Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: JamiiForums Premium Member Subscription

    Report Post
    Page 5 of 17 FirstFirst ... 3456715 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 328
    1. #1
      Mike McKee's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 10th February 2006
      Posts : 332
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      590
      Likes Given
      759

      Default JamiiForums Premium Member Subscription

      Ndugu wana JF

      Awali ya yote, niwashukuruni nyote!

      Tumeliongelea hili jambo kwenye andiko hii, Na sasa ni utekelezaji wake.

      Lengo kubwa la kuanzisha utaratibu huu ni kuiwezesha JamiiForums kujiendesha kwa ufanisi zaidi ndani na nje ya Tanzania.

      Tunayo mikakakati tuliyoianda ya jinsi gani tunafikiri JF inatakiwa iende, na tunaahidi kuwashirikisha kwanza "Premium Members" wetu kabla haijaanza kutekelezwa.

      Hizi alama maalumu zitadumu kwa mwaka moja.

      Baada ya mazungumzo marefu ya jinsi ya kupanga hii michango tulikubaliana hivi

      Annual Membership Subscriptions

      JF Bronze Member 20,000 - 99,000

      JF Gold Member 100,000 - 249,000

      JF Platinum Member 250,000 - 490,000

      JF Tanzanite Member 500,000 - Na zaidi...

      Utaratibu wa Malipo

      M-Pesa

      Tumefanikiwa kupata utaratibu mzuri sana wa kulipia kupitia M-Pesa. Utalipia Subscription Fee kama vile unavyonunua Luku au DSTV na kutuma kwenda kwenye number 888 888

      Jinsi ya Kutuma

      1. *150#

      2. Bonyeza 4 (Pay Bill)

      3. Bonyeza 1 (Enter Business Number)

      4. Weka 888888

      5. Enter Reference No. (tumia 1234)

      6. Enter Amount (Weka kiasi unachotaka kutuma)

      7. Weka password yako na kisha utume.

      Ukishatuma, tuma PM kuja kwangu Mike McKee ukituambia receipt no. uliyoweka na jina lako unalotaka liwekewe Premium Member au tuma email kwenda [email protected] ukituambia receipt number.

      CRDB Bank

      Account Name: Jamii Media Company Limited
      Account Number: 0150413278400
      Branch: CRDB Waterfront

      Ukishaweka pesa tuma SMS kwenda number hii 0755 642 929 kutuambia jina gani umetumia wakati unaweka hela, na nikiasi gani umeweka, na kutuambia jina unalotaka liwekewe alama maalumu (premium membership).

      Sisi tutaithibitisha kwa alama maalum (icon) na kukuwekea kwa hilo jina.

      Kwa wale watakaotumia malipo kwa njia ya mtandao (online transfer) ya CRDB, wanaweza wakatutumia receipt kwenda kwenye email ya [email protected]

      WesternUnion

      Name: Mike Mushi
      Address: P.O.BOX 4203 Dar es Salaam
      Phone: 0755 642 929
      Email: [email protected]

      PayPal

      Tuma kwenda kwenye email hii [email protected]

      Maswali na Majibu

      Alama maalumu kwa mtumiaji(Verified User) ni nani?

      Verified Users ni wale wanachama wa JF wanaotumia majina yao halisi. Sisi tuna hakikisha kujua kwamba yale majina ni yao kweli na kuwawekea alama maalumu inayoonesha kweli anayeandika kwa jina hili ni yeye halisi.

      Naweza kulipia kwa kidogokidogo?

      Malipo kidogokidogo yanaruhusiwa kwa wale Platinum na Tanzanite members na zinatakiwa kukamilishwa ndani ya miezi minne.

      Nataka kuchangia ila sitaki kuwekwa kwenye makundi

      Unaweza ukachangia kwa kutumia viwango hapo juu na usiwekwe kwenye hayo makundi ila ukawekewa “alama” ya premium member inayoonekana hapo juu.

      Kuna faida gani nikiwa Bronze Member na nikiwa Tanzanite Member?

      Lengo la hii program ni kuwezesha JF, hapa kinachofanywa ni uchangiaji na sisi tunachofanya ni kukutunuku “badge” kutoka na ulichochangia ili kutambua na kuthamini uchangiaji wako.

      Lengo letu ni mwakani tuweze kutoa packages nzuri kwa kila package. Na sisi pia inatupa mwangaza wa kutambua ni watu kiasi gani wapo, na wenye nia ya kuchangia na kununua hizo packages zitakapoanza.

      Kwa kipindi cha mwaka mzima kuna vitu vingi vitakuwa vinaanzishwa na vingi mtakuwa mnatuambia “premium members” mnataka nini.

      Hivyo vitu watakaokuwa wa kwanza kujua na kuvitumia kabla havijaanza kuwa wazi ni hawa premium members wetu. Maana yake maoni, ushauri unaanza kutolewa na hawa kwanza.

      Kuchangia JF na kuwa premium member kunakupa nafasi wewe kuwa mmoja ya wanachama muhimu watakaoongoza mabadiliko na kuwa mmoja wa watakaoshuhudia mabadiliko hayo ya JF.

      Je Subscption fee yangu ya mwaka mzima inaanza lini?

      Subscription fee yako ya mwaka mzima inaanza pale utakapolipia. Kama utalipa July, itakwisha july mwaka kesho.

      Kwanini hakuna malipo ya TigoPesa na Airtel Money?

      Utaratibu kama tulioupata Mpesa ndio tulikuwa tunautaka kama huo TigoPesa, sasa TiGo wamesimamisha hiyo huduma mpaka mwezi wa nane. Hatuna tunachoweza kufanya ni kusubiri mpaka mwezi wa nane. Njia ya kawaida ya kuchukua line ya tigopesa na kuiweka hapa sio salama na wote tunafahamu hii, mtu anaweza kudurufu laini na akaenda kuchukua hiyo pesa.

      Airtel Money bado tupo kwenye mchakato wa kupata utaratibu mzuri, na itakapokamilika itawekwa hapa.

      Je, inamaana nisipolipia premium members sitoweza tena kuipata JF?

      Hapana, JF itaendelea kuwepo kama kawaida.

      Hamuoni kuweka hizi “levels” mtaleta matabaka ya waliokuwanacho na wasiokuwa nacho na wachangiaji watawaogopa Tanzanite au Platinum members?

      Kwanza lazima tuelewe kwamba “levels” zipo kama “incentive” ya kuwapa hao waliochangia na kiasi gani wamechangia pia kuvutia wengine wachangie. Hii ni kama harambee hivi. Na pia unaweza ukachangia na pia usitake kuwekewa hiyo “alama” ya premium member wala hizo “badge” za levels ukabaki kama kawaida.

      Na pia kama kweli utaogopa username ya mtu yenye “alama” ya tanzanite na utashindwa kuongea au kubishana kwenye mada kwasababu unaogopa labda anapesa, sasa hapo tatizo ni kwako wewe. Inakuwaje unaogopa username ya mtu na inakunyima wewe uhuru?

      Na kama kweli italeta matabaka na itaondolea watu uhuru wa kuongea, basi itakuwa haina faida na hatutasita kuitasitisha.

      Mwisho wa siku, kama wewe ni tanzanite member na hufuati sheria za JF, unapata BAN kama kawaida.

      .......

    2. Miaka 50

    3. #81
      Mike McKee's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 10th February 2006
      Posts : 332
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      590
      Likes Given
      759

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By Oxlade-Chamberlain
      Mkuu, nimekumbuka kitu baada kuona hio post ya Bob G.

      Jaribu kutafuta mpango ambao utawezesha watu wanao weka biashara zao ndogo ndogo kama laptop, magari wawe wanatoa japo kamchango kidogo wa kuweka tangazo.

      Kwa vile inaweza kuwa ngumu kuwachaji watu bila kuuza na ni ngumu kujua kama mtu kauza , unaweza kufikiria njia nzuri zaidi hili watu wenye matangazo ya biashara nndogo ndogo waweze kutoa mchango.

      Njia moja nimefikiria ni kwamba mtu lazima awe na status ya premium member na zingine zinazoonesha kwamba kashawai kutoa mchango wowote hili kuweza kuweka tangazo la biashara yake ndogo ndogo.
      Najua kuna members wengine wamechangia lakini hawa status hizo, nina huakika mtakua mnawajua na kuweza kuruhusu matangazo yao.

      Baaadae pia mnaweza kuwa na jukwaa lime list items zinazo uzwa namembers humu hili watu wawe wanaenda huko moja kwa moja na kuona vitu ( kama ebay) na kikiuzwa kinatolewa.

      Ni wazo tu mkuu hili kuwezesha JF kujiendeleza zaidi.
      Mkuu,

      Hilo ni bonge la wazo. Tulikuwa katika mkakati wa kutengeneza site maalum kwaajili ya matangazo madog madogo ila kwa kipindi hichi tunaweza weka kwamba watakao kuwa wanaweza kufungua thread mpya huko ni lazima wawe atleast bronze member. Huku mkakati ukiendelea kufanyika.

      Idea nzuri sana..

      Quote By Remmy
      Tumekusoma, duuuuuuuuuu.....
      Remmy Tunasubiri yako..

      Quote By Maane
      Asante sana Mkuu Mike kwa kazi nzuri and taking into consideration our opinion,
      Sasa naona mambo yako vizuri zaidi. Ni action tu zinatakiwa sasa ili JF isonge mbele.
      Maane Mkuu, mawazo yenu ni muhimu sana..

      Quote By UKI
      Ila mkuu kweli kuna mtu kauliza swali hapo kuwa kwa walipaji kutumia mtandao kugundulika ni rahisi sana na vile vile navyojua bongo kitu privacy watu kutunza ni ngumu sana je mmejiandaaje na changamoto hizi kaka? Maana unaweza kumsema rais wako kwa kitendo kibaya cha ukweli aichokifanya ila afunike aibu anaweza kutumia mamlaka yake kukutafuta mpka uchochoroni kukupata na hapo ni kwa kuanzia kwenye hayo malipo. Please naomba hili nifahamishwe bro. Na nyie mko tayari kusimamia kwenye usiri??
      UKI Mkuu hatujawahi kutoa information za members wetu wala hatutoa toa kamwe.

      Quote By Adharusi
      Nitajitahidi niwepo katika Msafara
      Vox populi,Vox dei
      Adharusi Tunakusubii Mkuu
      Quote By Ritz
      JF Daima Paw
      Ritz Cheers

    4. #82
      MESTOD's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th November 2010
      Posts : 2,558
      Rep Power : 943
      Likes Received
      677
      Likes Given
      131

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Mkuu mfano sasa hivi uwezo wangu ni kuchangia sh 20,000 na baada ya muda nikawa na uwezo wa kuchangia sh 80,000 na pengine ukiwa imebakia miezi sita, mtaunganisha iwe sh laki moja na kumove hadi level ingine ya membership?

      Rai yangu ni kuwa hizo package ziangaliwe kwa minajili ya asante tu, maana jf imekuwa threat sana kwa watawala, ukisema hao premium members pekee ndo watakuwa wa kwanza, wanaweza wengi wakachanga na kutoa mawazo ambayo yatasababisha jf kutokuwa chombo cha habari ambacho kinatuhabarisha na hao wakalinda maslahi yao.
      Pia kama wadau wengine walivoshauri, muwe na marketing strategy nzuri. Ukiangalia blog ya michuzi na mjengwa utakuta wanamatangazo mengi sana, i think mnahitajika sana kuangalia upande wa masoko.
      Mike McKee likes this.

    5. #83
      Mgongo wa paka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd October 2011
      Posts : 397
      Rep Power : 464
      Likes Received
      23
      Likes Given
      0

      Default

      safi.wanapoongezeka watu wengi na post nyingi je mnaongeza nini kinacho wa gharimu pesa zenu za mifukoni?
      Mike McKee likes this.

    6. #84
      Zion Daughter's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 9th July 2009
      Location : Mlimani
      Posts : 7,589
      Rep Power : 13883
      Likes Received
      3249
      Likes Given
      1768

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By Ritz
      JF Daima Paw
      Hongera kwa kulipia na kuonyesha mfano
      Mike McKee likes this.

      The POWER of LOVE !!!!

      Its true that we don't know what we have got until we lose it and we don't know what we have been missing until it arrive.

    7. #85
      Mike McKee's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 10th February 2006
      Posts : 332
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      590
      Likes Given
      759

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By MESTOD
      Mkuu mfano sasa hivi uwezo wangu ni kuchangia sh 20,000 na baada ya muda nikawa na uwezo wa kuchangia sh 80,000 na pengine ukiwa imebakia miezi sita, mtaunganisha iwe sh laki moja na kumove hadi level ingine ya membership?

      Rai yangu ni kuwa hizo package ziangaliwe kwa minajili ya asante tu, maana jf imekuwa threat sana kwa watawala, ukisema hao premium members pekee ndo watakuwa wa kwanza, wanaweza wengi wakachanga na kutoa mawazo ambayo yatasababisha jf kutokuwa chombo cha habari ambacho kinatuhabarisha na hao wakalinda maslahi yao.
      Pia kama wadau wengine walivoshauri, muwe na marketing strategy nzuri. Ukiangalia blog ya michuzi na mjengwa utakuta wanamatangazo mengi sana, i think mnahitajika sana kuangalia upande wa masoko.
      MESTOD Yes, mkuu ukichangia sh 80,000 baadaye na imebaki miezi sita tutaku move hadi kwenye level ingine ya membership

      Ni kweli levels zipo kwaajili ya asante na sisi kuwashirikisha hawa premium members katika maswala mbali mbali ni sisi kuweza ku analyse maoni yao na sisi inatupa mwangaza watu wanataka nini.

      Nimeongelea hapo juu swala la marketing. Unaposema tuangalie blog za michuzi na mjengwa wanapata matangazo kumbuka kwamba sisi sio BLOG na wao wana manage content zao maana yake makampuni yanapenda kitu cha aina hicho. Huku wakikupa tangazo wanakuja na sheria na vigezo vingi mfano kampuni yao isiongelewe vibaya au CEO au wanasiasa wanaowataka wao wasiongelewe kabisa vibaya. Sasa mkuu ni kitu unachotaka kukiona hapa JF?

      Quote By Mgongo wa paka
      safi.wanapoongezeka watu wengi na post nyingi je mnaongeza nini kinacho wa gharimu pesa zenu za mifukoni?
      Mgongo wa paka Sijakuelewa

    8. FemaTV & Radio

    9. #86
      Nyalotsi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th July 2011
      Posts : 2,620
      Rep Power : 920
      Likes Received
      575
      Likes Given
      46

      Default

      Quote By Remmy
      Tumekusoma, duuuuuuuuuu.....
      kuna uwezekano wa kuanza kudharauliana humu. Sisi memba wa kawaida ukijibizana na tanzanite si utaambiwa ye ndo anayeiendesha jf? Na wale jamaa wa office za legelege wanaotuletea info itakuwaje? Maana siri nchi hii ni tabu sana kuimantain. Mf kuna kipindi tuliambiwa humu kwamba kuna mkurugenzi wa shirika moja alifukuzwa kwa kutengenezewa visa kwamba analeta madudu ya ofisi yao jf, sasa hii mitandao ya kina rostam siri itakuwepo?
      Mike McKee likes this.

    10. #87
      asigwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Location : TANDHANIYA
      Posts : 4,388
      Rep Power : 1264
      Likes Received
      1207
      Likes Given
      1253

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      SWALA HILI NI ZURI..kwa nini msianzishe utaratibu wa kuweka matangazo ya biashara pembeni mwa page kama most of the sites ili kupata pesa za kuendeshea JF?? maana najua kwa siku ni zaidi ya watu 30,000 wanalog in JF au hili hamjalitazama bado??
      Mike McKee likes this.

    11. #88
      ndetichia's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th March 2011
      Location : Mwime - Buswangili
      Posts : 18,178
      Rep Power : 5096
      Likes Received
      2769
      Likes Given
      231

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      well done Mike McKee
      Mike McKee likes this.

    12. #89
      Mike McKee's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 10th February 2006
      Posts : 332
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      590
      Likes Given
      759

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By Nyalotsi
      kuna uwezekano wa kuanza kudharauliana humu. Sisi memba wa kawaida ukijibizana na tanzanite si utaambiwa ye ndo anayeiendesha jf? Na wale jamaa wa office za legelege wanaotuletea info itakuwaje? Maana siri nchi hii ni tabu sana kuimantain. Mf kuna kipindi tuliambiwa humu kwamba kuna mkurugenzi wa shirika moja alifukuzwa kwa kutengenezewa visa kwamba analeta madudu ya ofisi yao jf, sasa hii mitandao ya kina rostam siri itakuwepo?
      Nyalotsi Mkuu, kuwa na tanzanite member haimanishi kwamba ndio unatakiwa ku abuse member wenzako na tukiona unafanya hivo basi tunaiondoa hiyo status ya tanzanite member. Tunawapa watu levels kama kusema asante, hicho tuu. Kuhusu jamaa wa office za legelege hapo sijakuelewa.

      Quote By asigwa
      SWALA HILI NI ZURI..kwa nini msianzishe utaratibu wa kuweka matangazo ya biashara pembeni mwa page kama most of the sites ili kupata pesa za kuendeshea JF?? maana najua kwa siku ni zaidi ya watu 30,000 wanalog in JF au hili hamjalitazama bado??
      asigwa Nimesema tena na nitarudia. Tatizo sio sehemu ya matangazo tatizo ni kwamba hakuna anayetaka kutangaza unless anatimiziwa masharti yake. Wewe utapenda sisi tuweke tangazo alafu tusiruhusu mfano CEO au Kampuni ya hiyo tangazo isiongelewe huku JF? Au kuweka tangazo na kupewa masharti kwamba mwanasiasa fulani asiongelewe? Tatizo sio sehemu ya matangazo tatizo ni masharti yanayokuja ya sisi kupokea hayo matangazo.

    13. #90
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,650
      Rep Power : 715
      Likes Received
      289
      Likes Given
      36

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Niwashukuru tena kwa kazi nzuri na uharaka wenu ktk kuamua jambo. 2po pamoja wakuu wangu
      Mike McKee likes this.

    14. #91
      SALOK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th September 2011
      Location : Some where!!
      Posts : 1,169
      Rep Power : 620
      Likes Received
      222
      Likes Given
      207

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Pongezi maradufu sana kwenu JF TEAM kwa hili, Mungu awazidishie maarifa na Afya mzidi kuitumikia JF. Kuna kitu nadhani mmekisahau naomba nikiseme kidogo! binafsi michango naona mmewaangalia wanaokaa maofisini pekee kumbe JF inawahusisha hata wachoma mkaa na wauza nyanya na vitunguu masokoni ambao nao wanahamu ya kuchangia kulingana na hali zao! kwanini viwango visingeanzia 5000/=, 10000/= na ........>>> ili kuufanya mtandao uwe milki ya watu wenye hali zote? au 5000/= na 10000/= hamna cha kufanyia hapa JF?
      Mike McKee and bombu like this.

    15. #92
      gfsonwin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 12th April 2012
      Posts : 10,669
      Rep Power : 21308
      Likes Received
      10026
      Likes Given
      13924

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      aaaah! sikujua kuwa watu walichangia anyway to me sioni tabu ya kuchangia kama kweli lengo kusudiwa litatekelezwa yaani jf itaendelea kuboreshwa.

      Pia hamuoni haja ya kwenda mbele zaid ya hapo kwenye kuchangia na kuwapa prestige tu hao premium members? manake nafikir mnapaswa kufikiria motivational means ambayo kweli itafika mahali watu watakuwa wanajitolea wenyewe pasi hata kupigiwa jalamba kama hivi. anyway kuwapa package ama nin ni one way but you have to more than that manake this is media group lazima muwe na perfect and convenient means of soliciting funds.

      sijui kama mmewaza ikitokea kama watu wakiacha huo umember for one one reason or another ambao walikuwa ndio sole contributors kiasi cha kushusha income yenu what will be the alternative.

      Pia nimefurahishwa sana na kwamba yawezekana mtu hatak hilo chata, lkn akachangia ni demokrasia nzuri but je kama akifanya hivyo mtamshirikisha kwenye maamuzi ya kuijenga jf? na je kuna wengine ndio wamejiunga tu au hawana uwezo wa kuchangia lakin michango yao ina value je wao pia mtawatumia katika kuijenga jf?

      kama nikipata majibu mazuri na ya kuridhisha katika haya maswali basi nitaamua accordingly.
      Mike McKee likes this.

    16. #93
      Mike McKee's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 10th February 2006
      Posts : 332
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      590
      Likes Given
      759

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By SALOK
      Pongezi maradufu sana kwenu JF TEAM kwa hili, Mungu awazidishie maarifa na Afya mzidi kuitumikia JF. Kuna kitu nadhani mmekisahau naomba nikiseme kidogo! binafsi michango naona mmewaangalia wanaokaa maofisini pekee kumbe JF inawahusisha hata wachoma mkaa na wauza nyanya na vitunguu masokoni ambao nao wanahamu ya kuchangia kulingana na hali zao! kwanini viwango visingeanzia 5000/=, 10000/= na ........>>> ili kuufanya mtandao uwe milki ya watu wenye hali zote? au 5000/= na 10000/= hamna cha kufanyia hapa JF?
      SALOK Wazo lako ni zuri mkuu. Na sisi tunaamini pia kwamba hata wachoma mkaa na wauza nyanya na vitunguu masokoni wanaweza kulipa ada ya tshs 20,000 ya mwaka mzima. Kwanini tunawadharau kwamba hawawezi kulipa hiyo 20,000. Sisi tunaamini wanaweza kabisa kulipa.

      Quote By gfsonwin
      aaaah! sikujua kuwa watu walichangia anyway to me sioni tabu ya kuchangia kama kweli lengo kusudiwa litatekelezwa yaani jf itaendelea kuboreshwa.

      Pia hamuoni haja ya kwenda mbele zaid ya hapo kwenye kuchangia na kuwapa prestige tu hao premium members? manake nafikir mnapaswa kufikiria motivational means ambayo kweli itafika mahali watu watakuwa wanajitolea wenyewe pasi hata kupigiwa jalamba kama hivi. anyway kuwapa package ama nin ni one way but you have to more than that manake this is media group lazima muwe na perfect and convenient means of soliciting funds.

      sijui kama mmewaza ikitokea kama watu wakiacha huo umember for one one reason or another ambao walikuwa ndio sole contributors kiasi cha kushusha income yenu what will be the alternative.

      Pia nimefurahishwa sana na kwamba yawezekana mtu hatak hilo chata, lkn akachangia ni demokrasia nzuri but je kama akifanya hivyo mtamshirikisha kwenye maamuzi ya kuijenga jf? na je kuna wengine ndio wamejiunga tu au hawana uwezo wa kuchangia lakin michango yao ina value je wao pia mtawatumia katika kuijenga jf?

      kama nikipata majibu mazuri na ya kuridhisha katika haya maswali basi nitaamua accordingly.
      gfsonwin

      Mkuu hii sio end game kwetu, hii haitokuwa the only revenue channel kwetu bali hii itatupa nguvu sisi ya ku explore other revenuer channels na tunafanya hivo. Hii itatusaidia sisi kupata funds kwaajili ya kuendesha mambo ya kila siku na kutupa sisi nafasi ya kuexplore revenue models zingine ndio lengo kubwa la hii program.

      Tunaamini kama tukiendelea kuitumia mwaka kesho basi hizi packages zitakuwa na advantages nyingi.

      Mfano, tupo kwenye hatua za mwisho na muda si mrefu tutakuwa na JF SMS Alerts ambayo watu wata subscribe huku Tanzania then sisi tukipata breaking news na tuka verify then tunawatumia SMS haraka sana. Sasa na hii pia ni revenue channel kwaajili ya JF. Mfano tukifanikiwa kupata subscribers 10,000 then tutakuwa tupo mbali sana.

      Ukiwa umechangia na hutaki hizo levels still tutakupa access kwenye Jukwaa La Premium Members ambalo utaweza kuchangia na kutupa maoni yako na pia hata kama ujachangia na una uwezo wa kutupa mawazo yako sisi tuna yasikiliza pia. Lengo kubwa la kushirikisha hawa preimum members na kutaka kuchukua maoni yao inatupa sisi urahisi wa kujua nani ni mzuri katika sector gani kwasababu katika maongezi kila mtu atakupa experience yake yeye.

      Tuna jukwaa la malalamiko na maoni tunafanyia kazi maoni ya malalamiko ya watu kila siku na wala sio preimum members hawa.

    17. #94
      gfsonwin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 12th April 2012
      Posts : 10,669
      Rep Power : 21308
      Likes Received
      10026
      Likes Given
      13924

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      count me in.
      Mike McKee likes this.

    18. #95
      Mike McKee's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 10th February 2006
      Posts : 332
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      590
      Likes Given
      759

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By gfsonwin
      count me in.
      Cheers!!!!

    19. #96
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,135
      Rep Power : 604
      Likes Received
      345
      Likes Given
      303

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Nilikuwa sina line ya vodacom naenda kuinunua sasa!.
      Mike McKee likes this.
      "Ikulu ni mahala PATAKATIFU,
      mimi sikuchaguliwa kuja kupageuza kuwa pango la wala RUSHWA."
      By J.K. NYERERE.

    20. #97
      Mvaa Tai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th August 2009
      Location : Ngudu, Mwanza
      Posts : 3,394
      Rep Power : 1175
      Likes Received
      1388
      Likes Given
      905

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By Mike McKee
      Mwisho wa siku, kama wewe ni tanzanite member na hufuati sheria za JF, unapata BAN kama kawaida.

      .......
      Nime kupata sana mkuu, hata mimi niliuelewa vibaya u-premium member, siku nilipo upata na nikachemsha kitu naku-gongwa ban kama kawa ndiyo nilielewa, ndiyo maana hata sasa nategemea kuchangia kutokana na uwezo wangu na siyo kwasababu ya hizo badge
      Mike McKee likes this.
      Mnang'oa meno ya Tembo ili mukayauze, mnang'oa meno na Kucha za Watanzania wasio na hatia ili iweje?

    21. #98
      Jiwe Linaloishi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th May 2008
      Location : Mlimani
      Posts : 3,106
      Rep Power : 17238
      Likes Received
      1622
      Likes Given
      1122

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Fillga kumbe upo mkuu kwema? mbona Mac hajanipa hizi habari? soon tutajumuika pamoja.
      Mike McKee likes this.
      SEMA UKWELI UMWAIBISHE SHETANI

    22. #99
      ntamaholo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2011
      Location : Mwilavya
      Posts : 4,116
      Rep Power : 1386
      Likes Received
      918
      Likes Given
      412

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      kwa hiyo wenye 1,000-5,000-10,000 haturuhusiwi kuchangia? mbona una taja madu makubwa makubwa?
      Mike McKee likes this.
      UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

    23. #100
      Ditto's Avatar
      Member Array
      Join Date : 30th August 2010
      Location : Johannesburg, South Africa
      Posts : 50
      Rep Power : 452
      Likes Received
      23
      Likes Given
      40

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Mike McKee asante kwa ufafanuzi na ntajipanga kuchangia.. Ila kwanini msiangalie na namna nyinigne ya kujiendesha zaidi ya kutegemea michango ya members? woga wangu huu utaratibu unaweza kusababisha baadhi ya watu kuona kuna risk dependecy especially kwa wachangiaji wakubwa.

      Kwanini msiangalie suala la kuuza shares au kujitanua kwa kutafuta source nyingine za funds zaidi ya matangazo na michango?
      Mike McKee likes this.

    24. Study Abroad
    Page 5 of 17 FirstFirst ... 3456715 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...