Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".
Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.
Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".
Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?
Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.
Pamoja na yote Kindafu, imetuuma sana sisi tunaoamini kuwa Kiongozi yeyote huchaguliwa na Mungu, hivyo kumdhihaki na kumvunjia heshma ni sawa na kudhihaki/kuvunjia heshma wale wote anaowaongoza including wewe.
Mkuu Ngoromiko, hata mie naamini sana tu kwamba kiongozi huchaguliwa na Mungu, ila naamini pia kuwa kiongozi anaposhindwa kusimamia haki na usawa kwa watu wa Mungu anapoteza heshima yake mbele ya watu na hata mbele za Mungu pia! Naamini hata huyo Mungu hafurahi kuona wanachi wakipigika kimaisha kiasi hiki huku wachache wakitapanya mali na utajiri wa nchi na aliyekabidhiwa rungu la kuongoza hachukui hatua zozote!
Magamba bwana utawajua tu,hata mkikasirika ukweli ndio umeshasemwa.Eti rais tuliyemchagua,nani kamchagua kama sio wewe na magamba wenzio kuiba kura na kuchakachua,ila mwisho wenu utafika tu.
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".
Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.
Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".
Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?
Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.
Kikwete humuwezi.
zomba, utashangaa kusikia kwamba Kikwete mwenyewe is very cool about the whole thing. Ni mwanasiasa mwenye ngozi nguvu. Wanaolia-lia ni walamba miguu kwa kuhofia kupoteza kibarua kama hawakumsifia mfalme. Na wabunge wa CCM wanakuza hili kwa sababu hawana hoja.
Zomba unatangaza vita na Tz
Si wote tunaofaidi matunada ya CCM kama unavyo faidi wewe.
Unge kuwa makini ungechukua hatua wakati CDM walipotangaza list of shame, Akiwapo JK Fisadi.
Neno fisadi na udhaifu unapanuaje?
CCM ni ya wenye hisa na walifunikwa blanketi la giza ya CCM (walionyimwa elimu ya kujua haki zao)
Unatafuta ushahidi rais gani kafanya zaidi. Baba wa taifa aliacha viwanda vyote vina fanya kazi zote sasa ni magofu.
CCM ni ya Nyerere si ya wasanii wa sasa.
zomba, utashangaa kusikia kwamba Kikwete mwenyewe is very cool about the whole thing. Ni mwanasiasa mwenye ngozi nguvu. Wanaolia-lia ni walamba miguu kwa kuhofia kupoteza kibarua kama hawakumsifia mfalme. Na wabunge wa CCM wanakuza hili kwa sababu hawana hoja.
Mimi inawezekana simuwezi kwa kuwa sipo pale mjengoni wala Serikalini, lakini nasema Mnyika Kikwete hamuwezi. Amuone vile vile anacheka cheka, lakini "mtoto akichezea wembe muache". Sisi tunalitazama hili sakata litaishia wapi.
Hatutomwachia kabisa "mpaka kieleweke", kitoto kidogo kile hakiwezi kuja kututukana tukakiacha kicheke cheke hovyo. Lazima ajuwe maana ya Serikali ni nini, maana ya Rais ni nini, maana ya Bunge ni nini na maana ya kutukana ni nini.
Naanza kampeni rasmi, ya kuhamasisha kushikishwa adabu. Na hapa nimeanza tu, kukumbusha kuwa Mnyika Kikwete hamuwezi.
nashurukuru kwa kumhakikishia usalama mnyika, vinginevyo chochote kitakachompata tutajua kuwa ni nyinyi hivyo tutakula na nyinyi sahani moja. na rest assured kwamba you will not survive our defensive strike. kwa taarifa yako we determined to keep our leaders safe in the name of the redemption of our beloved counrty. nikiwa mkuu wa kitengo cha LAS, nakujulisha kuwa you are under intensive watch!
Zomba na wewe mwanadamu tu,huku kujiapiza namna hii unataka kumtisha nani asiyejua kuwa kifo ni mara moja kwa shujaa na mijitu mioga hufa siku nyingi kabla ya siku ya umauti wa kweli?JK DHAIFU!
Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".
Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.
Kwani who is KIKWETE ??? Ni JIIZI wengine. Sisi WaTanzania tunasema kama Mnyika atweza KIKWETE basi atuweze sisi WATANZANIA. He should ask GHADAFI na MUBARAK na wengineo imekuaje ??? THIS IS JUST AN ALARM FOR KIKWETE ---- AJARIBU TUU --- We are warning him that we have had enough kutuona WAJINGA na KUTAFUNA pesa zetu na mtoto wake is enough. TUNAMABIA anatangaza VITA na Wananchi wa TANZANIA. THIS IS A WARNING TO KIKWETE AND HIS FOLLOWERS AJARIBU
naanzisha dhehebu ambalo mungu wetu atakuwa jk, miongoni mwa sheria zetu itakuwa ni kutokosoa maouvu ya rais na kutumia sadaka kuficha maouvu na mapungufu ya kiutendaji.
ni mbaya sana kua unaongozwa na ushabiki na si uwezo wa kufikiri mi nadhani most of u hanjui mnachotaka udhaifu bwa kikwete ni chimbuko lenu wenyewe maana hakuna msafi bila uchafu, fikirieni sana maana kama mnadhani kikwete ni dhaifu nani c dhaifu mbele yenu maana hao mnaowaona c dhaifu mpaka leo hamjui c ridhki ama vp,darm u ol wavivu wa kufikiri na majuha wa ushabiki.
mheshimiwa zomba, pole mkuu, mie navyojua mbunge anapokwenda kinyume na taratibu za kikao hupewa alternative mbili 1.kufuta kauli yake au 2.kuthibitisha alichokisema. Wampe mnyika nafasi ya kuthibitisha udhaifu alionao kikwete.
we si ndio watalia kabisa maana jamaa ni dhaifu sana haina haja ya kuthibitisha.
Ni Kweli Myika hawezi lakini nguvu ya umma inaweza!!!!
Wapeni uhuru watoto wadogo ni aibu kuwavalisha watoto magwanda bila ridhaa yao Haki Elimu mpo wapi watoto wadogo wanadhalilishwa watoto wana haki ya kuchagua nguo za kuvaa sio magwanda
Zomba Zomba mkuu wangu nini hamaki kama vile sii wa Mujini babu?.. Lini neno Dhaifu likawa tusi kama sii Utindiga?. hata weye basi..JK amekuwa mtume mara!...Nina hakika yeye mwenyewe hapo alipo anawashangaa maanake hili neno la kawaida kabisa. Mangapi mmemtukana Dr.Slaa, mzee Mtei na hata Mbowe tena tunzi za uongo juu ya viongozi wa Upinzani ili kuwachochea wao watafute jinsi ya kujitetea?. Hii ndio siasa mkubwa! Huu ulikuwa mtihani kwenu kaa mnaona JK sii dhaifu mngesema haya yote kuonyesha ungangari wake badala ya kumfukuza Mnyika bungeni.
Kama siasa hamuziwezi kaeni pembeni, Na nitarudia kusema hivi leo hii mimi najiona Dhaifu sana sikwenda hata kazini (I am weak) Je nimejitukana?.. Kinachokatazwa ni kusema UONGO kusingizia udhaifu pale ambapo hakuna lakini Mnyika kaonyesha udhaifu wa JK ambaye alitakiwa kuhakikisha Bajeti yetu inakidhi shughuli za maendeleo zaidi ya matumizi ya ndani. Udhaifu huu JK anao maanake hata EL alimsemea mbovu mbele ya CC ya chama JK akabakia kuitikia kwa kichwa tu..Mbona hamkumtoa EL nje ya kikao badala yake mkamjengea sifa za kwamba Richmond sii yake bali ya JK..
Fedha zinaliwa hovyo vipaumbele havimsaidii mwananchi iwe wewe mwana CCM au mimi hapa. Sasa iweje Mnyika anayetetea maslahi yako ndiye awe mkosa?.. Acheni nidhamu ya woga, hii vita ya vyama iwe Chadema au CCM isituingie vichwani tukakosa hata kufikiri kwamba Bungeni sisi wote tutazame maslahi yetu na sii ya chama wala Rais. Unasema rais gani kafanya mengi kuliko JK wakati unashindwa kuelewa hawa wote ni viongozi wa CCM yaani hata chama chako mwenyewe unaona nafuu ya JK kuliko waliotangulia wakati nchi yako ipo ktk kiza, hakuna maji safi, madini yanachukuliwa ovyo, mikataba feki, walioiba EPA wamerudishwa bungeni kina Meghji na kadhalika haya maswala humuhitaji Mnyika kuyaona na kuyakemea hivyo yeyote atakaye simama kwa ajili yako wewe ndiye mwokozi wako.
Jambo moja muhimu sana ulifahamu, Bajeti hii ikipita kwa sababu ya hasira zenu juu ya Mnyika ndio mjue tumeliwa!.. Tazameni malalamishi ya Mnyika na kuyaunga mkono au kuyapinga lakini sio neno DHAIFU likupumbazeni...Hii inaonyesha nidhamu ya woga mlojengwa na Nyerere yule yule mnayemtukana kila siku hapa kijiweni.
Mkuu wangu Mkandara, hivi wewe hukuitwa mpuuzi hakuna tatizo kwako au utafurahia?
Kwa maoni yangu, sidhani kama kulikuwa na jambo kubwa sana kwa Mnyika kutimuliwa mjengoni, nafikiri naibu spika halipaswa kuwa na kauvumilivu ili Mh. Mnyika alieleze bunge udhaifu wa Mh. raisi kwa tafsiri aliyokusudia na kama itaonekana aliyoyasema ni uongo then zipo taratibu na kanuni za bunge zinapaswa kufuatwa. Hili la kumuita fulani dhaifu si tusi, kwani hakuna aliye na streghts pasi na kuwa na weaknes. Inabidi watanzania tubadilike kutokana wakati, huko nyuma kijana ( ama mtoto wako) alikuwa hawezi kuhoji uwezo wa Mzee ( ama baba) ata kama Mzee atakuwa na mapungufu mengi, lakini kizazi tulichonacho na kinachokuja hii itakuwa jambo la kawaida. Si ajabu mtoto wako, tena wa shule ya msingi akakutamkia " Baba wewe ni mzembe...na ndiyo maana familia yetu inakosa hiki na kile". Mwisho, sidhani hapa kuna person attack yoyote kwa Mh. Raisi ama kisasi kati Mh. Raisi and Mh. Mnyika. Watanzania inabidi tuongee.
Follow Us Here