaendelea kuwa mbaya tu; hili ni tatizo la ki-MFUMO.

    21. #98
      tusichoke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2011
      Posts : 657
      Rep Power : 543
      Likes Received
      77
      Likes Given
      8

      Default

      Quote By Kadakabikile
      Kwani njia nzuri ya kufanikisha madai yao hadi wagome? Je njia ya majadiliano isingesaidia?
      WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
      Sina hakika kama unaandika ukiwa tanzania,kwani wanaofaidi keki ya taifa ni wasomi au watawala? Mbona hatusikii mishahara ya wanasiasa ikilipwa kulingana na elimu ya mtu? Kumbe ulishoandika ni opposite yake

    22. #99
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,024
      Rep Power : 0
      Likes Received
      227
      Likes Given
      1

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      mimi nawasihi madaktari kutokuwakomoa wagonjwa,ni vyema sana kuwahudumia watanzania huku mkiendelea na mashauriano na serikali,mkiwakomoa watanzania mnawaonea,kwani anayeathirika sio serikali.

    23. #100
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,024
      Rep Power : 0
      Likes Received
      227
      Likes Given
      1

      Default Re: Madaktari wagoma - Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela

      huu ushabiki wa kufurahia mgomo ni ulimbukeni wa hali ya juu kabisa,ivi bibi yako au mama yako angekuwa anaumwa ungeweza kushabikia hii kitu????

      Watanzania mbona tumebadilika kiasi hiki????

      mbona tumekuwa na roho mbaya hivyo????



      mi naomba kati ya nyie mnaoshadadia mgomo wa madaktari mpatwe na maradhi katika familia zenu hasa wale mnaowapenda na kuwathamini

    Page 5 of 6 FirstFirst ... 3456 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...