Nipo Mkoani Mtwara kikazi kwa wiki karibu mbili sasa.
Njia ya kuelekea Masasi mbele kidogo na ile round about yanapopaki magari ya zimamoto mbele kidogo ya njia panda ya airport kuna mhadhara unafanyika wiki ya pili sasa.
Mashekhe hao ambao wamepita katika kila eneo ambalo chadema wamepita na kufanya mihadhara wanapita na wao kueneza chuki na ghiliba za kidini kuwa asili ya chadema ni ukristo na malengo yake ni kustawisha ukristo
Wanakwenda mbali zaidi kwa kusema Adui wa muislam ni mkristo hivyo hakuna haja ya kukishabikia chadema.
Ingawa hawasemi chama gani kiko neutral wala hawasemi wafuasi wao wanatakiwa wafuate chama gani lakini wanawahamasisha wahakikishe kuwa kuna haki na usawa
Kampeni hii ambayo inafanyika katika mwavuli wa mikutano ya dini ambapo huanza kwanza kwa kuikosoa biblia kwa kutumia quran mwishowe humalizikia kwa kuiponda chadema kidini.
Nimefanikiwa kuhudhuria mkutano mmoja na nimesikiliza mwanzo hadi mwisho, kwa kweli wanafanikiwa kupata wafuasi na waamini wengi. Akili za vijana wengi ambao hapo awali tulidhani zimekombolewa kwa ujio wa cdm zimerud kule kule kwenye enzi za ujima na udini
MUNGU INUSURU TANZANIA NA DHORUBA INAYOWEZA KUTOKEA ANY TIME


Reply With Quote

Follow Us Here